MUHUNI PIPI YAKO NITAIWEZA KWELI?
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
SEHEMU YA 6
Sikua na kingine cha kupoteza getoni kwa Chiba hivyo nilifunga mlango na kurejea nyumbani kwetu, nilikua mwenye mawazo sikujua taratibu zozote za polisi ubaya zaidi nilikua nawaogopa sana watu hao. Nilibaki nyumbani nikiwa
Maamuzi ambayo yalinijia kichwani nilichukua simu na kuipiga namba ya askari mmoja ambae kuna wakati tulikua karibu sana.
“Mambo vipi Michael?” nilisalimia baada ya simu kupokelewa upande wa pili.
“Poa, leo umenikumbuka mrembo ni miaka miwili nimekua nakueleza hisia zangu namna ninavyo kupenda ila umekua ukinifungia vioo sana, hisia zangu hazikumi juu yako, nakupenda sana Lau wangu” Michael aliendeleza vitendawili vyake vya kila siku.
“Sawa Michael nakuelewa hayo tutaongelea baadae ila ujue nna tatizo mwenzako na sijui nafanyaje?”
“Tatizo gani tena mamii?”
“Kaka angu kakamatwa na bhangi, mimi mwenzako na mambo ya polisi ndo siyaelewi kabisa, naomba msaada wako katika hili” niliamua kufunguka shida yangu mbele ya askari huyo.
“Kaka ako anaitwa nani na anamepelekwa kituogani cha polisi?”
“Wale askari wamesema wanampeleka kituo cha kati, jina lake anaitwa Chiba”
“Sawa funga safari tukutane hapo kituoni, ila usisahau badae usiku ni lazima tuonane ili tuzungumze vizuri”
“Sawa hakuna shida” nilielewa askari huyo ni mazungumzo gani aliyataka ila kwa upande wangu kumwona Chiba anatoka ndo jambo la kwanza na muhimu.
Nilijiandaa na kwenda kituo cha polisi cha kati, kwa bahati nzuri nilimkuta yule askari yupo nje ananingojea nilisalimiana nae japo yeye alitaka nimkumbatie nami nilimkumbatia japo sikulifurahia kumbatio lenyewe, nilifanya ilimradi tu kwakua nilikua na shida ya Chiba kutoka, aliniambia nimsubiri pale nje. Aliingia ndani, nilihisi Michael alikua na cheo kuliko askari wengine kwani alipokua akikutana na askari walikua wanampigia saluti sana kwa heshima.
Baada ya dakika kumi alitoka nje akiwa ameongozana na Chiba angalau hata akili yangu ilipata utulivu kidogo na hata ule mzigo ambao niliubeba kichwani niliona umepungua uzito.
“Kijana nimekutoa kwasababu ya huyu Lauryn ila bila ya hivyo ungepelekwa mahakamani ambapo ungekutana na kifungo chako gerezani kwahiyo kuwa makini kwenye mienendo yako yote kuanzia sasa” Michael alimsisitiza Chiba, mpenzi wangu nae hakugoma bali alimuitikia sawa kwamba atakua makini, Chiba alijisogeza karibu yangu kunikumbatia nami sikumnyima kumbatio, kwani kufanya hivyo ningemkasirisha na wakati huo ametoka kwenye matatizo.
Shida ilikua kwenye namna tulivyokumbatiana kwani tuligusanisha viuno, si unajua tena kumbatiana ya wapenzi ni tofauti na ile ya kaka na dada.
“Heeeeee inatosha sasa, wee jamaa unamkumbatiaje hivi dada ako?” Michael aliingiwa na wivu ukampelekea atuachanishe kwamba hatukupaswa kukumbatiana hivyo.
“Oya weeeh mbona unaingia kwenye kumi na nane zangu huoni unajijaza kwenye mfumo wangu, nani kakwambia huyu ni dada angu, wee mzee ujue huyu ni demu wangu halafu mambo ya dharau eti kisa wewe polisi sipendelei”
“Bhasi baba angu emu tuondoke” niliamua kuingilia na kumtuliza Chiba kwani nilihofia huenda akaleta shida akajikuta anarudishwa lock up tena.
“Lau unasemaje unamwitaje huyu jamaa na unaona anavyonitishia nitawaita vijana wamkamate na kumrudisha ndani”
“Oya weee huna chochote cha kunifanya, wee kipere tu, wahuni tunaweza kukikuna muda wowote” Chiba aliongea maneno ambayo yalimkasirisha zaidi Michael, hakutaka kuendelea kubishana bali alitoa simu yake na kuibonyeza kwa lengo la kupiga simu, hapo nilikua nimechanganyikiwa sijui nizimaje moto wa mahali hapo.
SEHEMU YA 7
“Michael emu subiri kwanza, naomba usiwaite vijana wako naomba nisikilize mimi nakuomba sana?” Nilijishusha na kumnyenyekea zaidi Michael, niliona ananielea akasitisha zoezi la kupiga simu na kunipa nafasi ya kuongea.
“Nitakutafuta baadae ili tuweze kuzungumza zaidi kwa hapa hatutaelewana, tuachie sisi twende halafu mimi na wewe tutayajenga zaidi”
“Kwa heshima yako nawaacha muende ila ukumbuke ahadi yako ya kunitafuta” Michael alisisitiza.
“Oyaa wee boya kama maboya wengine tu, demu wangu akikutafuta labda mimi sio Chiba mnyama nakwambia” Chaba aliendelea kurusha maneno, ikabidi nimvute na niweze kuondoka nae, niliita boda na tukaondoka hapo, tulienda moja kwa moja mpaka getoni kwake, huko ndipo vita ya tatu ya dunia ilipoiburiwa.
“Kwahiyo unamthamini sana yule bwege ndo maana ukamwambia utamtafuta baadae sio?” Chiba aliongea huku akipiga ngumi ukuta kwa hasira.
“Punguza jazba baba angu wee, mimi sina huo mpango wa kumtafuta kabisa na hata leo nilimtafuta kwasababu sikuona kama kuna njia nyingine ya kukutoa polisi zaidi ya ile najua nimekosea na kukuumiza naomba unisamehe ujue naumia nikikuona kwenye hiyo hali”
“Mimi polisi kutoka ningetoka tu kwasababu sio mara yangu ya kwanza kuingia kule halafu jambo lingine mimi wakiume siwezi kuogopa polisi kabisa, jambo la tatu ujue siku nyingine nikiwa kwenye matatizo usitumie short cut kama za leo, hawa mabwege kama Michael watakuja kukugonga halafu muhuni kugongewa demu wako sio safi ni aibu na fedheha kubwa sana kitaani, tutakuja kubwagana ujue na hiyo stage mimi sitaki tufikie aiseh” Chiba aliniambia nami nilikubali kumsikiliza bado alikua na hasira kumwacha kwenye hali hiyo wala isingekua nzuri kwa afya hivyo nilimwita.
“Hebu njoo kitandani mara moja nikwambie kitu?”
“Kitu gani si useme hapo hapo” kijana alionesha ubishi.
“Njoo unyonye” nilimwambia kwa mapozi mengi sikuishia hapo kwani nilitoa tisheti langu kabisa, chuchu zilisimama dede, zikimkonyeza mhuni, kwani mhuni hana hisia kwani mhuni anajua kukaza milele, niliona anajisogeza taratibu, akaiwahi ya kushoto na kuifakamia kama mtoto, nyie kweli wanaume hawakui hata awe na umri mkubwa kiasi gani kwenye mambo ya kunyonya wanapenda kinoma, tulijikuta mmoja chini mwingine juu, tulikamiana na kupeana uhondo, unajua kesi nyingine zinamalizika kitandani, zile sauti za mahaba tu zinatosha kabisa kutatua na kuua kila aina ya mgogoro, ilipofika saa tatu kamili, niliona ni muda wa kurudi nyumbani hivyo nilijiandaa, nilimpiga busu kipenzi changu Chiba na kumkumbatia kimbembe kikawa kwenye kuniachia eti hataki kuniachia anadai anataka aendelee kunikumbatia nyie wahuni wakipenda wanapenda vibaya sana na wanakua ving’ang’a kweli kweli, nililalamika ndipo aliniachia, tulitoka na kutembea mpaka karibu na mtaani kwetu sikutaka niende nae sana kuepusha macho ya watu ambayo yangempelekea taarifa kamili kaka angu, nilitembea nikiwa mwingi wa furaha, nilikuta mlango upo wazi kwa maana kaka amesharudi, niliingia ndani sebuleni nilimkuta kaka akiwa anavuja damu usoni, alitumia kitambaa kujifunga na kujizuia damu hiyo ili isiendelee kumtoka, nilipigwa na butwaa sana na jambo hilo, kaka angu alikua kwenye hali mbaya.
SEHEMU YA 8
“Heeee jamani nini tena kaka, umefanyaje hapo?”
“Acha tu mdogo angu naomba unisaidie hii damu ikate”
“Nikupeleke hospitalini sasa kaka hali itakua mbaya”
“Hospitali uongo watataka vibali vya polisi halafu kuvipata hivyo vibali ni kazi sana, nisindikize kwa Dr Luago yeye atanisaidia kushughulila na hili jeraha” tuliongozana na kaka mpaka nyumbani kwa Dr Luago, yeye alikua daktari mstaafu hivyo alikua na pharmacy nyumbani kwake alitupokea vizuri na kuanza kushughulika na jeraha la kaka alimshona kwa nyuzi kadhaa tulimlipa pesa na kurudi zetu nyumbani, nilimpa dawa za kutuliza maumivu kwanza sikutaka kumhoji ni jambo gani lilimkuta nilitaka atulie kwanza kwakua kesho yake ni jumapili bhasi tungepata wasaa wa kuongea vizuri.
Siku mpya ilipoingia nilimgongea kaka, tukasalimiana nilimpa dawa zake zq maumivu na kutoka nje kwenda kumuandalia kifungua kinywa, alijitahidi na kutoka nje hivyo tulikunywa chai, alinieleza anaendelea vizuri ndipo nikamuuliza ni kitu gani kimemtokea mpaka kuumia namna ile.
“Mdogo angu mama angu, Mungu amrehemu huko alipo alikua mwanamke na wewe ni mwanamke ila mtanisamehe kwa kusema kwamba wanawake ni mashetani tena wanq roho mbaya sana”
“Heee kuna nani mpaka useme hivyo kaka ni maneno makali sana dhidi ya viumbe vilivyoijaza dunia”
“Lau mdogo angu yule mwanamke Sharifa ni zaidi ya muuaji, kumbe ana mwanaume mwingine na ndie analipa kila kitu kuanzia kodi na mambo mengine, jana nikiwa nyumbani kwake, sindio akaja huyo mwanaume kunikuta mimi ndani tukaanza kupigana, alinipjga vibaya hapa usoni ndio maana ya hizi damu, bahati nzuri nilitoroka kabla ya marafiki wa yule bwana hawajaja kwani wangefika na kunikuta pale labda wangenifanya kitu kibaya zaidi” kaka aliongea kwa manung’uniko makubwa sana, nikampa pole kaka angu kwani huyo Sharifa alikua anapendwa sana na kaka angu tena kamtenda vibaya sana.
“Ndio maisha hayo wanawake wamejawa tamaa nyingi, tuachane na hayo mambo ya mahusiano tuongeze nguvu kwenye kutafuta pesa kaka angu”
“Hilo sahihi sana mdogo angu, tufanye hivyo ili maisha yaendelee”
Bhasi nilipika chakula cha mchana tulikula, nikaa tu nachat chat na mpenzi wangu Chiba, nilikua namwelezea namna tumbo la mshahara wa mwezi lilivyokua linaniuma, bhasi ananipa pole na kunambia kama ingekua uwezo wake bhasi angeomba maumivu hayo yote ayabebe yeye, bhasi mimi kusikia hivyo najisikia vizuri weee.
“Hebu toka nje ukutane na surprise yako” jumbe ya Chiba ilisomeka namna hiyo, sikujua anamaanisha nini maana muda wote nilikua nachati nae sikujua kama anakuja, nikamwambia aachane na masikhara akaniambia kweli yupo karibu na kwetu, kwa furaha nikatoka nje mpaka alipokua kasimama, nilimkumbatia kwa nguvu.
Mhuni wangu hakua mwenyewe bali alikua na vitu vilivyo msindikiza alikua na kimfuko mkononi mwake, alinipa na kunambia hiyo ni period package, weee Mhuni na mambo ya kizungu tena mbona nilihisi kama napaa mwenzenu sijawahi fanyiwa kitu kama hiko kwenye mahusiano yangu yote yaliyopita, yaani niwe kwenye siku zangu mwanaume alinibebee pedi, vibiskuti, chocolate, youghurt na juice ya embe haijawahi tokea nilikua nasikia kwa rafiki zangu tu wametendewa hivyo na wapenzi wao ila ajabu na mimi nilikua natendewa na Chiba wangu, hakua na pesa nyingi ila alijitahidi sana kunijali, jamani kuwa na mwanaume ambae anakukumbuka hata lwa kidogo anachopata hiyo ni baraka kubwa, kuliko hata kuwa na wale mabwana wamiliki crown ila ni wachoyo balaaa, ukitaka kupata zawadi zake ni wakati wa kukutongoza sasa hizo pesa zake ni mpaka wakulale.
Chiba wangu alikua ananiteka moyo wangu hatari, kwanza alikua amependeza amevaa zile nguo tulinunua pamoja na kuachana na vile vinjunga vyake, mbona utampenda.
“Weeee Lau, hebu njooo huku” nilisikia sauti ya kaka ikiniita kwa nguvu, nikaagana na Chiba wangu kwa kumpiga busu la mbalimbali nae aliondoka zake, nilirudi na kumkuta kaka ana maswali mengi sana.
SEHEMU YA 9
“Mdogo angu umetoka kunishauri tuachane na huyo mdudu anaeitwa mapenzi na wewe umekwenda kuuvagaa ili ukung’ate wote tuwe wagonjwa, hebu tuwe watu wa kuyaishi maneno yetu sio kuongea ongea kama mbishi sawa endelea mpaka yakukute yaliyonikuta mimi”
“Kwahiyo kaka unaombea mabaya yanikute na mimi jamani?” nilimuuliza maana maneno yake sikuyaelewa elewa vizuri.
“Siombei hivyo mdogo angu ila uhusiano usio na mwelekeo mara nyingi hutupeleka kwenye shimo, kwa upande wangu ni mara nyingi sana nilikua namwomba Sharifa nimuoe, alikua ananizunguusha wee kumbe alikua ananijua kwamba kuna mwanaume mwingine anampenda zaidi yangu, kwahiyo sitamani na wewe uingie kwenye huo mkumbo wa shida” nilimkubalia kaka kwamba nimemwelewa sikutaka aendelee kunipa nasaha zaidi, niliona kama penzi langu na Chiba halikuhitaji ushauri wowote tena namjua kaka Wille alivyokua mzuri kwenye kuongea na kushauri, ngoja kinirambe siku moja ndipo nimkumbuke kaka Wille na nasaha zake.
Tuliongea mambo mengine ya ucheshi ya kusukuma siku na jumapili ilipopita, jumatatu niliingia kazini kama kawaida niliwahi mno, nilifanya usafi, baada ya muda alifika boss wangu Samir.
“Hey Lauryn mambo” boss alinisalimia kwa uchangamfu kama wote, nilijisemea moyoni siku imeanza vizuri kweli kwani boss wangu nilimjua kwa kuwa kauzu sana.
“Poa boss vipi”nilijibu kwa kifupi japo katika hali ya ucheshi.
“Salama kabisa, weekend yako ilikuaje?”
“Poa tu haina mambo mengi”
“Ooh sawa” boss alijibu na kuingia ofisini kwake.
Ulipofika muda wa chai aliniita na kuniagiza.
“Mimi niletee chai ya maziwa na chapati nne, pesa inayobaki nunua chochote unachotaka” Boss Samir alizidi kunishangaza siku hiyo, nami nikashukuru nikajua muamko wa siku hiyo ulikua mzuri kweli.
Nilienda mpaka kwa mgahawa ambapo huwa tunaagiza chai, niliagiza chai mbili za rangi na chapati sita, niliona chapati mbili zinanitosha kabisa sikutaka kuleta tamaa yoyote.
Nilirudi ofisini baada ya muda walituletea vitu hivyo nikatenga vyangu na kuweka mezani vile vya boss nikampelekea ofisini kwake.
Asubuhi ikapita ilipofika mchana hali ilikua ile ile akaniita nikaagize chakula cha mchana, yeye alitaka ugali kuku, mimi nikaamua nijinafasi kidogo nikaagiza chips kidali na pepsi ya baridi.
Niliporudi boss hakuniuliza kuhusu change yake wala nini, tajiri alikua kacheka vizuri sana hivyo ni mwendo wa ofa na kufurahia mchezo.
Ilipofika jioni muda wa kuondoka aliniita ofisini kwake na kuniambia.
“Unajua Lauryn, mimi na kaka ako tunajuana muda mrefu lakini sijawahi kujua anaishi wapi, sasa kama watu mnaojuana na hujui mwenzako anaishi wapi hilo ni kosa kubwa sana kwani siku akiwa na shida itakua ngumu kwako kufika kwake, kwahiyo leo tungeenda wote mpaka nyumbani kwenu ili nipajue mnapoishi” Boss Samir aliongea huku akijichekesha chekesha, nilijua kazi ipo kumbe mazingira yalianza kutengenezwa tangu asubuhi kwa vijichai, mara chakula cha mchana, yote kunitengenezea mimi wepesi, ila wanaume wakilitaka jambo lao mmmmmh.
“Sasa kaka amesafiri kidogo na mimi naelekea kwa shangazi leo kwani kulala peke angu pale nyumbani ni jau kidogo” nilitunga uongo wa haraka haraka hapo, nilijua Boss Samir kuna kitu alikua anakitaka kwangu maana hata angalia yake alikua ni mtu mwenye matamanio na mimi.
“Ngoja nimpigie simu hata nimuulize anarudi lini?” Boss Samir aliongea huku akitoa simu yake, alionesha kutokuniamini hivyo alitaka kuhakikisha kama kweli kaka kasafiri au yupo, kwangu sikupata utulivu kabisa kwani niliona nakwenda kukamatika muda huo huo.
SEHEMU YA 10
Sikutia neno nilisubiri mambo yawe yatakavyokua kwani kuongea hapo ingesababisha nionekane muongo zaidi.
Boss Samir alipiga simu zaidi ya mara tatu kuonesha kweli alidhamiria kuongea na kaka, lakini mara zote hizo tatu, namba ya simu ya kaka haikua ikipatikana, nilimshukuru mungu kwa hilo kwani aliniepusha na kuonekana mwanamke mwongo.
“Kwani ameenda wapi maana naona simu yake haipatikani kabisa?” Boss Samir aliniuliza.
“Ameelekea kijijini huko ameenda kufuata mzigo wake wa mkaa, kama atakuta mzigo tayari wiki hii hii atarudi, kama mzigo bado anaweza tumia wiki mbili ndipo asafirishe na kurudi nao mjini” nilitunga uongo mwingine, yaani mtu ukitaka kujinasia sehemu ni mchezo wa haraka haraka tu kupata akili mpya na kitu cha kuongea.
“Aiseeh kweli Wille ni mpambanaji sana, tena anazijua kazi ngumu ngumu mno, kuna kipindi nilimwomba aje hapa tufanye wote kazi maajabu alinikatalia eti kwa madai hataki kuajiriwa anataka kufanya kitu chake kwani hiko kitamfanya ajitoe kwa nguvu zote kwani anajua anayajenga maisha yake, binafsi nilimuelewa yule kaka ako ana akili ya kitajiri sana na ipo siku atafanikiwa sana” Boss Samir alimwaga maua kwa kaka angu japo sikujua kama maua hayo yanaukweli au ndio njia ya kulainisha moyo wangu huku akisukuma kete za kutaka kuninasa kwenye himaya yake.
“Amen amen, anajituma sana kaka angu, sasa boss mimi nikuache niwahi huko kwa shangazi” nilionesha kuwa na haraka.
“Mmmmh saa kumi na mbili hii na nusu, angalau ingekua unaenda nyumbani tungesema unawahi kupika ila kwa shangazi ako utakuta wameshakupikia kwani taarifa ya kwenda si ulishawatolea” Boss Samir aliendelea kunibananisha kwenye kona, nami niliitikia nikweli nimetoa taarifa.
“Kuna jambo limenijia akilini mwangu haraka haraka hapa, natamani tukakae mahali angalau risaa limoja, tule tunywe halafu tuongee mambo fulani fulani hivi mazuri sana”
“Mmmh Boss jamani kwanini tusifanye weekend”
“Hapana maneno yangu nataka uyasikie leo, sitaki baadae uje uniambie yaani umechelewa jana tu nafasi ikajazwa linalowezekana leo lisingoje kesho, halafu kwa hilo lisaa limoja nitakulipa laki moja sio kinyonge utaingiza kitu cha kukusaidia kununua vipodozi kidogo ili uendelee kuwa mrembo” Boss Samir alisukuma kete ya mwisho ambayo ilinimaliza kabisa yaani Laki moja ndani ya risaa limoja, kukataa hiyo pesa ningeonekana mwendawazimu, waswahili wanasema kubali wito, kataa maneno, tuliongozana mpaka kwenye bar moja iliyokua ng’ambo ya pili ikitazamana na ofisi yetu.
Tuliagiza nyama choma na vinywaji pale, mimi niliamua kushtua koo na serengeti light huwa nazigusa gusa japo kidogo na nilikua na uhakika haziwezi kunilewesha, yeye aliagiza Safari tatu hivi, ilipofunguliwa moja aliipiga chap chap mikupuo mitatu, chupa haikua na kitu tena, alifungua na nyingine nayo aliipiga chap chap ikaisha, chupa ya tatu hiyo ndio ambayo ingesukumia mazungumzo yetu wakati tunaongea mambo ya hapa na pale hasa yale aliyoniitia, nilikitafsiri kitendo cha kunywa bia haraka vile ni sawa na kuondoa aibu mbele yangu, alianza kuongea kwa kujiamini sana.
“Lauryn siku ya kwanza unakuja ofisini kwangu nilikuona ni mtu dhaifu sanaa, usieweza kazi hii lakini siku nilizokaa na wewe ofisini nikagundua kitu kipya wewe ni genius, unaijua biashara vizuri kwamba ukiwekeza vizuri akili yako kwenye kampuni yetu ndani ya miaka mitano tutafanikiwa sana sio kampuni tu hata kwenye maisha yangu binafsi mambo yataniendea vizuri, wewe mwanamke unaakili sana, utanifaa mno maishani”
“Ahsante boss japo sijajua unamaanishaje unaposema nitakufaa maishani mwako?” nilimuuliza ili afafanue zaidi.
“Kiufupi nakupenda nataka kukuoa uwe mke wangu, unajua nimezunguka kwa wataalamu kadhaa baada ya kukuota wewe mara tatu mfululizo, mara hizoo tatu yaani nakuota wewe tu, wataalamu wakaniambia kwamba wewe unanyota kali sana ya mali, kama itaungana na mimi tutakua matajiri wakubwa sana” Boss Samir kumbe alienda kwa waganga ndio wamemueleza kwamba nina nyota kali ya utajiri, nilijiuliza kwamba alikua ananipenda kweli au alitaka kuwa na mimi ili apate huo utajiri ambao aliusemea, nilikua katika tafakuri pana kabla ya kusema neno lolote.
Inaendelea……..

