MUHUNI PIPI YAKO NITAIWEZA KWELI?
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
SEHEMU YA 16
“Historia yangu ya maisha sio ndefu sana kama watoto wengine nikiwa mdogo nilipelekwa kwenye kituo cha kulelea yatima na wazazi wangu. Binafsi sikujua ni kwanini wazazi wangu hawakutaka kunilea wenyewe wakaona kunipeleka kituo cha kulelea watoto ndio sahihi kwa makuzi yangu, kuna muda nilitamani kurudi nyumbani kwao lakini jitihada zangu zote nilikua zinagonga mwamba mara nyingi wazazi hawakunihitaji tena nami nilifunga ukurasa wa maisha pamoja na wao, na mimi sikuwahitaji kabisa kwenye maisha yangu, nilisoma shule nikiwa kituoni, kutokana na mambo ya wazazi na hapa na pale nilijikuta sielewi chochote shuleni, nikafeli kidato cha nne, sikutaka kuendelea na shule japo walezi wa kituo walitaka nikarisiti au niende veta nikasomee ufundi yote hayo nilikataa, niliwaomba ombi moja tu kwamba nataka niondoke nikajitegemee mtaani, walisikitika sana kwa kuwaza maisha ya mtaani yalivyo magumu, walikaa na mimi wakinishauri nikubali kwenda veta ili nikiingia mtaani niwe na ujuzi.
Mimi niligoma bado kiu yangu ilikua kuingia mtaani, walinikubalia nikaingia mtaani kibishi kibabe, maisha yamesonga mpaka leo unapata unakula, ukikosa bado unaendelea kumshukuru Mungu, harakati za mtu mweusi hazijawahi sahaurika na kudra za mwenyezi Mungu hivyo ipo siku nitatoboa tu kibingwa” Chiba aliweka kituo hapo, historia ya maisha yake ilikua inaumiza kwa upande mmoja ama mwingine, nilimpa pole na kumuuliza.
“Vipi una ndoto ya kukutana na familia yako siku moja?”
“Ndio ndoto ninayo kubwa sana, mtu wa kwanza kwenye familia yangu ni wewe na mtu wa pili ni mtoto atakaekuja kupitia tumbo lako hili, sihitaji familia nyingine zaidi ya hii hapa” Chiba aliongea kwa hisia sana huku akilibusu tumbo langu kama limebeba mtoto vile, taratibu alijilaza kwenye mapaja yangu nami nilikua nampapasa taratibu kichwani, nilimuelewa Chiba kwa aliyoyapitia hakutaka kukutana tena na familia yake ya zamani, hivyo uamuzi ambao niliona unafaa ni kutomtajia kaka angu mahali anapopatikana Chiba, sikutaka wamchukue Chiba kutoka mikononi mwangu kwani niliamini ndoto zangu za baadae zinamhitaji sana Chiba kuliko mwanaume yeyote, nilipenda katika namna ambayo sijawahi jisikia kupenda namna hiyo, Mhuni nae hakua na mambo mengi alinipenda.
Watu ambao wamewahi sema kwamba wahuni huwa hawacheat yaani wao ni kula bhange yao, mwanamke mmoja halafu wanafocus na maisha walikua sahihi kabisa.
Tulipika, tukala chakula na ilipofika jioni niliona ni kheri nirudi nyumbani ili nikajue kaka amefikia wapi kwenye swala la kumtafuta Chiba ili kama kuna mahali amefika penye hatari zaidi niweze kumweleza Chiba awe makini kwani familia yake inamtafuta kwa mamilioni ya pesa ili wampate.
SEHEMU YA 17 + 18
Niliporudi nyumbani baada ya dakika kumi kaka nae aliingia alikua amechoka sana, kazi ya kumtafuta mtu ambae hujui yupo wapi ilikua imemchosha sana, alitembea kila upande akiwa na picha hiyo lakini hakufanikiwa kumpata Chiba wala fununu za mahali alipokua, aliniuliza vipi kwa upande wangu kama kawaida nilisema kwamba sijamwona mtu huyo, nilipika chakula cha usiku, wakati tunakula nilipata wasaa wa kumuuliza maswali kaka.
“Hivi kaka wewe angalau unayajua mambo ya kimila na desturi za kabila letu, hivi kwenye swala la kuoa au kuolewa kati yangu na wewe nani anatakiwa kuanza?”
“Kiuhalisia mpaka leo hii nilitakiwa mimi niwe nimeoa tayari kwani mkubwa ndo anatakiwa kutangulia kwa hizo mila za kwetu, ila kwasababu mbalimbali hasa za maisha, zimenifanya sijaoa mpaka leo hii, ila usijivunge mdogo angu tayari umeshakua mkubwa hivyo akitokea mwanaume anataka kukuoa na wewe umeridhika nae mpe nafasi tu pasipo kuwaza labda kaka ndo anatakiwa kuwahi kuoa wala nini kwani mipango ya Mungu ni mingi tena huwa inaenda mbali na mafikirio ya akili zetu.
“Hapo sawa nimekuelewa kaka na vipi kuhusu mahali unahisi mahali inaweza kuwa bei gani?”
“Hahahahaha eti bei wewe sio bidhaa na sitokuuza mdogo wangu ila mahari husimama kama shukrani ya malezi tu, hivyo bhasi ahsante hiyo wakinipa milioni tatu kutokana na usomi wako na akili kubwa ya maisha uliyonayo nazani itakua sio vibaya, mbona unauliza uliza sana maswali ya ndoa, vipi umepata shemeji nini huko hahaha”
“Hahaha hapana kaka, akipatikana atakuja tu, mwanamke kuolewa ndoa ya heshima nayo ni fahari kwahiyo akija tu huyo shemeji yako muoaji nitamleta haraka hapa ili akulipe chako, mimi niende huko nikatumikie ndoa” tuliongea mambo mengi sana usiku huo, kuhusu mambo ya ndoa tulipeana ushauri mwingi wenye kutusaidia katika maisha.
Muda wa kulala ulipofikia kila mmoja alielekea chumbani kwake, namimi nililala zangu asubuhi palipokucha, kaka alinigongea mlango na kunambia kwamba anaenda kumtafuta Chiba kwa mara ya mwisho asipompata siku hiyo bhasi anaachana na utafutaji huo.
Mimi nilimsapoti kwa wazo hilo la kutaka kuacha kumtafuta Chiba kwani nilijua ndo salama ya mpenzi wangu kuwa salama, kaka alipoondoka tu na mimi nilimtafuta Chiba, aliniambia hayupo nyumbani kuna mishe kaenda kukimbiza ila mchana atakua amerudi hivyo atanishtua ili niende, nilikubali niliamua kutoa manguo na kuanza kuyafua ilipofika saa tano nilikua nimemaliza, nilimuuliza kaka kama atakula mchana alinijibu hatorudi hivyo niliona uvivu kupika nikaenda banda la chips nikajinunulia chips yai na kurudi nyumbani, nilikula nilipomaliza nilisikia mlio wa meseji kutazama vizuri, ilikua meseji kutoka kwa Chiba akinitaka nipendeze halafu niende kwake kwani siku hiyo alikua na mpango wa kunitoa, nilifurahi sana mitoko kwa wanawake ni vitu vilivyopo moyoni kabisa.
Nilivaa na kupendeza, nilikamia haswaa, nilienda mpaka nyumbani kwa Chiba, nae aliingia bafuni kuoga aliporudi nilimchagulia nguo nzuri kabisa ambayo akivaa nilijua atapendeza sana, tulivaa tukajisaminisha tuliona tuko sawa kabisa.
Mlango ukaanza kugongwa hodi. Chiba alipofungua mlango alikutana na mwanaume amemshikia bastola.
“Jackson leo tunaondoka wote, umejificha sana kwa muda mrefu leo sitokuruhusu uendelee kujificha zaidi, toka nje” mwanaume huyo aliamrisha huku akimwita Chiba jina la Jackson.
Chiba alitii na kutoka nje nami nilitoka nje, nilishangaa kumwona kaka akiwa na watu hao, nikaunganisha doti kwamba mwanaume ambae alimshikia bastola mpenzi wangu Chiba ndie kaka ake, lakini maswali nilijiuliza kwanini amshikie bastola na kumshinikiza aingie kwenye gari, wakati huo kaka alikua amenitolea macho makali yenye maswali mengi kwa kuniona natoka kwenye geto la msela, kaka aliamua kupisha kwanza watu hao waondoke na ndugu yao ndipo mimi na yeye tukahojiane vizuri nyumbani.
“Naona umeniwinda mara nyingi sana kuniua leo ndo umenipata naiona furaha yako mpaka jino la mwisho” Chiba alifungua kinywa chake na kuzungumza.
“Hahahahaha siawahi pata furaha hata mara moja, nilijua ukiondoka nyumbani nitapata furaha lakini wapi, wazazi wamekua wakikuulizia mara kwa mara na siku zinavyokwenda wamezidisha hiyo hali nimeamua nikutafute ili nikuue kabisa, ili mimi niwe mrithi pekee wa zile mali hahaha” kaka wa Chiba aliongea kauli yake hiyo na kuiweka vizuri bastola yake, Chiba alikua kageukia upande akilitazama gari hivyo hakuona kitendo ambacho ndugu yake alitaka kumtendea, kabla hajafyatua risasi, mimi niliwahi na kumkumbatia Chiba kwa nyuma, risasi ilitua mgongoni mwangu, nilihisi kuvuta pumzi kwa shida nguvu zikaanza kuniisha nilishindwa kumshikilia Chiba nilikwenda chini moja kwa moja.
SEHEMU YA 19 + 20
“Lauuuuuuuuuuuuuuuu” Kaka aliniita kwa nguvu, huku akimfuata kaka ake Chiba walikamatana kwa nguvu, walishindana nguvu huku kaka wa Chiba akitaka kufyatua risasi kumuua kaka, risasi zilikua zinapiga pembeni mpaka bastola ilipoishiwa ndipo alipigwa mpaka kukaa chini kwa upande wa Chiba nae alimzidi nguvu mlinzi mmoja wa kaka ake.
Polisi walifika kwa haraka walimkamata kaka ake Chiba na mlinzi wake.
Chiba na kaka waliniingiza kwenye gari kwa lengo la kuniwahisha hospitalini, gapo nilipoteza ufahamu nilikuja kuzinduka baada ya siku nne, nilifungua macho na kutazama sikua eneo la hospitalini bali nilikua kwenye chumba kikubwa chenye vitu vingi, chumba kama hiko sikuwahi lala tangu nazaliwa, nilijifinya shavu kujua kama nipo duniani au nipo mbinguni kwani sikujua hapo nimefikaje fikaje mara mlango ulifunguliwa aliingia Chiba akiwa na bakuri la mchesho wa nyama, ndizi na viazi, mwonekano wake ulikua tofauti, nywele zote alizokua kasokota aliziondoa, zilibaki nywele fupi ambazo alizichana vizuri na zilikua zinang’aa kwa black, nilijikuta natabasamu tu kwani mwonekano huo ndio ambao nilikua natamani siku moja awe nao Chiba wangu.
“Oooh umeamka malkia wangu, ni bora umeamka maana nilikumiss sana” Chiba aliongea huku akikaa pembeni yangu hakuishia hapo bali alinibusu kabisa.
“Chiba niko wapi hapa?” Nilimuuliza
“Shiiiiiiiiii hapa niite Jackson sio Chiba tena sawa”
“Sawa Jackson niko wapi hapa?”
“Tupo kwetu, hapa ndipo wanapoishi wazazi wangu, nilizaliwa hapa na kuishi miaka kadhaa ndipo niliingia mtaani, nilikudanganya kidogo kuhusu historia ya maisha yangu, ukweli ni kwamba naitwa Jackson Malanda, niilisoma mpaka kidato cha sita ndipo ambapo nilikutana na msala wa kufukuzwa kwetu sababu ya kufukuzwa ni kaka yangu wa kambo yaani kazaliwa na mama mwingine, kaka angu aliiba pesa nyingi sana na kumpelekea mama ake na humu ndani alitengeneza mazingira kwamba mimi ndo nilichukua kwakua baba yangu hakupenda mtoto mwizi hata siku moja akaamua kunifukuza nyumbani, niliomba mara nyingi nirudi nyumbani lakini baba aliweka ugumu kabisa, niliingia mtaani kujitafutia na mara nyingine mama alikua ananitumia pesa za matumizi kwa siri sana ndio maana niliwahi mlipa Boss wako Samir.
Millioni tatu tena bila mawazo yoyote yale, kwasababu pesa nilikua napewa na mama, matumizi ya bhangi na sigara ni kutokana na maisha ya mtaani yalinibeba ila sasa nitajitahidi kuacha kabisa uvutaji wa chochote.
Kaka angu Jofrey amehukumiwa kifungo cha miaka thelathini jera kwa kutaka kuniua ili aweze kurithi mali zote za wazazi, ilivyokua bahati yangu wazazi wamenipa mali zote na mimi ndo msimamizi mkuu wa mali hizi, na kaka yako nimeshampa kitengo kwenye moja ya kampuni ninazoziongoza.
Tutafunga ndoa na kuendeleza maisha yetu, kama ulinipenda katika hali ile huwezi shindwa kunipenda katika hali hii, pia uliyaokoa maisha yangu nakupenda sana Lauryn wangu.
Tulikumbatiana kwa furaha na huo ukawa mwanzo wa miaka mingi ya furaha kati yangu mimi na Mhuni wangu Chiba au Jackson. Mwenye karamu ni mimi mwandishi wako Doctor Hisia, naamini umeburudika sana ahsante kwa kusoma mpaka hapa na Mungu akubariki sana, tukutane kazi inayofuata kwangu ni kazi juu ya kazi.
**MWISHO**

