NDOA YA SITA, SINA MTOTO, MGANGA AMENIAMBIA…..
Habari Raha Special, naomba unipostie nipate ushauri, mimi ni mwanamke wa miaka 44, lakini sijawahi kushika ujauzito wala kuwa na mtoto naumia sana, kwani sjawahi kuwa na furaha kabisa nimekaa kwenye ndoa hii sasa ni ya sita wanaume tofauti wote wananiacha kisa sizai.
Mwezi wa kwanza nilienda kumtemberea mdogo wangu huko kijinini, akanishauri kuna mganga anatibu shida kama hizo nikakubari nikaenda turipofika mganga akanipima na kioo akasema mayai ninayo ila yako mbari akaniambia kama ninania nimperekee laki sita nitapona kabisa. Wakati huo mm sikuwa nahela nikarudi kusubiri hera yangu ya mchezo nikapokea nmepata hiyo laki sita.
Nimerudi kwa mganga, cha ajabu ananiambia dawa mpaka nilale nae ili anipitishie dawa asafishe njia, jaman naomba munisaidie sina hamu nakula sishibi mwenzenu