KIBUYU CHA BABU
Sehemu Ya 1
SUDY alikuwa kijana mwenye umri wa miaka ipatayo Kumi na tisa….alipenda sana mchezo wa mpira wa miguu…
Alikuwa akiishi na babu yake…huko MAGU jijini mwanza…tangu utoto wake alilelewa na babu yake baada ya wazazi wake kufariki baada ya tukio la ajali ya moto iliyounguza nyumba yao na kuteketeza kabisa””,, ama kweli Mungu sio Athumani…Sudy alinusurika yeye peke yake baada ya kuokolewa katika ajali hiyo ya moto.. wakati huo alikuwa mtoto wa miezi kumi na moja….hivyo babu yake ambaye anaitwa mzee MKUMBO hivyo yeye pamoja na mkewe walichukua jukumu la kumlea sudy…
sudy aliendelea kukua na hatimae akatimiza miaka kumi na tisa…sikumoja aliamka usiku ili kwenda kujisaidia haja kubwa”””” ilikuwa ni mida ya saa nane usiku…alipotoka nje alishangaa kuona watu wamevalia kaniki nyekundu wamekaa chini huku wamekizunguka kibuyu cheusi miingoni mwa watu wale alikuwemo babu yake..alistahajabu sana hakuwahi kuona hayo anayoyaona…
kumbe babu yake alikuwa ni mkubwa wa WACHAWI katika kijiji hicho”” kumbe watu wale walikuja nyumbani kwa mzee MKUMBO kwajili ya kikao”,, .kikao hicho kilihusu mambo yao ya kichawi…wakati Sudy akishangaa hayo anayoyaona aliogopa sana akaamua kurudi ndani”” alijikaza kisha akapanda kitandani kwake…hakuweza kupata usingizi ndipo aliamua kunyanyuka kitandani ma kuelekea kwenye dirisha la chumbani kwake ili aone kinachoendelea kule nje…aliona watu wale wamesimama wakiimba huku wanakizunguka kibuyu kile…..wakati huo mzee Mkumbo akiwa amekaa….
sudy alizidi kukodoa macho alitazama kwa umakini wa hali ya juu” ghafla watu waliongezeka kwenye kikao hicho watu hao walikuja na mtu wakiwa wamembeba”” mtu huyo alionekana kama maiti yani mtu aliyekufa muda si mrefu..mzee mkumbo alisimama kisha akachomoa kisu alichokuwa amekiweka upande wa kushoto kwenye kiuno chake””kisha akakipeleka shingoni mwa mwaiti ile,,Sudy alipoona vile alistuka akashika mdomo wake kwa viganja vya mikono yake,, “aliingiwa na woga wa hali ya juu..almanusura aachie haja kubwa””,,
mzee Mkumbo alikata shingo ya maiti ile ambayo inaonekana ni ya mtu aliyekufa dakika chache zilizopita” na kisha akaweka mdomo wake kwa ajili ya kunyonya damu..alipomaliza ndipo wale watu wengine wakaanza kukata baadhi ya viungo na kuanza kula huku wakiimba nyimbo zisizoeleweka.. kisha nikamuona babu anavuta maini kutoka tumboni kwa maiti ile baada ya kupasuliwa tumbo…alikula maini yale…nilijihisi kutapika baada ya kuona kitendo hicho…
baada ya wote kumaliza kula nyama hiyo ya mtu aliyekufa.. walikaa kimya kisha nikaona babu akiongea…sikuweza kusikia maneno yale kutokana na umbali wa chumba changu mpaka hapo walipo…baada ya dakika kadhaa watu wale walisimama kisha wakanyoosha mikono kama mtu anayetaka kupaa..ghafla watu wale walipotea ni kitendo cha sekunde pia sikumuona babu. nilipo tazama kwa makini niliona kibuyu kile cheusi pekee kimebaki punde si punde nacho kikatoweka ..nilistuka nikarudi kitandani kwangu haraka nikajifunika shuka mpaka kichwani….nilihisi labda babu kaniona….niliogopa sana..huku mapigo yangu ya moyo yakipiga kwa kasi kama mtu aliyekimbia umbali mrefu..
ilipita kama nususaa hivi..bila kusikia chochote ndipo nikafunua shuka taratibu nikidhani labda watu wale ameingia chumbani kwangu..nikaangaza macho pande zote za chumba sikuona mtu yoyote..”” inamaana babu yangu ni mchawi?? haiwezekani au nilikuwa naota..lakini hapana nilishuhudia kwa macho yangu…nilijisemea hivyo moyoni…
******
kiukweli nilikuwa nimejawa uwoga wa jali ya juu..niliwaza sana bila kujua nini cha kufanya.. baada ya muda kidogo Sudy alipitiwa na usingizi akasinzia…
palipokucha sudy aliamka akajiandaa kwenda shule. …lakini alitafakali sana juu ya yale aliyoyaona jana alijiuliza hivi ilikuwa ni ndoto au?? hakupata jibu…ghafla alitokea babu yake sudy alistuka kumuona babu yake…kisha akamsalimia shikamoo babu” babu yake aliitikia salamu yake..kisha akamwambia leo umeamka mapema ni viziri kuwahi shule….wakati huo sudy alikuwa akimtazama babu yake kwa uwoga…babu yake aliondoka na kuelekea shambani.
SUDY alipomaliza kujiandaa alitoka nje kisha akaanza safari ya kuelekea shuleni…wakati anazipiga hatua..alikuwa anajiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu kichwani mwake…..alifadhaika sana kwa kile kitendo alichokiona usiku wa jana”,, mbaya zaidi pale alipokumbuka kuwa alimuona babu yake akinyonya Damu kisha kula maini ya binadamu tena yakiwa mabichi…..alikunja sura kama mtu aliyehisi kupatwa na kichefuchefu..kisha akatema mate….alizidi kuzipiga hatua na hatimae alifika shuleni….alihesabu namba na baada ya muda kidogo iligongwa kengere kwa ajili ya kuingia darasani kwa ajili ya kuanza vipindi vya masomo”,,
**************
mwalimu alikuwa anafundisha lakini Sudy mawazo yake hayakuwa hapo darasani. aliwaza kisha akajisemea moyoni inamaana hata nyama tunayokula hapa nyumbani anayoileta babu labda itakuwa ni ya binadamu…mmh!!! lakini mbona huwa inaonekana kama ni ya ngo’mbe? alijiuliza bila kupata jibu””,, alikohoa..
kho kho kho……”””ghafla akashika mdomo wake kwa kiganja chake cha mkono wa kulia kisha akanyanyuka kwa kasi huku akizipiga hatua za harakaharaka kutoka kwenye dawati alilokuwa ameketi utadhani mtu ni mtu anayetaka kukimbia…””” ,,, wanafunzi wenzake walimshangaa wakawa wanajiuliza nini kimempata mwanafunzi mwenzao!!! Sudy alizipiga hatua haraka ili atoke nje,, “” kabla hajafika mlangoni alishindwa kujizuia alitapika mbele ya darasa””,,…wanafumzi wote akiwemo mwalimu wao”,, wa somo la hisabati. walistahajabu sana…wakati huo Sudy alikuwa kachuchumaa jirani kabisa na mlango wa darasa hilo…..mwalimu alimkaribia huku akimtazama kwa macho ya mshangao..akamuuliza nini kimekupata??? au unaumwa? sudy hakupemda mtu yeyote afahamu chochote kuhusu kutapika kwake..hivyo aliamua kudanganya””,, alimdanganya mwalimu kuwa anajisikia vibaya hivyo anahisi atakuwa na homa…..mwalimu alimuonea huruma sana sudy..wakati huo wanafinzi darasa zima walikuwa wamesimama kutazama kinachendelea kule mbele alipokuwa amechuchumaa Sudy…
**********
Mwalimu alisitisha kufundisha kwa muda kisha akamchukua Sudy nakwendanae mpaka kwa mwalimu wa zamu,,”” ili Sudy aandikiwe taarifa ya ruhusa hivyo aende akafanyiwe vipimo…kisha akarudinae mpaka darasani akaamuru mwamafunzi mmoja ampeleke Sudy nyumbani kwao…
Sudy alichukua begi lake kisha wakaondoka pamoja na mwanafunzi mwenzake kuelekea nyumbani…
**********
walipokuwa njiani Sudy alikuwa kimya mda wote yule mwanafnzi alikuwa akimuuliza maswali sudy…lakini sudy hakujibu chochote.
baada ya muda sudy alifika nyumbani kisha yule mwanafunzi mwingine akarudi shule..
wakati huo babu yake sudy hakuwepo nyumbani… bado alikuwa shambani…..sudy aliingia moja kwa moja chumbani kwake kisha akapanda kitandani na kuanza kuutafuta usingizi,, “baada ya dakika kadhaa alipotiwa na usingizi…
na ilipofika mida ya saa kumi hivi Mponda alikwenda nyumbani kwa kinaSudy,, “Mponda ni rafiki wa karibu wa sudy alikwenda nyumbani kwa kinaSudy kwaajili ya kumpitia waende kucheza mpira……lakini leo Sudy hakujisikia kwenda mpirani….Mponda aliamua kuondokazake
**********
Punde Mzee Mkumbo akarudi nyumbani kutokea shamba….alistahajabu kumkuta Sudy akiwa katika hali ya unyonge””,,, Shikamoo babu” sudy alimsalimia kisha babu aliitikia marahaba mjukuu wangu kulikoni!!! mbona waonekana kama hauna furaha…sudy alidanganya nilikuwa na uchovu tu. hivyo nililala ndio naamka sasa hivi….
kisha babu akaingia chumbani kwake…
**********
ilifika jioni na hatimae giza likatanda… walikula chakula cha usiku Sudy na babu yake….. kisha babu yake Sudy akanza kumsimulia hadithi mjukuu wake….mzee mkumbo huwa anafanya hivyo kila siku””” Alimpenda sana mjukuu wake huyo wa pekee.
Hadithi ilipofika katikati sudy alistahajabu sana kisha woga ukamjaa…hadithi hii ya leo ilikuwa tofauti sana na aina ya hadithi alizo zoea kusimuliwa na babu yake.. kadri babu alivyozidizi kusimulia hadithi””,, iliendana kabisa na yale matukio niliyoyaona jana usiku..niliendelea kusikiliza kwa umakini wa hali ya juu….ghafla nilistuka baada ya babu kusimulia kuwa yule kijana akarudi ndani na kuanza kuchungulia kupitia dirisha la chumbani kwake ili aone kinachoendelea huko nje….niliogopa sana nikadhani labda babu aliniona kipindi nachungulia dirishani wakati wanakula nyama ya binadamu…… babu alinitazama usoni””” tulipokutanisha macho mimi nikakwepesha macho na kuangalia chini..
mmh!!! nahisi itakuwa babu kaniona na ndio maana kaamua kuniambia kwa kupitia hadithi.. lazima kunakitu hapa!!!!
nilijisemea moyoni
niliogopa sana…lakini nilijipa moyo kutokana Babu alikuwa akinipenda sana sikuwahi kumuomba kitu chochote akaninyima”,, hivyo basi hawezi kunidhuru…baada ya kumaliza kunisimulia hadithi hiyo iliyonistahajabisha kisha babu alichukua kiko kwenye mfuko wa koti lake la suti ya kizamani kisha akaweka tumbaku na kuanza kuvuta…..sikushangaa kwa sababu nilizoea kumuona akivuta tumbaku kwenye kiko hiyo tangu nilipokuwa mtoto mdogo….
********
Tulikaa hapo nje mpaka mida ya saa sita usiku kisha..babu akaniambia nizunguke nyuma ya nyumba nikahakikishe kama banda la kuku limefungwa…kwani yeye hakumbuki vizuri kama alifunga au Lah!!! kisha akanyanyuka nakuanza kuzipiga hatua za mwendo wa kizee kuelekea ndani””,,…mimi nilifanya kama alivyoniagiza wala sikushangaa nilijua wazi kuwa kutokana na umri wake kuwa mkubwa hivyo mara nyingi huwa anapoteza kumbukumbu”” huenda alifunga banda hilo kisha amesahau”,,…wakati nazipiga hatua kuelekea huko nyuma ya nyumba…uwoga ulikuwa umetanda juu yangu…siku hiyo hakukuwa na nuru ya mbaramwezi””” hivyo giza lilikuwa nene….pia lile tukio nililoliona jana wakati babu akinywa damu na kula maini ya binadamu aliyekufa!!!
kwa upande wangu picha hiyo iliniijia mara kwa mara akilini mwangu…hivyo nikawa na uwoga na wasiwasi zaidi kutokana nilikuwa nje peke yangu…nilizipiga hatua za mwendo wa polepole huku naangaza angaza macho yangu” kushoto kulia kwa kuhofia labda watu wale niliowaona jana huenda wapo maeneo hayo….nilizidi kuzipiga hatua…nilipolikaribia banda nilipiga hatua mbili za haraka kisha nikaugusa mlango wa banda kwa kuuvuta”” ndipo nilipogundua kuwa ulikiwa umefungwa….nianza kurudi kwa hatua za mwendo
wa haraka kurudi ndani….baada ya kupiga hatua kama tatu hivi….nilisita kutembea naada ya kuona taa ya chemli imewasha chumbani kwa babu na kwa sababu dirisha lake lilikuwa wazi niliamua kuchimgulia ili nione ni nini anachokifanya…kwa sababu kipindi napiga hatua nilihisi nimeona kama babu kashika kitu mikononi alafu mikono yake ikiwa juu kama mtu aliyesalimu Amri!!!! nilisogea taratibu kwa kunyata…ili nione ni kitu gani kashika na ni kwanini kainua mikono yake juu…nilipochungulia nilitazama kwa makini kitu kile alichoshika babu….nilistahajabu sana””
baada ya kukiona kiile kibuyu cheusi nilichokiona jana pale nje kikiwa chini kisha kikatoweka…pia wakati babu bado kakishikilia kibuyu kile alikuwa akiongea”” niliyasikia maneno yale lakini sikuweza kutambua ni lugha gani anayoongea!!!! kwa sababu hakikuwa kiswahili wa haikuwa lugha yetu ya KISUKUMA!!! nilizidi kukodoa macho nikitszama kwa umakini wa hali ya juu” niliona babu anashusha mikono yake kisha.. akakipeleka kibuyu kile upande wa nyuma kwenye makalio yake kisha akakirudisha upande wa mbele…
**********
baada ya babu kufanya hivyo,, niliona ameinama kutoa kitu uvunguni na aliponyanyuka niliona katoa ungo kakiweka kibuyu kile kwenye ungo kisha akarudisha ungo ule uvunguni!!!! niliogopa almanusura nikimbie lakini nikajikaza ili asijue kuwa kunamtu anamuona hicho anachokifanya”” ,,
babu alipanda kitandani na kisha akazima chemli…nilihisi kuchanganyikiwa baada ya chemli ile kuzimwa hivyo nilihisi babu kaniona…..nilinyata kutoka pale dirishani nilipoona nipo mbali na usawa wa dirisha lake nianza kuzipiga hata za mwendo wa haraka…nilipoukaribia mlango”,, niliogopa kuingia ndani nikasimama…..nilipogeuza shingo yangu kuangalia nyuma niliogopa zaidi kutokana na giza nene lililokuwa limetanda siku hiyo”””” niliingia ndani haraka na kisha nikafunga mlango…mwili wangu ulikuwa unatetemeka kutokana na uwoga wa hali ya juu hivyo niliogopa hata kulala chumbani kwangu..nilisimama kwa sekunde kadhaa kisha nikajisemea moyoni huyu ni babu yangu hivyo hawezi kunidhuru”””
kutokana na uwoga wa kulala peke yangu….nikaamua kugongs hodi kwenye mlango wa babu kwa lengo la kulala chumbani kwa babu.. niligonga mlango lakini babu hakuitikia…ndipo nikaamua kusukuma mlango taratibu kisha nikaingia ndani…niliita babu….babu…lakini babu hakuitika…
*********
kwa sababu taa ilikuwa imezimwa hivyo basi chumbani mule palikuwa na giza nilirudi sebuleni haraka nikachukuwa chemli iliyokuwepo sebuleni.
kisha nikaridi chumbani kwa babu nilipomulika kitandani sikumuona babu.
nilistuka nikaogopa zaidi kisha nikatoka chumbani mule haraka….nikapitiliza moja kwa moja nje huku nimeishikilia chemli mkononi…..
nilipofika nje sikujua nielekee wapi nilibaki nimesimama kama sanamu….kisha nikaizima chemli ile haraka….””ghafla wazo likanijia kwamba nisilale hapo nyumbani hivyo niliamua kutafuta nyumba iliyopo jirani……niliiweka chemli chini kisha nikaanza kuzipiga hatua za harakaharaka kama askari jeshi anapokuwa kwenye gwaride la mwendo wa haraka…..nilizipiga hatua hizo nusu nikimbie……
***********
kwa pale kijijini kwetu nyumba zilijitenga kutoka nyumba moja mpaka nyumba nyingine”” hivyo nyumba ambayo ilikuwa jirani na kwetu””,, ni umbali wa kilometa moja hivi….nilitembea hatimae nilianza kukimbia kwa kuhofia wanyama wakali huenda wakawa mawindoni usiku ule”””” nilikimbia bila kusimama nilipo ikaribia nyumba ya jirani yetu….nilianza kupunguza mwendo..nikaanza kutembea…kwa mbali niliona moto mkubwa umewashwa….kisha nikaona kama kunawatu wengi kiasi….kwenye ile nyumba ya jirani yetu””‘…nilisita kusogea nikaamua kujibanza”” yani kujificha sehemu ili nisionekane…nilipoangalia vizuri watu wale nilistahajabu ni watu walewale niliowaona sikuile…lakini leo aliongezeka mwanamke mmoja…nilipo mtazama kwa makini mwanamke yule niligundua kuwa ndiye yule mwalimu wetu anaefundisha somo la hisabati…nilistahajabu sana….ghafla niliona akiingia ndani ya nyumba na kisha kutoka na kinu kikiwa na mwichi wake ndipo nikagundua kuwa huenda pale ndipo anapoishi..yani nyumbani kwake.sikuweza kuona vizuri kile kilichokuwa kinaendelea pale….nikaamua kunyata nikasogea karibu kabisa…kutokana na moto mkubwa uliowashwa kwa kutumia kuni….niliweza kuona kila kitu…niliona mwanaume mmoja kajitokeza huku kabeba katoto kachanga….nilistuka nikakodoa macho kwa umakini wa hali ya juu…ili nione nini kinatendeka pale….nilimuona mwalimu wangu akimpokea yule mtoto mchanga kutoka mikononi wa mwanaume yule kisha akamuweka mtoto yule mchanga ndani ya kinu….nilistuka sana nikajawa uwoga…nilijiuliza sasa wanataka kumfanya nini yule mtoto mchanga kwanza sasahivi ni usiku yapata mida ya sasaba…itakuwa wanataka kumdhuru mtoto huyu.nilijisemea moyoni huku nikitazama nione kinachoendelea..
Sehemu Ya 2
kutoka mikononi wa mwanaume yule kisha akamuweka mtoto yule mchanga ndani ya kinu….nilistuka sana nikajawa uwoga…nilijiuliza sasa wanataka kumfanya nini yule mtoto mchanga kwanza sasahivi ni usiku yapata mida ya sasaba…itakuwa wanataka kumdhuru mtoto huyu.nilijisemea moyoni. huku nikitazama nione kinachoendelea..
baada ya yule mwalimu wetu kumuweka yule mtoto mchanga ndani ya kinu…alichukuwa mwichi…eeeeh nilipoona hivyo nilisimama haraka huku mapigo yangu ya moyo yakipiga kwa kasi ya ajabu….ghafla nikaona anatwanga ndani ya kinu kile…nilipoona hivyo nilitimua mbio kurudi nyumbani…..ingawa kulikuwa na giza nene lakini nilikimbia pasipo kujikwaa wala kuanguka….nilikimbia kwa kasi sana na nilipokaribia maeneo ya nyumbani nilipunguza mwendo kisha nikaanza kutembea”,,
kwa mbali nilimuona babu akiwa peke yake alikuwa amekaa chini””,, palepale nilipomuona kakaa jana…huku moto unawaka….nilipotazama kwa mbele yake kulikuwa na kibuyu kile cheusi…..niliogopa sana nikaanza kuzipiga hatua za harakaharaka….nilipoanza kuingia kwenye kiwanja cha nyumnani kwetu..nilisita kutembea nikachchumaa huku nikitazama ule upande aliokaa babu..ghafla niliwaona watu wawili wakitokea angani wamevalia kaniki nyekundu huku wapo juu ya ungo…kisha wakatua chini…
kitendo kile kilinifanya niogope kiasi ambacho haja kubwa ilinitoka…pia nikashusha vijampo vya mfululizo……uwoga ulitanda juu yangu nilikuwa nikisimuliwa kuhusi wachawi wakipaa na ungo usiku nilikuwa siamini lakini leo nimeshuhudia kwa macho yangu….nilijikaza nisipige kelele…niliendelea kukodoa macho mara ghafla waliomgezeka watu wawili wengine…wakitokea angani wakiwa juu ya ungo kisha wakatuwa chini watu wale walikuwa wamejipaka unga mweupe kwenye nyuso zao hivyo sikuweza kuzitambua sura zao…ghafla babu alitoweka…sikuona alipoelekea kwa sababu kilikuwa ni kitendo cha sekunde… baada ya sekunde kadhaa alijitokeza tena…..niliona mtu mwingine akiongezeka lakini mtu huyu sikumuona akitua kutokea angani”” ila mtu huyu alikuja kama upepo nilistukia tu namuona”””,, alikuja kambeba mtu lakini nilipotazama vizuri niliona mtu yule aliyekujanae alikuwa kafungwa kamba…kisha akamlaza chini….niliogopa sana nilimuonea huruma mtu yule alikuwa akilia kwa uchungu lakini haikusikika sauti yake… kisha nikamuona babu anakitoa kisu chake kwenye kiuno..
kisha akakishika baraabara..niliona babu akisimama kisha akapiga hatua mbili kielekea pale alipokuwa amelazwa yule mtu aliyeletwa…..akakipeleka kisu kile moja kwa moja mpaka kwenye shingo ya mtu yule”” ,,nilimuonea huruma sana lakini sikuwa na uwezo wa kwenda kumsaidia…babu alikata shingo ya mtu yule kisha akapiga magoti na kuanza kufyonza damu ya mtu yule kupitia ile sehemu aliyo ikata kwa kisu”” ,,mtu yule alirusha rusha miguu kutetea pumzi yake ghafla mtu yule alitulia tuli”” baada ya babu kumaliza kifyonza damu aliinua kisu chake na kukidunga kwenye tumbo la mtu yule. kisha akapasua tumbo lile na kuingiza mkono wake niliona ametoa moyo akauweka pembeni..kisha akaingiza mkono tena”” alipouchomoa mkono alitoka na maini kisha akasimama na kuanza kula maini yale yakiwa mabichi…
niliogopa sana..nikafumba macho….wale watu wengine walianza kuimba nyimbo zisizoeleweka huku wakicheza kwa kushangilia ushindi wa kazi waliyoifanya isiku huo….nilipofumbua macho niliona watu wale pia wakila nyama ya mtu yule….”” kwa mbali niliona mwanga”” ,, mwanga ule ulikuwa ukimulika kuelekea upande wangu!!! niliogopa nikaamua kula chini…nilipotazama vizuri niligundua ni taa ya baiskeli hivyo nikajua kuwa kunamtu anaendesha baiskeli ile…sikumjali nikageuza shingo kuendelea kutazama kule walipokuwepo akinaBabu na washirika wake…..ghafla waliacha kuimba nikakodoa macho kuona nini kitatokea…ghafla babu alitoweka….
ni kitendo cha sekunde.”” ,, nikazidi kuogopa huku naangaza angaza macho kushoto kulia…ghafla nilisikia mtu yule akipiga kelele!!! nilipotazama upande ule ambo kelele hizo zilitokea niliona baiskeli iko chini…kisha nikaona mtu yule akitimua mbio na kutokomea kabisa…mapigo yangu ya moyo yakaanza kwenda kasi huku jasho likinitoka… nilipotazama kule walipokuwepo watu wale nikamuona babu sikujua alirudi vipi pale…walikaa kimya kwa muda wakimsikiliza babu anachoongea…kiukweli sikusikia maneno yale kutokana na umbali niliokuwepo..ndipo watu wale wakasimama kila mmoja kwenye ungo wake..nakuanza kupaa angani….nakutoweka kusikojulikana
***********
alibaki babu peke yake yeye na kibuyu chake….ghafla na yeye akatoweka kisha kikafatia kibuyu chake….na ule moto uliokuwa ukiwaka ukazimika ghafla pakawa na giza nilizidi kuogopa..nikajiuliza sijui mlango utakuwa umefungwa?? aah kwa baridi hili siwezi kulala nje nilinyanyuka pale chini…kisha nikaanza kuzipiga hatua za kunyata.. ghafla wingu kubwa lilitanda likazifunika mbaramwezi na nyota pakawa na giza nene ikiambatana na ngurumo radi”” punde mvua ikaanza kunyesha….
ilianza mvia ya manyunyu na baada ya muda ilianza kunuesha mvua kubwa sana…niliogopa sana baada ya ngurumo za radi kuzidi niliamua kukimbia kuufata mlango..nilipojaribu kuusukuma.. kumbe mlango ulikuwa wazi..nilijiuliza sana inamaana babu hakugundua kuwa mlango upo wazi?? je alipitia wapi? nilisita kuingia ndani ghafla radi ilipiga nikaogopa nikaingia ndani na kufunga mlango
niingia moja kwa moja mpaka chumbani kwangu
nikapanda moja kwa moja kitandani kwangu.. sikuweza kupata usingizi usiku huo…nilibaki macho mpaka kukakuchacha…
*********
niliamka na kujiandaa kwenda shule….”” mara kwa mbali nilisikia tangazo”” niligundua tangazo lile ni la msiba nilistuka sana nikawaza msiba huu itakuwa yule mtu aliyechinjwa na babu yangu usiku wa jana kisha wakala nyama ya mtu yule babu na washirika wake….
punde babu aliamka kisha akaniambia anajiandaa kwenda msibani baada ya kusikia taarifa hiyo ya msiba iliyotangazwa namjumbe wa nyumba kumi.
nilimtazama babu kwa macho ya mshangao…sikuamini kama ndiye huyu babu niliyemuona jana usiku..akinywa damu na kula maini ya binadamu””,, kisha nikaendelea kujiandaa ili niende shule….babu alimaliza kujiandaa kabla yangu kisha akatoka chumbani kwake… alinikuta niko sebuleni navaa viatu vyangu…alitoa noti ya shilingi mia tano kisha akanikabidhi akasema utakunywa chai huko shuleni..kisha akatoka na kuondokazake”,, nilimchungulia dirishani ili nihakikishe kama atakuwa amefika mbali..niingie chumbani kwake nikaangalie kibuyu kile cheusi kina nini ndani yake…..nilipoona katokomea kabisa yupo mbali na nyumbani niliingia chumbani kwake..nilistahajabu sikukuya kitu hata kimoja chumbani mule yani hata kitanda chake sikukiona!!! chumba kilikuwa wazi utadhani labda hakai mtu ndani yake…niliogopa nikatoka haraka chumbani mule kisha nikachukua begi langu haraka nikatoka nje…..nilirudishia mlango kama kawaida nilivyozoea tangu nilipokuwa mtoto mdogo…nakumbuka babu alishawahi kuniambia kuwa hakuna mtu anayeweza kuja kuiba kitu chochote pale nyumbani yani hata kipande cha kuni……
*********
nikaanza kuzipiga hatua kuelekea shule….wakati nikiwa njiani alitokea mwalimu wetu wa kiume alikuwa anafundisha somo la kiswahili..alikuwa akiendesha baiskeli kuelekea shule…alisimamisha baiskeli na kuniambia nipande kwa sababu na yeye anaelekea hukohuko shuleni..nilipanda na tuianza safari…
nilipofika shule nilihesabu namba ghafla kengele iligongwa wanafunzi wote tukakusanyika…kisha mwalimu mkuu akasema wanafunzi wote wa darasa la saba mnatakiwa kwenda msibani kwani mwanafunzi mwenzenu kafiwa na baba yake mzazi..”””” kisha akaamuru tutawanyike na ikawa hivyo kama mwalimumkuu alivyoamuru
********
Sudy……sudy ilisikika sauti ya rafiki ysngu mbonde kisha nikageuka nilimuona anakuja akikimbia ule upande niliokuwepo….mambo vipi mbona sikuizi umekuwa zobazoba hata mpirani hutaki kuhudhulia au babu yako kakukataza usicheze mpira?? aliuliza hivyo mbonde….
sikumjibu kitu nilikaa kimya kwa sekunde kadhaa kisha nikaamua kumdanganya ili asijue kinachonitatiza….nikamwambia sikuizi ule muda wa jioni huwa najisomea kwa ajili ua kujiandaa na mtihani wa Taifa.. basi sawa rafiki yangu ni jambo jema alisema mbonde.. kisha tukaanza safari ua kuelekea msibani…
********
Tulipofika msibani tulikuta mkusanyiko wa wanakijiji…wanafunzi tulikaa upande wetu…lakini mimi na mbonde tulijitenga tulikaa peke yetu..ghafla nilimuona babu nikastahajabu sana jinsi alivyoondoka asubuhi alikuwa amevaa suluali na shati alafu kavalia koti la suti ya kizamani…alafu namkuta huku kavaa mavazi mengine tena yale anayoyavaa usiku akiwa na washirika wake kwenye vikao vyao vya kichawi…
alikuwa kavalia kaniki yake nyekundu….nilostahajabu sana sikuwahi hata sikumoja kumuona kavaa hivyo mchana kweupe.. alionekana kutisha kutokana na sura yake ya kizee iliyokunjamana ikiambatana na madevu yake marefu meupe kidevuni……sikutazama sehemu yoyote zaidi ya ule upande aliokuwa amesimama babu….ghafla waliongezeka watu wawili sikujua wametokea wapi niliwatazama watu wale sikuwatambua…lakini nilipovuta kumbukumbu niwakumbuka watu wale”””” ni wale wanaokuja kila siku nyumbani wanakula nyama za binadamu pamoja na babu….watu wale walikuwa uchi…nikamtikisa mbonde…alipogeuka nikamnongoneza ona watu wale wapo uchi…..mbonde alipotazama hakuona kitu chochote aksema mbona sioni kitu!!!!! nikagundua kuwa watu wale pamoja na babu naona mimi pekee..niiliogopa sana..
*******
ulipofika muda wa kuaga maiti…watu wakijiandaa kupanga mstari..nilimuona babu akinyoosha mkono wake mmoja juu”””ghafla nikaona kibuyu kile kinatua kwenye mkono wa babu!!!! kisha akasogea mpaka kwenye jeneza na wale watu wawili waliokuwa uchi wa mnya walimfuata…babu alisimama upande wa kichwani kwenye jeneza kisha wale watu wawili ambao wako uchi walisimama pembeni mwa jeneza….nilistahajabu ule umati wote wa watu…hakuna hata mmoja aliyeweza kuona jambo hilo ila ni mimi pekee..
********
Wanakiniji waanza kupita moja baada ya mwingine wakaaga mwili ule wa marehemu…walipomaliza watu wote kuuaga mwili wa marehemu…nikamuona babu akiweka kibuyu chake kwenye paji la uso wa marehemu kisha maiti ile iligeuka kuwa gogo la mti….niliogopa sana…nilisikitika nilipoona mke na mtoto wa marehemu wakilia kwa uchungu huku wakigusa mwili wa marehemu….nikajiuliza inamaana watu wote hawa hawaoni kuwa hiyo siyo maiti bali ni gogo la mti….nilimuonesha mbonde lakinj hakuona kitu chochote…
kaka mkubwa wa marehemu alifunga jeneza kwaajili ya maziko…
INAENDELEA

