MAMA ALIVYO MVIMBISHA KORODANI MWANAE ALIEMZAA KWA UCHUNGU
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
Ugomvi wa mama na baba umepelekea familia imejitenga makundi mawili mama yupo upande wa watoto wa kike na baba upande wa watoto wa kiume
Mwanzo tulikua tukipika tunakula wote na kukaa nyumba moja kama familia zingine na tulikua na furaha sana kwakweli Ugomvi wa baba na mama sikuwahi kujua chanzo maana nilikua namuuliza mama hanipi majibu na tena nikimlazimisha hanijibu kuwa nini kilipelekea mpka wagombane tena inafika hatua anakua na hasira sana ananipiga Sana
Kwenye familia tupo wa 5 wakiume wawili na wakike tupo watatu sasa kwa ugomvi ule mama nae alijenga nyumba apo sasa tukawa tunaishi tofauti yaani nakuambia hata maji hatuombani yaani mama alitujaza SUMU sana kiasi kwamba hata upande wa pili mfano kaka aumwe au baba aumwe mama alikua anatukataza kabisa sasa tukawa tunashindana sasa mfano wakiume wakinunua hiki na Sisi tunafanya hivo hivo Ila kwakweli naamini mama ndio chanzo cha ugomvi maana ni mda wote anamsema baba vibaya anamtukana matusi mazito mazito.
Sasa mama alikua ni mfanya biashara tu alikua na uchumi mzuri kuliko baba ambae alikua ni mkulima kwaiyo maisha ya upande wa baba yaani kaka zangu walikua na lishe duni lakini mwanaume ni mwanaume tu maisha ya baba yalibadilika pale alipolima nyanya zikakubali alivouza kaka zangu walibadilika ghafra yaani kila mmoja akamiliki duka na nyumba yao wakaipiga plasta ikapendeza na kubadilisha bati mafanikio hayo sasa mama hakupendezwa nao na hapo mashamba waligawana alichokifanya mama ni Alienda kuchukua dawa kwa Mganga akaenda kuweka dawa kwenye mashamba ya baba ili asipate mazao mengi
Nilishangaa sana japo dada zangu walikua mbele mbele na mama Ila mie kwakweli nilikua natamani nikamsalimie baba na kaka zangu Ila nikawa naogopa sana
Sitosahau hii siku ambayo mama alijua kua kaka yetu ameoa jamani jamani inawezekanaje ubebe mimba miezi tisa unyonyeshe mpka atimize umri wa kuoa uwe na roho mbaya na watoto uliowazaa kwa uchungu nilishindwa kuvumilia nilijitosa nikaenda kumuona kaka maana nilikua naona asubuhi wanamtoa nje wanamuanika juaani harafu mda frani wanamrudisha ndani
Sikuhofia chochote maana Hawa ni ndugu zangu wa damu japo mama alikua hayupo na dada pia alikua hayupo nilimfata baba nikamsalimia pale tukaongea pale mwisho akaniambia kaka yako kaumwa juzi baada ya kuoa yaani ni wiki sasa ndo halo hii imetokea tuliongea mengi sana mwisho akaniambia nirudi ili mama asikukute hapa
Mama alikuja usiku sana akiwa anatukana sana akasema na bado yaani yeye ni wakunizidi mimi atanitambua mimi pekee ndo nilikua siungani naye Ila dada zangu walikua njia moja japo sikuonesha dalili zozote
Kaka aliumwa sana yaani nikawa namuona baba na kaka zangu wanahangaika kumpeleka hospital kwakweli nilikua naumia sana mpka nilipopata mda wa kwenda kumuona nililia yaani inawezekanaje mama amfanyie hivi mwanae wa kumzaa kisa tu ugomvi wait na mumewe yaani nikama madude yale ya wanaume sijui niyaiteje kwakweli yalivimba sana mithiri ya mtu mwenye busha hivi Ila Alienda kufanyiwa opelesheni lakini Hari ile ikajirudia tena sasa nipo hapa sielewi nimueleze tu baba kuwa mama ndo anayafanya haya yote maana pia namuogopa mama kama anayafanya haya kwa mwanae wa kiume je mimi nikijaribu kumuambia baba si ataniua kabisa

