666 NYAYO ZA KUZIMU
Sehemu Ya 3
“vipi tena si ulisema hutoki nje??”
aliuliza mzee Patili,
“eh! Yani mie nibaki peke yangu ndani??..wale mabibi si watanifuata!!”
akajibu Julina huku macho ya uoga yakipendezesha uso wake mwembamba mweusi.Punde si punde mama Halima nae alitoka nje na kujumuika na Julina na mzee Patili aliembebelea mtoto,walianza kuteta kuhusu wale mabibi na pia bila kusahau ndoto ya
mzee Patili iliyowashangaza na kuwaogopesha wakina Julina kwa kiasi kikubwa!
“mito ilikua miekundu,haikuskika tena sauti za ndege,milio ya shida na malalamiko ndio iliyotawala,harufu ya kifo na umauti ndio iliyoshika hatamu,miti ilipendezeshwa na miili iliyoning’inia kwa kunyongwa,na mioyo ya binadamu ilikua ni ya wanyama,tena wanyama haswa!!!”
alizidi kudadavua mzee Patili ile ndoto huku macho ya wakina Julina yakiwa yanakaribia kutoka kwa mshangao!!
Akaendelea,
“kila mmoja niliemuona alikua na chapa ya namba mwilini mwake!”
“chapa!!..ipi tena??”
Julina aliuliza kwa mjazo wa kutaka kujua,kwa masikitiko alijibu mzee Patili
“chapa yenye namba tatu,sita zilizorudiwa mara tatu,yani 666!!!..cha kutofautisha tu kilikua ni wapi hiyo chapa
ilipokuwepo,wengine kwenye mapaji ya uso,wengine mikononi,wengine mapajani na kadhalika! Maisha hayakua kama yalivyo,maisha hayakua kama tunavyoyajua,kila mtu muoga na maisha yake alikubali kubandikwa chapa itakayomuwezesha kuendelea kuishi,na wale wenye misimamo yao,walinyongwa kama kuku!!!”
maneno hayo yalizidi kuteketeza amani ndani ya mioyo ya wakina Julina na pia kuzidi kupalilia roho ya uoga iliyochipukia kwa kasi!!….taswira ya kile kilichokua kinaelezewa na mzee Patili ilikua imejengeka ndani ya vichwa vyao hivyo kuipa mwanya hisia za uoga kukumbatia mioyo yao iliyokua inaenda mbio!!
Udadavuaji wa ndoto ulizidi kutolewa na mzee Patili,lakini kabla ya kumalizika alikuja mama Tito kwa kasi huku akiwa kashikilia
kichwa na anapiga ukunga,ilikua haiitaji vipimo kujua ya kwamba alikua kwenye matatizo!!
“uuuuwwwiiiiiiii!!!!….Maamaaa weee!!! Mungu wangu eeeenhh!!!…jamaniiiiii!!!!”
“mama Tito vipi tenaa???”
aliuliza mzee Patili kwa hamaki huku wakina Julina wakiwa wameishiwa pozi kwa mshangao!!
“mume wangu jamaniii!!!!…mume wangu..mungu wee!! Mume wangu Jamanii!!!!!”
“sasa mume wako kafanya nini???”
“nimemkuta mume wangu kanyongwa kule shambani,jamani baba Tito wanguuuuuwwii!! Mume wangu mie ntaishijeee!!!”
sauti kali ya kilio ya mama Tito iligonga kwenye masikio ya wanakijiji,haraka lile eneo lilifurika watu,habari za kunyongwa Baba Tito zilihamsha taharuki,msururu wa watu ulianza safari na kuelekea eneo la tukio wakiwemo mzee Patili na wakina Julina ambao hawakutaka kabisa kubaki pale kijijini.
Sauti za vilio vya wanawake ilipata kusikika vizuri,tahamaki ilimshika kila mtu,kuona mwili wa baba Tito ukiwa unaning’inia kwenye mti ule wa muembe halikua tendo la kawaida kabisa machoni mwao! Hisia za uoga zilitawala na baadhi yao wenye roho ndogo walizirai akiwemo Julina!!
Nani amefanya haya?? Na amefanya kwa madhumuni gani?? Kila alieshuhudia lile jambo alijiuliza na kuwauliza wenzake pia,sauti ya kilio cha mama Tito iliyokua inazidi kupotelea kutokana na kukaukiwa sauti ilizidi kuchimbua na kumwagilia huzuni iliyodamiri lile eneo,na pia tukio la kumpepea Julina aliezimia liliendeleza hofu mioyoni.
Mwili wa Baba Tito ulishushwa na kufunguliwa toka kwenye kile kitanzi,na taratibu ulibebwa kupelekwa kijijini kwa ajili ya shughuli za mazishi huku bado maswali mengi yakizaliwa ndani ya vichwa vya watu waliokua pale juu ya kipi hasa kinachoendelea.
Wakati safari ya kurudi kijijini ikiwa inaendelea ghafla mjadala mzito ulianzishwa,mjadala uliokua unaongelea juu ya ujio wa Mzee Otongo na mama Kadogo kama sababu kubwa iliyopelekea ile hali,yani ujio wao ndio umeleta laana pale kijijini na ndio mana mambo ya ajabu yameanza kuchukua nafasi!!
Asilimia kubwa ya watu walionekana kuafiki hilo jambo isipokua Mzee Patili aliesimama kidete kukanusha hilo kwa nguvu zote na kutetea tendo lake la kuwapokea wale watu kwamba lilikua sahihi.
Mama Halima hakua na la kuchangia kwani hakushuhudia hayo mambo na pia Julina hakupata hiyo fursa kwani alikua bado hajazinduka,mtoto wake alikua amebebwa na mzee Patili na mwili wake ulikua mgongoni mwa Mama Halima!
Je itakuaje? Na ni nani anahusika na hayo mauaji? Wakina mze Otongo watakua salama mbele ya wanakijiji?
Kwa mbali sauti za vilio zilifika kwenye masikio ya mzee Otongo,mwili wake bado ulikua unavuta kwa maumivu japokua fursa ya kuishi bado ilikuwepo mikononi mwake,tumbo lilikua linamuuma kwa sana ilihali na kichwa kutokana na dhoruba kali aliyokumbana nayo ya Jeshi! Jeshi! Jeshi la 666! Alitaka kujiinua,mungu wangu!! Alisikia mpasuko wa maumivu umepita mgongoni pahh!!…ka sauti ka kulalamika kakaitika..aaaahh!!! Kilichoashiria ya kwamba maumivu yamegota penyewe,aliurudisha mwili wake chini na kugeuza shingo kutizama pembeni alipomuona mama Kadogo ambaye bado fahamu hazikurudi kwenye makao yake,alipandisha na kushusha macho yake juu ya mwili wa mama Kadogo na kushuhudia jinsi gani majeraha yalivyoshika utawala,kila pande ya mwili wake ilikua na jeraha na hata alivyojiangalia mwilini mwake aligundua hilo,macho yake yakaanza kubarizi lile eneo alilokua,kuanzia juu chini na pembezoni,umbali wa hatua tano toka alipokua kulikua na jiko litumialo kuni,na sufuria ilikua juu ya mafiga.kilichomo ndani ya sufuria kilionekana kuchemka kwani sauti ya kutokota kupita kiasi na mvuke mkubwa kutoka kwenye sufuria zilithibitisha hilo,mzee Otongo alitambua hicho kitu lakini mwili wake usingeweza kumruhusu kusogea kutokana na mzigo wa maumivu aliokua nao,sauti za watu zilizidi kufika masikioni mwake na mwishowe alisikia mlango unafunguliwa,alikua ni mzee Patili,macho yao yaligongana na kidogo kamshangao kiliwapitia,taswira ya mzee Patili haikua ngeni machoni mwa mzee Otongo ila haikua hivyo kwa mwenzie ambae ilikua vigumu kumtambua kutokana na kile kipigo kumchakaza sura yake kwa kiasi kikubwa,hawakuongea kitu,mzee Patili alifunga mlango na mkono wake mmoja uliokua haujamshikilia mtoto na kufanya sauti za wanakijiji zilizokua bado zinaruruma kwa nje juu ya ujio wa wageni pale kijijini zififie kidogo,
“vipi unaendeleaje??”
mzee Patili aliuliza,
“…mmm..kichwa kinanigonga mno,mgongo nao,vilevile tumbo!!!…issshh!!”
alilalamika mzee Otongo,
“usihofu,mpaka jioni utakua ushapata unafuu kwani hiyo dawa niliyokupaka ni nzuri sana kwa majeraha na kutuliza maumivu..”
“ahsante sana!..eti,kwani hapa ni wapi??”
aliuliza mzee Otongo ili kupata uhakika wa pale alipo baada ya nafsi yake kumtonya kwamba ni utowele,
“upo kijiji cha Utowele kwa sasa,kwani nyie mlikua mnatokea wapi na mnaelekea wapi??”
“tulikua tunatokea Igesambo,na safari yetu ilikua ni kuja hapa Utowele..”
“mmmh…kufanya nini??”
aliongezea swali lingine,mzee Otongo alijivutavuta huku akipambana na maumivu na mwishowe akakaa,kisha akajibu kwa tabu..
“lengo letu lilikua ni kumuwahi mtoto aliezaliwa..”
kauli hiyo ilimshtua mzee Patili! Hakuna mtoto aliezaliwa kijijini zaidi ya yule aliembeba,mtoto wa Julina!!!”
kwa hamu ya kujua akaongeza swali lingine..
“mtoto aliezaliwa?? Wa nini hasa??”
“huyo mtoto ndie uhai wetu,ndie tumani letu na utawala wa giza ulilijua hilo na ndio mana walitujeruhi,kutudhoofisha na kufanikisha lengo lao la kumuwahi,na hata huku kuchomoza kwa jua ni ishara ya uzao wake….ila yu hatarini na inabidi alindwe kwa nguvu zote kwani jeshi! Jeshi! Jeshi la 666! Wanamsaka kwa hali na mali wamtokomeze!!”
maneno yale yalipenya mpaka kwenye mishipa ya damu ya mzee Patili na hapo ndipo alipoanza kupata mwanga juu ya ndoto aliyoiota,lakini kuna kitu aligundua! Haraka akauliza
“wewe ni Otongo??”
“naam…ndie mimi!..bila shaka wewe ni Patili!”
“haswaa mie ndie!”
kile kitu kilimshangaza sana mzee Patili,ni muda mrefu umepita toka walipokua pamoja kutokana na uhusiano wao wa kikazi wa kiganga na hakutegemea kama wangekutana katika ile hali!!
Ila bado mawazo yalizidi kumsonga kichwani!!!
* * * *
nje ya kijumba cha mzee Patili bado wanakijiji walionekana kuteta hasa juu ya kifo cha baba Tito ambaye mwili wake ulikua ushahifadhiwa ndani kwake,kutokana na ugumu wa kujua kinachoendelea kila mwanakijiji alitupia hisia zake juu ya wale wageni waliofika ya kwamba kwa njia moja au nyingine wanahusika,nani unadhani?? Ni hawa hawa tu!! Mbona hayajawahi kutokea tangu na tangu?? Hii ni laana!!! Hawa watu wametuletea laana!! Tutakwisha jamani!!! Wanakijiji walipayuka,ngebe za wanakijiji zilizopamba moto juu ya kukemea na kulaani tendo la ujio wa wale wageni bado hazikubadilisha kitu!!!
ALINYONGWA MWINGINE MTU MWINGINE!!! NA TENA ALIKUA NI MAMA TITO!!!…PEMBENI YA MAITI YA MUMEWE!!! nani anafanya haya mauaji? Kwanini anaua?? Amedhamiria nini?? Nini hatma ya wakina Mama Kadogo mbele ya kiza cha jamii??
Mama weee!!!..mama Tito kanyongwa jamaaanii!!! Mungu eeee!! Tunakwisha uuuwii!!! Ndivyo alivyosikika mama Kurwa alietoka kwenye nyumba ya mama Tito kwa lengo la kumpa pole kwa kifo cha mumewe,huku akikimbia mikono kichwani mithili ya mtu aliechanganyikiwa machozi na uoga ilionekana kuitawala sura yake!! Hakuna alieamini hizo habari mpaka walipoenda kushuhudia na kukuta jambo lile ni kweli limejiri!! Macho yao yalishudia Mama Tito akiwa kaning’inizwa na kamba nyekundu
kama ile iliyomnyonga mumewe muda si mrefu,ulimi ulikua nje na damu ilionekana kutoka puani na masikioni!!!!
Mchanganyiko wa hasira na uoga ulitawala mioyoni mwa wanakijiji,kifo kwa mara ya pili mfululizo!! Hata masaa hayajapita,tena mume na mke!!!..ni nani anaeyafanya haya?? Jamani hii si bure…ni laana inatuua!!!…ni nani aliewaleta wale watu lakini?? Ni
baba Madhifa!!…haraka wanakijiji wasiopungua idadi ya watu thelathini,wake kwa waume,watu wazima kwa watoto kwa jazba kubwa walianza kuelekea kwa baba Madhifa!!…chuki iliyokuwepo kati ya jamii ya wakulima na wavuvi juu ya wawindaji ilizidi kushamiri kwa kiasi kikubwa,baba Madhifa sasa ndie alieokana kama chanzo,kitendo chake cha kuwaokoa wakina mzee Otongo ilikua ni hukumu tosha!
Mawe na dhana zingine kama mapanga mikononi mwa wanakijiji zilikua ni kipimo tosha cha kuonyesha kinachoenda kujiri,hakukua na amani tena!!
Masikini baba Madhifa,hakua na hili wala lile,kuzaliwa kwake kwenye jamii ndogo ya wawindaji ndio kosa lake kubwa,hakuna wa kuwatetea mbele ya wanakijiji wengine,hakuna wa kuwasikiliza!!
Walipowasili kwenye uwanja wa nyumba yake haraka shughuli za ubomoaji na uharibifu zilianza!! Mawe yalirushwa kama risasi kwenye nyumba ile ya udongo bila hata kuangalia na kuuliza kama mna watu ndani,sauti za kejeli matusi na kebehi zilisindikiza
bara-bara shughuli hiyo na hatimaye waliamua waichome kabisa waridhishe roho zao zilizokua za kinyama baada ya kushuhudia mauaji ya wenzao wawili,je hilo ni suluhisho?? Hawakufikiria hicho!!
Baba Madhifa na wanae hawakuwepo,walirudi msituni kuendelea na shughuli zao na hata Mama Madhifa vilevile alikua kisimani akichota maji,Mungu alikua upande wao kwani kama wangelikuwepo ni dhahiri wangelikua mishikaki!!
Lile zoezi halikuishia pale tu kwa baba Madhifa,liliendelezwa kwenye nyumba zingine zote za jamii ya wavuvi zilizokuwepo karibu na kuwafanya wabakie mithili ya vifaranga waliokimbiwa na mama,hawakuweza kufanya kitu,hawakua na uwezo huo,ila waliumia sana rohoni! Kwanini wao?? Au ni kwasababu wao hawahesabiki ndani ya kile kijiji?? Walikua kama yatima,walishindwa kuyazuia machozi.
Sasa wamebaki wakina mzee Otongo,je kipi kitawakuta?? Wale wanakiji baada ya kuridhika na walichokifanya hawakutaka kupoteza muda,miili ya Baba Tito na mkewe ilizikwa na kuhitimisha zoezi la kumuacha Tito yatima kamili,majonzi na simanzi zilitawala lile eneo bila kusahau na hisia za uoga,
Julina na Mama Halima ni miongoni mwa watu waliokuwepo eneo la tukio japokua hawakuhusika kurusha hata jiwe moja kwenye nyumba ya baba Madhifa,chozi lilitiririka kwenye kila jicho la mmojawao ila hasa mama Halima,moyo wake ulikua umebeba siri
nzito juu ya vile vifo,siri ambayo hakuna hata mmojawao anayoijua isipokua yeye,ni yeye pekee aliekua anafahamu ya kwamba mama Tito hakuuwawa bali alijiua kwani alimshuhudia mama Tito kwa macho yake akiichukua ile kamba iliyomnyonga mumewe kule shambani na ndio hiyo aliyoitumia kujimalizia na yeye pia,aliogopa kusema!! Na chozi lilizidi kumshuka haswa!!!
* * * * *
Mama Madhifa baada ya kuweka ndoo yake ya maji kichwani taratibu alianza kujivuta kuelekea nyumbani kwake,macho yake aliyoyatupia mbele ya safari yalimruhusu aone moshi mzito ukitokea kijijini,alipata mashaka,maswali yalikuja kichwani juu ya nini hasa kinachojiri huko kijijini,masikini hakufahamu ya kwamba nyumba yake na za wenzake ndo zinateketea.
Aliongeza kasi kidogo inayoendana na umri wake wa miaka hamsini na tatu ili aweze kuwahi ila ghafla alikabwa na mtu tokea nyuma!!! Puuh ndoo ilidondoka na maji yakamwagika!!! Aliangaika kutetea uhai wake lakini hakufanikiwa!!..mara haraka akavishwa kitanzi chekundu tayari kwa KUNYONGWA!!!
Alikabwa kwa nguvu mno akashindwa kupumua kabisa,macho na ulimi vilitoka nje!! Aliburuzwa kama zigo la maganda ya viazi na ile kamba shingoni mpaka ulipo mti mmoja mkubwa wa mkaratusi,akaning’inizwa mithili ya nyama buchani,maisha yake yakakomea hapo,kikatili mno aliuwawa,hakupata hata fursa ya kujua yaliyotokea kule kijijini,hakupata hata fursa ya kumuona mumewe tokea muda wa asubuhi,hata mwanae wa mwisho ampendae,Madhifa.
Hakuna alieshuhudia chochote,hakuna jicho lililoona lolote hivyo bado ilikua ni siri juu ya nani anaeua na kwanini anaua vilevile,kwanini anatumia kamba nyekundu?? Pia lilikua ni swali ambalo bado wanakijiji walikua hawajalipa nafasi vichwani mwao,hali ilizidi kuwa tete na ya kuogofya…ndani ya masaa yasiozidi matano tayari watu watatu walikua washaenda na maji kwa kifo kinachofanana!!
Baba Madhifa na wanae wawili walikua washawasili kijijini,hali ya kuona moshi mzito toka kijijini iliwafanya waache shughuli zao za uwindaji na kwenda kujua kinachojiri,walipofika kijijini hawakuona watu kama inavyokuwaga ni dhahiri walikua wameenda sehemu fulani ambayo wao hawakuifahamu,haraka walielekea ilipo nyumba yao,hawakuamini macho yao,hawakuamini
walichokiona,nyumba yao ilikua tayari gofu na nyumba zingine za wenzao nazo ndio zilikua zinamalizikia kwa moto,haraka waliwafuata wenzao waliokua wamejikusanya kihuzuni hatua kama kumi toka walipo kwa dhumuni la kuuliza ili kujua hasa kilichotokea,kiunyonge waliwajibu ya kwamba wanakijiji ndio wamefanya hayo,baba Madhifa alipata hofu kubwa moyoni!! Mke
wangu yu kwapi?? Aliuliza haraka kwa taharuki akajibiwa ya kwamba alienda kisimani,bila ya kuchelewa aliwaagiza wanae wawili ambao walikua ni wa kiume;Madhifa na Khadhifa kwenda kumjulia hali mamayo huko kisimani,haraka walikimbia
kuelekea huko! Masikini hawakujua ya kwamba mama yao tayari alishaning’inizwa ni ndege tu wa mizoga ndio wanaofaidi,walikimbia kwa kasi na nguvu zao zote huku mioyoni mwao wakiwa wanasali mama yao awe salama,Madhifa alishindwa kuzuia machozi na hofu kubwa ilishika wake moyo,alimpenda sana mama yake.
Baada ya mwendo wa robo saa walikuta ndoo chini waliyoitambua ya kwamba ni ya kwao lakini hawakumuona mama yao!! Ilibidi waanze kufuatilia alama zilizoashiria ya kwamba mtu aliburuzwa toka eneo lile zilizowapeleka mpaka karibu na eneo ambapo mama yao alinyongwa,ndege wa mizoga walisaidia kuhitimisha zoezi.
“Khadhifa!!!..yule anaening’inia pale mtini ni nani???…sio mama yule!!!”
sauti iliyotepeta uoga ya Madhifa iliuliza,
“He!! Mbona kama ni yeye!!!!”
alijibu Khadhifa,haraka walisogea na kugundua ya kwamba walichobashiri ni kweli,alikua ni mama yao! Damu zilitawala dela lake kwa kiasi kikubwa kutokana na kunyofolewanyofolewa na ndege wa mizoga,macho yake yaliokua nje yalikua yashanyofolewa na hata ulimi pia,sura yake ilikua ngumu kutambulika!!!
Haraka Khadhifa ambae ndie mkubwa alifukuza wale ndege na kupanda juu ya mti kwa ujasiri na kufungua ile kamba kuruhusu mwili wa mamaye kushushwa chini,walimshusha na kumbeba kisha safari ya kuelekea walipotoka ambapo baba yao anawasubiri ilianza,hawakua na mama wala nyumba tena,uchungu usioelezeka ulitawala mioyo yao,moja kwa moja walifahamu
ya kwamba waliochoma nyumba yao ndio wanaohusika na kile kifo,yani wanakijiji!!
Chuki kubwa ilipandikizwa mioyoni,roho ya kisasi ilikamata hasa vichwa vyao,hawakutaka kukubali lile jambo liende vile vile tu,hawakukubali roho ya mama yao iende peke yake yani bure kabisa kwa ule unyama aliofanyiwa,hisia za kuwa wawindaji wa watu badala ya wanyama zilizuka!!
Baada ya muda kidogo waliwasili kwenye uwanja wa nyumbani kwao sura zao zikiakisi vya kutosha mioyo yao ilivyo na uchungu,walihisi kama wamekabwa rohoni tena hisia hizo zilizidi hasa baada ya kumuona baba yao,walishindwa kupata jibu juu ya nini watamueleza kwani walimuonea huruma,lakini ghafla walianza kulia kama watoto,kilio ambacho walijitahidi kukizuia tokea muda mrefu,kilio ambacho kilimfanya baba yao ashtuke,kilio kilichofanya baba yao aanguke kwa presha kama kiroba!!
* * * * * * *
upande wa pili wanakijiji waliokua kwenye mazishi ya baba na mama Tito walimaliza shughuli zao,walijiondoa toka kwenye lile eneo la makaburi huku bado habari za uoga juu ya ile hali zikitapakaa,bado hofu iliwashika na walishasahau kabisa dhambi waliyotoka kuitenda ya kuchoma nyumba za watu wanaowahisi wao ni chanzo,walikua kimakundi makundi lakini ghafla mama Halima alimvuta pembeni Julina na kumwambia kwa kumnong’oneza kiumbea..
“mama Tito hakuuwawa!!”
“unasema??”
“ndio hivyo kama ulivyonisikia..!”
“we umejuaje??”
“nilimshuhudia kwa macho yangu akiichukua ile kamba iliyomnyonga mumewe,na ndio hiyo kajinyongea!”
“weeeh!!”
“we si ulizimia,ungeyaonea wapi?? Ila!!..uufunge huo mdomo wako,tena uufunge hasa!”
“ntaweza kweli??”
alidakia Julina.
“kwanini usiweze??…ushaanza!!”
kwa ukali kidogo mama Halima alitamka,
“sawa mama nitajitahidi kadri ya uwezo wangu”
Julina alimtia moyo,waliendelea na safari yao ya kuelekea majumbani taratibu huku wakiwa washaachwa nyuma na wenzao,stori ndogo ndogo zilitawala maongezi yao hasa juu ya tendo lile la uchomaji moto wa nyumba zakina Madhifa kitu walichoonekana kupinga kupinga kabisa japokua walikua hawana uwezo wa kuongea mbele ya umati wa wanakijiji,wangeonekana wasaliti.taratibu walitembea bila hofu walishasahau
kidogo mambo ya vifo kutokana na kupumbazwa na vijistori vidogo vidogo vya hapa na pale,ila ghafla Julina alisimama kisha akasema..
“mama Halima,nina hofu”
“nini tena Julina mwanangu? Mwanao si yupo kwa mzee Patili..”
alisema mama Halima huku akirudi nyuma kumfuata,
“sio juu ya mtoto wangu Mama,ni juu ya mume wangu Kitanzi!…ni muda sasa hajarudi,sijui nae atakua ashanyongwa??”
“mh-mh,usiseme hivyo bwana kwanza embu twende nyumbani ukapumzike mana tokea usiku ulipojifungua upo kwenye heka heka tu hata mtoto wako atakua anakuhitaji mno kwa sasa,tafadhali twende!”
kidiplomasia mama Halima alipooza jambo lililotaka kuzuka,alimshika mkono Julina na kumvuta waende.
Nyuma ya mama Halima na Julina alionekana mtu anakuja kwa kasi! Pande la mtu,pande la mbaba! Mweusi tii kwa rangi na kichwani alikua hana nywele kabisa,yani upara!!
Mikono yake miwili mikubwa iliyoshiba ilikua imeshikilia kamba nyekundu,macho yake makubwa mekundu yalisadifu hamu kubwa iliyo moyoni mwake,masikio yake yalizoea makelele ya kuomba msamaha ya watu mbalimbali na hata pia mikono yake ilizoea kunyofoa roho za watu,alikua ni mnyongaji!!!
Ghafla mama Halima alihisi kitu akageuka nyuma haraka,hakuona kitu!! Wasiwasi ulimteka moyo,akamwambia Julina
“nahisi kuna kitu!”
huku akigeuka geuka nyuma,
“nini tena hiko??”
Julina mama uoga haraka aliuliza,
“bado sijafahamu! Ila tuongeze mwendo Julina,twende!!”
haraka mbio zikaanza,maumivu bado yalikua na Julina kwani si muda mrefu toka atoke kujifungua lakini uoga wake ulimsaidia mno kumkimbiza,tayari moyo wake ulishawasha jenereta,ulikua mbio mno kuliko hata wa yule aliehisi kitu,yani mama Halima!! Joto lilipanda mwilini mwake,kajasho kauoga kalimteremka! Mungu wangu nisaidie!! Alijiambia moyoni.
Baada ya muda kidogo waliwafikia wenzao wakaungana nao,walishusha pumzi ndefu ya kutoamini kama wamefanikiwa huku mioyo yao ikianza kutulia taratibu,walijuta kwanini walibaki.
Lile jitu lilitokomea,halikuonekana tena,halikujulikana lilielekea wapi!! Lilichokipanga hakikufanikiwa,wakina
mama Halima waliponea chupuchupu watiwe kitanzini kama isingelikua hisia zao zilizowastua,hivyo nani anafuata?? Hiko kilikua ni kitendawili.
Upande wa pili wa shilingi nyumbani kwa mzee Patili maongezi madogo madogo yalichukua nafasi,fahamu
zilishamrudia mama Kadogo japokua majeraha bado mwilini yalimsumbua na pia vilevile kichwa kilikua kinamuuma,dawa alizopewa na yule mzee sio siri zilimsaidia vilevile mzee Otongo.
Maongezi yao yaliokua yanaendelea yalishindwa kufikia hitimisho kwani kila walipojadili kuhusu vilivyotokea huko nyuma bado hawakupata jibu kwamba vimeishia wapi,ni ngumu kuamini kama lile jeshi limewaacha tu
vilevile,walipata kidogo mashaka,walikua hawafahamu ya kuwa kuna mauaji yanaendelea kijijini,walikua hawajui kabisa juu ya hilo,walikua hawafahamu ya kwamba sasa jeshi la 666 limekuja kivingine!!
Muda ulianza kuruhusu jua lizame,taratibu giza likaanza kuingia,wanakijiji kutokea kwenye mazishi walianza
kuitia miguu yao ndani ya kijiji,mila zao na desturi haziruhusu kulaza maiti,hivyo mtu akifariki mapema tu anazikwa akapumzike kwa amani,kila mwanakijiji alielekea kwenye nyumba yake,tito aliekua yatima yeye alichukuliwa na mama Kurwa,mmama mmoja muongeaji sana mwembamba ambaye ni jirani yao,mama
Halima na Julina moja kwa moja walielekea kwenye nyumba ya mzee Patili,kumpasha habari na kumchukua mtoto waliemuacha hapo kwa muda.Habari zile ziliwashtua sana! Mauaji ya watu wawili ndani ya kijiji kwa kunyongwa kilionekana kuamsha hisia ya kwamba ujio wa jeshi la 666 umewadia!
Mama Kadogo na mzee Otongo pia walihisi vivyo hivyo!
Upande wa pili mzee patili na wakina mama Kadogo walijisikia vibaya juu ya taarifa ya kuchomwa kwa nyumba za wakina baba Madhifa na walijiona wakosefu mbele zao.
Ngo! Ngo! Ngo! Hodi iliita,mzee patili aliinuka na kwenda kufungua,alikua ni Khadhifa! Alikuja kumuita mzee patili akawasaidie kwani baba yao yupo kwenye hali mbaya!! Mzee Patili alishangazwa na zile habari na hasa alishangazwa zaidi baada ya kuambiwa hicho kitu kilijiri baada ya kuleta mwili wa mama yao waliokuta umenyongwa maeneo ya kisimani,haraka mzee Patili alichukua madawa fulani kisha mbio zikaanza kuelekea eneo la tukio!
Kutokana na kaumbali kalichopo walichelewa,walipokaribia walisikia sauti ya kilio waliyoitambua ni ya Madhifa! Hofu zikajazwa mioyoni mwao! Nini tena hiki jamani?? Walijiuliza huku wakiongeza kasi!!
kutokana na kaumbali kalichopo walichelewa,walipokaribia walisikia sauti ya kilio waliyoitambua ni ya Madhifa! Hofu zikajazwa mioyoni mwao! Nini tena hiki jamani? Walijiuliza huku wakiongeza kasi! Haraka waliingia ndani,mzee Patili bila kuchelewa alichukua madawa yake aliyoyabeba na kuanza shughuli ya kumpakaa dawa baba Madhifa alielazwa chini na kidogo alimmezesha kwa kumfungua kinywa,ilikua ni dawa ya kumrudisha kwenye fahamu,aliwaambia hivyo wakina Madhifa waliokua na hofu kubwa ya kumpoteza baba yao kama walivyompoteza mama yao,uzoefu wa mzee Patili kwenye yale matukio ulifanya jambo lisiwe gumu kihivyo,baada ya kupaka ile dawa aliwahitaji watulie ifanye kazi na baada ya muda kidogo itaonyesha matunda,aliutumia huo muda kwena kuangalia maiti ya mama Madhifa iliyokua imefunikwa gubigubi,ilimtetemesha mno na kumuogopesha,maiti ilikua haitamaniki na yenye kutisha kutokana na majeraha makubwa iliyonayo,shingoni kulikua na alama ya kamba iliyoashiria ya kwamba ilimkaba vilivyo,aliifunika kisha akayarushia macho yake kwa wakina Madhifa,hawakua na amani hata kidogo,roho ya chuki na kisasi ilichipukia mioyoni mwao,hofu ya kumpoteza baba yao na uchungu wa kumpoteza mama yao uliwafanya machozi yatiririke yakisindikizwa na kwikwi za kilio,aliwaonea huruma sana na kichwani akajiuliza leo hawa watoto watalala wapi?? Akatikisa kichwa kwa masikitiko kisha akaangalia anga lililokua kiza kuashiria giza lishaingia.
Baada ya muda usiopungua robo saa baba Madhifa alianza kupiga chafya! Alirudi duniani!! Wakina Madhifa hawakuamini lile tukio,ilikua ni kama miujiza mbele ya macho yao!! Haraka walimkimbilia baba yao kwa kutaka kumjulia hali,tabasamu zilizoambatana na machozi zilionekana kwenye nyuso zao,walimkumbatia baba yao kwa nguvu huku wakilia! Walitia huzuni,mzee Patili nae chozi lilimshuka taratibu,lile jambo lilimgusa wake moyo.
Hakukua na muda tena wa kupoteza,walifahamu hakuna msaada wowote wangeupata toka kwa wanakijiji na ukizingatia hawakuhuitaji hata kidogo,waliungana na wanakijiji wenzao na mzee Patili wakauzika mwili wa mama yao,hisia za kwamba alinyöngwa na wanakijiji zilifutwa baada ya mzee Patili kuwapa tahariri ya kua yale mauaji hayahusiki na mwanakijiji yoyote bali ni kwamba yanafanywa na jeshi la 666 lililowadhuru wale watu waliowaokoa japokua kwa kiasi kimoja yameleta mkanganyiko,hisia za uoga ziliwatetemesha na ukizingatia kwa ule usiku iliwabidi walale nje baada ya nyumba zao kuchomwa.
* * * *
pembeni ya nyumba ya mama Kurwa upande wa kushoto kulikua kuna mti mkubwa wa muembe ambao ukitoka huo nyumba ya mzee Yosso ndio ilikua inafuata,hali ya giza iliyokuwepo ilifanya mti ule kutoonekana vizuri na kutisha kidogo,pembeni yake alikua ameegemea mwanaume mmoja alieshikilia kamba mkononi akipiga mahesabu kichwani,ni lile jibaba pande la mtu lililowakosakosa wakina mama Halima,ni yule mnyongaji!!! Mungu wangu! Sasa lilikua ndani ya kijiji tena karibu na nyumba ya mama Kurwa na mzee Yosso au baba Matata,lilikua linafanya nini pale?? Hilo halikufahamika ila taratibu lilianza kujongea na kuusogelea mlango wa mzee Yosso au baba Matata,lilipokaribia liligonga mlango….ngo! Ngo! Ngo! Hodiiii! Kwa sauti ambayo haikuendana hata kidogo na mwili wake! Ilikua ni sauti ya kike tena ya mama Kurwa ambaye ni jirani!!… Karibuu! Alijibiwa tokea ndani,kwa kua halikua na lengo la kuingia ndani lilibakia pale nje likisubiri mlango ufunguliwe,mama Matata aliekua na mumewe ilihali na mwanae wakila ilimbidi ainuke taratibu na kuelekea mlangoni kumfungulia aliegonga,ni kosa kubwa alilitenda hakujua kama alipeleka nafsi yake kifoni!! Alipokwa kama pochi! Lile jibaba leusi kama giza lililokuwepo lilimbeba mama Matata na kuanza kupotelea nae maporini!! Makelele ya mama matata ya kuomba msaada yalisikika vizuri kutokana na utulivu wa mawimbi usiku hivyo kupelekea wanakijiji kushtushwa kwa kiasi kikubwa bila kusahau mumewe ambaye ndie aliekuwa wa kwanza kutoka nje kwa hamaki! Hakumuona mkewe! Alianza kukimbia kufuatilia sauti aisikiayo huku akiita jina la mkewe kwa nguvu! Ile sauti haikuskika tena! Ilitokomea na lile jibaba,ilitokomea porini!! Baba Matata hakuona kitu,mkewe akawa tayari ashakwenda!!
Alieka mikono kichwani huku akilia kama mtoto,hakua na la kufanya aligeuza na kuanza kurudi kijijini kichwani mawazo yakimsonga na moyoni hofu ikimtinga!! Akili yake yote ikawa sasa ni kwa mama Kurwa kwani sauti ya yule aliekua anagonga ilikua ni yake,alikimbia,alipofika kijijini alikuta watu wameshajazana,sauti ya mama Matata iliwatoa majumbani mwao hasa ukizingatia hofu zao zilishawashwa tokea mapema siku ile,minong’ono ilitawala,baada ya kumuona baba Matata,walimfuata na kumuuliza kilichojiri,hakujibu kitu,alimfuata mama Kurwa huku akitoa macho,akauliza kwa ukali!
“mke wangu yuko wapi???”
huku akimnyooshea kidole! Mama kurwa alibanwa na kigugumizi,hakua na la kujibu! Ghafla mmama mmoja akaropoka..
“jamani kuna mtu pale kwenye mti ananing’iniaa!!!”
alimnyookea moja kwa moja mama kurwa huku akitoa macho,kwa ukali akauliza!
“mke wangu yuko wapi??”
mama Kurwa alikosa cha kujibu,kigugumizi kilimbana,ghafla mmama mmoja aliropoka!
“jamani kuna mtu ananing’inia pale mti!!!”
Baba Matata aliachana na mama Kurwa na kukimbilia kwenye huo mti kushuhudia alichosikia,hakuamini macho yake kwa alichokiona! Alikua ni mkewe!! Alivishwa joho jekundu kitanzi kikimning’iniza! Damu zikiwa zinamtoka puani na masikioni! Aliishiwa nguvu za miguu akakaa chini na kuanza kulia!! Matata nae aliposhuhudia mwili wa mamaye unaning’inia katika ile hali kilio kilizidi kuchukua nafasi!! Baba na mwana wakawa wanalia kilio kilichoshindwa kutofautisha mkubwa na mdogo.Mwili wa mama Matata ulishushwa na kitanzi kikafunguliwa,wanakijiji walitawaliwa na hofu mara mbili ya ile iliyokuwepo mwanzoni,kushuhudia watu kunyongwa kwa siku mara tatu kama dozi haikua kitu cha kawaida,haikua kitu cha mzaha kabisa,ni kitu cha kuogopesha mno!! Kila mwanakijiji aliruhusu chozi la hofu na uchungu litoke huku wakiwa wanajiuliza mioyoni kwamba ni nani anaefuata sasa baada ya wale,miili ilikua inatetemeka na msamiati ‘hamu ya kulala’ haikua kabisa kwenye kitabu chao cha ile siku,nani alale kwa ile hali?? Hata mtu kukaa peke yake ilikua ni mtihani!!!
Wakati baba Matata na mwanae wakiendeleza kilio baadhi ya wanaume waliokuwepo pale walijivuta pembeni na kuanza kuteta jambo,
“sasa jamani ndio hivyo kama tunavyoona,tunazidi kutokomea! Sasa tunafanyaje sisi kama wanaume??”
alieleza mzee Rama,baba wa watoto saba akaae nyuma ya nyumba ya mama Kurwa,alikua ni kiongozi mkubwa wa kuwashawishi wanakijiji wakachome nyumba za wakina Madhifa,
“mh kusema ukweli hata mie naogopa hapa nilipo,ujue hiki kinatisha!”
“ah-ah! Kila mtu anafahamu kuhusiana na hilo,sisi kama wanaume tumejivuta pembeni ili tuangalie ni jinsi gani tutakavyolikabili,hatuwezi tukakaa tu hivi,tutakwisha!”
Mzee Rama alimdadavulia Tambwe alieonekana kutia mushkeli,
“kusema ukweli hili jambo si la mchezo hata nukta,mimi nadhani ya kwamba si binadamu wa kawaida anaefanya haya!…Nilisikia kwa masikio yangu sauti ya mama Matata ikielekea msituni lakini cha kushangaza tumemkuta kaning’inizwa kwenye ule mti!!”
mwalimu Baraka alichangia huku akiunyooshea kidole ule muembe,
“hata mie nahisi hivyo,hiki kitu kitatuwia vigumu sana,kumdhibiti mtu asiye wa kawaida yataka moyo ukizingatia hatujui hata yupoje!”
mzee Rama alisema,Lutiko aliekua kimya nae akachangia baada ya mzee Rama
“mi nadhani mtu mkubwa ataetusaidia ni mzee Patili,yeye ana ujuzi na haya mambo!”
“ni kweli! Hilo wazo zuri,nadhani mnaelewa ya kwamba nyumba ya mzee Patili ipo mbali na za kwetu na hata yaliyojiri hapa bado hayafahamu,sasa inabidi tumjuze!”
wazo hilo lilionekana kuungwa mkono na wale waume,kazi ikawa ni nani atakaejitolea kwenda kumpa taarifa mzee Patili,kila mtu alikua anahofia kwenda kule kwa kale kaumbali mwenyewe ilikua ni kama kujitoa sadaka,hakuna alietaka,kila aliechaguliwa aliuliza kwanini mimi?? Hivyo ikawa ngumu kufikia hitimisho.
Wakati hayo yanachukua nafasi Matata aliufata mwili wa mama yake na kuanza kuuangalia kwa kutoamini huku machozi yakimtoka,alijiuliza juu ya ile nguo aliyovishwa mama yake hakupata jibu,kuna kitu aligundua kwenye ile nguo haraka akaita Babaaa!! Sauti iliyowastua na kuwateka hisia wanakijiji wengine,baba Matata bila kuchelewa alifika eneo aliloitwa na mwanae akauliza
“nini mwanangu??”
huku macho yakiwa mekundu kama nyanya kwa kulia,
“kuna kitu kimeandikwa kwenye hii nguo aliyovalishwa mama!!”
“nini tena hiko??”
aliuliza Baba Matata,kutokana na kutojua kusoma aliamuru mwanae amsomee,matata akasoma kisha akasema..
“imeandikwa BADO KIDOGO!!!”
* * * * *
Baada ya shughuli ya mazishi kuchukua nafasi ilimbidi mzee Patili afunge safari ya kurudi kwake,aliwaaga wakina Madhifa waliokua wanatayarisha tayarisha kwa ajili ya usiku ule,walimshukuru kwa msaada na pia vilevile aliwahaidi atakuja kesho kuwasaidia shughuli za ujenzi,walifurahi kusikia hilo ila bado nyuso zao zilishindwa kujifungua kwa furaha,mioyo yao bado ilikua na huzuni.
Ilikua ni tendo la ajabu kwa mzee Patili kuondoka na kuelekea nyumbani mwenyewe kwa ule muda ukizingatia vitu vya kutisha vilivyochukua nafasi kijijini,alikua na hofu lakini hakutaka iwe sababu ya yeye kubaki,aliamini kama siku imewadia hawezi likwepa hilo,mikono aliweka nyuma na kwa kasi kidogo alikua anatembea akipita miti na vichaka huku sauti za wadudu wa usiku zikigota masikioni mwake na kumfanya ageuke geuke mara kwa mara,baada ya muda kidogo alikaribia na kwake,macho yake aliyoyarusha mbele yalimruhusu aione nyumba yake ya udongo vizuri,ghafla alisimama!! Macho yake yalimshuhudia pande la mtu likiwa linasogelea mlango wake na mkononi akiwa na kamba,hofu ikagota moyoni,mtu yule alikua mgeni machoni mwake na alihisi vibaya juu yake,akasogea karibu huku akinyatanyata aweze kumuona vizuri,mara lile jitu likagonga hodi Na mtindo ule ule alioutumia kwa mama Matata!!
akasogea karibu huku akinyata aweze kumuona vizuri,mara lile jitu likagonga hodi kwa mtindo ule ule alioutumia kwa Mama Matata! Nini hiki? Alijiuliza mzee Patili,kutokana na uoga wa watu waliokuwepo mule ndani tendo la kufungua mlango lilichukua muda,mama Kadogo na mzee Otongo hawakuweza kufungua
kutokana na miili yao yenye majeraha na maumivu kutowaruhusu,mama Halima na Julina walio wazima walikua na hofu hivyo kufanya lile zoezi lichukue muda kutendeka,lakini lile jibaba lililokuwepo mlangoni lilihisi kitu,lilipepesa macho yake huku likinusanusa na kugundua jambo,lilisikia harufu ya binadamu hivyo likafahamu ya kuwa haliko peke yake pale nje,haraka lilitoweka! Mzee Patili alijitahidi kufikicha zake mboni
lakini hakuona kitu! Alishangazwa mno na lile jambo,haraka alikimbia mpaka mlango ulipo na kuanza kubisha hodi huku akitamka kwamba yeye ni mzee Patili! Maswali na hofu yalijazana vichwani mwa waliokua ndani,mara ya kwanza walipoisikia hodi iliambatana na sauti ya kike ila sasa hivi wanaisikia sauti ya kiume tena ni ya mzee Patili! Walisita kufungua.
Tendo la busara lililofanywa na mama Halima la kuchungulia dirishani ndilo lililowashawishi kumfungulia mzee Patili baada ya kugundua ndie,aliingia ndani na kuwaeleza yote aliyoyashuhudia tokea alipotoka mpaka alipomuona lile jitu mlangoni,walishtuka sana na vilevile walishukuru hawakuifungulia hodi ile kwani ingekua
ni hadithi nyingine sasa hivi,mzee Patili alizidi kulielezea lile aliloliona..
“yule mtu alikua ameshikilia kamba nyekundu! Na hasa zinafanana na zile zilizotumika kuwanyongea wakina baba Tito! Hicho kitu kilinishangaza sana!”
“mungu wangu! Jamani tuhame hiki kijiji tutakwisha!”
kiuoga alinena Julina akiwa anamnyonyesha mwanae,
mama Kadogo akasema,
“sidhani kama hilo ni suluhisho,kila tutakapoenda watatufata mpaka pale watakapohakikisha ya kwamba lengo lao limefanikiwa!”
kauli ile iliwashtua mama Halima na Julina waliokua hawajui kiendeleacho,haraka wote wakauliza
“lengo! Lengo gani hilo??”
mama Kadogo akazidi kunyumbua,
“haya mambo yote yajiriyo ndani ya kijiji chenu yalitokea vilevile kijijini kwetu Igesambo,watu wetu wengi wa karibu wameuwawa na wengine wamejiunga kwenye jeshi la 666 lililo na itikadi moja tu ya kuusambaza utawala wa Ibilisi wao alieingizwa duniani,ilibidi tukimbie kuokoa maisha yetu kwasababu hatukutaka abadani kuungana na mashetani wale,lakini kuonyesha ya kwamba mungu yu upande wetu,alizaliwa mwana mwingine! Mwana ambaye ndie tumaini letu na vilevile anaweza akawa kifo chetu!”
“nani huyo??”
Julina aliuliza kwa papara huku akimtizamatizama mwanae,
mama Kadogo akaendelea,
“huyo mtoto ndie hasa lengo la hawa watutafutao na watuuwao,namaanisha jeshi la 666 kwani ni hatari kwao na huyo mtoto ndie hasa yatubidi tumlinde kwa hali zote kwani ndie tumaini na mwanga wetu,tukimruhusu afe,tumeruhusu utawala wa kiza!”
mzee Otongo nae akadakia
“mtoto huyo ana alama kwenye paja lake la kushoto kwa chini,alama ya nyota!”
mama Halima na Julina walishtushwa na ile kauli! Kwani mtoto yule alikua na hiyo alama! Macho ya Julina yakatoka kwa uoga! Huku akitetemeka akasema
“haiwezekani!! Ah-ah! Haiwezekani jamani,haiwezekani!!! Mtoto wangu! Hapana!”
* * * *
Bado wanakijiji walikua wamekusanyana mbele ya nyumba ya mama Kurwa na baba Matata,hakuna hata mmoja alieonekana na dalili wala hamu ya kurudi kwenye viota vyao na kulala,hali ilikua tete mno mioyoni mwao! Mada kubwa iliyokua inaongelewa ni juu ya ule ujumbe uliokutwa kwenye lile joho alilovishwa mama Matata baada ya kunyongwa uliosomeka BADO KIDOGO!! Hawakuelewa ulikua unamaanisha nini? Kila mtu alisema yake juu ya hilo.
Kutokana na hofu kulowanisha nafsi zao waliamua kukaa pale pale mpaka usiku utakapokwisha na kuiona adhuhuri,hawakua na lingine la kufanya zaidi ya hilo waliloona ya kwamba ni salama kwa maisha yao.Baba Matata na mwanae walikuwepo sebuleni,huzuni iliwafanya wakose cha kusema na kuwa kimya,ilikua ni
ngumu bado kuamini ya kwamba mtu waliekua nae muda si mrefu ni marehemu sasa hivi! Baba matata aliona mzigo wa majukumu waongezeka,Matata mwenye miaka tisa bado alikua anahitaji malezi ya mama yake na ukizingatia yeye si mkaaji nyumbani,kichwa kilivuruga.
Ghafla upepo mkali ulipiga lile eneo!! Upepo usio wa kawaida kabisa!! Vibatari vilivyokua vinatoa mwanga vyote vilizima na kufanya giza totoro kushika hatamu!! Wakina mama walipiga makelele ya uoga na kila mtu hofu iliita ndani yake! Miili ilitetemeka kwa uoga,mioyo ilizizima kwa hofu!!
Mchakato wa kuwasha vibatari ulipofanikiwa watu wawili hawakuonekana!! Hawakujulikana walielekea wapi…hawakujulikana walibebwa na nani!! Mtoto mmoja wa mzee Rama na mmama mmoja wa makamo walishabebwa!!!
Mungu wangu! Sauti zao zilisikika zikiishilia kama ilivyokua kwa mama Matata!!
Matumbo yalichemka,jasho liliteremka!! Wengine walizirai kwa uoga,na wengine walitamani kujimaliza!!!!
Sehemu Ya 4
Matumbo yalichemka,jasho liliteremka!! Wengine walizirai kwa uoga,na wengine walitamani kujimaliza!!
Vilio vya wamama na watoto vilimeza ukimya wote wa usiku,ile sehemu haikukalika kabisa! Wake waliwakimbilia waume zao ilihali na watoto vilevile!
Mzee Rama na mkewe waliumia sana kumpoteza wao mwana,japokua walikua saba lakini hawakuhitaji kumpoteza hata mmoja wao machoni pao,machozi vilio na mafua ya uoga na uchungu vilitawala,kila mtu akawa anatizamatizama nyuma kwa hofu ya usalama wake binafsi.
Wakati taharuki bado imeshika nafasi,miili ya watu waliobebwa koroboi zilipozima ilionekana tena ikining’inia kwenye ule ule mti wa muembe aliotundikwa mama Matata!! Mavazi yao waliyokua wamevaa
hayakuonekana wala kujulikana yalielekea wapi,walikua wamevishwa majoho mekundu kama alilovishwa mama Matata na yote yakiwa na ujumbe ule ule uliosomeka BADO KIDOGO!! Masikio yao na midomo ilikua inavuja damu na huku macho na ulimi vikiwa vimetoka nje!! Walitisha sana,hasa wakionekana wakibembea na kamba zao nyekundu shingoni! Idadi ya waliokufa na kamba kwa ile siku ikawa ni tano tayari.je mchezo
utaendelea vilevile?? Na sasa ni yupi alie kwenye zamu?? Maswali hayo yalijaza vichwa vya wanakijiji.
Ilibidi kifanyike kitu sasa,kukaa tu pale kwa kutegemea ni salama ilikua si sahihi,mzee Rama na mwalimu Baraka walijitolea kwenda kwa mzee Patili kwa lengo la kumpa taarifa ili awasaidie kwa lolote kunusuru maisha yao yaliyo mikononi,waliwaaga wanakijiji huku wakiwaomba wawaombee wafike salama kwani safari
iliyombele yao ni ya kutisha,hofu ilikuwemo mioyoni mwao lakini hakuna jinsi jambo lile ilibidi litendeke,mke wa mzee Rama na wanae sita waliobaki walikua hawana matumaini kama baba yao atarudi,walimuangalia kwa huzuni huku wakimpungia mkono wa kheri,mwalimu Baraka nae alikua anajilaumu nafsini kwanini alikubali kuja kufundisha kijiji kile,ndio serikali ilimpangia lakini aliona alifanya kosa kuja lile eneo,ni bora angekataa hata kama ingehatarisha kibarua chake,mambo yanayojiri yataka moyo.
Safari ilianza,taratibu mwalimu Baraka na mzee Rama wenye baraka za usalama kutoka kwa wanakijiji walikua wanajongea,hofu waliyonayo mioyoni iliwafanya washindwe kujizuia kugeukageuka nyuma na mioyo kwenda mbio,lakini nyuso zao zilificha hayo,kila mmoja alikua anataka kudhihirisha kwa mzenzie kwamba haogopi.
Wakiwa kwenye mwendo mwalimu Baraka aliitoa simu yake iliyofeli mtandao tokea majuzi kwa lengo la kujua wakti,alishtushwa sana na alichokiona,muda uliokua unaonyeshwa na simu yake haukumwingia kabisa akilini! Ni muda mrefu umepita tangu giza liingie lakini bado saa ilikua inasema ni saa MOJA NA NUSU
USIKU!! lile jambo lilimfanya mwalimu Baraka ahisi saa yake imepoteza majira lakini bado alipata maswali kichwani kwamba hii tabia ya kupoteza majira imeanza lini kwani alikua ameiseti saa yake hivyo hata likitokea jambo lolote bado majira huwa palepale,alipata hofu lakini hakutaka kumshirikisha mzee Rama,alinyamaza na safari ikaendelea,lakini ukweli ni kwamba muda ulikua hausogei,yani ulisimama palepale!
* * *
Julina baada ya kupewa somo zito na wenzake,aliituliza hofu yake,akatambua thamani ya mwanae na hakuwahi tarajia kwamba angekua mtu wa kumzaa mtoto ambaye angehitajika kwa ule muda,alijivunia hilo.Mzee Otongo hakutaka kumficha Julina,bayana alimjuza ya kuwa asipoteze muda kumsubiria mumewe kwani ni dhahiri atakua ameuwawa na Jeshi la 666 tangu yeye ni baba wa kiumbe hatarishi kwao,hii habari
ilimsikitisha sana Julina japokua nae alikua na hisia hizo hizo japo hakua na uhakika,chozi lilimdondoka,alimpenda sana mumewe Kitanzi na hata ndoa yao haikufikisha hata miaka miwili,bado alikua na hamu nae na ukizingatia hajamuona mtoto ambaye mkewe alimleta ulimwenguni,ilitia huruma.
Kila mtu alie mule ndani aliuona usiku ni mrefu,walitamani kuona mwanga wa jua ukipendezesha tena macho yao,waliona usiku ni hatari kwao hivyo mioyo yao ilishikwa na tamaa kubwa ya kuona tena miale ya jua itakayoamsha matumaini yao,sauti za wadudu ziendeleazo huko nje zilizidi kuwaogopesha,hasa Julina.
Ngo! Ngo! Ngo! Sauti toka mlangoni iliwasili masikioni na kuwashtua kidogo,kama kawaida mama Halima alikimbilia dirishani na kuchungulia ni wakina nani,kisha akawatonya wenzie “ni wakina Madhifa!”
“wafungulie!”
mzee Patili akasema,
wakina Madhifa waliingia ndani kwa haraka huku wakihema kwa nguvu hali iliyowatisha na macho yao yalikua yanamimina machozi,kwikwi ikiwabana na kuwazuia kusema walilodhamiria,ilibidi mzee Patili awatulize kwanza ili waweze shusha presha na kusema kilichowaleta,baada ya kutulia wakasema
“Mama Linda na mumewe wamenyongwa!!”
kauli hiyo iliwafanya wakina mzee Patili mioyo ipasuke kwa mshangazo na kuanza kwenda kasi!!! Ilikua ni kama tamthilia kwenye masikio ya mzee patili aliewaona hao watu muda si mrefu,wakiwa kwenye taharuki na butwaa wakasikia hodi tena!! Ya Mara hii ilikua ni ya wakina mzee Rama na mwenzie mwalimu Baraka! Je itakuaje?
Nao pia wakasema kilichowaleta,watu watatu ambao ni mama matata,mtoto wa mzee Rama na mmama mmoja wa makamo wamenyongwa katika mazingira ya kutatanisha na aliewanyonga hajulikani,kwa ujumla taarifa za vifo zilizomfikia mzee Patili zilikua tano!! Alishangazwa na hiyo
idadi,na si tu yeye hata wakina mzee Otongo na wakina Julina!! Hofu ziliwashika mpaka kwenye ukucha,puh! Julina akadondoka na kupoteza fahamu!! Mtoto aliekua amembeba aliwahiwa
haraka na mama Halima na ilikua rahisi kwake kwa kua walikaa karibu,shughuli za kumpepea kumrudisha kwenye fahamu zikaanza haraka!! Mzee Rama na mwalimu Baraka wakapata kibarua cha muda cha kupepea huku wakina Madhifa wakiwa tu pembeni wakishuhudia hayo,uadui bado uliwatenganisha.
Baada ya kamuda kadogo Julina alirudi kwenye fahamu zake.
Uhasama uliokuwepo baina ya makundi mawili yaliyokuwepo pale ulionekana dhahiri,wakina Madhifa walijitenga kabisa na wakina mzee Rama kwani ndio wanahousika na uchomaji wa
nyumba zao,vilevile mzee Rama hakujumuika nao kwa kudhani ku yote yajiriyo chanzo ni wao na alikua anawatizama wakina mzee Otongo kwa jicho baya kutokana na imani yao kua wale wageni pia huchangia kutokea kwa hali husika,mwalimu Baraka yeye hakua upande wowote kwani yeye si mwenyeji pale kijijini,mzee Patili aligundua huo mkanganyiko,kazi ya kuwatuliza wale watu wenye imani tofauti ziendeshazo mioyo yao ilibidi ifanyike,aliamini ya kua umoja utakaokuwepo
baina yao ndio utakaokua silaha kubwa ya kujilinda na kukabiliana na linalowasibu,elimu hasa juu ya kinachoendelea ilihitajika kwenye vichwa vyao na vya wanakijiji wote ili iwe kama chachu ya mabadiliko na mwanzo wa mapambano,alitumia busara,aliwauliza wakina mzee Otongo kama
wanaweza jongea wakajibu watajitahidi,akawapa ujumbe wakina Madhifa ya kwamba wakawaite wenzao yani jamii ya wawindaji na wakutane kwa mama Kurwa,walitii walichoambiwa,wakatokomea kwenda kuwasilisha,kisha akawaambia wakina Julina na wakina
mzee Otongo wainuke na safari ianze ya kuelekea huko walipotokea wakina mwalimu Baraka,yani kwa mama Kurwa ambapo ndipo wanakijiji walipokusanyika,akachukua vibuyu vyake viwili kisha safari taratibu ikaanza wakiwemo watu nane;mama Kadogo na mzee Otongo
waliokua wanachechemea,Julina na mama Halima aliembeba mtoto,mzee Patili mwalimu Baraka na mzee Rama.Japokua walikua wengi lakini bado kale kamchezo ka kuangaliangalia nyuma hakakukoma,kila kaupepo kalipopiga miili yao iliiteka misimko ya kioga hasa Julina
alieng’ang’ania awe katikati ya watu,ni sauti za miguu yao tu ndio ilyosikika walipokua wanapita,kote kulikua kimya ukiondoa vikelele vidogodogo vya vijidudu vya usiku,muda huo wote waliokua njiani mzee mzee Patili alikua anafanya kazi ya kuvitikisa vile vibuyu vilivyomkononi,haikujulikana kazi yake ni nini na hakuna mtu aliemuuliza,walimuacha afanye mambo yake kwa uhuru.
Hatimaye walifika walipokua wanaelekea,watu waliokua wamejikunyata kwa kukosa matumaini waliamka na kumlaki mzee Patili,aliwapa mwanga wa kufanikiwa,akikua mwema kwao kwa ule muda,walisahau kabisa walichokifanya huko nyuma,ila ujio wa wakina mama Kadogo na mzee Otongo uliwashtua wanakijiji,moja kwa moja minong’ono ikaanza kururuma….mzee Patili hakuvumilia hilo,aliufungua mdomo wake kwa ukali akasema
“acheni upumbavu wenu usio na msingi!! Huo ujinga ndio upelekeao hali kua mbaya zaidi na hautupi unafuu wowote! Nani asiemjua huyu mzee Otongo?? Si nawauliza nyie! Ni mara ngapi alikua anakuja hapa kijijini na kuwasaidia matatizo mbalimbali?? Iweje leo unaufungua mdomo wako na kumnyooshea kidole,mshausahau wema wote alioutenda kwenu? Mbona mnakua na vichwa vya panzi na mioyo y kutu!”
wanakijiji wote walitulia na kusikiliza kwa makini na roho zao zilianza kuwasuta,mzee Zptili akaendelea kunena…”umoja wetu ndio unaohitajika,kugawanyika kwetu ndiko kunapoipa mwanya kushindwa kwetu,nawaambia kama tusipokua pamoja,shingo zote zilizokuwepo hapa zitaonja kamba nyekundu kama waliopita!! Tutanyongwa kama kuku!!”
alizidi kusisitiza kwa sura ya mkazo,muda si muda wakina Madhifa wakaingizana,ukimya bado ukawa umetawala,masikio na macho yao alipewa mzee Patili aliesimama mbele.Baada ya mzee Patili kurudufisha imani za waliokua wanamsikiliza,aliwakaribisha wakina mzee Otongo na mama Kadogo kwa lengo la kutoa somo juu ya hali iliyojiri,waliwadadavulia na kuwanyumbulia wanakijiji kwa undani tangu walipotokea na nini kimewaleta hasa.
waliwadadavulia na kuwanyumbulia wanakijiji kwa undani tangu walipotokea na nini kimewaleta hasa.Maneno na maelezo yaliyotolewa na wakina mzee Otongo yalionekana kuwatisha zaidi wanakijiji,habari za jeshi la 666 zilikua ni za kuogofya na zenye kutaka ujasiri kuzisikia,hakukua
na jinsi ilibidi waambiane ili wapate pa kuanzia,elimu hasa iliyokua inatolewa juu ya kiendeleacho ndicho kilikua cha kwanza kisha hayo mengine yachukue nafasi,zoezi lilifanikiwa na kumalizika salama huku likianzisha ukurasa mpya wa maisha yao ambao walikua hawajautambua,nia na
nguvu yote ya wanakijiji ilielekezwa juu ya kumlinda yule mtoto aliezaliwa na mengine pia kama watakavyoelekezwa kufanya na viongozi wao waliowateua ambao ni Mzee Patili,mama Kadogo na mzee Otongo,hakukuwa na ubishani tena wala minong’ono isiyo na msingi,sasa kila tendo lililochukua nafasi lilikua ni maelekezo dhabiti toka kwa viongozi wao,hakuna alietia dosari.
Mzee Patili aliwataka wanakijiji wajipange mistari miwili ya kijinsia,bila kuchelewa wakajipanga,alivichukua vibuyu vyake na kimoja akamkabidhi mama Kadogo kisha akampa maelezo madogo tu yaliyofanikisha kumjuza kiendeleacho,zoezi la kuwapaka wanakijiji dawa
usoni na mikononi kwa lengo kuu la kudhoofisha nguvu za adui wao lilichukua nafasi,mzee Patili akiwa anapakaa mstari wa wanaume na wavulana huku mama Kadogo akiwa anashughulika kwenye mstari wa wanawake na wasichana,idadi ya wanakijiji iliyokuwepo haikuendana na kiasi
cha dawa husika hivyo ilipelea,watu kama ishirini hawakua wamepakwa dawa kitu kilichompa maswali mzee Patili juu ya nini hasa cha kufanya,baada ya kufikiria kidogo aliwachagua wanaume wawili (mrisho na tabwe) kisha akawaagiza waende nyumbani kwake kwa lengo la
kuchukua dawa ili apate malizia waliobaki,ujasiri waliopewa na dawa walizopakwa ziliwafanya wasijifikirie mara mbilimbili,haraka walijiondoa lile eneo na kueleke walipotumwa.
Wakati hayo yote yanachukua nafasi lile jibaba linyongaji lilikua likishuhudia,kwa mbali lilijificha
kwenye mapori ila macho yake mekundu makubwa yalimfanya aone vizuri kilichokua kinafanyika,hakua peke yake kwa sasa hivi kama ilivyokua,pembezoni yake alikuwepo mwanamke mmoja mwenye macho ya paka na ulimi mwekundu!!! Alijivika kaniki nyeusi na
kiremba chekundu kilichositiri mapembe yake vizuri,ngozi yake ilikua na rangi ya kijivu na masikio yake yalikua marefu ilihali na kucha za mkononi,sasa walikua wawili kwa idadi,jeshi la 666 liliongeza mashambulizi!!! Wanakijiji watahimili hili??
Lile pande la mtu jeusi na yule mwanamke mithili ya paka walitabasamu na kuruhusu meno yao ya kutisha kuonekana,walipeana ishara,wakashika njia na kuelekea kule wale wanaume walipotumwa,yani kwa mzee Patili kwa lengo la kuzuia zoezi la uletaji dawa,lile Pande la mtu mkononi lilishikilia kamba nyekundu kama ilivyokawaida yake na yule mdada mithili ya paka akiwa na kisu kirefu!!!
Matamanio yao ya kuua bila kuchelewa na kufanikisha lengo lao yaliwafanya wajione wanachelewa kwa kutembea,hivyo walianza kukimbia huku macho wakiwa wameyatupia mbele!!
* * * * * * *
mrisho na mwenzake walishafika eneo husika,walikua ndani ya kijumba cha mzee Patili wakifanya jitihada za kusaka dawa waliyotumwa,uwepo wa dawa nyingi mule ndani ulifanya zoezi liwe gumu kwani kila dawa waliyoipata walipoinusa waligundua sio yenyewe,ilichukua kama
muda wa dakika saba mpaka walipoitia mkononi iliyolengwa,waliangaliana kwa tabasamu kisha wakaelekea mlangoni,Mrisho aliunyoosha mkono wake na kuuvuta mlango,mlango ukagoma kufunguka!! Alizidi kutumia nguvu zaidi lakini bado matokeo yakawa yaleyale,mlango uligoma
kabisa kufunguka!!! Ikabidi amuachie Tabwe nae ajaribu lile zoezi,hakuna aliefanikiwa,bado hawakuweza kuufungua,hofu ilianza kuchochewa mioyoni mwao,wakaangaliana kwa uoga huku kajasho kakitirika,Tabwe huku akitetemeka akasema..
“Mrisho..tunakufa…!!”
Mrisho akameza mate,moyo ulikua unampwitampwita na macho yakimtoka,alipata wazo kichwani haraka akamwambia mwenzie
“Tabwe…tu..tu..tuvunje mlango!!!”
Tabwe alionekana kukubaliana na hilo wazo lililoonekana ni pekee kwa ukombozi wao,bila kuchelewa harakati za uvunjifu zikaanza kikamilifu kwa kutumia mateke,hawakua na habari ya kuwa lile jibaba linyongaji na yule mdada mithili ya paka walikua kwa nje wakiwasubiri kwa
hamu zote ili kuongeza idadi ya waliokwenda na maji na kusafisha njia ya kufanikisha lengo lao,puh!! Mlango ukatupwa kule na nguvu ya teke zito la wakina Mrisho!! wakatoka nje,he!!! hawakuamini walichokiona!! Kitendo cha kugonganisha macho na yule mdada mithili ya paka
lilikua ni kosa kubwa!!! Walinyong’onyea na kupoteza nguvu,wakadondoka chini kama mizigo tii!!! Lile Jibaba likasogea karibu yao huku likitengenezea vitanzi tayari kwa ajili ya
kuwanyonga,macho ya yule mdada yalishalainisha zoezi kwa kudhoofisha ile dawa waliyopakwa hivyo kuruhusu zoezi la unyongaji kuchukua nafasi kama kawaida!!!!
Lile jitu baada ya kuwafunga vitanzi wakina Mrisho alianza kuwaburuza kama nyama!! Halikujali kitu chochote juu yao na wala sura yake haikuonyesha hata chembe ya kulifikiria hilo.Walipowadia kwenye mti mmoja wa mkuyu,waliwatundika wale watu,wakaungana na shingo zingine zilizoonja kamba nyekundu, utofauti wao na wale waliotangulia ni kwamba wao walinyongwa bila mioyo yao iliyochukuliwa na yule mdada mithili ya Paka aliekua na mahitaji nayo,walibaki na mashimo tu yaliyokua yanamimina damu!!!
Ile Mioyo iliingizwa kinywani mwa yule dada na moja kwa moja ilianza kutafunwa mithili ya keki huku lile jibaba likishuhudia,baada ya kumaliza lile tendo ghafla walibadilika na kuchukua sura za waliowauwa!! Lile jibaba liligeuka na kua Tabwe huku yule mdada akiichukua sura ya Mrisho!! Taratibu huku wakiwa wameshikilia mifuko isiyojulikana ilitokea wapi walianza safari ya kuelekea kule wanakijiji walipo!! Hapakukalika tena!! Hatari ilizidi kuchukua nafasi!!
* * * * * * *
Baada ya muda mrefu kupita bila ujio wa wakina Mrisho mzee Patili na wanakijiji wengine walianza kupata hofu,akili zao zilianza kuruhusu mawazo mabaya kupenya na mioyo yao ilianza kupokea taarifa za simanzi,wanakijiji waliokua hawajapakwa dawa walikua na hofu mara mbili kwani wao walijiona si salama ulikilinganisha na wenzao,walitamani wakina Mrisho waje haraka ili nao miili ipate kunawiriwa na dawa ambayo waliiamini kwa asilimia zote itakua kinga madhubuti kwao dhidi ya hali endelevu,walisali mioyoni,waliomba sana mungu wao apate kutanakabali sala zao.
Muda si muda Mrisho na Tabwe feki waliingia,wanakijiji waliokwisha kata tamaa walilipuka kwa furaha na kuwalaki kwa upendo ulioonyesha matumani,masikini ya mungu hawakufahamu kwamba wale siyo,mzee Patili aliupokea mfuko aliopewa na haraka akawaambia wale waliokua bado hawajapakwa wajipange mstari,wakapanga,akaanza kuwapakaa kama ilivyokua mwanzoni ila sasa hivi alihusika kwenye kuwapaka wote yani wanaume na wanawake wakiwa wamepanga mstari mmoja tu,kutoka na dawa waliyopakwa wanakijiji wengine Tabwe na Mrisho walishindwa kustahimili,walisogea pembeni mbali na wanakijiji wengine,kujitenga kwao kulimpa kidogo maswali mwalimu Baraka alieamua kuwafuata kwa lengo la kuwapongeza kwa ujasiri wao,alipowakaribia aliwapa mkono wa kheri uliopokelewa na Mrisho ambaye ni yule mdada mwenye roho ya paka,kha!! Alishtuka mno mwalimu Baraka!! Mkono wa Mrisho ulikua wa baridi mno mithili ya barafu,hali hiyo ilimpelekea autoe mkono wake haraka na kuuliza…
“we Mrisho mbona mkono wako wa baridi hivi???”
“kawaida tu,si unajua tulikua tunakimbia ili tuwahi!!”
alijibu Mrisho,mwalimu Baraka hakuridhika na lile jibu hivyo akauliza tena
“sasa kama mlikua mnakimbia mbona mlichelewa??”
swali hilo lilifanya kidogo Mrisho akwame,alimuangalia mwenzie Tabwe aliewahi akajibu,
“tatizo kule kwa yule mzee ndo’ kulituchelewesha,madawa yaliku mengi mno!!”
“ah-ahaa! Ila poa haina tatizo,hongereni bwana kwa ujasiri wenu mliouonyesha! Bella alikua ana wasiwasi kweli..teh! Teh!”
mwalimu Baraka alimtania Tabwe kuhusu mchumba wake Bella,cha ajabu uso wa Tabwe ulimdhihirishia mwalimu Baraka ya kua halikua hajui kiongeleachwo,
“Bella?? Ndio nani??”
aliuliza Tabwe swali lililozidi kumshangaza mwalimu Baraka!!
Moyo wa mwalimu ulisita,alipata hofu,hakutaka kukaa tena pale,taratibu aliaga na akajiondoa lile huku maswali kichwani yakizidi kupapaliwa na kuchipukia.
Lile jibaba lilimuangalia mwenzie alie ndani ya sura ya Mrisho kisha akamuuliza..
“unadhani atakua amegundua chochote??”
“sidhani,ila kama ukiniuliza ni moyo wa nani ninaoutaka kwa sasa,dhahiri nitakujibu ni wake!”
“ile dawa waliyopakwa nayo itaanza kufanya kazi muda gani? Mbona kama inachelewa??”
“tuliza munkari,ipe kama nusu saa,utaona majibu yake nadhani unafahamu huwa sibahatishi”
alijigamba bimdada,
“nafahamu hilo,ila ile dawa waliyoipakaa ni kali mno! Nadhani uliona jinsi tulivyokua tunapata shida alipokuwepo yule mbaba”
“ni kweli,ila siwezi kuondoka mpaka nione ikifanya kazi!”
“sawa.”
maongezi yakakomea hapo.
Hayawi hayawi yakawa!! Dawa waliopakwa watu wa awamu ya pili ilianza kufanya kazi bara-bara!! Miili yao ilianza kuwasha hatari!! Na kila walipojikuna ngozi ilitoka na kuruhusu damu iruke kama bomba!! Makelele ya kuomba msaada yaliteka ile sehemu!! Muwasho wa ajabu usiovumilika uliwafanya wawe machizi kwa kuranda huku na kule wakipiga makelele kwa nguvu!!!! Mzee Patili alishikwa na butwaa!! Wanakijiji walitawaliwa na taharuki!! Walipotizama wakina Mrisho wako wapi,HAWAKUWAONA!! Mungu wangu!! Wale waliokua wanawashwa wakaanza kukauka na kuwa magofu meupe kama chumvi!!
Wale waliokua wanawashwa wakaanza kukauka na kua magofu meupe kama chumvi!!!
Kilio kilichobeba uchungu na uoga kilipata kutoka vizuri toka kwenye midomo ya wakina mama na watoto,vilevile mioyo ya wakinababa ilikita kwa nguvu na macho yao yalitoka kwa kutoamini,ulikua ni kama mchezo wa kuigiza,sehemu ile yote ilitawaliwa na magofu ishirini na mawili yote yakitokana na ile dawa ya awamu ya pili! Wanakijiji walipungua kwa kiasi kikubwa,watoto wengi walipoteza wazazi,wanawake wengi walipoteza waume zao,na hata vile watu wengi walipoteza watu wao wa karibu,simanzi iliyoje!!!
Mzee Patili alichanganyikiwa kabisa,hakujua cha kufanya japokua mzee Otongo alikua anajitahidi mno kumtuliza,alijiona yeye ndie muuaji na hata baadhi ya wanakijiji walianza kufikiria hivyo,walifikiria ya kwamba vile vifo ni dhahiri vimesababishwa na mzee Patili ilihali wengi wao bado walikua kwenye tahamaki ya njia panda hasa baada ya wale walioleta dawa kupotea kiajabu machoni mwao!!
Mama Kadogo aliutumia ule mwanya kuita rai na kuteka hamsha za wanakijiji,kwa kujiamini alisimama mbele yao na kusema
“Jamani..jamani!! Naomba tusikilizane! (ukimya ukatawala lakini bado vikwikwi na vimafua vya vilio vilikua vinachukua nafasi)….katika vita hii tunayopambana nayo kufa kwa mtu au watu isiwe kitu cha kutushangaza,mtu yeyote kwa muda wowote anaweza akafa kwenye mapambano haya hilo inabidi liwe kichwani,naomba tusiruhusu roho za simanzi ziweke kiza kwenye njia yetu bali roho ya ushupavu na ya kusonga mbele,ni hakika tumezidiwa akili na hili jeshi la 666 katika huu mchezo,waliutumia ipasavyo ule mwanya tuliowapa wa kuwatuma wale vijana,nadhani hilo halina maswali…tumeona kwa macho yetu walivyopotea kiajabu na kuudhihirishia uma ya kwamba wao sio wale tuliowategemea!”
haraka Mwalimu Baraka alidakia
“hakika mama,hakika!! Wale hawakua wakina Mrisho kama tulivyodhani,mie mwenyewe naweza nikasema hivyo kwa ushahidi wangu mdogo nilioushuhudia,walikua ni watu wa baridi mno! Na hata baadhi ya maswali niliyowauliza walishindwa kabisa kujibu,kusema ukweli nilipata hofu lakini sikuwa na uhakika asilimia mia hivyo nikaamua nijitoe lile eneo kimyakimya!”
maneno hayo ya mwalimu Baraka yaliamsha minong’ono miongoni mwa watu,mama Kadogo aliwatuliza na kisha akaendelea kunena..
“ni matumaini yangu dawa tulizopaka zina msaada kwetu,bado ninaamini hivyo japokua hili tukio la wakina Mrisho linaweza kuwatia mashaka mioyoni,hapo ndipo tunapoweza kurudia kauli yangu ya mwanzoni ya kwamba walituzidi akili,nahisi kuna kitu walichokifanya hawa jeshi ambacho bado hatujakifumbua….”
(kabla hajamalizia mzee Rama kwa jazba alidakia)
“sasa tufanye nini?? Hamuoni ya kwamba tunaendelea tu kufa!! Au nyie bado hamjatosheka???”
kauli ya mzee Rama ilizua tena minong’ono na malumbano,baadhi ya wanakijiji walionekana kumuunga mkono na baadhi yao walionekana kumpinga,makundi mawili yakazaliwa miongoni mwao!! Ni dhahiri imani zao haba zilianza kuwachonyota,mzee Patili taratibu alisimama na kuelekea pale alipo mama Kadogo kisha akawaomba utulivu kwa muda ili apate kunena,wale waliokua bado na imani nae walifunga midomo yao na kumpa masikio lakini wale ambao imani zao zilitiwa doa hawakujali hilo,waliendelea kururuma tu,mzee Patili akatoa tamko..
“kama imani yako haiko nami tena,sitofanya jitihada zozote kuiinua maana umeamua hivyo,kama nilikua nanyi tokea ujana nikiwahudumia na bado imani zenu zina madoa kuhusu mimi,hakuna chochote ninachoweza fanya kwenu kwa sasa.Ninaelekea upande wa kulia nilipotokea,kama bado una imani nami waweza nifuata,kama huna imani nami waweza kubaki..”
sura ya mzee Patili ilionekana si yenye furaha,alikua anawaza jambo na dhahiri alionekana ameumia,alishika njia ya kuelekea nyumbani kwake na kundi la watu huku nyuma lilimfuata akiwemo Julina mwenye mtoto aliebeba matumaini yao,bila hata kuonyesha aibu usoni mzee Rama nae na wenzake walioonyesha kutia shaka juu ya mzee Patili nao walikuwemo ndani ya msafara wakiivuta miguu yao kumfuata,hawakufanya hivyo kwa kupenda bali iliwabidi kwani mtoto ambaye ndie ngao ya matumaini alikua upande ule hivyo hawakua na jinsi,mzee Rama bado alikua na gubu jeusi lililokua linamkereketa,hakupendezewa kabisa na ile hali ya uongozi wa mzee patili,wivu ulimkua unamsumbua kwa kiasi kikubwa,alitaka yeye ndie awe anasikilizwa na yeye ndie awe anatoa amri,wivu ulimshika mishipa yake ya damu,akili yake ilimtuma amuibe yule mtoto wa Julina,alifahamu fika ya kua akimmiliki yule mtoto jamii nzima itamsikiliza yeye kwani ndie atakaekua ameshikilia matumaini yote ya wanakijiji,atafanyaje sasa?? Alijiuliza kichwani mwake,baada ya kupata jibu haraka alimvuta mwenzie pembeni na kumwambia..
“unataka kufa na wewe,ama??”
swali hilo lilimshangaza alieulizwa,kiuoga nae akajibu..
“hapana!!”
“sasa nisikilize nitakayokuambia…”
“unataka kufa na wewe ama??”
swali hilo lilimshangaza alieulizwa,kiuoga nae akajibu
“hapana!”
“sasa nisikilize nitakayokuambia..”
“enhe..”
“najua wewe ni mwenzangu na ninakuamini hautoniangusha,hivi we unadhani haya yote yanayojiri ni sababu ya nani??”
“mh…kusema ukweli mie sijui!”
“we unahisi ni nani??”
“mmmh….labda ni hawa wageni au….”
“ah-ah! Hawa wageni waliruhusiwa na nani??”
“…….mzee Patili!”
“unavyodhani ni nani sasa hivi anatuua??”
“si lile jeshi la 666 walilotuambia!!”
“..kwani wale ndio waliowapakaa nyie dawa??”
“hapana! Ni mzee Patili!”
“majibu yote yapo wazi kama unavyoona,huyu mzee ndio kikwazo kwetu,na hivi ninavyokuambia ni kwamba lengo lake si kukabili jeshi la 666 kama anavyotudanganya bali anataka amtumie yule mtoto kwa malengo yake binafsi,yani kujinyanyua na kufanikisha hamu yake ya uongozi!! Hivyo basi ili atudhoofishe na asafishe njia yake anatupunguza idadi kama unavyoona…!!”
haikuishia hapo tu,kukaa kwake nyuma ya ule msafara alikutumia kama ngazi ya kuigeuza mioyo ya wanakijiji,alipenyeza uongo kwa walio karibu na kufanikiwa kuiteka mioyo yao yenye imani haba,na alitamani zaidi.
Baada ya muda msafara wa wanakijiji uliwasili kwa mzee Patili,walishangazwa na hali waliyoikuta ikiwemo mzee Patili mwenyewe,mlango haukuwepo sehemu yake na mwanga wa mwezi uliokuwepo uliruhusu kuonekana unga fulani wa manjano chini mzee Patili aliougundua kwamba ni dawa ile aliyoiagiza,alama za miburuzo zilizokuwepo chini ziliwatia mashaka hivyo
wakasogeza koroboi na kuanza kuzifuatilia mpaka pale zilipowafikisha kwenye miili ya wakina Mrisho iliyokua imetundikwa!
Macho yaliwatoka kwa kushuhudia zile maiti zilizokua zinaning’inia na mashimo vifuani,machozi na simanzi havikuzuilika kuwa miongoni mwao,miili ile ilishushwa na kumpa ruhusa mzee Patili kuikagua kisha akatoa neno..
“watu waliotumwa ni wazi walivamiwa! Nadhani mazingira husika yanaeleza hivyo,dawa niliyoiagiza tumekuta imemwagika,mlango umevunjwa,vilevile wamenyongwa! Hiki ni kielelezo tosha ya kua dawa iliyoletwa kule haikua sahihi..”
alivuta pumzi kidogo kisha akaendelea
“miili ya wakina Mrisho japokua imenyongwa kama ile mingine lakini kuna utofauti juu yao,utofauti huu unatudhihirishia ya kwamba kuna kiumbe kingine ambacho ni hatari kwetu kimeongezeka,na ndio hasa kinachohusika na hii mioyo iliyobebwa! Inatubidi tuongeze kinga yetu!”
mzee Patili akanyamaza kidogo,ila taratibu mzee Otongo alimkaribia na kuanza kumnong’oneza kitu hali iliyohamsha vimaongezi vya chinichini hasa kutoka kwa mzee Rama aliekua anapigilia misumari maelezo yake ya uongo aliyoyaingiza ndani ya vichwa vya watu huku akihakikisha mzee Patili hagundui hilo.
Baada ya mzee Patili na Otongo kujadili waligundua cha kufanya japokua ilikua vigumu kuwaeleza watu,kazi ngumu ilibidi ifanyike na pia ilihitaji watu jasiri watakaojitolea kuifanikisha,baada ya kujiulizauliza sana mzee Patili aliamua apasue jipu,
“tunahitaji dawa kwa ajili ya kuongeza kinga yetu madhubuti,kama nilivyowaambia hapo kabla ya kwamba ni lazima kinga yetu iendane na mazingira husika,sijamaanisha ya kuwa tuliyonayo haifai,hapana,ila inabidi tuiongeze nguvu…”
alishindwa kuendelea,mzee Otongo ikabidi aendeleze alipoishia..
“tunahitaji Mdigidigi!!”
“Mdigidigi!!!”
wanakijiji walihamaki,
“ndio Mdigidigi!!…na kama tunavyojua haipatikani hapa karibu…….”
“ndio! Ni mpaka mtoni!!”
“haswaa!..Mpaka mtoni!…inabidi tuwe na ule mti ili tuweze tengeneza dawa,tatizo ni kwamba tutaipataje?”
Otongo aliuliza,
mama Kurwa akatoa maoni yake
“inabidi watu wafuate kama ni hivyo!!”
kauli hiyo ilizua mjadala mzito,hakuna mtu alieonekana yu tayari kufanya hicho kitu kwani waliona ni kama kujiingiza kwenye mdomo wa kifo wenyewe,kila mtu alitaka kuilinda roho yake.
Katika hali ya kushangaza mzee Patili alinyamazisha watu na kuwataarifu ya kwamba ataenda yeye mwenyewe,taarifa hiyo badala ya kunyamazisha mjadala iliuzua zaidi,uamuzi wa mzee Patili kwenda kutafuta ule mti ilipokelewa na mawazo tofauti,asilimia nyingi ya watu walionekana kutoafikiana nalo huku wengine wakiliunga mkono….wakati taharuki bado ikichukua nafasi sauti ya mzee Rama tokea nyuma kabisa ilipata kusikika ikisema..
“mimi nitaenda huko mtoni!…mimi nimejitolea kwenda!! Nitumeni!”
hakuna mtu alietegemea kuisikia hiyo kauli tena toka kwenye kinywa cha mzee Rama,miguno na maswali ya chinichini ilizuka lakini hivyo vyote havikubadilisha uamuzi wake,alijisogeza mbele kabisa ya umati huku akimtizama mzee Patili,kisha akarudia kauli yake..
“nitume mimi!!”
“nitume mimi!”
mzee Rama alirudia kauli yake huku akimtamzama mzee Patili machoni,macho yao yaliyokua yanatazamana yalihakisi hali ya shari,tabasamu alilokua nalo mzee Rama halikua la wema,lilificha uadui mkubwa wa wivu ndani yake na pia malengo makubwa ya kimapinduzi.
Mzee Patili aliwageukia wanakijiji huku akiwa na sura ya kufikiri akasema…
“ameamua kujitolea,siwezi nikamzuia,maombi yetu yawe nae aweze fanikisha kile tulichodhamiria.”
baada ya kusema hayo maneno aliingia ndani na kuchukua fimbo fulani akamkabidhi mzee Rama kwenye mkono wa kuume kisha akamshika bega na kumpa maelekezo madogo juu ya ile fimbo,jinsi gani atakavyoitumia kumlinda,pia akamtakia safari njema.Mzee
Rama baada ya hayo maelekezo alimuaga mkewe na wanae huku akiwahaidi ya kwamba atarudi,akamfuata kijana mmoja aitwae Sadiki ambae ndie wa kwanza kumrubuni juu ya mzee Patili kisha akamuambia waende pamoja,alikubali na safari ikaanza.
Mzee Rama aliamini ya kwamba ile ni moja ya fursa adimu aliyokua anaitafuta kwa muda mrefu,japokua ni ya hatari lakini hakujali hilo,aliweka maisha yake rehani,eidha afe au afanikiwe kumpindua mzee Patili.
Safari ilitawaliwa na ukimya wa hali ya juu kutokana na kila mmoja wao kutoruhusu mdomo wake ufunguke,mwanga mwanana wa mwezi uliokuwepo uliwafanya waone wakanyagapo hivyo kutokua na hitaji la koroboi,mioyo yao ilikua inasema na mungu wao lakini ilikua ni zaidi ya hivyo kwa mzee Rama aliekua anasema na akili yake hasa juu ya nini atakachofanya afanikishe lengo.
Huku safari ikiendelea wingu zito taratibu lilianza kufunika mwezi uliokua unatoa nuru,giza totoro likaanza kuingia na kuwapa wakati mgumu wakina mzee Rama kwa kutoona walipokua wanaelekea! Sadiki aliekua ameshikwa na uoga maradufu alivunja ukimya
“..sasa mzee tutaendaje na hili giza??…si bora turudi tu!”
mzee Rama alitulia kwa muda bila kujibu,kisha kwa sauti ya msisitizo akasema…
“hatuwezi kurudi hilo sahau kabisa,tumeamua kujitolea na hii ndio maana ya kujitolea,wingu lipitalo lisikufanye ukageuza wako moyo,baada ya muda hali itarudi mahali pake”
baada ya mzee Rama kutoa hilo jibu ukimya ukarudi tena,hakuna alieongea zaidi,miguu yao ilizidi kusogea mbele taratibu kwa kukisia njia huku wakiyatoa macho yao ili yapambane na hali ile ya kiza iliyotawala,bado sadiki alikua na kinyongo moyoni lakini lile jibu alilopewa lilimfunga mdomo wake,hakua na jinsi,ilimbidi afuate kile atakachoelekezwa na ilikua ni robo saa sasa tangu waanze safari,walishakiacha kijiji chao kwa umbali wa kutosha japokua umbali wa maana bado ulikua mbele yao,walipiga konde.
Wingu jeusi taratibu lilianza kuacha mwezi uchomoze hivyo kuruhusu mwanga urejee na kuamsha matumamini ya wakina mzee Rama,waliongeza kasi sasa baada ya uhakika wa njia huku bado vinywa vyao vikiwa vimefungwa na macho yakitizama wanapoelekea,ghafla walisikia sauti za watu tokea nyuma zikiwaita!!! Mioyo yao ililipuka kwa uoga puh!! Kusikia majina katika hali kama ile ni kitu kilichowashangaza mno!! Mzunguko wa damu ukaanza kwenda kama mbio za marathoni! Shingo zao zilizowageuza nyuma hazikuwashuhudisha chochote,hawakuona kitu ila walisikia sauti!!..Miili ilitetemeka!!
“kimbiaaa Sadiikii!!” kauli hiyo ya mzee Rama ilikua kama kipenga kilichoruhusu mbio zianze,kila mmoja alikimbia kadiri ya uwezo wake huku akitizamatizama nyuma kuangalia kama wanafuatwa,umri wa mzee Rama ulikua ni kikwazo kikubwa kwani ulimfanya asiweze kukimbia kwa kasi kama Sadiki aliekua mbele yake,kila alipojitahidi kuvuta makasia ya mbio alihisi miguu inauma japokua alijitahidi kujizuia asisimame,mioyo yao ilikua inagonga kwa nguvu mno na jasho lilianza kutotesha nguo zao huku wakihema kama mbwa!! Fikra za kujutia uamuzi alioufanya zilianza kumtawala Sadiki mloe,atafanya nini sasa katikati ya ile safari?? Hakua na jinsi zaidi ya kuifungua miguu yake iokoe maisha yake.
Upepo mkali wa baridi ulimpita ghafla mzee Rama na kumfanya mwili mzima uite kwa msisimko wa ajabu!! Cha kustaajabisha ule upepo ulipomfikia Sadiki ulimbeba na kutokomea nae maporini!! Sauti yake nzito ya kuomba msaada ilifika vema kwenye masikio ya mzee Rama aliekua hana cha kufanya zaidi ya kutoa macho kwa kutoamini anachokiona,kama mchezo wa kuigiza Sadiki alipotelea kabisa..sauti yake nayo pia ikatokomea huko!!!
Mzigo wa hofu lawama na majuto ukatuama ndani ya moyo wa mzee Rama,alisimama huku mikono ikiwa kichwani,macho yakimtoka na jasho likimchuruza,alijiuliza mara mbilimbili kwanini ule upepo haukumbeba yeye akakosa jibu kabisa,hakujua ya kwamba ile fimbo iliyomkononi ndio iliyomuokoa,mkojo taratibu ulianza kutiririka katikati ya mapaja yake na kufanya nguo aliyoivaa iloe chepechepe,haraka wazo la kutaka kurudi kijijini likamjia kichwani,kwa macho ya uoga alitizama alipotokea na kuona kiza kimetawala,alipotizama na anapoelekea aliona hali ileile!! Harufu ya kifo ikaanza kugonga puani kwake,makelele ya umauti yakaanza kuita masikioni mwake!!
Harufu ya umauti ilianza kugonga puani,makelele ya kifo yalianza kugonga masikioni!! Alitembea kama hatua tano kurudi nyuma alipotokea akahisi moyo wake unamsuta,alikumbatia kile kifimbo alichokua nacho kisha akageuka tena na kuendelea na safari kama kawaida,tumbo likichemka na mwili ukitetemeka huku nguo ikiwa imelowa ndembendembe.
Nyuma ya mzee Rama hatua kama ishirini walikuwepo watu wawili wanasogea taratibu huku macho ya mmoja wao yakiwa yanang’aa mithili ya paka,mungu wangu!! Walikua ni wale mapatna wauaji,lile jibaba na yule mdada mwenye roho ya paka! Walionekana wanajadiliana jambo fulani lililoonekana kuwateka hisia,baada ya muda kidogo walinyamaza na kuendeleza zoezi lao la kumfuata mzee Rama taratibu bila
mwenyewe kusikia,masikini mzee Rama aliekua mwenyewe alikua hana hili wala lile,alikua hatambui ya kwamba bado anafuatwa na wale watu waliowaita,alikua hatambui ya kwamba nae anaundiwa mipango kabambe ya kumalizwa.
Dakika kama kumi na tano tu zilibakia ili mzee Rama aweze kuufikia mto Inguvai,miti ya midigidigi aliyotumwa ilikua inapatikana tu kwenye kingo za mto huo na si pengine popote,masikio yake yalianza kusikia sauti za maporomoko ya maji na sauti hiyo ilizidi kufika masikioni
mwake kila alipozidi kujongea,alishukuru mungu anakaribia lakini kichwa kilikua bado kizito kuchambua ya kwamba atafanikiwa kurudi kijijini au la! Hicho kitendawili alishindwa kabisa kukitegua.
Penye nia pana njia wahenga hawakukosea hata chembe kusema hivyo,nia ya mzee Rama kufanikisha lengo lake ilianza kuchomoza pale alipofanikiwa kuupata mdigidigi alioagizwa,hakutaka kuvunga muda,haraka alinyofoa matawi kadhaa,alipoona yanatosha hakuondoka kama ilivyotakiwa afanye,alianza shughuli za kutafuta mti mwingine aina ya Mtiriri tena kwa juhudi kubwa! Na hata alivyoupata aliunyofoa matawi
mengi ukilinganisha na aliyoyatoa kwenye mti wa mdigidigi,si kwa sababu miti ile ya mitiriri ni mifupi na rahisi kupatikana,hapana! Alikua ana malengo binafsi,matumaini yake ya kishenzi yalilala kwenye ule mti ambao ni sumu kubwa na mti hatari zaidi,alikua na lengo gani nao?? Je malengo yake ni kuua wanakijiji?? Hayo yote yalikua moyoni mwake binafsi,safari iliyotawaliwa na hofu ya kurudi alipotokea ikaanza rasmi taratibu huku kichwani kwake akijenga picha ya kufanikiwa.
Mzeee Ramaaaaaaa!!!! Sauti ya kike yenye nguvu ilisikika toka nyuma ikimuita! Mama yangu!! Mzee Rama alichanganyikiwa kabisa! Mara ya kwanza alipoisikia ile sauti Sadiki alibebwa,je sasa hivi kuna mwingine zaidi yake?? Hapana! Alikua ni yeye tu! Hakua na mkojo tena wa kutoka,moyo wake ulianza kudunda kwa pupa na miguu yake ya kizee ilianza kuchanganyia mbio!! Mkono wa kulia akishikilia fimbo na
matawi aliyoyakunjakunja ya mdigidigi na huku wa kushoto akibebelea majani ya mtiriri,magoti yake ya kizee yalianza kumvuta kwa maumivu,alijitahidi mno asisimame ili auokoe uhai wake lakini mwisho alishindwa,maumivu yalizidi mno na hata pumzi haikua nae tena!! Alisimama akihema kwa pupa huku sura yake ikitawaliwa vilivyo na uoga,alikodoa kutizama nyuma hakuona kitu kama kawaida!! Nafsi yake
ikamtonya kifo kimewadia,alipogeuza macho yake mbele aelekeapo uso kwa uso alikutana na yule mdada!!! Mzee Rama alifanya kosa kubwa kumtizama machoni kwani ndipo nguvu kubwa ya lile jini ilipo,alipoteza nguvu kabisa na kudondoka chini kama zigo..Fimbo kule!!
Lile jini lilimsogelea mzee Rama aliedondoka,macho yake mithili ya paka yaking’aa kama mwezi,masikio yake marefu yakichezacheza na ngozi yake ya kijivu ikitoa jasho,kiremba chekundu kilichokuwepo kichwani kilificha mapembe yake na kupunguza kidogo ubaya wake wa kutisha.Alipiga makofi mawili kwa mtindo wa mkono wa kushoto kuufuata wa kulia,ghafla mwili wa mzee Rama uliokua chini ukainuka
kimaajabu huku uso wake ukionyesha ya kua hajui kinachoendelea,yani hana fahamu,lile jini likapiga tena makofi ila ya sasa hivi yalikua ya haraka na pia kiganja cha kulia kilifuata cha kushoto,ghafla akapotelea na kua kama upepo! Kisha kwa madaha likamvaa mzee Rama!! Macho yaliyokua yamefumba yakafunguka! Mwili uliokua umelegea na kunyong’onyea ukapata nguvu ya ajabu!! Majani ya mtiriri na matawi
ya mdigidigi yaliyotawanyika chini yakaokotwa na kutiwa mkononi kisha tabasamu mwanana lililoakisi furaha ya yule jini alie ndani likajaza uso wa mzee Rama,taratibu kwa maringo yote likaanza kujongea kukitafuta kijiji cha Utowele alipo adui wao mkubwa waitajie kumtokomeza,ili kuifanya safari yake iwe ya kuvutia na kufurahisha alikua anaimba njia nzima huku akiuchezesha mwili ule wa kizee,lile jibaba linyongaji nalo ghafla likatokea na kumpa kampani mwenzie.
Je wanakijiji watapona?? Au ndio watapukutika kama mwanzoni?? Awamu hii mzee Patili ataeleweka?? Na vipi kuhusu mzee Rama na malengo binafsi??
Sehemu Ya 5
Safari ilikua kabambe mno,walicheza na kuimba bila woga wowote kwani walishafahamu ya kwamba muda si mrefu watakamilisha kile walichoagizwa,kazi ilikua kwa wanakijiji waliokua wanasubiria dawa ingali wanaletewa kifo!! ‘ya nini uepuke chumvi ingali jirani ni bahari?’ huo msemo ni dhahiri ulikua unaendana na tukio halisi kwani wanakijiji walionekana wakisumbuka
kweli kukwepa kifo bila kufahamu kwamba kilikua pembeni (jirani).Zilibakia dakika chache tu kuingiza miguu kwenye kijiji cha Utowele,lile jibaba linyongaji lilipotelea kusikoju likana na kumuacha yule bimdada aliekua ndani ya mwili wa mzee Rama aendelee na safari,mkono wake wa kushoto alioshikilia baadhi ya majani ya mtiriri sumu aliusogeza karibu na macho
yake,alichezesha kope zake kwa muda tu na ghafla yale majani yalibadilika na kua ya mdigidigi!! Kwa madaha aliyachanganya na yale ya mdigidigi halisi yaliyokuwepo mkono wa kuume,kama kawaida tabasamu likachomoza usoni mwake na kwa maringo akamalizia kaumbali kalikobaki.
Wanakijiji waliokua wamejikunyata kwa hofu na ukimya ukiwa miongoni mwao walilipuka kwa furaha baada ya kumuona mzee Rama,ilikua ngumu mno kuamini macho yao hasa familia yake!! Kusema ukweli ni asilimia ndogo iliyokuwepo mioyoni mwao iliyokua ikishuhudia kufanikiwa kwake,walimlaki kwa furaha huku wakimbeba na kumrusharusha mithili ya mtoto! Nyimbo za
kishujaa zikipamba tukio na wakisahau kabisa kuuliza yu wapi alieenda nae(sadiki).Mzee Patili,mama kadogo na mzee Otongo walikuwepo ndani wakifanya shughuli ya upakaji dawa,walitoka nje baada ya kusikia makelele ya wanakijiji,ilikua ngumu pia kwao kuamini macho yao pale yalipomshuhudia mzee Rama aliekua anarushwa na wanakijiji,muda mfupi tu baada ya wakina mzee Patili kutoka ndani wanakijiji walimshusha mzee Rama ili apate fursa ya kuwasilisha kile alichoagizwa,mzee Rama nae
hakufanya ajizi,taratibu alianza kujongea huku akishikilia yale majani akielekea walipo wakina mzee Patili,mzee Patili aligundua jambo la tofauti haraka akauliza..
“sadiki yupo wapi??”
“ameuwawa!!”
kifupi alijibu jini lile lililojivika mwili wa mzee Rama na kuwashtua wanakijiji,bado mzee Patili alitia wasi,akauliza tena
“fimbo niliyokukabidhi ipo wapi??”
lile jini lilijing’atang’ata kutoa maelezo yaliyonyooka hali iliyoanza kumpa mashaka mzee Patili na hata pia wakina mama Kadogo,mzee Patili hakutaka kuuliza swali lingine,alimshukuru mzee Rama kwa niaba ya wanakijiji na kumtakia baraka toka kwa mungu kisha aliingia na yale majani ndani na kumuacha mzee Rama akiwa amesimama pale nje karibia na mlango.
Udhaifu mkubwa wa yule jini kwenye mioyo ya binadamu ulianza kujionyesha,harufu ya binadamu iliyokua inagusa pua yake ilianza kumpa hamu kubwa na kuruhusu mate kuchuruza!! Mama Kadogo aliekua pembeni hofu ilianza kumteka akamshtua mzee Otongo ashuhudie lile jambo,si mate tu! Hata macho yake yalianza kubadilika badilika!! Kutokana na kuwapa mgongo
wanakijiji hakuna alieshuhudia hayo zaidi ya mzee Otongo na mama Kadogo,tamaa ya kula mioyo ilizidi kumtawala kichwa kumpelekesha na kumsahaulisha kusubiria malengo yake yatimie,taratibu lilianza kusogeza miguu yake na kuelekea ndani alipo mzee Patili!!!
Mama Kadogo alishindwa kunyamazia hilo akapayuka kwa nguvu..
“mzee Patili huyo anaaakujaaaa!!!!”
huku akinyooshea kidole na macho yakimtoka,sauti ile kali ya tahadhari iliwastua mno wanakijiji ilihali na mtu lengwa ambae ni mzee Patili,haraka mzee Patili aliuvuta mkono wake uliokuwepo ndani ya mfuko fulani mweusi na kumrushia unga wa kahawia lile jini usoni!! Sauti kali mno ya kulalamika mithili ya paka ilisikika toka kwenye kinywa cha yule jini!! Alijibamiza huku na huko na
kuhangaika mno huku akifikicha fikicha macho yake yaliyopokea ile dawa!!! Ilikua ni kama ndoto kwa wanakijiji waliokua wanashuhudia lile jambo kwa macho na mioyo ya hofu,walishuhudia mwili wa mzee Rama ukipotea na kuwa wa lile jini halisi!! Kiremba chake kinachoficha mapembe yake kiliruka huko na kuruhusu pembe zake mbili mithili ya mbuzi na chapa yake ya 666
kuonekana!!! Liliangaika mno huku likilia kila aina ya mlio,macho yake yaliyoingia dawa yalianza kufuka moshi ulioashiria ya kwamba nguvu yake inateketea na taratibu lilidondoka chini na kutulizana!!!
Wanakijiji wakiwa bado wameshikwa na mshangao na wasijue la kufanya walisikia sauti nzito isiyoeleweka ilalalamikayo inasogelea lile eneo!!!…..loh!! Walipogeuza macho yao kushoto walimuona lile jibaba linyongaji likija kwa kasi ya ajabu na
kamba yake mkononi!!!
Macho yakimtoka na sura ikiakisi ghadhabu kubwa aliyokua nayo!! Kabla hata halijafanya chochote kwa nakijiji walioanza kukimbia huku na kule kuokoa maisha yao jua lilianza kuchomoza!!! Mwili wake mkubwa mithili ya tembo ulianza kufuka moshi kama sigara kali!!! Nalo likaanza kutapatapa kama samaki nchi kavu!
* *
lile jibaba nalo likaanza kutapatapa kama samaki nchi kavu!! Macho ya wanakijiji waliokua wemejificha hayakuamini yalichokishuhudia,lile Jibaba ilikua kama mtoto kwa jinsi lilivyokua linajibaraguza na kurukaruka huku na kule kwa mitindo yote,ni dhahiri miale ya jua lililochomoza ilimuunguza kupita kiasi na alishindwa kabisa kuvumilia hilo,alitia huruma mno kwa jinsi alivyokua
akilalamika,waweza sahau mabaya yote aliyoyatenda kwa jinsi alivyokua anateseka,hatimaye mwili wake ulikua majivu kabisa na wa yule mdada pia,hakuna kilichobaki juu yao na huo ndio ukawa mwisho wao,chereko nderemo na vifijo zilitawala.
Je wanakijiji wataishi kwa amani sasa?? Ni swali lililohitaji ufumbuzi mzito.
* * * * * *
(Dar es salaam,Msasani)
mchungaji Josiah alikua amejipumzisha juu ya kitanda chake sita kwa sita akiitawanya miguu na mikono kwenye pande zote nne za kitanda,ni dhahiri huduma ya kiroho aliyoifanya jana usiku ilimchosha mno kwani japokua jua lilikua lishachomoza mwili wake bado ulionekana kutamani kitanda ambacho hakikushushiwa hata neti ya kumzuia na mbu,alijigeuza kivivu na kuendelea kuvuta makasia ya usingizi mpaka pale aliposhtushwa na mlio mkali wa simu yake ya kichina yenye muito wa nyimbo fulani ya injili ya muimbaji
maarufu nchini,macho yake yaliyotawaliwa na mang’amung’amu ya usingizi yalifunguka kwa mbali kuangalia ni nani anaepiga,alishtushwa kuona ni Askofu Emmanuel haraka aliiweka simu sikioni..
“shalom Askofu!”
“shalom Josiah…vipi unaendeleaje?”
“safi tu namshukuru mungu aisee..”
“ni kweli mungu aliejuu ashukuriwe,sasa Josiah…”
“naam Mtumishi!”
“embu fika hapa kanisani mara moja kuna kitu cha muhimu inabidi tujadiliane”
“haina shida mtumishi wa mungu,nitakuwepo hapo muda si mrefu!”
“sawa,bwana mungu awe nawe..”
“amina,awe nawe pia mtumishi..”
maongezi yakakata,mchungaji Josiah aliekua amechoka kama mbwa kutokana na shughuli pevu aliyofanya jana aliamka kwa kujivutavuta na kuelekea bafuni kupata maji,hakuweza kabisa kumbishia Askofu hivyo hakua na jinsi zaidi ya kutekeleza kile alichoambiwa na mkubwa wake ukizingatia yeye bado ni mchungaji mwanafunzi kwani si muda mrefu tangu aanze rasmi shughuli zile
za uchungaji.Ilichukua kama dakika thelathini na tano kwa mchungaji Josiah kumaliza kabisa zoezi la kujiandaa,alipanda daladala chapchap na kufika kanisani haraka tu kutokana na ukaribu uliokuwepo,alipoingia tu kanisani macho yake yaliweza kumuona
Askofu Emmanuel akiteta jambo na mtu fulani alievalia suti nyeusi,kabla hata ya yeye kufika walishamaliza maongezi yao na yule mtu akapanda gari na kuondoka,Askofu Emmanuel alimkaribisha mchungaji Josiah na moja kwa moja walielekea ofisini walipowakuta watu kama kumi wenye vialama vyeupe shingoni vilivyoashiria ya kwamba ni wachungaji,baada ya salamu za hapa na
pale majadiliano yalianza baada ya kufunguliwa na sala nzito toka kwa Askofu,kikao kile hasa kilikua kinahusu usambazwaji na uenezaji wa neno la bwana kama ilivyoagizwa,kilikua ni mahususi kwa ajili ya kujadili mikakati itakayowezesha injili kufika mahali ambapo hapajafikika,kanisa lilihitaji kufungua matawi yake zaidi ili iweze kuwafikia watu wengi zaidi waliohitaji huduma za kiroho
sehemu mbalimbali za nchi hasa vijijini,baada ya masaa mawili kikao kilikwisha kwa kumteua mchungaji Josiah asimamie shughuli ya kwenda kusambaza injili mkoani mbeya na kutia msingi wa kanisa,hakuamini kilichotokea kwani aliona ile ni kazi kubwa ambayo hakustahili apewe,haikua na jinsi,Askofu Emmanuel alimuamini na ukizingatia mchungaji mzoefu Isaya alikuwepo mkoani Arusha
kiroho,ilipangwa siku ya kufunga safari na idadi ya watu watakaokuwepo kisha mchungaji Josiah alirudi nyumbani kwake kwa ajili ya kuendelea na mapumziko.
Alipojirusha kitandani usingizi haukuja kama alivyotegemea,moja kwa moja akili yake ilianza kupitia kile alichoambiwa na kidogo kupata mawazo,ila katikati ya yale mawazo taratibu tabasamu lilichomoza usoni mwake na kuupendezesha uso wake mrefu wenye dimpoz,hakuna mwingine alieleta hilo tabasamu zaidi ya Rachel Mwakatwila mwanakwaya mahiri pale kanisani aliyewekwa kwenye
orodha ya wale waendao kutoa huduma,moyo ulilifurahia hilo,fursa adimu aliyokua anaisaka imekuja mikonomi mwake,nini nataka zaidi?? Kazi ni kwangu!! Alijiambia mchungaji Josiah.
* *
Jumatano alfajiri na mapema mchungaji Josiah,Rachel na watumishi wengine wawili walianza safari ya kuelekea mkoani mbeya kwa kutumia bus,kitendo cha mchungaji Josiah kupewa fursa ya kukata tiketi ilitumika vema kwani aliutumia ule mwanya kukata tiketi iliyomueka karibu na Rachel kitulizo chake cha moyo,safari nzima ilitawaliwa na vijistori vya hapa na pale na vicheko vya haja,Josiah alisahau kabisa cheo chake cha uchungaji mbele ya Rachel,stori zilinoga,ila mwishowe Rachel alibebwa na uchovu wa safari akamlalia mchungaji Josiah begani.
kila mara Josiah alipomtizama Rachel alielalia begani kwake alijihisi amani,alitamani alalie na kwenye moyo wake vilevile,hakujua cha kufanya ili aweze muingiza Rachel kwenye system ukizingatia cheo chake cha uchungaji,kuhisiwa vibaya mbele ya jamii na kunyooshewa kidole vilimtia hofu pia hisia za kukataliwa zilizidi kumtisha,alisema tu na moyo wake mkavu unaoumia.
Mwendo wa kasi wa bus ulifanya baadhi ya abiria walipuke kwa maneno wakimshutumu na kumsema dereva,makelele na malalamiko yao yalimuamsha mchungaji Josiah toka kwenye usingizi mzito wa mawazo juu ya Rachel aliokua nao,hakuchangia chochote kwani hakuna alichoshuhudia ila aliona watumishi wenzake wawili David na Rio wakijibizana na baadhi ya abiria juu ya mwendokasi wa gari,alipomtizama Rachel alikua bado amelala hivyo nae hakujua lolote linalojiri.
Baada ya muda kidogo bus lilipaki kwa ajili ya kuruhusu abiria wapate cha kutia tumboni,mchungaji Josiah alimuamsha Rachel aliekua bado amelala kisha wakaenda kupata msosi na kurudi ndani ya gari,muda si mrefu gari nalo lilijiondoa lile eneo na kuendelea na safari ya kuelekea jijini mbeya,shibe na uchovu vilimlemea mchungaji Josiah na sasa ikawa ni zamu yake
kulala,usingizi mzito uliombeba ulimpeleka mpaka kwenye ardhi ya ndoto ya ajabu isiyopata kusemeka,alijiona yupo kwenye giza zito nene na hajui pa kuelekea,miguu yake iliyokanyaga chini ilihisi baridi kali na kufanya mwili wake uitike kwa mtetemeko,moshi mzito ulimzunguka na kumfanya akohoe huku akihangaika kuitafuta pumzi kwa hali na mali ilhali moyo na akili yake vikishika kasi ya uoga,alikohoa na kukohoa,alikohoa mno mpaka kifua kikaanza kuita kwa maumivu!! Alikohoa mpaka
macho yakaanza kububujika machozi na kuhisi kichomi!! bado kikohozi hakikukoma hata kidogo,aliendelea kukohoa tena zaidi na zaidi mwishowe akaanza kukohoa damu!!! Mapigo ya moyo yalienda sawa na mbio za farasi wa mashindano,mzunguko wa kasi wa damu ulifanya baridi alilokua nalo lipotelee,joto liingie na kuruhusu vijasho kuchuruza mpaka sehemu za siri,kila alipojitahidi kuzuia kile kikohozi ule moshi ulizidi ongezeka na kumpalia hivyo kutompa machaguzi,mishipa ya uso ilimsimama
na koo nalo likaanza kuuma!! Koh!-koh!-koh!-koh!-koh! Bado alizidi kukohoa!!….mchungaji Josiah alianza kushindwa kumudu mwili wake,mkojo ulianza kumchuruza na kufanya nguo yake ya ndani kuwa tepetepe,bado kikohozi hakikukoma wala kupungua kasi!! alitia huruma na imani mno kwa jinsi alivyokua anahangaika,alishindwa kabisa kusimama kwani miguu ilikwisha nguvu hivyo akapiga magoti na kuendelea na lile zoezi la kukohoa tena sasa akihisi mkono umemkaba shingo!!! alizidi kutoa damu na
kutapatapa mpaka pale alipoisikia sauti nzito isiyojulikana imetokea wapi ikimwambia RUDI ULIPOTOKA!!!! kisha kufuatiwa na kicheko kikali cha kishetani!! Ha!-ha!-ha!-ha!-ha!-ha!-ha!
Baada ya hayo maneno mchungaji Josiah alishtuka toka kwenye usingizi huo mzito kwa pupa na kuwastua abiria wengine waliokuwepo karibu ikiwemo Rachel alie jirani.Rachel kwa tahamaki alimuuliza mchungaji…
“vipi mtumishi,kuna nini???”
mchungaji Josiah alishindwa kujibu,alionekana akihema kwa pupa huku akipepesapepesa macho kushoto na kulia kuhakikisha mazingira aliyopo,baada ya kutulia kidogo ndipo alipoanza kumuhadithia Rachel kile alichokiona kwenye ndoto,Rachel alishtushwa pia na zile habari na kumtaka mchungaji Josiah wasali ili mungu atie mkono katika safari yao,walishindwa kuwashirikisha watumishi wenzao kwani walikua usingizini,wakiwa katikati ya sala walisikia sauti kali za abiria kisha ukafuata
mlio mkali Puh!!!! presha kali iliwasukumiza mpaka mbele na kujigonga kwa nguvu!! gari liligonga!!….muda si muda gari nalo likaanza kubiringita kwa nguvu!!! Vilio vya maumivu na uoga vilitawala ndani ya gari!! Baada ya dakika kama tano gari lilitulia huku bado vilio vya baadhi ya abiria vikiskika kwa nguvu vikiomba msaada,wengi wao walikua kimya huku miili yao ikivuja damu,wengine walionekana wakilia huku wakigusa sehemu waliyodhurika au kujeruhiwa,watoto wadogo wawili wenye miaka si
juu ya mitano walionekana wakiwa wamelaliwa na gari hivyo sehemu kubwa ya miili yao ikawa imesagika,haikuhiaji utaalamu wowote,walikua wamekufa,hamaki mmama mmoja mjamzito alionekana tumbo limepasuka!! Ilitia huruma na ilisisimua kwa kutisha!! Damu iliyomwagika ilifanya nyasi zote zilizokuwepo kuwa nyekundu,lile eneo lilikua kama machinjioni!!
Huku akijikokota taratibu kutokana na maumivu mazito aliyokua anapata mchungaji Josiah alipata kuita kwa taabu..”Reeecho!!” hakuna aliyeitika,nae muda si muda alipoteza fahamu!!
“Reeecho!!” hakuna alieitika,nae muda si muda akapoteza fahamu!! Watu waliokaribu walianza kusogelea eneo la tukio huku wakitoa macho kwa kutoamini,wengi wao walishika vichwa na sura zao zilionekana zenye huzuni na masikitiko makubwa,dhahiri lile tukio liliteka hisia zao mno kwani macho yao hayakuwahi kushuhudia ajali mbaya kama ile.Shughuli za uokoaji zilichukua
nafasi,wakazi wa yale maeneo walionekana kujitolea mno kutoa miili ya watu iliyokwama ndani ya gari ambayo mingi ilipoteza uhai na kuharibika vibaya,ilikua ngumu kuitambua kwa urahisi kutokana na kuchakazwa na ajali,palinuka damu lile eneo na pia vilio vya baadhi ya walionusurika kufa na washuhudiaji vilevile vilitawala,ilikua ni zaidi ya msiba.
Ilichukua kama dakika hamsini na tano kwa ambulance ya hospitali kuu ya Iringa kufika eneo la tukio,udogo wa ambulance hiyo ulifanya zoezi liwe gumu hivyo wengi wao waliozidiwa walipoteza maisha ukizingatia na umbali uliokuwepo mpaka hospitalini,zoezi lile lilidumu mpaka saa mbili ya usiku ambapo ndipo taarifa ziliposambaa na kwenye vyombo vya habari juu ya ajali hiyo mbaya
kuwahi kutokea,ilimshangaza kila alieshuhudia na pia kila alieisikia,hofu kubwa ilitanda mioyoni mwa watu waliohisi eidha ndugu jamaa na marafiki walipanda lile gari kwani taarifa zilionesha kuwa ni idadi ndogo ya watu iliyopona ukilinganisha na ya waliobakia majeruhi,miongoni mwa hao watu alikua ni Askofu Emmanuel aliezipata hizo habari kwenye breaking news ya Redio moja maarufu,alichanganyikiwa mno kwani alijua fika watumishi wake walipanda lile gari,aliwajulisha wenzie na mkakati wa kuelekea
hospitali kuu ya Iringa ulipangwa ufanyike haraka iwezekanavyo kesho yake asubuhi kwa kutumia gari la Dayosisi.
Mochwari ya hospitali kuu ya Iringa ilijaa hivyo baadhi ya maiti zilifunikwa tu na kuachwa mawodini,ilikua siku bize sana kwa wauguzi wachache waliokuwepo pale,hata pia madaktari wengine ambao hawakua na zamu na walio likizo waliitwa kazini wasaidie jahazi,bado walikua wachache mno kukidhi matakwa yote.
Mchungaji Josiah bado fahamu hazikumrudia,kichwa chake kilizungukwa na bandeji nzito iliyoshiba nyeupe huku sindano ya dripu ikipenyeza dawa mwilini mwake,uso wake ulionekana umejaa kutokana na kuvujia damu hata mikono yake vilevile ilivishwa P.O.P,alikua ndani ya wodi ya wanaume sanjari na David isipokua tu Rio alieaga dunia kutokana na kupasuka fuvu la kichwa,upande wa wodi ya wanawake bibie Rachel alikua hana hali nzuri pia,mashine ya kupumulia ilijaza uso wake kutokana na mfumo wa upumuaji kushindwa kufanya kazi baada ya uvunjikaji wa mbavu,vilevile mguu wake wa kushoto ulivunjika,alitia huruma.
Wakati mchungaji Josiah akiwa bado hajarudi katika hali yake ya ufahamu alipata kuota tena kwa mara ya pili,sasa hivi alijiona amekaa na Rachel pembeni wakiteta jambo,matabasamu yaliyopendezesha nyuso zao ziliashiria ya kwamba walichokua wanaongelea kiliwakonga nyoyo,kila mtu alifurahi na dhahiri stori zilikua zinasonga vema.Ghafla Josiah alihisi ameshikwa begani na
mtu tokea nyuma,alipogeuza shingo yake kutizama ni nani aliefanya hivyo hakuona kitu na hata uso wa Rachel ulionyesha hauna habari na lile tendo,aliamua kupotezea na stori kama kawaida zikaendelea,kale kamchezo bado hakakukoma! alihisi tena mkono umemgusa begani kwa mara ya pili na alipogeuka hakuona kitu tena!! alianza kupata hofu,alipomtonya Rachel juu ya hilo alipuuzia
na kumwambia ni stress tu hizo hivyo kufanya mchungaji Josiah atulie tena ila kwa imani ndogo na hofu ya kuonekana muoga mbele ya mwanamke,baada ya dakika mbili tatu ule mchezo uliendelea!!….mchungaji Josiah alihisi mkono umemgusa tena begani,alipogeuka haraka kuangalia hakushuhudia chochote!!…akili yake ikamtonya kwamba pale si pa salama,alimuambia tena Rachel juu ya hilo na sasa wakalichukulia jambo serious,waliinuka na kuanza kujiondoa lile eneo,wakiwa njiani walihisi watu
wanaongea na kucheka nyuma yao ila kila walipotizama hawakuona chochote!!..tendo hilo lilizidi kujirudia na kuwatia uoga maradufu,mbio zilianza huku wakiwa wameshikana mikono! Kila mara waligeuka geuka nyuma kutizama kama wanafuatwa,japokua hawakuona kitu ila bado sauti za watu zilifika masikioni mwao!! kitendo hicho cha kutizama tizama nyuma mara kwa mara kulifanya Rachel ajikwae na kumpa Josiah kazi ya kumdaka,cha kushangaza Rachel alipounyanyua uso wake
ulionekana si wa Rachel yule ajulikanae,macho yalikua makubwa na meno yalitokeza nje kama mamba!!! Uso wake wa maji ya kunde ulikua mweusi kama mkaa na masikio yake yakawa marefu kama punda!!! Mungu wangu! mchungaji Josiah aliyatoa macho kwa kushangaa,bila kujiuliza mara mbili mbili alianza kukimbia kwa kasi toka pale Rachel alipo,katika hali isiyo ya kawaida Rachel aliebadilika sura alikua anamkimbilia Josiah huku akilalamika kwanini anamkimbia kwa sauti yake ileile halisi!! Ghafla mchungaji Josiah alizinduka toka ndotoni huku akipiga makelele makubwa na kustua watu waliopo mule wodini!!!
*
ilibidi muuguzi aje haraka kumjulia hali,Josiah alionekana akigugumia kutokana na maumivu makali aliyokumbana nayo,kichwa chake kilichofungwa bandeji kililemewa na maumivu vilevile mkono uliofungwa P.O.P ulimvuta bila kusahau uti wa mgongo,alitulia kitandani kama alivyoelekezwa na muuguzi ya kwamba anahitaji mapumziko,ila
kabla ya muuguzi kuondoka Josiah aliomba jambo fulani lililodhihirisha ya kwamba fahamu zimerudi mahala pake,huku akivumilia maumivu aliyokua anayapata alimwambia yule muuguzi akamuangalizie mwenzie ambae ni
Rachel huku akiambatanisha na maelezo ya mtindo wake wa nywele alionao na nguo aliyovaa,bila kinyongo yule muuguzi alilipokea lile ombi,alimtaka Josiaha apumzike wakati yeye akienda kulitekeleza hilo,roho ya Josiah sasa ikawa imetulia huku ikisubiria taarifa kwa hamu kubwa isiyoelezeka.
* *
Mwanga uliochipukia baada ya wale viumbe wauwaji kufa iliwawezesha wanakijiji kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo ujenzi,nyumba za wakina Madhifa zilijengwa kwa ushirikiano mkubwa wa wanakijiji,nyumba ya mzee Patili vilevile.Ilikua ni saa tatu ya usiku hivyo mwanga ulishamezwa na giza,kila mwanakijiji alikuwemo ndani ya kiota
chake akiendelea na shughuli mbalimbali hivyo kufanya huko nje kua kimya! hakuna kilichoendelea huko nje zaidi ya upepo wa taratibu kutikisa matawi ya miti na kutengeneza sauti fulani,milio ya bundi nayo ilipamba tukio.
Julina alikua ndani kwake akimnyonyesha mwanae wa pekee aliebeba tumaini la watu huku akimchezeachezea
mashavu na kumfanya mtoto atoe tabasamu la kupendeza,furaha ya mtoto ni furaha ya mama hilo lilionekana kwani kila mwanae alipotabasamu nae alishindwa kulizuia la kwake,alisahau kabisa upweke aliokua nao kwa kutokuwepo mume wake,kila alipotizama sura ya mwanae mwenye afya alipata amani na furaha moyoni kwani ndicho kitu pekee alichokua nacho kwa sasa,furaha yake iliingia dosari pale tu masikio yake yalipoisikia hodi
tokea mlangoni,asili yake ya uoga ilimfanya achungulie dirishani kuhakiki ni nani,alipogundua ni mama Halima alimfungulia mlango hasa ukizingatia ujenzi uliofanyika mchana ulifanya nyumba yake iwe katikati ya nyumba za wanakijiji hivyo hofu kuwa adimu kwake,vijistori vya hapa na pale viliendelea kati ya Julina na mama yake wa hiari
mama Halima,baada ya muda kidogo Julina alimkabidhi mama Halima mtoto wake ili aweze mpakulia japo chakula atie sunna,ilikua ni kosa kubwa!! Mama Halima hakua mama Halima aliedhaniwa,mama Halima halisi alikua yu nyumbani kwake akipika chakula,baada tu ya mama Halima yule feki kupewa yule mtoto alijiinua taratibu
huku akizuga kumbembelezabembeleza na kumuimbia nyimbo za kikabila mtoto alieonekana kumkataa kabisa kwa kulia kwa sauti kubwa huku akirusharusha mikono,hali ile ilimshangaza kidogo Julina kwani mwanae hana tabia hiyo ukizingatia huwa anatulia tuli akibebwa na mama Halima,hakulichukulia kwa uzito hilo jambo hivyo
aliendelea kupakua wali kwa ajili ya mama Halima,alipomgeuzia mgongo tu yule mama Halima feki aliutumia ule mwanya kuufungua mlango taratibu huku akinyata na kutoka nje na mtoto!!! Julina alihisi sauti ya mtoto wake anaelia imefifia hivyo aligeuza haraka shingo yake kutizama,moyo wake ulikita puh!!! Hakumuona mwanae na masikio yake yalizidi kusikia sauti ya mwanae inazidi kufifia!! haraka alitoka nje huku akipiga makelele ya nguvu
yaliowashtua wanakijiji!! makelele yake na ya mwanae aliekua anakimbizwa na yule mmama yalitosha kabisa kuwatoa wanakijiji nje ya nyumba zao, haraka habari zilisambaa na haraka wanaume walianza kumkimbiza yule mama aliekua amemshikilia mtoto huku akiwa na sura ya mama Halima!! mikono yao ilishika silaha mbalimbali za
jadi tayari kwa ajili ya kupambana kumuokoa mtoto alie tegemeo kwao!! wanakijiji waliobakia walishikwa na simanzi kubwa,walimshirikisha mungu wao kwenye sala awasaidie lolote baya lisije likajiri kwani ni dhahiri walifahamu ya kua endapo yule mtoto akipotea basi hawana budi,watakua chini ya utawala wa CHERNOBOG,yani mungu mweusi! Nini kitakachojiri? Jasho jembamba la hofu lilitirika!
*
Baada ya mchungaji Josiah kurudishiwa majibu kwamba Rachel yu hai moyo wake ulijawa na furaha,alimuona pia David pembeni yake hivyo hofu yake ikawa ni kwa Rio ambae hakumtia machoni,saa nne usiku juu ya alama ikawadia.
Wodi ilikua kimya mno,macho ya mchungaji Josiah hayakua na usingizi hata kidogo kutokana na kulala mno ndani ya basi hivyo yalikua tu yakipepesapepesa vitanda mbalimbali vilivyopo,baada ya muda kidogo Josiah alitekwa na mawazo mazito,mawazo hasa juu ya ndotoa alizoziota ile siku,alitafakari sana lakini hakupata jibu la ndoto hata
moja hivyo akakosa amani.Huku bado akili yake ikiwa inabarizi ndani ya kisiwa cha mawazo alihisi mlango wa wodi unafunguliwa! Ukimya uliokuwepo ulifanya sauti ya mlango kufika vizuri masikioni mwake,haraka alirushia macho kwenye ule mlango!!
Baada ya mlango ule kufunguliwa hakuna mtu aliyeingia,ulikua unaenda tu mbele na kurudi nyuma ukisindikizwa na sauti za malalamiko,moyo wa mchungaji Josiah ulitokota kama maji mafigani na alipotizama ni nani mwingine anashuhudia hakuona mtu! Wote walikua wamelala na wengine walikua washakufa,alimeza mate,sala fupi ya kuwa salama ilifuata kimoyonimoyoni.Kila alipojitahidi kupotezea lile swala alishindwa! Aliuona usiku ni mrefu,kuinuka na kwenda kuangalia pia alishindwa kutokana na majeraha aliyonayo hivyo alibakia tu na gubu moyoni.Ule mchezo wa mlango kufunga na kufunguka wenyewe ghafla
ulisimama,mchungaji Josiah akakazia macho kuangalia kunani,hakuna kitu kilichoendelea ila kwa mbali sauti ya nyimbo ilianza kusikika,nyimbo isiyoeleweka inanena lugha gani! Wala nyimbo isiyoeleweka ina maanisha nini! Mara ya kwanza mchungaji Josiah alidhani masikio yake yanamdanganya ila alivyozidi kuisikia ile sauti ndipo alipoamini ya kwamba asikiacho ni sahihi,haikutosha hiyo tu…sauti ya kugonga gonga ilisikika toka juu ya paa!! nini hiki?? Mchungaji Josiah alijiuliza,sauti ya nyimbo za ajabu na za kugongwa paa zilizidi kumchanganya na kumuogopesha,imani yake ilianza kuterereka.Baada ya muda kidogo zile sauti
zilikoma,hazikusikika tena hivyo kuruhusu ukimya utawale na mchungaji Josiah kupumua,kuisha kwa kioja kile ulikua ni mwanzo wa kingine,sauti za miguu ikitembetembea ndani ya wodi ilianza kufika vema katika masikio ya Josiah,mungu wangu!!…mwili ulianza kusisimka na moyo ukaanza kudunda kama kitenesi pale alipohisi ile sauti ya miguu itembeayo inakaribia kwake!!…mchungaji Josiah alijifunika na shuka gubigubi kwa uoga asione kitakachoendelea huku joto na hofu vikimmimina jasho vya kutosha,mkono ulimgusa mgongoni na sauti ya kike ikaskika..
“kaka! nini shida??”
* * *
Jitihada za wanakijiji kumkimbiza yule mmama zilianza kuzaa matunda,ni hatua chache tu zilisalia ili wafanikishe lengo la kumkamata aliemuiba mtoto,yule mmama baada ya kuona anazidi kukaribiwa na wale wanaume alianza kuhofia usalama wake hivyo alimrusha mtoto huko!! wanaume wanne waliokua wanamkimbiza walisitisha lile zoezi na kwenda haraka kumtizama mtoto na kumuachia upenyo yule mmama wa kupotelea maporini,walimuinua yule mtoto na kuanza safari ya kurudi kijijini kwao,kitendo cha kumuokoa yule mtoto kilikua ni cha faraja mno kwao na hata wanakijiji walilifurahia hilo kwa kiasi kikubwa! matumaini yao yaliyopotea
yalirudi mahala pake na hapo ndipo mtoto alipopewa jina,akaitwa RENZO ikimaanisha TUMAINI kwa kilugha chao.
Baada ya furaha ya muda juu ya lile jambo wanakijiji walirudi tena majumbani mwao,ulinzi wa yule mtoto haikua tu inamhusu Julina bali kila mwanakijiji hivyo walihamasishana juu ya hìlo,vikoroboi vilizimwa na vitanda vikalaliwa.
Upande wa pili wa kijiji cha Igesambo ambapo ndipo yaliyopokua makao ya jeshi la 666 mambo hayakua mambo!..kushindwa kwa jaribio la kwanza la muda usiosogea na la pili la kumuiba mtoto kulifanya kusilalike wala kusilike,ni dhahiri viongozi wao
walichukizwa mno na lile jambo na ilibidi mipango mizito iundwe,kikao kizito kiliitishwa,wazee watano waliovaa majoho mekundu na meupe walikusanyika na baada ya muda kidogo alikuja mwingine alievalia joho jeusi tii! sura yake ilikua nyeusi na macho yake yalikua meupe,wale wengine watano walisimama na kumuinamishia kichwa yule alieingia na kudhihirisha ya kwamba ni mkubwa kwao,baada ya kufanya hivyo wale wazee wote ikiwemo na yule mkubwa wao waliinama na kusujudu huku wakitaja jina la mungu wao CHERNOBOG,kisha kikao kizito kilichukua nafasi..
“ni kwanini hasa tunashindwa???”
aliuliza yule mzee aliekua ameketi kwenye kiti kikubwa akizungukwa na wengine watano,kwa jina Abbadon.
“majaribio yetu hayakua na nguvu Oh shalom Abbadon,hivyo yaliweza kupanguliwa kiurahisi na wale binadamu”
alijibu mzee wa kwanza kabisa toka kwenye mkono wa kushoto wa yule mkuu wao,
“mnashindwaje na binadamu?? mnashindwaje na damu na nyama?? mnataka niambia kwamba wamewazidi akili??”
aliuliza tena Abbadon,mzee wa pili tokea mkono wake wa kulia akajibu..
“hatukufanya udadisi wa kutosha ili tuweze fahamu wapi ni nguvu yao na wapi ni udhaifu wao hicho ndicho kilipelekea hasa kushindwa kwetu..”
“kipi hasa ni nguvu yao??”
“kuna mzee aitwae Patili alie kijijini kwao,ni kikwazo kikubwa kwetu kutokana na kuwa na utaalamu utupao mushkeli!!”
“kwahiyo mmeamua kufanya nini sasa??”
Abbadon kwa msisitizo aliuliza,mzee mmoja aliekua kimya tokea kikao kianze alinyanyuka taratibu na kusema..
“Oh Shalom Abbadon,mimi kama Alvah mratibu mipango ningependa kuchukua fursa hii kuomba radhi kwa kushindwa kufanikisha majaribio yangu ila ningependa nipewe nafasi ya mwisho na endapo nisipofanikisha lengo nitawajibika”
hiyo kauli ilionekana kuwastua wazee wengine na kumpenya Abbadon moyoni,akaendelea
“naomba nipewe jaribio la mwisho,jaribio litakalobeba imani yangu kwako Shalom Abbadon na kwa mungu wangu CHERNOBOG..!!!”
Palikua kimya vya kutosha,kila mtu alie kwenye kile kikao alimpa masikio ya uelewa Alvah mratibu wa mipango kama alivyoapishwa mapema tu baada ya uzao wa mungu mweusi CHERNOBOG,huku akijiamini na akiyanyoosha maelezo yake ya msingi juu ya jaribio lingine lifuatalo baada ya yale mengine kugonga mwamba,jaribio lililozito na jeusi,jaribio lililobeba ushindi na
kushindwa,jaribio litakalotabiri yatakayojiri,jaribio lililoshika nyadhifa yake na mwanzo au ukomo wa Mungu wake,ilikua hatari mno na ni dhahiri vita ilitangazwa.Macho ya Alvah yaliakisi mno kile alichokinena,yalikua makali na ya msisitizo vilevile yaliendana na uzito wa lile jaribio alinenalo,huku akinyoosha kidole alipata sema
“kafara ya watu ishirini yahitajika upesi! tuliyoipata leo jioni ilikua ni thelathini tena kwa mkupuo baada ya kupindua basi liendalo jijini mbeya,idadi iliyopelea ni ishirini ili niweze fanikisha lengo,ili niweze fanya jaribio zito litakalotusafishia njia kufikia mafanikio yetu hakika!!”
Abbadon alipata yasikia hayo yote na kumpenya,alimuamini Alvah vya kutosha kwani ni mchapakazi na dhahiri alikua anastahili kile cheo alichokua nacho,japokua alishindwa kwenye majaribio ya mwanzoni bado imani ilikua upande wake,hakukua na mtu aliyeonyesha kutilia shaka alichokinena hivyo kufanya hitimisho lipatikane kwa urahisi na kikao kufungwa ili kuruhusu shughuli za upatikanaji wa kafara za kuongeza nguvu jaribio zifanyike,waliinama na kusujudu kama mwanzoni wakiongozwa na Abbadon huku wakitamka baadhi ya maneno kwa sauti nzito ya kutisha “Oooh…Shalom CHERNOBOG!..eeeehh!…Shalom CHERNOBOG! Ukapate kutwaa!!”
kisha kikao kikafungwa kwa kunyunyuzia damu ya mbuzi aliechinjwa muda huohuo.
* *
Sauti aliyoisikia mchungaji Josiah akiwa ndani ya shuka alilojitwika ilimstua zaidi kwani ilikua inafanana na ile ya muuguzi aliemjulia hali muda si mrefu,hakujibu chochote,mdomo ulikua mzito na alikua anatetemeka mno,moyo uliokua unaenda kasi mithili ya maporomoko ya mto Owen ulikua unaomba mkono wa mungu utanakabali huku akizidi kujikunja kama kifaranga cha kuku kilicholoana na kuachwa na mamae,
“kaka vipi kwani???”
sauti tena ileile ya kike ilisikika huku ikiambatana na zoezi la kumgusagusa Josiah alieloa uoga ndembendembe.Bado Josiah hakujibu lolote hali iliyompa mashaka yule muuguzi aliekua anamsubiria atoe kauli,
“jamani we kaka kuna nini??”
muuguzi wa watu alievalia nguo ya rangi ya karoti aliuliza tena kiupole,bado Josiah hakujibu chochote ila aliruhusu macho yake yapenye na kuchungulia kupitia shuka lile jepesi na kuhakikisha aongeae,alimuona muuguzi yule mweupe saiz ya katikati akiwa na sare zake zilezile alizokua nazo muda ule,hofu kidogo ikapungua akalishusha shuka lile lililokua limemfunika mpaka kichwani na kumuangalia muuguzi yule kwa macho ya aibu,huku akitabasamu akasema
“za saa hizi dada??”
“safi tu kaka,vipi kwani mbona ulikua katika ile hali???”
“ah! Kawaida tu dada,ni maumivu tu yalikua yananisumbua kusema ukweli”
“maumivu???”
“ndio!”
“ehh!! wapi panakusumbua kaka yangu??”
“huu mkono mlionifunga hii P.O.P unaniuma sana,kichwa nacho kinanipasua!”
“pole sana,usihofu lakini utazidi kupata nafuu kadiri unavyozidi kusonga mbele,cha umuhimu upumzike vya kutosha na usiwe unajikunjakunja kama ulivyofanya kwani utajisababishia maumivu zaidi na hiyo sindano ya dripu yaweza kuchomoka!”
“sawa dada,haina shida!!….naa vipi kuhusu yule dada niliyekuagizia mchana,anaendeleaje??”
“usihofu yupo sawa tu,sasa hivi anapumzika..”
mchungaji Josiah alitamani yale maongezi yasiishe kwani alijihisi ana amani zaidi kutokana na ule uwepo wa yule mdada,ila yule muuguzi ilibidi aondoke ili akawajulie hali na wengine hivyo alimuaga mchungaji Josiah na kujiondoa lile eneo.
*
Sauti kali za mbwa na bundi zilipamba usiku ule wa saa saba,mwezi ulikua unang’aa mno kutokana na kutokuwepo kwa mawingu angani na pembeni yake kulikua na nyota mbili zing’aazo,nyota ya upande wa kushoto ilikua inang’aa kupita nyingine hivyo kuashiria ya kwamba kuna litakalojiri,upepo wa baridi nao ulipuliza taratibu na kufanya miti na majani viiname,haikua ya kawaida,nyota ile
ing’aayo zaidi ilizidi kung’aa na kufanya mwanga wake kuwa mkali mithili ya mwezi,hakuna aliyeligundua hilo kutokana na watu kuwa vitandani kwa muda huo na hata baadhi yao waliokua macho sehemu mbalimbali kama kwenye kumbi za starehe na kwenye magari ya masafa marefu hawakulitambua hilo,ulikua ni wakati wa jeshi la 666 kutawala!!!! ile hali yote iliyokuwepo ilikua ni
kionyeshi ya kua usiku ule ulikua ni wa kafara,watu walikua wanatafutwa kwa ajili ya kafara ya kuongezea nguvu jaribio la kumtokomeza RENZO,mtoto pekee alieye kikwazo kwao kuushika ulimwengu,idadi ya watu kama ishirini na tano ikiwa imevalia majoho yenye rangi nyeupe na nyekundu na huku nyuso zao zikiwa na chapa ya 666 walishika njia kuelekea mahospitali yalipo,walianza na hospitali kuu ya Iringa!! Mchungaji Josiah na wenzake waliopo huko watapona??
(mwanga wa giza)
walianza na hospitali kuu ya Iringa!! Hatari ilioje?? Waliingizana taratibu huku wakinyata,kila kilichonenwa na kiongozi wao aliyekua ni mama Marinda ndicho kilichotekelezwa,macho yao yaliyoakisi mwanga wa mwezi yaliwafanya waonekane mithili ya paka! Masikio yao marefu na mjazo wa tarakimu 666 kwenye mapaji ya uso ilizidi kuwafanya waonekane wanyama ukiachilia
mbali na miili yao yenye rangi ya kijivu.Geti la hospitali lililo kuu kuu hata halikuguswa hivyo hamna kelele iliyozalishwa.Miguu yao iliyo peku ilikanyaga chini kiustaarabu huku macho yao yakiangaza angaza huku na kule kiusalama zaidi.Mikono yao yenye kiu ya kutekeleza walichoagizwa ilianza kufanya kazi kwa mlinzi mzee waliemkuta fofofo kwa usingizi.Walimnyonga kama kuku bila
kumpa fursa hata ya kusema lolote,akajazilishia idadi.Macho yao yakaelekezwa kwenye wodi ya wanaume alipo mchungaji Josiah,taratibu wakaanza kujongea huku wakipangana mstari,mbele akiwa mama Marinda kiongozi,walikua wanatisha mno na vilevile walikua wananuka kifo! Hilo ndio jeshi la 666.Mkono wa mama Marinda wenye michirizi ya mishipa na kucha ndefu ulishika kitasa na kufungua taratibu kisha akachungulia,baada ya kurudisha kichwa chake alitoa amri iliyotekelezwa bila ya maswali,waliingia watu watatu,wanaume wawili na mwanamke mmoja wakanyooka mpaka kwenye kitanda cha kwanza
kabisa,walipogundua ya kwamba alielala pale ashafariki waliachana nae na kujongea kwenye cha pili,wakamkuta aliepale mzima ila usingizi mzito umembeba,haraka wakatawanyika na kukizunguka kile kitanda kutokana na idadi yao,wakafumba macho na vinywa vyao vikaanza kutetema maneno fulani ya lugha ya ajabu yenye maana ya kutanakabali kafara yao,mara ghafla yule mtu aliekua amelala pale akatapatapa kama anaenyongwa na baada ya muda kidogo akatulia tuli kumaanisha ashakufa! Mtindo ukawa ni
uleule,wakasogea kwenye kitanda kinachofuatia.Wakati hayo yote yanachukua nafasi mchungaji Josiah alikua hana habari,alikua akikoroma kutokana na usingizi mzito uliombeba na kitanda chake kilikua ni cha sita tokea walipo wale wauaji wa kafara.
Macho yakafumbwa tena na sala ya kuitanakabali kafari ikafanyika,mwingine wa kitanda kinachofuata nae akaenda na maji,wale
watu watatu wauaji wakasogelea kitanda kingine kifuatacho wakakuta aliepale kafariki hivyo wakakiruka na kwenda kingine,idadi ya vitanda vilivyobaki ili mchungaji Josiah akutwe vikawa ni vinne tu.Kama kawaida mchezo ukaendelea,mgonjwa aliyekuwepo pale nae akarusharusha miguu kisha akaenda na maji kwa ajili ya kafara.Idadi ya waliouwawa ikawa ni wanne akiwemo mlinzi
aliefungua dimba.Bado haikuwatosha,walisogelea tena kitanda kifuatacho alipo mzee mmoja asumbuliwaye na figo,kitambi chake kilikua kama kichuguu kwani alijifunika na shuka gubigubi akilala chali.Hawakutaka kupoteza muda,kama kawaida waliyafunga macho yao wote na kutetema maneno fulani kwa lengo la kuitanakabali kafara yao,yule mzee akarusharusha miguu yake kuitetea roho yake lakini mwishowe akatulia tuli na mapigo ya moyo yakazizima.Wakasogelea kitanda kingine!!!
* *
Ndani ya kanisa la Under the God Fontain sala nzito ilikua inaendelea ikiongozwa na askofu Emmanuel Mgaya,wachungaji watano pia walikuwepo kwenye mkesha ule wa dharura ulio maalum kwa ajili ya kumuomba mungu awaweke mikononi watumishi wake waliokumbwa na ajali wakiwa njiani kwenda kumtumikia.Kila aliyekua pale alisema na mungu kwa njia na uwezo wake.Sauti zao pekee ndizo zilizosikika kwa ule muda wa usiku totoro,wakiomba kwa nguvu huku sura na matendo yao vikiakisi ni kwa jinsi gani lile jambo lilivyo serious kwao na jinsi gani linavyowagusa.Miili yao iliyokua ikipata joto kutokana na sala hiyo nzito ilikua inapoozwa taratibu na feni aina ya SOLCE hivyo basi kuwafanya wazidi kudumu kwenye maombezi.
* * *
Wale watu watatu wauaji waliwadia rasmi kwenye kitanda cha mchungaji Josiah,walikizunguka kama kawaida na bila kupoteza muda walifunga macho yao na kuanza kutetema maneno kama walivyofanya kwenye vitanda vilivyopita.Baada ya muda wakafungua macho yao kutizama majibu,Josiah bado alikua anahema,waliangaliana kwa mshangao kisha wakarudia tena lile tendo kwa uhakiki zaidi.Walipofungua tena macho yao wakamkuta mtu bado mzima,walishangaa sana juu ya hilo huku wakijiuliza ni wapi wamekosea,wakiwa wamepigwa bumbuwazi walisikia sauti ya makofi tokea kule mlangoni iliyowaashiria ya kwamba wanaitwa,wakageuza na kuanza kukimbia kuelekea langoni na kisha kupotelea kabisa.Josiah alishtushwa na sauti na sauti za watu zilizokua zinaishia,alipotizama huku na kule hakuona kitu,muda si mrefu yule muuguzi akaingia mule ndani akiwa na sura iliyojaa uoga.
MWISHO


10 Comments
I’m still learning from you, but I’m trying to reach my goals. I definitely love reading everything that is written on your blog.Keep the stories coming. I enjoyed it!
There’s noticeably a bundle to learn about this. I assume you made certain good points in options also.
Greetings! I know this is kind of off topic but I was wondering which blog platform are you using for this website? I’m getting tired of WordPress because I’ve had issues with hackers and I’m looking at options for another platform. I would be great if you could point me in the direction of a good platform.
Thank you for sharing with us, I conceive this website truly stands out : D.
What i do not realize is if truth be told how you’re not really much more well-preferred than you may be right now. You’re so intelligent. You realize therefore considerably when it comes to this subject, made me individually consider it from a lot of various angles. Its like men and women are not involved except it is something to do with Girl gaga! Your individual stuffs excellent. At all times maintain it up!
whoah this blog is excellent i love reading your articles. Keep up the great work! You know, a lot of people are looking around for this information, you can help them greatly.
I was very pleased to find this web-site.I wanted to thanks for your time for this wonderful read!! I definitely enjoying every little bit of it and I have you bookmarked to check out new stuff you blog post.
Thank you for any other fantastic post. The place else may just anyone get that type of info in such an ideal manner of writing? I have a presentation subsequent week, and I’m at the search for such information.
Good write-up, I am normal visitor of one¦s website, maintain up the excellent operate, and It is going to be a regular visitor for a long time.
You have mentioned very interesting details! ps decent web site. “Mediocrity knows nothing higher than itself, but talent instantly recognizes genius.” by Conan Doyle.