MUHUNI PIPI YAKO NITAIWEZA KWELI?
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
SEHEMU YA 11
“Unanipenda kweli au unataka kuwa na mimi sababu waganga wamekuambia ukiwa karibu yangu tutakua na pesa nyingi” nilimtandika swali.
“Haki ya mungu nakupenda mimi, huuu moyo wangu ukiupasua pasua unamkuta Laurina kajaa vyumba vyote vyote, nikubalie Laurina wangu jamani mimi nateseka mwenzio” Boss Samir aliongea kwa matamshi ya kilevi, niliwaza kidogo maneno ya kumpa ili nisiharibu kazi na mimi nisijisikie vibaya kwani ndani ya moyo wangu kulikua na mwanaume mmoja tu ambae ni Chiba hivyo kumwongeza na Boss Samir ningekua najidanganya mwenyewe na jambo lingine sikuwahi tamani kuolewa na mwanaume mshirikina kama boss Samir kwani watu hao huthamini mali kuliko chochote haoni shida kukutoa kafara ili mambo yake yote yaweze kwenda vizuri.
“Sasa sikia boss, uhusiano wowote wa kimapenzi huanza kwa urafiki ndipo mnahamia kwenye hatua nyingine, urafiki husaidia kufurahia upendo wenu, kwakua hili jambo sikuwahi fikiria utaniambia, nipe muda nikuzoee kwanza huko mbeleni tutaona tutakwendaje sawa” nilimjibu kisiasa hiyo inaitwa kuuma na kupuliza, sikutaka kupoteza kazi yangu bhana, akili kali ilibidi itumike hapo.
“Sawaa mimi sina shida nakupa muda unifikirie ukiniridhia utanyonya sana maisha kwenye hii dunia, mwaaaaah nakupenda” Boss Samir alinipiga busu halikua la kugusanisha midomo bali aliweka mkono wake mdomoni mwake alipiga busu na kuniwekea shavuni, nilikwazika ila sikua na jinsi, alinipatia laki na hamsini eti myingine kama pongezi ya kumjibu vizuri kwani wangekua wadada wengine labda wangemshushia mvua ya matusi, mimi niliishia kucheka tu na kuichimbia pesa yetu mfuko wa pochi hapa ndipo ilipo tofauti kati ya wanaume na wanawake.
Sisi wanawake kuna mazingira unaweza pata pesa kwa urahisi sana kama nilivyopata kwa boss Samir ila kwa wanaume pesa nyepesi haipo, kila pesa ni lazima ukimbizane nayo kwa damu na jasho, wakati mwingine wanatumia nguvu nyingi ila malipo ni kidogo sana, haya tuachane na hao wanaume tuendelee na mimi.
Nilitoka hapo bar na kutembea kuelekea nyumbani kwa upande wa boss Samir alirudi ofisini na kupanda gari lake na kuondoka zake.
Niliamua kutembea kwani sikutaka kupunguza hata mia kwenye hiyo laki na hamsini, nilishaipigia mahesabu kabisa ila wanawake na mahesabu mmmh hatari.
Nyumbani hakukua mbali sana hivyo niliona itakua rahisi kutembea na kufika haraka tu.
Mwendo wa dakika kumi, niliona gari limepiga breki ya nguvu mbele yangu, walishuka wanaume wawili walioshiba miili vizuri, nilijikuta na duwaa.
“Wewe sindo Lauryn, kaka ako nilimfumania na demu wangu Sharifa akajifanya mjanja kunitoroka hivyo sasa, tunakuchukua mpaka ajilete tumalizane nae ndipo tutakuachia sawa” mwnaume mmoja aliniambia kuhusu uwepo wao kumbe ni kuniteka, weee usinitanie nikaanza kukimbia walinikamata kwa nguvu na kunirudisha nilijitahidi wasiniingize ndani ya gari kwani nilijua nikiingia tu nimeisha, niliomba msaada ila watu waliogopa kusogea.
Nilianza kulia kuomba watu hao waniachie.
“Nyie madem mbona mnamvuta hivyo mwanamke mwenzenu” sauti nzito ilisikika kutoka nyuma yangu.
Alieongea alionesha dharau kubwa kwa watu hao mpaka kuwaita madem angalau nilipata tumaini la kusaidiwa.
SEHEMU YA 12
Chiba alifika mahali hapo nilimtizama kwa macho yenye kuhitaji msaada.
“Hahaha hahaha wee mtoto wa mama bhange za mia tisa nd’o zinakufanya unaweza kuupiga ulimwengu, ngoja nikufundishe adabu” mwanaume mmoja aliniachia na kumsogelea Chiba huku akipiga piga kifua chake.
Chiba hakufanya mambo mengi aliukamata mkono uliorushwa na jamaa, kisha alimpiga banzi moja tu jamaa alikwenda chini mzima mzima, alipotaka kunyanyuka alienda chini tena, mwenzake aliniachia na kutaka kumshambulia Chiba lakini aliekua chini alimzuia akimaanisha hatari, walinyanyuana na kuingia kwenye gari.
Waliwasha na kuondoka mahali hapo kwa mwendokasi wakishindwa kunikamata kabisa.
Nilimkimbilia Chiba nikimwona mwokozi ambae aliniokoa dhidi ya mambo mabaya ambayo yalitaka kunikuta alinituliza kwa kunikumbatia aliniambia nisilie kabisa kwani nipo mikono salama, tuliondoka taratibu, alinisindikiza mpaka karibu na nyumbani kwetu tuliagana kwa makumbatio na mabusu ya hapa na pale mimi niliingia nyumbani na yeye alielekea kwake.
Nilimkuta kaka amechangamka hata ameweza kupika nilimpa pole kwani alijikaza kupika wakati alikua mgonjwa, akaniambia yeye ni mwanaume anajikaza.
“Hata hivyo mbona nilitoka nikaingia barabarani kutafuta mia mia ili niishi”
“Kaka jamani sasa mimi mdogo ako si nafanya kazi, muda mrefu sana ulikua unanisaidia saivi uko mgonjwa lazima upumzike nami nikusaidie kaka angu, nafanya kazi mimi usisahau hilo”
“Ni sawa mdogo angu unapiga kazi lakini mimi ni mwanaume natakiwa kuwa na pesa hata kama sio za sasa huko mbeleni zitahitajika sana, huu mwili wangu nikifikisha miaka sitini sitokua na nguvu tena kama nilizonazo sasa, lazima nipige kazi ili muda huo ukifika nipate kupumzika”
“Nakubaliana na wewe ila jali afya yako kwa wiki chache ukipona utakua vizuri halafu huko nje sio salama kaka, kuna watu wanakutafuta leo ilikua kidogo nitekwe asingetokea mtu kunisaidia ujue nilishakwenda” nilimwelezea kaka kila kitu kilichotokea.
kaka alisikitika sana kwa jambo hilo japo aliniambia kwamba wametangaza vita ama zake ama zao popote atakapokutana nao ni lazima moto uwake, nilijitahidi kumtuliza kaka aachane na mawazo hayo mabaya ya kupambana na wale watu ambao walionekana ni wenye nguvu, kaka alinikatalia kata kata na kunambia kwamba ni lazima akiwashe mtoto wa kiume ni vibaya na aibu kuogopa vita.
Mwenzenu nilijitahidi wee lakini kaka angu alinizidi kwa ubishi nikaona ni kheri nikubaliane na hilo swala kwani vita ya ubishi nisingeshinda, nilimtaka tu kuwa makini, pia nilimkumbusha kwenye maisha yangu ninae yeye tu ninae mtegemea. Maisha ya kaka angu yalikua hatarini akiwindwa na huyo mwanaume wa Sharifa, mapenzi wakati mwingine ni uadui.
SEHEMU YA 13
Siku tatu zilipita pasipo kuonana na Chiba, tulikua tukiwasiliana tu kwenye simu, kwa upande wa ofisini kazi zilikua zinaendelea kama kawaida ila changamoto ilikua kwa Boss Samir akinisumbua nimpe majibu yake ya upendo wangu kwake, nami nilikua namzungushs zungushs nilifanya hivyo ili siku atakayonipatia mshahara ukichanganya na pesa alizokua ananihonga, nimkatae najua yeye atanifukuza kazi na muda huo nitakwenda kuanzisha biashara yangu mwenyewe, mpango huo niliuchora vizuri akilini mwangu kwani niliamini kuwa na chakwako ni muhimu zaidi kuliko kujishikiza kwenye kazi ya mtu mahali ambapo unakutana na kila aina ya manyanyaso.
Nikiwa kazini nilipigiwa simu na kupewa taarifa kwamba Chiba amekamatwa na yupo kituo cha polisi, nilimuuliza yule askari ni kosa gani amelifanya Chiba mpaka kukamatwa, yule askari hakujibu zaidi ya kuniambia kama nataka kumsaidia Chiba niende kituo cha polisi na huko nitajua kila kitu kuhusu kesi inayomkabili Chiba, niliwaza akilini mwangu haraka haraka ni kosa gani ambalo atakua kalitenda Chiba wangu, nikajua litakua kakamatwa na bhange kwani nilijua Chiba hana biashara nyingine yoyote inayomuingizia kipato zaidi ya kuuza bhange na nilikua kwenye mpango wa kumwambia aachane nayo, kama unavyojua kwenye kumbadilisha mtu tabia unapoingia kwenye maisha ya mtu hutakiwi kwenda haraka haraka kwani ataona kama unampangia au unataka kumpanda kichwani, hilo sikutaka kuliruhusu nilitaka twende taratibu, kabla ya kufikia kwenye hatua nzuri Chiba anakamatwa, iliniumiza ila niliazimia kumsaidia mpenzi wangu.
Niliingia ofisini kwa boss kwa lengo la kuomba ruhusa.
“Boss nimepigiwa simu shangazi ni mgonjwa sana kawaishwa hospitalini naomba ruhusa niwahi mara moja nikamwone” nilidanganya kidogo ili nipate ruhusa ya haraka haraka.
“Pole sana, twende wote tukamwone shangazi” Boss Samir alitaka kufakamia safari.
“Hapana boss utakuja kumwona tu badae au kesho ngoja kwasasa niwahi kwenda kwanza nitakupa taarifa zote” nilimkataa kiania.
“Sawa shika hii elfu sabini kama mchango wangu kwenye hayo matibabu ya shangazi”
“Ahsante boss ubarikiwe sana, kwaheri” nilipokea pesa ya Boss Samir na kutoka ofisini kwa mwendo wa haraka, nilisimamisha boda ilinipeleka mpaka kituo cha polisi cha kati.
Kabla ya kuingia ndani nilipata wazo la kumpigia Afande Michael, majibu aliyonipa yalinikatisha tamaa kabisa.
“Wewe unapenda kusaidiwa tu, ila kutoa aah, ukitaka msaada wangu tukutane gesti tufanye yetu, halafu huyo mtu wako tutamtoa hata badae, kwanza jera sio kaburi kwamba akiingia hawezi kutoka milele, njoo nijilie vitu vyangu namimi nifanye kazi yako” Afande Michael alinijibu majibu hayo, niliamua kukata simu sikuona kama nitaweza kupata msaada wowote kutoka kwa mtu huyo, kwani alitaka kunila ndio anisaidie, niliingia kituo cha polisi, nikajitambulisha jina na mtu niliemfuata mahali hapo.
“Aaah kumbe ni lile lijambazi lililopiga manesi kama lile bila laki tano halitoki hapa bora akafungwe” askari aliekua kaunta alihitaji rushwa kweupe bila hata kificho, nilijitetea kwamba nna laki tatu, askari walinikatalia kata kata kwamba kama nina pesa yote ndipo watamtoa.
Niliomba nimwone kidogo napo walinikataza, nilitoka nje kama mtu niliechanganyikiwa sikujua ni wapi nitapata laki mbili za kuongezea ili nimtoe Chaba nje.
SEHEMU YA 14
Nilichekecha kichwaa nilifikiria nani wa kumpigia simu haraka haraka na kunipa pesa nilimuwaza kaka Wille, nilikumbuka ni wiki hajafanya kazi yoyote, nikajua nikimwomba nitamwongezea stress za bure kaka angu, msaada pekee nilioona ni kumpigia Boss Samir.
“Boss samahani nimefika hospitalini hali ya shangazi sio nzuri kabisa, wamemwingiza ICU na huko anatumia oksijeni kuna kiasi cha pesa kinahitajika hapa kama laki tatu najua mwisho wa mwezi haujafika ila naomba unikopeshe hiyo pesa ili niweze kunusuru maisha ya shangazi yangu, halafu utanikata kwenye mshahara wangu”
“Haina haja ya kukukata huyo ni shangazi yetu wote kama nitashindwa kukusaidia wakati huu ni muda gani nitakusaidia nakutumia laki tatu na nusu ili shangazi yetu apone” Boss Samir alionesha kunijari sana kwani alinitumia kiasi hiko cha pesa, namna alivyonijari alistahiri kupendwa upendo ule mzito kabisa, ila kwangu kila nilipojitahidi kumpokea angalau kumpa hisia nusu za kumpenda nilijikuta nashindwa kabisa kufanya hivyo, moyo wangu ulikua kwa Chiba ambae haishiwi matatizo ila huko huko ndipo ambapo nilipenda mazima nilikwenda kibanda cha wakala nilitoa pesa yote kwenye simu.
Nilirudi tena kituo cha polisi. Polisi walinieleza kwamba faini imezaa kwakua nimechelewesha kuileta hawataki tena laki tano, wanataka laki sita, mimi bila mawaa nililipa hiyo pesa yote waliyotaka, ndipo walimwachia Chiba, tulipanda pikipiki mpaka nyumbani kwake, nilipika chakula, tulikula, baada ya hapo alitaka kunivuta kitandani, mimi nilipinga swala hilo nilimwambia kwamba kabla ya kufanya chochote kwanza anieleze ilikuaje akawapiga hao manesi, kwanza alicheka sana na kunijibu.
“Unajua nilikua kwenye mitikasi yangu huko kitaa, kama unavyojua nakatiza mtaa kwa mtaa ili mkono uzame kinywani, sasa kuna mtaa mmoja nilikatiza nilimkuta mtoto mmoja wa mtaani, dogo alikua kalegea sana nikamchukua mpaka banda la mama muuza, hapo nikamchapa wali nyama wa buku mbili na maji ya baridi ila dogo alishindwa kula kabisa nilipomuuliza nini shida, dogo akanichana kwamba anajisikia kuumwa, nikampima joto kweli mtoto alikua na joto kali, nikamchukua mpaka hospitali moja ya serikalini, kufika pale tukakaa foleni, subiri wee, subiri na wewe muda ukazidi kuyoyoma, kilichonikera sana ni kwamba dogo alikua kazidiwa halafu kuna hao manesi walianza kuwaruhusu ndugu zao wakamwone daktari wakati wamefika kwa kuchelewa hapo ndipo wakakijua kichaa changu, niliwafokea na kuingia na dogo kwa nguvu kwa daktari, ile natoka manesi si wakaanza kucheka kinafki huku wakinitupia maneno ambayo sikufurahishwa nao, hapo nikawaonesha wao ni wanawake na mimi ni mwanaume, niliwapiga mabanzi mazito, wakazimia, walinzi wa hospitali walinikamata na kunipeleka polisi, kwahiyo mchezo ulikua hivyo tu, sikutaka noma wao ndio walileta noma” Chiba alifunguka kila kitu, mimi nikakumbuka uzani wa mabanzi yake nikajua ni haki hao manesi kuzimia maana sio poa, Mhuni wangu alikua anapiga hatari ila kwangu tu ndio nilikua kiboko yake.
“Sasa baba angu siku nyingine upunguze hasira kuna watu wanatembea na magonjwa yao wanatafuta pa kufia, wewe ukimpiga hivyo unamsindikiza kaburini moja kwa moja, punguza hasira sawa mpenzi” nilimwelekeza kwa kumbembeleza ili anielewe vizuri, sauti yangu ilikua na utamu wake, kijana akakubali kwamba atafanya hivyo chezea mimi kubwa la maadui, eti si akaanza kuniita kitandani, nikacheka kwanza.
“Niko danger utaitwa baba bure em ngoja niwahi nyumbani mie” nilimjibu na kuanza kukusanya vitu vyangy nilikua siku za hatari nikiruka kidogo tu imoo.
“Aiiiiii jamani sawa bhana unaniacha na hamu zangu, siku nikikukamata utajua ani”
“Kwendraaaa si hata mimi huwa nakushinda kwenye vita ya kitanda unaugumia mwenyewe muone” niliondoka kwa kukimbia baada ya kumwona anataka kunikamata, mapenzi raha nyie, hasa umpate anaekubali kurudi na wewe utotoni hahahahaha.
SEHEMU YA 15
Nilirudi nyumbani na kumkuta kaka angu akiwa mwingi wa furaha kweli kweli, nilimuuliza kuna siri gani juu ya furaha hiyo, kaka alinijibu.
“Mdogo angu kuna madili mtu unaweza kukutana nayo, ukiyatazama kwa ukaribu utaona ni Mungu ndie kakuletea moja kwa moja” kaka aliendelea kujenga shauku ndani yangu.
“Kuna nini kaka si uniambie unataka niweuke jamani kwa hiyo hamu”
“Sikiliza mdogo wangu angalia hii picha, huyu dogo anatafutwa na wazazi wake kwa nguvu zote, tena huyu dogo anatokea kwenye familia ya kishua, nilikutana na kaka ake akaniambia kama nitafanikisha kupatikana kwa mdogo wake bhasi atanipa millioni tano hapo hapo, si baraka hii mdogo angu” niliipokea picha kutoka mkononi mwa kaka angu, picha ilikua na wanaume wawili wote walikua na sura zenye kufanana kwa kiasi fulani japo mwingine alionekana kuwa mkubwa na mwingine ni mdogo, nilikaza macho kwenye hiyo picha kwa wanaume hao waliokua wamevalia suti za kufanana.
Mwanaume mdogo sura yake ndio ilinifanya nitazame zaidi picha hiyo kwani hakua mwingine bali Chiba wangu, nilistaajabu mambo hayo.
“Vipi dogo mbona unaangalia sana au jamaa unamjua nini, kama unamjua sema tupige pesa chap chap, tukimbie umaskini kuishi na umaskini sio sifa nzuri mdogo angu” kaka alinitandika swali.
“Ha hapana kaka sizani kama nimewahi kumwona ila nikimwona tu nitakwambia, lakini mgao wangu utakua sh ngapi sasa hapo hahaha”
“Aaah dogo ushaanza kuwaza mambo ya mgao wakati kazi ya watu hatujaifanya, haya nitakupa millioni moja na mimi nitachukua moja halafu hizo tatu zitatumika kwa matumizi muhimu ya haoa nyumbani, hapo imekaa vizuri sindoo”
“Imekaa vizuri mno ngoja niingie kazini” tulikubaliana na kaka kuifanya kazi hiyo ya kumtafuta mtu ambae nilikua najua ni Chiba, kwa wakati huo sikutaka kumchoma Chiba wangu kabla ya kuongea nae.
Siku hiyo ilipita, siku inayofuata sikwenda kazini nilimdanganya boss Samir kwamba nitakwenda hospitalini nae alinikubaria nakuniaga kwamba alikua na safari ya mara moja ya kuelekea India ambapo atakaa wiki moja hivyo wiki hiyo nilikua huru kufanya mambo yangu, kalikua kama kalikizo flani hivi, niliruka ruka sana kwa taarifa hiyo nzuri.
Nilipika chai baada ya chai tu, kaka aliondoka kwenda kumtafuta Chiba na mimi niliondoka kuelekea nyumbani kwa Chiba, nilimkuta, alinipokea kwa furaha, tulidendeka kidogo, makubaliano yakiwa tusifike kwenye mchezo husika kwani tutaitwa wazazi siku sio nyingi, halahala tukajikuta tuko kitandani tukisakata sebene, tumefikaje, mimi sikujua kwani nilizidiwa sana, kiufupi sikujitambua, nilinuna kwa kiasi flani kwanini anifanye na nipo kwenye siku za hatari nilimtaka akaninunulie P2 alinizuia na kuniambia kwamba anataka kuzaa na mimi ndio maana amenifanya, nilimwuliza vipi kuhusu nyumbani kwetu, alinijibu yupo tayari kuja kunitolea mahari na kila kitu ili aweze kunifanya mkewe wa maisha, nilifurahi sana kwenye kilele cha furaha hiyo, nilimchapa swali nilitaka kujua ni ipi historia ya maisha yake nae alikua tayari kunieleza kila kitu kuhusu yeye.
Inaendelea………….

