SHEMEJI NIMETEGEKA ASANTE
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
Sehemu ya 21
👉 wakachukua pesa na kuondoka kwenye jiji,
Dah yani…👇
Kaka anajua pesa hipo wapo hotelini sasa na pesa kidogo wanafanya mahaba yao,
Yani sauda lipende anamwigizia kaka kama anampenda kweli,
Uku kichwani mwake anawaza kupanda ndege kwenda uharabuni,
Na kaka anawaza kutafuta biashara ya kufanya na pesa kidogo atafute japo kibanda cha vyumba vitatu maisha yahendelee,
Sasa wote wapo na mawazo yasiokamirika,
Sauda anampa penzi kaka moyoni anasema ndio la mwisho mwisho hili utaisoma namba.
Kaka yeye anashindua tu kwa raha zake anajua pesa hipo benk kwenye akaunti ya sauda lipende,
” Upande wa mume wa aliyekuwa mke wa kaka yani shemeji,
Aliwaagiza mafundi wapige rangi nyumba yani mkewe aje akute nyumba safi yenye mvuto mwenyewe yupo zanzibar anakura raha ya ndoa taratibu,
Asikwambie mtu penzi la ndoa ni tamu kuliko la kudhini kama ujaolewa omba kwa Mungu wako upate mume kwa wewe mwanamke kwa wewe mwanaume fanya mahamuzi ya kuoa,
Basi shemeji ambaye alikuwa mke wa kaka yupo na mumewe lakini ajaacha kusikiliza mawaidha yani anafunguria redio anasikiliza maneno yenye tija sio anasikiliza,
Vipindi vya ajabu ajabu kuchambana mtaani,
Basi mawaidha yalikuwa siku iyo yanasema ivi..
” Tuwaheshimu tuliyo nao sababu kuna watu wamekosa fursa hiyo ndoa ni neema kubwa kuliko ujuavyo hakika ya mapenzi ni vile utakavyoyaweka ndo yatakaa hvo hvo ikiwa Shari yatakaa kishari yakiwa ya kher yatakaa hvo hvo kikheri busara nidhamu utu heshima na kujali hubebwa na neno “NAKUPENDA”
Ndo wako hata kama hana kitu muheshimu mjali mthamini heshima ni kitu adimu hulinda CV yako na ni urithi Mkubwa kesho kwa wanao Basi tujiheshimu tupate kuona fahari kwa watoto wetu na tuheshimu ndoa zetu tupate kuwa na vizaz vyema Allah atuhifadhi sote Ammyn.
” Jamani shemeji akamwambia mumewe nakupenda,
Na mumewe akamwambia shemeji nakupenda,
Kilichoendelea hapo wale waliolewa wanajua yani wanafanya yao tena kimpango wao raha ya Saba wanakura.
” Sasa upande wa kaka siku ikafika sasa anataka akafanye biashara,
Asubui asubui kwanza amuoni sauda lipende,
Akajua kuwa ameenda labla kutafuta chakura,
Sasa anatoka nje ya hoteli anasikia kuna mwanamke mjamzito amedondoka nje ya bank,
Ikabidi aende uko bank,
Picha inaanza sauda kadondoka KCB BANK,
na pesa aliweka NMB BANK,
Sasa kumbe kabla ajadondoka alisema alimwamishia pesa mwanaume na mwanaume kumbe katoa pesa zote ajui yupo wapi?
Taarifa zile kaka alivyozipata mkojo ulikuwa unamtoka habari ana anajiuliza anaota au ni kweli,
Sauda anapakiwa kwenye bajaji anapelekwa hospital,
Kaka anajikuna kichwa anaisi kama ana sisimizi kichwani,
Na wauni sasa wanasema,
” Yule mwanamke kashapigwa na bwana ake itakuwa mjini hapa unakuja kichwa kichwa macho juu juu unadhani kila mwanaume ni mwanaume wako wengine wezi tu kwenye mapenzi.
” Maneno ya wauni yanasababisha kaka atoe machozi na alie kama mtoto mdogo na ndipo alipoonekana amejikojorea.
” Sasa wanamuuliza kulikoni ndugu mbona kojo kama lote chozi mwamwamwa.
” Jamani wauni si watu wazuri wanamuuliza uku wanapita na simu yake na akiba ya pesa ndogo aliyonayo,
Kaka kachanganyikiwa ajui aseme nini,
Wakati akili inamjia yani anajua sasa anafanya nini ndio simu ana na pesa ya akiba ana na wahuni washasepa,
Wenyewe wana kauli yao kufa kufaana kaka alikufa kifkra dk 3 wao wakapita nae,
Kaka Jamani aliweka mikono kichwani yani alipiga kelele kama vile wanawake wanavyolia wakiwa wanafika eneo la msiba,
Dah yani…
Sehemu ya 22
Kelele zake azikuwa msaada kwake bari zilifanya wengi wajue mengi,
Upande wa hospital sauda alizinduka akaongea ukweli wote yaliyomfanya aanguke,
Sasa akawa anaomba msaada wa nauri arudi kijijini tu,
Sasa alipomaliza kusema ukweli kuna dokta mmoja akasema,
” Jamani hili sio swala geni kwenye ulimwengu huu ila hili swala mfano wake samaki kala mtu,
Kwanini nimesema samaki kala mtu?,
Nafafanua ivi kila siku samaki anariwa na watu ila akuna taharuki ila samaki akila mtu kunakuwa kama ivi,
Kwa sababu wanawake wengi wanafanya matendo aya aliyofanya faki kwa uyu sauda,
Wanaume tunaumizwa sana na wanawake mpaka tunafirisika ila inakuwa kimya kimya,
Sasa Leo mwanaume kamliza mwanamke,
Mambo yamekuwa mengi ila neno langu kubwa kupitia tukio hili kuna cha kujifunza acha niende kumtafuta uyo Rama ambaye ndio mwanaume aliyeuza nyumba na pesa kampa mwanamke na mwanamke kadhurumiwa,
” Basi manesi walimpa msaada sauda na akarudi kijijini kwao akutaka ata kuonana na kaka maana ajui ata atasemaje,
Sasa yule dokta alienda kumtafuta kaka na akamwambia ukweli wote ambao alikuwa aujui,
Sasa bahati mzuri kaka alikuwa na rafiki zake wakawa wanamwambia,
” Wewe umekosea kumuacha mkeo ambaye alikuwa ni msaada mkubwa kwako na kwa mzazi wako sasa iyo ndio faida ya ujuaji sana kama ungekuwa na utulivu wa akili,
Usingefanya uliyoyafanya ona sasa faki kafanya yake kwa mwanamke wako uliyemwita mzuri na kakuliza kwenye maisha yako ila umetufunza Sisi wengine tupende wake zetu Kwaheri.
” Kuna mwengine akamwambia mimi nakushauri nenda kwa uliyemuuzia nyumba kamwambie ukweli wote wa maisha yako yani aya yaliyokukuta hili akupe nauli na uwende kijijini kwa mama yako ukamuombe samahani,
Hii ni ladhi ya mama yako mimi nakwambia ukweli kwa sababu kama unakumbuka ushawai kuniambia ulimfukuza mdogo wako ukamfukuza mkeo na mama yako,
Hapo ulikosea sana unaona auna kazi na tatizo ilo limekufika ushauri wangu ni huo ukipuuuzia Kuna kubwa kuliko juu yako.
” Kaka akaona afanye ivyo aende kuomba msaada kwa aliyemuuzia nyumba,
Sasa anafika pale anakuta nyumba yake imepigwa rangi ya kisasa yani ina muonekano mzuri sana,
Bahati yake sasa ndio siku shemeji yani mkewe mwenyewe aliyemuacha kasharudi zanzibar anakuja kukabiziwa nyumba,
Sasa kaka yupo nje ya geti na gali prado imesimama,
Jamaa ambaye ndio mume wa shemeji akashuka ila mkewe yupo ndani ya gali,
Kaka ajamuona mkewe wa zamani sasa akawa anamwambia jamaa ukweli wa maisha yake na amuombe msaada wa nauli aende kijijini,
Yani aje uku,
Sasa jamaa akasema,
” Pole sana sasa acha nimwambie mke wangu akusaidie maana hili limekukuta ni kubwa sana na yote aya kwa sababu umeoa mwanamke asiye na hofu ya Mungu sasa sio kama nimekudharau kukwambia namwambia mke wangu akupe pesa ila tukio lako ni kama somo kwangu mimi na mke wangu ningependa kumshirikisha asome kidogo.
” Mume wa shemeji ajui kama yule alikuwa ndio mke wa uyo anayemwambia apewe msaada yani kaka,
Na shemeji kasikia yote wanawake wanavyopenda kujua mengi alishusha kioo kidogo maneno yote amesikia,
Sasa mumewe anafungua mlango wa gali,
Shemeji anashuka,
Kaka anamuona aliyekuwa mkewe ndio anashuka na ndio anapaswa kumpa msaada,
Yani macho yanakutana nga nga nga,
Jamaa anasema,
” Uyu ndio mke wangu acha nimwambie mimi kwa ufupi na akupe msaada maana hapa ni kwake hii nyumba nimemnunuria yeye.
” Kaka amebaki ameshangaa tu yani aelewi.
” Jamaa akamwambia shemeji yote na akamwambia mpe nauri arudi kijijini uyu..
” Sasa hapo mtihani upo kwa shemeji je atampa nauri au atamwambia ukweli mumewe uyu ndio aliniacha kwa dharau na mengineyo dah yani…
Sehemu ya 23
Shemeji akutaka makuu akaona kama dunia ishamwazibu aliingia kwenye pochi alimpa laki mbili.
” Shida aina adabu kaka anapokea pesa uku anaria,
” Shemeji yule akutaka mengi akarudi kwenye gali na mumewe mlinzi anafungua mlango wanaingia ndani,
Swala lilimuuma sana kaka sasa mwenyewe anarudi kijijini kuja kumuomba samahani mama,
” Sasa shemeji yule aliyekuwa mke wa kaka alituma mafundi kijijini waje wamjengee mama nyumba ya kisasa bado anampenda sana mama,
Na mimi nikawa ndio msimamizi wa iyo nyumba ya mama,
Kaka anakuja anaona ujenzi unaendelea nipo na mama,
Kaka anapiga magoti na kuomba samahani kwa mama na kwangu mimi,
” Damu mzito kuliko maji mama alimsamehe kaka,
Na kaka alisema yote yaliyojili.
” Mama alimwambia,
Rama mwanangu waswahiri wanasema asiyesikia la mkuu uvunjika guu,
Wewe usemi huu ukuwai kuufanyia kazi sasa umekuwa kituko taarifa zako zimeenea mtandaoni yani kabla ujaja Sisi taarifa tunazo.
” Kaka anashangaa mama anatumia tambo la maana yani amepewa na shemeji aliyekuwa mkewe,
Na mimi nipo na tambo la maana,
Kaka akazidi kujuta kwanini alimuacha mkewe mwenye maono.
Upande wa sauda lipende aliteseka na mimba na akajifungua mtoto wa kiharabu ambaye ndio faki yani mtoto wake anazidi kumkumbusha ujinga wake,
Sasa kaka akawa analima vibarua na akawa amerudi kijijini RASMI,
Mimi niliwaza sana juu ya maisha ya kaka na yangu kwa ujumra nikawaza juu ya shemeji nikapata jibu kumbe mwanamke anaweza akabadirika na akawa mtu mwema sana inategemea yupo na nani karibu,
Nasema aya kwa sababu shemeji alipokuja kijijini alikuwa na tabia za ajabu ila mama kupitia mawaidha amembadirisha shemeji,
Shemeji aliweza kunitega mpaka nimetembea nae aya yote yalikuwa ni sehemu ya maisha yake ambayo alikuwa ana mtu wa kumpa maneno yenye tija,
Sasa ubadirikaji wa shemeji wa tabia na mimi kuanzia Leo nimebadirika,
Inawezekana kumbe ukawa na tabia mbaya ila ukiamua kubadirika inawezekana,
Ukatoka upande wa shetani na ukawa upande wa Mungu nadhani uliyekuwa mwanzo wa simulizi hii kuna kitu umeona kuwa inawezekana hili nililosema hapa,
Naomba kama wewe una tabia mbaya Basi jaribu kubadirika,
Kama tabia yako IPO kama mimi nikitegwa nategeka badirika,
Kama tabia yako IPO kama ya shemeji kutega kaka au wadogo wa mumeo au marafiki badirika,
Ukiwa ivyo shetani yupo kazini na wewe,
Sina mengi nampenda mama yangu na aliyekuwa shemeji amemfanya mama kuwa na mtoto wa kike ambaye ndio yeye shemeji ametujengea nyumba,
Yote aya ni mabadiliko ya tabia,
Jamani sauda na kaka wanaishi kwa maumivu makari ila kaka ndio yamezidi sana nadhani akija kuoa tena atoweza kufanya aya aliyofanya kwa sababu ataki kabisa kumuona sauda lipende,
Ni mwiba kwenye maisha yake,
Sina mengi na hapa ndio mwisho wa simulizi hii,
Tuonane kwenye simulizi nyengine asante.
              *Mwisho*