MUHUNI PIPI YAKO NITAIWEZA KWELI?
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
SEHEMU YA 1
Nilikua zangu chumbani nimejifungia mawazo tele, sikua na hamu ya kufanya chochote wala kuingia kitu chochote mdomoni mwangu, unajua kwanini kwasababu sina kazi, nimemaliza chuo nipo tu nyumbani sina cha kufanya, bahati mbaya sikujua kusuka wala kushona kwa cherehani kibaya zaidi hata biashara sijawahi fanya kabisa kwenye maisha yangu, nilikua nimejiinamia mwenyewe niliona dunia yote inataka kuniangukia, sikuona mwanga wala pa kutokea kabisa.
“Weeee Lau weee Lau mpaka muda huu bado umelalala tu emu amka” nilisikia sauti ya kaka ikiniita nitoke, nilijivuta kutoka kitandani na kutoka nje, nilimsalimia kaka huku nikifikicha macho yangu.
“Mbona unalala sana mdogo angu, vipi umepika chochote humu”
“Hapana kaka, sijapika”
“Duuuh uko salama kweli?” Kaka aliniuliza huku akinitazama tumboni ni kama mtu ambae alitaka kuhisi kama nina mimba au laa.
“Unachohisi kaka hiko mimi sina, sina mimba ila nna mawazo mengi”
“Hebu kapike kwanza wakati wa kula tutaongea, chukua buku mbili pale mezani kanunue samaki wa mafungu” nilimkubalia kaka kama kawaida nikaenda gengeni, nilinunua samaki niliporudi niliwapika kisha tukakaa mezani mimi na kaka Wille, alikua kaka angu pekee na mtu pekee ambae nilikua nae kwenye familia yetu, kwani wazazi wetu wote walikua wameshafariki miaka mingi iliyopita hivyo kaka alinilea kwa kiasi kikubwa.
“Una nini nieleze?” Kaka aliniuliza.
“Kaka kinachoniumiza hapa ni kukosa kitu cha kufanya, nimezunguuka kwenye mainterview na maofisi ya watu mpaka sasa sijapata kazi, kwa umri huu sitakiwi kuomba sabuni ya kuogea kutoka kwako ni aibu kaka hiki ndicho kinaniumiza” nililalamika.
“Pole sana mdogo angu lakini ukumbwa ndio ulivyo najua umekujia bila taarifa lakini ni lazima ukubaliane nao, ukiona kazi umezikosa ujue Mungu anakutengenezea ile iliyo yakwako usipunguze imani.
Hata hivyo kuna kazi nimekuombea huko kesho mapema nitaenda kukukabidhisha”
“Kweli kaka?”
“Ndio mdogo angu ni kazi ya kukatisha tiketi za mizigo muhimu kuwa mchapakazi na kufungua moyo kazi za watu zina mambo mengi sana” nilimkubalia kaka kwamba nitaifanya kazi hiyo kwa moyo wote kwani nilikua na shida ya kazi haswaa, nilimkumbatia kaka angu na kumwambia yeye ni kaka bora kuliko kaka wote duniani, siku iliyofuata asubuhi na mapema tuliamkia ofisini hapo aliponiombea kazi alinitambulisha kwa huyo boss mmoja mwenye asili ya kihindi ila ni mbongo anaitwa Samir, yule boss alinitazama juu mpaka chini na kuniuliza.
“Hivi wewe utaweza kweli kazi ya hapa” nilimjibu ndio nitaweza.
“Mmh sawa ngoja tuone, kazi umepata kama sehemu ya majaribio tuone uwezo wako” nilifurahi moyoni huku nikisema kwamba nitamuonesha huyo mhindi uwezo wangu wa kujituma kaka aliondoka na kuniacha hapo.
Majira ya saa tatu hivi liliingia gari lililokua na mzigo wa vyombo ambao ulitakiwa kusafirishwa mkoani, wenye mzigo waliukabidhisha, walilipa pesa na wao kuondoka zao.
“Huu mzigo hautaondoka leo kwani magari yameharibika hivyo tuupeleke stoo halafu kesho utasafirishwa” boss aliongea nilitazama boksi lenye mzigo niliona mzigo huo utakua mzito kuubeba kwani walioingiza ndani ya ofisi walikuawa
wanaume wawili tena walikua wanaangaika sana kuubeba, nilitamani kumwambia boss si awaite vijana waubebe mzigo huo lakini niliogopa kama utani boss alisimama na kuniambia tuubebe mzigo, yeye alishika huku na mimi kule, nilikaza mikono yangu, nilibeba nilipofika nje kabla ya kufikia mlango wa stoo, mikono iliishiwa nguvu boksi liliangukia vidole vyangu nilipiga ukelele mamaaaa, sauti ya kuvunjika vitu kwenye boksi ilisikika.
Boss bila kunipa pole alianza kunilaumu kwa maneno makali alisogeza boksi kutoka kwenye miguu yangu hapo hapo alilifungua kutazama mzigo wa ndani, kumbe ulikua na vitu vya udongo na vingine vyenye asili ya glass vilikua vimepasuka.
“Umenisababishia hasara kubwa sana lazima utalipa, kampuni yangu haiwezi kubeba hii hasara ya millioni tatu, utalipia na kwambia utalipa” boss aliongea maneno hayo ya kunikandamiza, maneno yaliupa mwili wangu ganzi vidole havikuhisi maumivu tena, nilifikiria kuhusu hiyo millioni tatu ya watu. Nilijikuta nimeanza kulia nikiwaza pesa hiyo nitaitoa wapi mimi.
SEHEMU YA 2
Nilianza kupiga chafya baada ya pua zangu kuivuta harufu ya bhangi pembeni yangu alikua kasimama kijana mmoja kavalia kibukta cha jeans, juu kavalia shati kubwa ila lilikua limekatwa sehemu ya mikononi, kichwa alikifunika kwa bosholi, alikua anavuta bhangi bila hofu ya yeyote, kweli kijana alionekana amepinda ni mhuni kwa ufupi.
“Mbona unalia sister” Mhuni aliniuliza huku akiifinyanga bhange yake kwenye vidole vyake baada ya kugundua kwamba moshi wa bhange ulikua unaniumiza pua. Sikumjibu bado niliendelea kufuta machozi yangu, alinitazama mguuni nilipiga hatua moja nikiwa na chechemea.
“Aah kumbe ni mguu ndio una shida pole sana sister” Mhuni alitoa pole kisha aliinama chini kidogo na kuukamata mguu wangu aliunyoosha kidogo mguu ulitoa mlio ila nilihisi yale maumivu yamepoa.
“Sikia wewe Lauryn kama hulipi hiyo pesa ya mzigo wawatu ulioharibu nakufuta kazi na nakupeleka polisi, utatoka pale ambapo kaka ako atailipa hiyo pesa shenzii” Samir hakuonesha huruma yoyote juu yangu ndio aliendelea kunikandamiza.
“Kwani unamdai shillingi ngapi mbona wee mhindi koko unachonga sana kama mzaramo?” Mhuni alimuuliza boss wangu.
“Wewe nawewe hayakuhusu kama pesa unayo mlipie millioni tatu, sio unachonga chonga na kutaka kuingilia mambo ya watu yasiyokuhusu”
“Oyaa weee usinisemeshe kama hivyo, mimi mnyamwezi halafu nimenyooka kinoma, mbona ngenga nyingi wee kokoro, hebu nipe hiyo namba nikulipe hiyo pesa sio unamzalilisha mwanamke kama ulijizaa mwenyewe kudadadeki” Mhuni aliongea na kutoa simu yake, simu ilikua kitochi kimefunga na mipira mingi sana ambayo ilikua inakishikiria.
Samir alitaja namba yake ya simu baada ya sekunde chache nilimwona anatabasamu nikajua bhasi kawekewa pesa yake ndio maana alikua na furaha vile.
“Unabahati kakulipia bila hivyo ungejuta na ndo siku yako ya kwanza kazini, haya tubebe mzigo tupeleke ndani” Samir aliongea tena kumbe kipengele cha kubeba mzigo kilikua pale pale, nikaona kweli leo siku ngumu sana, nilimshukuru Mhuni japo yeye hakuzingatia sana hiyo ahsante yangu, nilimwona ni mtu mzuri mwenye moyo wa kusaidia watu japo kwa mwonekano wake na kiasi cha pesa alichokitoa ni vitu viwili tofauti yaani mbingu na ardhi.
Nikiwa najiuliza nifanyaje na huo mzigo, Mhuni aliubeba mzigo wote peke ake, kweli alikua na nguvu alimwomba boss wangu amwoneshe ni wapi pa kwenda kuuweka, walienda na boss mpaka huko stoo kisbha walirudi pamoja.
“Sikia wee mhindi, hii nchi nikiwa raisi mimi nyie wote wa ulaya sijui Asia mtarudi kwenu hiyo nikiwa raisi, ila ukitaka urudi kwenu huko leo au kesho bhasi mguse tena huyu mwanamke nikuoneshe show” Mhuni alimchimba mkwara boss wangu huku akiwasha tena bhangi yake, Boss ni kama alikua anamuogopa mhuni huyo asie na jina aliitikia kwamba hatonisumbua tena. Bila kutia neno lingine mhuni aliondoka huku akivuta bhangi yake, mwendo wake sasa ndo utacheka alikua anatembea kwa kudundika kinoma, nilifanya kazi ilipofika jioni ya saa kumi na mbili, niliruhusiwa kurudi nyumbani mfukoni nilikua nimepata ka elfu tano kangu nilikopiga ganja hivyo nilipitia kwenye meza ya kaka muuza kuku za kukaanga angalau ninunue ka paja nikapike tule na kaka angu, nikiwa kwenye kuagiza paja hilo la kuku, nilisikia kelele nyingi za watu.
“Mwiziiiiiiiii mwiziiiiiii huyo huyo kamata mwiziiiiiiiii kamata mwizi” niliporusha macho kutazama aliekua anakimbizwa na wingi wa watu, sikuamini nilimwona yule Mhuni alienisaidia asubuhi kunilipia milioni tatu ndie alikua anakimbizwa na watu hao, nilishika kichwa, nilitamani kumsaidia sana lakini sikujua nafanyaje ili nimsaidie na mimi, niliishia kushika kichwa huku nikizunguka zunguka tu nikichapa chapa miguu nilitamani Mungu afanye muujiza kijana wawatu asiuwawe.
SEHEMU YA 3
“Dada vipi unamjua yule?” Muuza kuku aliniuliza maana hali niliyokua nayo haikua nzuri kabisa nilionesha kuchanganyikiwa.
Sikujibu bali nilipokea kipaja changu cha kuku na kutoka mbio, nilikua nakimbilia kule kule walipoendea watu, baada ya umbali fulani nilisikia kelele nyingi huku watu wakisema.
“Uaaaaaa uaaaaa,pigaaa, pigaaa tia kibiriti huyo amezidi sana” nilihisi mwili wangu unaishiwa nguvu, nilishindwa kusogea zaidi kwani niliona watu wamezunguka duara huku wakimpiga Mhuni, moto uliwashwa nilishindwa kuangalia nikajikuta nalia, sikutaka kushuhudia mtu yule akiuwawa, nililia kwa machozi mengi sana, hakua ndugu yangu wala sikua namjua hata jina ila kifo chake kiliniumiza sana nilitembea kinyonge mpaka nyumbani, nilijikaza na kupika ugali kidogo sana huo ulikua kwaajiri ya kaka, mimi sikutaka kula kabisa, bado kifo cha Mhuni kilikua kinaniumiza sana. Kaka aliporudi nilimtengea chakula, aliponiuliza kwanini mimi sisogei kula wakati ni kitu cha kuku, mboga ambayo nilikua naipenda sana nilimwambia sijisikii kabisa kula, aliponitazama aliniona machozi mepesi yanatiririka usoni mwangu akanikandamiza kwa maswali nikajikuta namjibu tu kilichokua kinaniumiza nikamweleza kilichotokea kazini mpaka kifo cha Mhuni, kaka alinituliza akaniambia kwamba huenda ni malaika wa Mungu alikuja kuniokoa dhidi ya lile deni kubwa kisha akaondoka zake kurudi mbinguni.
Maneno ya kaka yalikua ya kufikirika ila kidogo nilimwelewa, tuliagana na kwenda kulala kila mmoja, asubuhi ilipoingia niliwahi kwenda kazini kwanza nilifanya usafi na kuweka mazingira yote vizuri, boss akaja tukaendelea na kazi pale, uliletwa mzigo wa kitanda ambao ulitakiwa kusafirishwa kwenda mkoani.
“Lau mwenye huu mzigo bado hajaja, halafu mimi nina safari ya kwenda benki hakikisha mwenye mzigo akija akuachie elfu thelathini ukitoza chini ya hapo mimi sitisafirisha huo mzigo labda uongezee hiyo pesa” Boss aliongea na kuondoka zake baada ya dakika tano alifika mbaba mmoja mwenye kitambi cha kupakata, nilimsalimia shikamoo nae aliitikia nikajisemea kweli huyo mbaba anauthamini ubaba wake kwani wangekua wababa wengine wangegoma kuitikia kwa madai ya kwamba nawasalimia ili niwanyime nini.
Baba huyo aliniulizia juu ya mzigo wake, alinioneshea visibitisho nami nilimtajia bei ya kuulipia mzigo huo ambao ulitakiwa kusafirishwa kwenda mkoani Singida, mimi nilimtajia elfu themanini, bei ya juu zaidi. Yule baba bila kuhoji wala kulalamika aliitoa pesa hiyo nami nilimwandikia risiti yenye namba ya mzigo wake, alishukuru na kuondoka nilitenda elfu thelathini ya boss na elfu hamsini pembeni, nilikua mwenye furaha sana, nilichukua elfu kumi na kumpatia mzee mmoja ambae alipita ofisini kuomba pesa ya matibabu ya figo.
Boss Samir alipofika jambo la kwanza kuniuliza ni juu ya pesa yake nami nilimpa elfu thelathini yake hakuamini na kuniambia kwamba alikua ananijaribu tu, uwezo wangu kwani mzigo huo husafirishwa kwa elfu ishirini na tano, boss alionesha kuniamini sana hilo nalo lilizidi kunipa nguvu na kuona mwanga kwenye kazi hiyo.
Ilipofika saa moja usiku niliondoka ofisini baada ya kutembea nilipita kwenye kiuchochoro kimoja nilishangaa sana, nilihisi miguu yangu ikitetemeka kwa hofu baada ya kumwona Mhuni mwanaume ambae niliamini amefariki alikua mbele yangu, alinisogea zaidi nilisimama alinipeleka ukutani alinishika mkono na uso wake ukiwa karibu zaidi na uso wangu.
SEHEMU YA 4
“Mbona unatetemeka sana mama mtu?” Mhuni aliniuliza.
“Wewe si uliuliwa nimekuoona” Niliongea huku nikiwa katika hali ya kutetemeka sana.
“Hahahhahahahahahhahahahahahahahah” Mhuni alicheka sana kisha alinipiga busu la mdomo, nilibaki nimeduwaa, busu lilinisisimua kwa muda, aliniambia
“Mimi sio mzimu bhana na sijafa si unaona nina ngozi kamili, umeamini sasa?”
“Ndi ndio nimeamini, nilijua umekufa niliumia sana jamani mimi aaaaaaaaah aaaaah” machozi mepesi yalinitoka nilijikuta namkumbatia kwa nguvu sana Mhuni sikujua niliona kufanya hivyo kutanipooza uchungu, tulikubambiana kwa dakika kumi ndipo tuliachiana.
“Naitwa Chiba, unaitwa nani mrembo?” Mhuni alijitambulisha.
“Lauryn” nilimjibu, “Sawa naomba nikusindikize kwenye hivi vichochoro inaweza kuwa sio salama kwa upande wako majira kama haya” nilikubali, alinishika mkono na kuanza kutembea nilijikuta niko huru na mwenye furaha kuwa karibu yake, tulipoingia mtaani kwetu aliniaga kwamba anarudi, nilijua kuna jambo moja kasahau nayo ni kubadilishana namba, nilimwomba namba ya simu na kila mtu alielekea nyumbani kwake, nilipika.
Kaka aliporudi alikua na maswali mengi kwangu “Lau kuna washikaji mtaani wameniambia kwamba kuna mwanaume umerudi nae nyumbani, tena mkiwa njiani mlishikana mikono kwa mahaba mazito hiyo tabia umeanza lini mdogo angu?” kaka alinichapa swali zito ambalo lilinifanya nifikirie cha kumjibu.
“Mmmmh mwanaume gani huyo kaka?” nilijifanya sijui chochote alichokiongea kaka kumbe alimwongelea Chiba wangu.
“Acha kutugeuza sisi wajinga, walioniambia hawawezi kukusingizia”
“Kaka jamani aliekwambia ni Sharifa huyo namjua alivyo na umbea mwingi” niliamini Sharifa ndie alituona na huyu mwanamke alikua na uhusiano wa karibu na kaka, nikajua kwenye stori zao walivyoishiwa cha kuongea wakaanza kunizungumzia mimi na Chiba.
“Acha kumsema vibaya Sharifa ninachotaka ukumbuke kwamba ni kweli umeshakua mkubwa na siwezi kukulinda tena, ila umakini ni muhimu sana, kama huyo mwanaume anakupenda si aje nyumbani ajitambulishe ili muwe huru, halafu haya mambo ya kutembea barabarani kujiona kwamba ninyi ndio mnamapenzi sana hilo jambo mimi silitaki kama mna mambo yenu si mkafanyie huko chumbani sio mnatembea barabarani kwa kujiachia mpaka watu wanawanyooshea vidole kwamba mimi ndo nionekane sijakulea vizuri, hebu Lau tusiharibiane CV huko mtaani” Kaka aliongea mambo mengi muhimu na mimi nilikubali kwamba nitayafuatisha mambo yote kwani yeye alisimama kama mzazi wangu na hata laana anaweza kunipa.
Tulikula na kwenda kulala, nikiwa kitandani nilimtumia meseji Mhuni lakini hakujibu, kitendo hiko kiliniuma sana siku tano zilipita nikimtafuta Mhuni wangu hakunijibu wala sikufanikiwa kumwona kitendo hiko kiliniuma sana, nilitamani kumwona hata mara moja lakini haikuwezekana. Ilifikia wakati nilikata tamaa ya kumwona kabisa Chiba jioni moja nikiwa natoka kazini natembea taratibu uelekeo ukiwa nyumbani, mara niliona mtu akinishika mkono pasipo kunisemesha alianza kuniongoza nilipomtazama alikua Chiba, nilimsalimia lakini hakunijibu badala yake alizidi kuniongoza nami nilikubali kumfuata tulikatiza vichochoro na kutokea mbele ya chumba kimoja, alitoa funguo na kwa pamoja tuliingia ndani ya chumba hiko, niliendelea kuwa mtulivu kwakua nilimmiss sana mwanaume huyo.
“Siku ile uliniuliza niliponaje kwenye kifo, nipo tayari kukuelekezea kila kitu kwakua nataka uwe msiri wangu, moyo wangu umebeba mambo mengi sana, nataka uwe sehemu ambayo nitakua natua mizigo yangu yote, kiufupi nakupenda sana Lauryn, wewe ni mwanamke wa ndoto yangu, nakuhitaji wewe mzima mzima kwenye safari ya maisha yangu, wahuni huwa hatupendi mara nyingi ila tukipenda sehemu moja huwa tunapenda kweli” Mhuni aliweka kituo hapo akisubiri majibu yake kutoka kwangu.
SEHEMU YA 5
Sikumjibu chochote zaidi ya kumkumbatia kwa nguvu sana, kwani hata mimi nilimuhitaji sikuona kama kuna maneno ambayo yangetosha kuwasilisha namna moyo wangu ulivyokua unajisikia juu yake nikajikuta namkumbatia tu, nae alinipokea, miili ilikoza joto hakuna ambae aliweza kujizuia katika hilo, nguo zilikua nzetu miilini mwetu tukajikuta tunaziondoa moja baada ya nyingine, burudani ya kitandani ilifuatia, tulipeana raha bila kunyimana eti kwanini tunyimane viungo ambavyo hatukuhusika kuviumba, mimi nilijikuta hoi zaidi baada ya shughuli si unajua tena nilishiriki na mtu aliezindua na kitu cha bhangi hivyo alinipandisha vilima vyote, niliimba nyimbo zote, mhuni wangu alikua anajua sana, alijua kunikata kiu haswaa.
Muda ambao niliibuka kutoka kwenye ulimwengu wa huba, nilisikia simu yangu ikiita, kasheshe ilikuja kwenye kuipokea kwani mpigaji alikua kaka angu, nilipomtazama Chiba usoni yeye alinipa ishara kwamba nipokee simu hiyo.
Nilijikaza na kuipokea, kaka hakunipa nafasi ya kuongea aliongea mwenyewe.
“Weee dogo mimi sitorudi nyumbani leo nitalala kwa washikaji, tukutane kesho usiku ndipo nitarudi sawa” Kaka alinipa taarifa.
“Mmmh kwa washikaji kweli, si useme tu unakwenda kulala kwa Sharifa wako” nilichombeza nilijua tu kaka anaenda kulala kwa mchumba ake Sharifa.
“Heeeeee we mtoto umeshaanza kuniona mimi babu yako eeeh, hahahah kesho uko” Kaka aliongea na kukata simu, taarifa ya yeye kutorudi nyumbani ilinifurahisha sana kidogo niruke ruke kwani hiyo ingenipa nafasi ya kuutumia usiku huo pamoja na Chiba.
“Nitalala hapa au kuna mwenye chumba itabidi aje usiku huu?” Nilimtania kwamba kuna mke mkubwa atakuja kwenye chumba chake.
“Hahahaha acha zako, wewe ndo mama mjengo hakuna mtu mwingine wa kuja hapa kwahiyo kuwa na amani tu mama mtu” sasa alivyokua anaongea kwa sauti yake nilijisikia raha ya ajabu kuna namna kuna ufahari kujua upo peke ako kwenye moyo na maisha ya mtu unampenda.
Chiba aliwasha bhangi yake na kuanza kuivuta, nilishindwa kumzuia kwani angeniona ni mpenzi wa ajabu, siku ya kwanza tu tayari nimeanza kumpa sharia nyingi, moshi ulinizidia na kuanza kukohoa, alinipa pole kisha alitoka nje kuvutia huko alikaa dakika kumi alipotosheka ndipo alirudi ndani.
“Enhe niambie siku ile ilikuaje mpaka watu wakaanza kukukimbiza na kukuitia mwizi?” nilisogeza swali mezani.
“Aaah siku ile bhana mimi sikuiba wala nini na vipato vyangu huwa sipati kwa kuiba kitu cha mtu na mimi nachukia sana wizi, ile siku nilikua kwenye mitikasi yangu kama kawaida, kumbe kulikua na mwizi wanamkimbiza sasa yule mwizi vaa yake ilikua inafanana na vaa yangu aliwapiga kona kadhaa, walipokutana na mimi wakaniungia mimi bila kujua kwamba mimi si mwizi wao, na mimi sikua kinyonge vichochoro nilikua na uzoefu navyo niliwapiga chenga huko mbele wakakutana na mwizi wao, wakamchoma moto, wakati wanamchoma moto wewe ukazani ni mimi, ndo ilikua hivyo”
“Daaaah pole sana sasa hapo itabidi ubadili mavazi maana wakati mwingine inaweza kuwa hatari kwa maisha yako na mimi sitaki kukupoteza”
“Umeongea kwa uchungu sana, kwasababu ya upendo wako niko tayari kubadilika” Chiba aliniambia nami nilifurahi sana niliona ipo nafasi ya kumfanya mwanaume huyo abadilike na kuwa vile ninavyotaka, tuliamua kulala na tulipoamka siku hiyo tulishinda pamoja, asubuhi chai na vitumbua, mchana ugali dagaa zenye pilipili nyingi hayo yalikua maisha ya Chiba wangu ila kwangu niliyafurahia sana si nilikua kwa mwanaume ninae mpenda sana, ilipofika saa kumi aliniambia anitoe tukaenda mpaka ufukwe wa bahari huko tulikula mihogo samaki baada ya kuenjoy na upepo wa bahari tulipitia maduka ya nguo, Chiba alikua na laki na nusu hivyo tulikwenda kununua nguo zake na zangu, Chiba wangu alivyobadili nguo na kuvaa mpya alipendeza sana, machoni mwangu alizidi kuwa mzuri nilimfurahia sana na kumkumbatia.
Tulitoka hapo na kurejea nyumbani kwake ili aache nguo na yeye anisindikize nyumbani kwetu kabla ya kutoka mlango ulifunguliwa bila hodi waliingia askari wawili walimkamta Chiba kwa nguvu na kumfunga pingu, wawili wengine walianza kupekua walikuta misokoto mingi ya bhangi, walimchukua na kutaka kuondoka nae, niliwalilia na kuwaomba waniachie Chiba wangu, askari mmoja alinijibu kwa nyodo sana.
“Huwa unafurahi sana akikuletea vizawadi vya nguo na mazaga mengine kwa kuuza hivi vitu haramu, ukimtaka mpenzi wako utakuja kituo cha kati hatuna muda wa kujibizana na wewe, ukizingua tunaondoka na wewe” Askari walimchukua Chiba wangu na kuondoka nae kumpeleka kituo cha kati waliniacha kwenye kilio kizito.
Inaendelea……..

