KIBUYU CHA BABU
Sehemu Ya 3
nilisikitika nilipoona mke na mtoto wa marehemu wakilia kwa uchungu huku wakigusa mwili wa marehemu….nikajiuliza inamaana watu wote hawa hawaoni kuwa hiyo siyo maiti bali ni gogo la mti….nilimuonesha mbonde lakinj hakuona kitu chochote…
kaka mkubwa wa marehemu alifunga jeneza kwaajili ya maziko…
baada ya kuzika kila mtu alitawanyika wakabaki ndugu na jamaa wa karibu wa marehemu…kipindi nipo njiani narudi nyumbani nilijiuliza maswsli mengi inamaana kumbe yule mtu aliyeliwa nyama jana usiku alikuwa ni baba wa mwanafunzi mwenzetu. ….nikaingiwa wasiwasi yawezekana hata wazazi wangu babu aliwala nyama..hivyo alinidanganya kuwa waliungulia mdani ya nyumba kwa ajali ya moto!!!!nilikasirika nikamchukia sana babu….
nilizipiga hatua za haraka nikafika nyumbani…nilikaa kama dakika kadhaa hivi kisha nikamuona babu akija kwa hatua zake za kizee..
aliponikaribia alisema amesikitishwa sana na kifo kile kuwa marehemu alikuwa rafiki yake…hapo ndipo nilipogundua kumbe wakiwa kwenye mambo yao ya kichawi huwa hawanioni bali mimi nawaona wao..
babu hakukaa sana tangu alipofika…..aliingia ndani kisha akatoka na kuniaga kuwa anakwenda kwenye kahawa….nilijisemea moyoni babu akitoka tu…itakuwa ndio muda mzuri wa kuingia chumbani kwake nidadisi kibuyu kile…ghafla nikakumbuka kuwa jana niliingia chumbani kwake lakini sikuona kitu hata kimoja yani hata kitanda anacholalia…sijui leo pia itakuwa hivyohivyo?? alijisemea moyoni sudy…
kisha baada ya dakika kadhaa kupita sudy aliamini kuwa babu yake atakuwa kafika mbali…
aliingia chumbani””” lakini leo haikuwa kama jana sudy alikitafuta kile kibuyu cheusi chumbani mule mpaka akakiona lakini aliogopa kukishika kibuyu kile kisha akasema potelea mbali liwalo na liwe akatichukuwa kibuyu kile na kutoka chumbani kisha akaelekea nje…alizunguka nyuma ya nyumba kwa hatua za harakaharaka…wakati anazipiga hatua hizo huku akitazama huke na kule kushoto kulia ghafla alijikwaa kwenye kipande cha jiwe lililokuwa limezama chini ya aridhi na kutokeza kidogo upande wa juu ya aridhi sudy alidondoka chini Tiiiiiii””” alikiachia kibuyu kile ili mikono yake ishike aridhi asijigonge uso wake kwenye aridhi….
kibuyu kilidondoka chini kikafunguka””” kilikuwa kimefungwa na kipande cha kaniki nyeusi.. ghafla. kilianza kufuka moshi”” moshi ule ulitoka kupitia upande wa juu ya kibuyu…sudy aliogopa sana akanyanyuka haraka pale chini…kisha akakimbia hatua kama kumi hivi akasimama na kugeuka kukitazama kibuyu kile….alistahajabu kuona vivuli vya binadamu vikitokea ndani ya kibuyu kile”” vivuli hivyo vilikuwa vingi sana havina idadi….sudi aliogopa sana mapigo yake ya moyo yalianza kwenda mbio…
***********
upande mwingine nako alionekana babu kule kwenye kahawa baada ya kibuyu kile kudondoka kunakitu kilimuingia akastuka sana!!!! akakiachia kikombe cha kahawa kutoka mkononi mwake kikadondoka chini na kupasuka…wale watu wengine waliokuwepo pale kwenye kahawa walistahajabu kumuona Mzee Mkumbo yupo katika hali ile kwani uso wake ulionekana kuwa makini na jambo fulani…kisha alikuwa kama kapigwa na bumbuwazi…walimsemesha lakini hakuwajibu kitu alibaki vilevile kama kapigwa shoti ya umeme…ghafla Mzee mkumbo alisimama kama roboti na kuanza kuzipiga hatua alijitahidi kutembea harakaharaka lakini kutokana na umri wake kuwa mkubwa alishindwa alijikuta anayumbayumba kisha akaendelea kuzipiga hatua zake za kizee””” ukimtazama mzee mkumbo uso wake ulionesha kuwa kunajambo linamtatiza kwa sababu alionekana kuwa na wasiwasi….”””
mzee mkumbo uzee unamsumbua”” au presha imepanda kutokana na kahawa nyingi aliyokunywa leo…ohooo hilo ndio tatizo la kahawa ukinywa nyingi tu..mapigo ya moyo yanaanza kwenda mbio utadhani unakimbia..
maneno hayo aliyasema kijana mmoja aliyekuwa miongoni mwa wale watu waliokuwa wanakunywa kahawa pale .
*******
kule nyumbani Sudy alizidi kuchanganyikiwa alistahajabu vivuli vile vya binadamu vilitoka kwa mfululizo…ghafla upepo uliovuma kwa kasi ya ajabu utadhani kimbunga ulitokea pale kibuyu kilipokuwepo…alipotazama sehemu nyingine hakuona upepo huo isipokuwa pale nyumbani kwao pekee tena ile sehemu ambapo kibuyu kilidondoka.””””,,,sudy aliogopa zaidi alipoona ule upepo unazidi kuwa mkubwa ukivuma kwa kuzunguka!!! kumfuata yeye….sudy alipoona hivyo aliamua kutimua mbio…alikimbia kama kawekewa mota miguuni….nadhani siku hiyo angeshindana na hunsen bolti basi sudy angeshinda shindano hilo la mbio….alikimbia bila kugeuka nyuma…
ghafla aligeuka sudy alipiga kelele baada ya kuona upepo ule uko karibu yake tena ukiwa umebadilika na kuwa na rangi nyekundu mara ghafla..
Sudy alikimbia sana hata pasipokujua anakoelekea….wakati anakimbia kwa lengo la kukimbia upepo ule mwekundu uliokuwa ukivuma kwa kasi ukiwa unazunguka huku ukimfata nyuma yake.. mara ghafla alikutana na babu yake njiani….
sudy alipomuona babu yake alikimbilia ule upande aliokuwepo babu yake…ghafla babu yake alifungua mdomo kisha akanyoosha mikono yake juu macho yake yalibadilika na kuwa mekundu….upepo ule uliingia moja kwa moja mdomoni mwa mzee mkumbo……wakati upepo huo ukiendelea kuingia mdomoni mwa babu yake…sudy alistahajabu”””,,,aliogopa sana kisha akaanza kutimua mbio kuelekea kusikojulikana….
*********
mzee mkumbo aliendelea kufumbua mdomo wake mpaka upepo ule uliishia mdomoni mwake….kisha kile kibuyu cheusi kilitokea angani kikadondokea mbele yake….macho ya mzee mkumbo yalirudi katika hali yake ya kawaida…kisha akakiokota kibuyu kile na kukiinua juu alisimama huku kakishika kibuyu kile kwa sekunde kadhaa kisha kibuyu kile kilitoweka ghafla….
shwaini huyu mtoto angeniletea balaa laiti kama upepo ule ungemgusa angeiaga dunia na nafsi yake ikaingia ndani ya kibuyu….
*******
upande mwingine sudy alionekana akikimbia huku akigeuza shingo yake huku na kule…wakati anakimbia alipata wazo aende nyumbani kwao mbonde… alikimbia bila kusimama mpaka kwa kina mbonde wakati huo mbonde wakati huo ilikuwa kama majira ya saa moja jioni..
mzee mkumbo alizipiga hatua na kuelekea nyumbani….alikasirika sana kwa kile kitendo cha sudy kuingia nda ya chumba chake bila ruhusa yake na kufanya yasiyomuhusu…kama kibuyu kimefunguka basi zile nafsi za watu niliowauwa kimazingala zitaniponza itakuwa balaa kubwa….alijisemea moyoni mzee mkumbo liwalo na liwe mimi ndio MKUMBO alijisemea moyoni”””
alizipiga hatua na hatimae akafika nyumbani…alipitiliza moja kwa moja mpaka ndani kisha akaingia kwenye chumba chake”” aliinama haraka akachungulia uvunguni aliuvuta ungo wake kisha akahakikisha kama vitu vyake vya kichawi vitakuwa salama….”””,,, aliona vitu vyake vyote vipo sawa isipokuwa kibuyu kile kilikuwa bado hakijafika….mara ghafla kilitokea kibuyu kile”””,, hapo nafsi yake kidogo ikatulia….alikichukua kibiyu kile kisha akakipeleka moja kwa moja mpaka mdomoni…kisha upepo ule alioumeza aliuingiza ndani ya kibuyu kile kisha akakifunga na kipande cha kaniki nyeusi…..
*********
kijijini hapo balaa likaanza….walionekana watu wengi walio fariki miaka mingi iliyopita watu hao walitisha sana walikuwa na nywele ndefu….kucha ndefu walitembea kwa mwendo wa kizembe huku udenda ukiwatoka mdomoni…kumbe watu hao waliuwawa kichawi na mzee mkumbo kisha akazifungia nafsi zao ndani ya kibuyu kile….
watu hao walionekana baada ya sudy kukidondosha kibuyu kile kikafunguka na nafsi zao zikatoka ndani ya kibuyu kile…….wakiwa MISUKULE tayari””””,,, wanakijiji walistahajabu sana….kuona ndugu zao waliofariki miaka mingi kumbe bado walikuwa hai,!!!..itakuwa kunamtu aliwauwa kichawi na kuzifungia nafsi zao….alisema hivyo mwanakiniji mmoja…
wale watu misukule walienea kijijini hapo walikuwa wengi hakuna mfano…….walitapakaa huku na kule
ilibidi aitwe mganga mkuu wa wachawi kutoka kijiji cha jilani ili kumtambua ni nani aliyesababisha hayo yote kisha auwawe hadhalani…alitumwa kijana mmoja kwenda huko kwenye hicho kijiji cha jilani kwa lengo la kumuita mganga yule mkuu wa wachawi…””” taarifa hizo alizipata mzee mkumbo….kwa njia ya kichawi kisha alicheka sana akajisemea moyoni nadhani hamjanitambua mimi ni nani yeyote atakayenifatilia nitamuonesha mimi ni nani……naanza na huyo mliomtuma…
wakati kijana yule akiwa njiani kuelekea kijiji cha jilani… hana hili wala lile mara ghafla..
Mara ghafla aliitokea kichawi mzee mkumbo mbele ya kijana yule..ni kitendo cha sekunde..
kijana yule aliogopa sana aliamua kutimua mbio kwa sababu hakuona mzee mkimbo akizipiga hatua alistukia tu yupo mbele yake…..kijana yule alizichanja mbuga mara ghafla mzee mkumbo alijitokeza tena mbele ya kijana yule…kijana yule kutokana na kasi aliyokuwa kikimbia nayo kijana yule alidondoka chini baada ya kusimama ghafla. kisha mzee mkumbo akanyoosha kidole kuelekea pale alipodondoka kijana yule…mara ghafla kijana yule alikiwa kipofu pia hakuwa na uwezo wa kuongea tena mzee mkumbo alimfanya bubu…kisha mzee mkumbo akatoweka ghafla.
********
kule nyumbani kwa kina Mbonde”””””….sudy aliamua kumueleza kila kitu rafiki yake….mbonde sliogopa sana kusikia yale aliyosimuliwa na sudy…sasa itakuwaje?aliuliza mbonde
hata mimi sijui cha kufanya” alijibu sudy..kisha akasema naogopa kurudi nyumbani babu ataniuwa najua atakuwa amekasirika….mbonde alianza kumuogopa rafiki yake sudy….kutokana na yale mambo ya kichawi anayoyafanya Babu yake….aliuliza je babu yako akijua kuwa upo kwetu itakuaje si atatuuwa na sisi….aah mimi naogopa itabidi urudi tu nyumbani ukamuombe msamaha…..sudy alinyong’onyea sana baada ya mbonde kumwambia hivyo…aliamua kuondoka bila kusema kitu chochote….
wakati sudy anazipiga hatua kuelekea kusikojulikana ilikuwa ni majira ya saa mbili usiku….ghafla alikutana na MSUKULE mmoja njiani…msukule yule ni mmoja kati ya zile nafsi zilizotoka kwenye kibuyu zikiwa kama kimvuli cha binadamu..””sudy aliogopa akatimua mbio….kabla hajafika mbali alikuta tena na MSUKULE mwingine…sudy alizidi kuchanganyikiwa…
*********
mzee mkumbo alionekana chumbani kwake ni baada ya kumpofua na kumfanya bubu kijana yule kisha akatoweka kichawi….mzee mkumbo alipanga mikakati madhubuti ili kuhakikisha anawanasa misukule wale wote waliotoka ndani ya kibuyu…kazi hiyo nitaifanya usiku wa leo…alijisemea mzee mkumbo. kisha akaanza kuandaa vitu vyake vya kichawi….
********
wakati sudy akiwa njiani aliamua kutimua mbio kuelekea nyumbani kutokana na uwoga baada ya kukutana njiani na misukule wale. alitimua mbio mpaka nyumbani alipofika jilani bisa na nyumbani kwao alipunguza kasi ya kukimbia hatimae akaanza kutembea…alizipiga hatua huku akigeuza shingo yake huku na kule…… slipotazama nyumbani kwao aliona mpaka muda huo taa haijawashwa…..alihisi huenda babu yake hayupo..alinyata akasogea kabisa mpaka kwenye mlango aliusukuma ukafunguka….alisita kuingia kisha akaamua kumuita babu…lakini babu yake hakuitika……mmmh!!!! sasa babu atakuwa kaenda wapi au ameuwawa na ule upepo uliovuma kwa kuzunguka huku ukiwa na rangi nyekundu.!!!!!! sudy aliogopa sana….alishindwa hata kuingia ndani…
Sehemu Ya 4
alihisi huenda babu yake hayupo..alinyata akasogea kabisa mpaka kwenye mlango aliusukuma ukafunguka….alisita kuingia kisha akaamua kumuita babu…lakini babu yake hakuitika……mmmh!!!! sasa babu atakuwa kaenda wapi au ameuwawa na ule upepo uliovuma kwa kuzunguka huku ukiwa na rangi nyekundu.!!!!!! sudy aliogopa sana….alishindwa hata kuingia ndani…
Mzee mkumbo alikuwa tayari kwa ajili ya kazi aliyopanga kuifanya usiku huo alionekana akiizungukia mitaa kwaajili ya kuikusanya MISUKULE ile airudishe ndani ya kibuyu… kumbe taarifa zile zilimfikia yule mganga mkuu “”” na yeye pia muda huo alikuwa akijipanga ili kwenda kumkabili huyo mchawi anayesumbua kijiji cha jilani ambaye ni Mzee mkumbo…
wakati mzee Mkumbo akiwa anazunguka zunguka kwenye mitaa ya kijiji hicho….. alihisi harufu ya jambo la hatari…alistahajabu arufu hiyo ilizidi kuongezeka…hiyo ilimaanisha kunajambo la hatari litatokea muda si mrefu…..alikasirika sana akajisemea ni nani hiyo anayetaka kuingilia himaya yangu……mzee mkumbo alianza kuingiwa wasiwasi….huenda kunamtu mchawi zaidi kuliko yeye…
*********
kumbe yule mganga mkuu kutoka kijiji cha jilani alikuwa ameisha ingia kwenye kijiji anachoishi mzee mkumbo……kisha akaanza kutega mitego ya kumnasa mzee mkumbo kwa kutumia madawa ya kichawi… mzee mkumbo akiwa hana hili wala lile mara ghafla..
Mara ghafla mzee mkumbo aliona..mwanga mweupe unakuja kwa kasi kumfata pale alipo….alipoona hivyo aligundua kuwa hizo ni nguvu za kichawi zimerushwa ili zidhibiti….macho yalimtoka…..kisha akanyanyua kibuyu chake ili kuzikabili nguvu hizo za kichawi….alijibu mashabulizi”” nguvu zile zilivyokutana zilishambalatika na kuyayuka…..yule mganga alistuka sana hakuamini kama kunamtu anayeweza kukabilia na yeye….yule mganga alipo ona hivyo aliamua kuongeza nguvu za kichawi mara mbili ya zile alizozirusha….zilimfata mzee mkumbo alikwepa kisha na yeye akajibu shambulizi…..uchawi wa mzee mkumbo zilionekana kuwa na nguvu kuliko uchawi wa mganga yule aitwaye MAZIKU…
zile nguvu zilikwenda moja kwa moja kumfata pale alipokuwa….maziku na yeye alirusha nguvu za kichawi ili kuzikabili zile skadi alizozirusha mzee mkumbo…..lakini haikusaidia chochote nguvu za kichawi za mzee mkumbo zilipenya katikati ya zile nguvu za mganga na kumpata…skadi ile ilimpiga kifuani yule mganga na kumrusha mbali sana…..kisha akatuwa na kudondoka chini…..
mzee mkumbo alicheka kwa saiti kubwa…..kwa kweli sauti hiyo ilitisha….kisha akasema Hakuna wa kupambana na mimi….
mimi ndio MKUMBO mkuu wa wachawi..
yule mganga alipata majeraha ni baada ya kupigwa na zile skadi za nguvu za kichawi alizozirusha mzee mkumbo..
************
kule nyumbani Sudy aliamua kuingia ndani aliogopa sana kuona misukule ile alifunga mlango kisha akaingia chumbani kwake….alipanda kitandani….aliwaza sana juu ya yale aliyoyaona”” hivi ni kweli au nilikuwa naota ndoto za chanamchana!!!!!!! aliamua kuutafuta usingizi kwa sababu alikuwa kachoka sana..hivyo ndani ya sekunde kadhaa alikuwa kashasingia kabisa…
********
Ule upande mwingine yule mganga mkuu alivyoona kajeruhiwa alitoweka akayeyuka kichawi…”””mzee mkumbo alitoa macho kutazama ni wapi alipoelekea lakini hakumuona…shwaini huyu anataka kunijaribu eee haya jitokeze tena nikuoneshe kazi ya kibuyu changu….
yule mganga mkuu alikwenda kijijini kwao kujipanga upya ili kumkabili mzee mkumbo…
mzeemkumbo alipojaribu kutazama kwa kutumia nguvu za kichawi aligundua kuwa mganga yule MAZIKU kwamba hayupo tena maeneo hayo…kisha akaendelea na ile kazi aliyokuwa ameipanga kuifanya usiku huo….ni kazi ya kuwakusanya misukule wale na kuwarudisha ndani ya kibuyu chake ili aendelee kuwatumia katika shughuli zake mbalimbali….kumbe mzee mkumbo alikuwa akiwatumia misukule wale kuwalimisha mashamba yake…wengine aliwatumia kuwaibia watu pesa kichawi(CHUMAULETE) alizungukia maeneo yote lakini hakuweza kufanikiwa kupata hata msukule mmoja kwa sababu walikiwa tayari wameshatoka ndani ya kibiyu kile hivyo haiwezekani tena kuwarudisha kwa namna yoyote ile”” mzee mkumbo alihisi kuchanganyikiwa….alijaribu kadri ya uwezo wake lakini ilishindikana kila akikutana na msukule akijaribu kumrudisha kichawi ndani ya kibuyu kile ilishindika……alijaribu mpaka ikafika usiku wa manane bila mafanikio….hakuamini macho yeke kama ameshindwa kuwarudisha misukule wale ndani ya kibuyu…..alikata tamaa akaamua kuondoka zake alistuka””””kumbe yule mganga karudi na nguvu mpya mara ghafla..
Mzee mkumbo hakuamini macho yake…shaabashi!!! huyu mwanaharamu karudi tena kwani anataka nini!!!!? alijiuliza mzee mkumbo kisha uso wake ukaonekana kujaa jazba na hasira za hali ya juu ukizingatia alikuwa ameshahisi kuchanganyikiwa baada ya kishindwa kufanikisha kazi aliyokuwa ameipanga kuifanya usiku huo kurudisha zile nafsi za watu aliowauwa kichawi misukule…”””” alinyanyua kibuyuchake kisha akarusha nguvu za kichawi kuelekea pale kwa yule mganga Maziku….mzee mkumbo alistahajabu sana shambulizi lile halikumfanya chochote mganga maziku….”””” mzee mkimbo alitoa macho kama mjusi kabanwa na mlango…
Mganga maziku alicheka sana hahahahah”” kitendo hicho cha maziku kucheka kilimfanya mzee mkumbo hasira zimpande kichwani mara tatu zaidi…alianza kuzunguruka kama jogoo anapomvizia jike…..kisha akanyanyua kibuyu chake juu…. ulitokea mwanga kama radi kisha mwanga huo ukafuata moja kwa moja mpaka pale alipokuwa amesimama mganga maziku…..hiyo ilikuwa balaa hatari sana…..maziku alitoa macho kisha na yeye akarusha nguvu zake za kichawi ili zizuie zile nguvu za mzee mkumbo lakini alikuwa amechelewa zilikwenda moja kwa moja mpaka katikati ya kifua cha mganga maziku…na kumrusha juu kisha mzee mkumbo akafungua kibiyu ili amnase mganga maziku aichukue nafsi yake aifungie ndani ya kibuyu..
kule nyumbani sudy alistuka kutoka usingizini..ni baada ya kuhisi kiu ya maji ya kunywa.. alinyanyuka kitandani akaelekea sebuleni aliwasha koberiti na kuchoma utambi wa chemli kisha ikawaka alifungua mtungi wenye maji ya kunywa kisha akaondoka zake kurudi chumbani kuendelea kulala…
************
kule kwenye vita ya kichawi kati ya mzee mkumbo na mganga maziku iliendelea…baada ya mzee mkimbo kufungua kibuyu ili amnase maziku…. mara ghafla zile nguvu za kichawi zilimuachia mganga maziku akiwa bado yupo juu kabla hajatua chini…kisha akatua chini bila kupata madhara yoyote..mzee mkumbo alistahajabu sana akajiuliza nini kimetokea???? mbona nimepoteza nguvu zangu ghafla..
kumbe wakati sudy anakunywa maji alisahau kuufunika mtungi akauwacha wazi bila kuufunika…hivyo ni kosa kubwa sana inapofika usiku wa manane kisha ukafungua mtungi kwenye nyumba ya mzee mkumbo kwani endapo mtungi ukifunuliwa mda wa usiku wa manane basi unazizuia nguvu zake kufanya kazi…….
mzee mkumbo alijaribu kurusha skadi za kichawi lakini ilishindikana”” ndipo mzee mkumbo akagundua kuwa kunatatizo nyumbani kwake bila shaka mtungi umefunuliwa majira hayo. ndio maana nguvu zake hazifanyi kazi!!!!! wakati akiwaza hivyo mara ghafla…alistuka amepigwa na skadi kifiani kwake akaanguka chini….kabla hajafanya kiitu chochote akapigwa tena na skadi nguvu hizo za kichawi zilitoka kwa mganga maziku….mzee mkumbo alipo ona kazidiwa aliamia kutoweka aliyayuka kichawi akatokomea kisikojulikana ni kitendo cha sekunse akafika nyumbani kwake….alipotazama ule mtungi wa maji ya kunywa ulikuwa wazi…… ilibidi amuite mjukuu wake sudy aje afunike mtungi ule…kwani ni mwiko kwa mzee mkumbo kushika au kugusa mtungi majira ya usiku wa manane…..emdapo angefanya hivyo angeweza kupoteza uhai wake papo hapo…aliita lakini sudy hakuitika ghafla alisikia harufu harufu hiyo ilimaanisha hatari inatokea muda si mrefu…..kumbe ni yule mganga maziku anakuja akiwa angani juu ya ungo kwa kasii ya ajabu.. ….aliitambua harufu hiyo kichawi””” mzee mkumbo ilibidi aingie haraka chumbani kwa sudy ili amuamshe sudy afunike mtumgi ule ili nguvu za kichawi za mzee mkumbo zirejee haraka kumkabili mganga maziku…..mzee mkumbo alipagawa alipoingia chumbani kwa sudy lakini hakumkuta sudy…nimekwisha””” alijisemea moyoni huku jasho likimtoka kama kamwagiwa maji.. kumbe sudy alijificha uvunguni kwa kuhofia huenda babu yake alikuwa anataka kumuadhibu…mzee mkumbo alitoka chumbani kwa sudy haraka ili aangalie namna ya kufanya”” ile amefika sebuleni mara ghafla..
Mara ghafla mganga maziku alirusha nguvu za kichawi zilikwenda moja kwa moja mpaka pale alipo simama mzee mkumbo mlangoni mzee mkumbo alikwepa… kisha akayayuka akatoweka kichawi ilibidia aingie chumbani kwa sudy alipojaribu kuangalia kichawi akamuona sudy yupo chini ya uvungu… alimbalidisha ufahamu akampachika mawazo kichawi…ghafla sudy alinyanyuka kutoka mvunguni haraka akaelekea sebuleni… alifunika mtungi haraka…. wakati huo sudy hakutambua alicho kifanya kwa sababu haikuwa akili yake…. alibadilishwa mawazo kichawi na babu yake… mzee mkumbo nguvu zake za kichawi zirirudi muda huohuo… alinyanyua kibuyu kisha akarusha nguvu za kichawi kuelekea pale alipo kuwepo Mganga maziku…. skadi ile ilikwenda moja kwa moja mpaka kifuani kwa mganga maziku… zilimrusha mbali sana huku akiwa anawaka moto…. sudy akuweza kushuhudia vita ile kutokana alifumbwa kimiujiza na babu yake…
mganga maziku alipotua chini alikuwa akiwaka moto kama mtu aliyemwagiwa mafuta aina ya petroli. “” alipo ona mambo yamekuwa magumu aliamua kutoweka kichawi””” lakini mzee mkumbo alimuona aliamua kumfuata….baada ya mzee kumbo kuona ameanza kuingia kwenye mpaka wa kijiji cha jirani alikata tamaa ya kumpata mganga maziku…. aliamua kurudi kijijini kwao kutokana ilikuwa inaelekea majira ya saa kumi na moja alfajiri….ni kitendo cha sekunde tayari alikuwa ameshafika nyumbani kwake….
*********
palipokucha sudy alistahajabu babu yake hajadamka mpaka muda huwo ilikuwa saa mbili kasoro…. za asubuhi. na si kawaida yake… kwani alizoea kumuona babu yake akidamka mapema wakati mwingine yeye ndiye huwa anamuamsha sudy aende shule aliingiwa na uwoga akaamua kwenda kugonga mlango wa babu yake””””mzee mkumbo alistuka kutoka usingizini…akaitika alipojaribu kuamka alihisi maumivu mwili mzima hii ni kutokana na ile vita ya kichawi aliyopambana jana usiku…alijikongoja mpaka mlangoni kisha akafungua mlango.. sudy alimsalimia babu yake na baada ya kumuona babu yupo salama sudy aliamua kuondoka na kuelekea shuleni…. alizipiga hatua na hatimae alifika sguleni.. alikuta wanafunzi wenzake wamo darasani wameshaanza vipindi vya masomo…aliingia darasani na kuanza kumsikiliza mwalimu akifundisha… mara ghafla walionekana misukule wakilandalanda shuleni hapo misukule hao walikuwa wengi sana walitembeatembea huku na kule kwenye eneo hilo la shule””” wanafunzi baada ya kuona hivyo waliogopa wakatoka madarasani wakakimbia kila mtu na njia yake… hata walimu walijiunga pamoja na wanafunzi kutimua mbio… sudy alistahajabu aliumia sana moyoni kwa kuwa alikuwa anajua misukule wale walitokea wapi!!!!! misukule hao walianza kuonekana baada ya sudy kudondosha kibuyu cha babu yake kikafunguka upande wa juu kilipofungwa na kipande cha kaniki nyeusi””” nafsi za watu wale zilitoka ndani ya kibuyu kile kisha zikawa huru….
Sehemu Ya 5
wanafunzi baada ya kuona hivyo waliogopa wakatoka madarasani wakakimbia kila mtu na njia yake… hata walimu walijiunga pamoja na wanafunzi kutimua mbio… sudy alistahajabu aliumia sana moyoni kwa kuwa alikuwa anajua misukule wale walitokea wapi!!!!! misukule hao walianza kuonekana baada ya sudy kudondosha kibuyu cha babu yake kikafunguka upande wa juu kilipofungwa na kipande cha kaniki nyeusi””” nafsi za watu wale zilitoka ndani ya kibuyu kile kisha zikawa huru….
sudy alitimua mbio hatimae akafika nyumbani kwao….kumbe mzee mkumbo alikuwa ameshazipata taarifa kichawi…sudy aliparamia mlango kisha akamueleza babu yake yale yaliyotokea huko shuleni kwao.. mzee mkumbo alirudi chumbani kwake… alichukua kibuyu chake…kisha akakinyanyua juu””” ghafla ilisikika sauti ikimpa maelekezo kwamba jinsi ya kuwarudisha misukule hao kwenye kibuyu…aliambiwa aende kwenye mto unaitwa MWADOVYA mto huo ni wa KICHAWI KUTOKA KUZIMU akatumbukize kibuyu kile kisha achote maji hayo…. atakaapokutana na misukule awamwagie maji yale na baada ya hapo nasfi za misukule wale zitarudi ndani ya kibuyu…
baada ya kupata maelekezo hayo kutoka kuzimu.. alijipanga kuelekea kwenye mto MWADOVYA… alipofika tu kwenye mto huo alikutana uso kwa uso na yule mganga mzaziku”””kumbe mganga maziku alikwenda kutibiwa ni baada ya kushambuliwa na nguvu za kichawi za mzee mkumbo kisha akaungua mwili mzima…. pia aliomba kuongezewa nguvu ili apambane na mzee mkumbo… awaokowe wanakijiji cha jirani…
mganga maziku aliongezewa nguvu za ajabu… mara ghafla…
mara ghafla mzee mkumbo aliingiwa na wasiwasi.. alijiuliza mganga maziku kapajuaje huko na kaenda kutafuta nini… mzee mkumbo hakuweza kufanya chochote kwa sababu alijua ni mwiko kileta vita eneo lile.. hata mganga maziku alijua kuwa haitakiwi kufanya vurugu au mapambano katika eneo hilo kisha mganga maziku aliyayuka na kupotea kichawi””” mzee mkumbo aliusogelea mto ule kisha akasujudu na kuchota maji ya mto ule kwa kutumia kibuyu chake… wakati anayachota maji hayo alikuwa akiwaza sana juu ya mganga maziku… hivi huyu ni nani ambae anafuatilia mambo yangu inamaana hakomi tu??? alijisemea moyoni mzee mkumbo…
baada ya kumaliza kuchota maji hayo alinyanyuka na kupotea kichawi.. ni kitendo cha sekunde ghafla alifika nyumbani kwake… alijitokeza ndani ya chumba chake cha kulala.. kisha akainama na kutoa ungo wake wa kichawi chini ya uvungu.. akaanza kuandaa mikakati jinsi ya kunasa nafsi za misukule waliotoka ndani ya kibuyu baada ya mjukuu wake sudy kuiba kibuyu na kukidodosha chini kikafunguka na nafsi za misukule wale zikatoka ndani ya kibuyu kile….
baada ya kufika majira ya saa sita usiku mzee mkumbo alijipanga kwa ajili ya kuizungukia mitaa ya kijiji hicho ili kuwanasa misukule wale na kuwarudisha kwenye kibuyu… punde alipotea kichawi ni kitendo cha sekunde aliingia kwenye mitaa ya kijiji hicho…..alianza kunasa mmoja baada ya mwingine….
*************
kule kwenye kijiji cha jirani alionekana mganga maziku naye akijipanga kwenda kumkabili mzee mkumbo…. ilipofika majira ya saa nane
usiku mzee mkumbo alikuwa ameisharudisha robotatu ya misukule wale ndani ya kibuyu chake.. alifurahi sana…. ghafla alihisi harufu ya hatari… tena hatari ya leo ilikuwa ni kubwa kuliko… alistuka… bila shaka ni yule mwanaharamu anayefuatilia mambo yangu sasa leo nitaondoa uhai wake. wakati mzee mkumbo akiwaza hivyo mara ghafla alipigwa na nguvu za ajabu alistahajabu… kidogo akimbie….kisha mganga maziku akajitokeza akasema leo ndio mwisho wa maisha yako kisha akarusha nguvu za kichawi zilimrusha mbali mzee mkumbo… eeeh mzee mkumbo alipo ona mambo yamekuwa magumu aliamua kupaa na ungo wake…punde mganga maziku alimfuata hukohuko juu aisee ilikuwa vita ya ajabu walipigana kwa nguvu za kichawi huko juu angani…. lakini ilionekana uchawi wa mzee mkumbo ulikuwa ni moto wa kuotea mbali… mapigo aliyokuwa anayatumia kurusha nguvu za kichawi.. yalimuogopesha mganga maziku….alizidiwa nguvu na kuamua kutimka kuelekea kijijini kwao mzee mkumbo alipandwa na hasira za hali ya juu… uso wake ulibadilika rangi na kuwa mweusi kama mkaa macho yakawa mekundu… hii iliashiria hasira za hali ya juu…. wakati mganga maziku anamkimbia mzee mkumbo…. alipogeuka nyuma aliogopa baada ya kuona uso wa mzee mkumbo umekuwa mweusi na macho yake kuwa mekundu…. ghafla alipigwa na skadi iliyotoka kwenye kibuyu cha mzee mkumbo mganga maziku alidondoka kutoka angani mpaka chini….kisha mzee mkumbo alijisemea shaabashi mimi sio mtu wa mchezo mchezo…hii ni fundisho kwa wengine watakaoendelea kunifatilia…. kisha akarudi nyumbani kwake.. hakutaka tena kuendelea kuwarudisha misukule wale usiku huo. aliamua akapumzike…kisha ataendelea na kazi hiyo kesho… ni kitendo cha sekunde alikuwa tayari kafika nyumbani kwake….. akapanda kirandani akalala…
*************
asubuhi palipo kucha sidy akiwa anafanya usafi nje ya nyumba kutokana siku hiyo ilikuwa jumamosi hivyo ni siku ya mapumziko sudy hakwenda shule siku hiyo… alidamka mapema na kuanza kufanya usafi wa mazingira yanayoizunguka nyumba yao… mara ghafla aliona mwanamke mzee akija upande wa nyumba yao… bibi huyo alipofika alimuulizia mzee mkumbo… sudy hakusita akaenda kumuamsha babu yake… mzee mkumbo alimkaribisha bibi huyo sebuleni..
kisha bibi huyo alimpa taarifa kuwa mtoto wako amefariki… usiku wa kuamkia leo….
kumbe mzee mkumbo alimbebesha mimba bibi huyo miaka 40 iliyopita na kumtelekeza bibi huyo aliamua kukimbilia kijiji cha jirani ili kuficha aibu ya kubeba mimba bila kuole kipindi hicho alikuwa na miaka 19.. mzee mkumbo hakuwahi kumuona huyo mwanae wa nje.. kwa hiyo yule aliyekuwa akipambananae usiku wa jana na kuondoa uhai wake.. kumbe alikuwa ni mtoto wake wa damu. ….
bibi yule alitoa picha ya huyo mtoto wake na kumuonesha mzee mkumbo….
mzeee mkumbo alistahajabu sana kuona ile picha si mwingine alikuwa mganga maziku.
Mzee mkumbo macho yalimtoka baada ya kusikia taarifa hiyo…… alisikitika na kujutia sana……baada ya lisaa limoja kupita bibi yule aliondoka… sudy alistahajabu kumuona babu yake akiwa katika hali ya majinzi alipojaribu kuuliza mzee mkumbo hakujibu kitu chochote alibaki kimya…. taratibu za mazishi zilifanyika…… mzee mkumbo alifunga safari kuelekea kule kijiji cha jirani ili kumzika mwanae mganga maziku…….alipofika huko taratibu za mazishi ziliendelea… mzee maziku alijiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu..alijuwa wazi kuwa nafsi ya mganga maziku ipo mule ndani ya kibuyu…na akirudisha nafsi ile ili iungane na mwili wa maziku inamaana atabainika kwamba yeye ndiye mchawi aliekuwa akiwauwa wanakijiji kichawi na kuzifungia nafsi zao ndani ya kibuyu ili watu wale wageuke misukule na kumtumikia katika shughuli zake mbalimbali… aliingiwa na wasiwasi kisha akajisemea moyoni natamani aana urudi tena katika uhai lakini wananzengo watanitenga na kunifukuza kijijini endapo nitakapotoa nafsi yako ndani ya kibuyu nafsi nyingine pia zitatoka…
ilipofika majira ya saa saba mchana wanakijiji wa hicho kijiji cha jirani waliiaga mwili wa marehemu mganga maziku… watu walikuwa wengi karibia kijiji kizima walimpenda aliwasaidia kwa mambo mengi pia alikuwa mpenda haki…. hakika mganga maziku alikuwa kipenzi cha watu. walijiandaa kuelekea makaburini ili kumzika mganga maziku”””mzee mkumbo ..
*****************
kule nyumbani kwa mzee mkumbo… sudy aliona huo ndio muda sahihi wakufungua kibuyu kile ili zile nafsi zilizotoka siku ile alipo dondosha kibuyu zirudi ndani ya kibuyu”””” sudy alifanya hivyo huenda babu yake akafurahi baada ya kukuta nafsi hizo zimerudi ndani ya kibuyu… kwa sababu hawaongei vizuri yeye na babu yake kama zamani… sudy alizoea kumuona babu yake akifurahi muda wote pia alipenda hadithi za babu yake lakini sikuhizi hasimuliwi tena.. sudy aliamua kuingia chumbani kwa babu yake…alivuta ungo uliokuwa chini ya uvungu wa kitanda anacholalia babu yake…. alikiona kibuyu alikichukua kwa ujasiri siku hii hakuogopa wala hakuwa na wasiwasi wowote… hata yeye alijishangaa kuwa katika hali hiyo… alikinyanyua kibuyu kisha akaanza kufungua kile kipande cha kaniki nyeusi kilichokuwa kimefungwa upande wa juu ya kibuyu hicho…… kabla hajamaliza kukifungua kibuyu kile kilimponyoka na kudondoka chini kikapasuka vipande viwili!!!! ikawa ndivyo sivyo alivyokuwa amekusudia…… moshi ulianza kutanda nani ya chumba kile huku vimvuli vya binadamu vikitokea pale chini kibuyu kilipodondokea na kupasuka”” sudy aliogopa alitoka chumbani akaelekea upande wa nje….. baada ya muda kidogo moshi ule ulikatika…ghafla walianza kuonekana watu wakitoka nje kupitia mlango wa mzee mkumbo…. watu hao walionekana kuwa na makucha marefu na nywele ndefu….. watu hao walitoka mfululizo aisee walikuwa ni wengi sana na kila mtu alipotoka nje alistahajabu kujiona katika hali ile ya kuwa na makucha marefu na nywele mdefu…. watu hao walipata ifahamu baada ya kibuyu kuvunjika…. baada ya lisaa limoja mfululizo watu wale waliacha kutoka nje kutokea upande wa ndani ya nyumba ya mzee mzee mkumbo……wanakijiji walijazana kuizunguka nyumba ya mzee mkumbo walistahajabu sana kumbe mchawi alikuwa ni mzee mkumbo…. mbona alionesha ushirikiano kwa kila jambo hapa kijijini loh!! ((UMDHANIAYE NDIYE KUMBE SIYE)) alisikika mama moja wa wanakijiji akisema hivyo….mwenyekiti wa kitongoji alimuhoji sudy””” sudy hakutaka kudanganya alimueleza kila kitu… wanakijiji walimuonea huruma sudy pia walimpongeza kwa sababu bila yeye wasingeweza kuwaona ndugu zao waliofariki miaka mingi iliyopita””” kumbe mzee mkumbo aliwauwa kichawi na kuzifungia nafsi zao ndani ya kibuyu ili misukule hao wamtumikie kwenye shughuli zake…
*********
kule makaburini walipotaka tu kuliweka jeneza ndani ya kaburi walisikia mganga maziku akigongagonga jeneza huku akitoa sauti nifungulieni”” watu waliogopa walikimbia kila mtu njia yake wengine wakisema maiti imefufuka… lakini mzee mkumbo alibaki hakukimbia yeye pamoja na mama yake mzazi mganga maziku.
mzee mkumbo alistahajabu sana akajisemea moyoni haiwezekani lazima kunakitu hapa hakijaenda sawa kule nyumbani kwangu…. mzee mkumbo aliingiwa na wasiwasi wa hali ya juu.. alilikaribia jeneza na kulifungua……kumbe mganga maziku alirudi katika uhai baada ya nafsi yake kuungana na mwili ni baada ya kibuyu kuvunjika nafsi yake ilikuwa huru angani ikitafuta kiwiliwili cha mganga maziku ……..mganga maziku alistahajabu kumuona adui yake kafunfua jeneza alipotoka ndani ya jeneza alistahajabu kumuina mama yake mzazi….. kisha bibi yule alimwambia mganga maziku mwanangu huyu ndiye baba yako wa damu”””” maziku hakuwa na namna ilibidi awe mpole…. alimsamehe baba yake wakakumbatiana huku machozi yakimtoka mganga maziku.. waliondoka makaburini hapo.. kisha maziku na mama yake walikwenda nyumbani..
mzee mkumbo aliondoka na kurudi kwake… alipofika jirani na nyumbani alistahajabu kuona mkusanyiko wa watu nyumbani kwake… akiwa anatahamaki mara ghafla wanaume wawili walimnasa na kumpeleka pale kwenye mkusanyiko wa watu nyumbani kwake… mwenyekiti wa kitongoji aliamuru mzee mkumbo atengwe na afukuzwe kijijini hapo kisha wakaichoma moto nyumba ya mzee mkumbo…..baada ya mzee mkumbo kuona hivyo presha ilimpanda akadondoka chini na kupoteza maisha….. sudy alichukuliwa na mwenyekiti wa kitongoji akawa anamlea na kumsomesha….
*MWISHO WA SIMULIZI YA KIBUYU CHA BABU*


3 Comments
Simply wanna remark on few general things, The website style is perfect, the written content is really excellent. “I have seen the future and it doesn’t work.” by Robert Fulford.
Excellent beat ! I wish to apprentice while you amend your web site, how could i subscribe for a blog web site? The account aided me a acceptable deal. I had been a little bit acquainted of this your broadcast offered bright clear idea
I am glad for writing to make you be aware of of the nice discovery my wife’s daughter had studying yuor web blog. She mastered so many details, including what it is like to have a very effective helping heart to get most people with no trouble gain knowledge of selected complicated issues. You undoubtedly did more than my desires. Thank you for rendering those precious, trustworthy, educational and as well as cool tips on your topic to Lizeth.