MTOTO WA KISHUA USIINGIZE WEWE NI ADUI YANGU
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
Chapter 1
“Jitahidi ukafanye kazi yako sawa mwanangu?”, alisema baba yake Graziella na mama yake pia akasisistiza “sitaki yatokee makosa, wale ndio sababau ya dada yako Lovenness kupotezaa maisha kumbuka hilo mwanangu”, “sawa mama sitakaa niwaangushe kabisa katika hili wazazi wangu mnayopitia yote nayaelewa hivyo naomba mniamini nahakikisha kwamba sitawangusha kwangu nyie ni wa thamani aliongea Graziella kwa muonekano ilionekana kama vile ni kiapo, kwa wazazi wake hivyo “sawa tunakuamini hakuna mwingine wa kufanya hivi bali ni wewe mama yake alisema huku baba yake akidakia akamwambia “watoto waangu wote wanajulikana na familia ya Mr Thomas kasoro wewe peke yako, kwahyo fanya kazi yako nishafanya dili pale ukafanye kazi mule ndani usiniangushe nakuaminia daktari wangu”, sawa baba sitovunja uaminifu wako…….
Na Graziella aliondoka moja kwa moja kuelekea kwenye familia ya Mr. Thomas, alifika getini akagonga kengele na kuingia ndani kwa kujiamini kabisa, alifika akamkuta mfanyakazi akamslimu “habari ninaweza kukutana na Mr. Thomas?” aliuliza Graziella yule mfayakazi alijibu akamwambia ‘ndio yupo kule juu kwenye sitting room”, “asante” alijibu Grazzy na kuelekea mahala alipoelekezwa na yule mfanyakazi wa mule ndani
Grazzy alifika akamsalimu Mr. Thomas na kisha. akaketi “wewe ndie uliekuja kufanya interview officine kwangu?” aliuliza Mr. Thomas huku akimtizama Graziella kwa makiini usoni Graziella akamjibu “ndio mkuu ndio mimi”, “mh sasa hapa kama tulivyosema miss. Agness David, umefanikiwa kabisa kupata kazi na sasa wewe ni daktari wa familia, je umekuja na vitu vyako? kabisa maana utakuwa unaishi humu humu ndani na kupewa siku moja ya off ili kwenda kuwasalimu ndugu zako”, “ndio mkuu nimekuja na kila kitu changu kwasababu nilipokea barua rasmi ya kuja kuanza kazi yangu mkuu, alijibu Graziella Roman, huku akiwa anajulikana kama Agness Daniel alifanya hivyo ili kutojulikan na iwe rahisi kufanya jambo lililomleta pale kwenye ile nyumba
Aliendelea kusema Mr. Thomas ‘mh usijali hapa wa kumuangalia ni mimi hapa nimekua na maadui wengi sana hivyo nimepitia mengi sana mpaka sasa nimenusuruka kifo na nipo hapa na maradhi mengi hivyo naoogopa sana kwenda hosptali mar kwa mara naeza nikapangiwa trick huko huko hospitali na maadui zangu hivyo nimetafuta muangalizi wa nyumbani ikiwa ni wewe hapo kam daktari wangu na wa familia nzima, Graziella alikuwa anamsikiliza tu na kwa jinsi alivyokuwa akimtizma Mr. Thomas ni wazi kabisa alikuwa anamtizama kwa hasira sana. ‘sawa mkuu ila kwanini sasa watu wanakuandama hivyoo mkuu?”, aluliza Grazzy kwa mtego, ‘ni mambo tu haya ya kibiashara tu unajua mtu ukiwa na nafasi hamna kingine kubwa serikalini pia kwenye vyanzo za kibiashara pia ukiwa vizuri inakuwa na visa vingi alijibu Mr. Thomas kwa dhahir kabisa ya kukatisha maswali ‘sawa mkuu ila yataisha yote”, alisema Grazzy muda huo akiwa kama Agness, unaeza kwenda kupumzika kwanza, chumba chako ni cha pili kutoka mwisho upande wa kushoto”, “sawa mkuu”, alijibu na kuondoka zake
Kufika chumbani anamkuta mwanaume yupo kifua wazi hee cha kushangaza hakushangaa ila akamsogelea “toka chumbani kwangu” aliongea Grazzy kwa mkazo, “kumbe we binti hujiheshimu? unaingia vyumba vya watu husemi , unaingia tu kam chooni sio? afu unasema toka chumabni kwangu” aliliongea huku kabana pua akijaribu kumgeza Grazzy, kabisa “mimi na wewe mwenye chumba hiki ni nani?”, aliuliza yule kijana, Grazzy akajibu akamwambia “hata kama. ni nyuma ya baba yako huwezi nifukuza chumba nilichoelekezwa nije nifikie mimi wewe mbona huna adabu na wageni au ndio nyie msiopenda wageni waje nyumbani kwenu?” aliiuliza Grazzy, ‘hivi wewe kwanza unaitwa nani?”
aliuliza yule kijana maana nakuona kamal
umepotea direction vile hebu angalia hichi
chumba ni cha wageni kabisa kinavyoonekana?”
, na kweli Grazzy akiangalia hakionekani kama ni
chumba cha wageni kwa sababu kila sehemu
kulikuwa na picha na vitu vya yulle kijana
alisoma kwenye picha moja inaonekana kama
cheti imeandikwa jina David Thomas, “kwahyo
nimeambiwa tofauti au?”
aliuliza Grazzy “usijali ngoja niulize kwanza alisema David huku akichukua simu na kumpigia baba yake akaongea nae kisha akamgeukia Grazzy “Sorry miss Agness umekosea chumba. umeambiwa cha pili kutok mwisho upande wa kushoto umeingia cha pili kutoka mwisho kulia hivyoo chumba chako ni hicho ambacho kinatizamana na changu ukifungua mlango wangu”, wee Grazzy aliona aibu kweli kwa jinsi alivyojifanya mbabe mbele ya mtu mwenye. chumba chake “sorry alisema Grazzy na kuondoka kuelekea chumbani kwake.
Chapter 2
Grazzy alienda chumbani kwake na kuanza kujicheka yeye peke yake maana alijiona kajifanya mwamba kumbe kweli yeye alikuwa amekosea akapotezea na kuendelea na mambo yake mengine “kwanza inabidi nifocus na mambo yaliyonileta hili lishatokea lishapita tayari hakuna haja la kuliwaza ila mimi jamani uhhh niache ujinga alijisema mwenyew Grazzy
Muda ulipita na sasa yule mfanyakazi akaja kumgongea “miss muda wa chakula tayari njoo ule alisema yule msaidizi wa ile nyumba “samahani unaeza niletea huku huku alisema Grazzy, yule mfanyakazi alishangaa yani mgeni siku ya kwanza anataka kuletewa chakula chumbani kama boss, tena na yeye ni mfanyakazi alijiwazia yule mdada wa kazi kabla hajaondoka sijui Grazzy alijishtukia akasema “sorry nakuja nilikuwa naongea na simu kuna vitu waniletee huku huku”, alisema Grazzy na kufungua mlango na kuongozana na mdada wa kazi wakaenda sebuleni
Walifika akawa kaketi mezani yule mdada wa kazi akamwambia “Grazzy, samahani sisi hatulii hapo”, Grazzy alishangaa, akakumbuka kumbe na yeye ni mfanyakazi, lakin Mr. Thomas alimzuia “unaeza keti hapa hapa miss, we ni daktari na sio mfanyakazi wa kawaida kwahyo unaeza kuketi kwenye meza bila wasi wasi wowote”, akatokea Gladyness ambae ni mdogo ake na David “mh afu kama nakufanisha na mdadal mmoja hivi nishawahi soma nae primary sema ashafarikigi jamani Mungu amlaze mahali pema peponi, aliongea Glady kwa huzuni kweli. “kwani yallyokwisha kutokea si yametokea tayri sasa kwanini tuyazungumzie kila siku alisema mama yake na David’, ‘mh miss jiskie huru sisi ni watu poa sana hivyo usiwe na wasi wasi kabisa mwanangu alisema Mr. Thomas akimkaribisha kwa mara nyingine Glaziella kwa wangejua jina lingine Agnes “mh ninavyowachukia wasingejaribu kuongea chochote hapa natamani niwaue hapa hapa ila sina jinsi, alikuwa anajiwazia mwenyew Glazzy “unawaza nini miss? aliuliza Glady “hamna bhana siwazi kitu nilikuwa tu nafikiria kuhusu dawa za baba, hapa inabidi zikafuatwe, alisema Glazzy ‘ooh kumbe kwani kaka David si utatoka? aliuliza Gladdy “yeah nitatoka nitaenda ndio naenda kwangu alisema David” “haa lakini bro, baba si alisema kwamba usiende leo kwako yapasa uende officine Gladdy alisema “mh usijari nitarudi kuna vitu nafata alisema David “okay unaeza pitia dawa za baba, miss unaeza muandika kaka na kaka akafuata hakuna tatizo”. Glady alikuwa akimwambia Grazzy, Grazzy aliandika zile dawa na kumpatia David lile karatasi na kuondoka zake
“Mh huyu msichana etty kaingia ndani kwangu afu akaleta ubabe jamani huyu mdada sijui ni waa aina gani mgeni lakini mbabe hivi” alisema David akimwambia dada ake Graddy “mh we nae si alikosea chumba, jamani ndio iwe mada? nashangaa leo mtu hajazibuliwa mkofi” alisema Graddy ‘mh sawa bhana sister baadae” alisema David huku akinyanyuka na kuondoka zake kuelekea kazini….
Upande wa Grazzy alikuwa ameenda chumbani kwake na alikuwa anaongea na simu na wazazi wake kuwajulisha kila kitu kinachoendelea pale ndani, na kuzidi kupanga mikakati mirefu sana ya kulipa kisasi, mara mlango unagongwa Grazzy akakata simu mapema na kumruhusu mtu aingie na ni Graddy alle ingia ndani
“Samahani lakini kuna kitu nataka kuongea na wewe miss alisema Graddy huku akimwambia Graazy au Agness “sawa hakuna shida niambie nakusikiliza, alijibu Grazzy “sawa lakini unafanania sana na yule rafiki yangu aliepotez maisha, nimejikuta natamani kuwa karibu yako muda wote Agnes alisema Graddy kwa hisia kali “anaitwa nani rafiki yako na kwa nini alikufa?’, aliuliza Grazzy kwa mtego pia ‘hhhh anaitwa Loveness msichana mpole, mwerevu, anaongea taratibu sana. mrembo sana natamani nimuone tena ni mtu mzuri sanal kwangu ni rafiki bora alisema Graddy huku akibubujikwa na machozi kwa wingi mno, ‘yani nina hamu nianze na wewe kwanza kukuua lakini sina jinsi ningekuwa na uwezo ningekuchoma kisu hapa hapa, ila nataka kujua kwanza sababu za dada yangu kufariki alikuwa akiwaza peke yake Grazzy “mh sawa naweza kujaribu kuwa kama huyo rafiki yako ila mpaka nijuee hadi kwanini alifariki na tabia zake zipoje Graddy naeza play part ya rafiki yako…..
Graddy alimkumbatia Grazzy kwa furaha asante sana ‘nina ahidi kusemaa kila kitu kama ukiwa mkweli kwangu na muaminifu nitakwambia kila kitu alisema Graddy akimwambia Grazzy “sawa utaniambia tu ukiwa tayari nasubiria kwa sasa sisi ni marafiki wa kweli hivyo tutakuwa wote kwenye kila kipindi chetu cha maisha ninaahidi hiloo kwako alisema Grazzy moja kwa moja akimwambia, Graddy
Graddy alitoka nje akiwa na furaha ya kweli kabisa ndani yake mh Ikni sio kwamba Grazzy ana furaha hapana ila kuna kitu anahitaji kutoka kwa Graddy
Mara mlango wake ukagongwa tena muda huo ulikuwa usiku tayari alikuwa kavaa night dress zake pale hana shida mwanzo alikuwa akidhani ni Graddy hivyo alienda kufungua mlango hee cha ajabu anamkuta ni David, tena alivyokuwa hana haya kaingia moja kwamoja chumbani yani mlango umefunguliwa nay eye huyo moja kwa zote chumbani…
Chapter 3
“Habari za usiku alisema David akimwambia Grazzy “salama unaeza kutoka humu ndani, kumbe huna adabu wewe unaingiaje chumbani kwa mwanamke hivyoo huoni nilivyoo hivi?” Grazzy alishout “okay mimi na wewe nani hana adaabu wewe pia si uliinngia ndani kwangu bila hodi na ulinikuta kifua wazi aliuliza?” kwa panic David “hee kumbe we mkaka ni chiz kwahyo ni kisasi baada ya hapo si ilijulikana kama nimewrong chumba au unatakaje labda nikuombe msamaha kwa magoti?” aliuliza pia Grazy wamekutana wote short temper basi hapo ni kupayukiana tu kam hawana akili sawa vile “ndio ni kisasi kwani huelewi aliongea David “wewe sikia sema shida yako sio unakuja hapa kuleta ujinga, kwanza nimekutuma dawa ziko wapi mbona unaleta mambo mengine hapa?, nipe dawa na utoke chumbani kwangu” alisema Grazzy “ohoo kwahio unataka kuleta ubabe?. mwanamke hatakiwi kuwa mbabe sawa haya omba dawa zako vizuri sasa, aliongea huku akimsogelea Grazzy
Mara mlango ukafunguliwa alikuwa ni Grady sasa anaingia ndani “ooh kaka vipi tena mbona kama unamtishia amani daktari wetu?” alisema Grazzy akimwambia kaka yake, “mh nilikuwa nampa dawa zake tu alisema huku akimpatia mfuko Grazzy na kutoka zake nje,
“Alikuwa anasema nini huyo nae” Graddy alimuuliza Grazzy “mh usijali ni mpuuzi hivyo achana nae tu asikupe shida wala nini upo powa lakini? Grazzy alimuuliza Graddy “yeah nipo fresh nilikuwa nimekuja kulala na wewe unajua kipindi nipo hostel na Loveness nilikuwa siwez kulala bila yeye hivyo nahisi kama amerudi tena baada ya kukuona wewe unavofanana nae yani kama vile ni ndugu yako”, alikuwa anaongea Graddy “hhhh ila wewe karibu tulale usijali jiskie huru mimi sio Loveness ila naweza kuplay part ya Loveness worry out nipo kwa ajli yako mimi ni wako kwenye kila hatua hivyo kuwa na amani”
Walilala wote usiku wote, na hatimae asubuhi ilifika Grazzy alikuwa wa kwanza kuamka akaelekea jikoni alikuwa wa kwanza kuliko hata mfanyakazi wa mule ndani alienda kupika chakula cha mgonjwa, na kwa kupika tu wee ni balaa, hana baya jikoni akapika chakula cha mgonjwa akawa ameweka mezani akarudi tena Jikoni saaa ngapi David asimfuate Grazzy
“Wewe ndy unapika?” David alimuuliza Grazzy. “hamna napakua” aliongea Grazzy huku anatabasamu “hivyo ndivyo unavyojibu waliokuajiri sio?” aliiuliza David kwa dharau kweli, “mhhh kahyo wewe ndio umeniajiri? hivi hujishtukii mimi sio mfanyakazi wa kawaida mimi ni daktari wa binadamu naeza kukuchoma sindano ya sumu ukafa kwahyo pisha mbele yangu nikafanye mambo yangu”
Grazzy aliondoka moja kwa moja na kwenda mezani, hapo alimuita Mr. Thomas na wengine japo Mr. Thomas alikuwa na chakula special na alikuja ili ale halafu ameze dawa
“Subiri, unaeza kula hicho chakula kwanza wewe ukaonja kwanza?” alisema David “hee kaka kwahyo umuamini na amekuja kam daktari aliuliza Grady?”, “mh unadhani ni rahisi kuamini mtu sasa hivi sina Imani cha kwanza ni usalam. wa baba yangu halafu mengine baadae” alisema David ‘mhh ila wewe sawa nitaaanza kukila na mimi na kwa sababu mimi ndio nilopika nitaonja vyote alisema Grazzy” (nilijua tu kama haya yanaweza kutokea ndy maana sikutaka kuwauwa kwa sumu ya kwenye chakula nyie mtakufa taratibu yaaani bila wasi wasi) alikuwa anayawazaa akilini mwake Grazzy akaonja kile chakula na kusema “kipo salama”
Walikula wakamaliza wakatoka mezani kila mtu akenda kwake ila David alikuwa anaenda kazini hivyo alienda kuchukua pc chumbani lakini kabla hajaondoka akaingia chumbani kwa Grazzy tena. bila hodi “kama nikihisi kuna mpango wowote mbaya unaendelea kuhusu familia yangu na unakuhusu ntahakikisha haubaki salama macho yako yanaonesha kuna kitu unaficha” alisema David akimwambia Grazzy, “kwahyo unanihisi vibaya mimi sio?” aliuliza Grazzy “siamini yoyote anaekuja kwenye hii nyumba, baba ana maadui wengi sana na sijui kwanini”. alisema David “hhhh sasa sio kila mtu ni adui wa baba yako wengine baba yako ndio adui yao elewa hilo GRAZZY alizungumza hilo kwa mafumbo sana akimwambia David “sawa mimi naenda kazini incase kama kuna chochote kitatokea nipigie” alisema David akichukua simu ya Grazzy kwa force akaaandika namba na kuondoka zake alipishana na dada yake. mlangoni “aya me natoka baaade tutaongea” akaondoka yake dada yake hakujibu kitu alibaki anamtazama tu maana hamuelei mambo anayoyafanya kaka yake
Chapter 4
Gladdy akaingia mule ndani “Agness tunaweza kutoka mimi na wew aliuliza Glady “hapana leo sio siku yangu ya off nitatoka kama nikiwa off nitatoka alijibu Glazzy “okay unakuwa free lini?” aliiuliza Graddy “mhh ni Jumapili pekee ndio nakuwa niko off but siku zote nakua nipo na kazi nafanya si unajua hapa ndio kula kwangu au hujui” Grazzy alikuwa anamwambia Graddy “sawa mimi natoka nikirudi nikuletee nini?” Graddy aliuliza “mhh chochote unachoona kinaendana na me wewe niletee tu wangu” Grazzy alijbu “oo okay nitaangalia cha kukuletea kisha akatoka mule ndani
Grazzy alikuwa anaongea na simu na mama yake ‘sasa mama yani leo ilikuwa nusu nikamatwe ningechukua plani yako yakutia sumu kwenye chakula ningekamatwa vibaya mnoo ujuee mama” mwanangu bora umejiongeza laasi hivyoo ungeumbuka huyo kijana nae kiherehere sana inabidi uanze na huyo huyo “lakini mama si umesema ambae ana makosa ni Mr. Thomas? sasa inakuaje na mtoto wake aingie kwenye makosa yasiyo muhusu?” aliuliza Grazzy wewe hy roho yako ya huruma itakuponza mwisho ushindwe kulipa kisasi cha dada yako ina maana hutaki dada yako apumzike kwa amani si ndio? mama yake aliuliza “hamna mama nimesema tu kwasababu mimi naona mwenye kosa ni mmoja sasa mnataka wawe wote mama sio sawa” alisema Grazzy kwahyo unatka kuniongoza kwahyo dada yako amefariki hapo na huoni uchungu? tena ikiwezekana uwa wote wao wote wanajua kwanini binti yangu alikufa, alisema mama yake Grazzy “lakini mama siwezi kufanya uamuzi ambao sababu yake siijui niambieni kwanza chanzo cha dada yangu kufariki aliuliza Grazzy fanya kazi iliokupeleka baada da ya hapo utajua kwanini dada yako alifariki sababu zipo wazi mama yake aliongea hivyo kisha akakata simu
“Kabla sijafanya chochote kile inabidi kwanza nijue sababu kwanini Loveness hayupo duniani ukute mimi ndio mbaya afu nawaona wabaya watu wengine sul kwanza nijue kwanini ndio mengine yataendelea” alikuwa anajiwazia yeye peke yake Grazzy akiwa mule ndani
Muda ulkuwa umeenda na sasa ilikuwa ni jioni anaona namba ngeni imeingia kwenye simu yake akapokea yani ile kupokea tu anasikia “ulikuwa unaonea na nani ambae baada ya Graddynesss kuja ukakata simu?”, alijua kabisa ni David “kwahyo umeniwekea camera ndani si ndio, umeniwekea camera sio?, kwahyo uamini kuhusu kazi ninayoifanya sio?”, aliuliza Grazzy “nimekuuliza kwanza maana nahisi nmesahau kuweka micropnone ili niskie ujinga uliokuwa unazungumza aliongea David, “uhhh” Grazzy akashusha pumzi ndefu akaanza kupanic “kwahyo nisiongee na wazazi wangu si ndio? kama hivyo basi muhudumieni mzazi wenu wenyewe mimi msinishirikishe kwenye mambo yenu maana naona mnanifuatilia sana na mimi sio kwamba nina shida nah ii kazi hapaana, ninataka kumsaidia baba yako kwahyo unahisi mimi naeza kutumwa sio? hivi wewe mkaka unajionjae labda?”, alingea Grazzy kwa panic kweli, “hhhhh sawa nenda tutatafuta daktari mwingine kwaheri alijibu David na kukata simu
Grazzy akajifanya kufunga nguo zake kutoka kabitini akaziweka kweny begi akatoka nje akapita sebleni Mr. Thomas akamuuliza unaenda wapi Dr. Agness”?, “mhh baba mimi naona mwanao anaweza kukuletea daktari bora sana”, alisema Grazzy “kwanini unasema hivyo? wakati wewe umefanya interview na umeajiriwa hapa kwa usahihi kabisa hakuna makosa yaliyotokea sasa kwanini unatka kuondoka tena? , na mwanangu kafanya kitu hasa mpaka utake kuondoka hivyo kwa hasira?” aliuliza Mr. Thomas “mh baba mwanao aniamini kabisa yaan kadiriki kuweka camera chumbani kwangu, aone kila ninalofanya amesema kasahau tu kuweka microphone kwenye chumba changu ananifuatilia sana kiasi cha kwamba sielewi yaani ananiona mim pia kama vile ni adui yake yaani najikuta sielewi sasa mambo anayoyafanya kabisa mwanao mimi simuelewi baba aananiona mimi sina nia nzuri kabisa na wewe” alisema Grazzy kwa kulalamika “usijari mwanangu wewe rudi ndani tena chumbani kwaako kakae tu mwanangu namsubiri huyo mpuuzi David mbona kawa na tabia za ajabu sana wakati sio kawaida yake kabisa yaani kawa wa kitofauti nakuwa simuelewi kabisa anakua kama mtoto alisema Mr. Thomas huku akimwambia Grazzy “sawa baba nimekuelewa alisema Grazzy akirudisha vitu vyake ndani kwake huku akigeuka akitabasamu kwa dharau kweli yaani
“Hivi David kawa na tatizo gani lakini? hii ni mara ya kwanza namuona David kwenye halii hii simuelewi kabisa au ana tatizo linamsumbua anashindwa kusema jamani hawa watoto wa kizazi kipya jamani wamenishinda tabia kabisa alikuwa anasema Mrs. Thomas akimwambia mume wake “mhh kuna tatizo hapa yabidi tumsubiri muhusika wa hili swala David mwenyew maana sijawahi kumuona kwenye haya mambo kuna kitu kinaendelea hapa hakuna lolote alisema Mr. Thomas “sawa mume wangu tumsubiri huyu kijana wetu maana kabadilika sijui kwanini anamfuatilia sana huyu mwanamke na hajawahi kujisughulisha na mambo ya kike kabisa: alisema Mrs. Thomas..
Chapter 5
Graddy alikuwa wa kwanza kurudi nyumbani kwao maana yeye alikuwa hajaenda kazini bali alikuwa ameenda kuzurura tu huko na mambo yake “baba shikamoo, mama shikamoo alisalimia Graddy huku akiendelea na safari zake
“Wewe suburi kwanza nataka kukuliza swali mama yake alimsimamisha Graddy “ndio mama niulize tu usijari,” “mh kuna nini kinaendelea kati ya kaka yako na yule msichana daktari?” mama yake aliuliza hilo swali “mama mimi sijui mimi mwenyew namshangaa sana kaka sijui kawaje jamani naona kawa na tabia za ajabu sana nakua nashindwa kumuelewa kabisa mambo. yake yanamaanisha nini yani maana anamfatlia sana huyu daktari” alisema pia Graddy “mh unavyoambiwa hapa kamuwekea camera chumbani kwake mtoto wa watu hana amani kabisa, anataka kuondoka kwenda kwao maana kaka yako anampa shida sana jamani ndio kwanza ana siku mbili hamtaki kumpa uhuru mtoto wa watu kwanini?” alisema mama yake Graddy “Jamani hii too much kwahyo kaka na yeye kaweka hadi camera mama there is something going on kabisa maana hii sio kawaida kabisa ya kaka, tumsubiri mwenyew pekee ndio mwenye majibu ya maswall tunayojiuliza sawa mama, alisema Graddy huku akiondoka kuelekea ndani kwake anapolala “kaka akirudi mtaniita” alisema pia Graddy na kuondoka zke kekulekea chumbani kwake
Chumbani kwa Grazzy yeye kachnganyikiw kweli maan kama maicrophone ingekuwepo hapa sijui ingekuaje maana leo ukweli wake wote ungejulikana wazi mlango ukafunguliwa akaingia Graddy akamkumbatia “pole bhana ujue najua kabisa una wasi wasi sana ila mama ataongea na kaka David na mambo yote yataka sawa usijari bwana, na wala usiondoke mimi nahisi kabisa nipo na Loveness hapa karibu yangu uwepo wako ni wa maana sana kwangu alisema Graddy, Grazzy acha aanze kulia kwa unafki “naogopa sana ujue kwahyo kama ningevua nguo hapa kabla kaka yako hajapiga ningeonekena hadi mwili wangu mimi kukaa hivi siwezi yaani bora tu niondoke maana nashindwa kuevaluate kwakweli” alisema Grazzy “hapana baba na mama watalishughulikia hilo sawa usijari sawa mama angu?” alisema Graddy “sawa nimekuelewa my friend” alisema Grazzy huku anafuta machozi pale
Mara simu ya Graddy inaita “hallo mama, Graddy alianza kuongea na mama yake “sawa mama tunakuja”, akakata simu akamgeukia Grazzy “mama kasema tushuke chini muda wa kula halafu kaka amerudi….”
Graddy alimwambia Grazzy au Agness kwaalivyojitambulisha pale kwao
Wakashuka chini sebuleni wanamkuta David. kaumia umia sana yani kama mtu aliopigwa sana mh Grazzy alishtuka akajua hawa n wazazi wake maana alimueelezea mama yake juu ya David kumfuatilia sana, “nini kimemkuta kaka David?” aliuliza Graddy “mh anasema tu alivamiwa na watu wakampiga sana na kumpa vitisho tu yaaani nusu afe kijana wangu” alisemaa mama yake, “jamani haya mambo mwisho wake lini jamani mbona wanatukosesha amani hivi lakini mara ya pili hii sasa, kaka hadi anashindwa kwenda kwake kwa ajili ya hivi hivi jamni kwanini tunakuwa hatuna amani na maisha yetu lakini? tunafatiliwa kila sekunde jamni hivi ni kwanini lakini mambo yanakuwa hivi?” Graddy alikuwa alalamika kila dakika “enhe tumpeleke sasa chumbani afu daktari tukimaliza kula utaenda kumuhudumia David sawa?” alisema Mrs. Thomas “kuhusu swala lako nishamuita fundi akatoe hyo cctv chumbani sawa binti?” alisema Mr. Thomas “sawa hakuna shida kabisa uncle” alijibu Grazziela wakampeleka David ndani wenyew wakarudi kula pia, wakamaliza
Graazzy akabeba chakula ampelekee David ndani kwake,
Akaingia chumbani kwa David ila hakwenda peke yake alienda pamoja na Graddy “haya ni muda wa kula amka” alisema Grazzy “sasa madaktari ni wangapi?ni Agness au Graddyness? aliuliza David “ni huyu Agness” Graddy alijibu “okay unaeza ukatoka ukamuacha daktari afanye kazi yake wewe ukaendelee na mambo yako sawa mdogo wangu?”, alisema David akimkazia macho Graddy, “sawa kaka mimi natoka ugua pole Graddy akatoka “na ufunge mlango sasa sawa?” alisema David, Grazzy anamtizama tu, Graddy akaondoka zake na akafunga mlango kama alivyoambiwa na kaka yake, ndani wakabaki Graziella na David
Inaendelea…..

