KWA MAPENZI HAYA LAZIMA TU NIMSALITI
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
SEHEMU YA 06
“Kufa wewe ambaye huna faida, mbwa koko wewe, wa matopeni, kenge mmoja, chitokonya husiyependwa, sijui hata kwanini nilipanda hii ndege ambayo wewe upo, natamani hata huko marekani nisiende kwa sababu sitaki kukaa nchi moja na katili kama wewe, hata hii sayari ya dunia ni bora nihame niende nikaishi Pluto huko!” Mdada aliendelea kunishushia maneno mazito akiwa ananitemea mate.
Mwanzoni mlinzi alitumia ustaarabu kututuliza lakini baadae aliamua kutumia nguvu, alichomoa pingu kisha alimfunga yule dada; alimpa ishara atulie hasipige kelele. Hata hivyo yule dada aliendelea kuropoka maneno mabovu, mlinzi alichukua plasta alimziba binti mdomoni, hapo sasa lile domo lilitulia. Baada ya kumalizana na mdada alinitazama mimi ambaye nilitulia, aliwaza anifunge au aniache? Alitambua kabisa kuwa sikuwa na shida ila ili kutengeneza haki sawa aliamua kunifunga pingu kisha aliniziba plasta mdomoni, baada ya kutuadhibu aliondoka. Ndege ilizidi kuchanja anga, ukimya mzito ulitawala, watu walikuwa wanatutolea macho lakini sisi wenyewe hatukutazamana, nilijua kabisa yule dada ana hasıra na mimi, nilitambua kuwa ananichukia vibaya mno, lakini sikuogopa kwa sababu hata mimi tayari nilimfutilia mbali, sikutaka hata kumuona.
Nilitazama saa yangu nilikuta ni saa 9 mchana, masaa matano tayari yalikatika, kutoka JKIA Nairobi hadi New York ni masaa 14, hivyo basi yalibaki masaa 9 hadi tufike huko tunakokwenda. Nilishangaa kuona mwendo wa ndege umebadirika, kumbe walikuwa wamebadili rubani, kulikuwa na marubani wanne pamoja na wahudumu 14. Wale wahudumu walianza kugawa vyakula, kila mmoja alipewa chakula alichohitaji, kwakuwa ni muda wa chakula yule mlinzi alikuja kutufungua, alituondoa pingu na ile plasta, hatimaye tulibaki huru, kutokana na kuhisi njaa kali nilikamata chakula changu nilianza kupiga menyu. Yule dada alikausha tu, nilimtazama kwa jicho moja niligundua kuwa alikuwa analia, sikutaka kumgusa wala kumbembeleza; kama ameamua kulia alietu.
Pasipo kuta raj i a ghafla yule dada alichukua chakula chake kisha alisimama, nilipagawa nikijiuliza anaenda wapi? hata hivyo nilijipa matumaini kuwa anaenda chooni, lakini chooni ndo aende na chakula? Hapana kwa kweli, niliacha kula nilimtazama tu, alipiga hatua hadi kwenye siti ya jamaa flani hivi, nilimuona akiongea nae kitu flani, mara yule jamaa alisimama alikuja kukaa kwenye siti yangu alafu mdada alikaa kwenye siti ya yule jamaa, hapo sasa kimoyomoyo nilisema “ngoma inogile ishabamba”. Yule jamaa aliyekuja kukaa na mimi alinitazama kisha alinicheka alafu alinikasirikia;
“Unaujua ule wimbo mtamu wa Snu sex Snura?” aliniambia akinitazama
“Upi huo?”
“Ndo basi tena ushaharibu uhuu! Kujifanya mjuaji ushaharibu uhuu!…Sasa we unagombanaje na mtoto mkali kama yule?” “Katika wakali huyo atapita? Huo ni mwili tu kila mtu anao, sasa kwani hata akiwa mzuri mi atanisaidia nini?”
“Maneno ya mkosaji hayo, demu hadi amekuacha hapa ukae pekeako, amekukimbia mbele za watu, huoni aibu?…Alafu hivi unajua kuwa anakuchukia? Kabla hajaniomba nimpishe kwenye siti yangu alininong’oneza aliniomba bastola, nilimuuliza ya nini alisema anajisikia tu ku u a, sasa jiulize unadhani angemuua nani humu ndani kama sio wewe? Tena bro nikuambie tu kuwa unatakiwa uwe makini, yule dem atakuua kweli, hivi unajua ni mtoto wa nani yule? Japo anaishi TZ lakini mara nyingi huwa anaelekea kwa baba ya ke ambaye ni mwanajeshi wa jeshi la marekani…Tena kwa jinsi ulivyo mweusi hivyo mbona wamarekani watakunyonga kwa sekunde tu. Watakuua kwa sababu umehatarisha uhai wa binti wa watu, pia umebishana na mtoto wa mkuu wa majeshi, alafu nilikusikia ukimtukana, braza nakuomba japo tupo kwenye ndege ila ni bora ushuke urudie hapa hapa”
Jamaa alianza kunijambisha kwa maneno yake. Kuna muda niliogopa ila niliondoa woga kwa sababu hadi muda huo sikujua nimefanya koşa gani kubwa ambalo litafanya wamarekani waniue. Jamaa alizidi kunitisha lakini sikumjibu, kwanza sikutaka tena mazoea na mtu, niliamua kutulia kivyangu, nina familia mie; yanini malumbano? nilijiweka pembeni kuepusha msongamano. Safari iliendelea, masaa 11 yalikatika, yalibaki masaa matatu tufike. Nilifurahi kwa sababu tayari nilichoka kukaa kwenye ndege, pia niliona bora nifike tu kuliko kukaa bila amani, nilimaindi kweli kweli yani.
Muda huo ilikuwa ni saa tatu usiku. Sasa likiwa limebaki saa moja tufike, nilitazama dirishani nilishtuka kuona wingu zito limetanda angani, wingu lilishona kila sehemu, lilibadilika rangi lilikuwa jeusii, pia radi kali zilipiga na kumulika, kuna muda mwanga wa radi ulitua karibu na dirishani kwangu kisha nilisikia “Paaaah” kwa mbali nilihisi kama nimekufa, masikio yangu yaliziba, watu wote walilala chini, ghafla nilishangaa kuona ndege i n ayu m ba, kule m bele kwa rubani zilisika kelele nyingi zikituambia kuwa kila mtu asali sala zake kisha ajiokoe mwenyewe, wahudumu walikimbizana wakituletea maparachuti, wenzangu waliyafungua maparashuti yao wakijiandaa kuruka dirishani kisha wajiokoe, lakini Kilaza mimi hata kufungua parashuti sikujua, na ukicheki hakukuwa na muda wa kuelekezana jinsi ya kutumia parachuti kwa sababu mambo yalikuwa ni moto! Mambo ni fayaa!!
SEHEMU YA 07
“Rukeni rukeni rukeni harakaa, ndege imekamata moto wa radi…” Ilikuwa ni sauti nzito ya kiume, hata aliyeongea sikumuona.
Madirisha yote yalifunguliwa, mlango wa emergency ulifunguliwa, alianza mtu wa kwanza aliruka lakini kwa bahati mbaya parachuti iligoma kufunguka, kilichotokea huko chini hata sikujua. Wakati mambo hayo yakifanyika wenzangu wote walikuwa wamejifungua mikanda walijaa mlangoni na madirishani, hata yule jamaa aliyekaa pembeni yangu nae aliniacha mimi nikiwa nimekaa kwenye siti. Sio kwamba nilitamani kukaa kwenye siti hiyo, sio kwamba sikutamani kujiokoa, hapana, tatizo ni kwamba kila nilivyojaribu kufungua mkanda haukufunguka. Nilizungusha macho nilimtazama yule mdada ambaye niligombana nae nilimuona akihangaika kujifungua mkanda. Ghafla ile ndege ilianza kuporomoka kwa spidi ya ajabu, wale waliokaa karibu na mlango walipeperushwa na upepo walidondokea chini, wengine ambao walikaa madirishani nao walivutwa na upepo; nilishuhudia baadhi wakivunjika shingo na wengine wakibamizwa huku na huko kutokana na mvurugano mkali. Kule mbele marubani walijitahidi kuweka mambo sawa lakini walishindwa, mwisho walikata tamaa, kutokana na ndege kushuka kwa kasi hata wao walishindwa kujiokoa kwa parachuti, rubani mmoja alijitosa kuruka lakini aliishia payaba! Nilipiga ishara ya msalaba nilimuomba Mwenyezi Mungu aniepushe na hicho kikombe, nilimtazama yule mdada nilimuona naye akisali akiwa analia kwa machozi ya huruma, hata hivyo kifo hakinaga huruma, hatimaye tulifumba macho tulisali tukijiombea kifo chema, nilimkumbuka m ke wangu na mwanangu; nililia kwa mara ya mwisho kisha nilicheka kwa mara ya mwisho! Ghafla nilisikia ndege ikijigonga kwenye miti mirefu, kishindo kilisikika “tiiiih” giza zito lilitawala ndani ya kichwa na fahamu zangu, mwili wangu wote uliacha kufanya kazi, kilichofuata hapo hata sikukitambua.
****
Nikiwa katika usingizi mzito kwa mbali nilihisi upepo na baridi kali, nilishtuka nilijikuta nipo kati kati ya msitu mkali, mwili wangu wote uliuma kwa maumivu makali, nilijaribu kuvuta miguu lakini nilishindwa, nilitazama kwa makini niliona chuma cha ndege kikiwa kimenibana miguuni, miguu ilikuwa inavuja damu, pia ajabu ni kwamba nilikuwa nimekaa kwenye siti yangu ile ile, tena nikiwa nimefungwa na mkanda wangu ule ule, pembeni yangu kulitapakaa moshi mwingi ambao ulitokana na mlipuko wa ndege, pia niliona miili ya abiria wenzangu ambayo ilikauka kwa moshi na moto wa ndege, sikuona damu zaidi ya miili iliyoungua. Niliendelea kuzungusha macho kila kona nikitafuta mtu wa kunipa msaada lakini sikubahatika kumuona mtu hata mmoja, ghafla kwa mbali niliona moto flani ukilipuka kidogo kidogo, ule moto ulilipuka ukiwa unanifuata mimi, kadri dakika zilivyosogea m bele ndivyo moto huo ulizidi kukolea, nilichunguza kwa makini niligundua pembeni ya kichwa changu kulikuwa na dumu likivujisha mafuta, mafuta h ayo yalitengeneza kibarabara, ule moto ulikuwa unalifuata lile dumu kupitia kile kibarabara, sijui nguvu nilizipata wapi, fasta nilijifungua mkanda wa siti kisha nilijivuta nikitoa miguu yangu kwenye lile chuma lakini nilishindwa, m baya zaidi kila nilivyojivuta chuma kilizidi ku n i kata, nilijikuta natoa machozi nikihisi naelekea kuteketea kwa moto.
Nikiwa sijui nini cha kufanya ghafla nyuma yangu nilihisi kama kuna kitu kinajivuta, niligeuza macho nyuma nilishtuka kumuona yule binti ambaye niligombana nae kwenye ndege; binti huyo naye alikuwa kakaa kwenye siti ya ke ile ile, ilionekana ametoka kushtuka, alijifungua mkanda kisha alijivuta ili ajiokoe na moto ambao ulimuandama, alifanikiwa kujinasua, alisimama akiwa haelewi nini cha kufanya, mimi nilimuona ila yeye hakuniona, kuna muda aligeuza macho alitazama upande wangu lakini hakuniona, nilimshuhudia akilia kwa sauti kubwa mara baada ya kugundua kuwa amebaki pekeyake katika msitu huo ambao hata jina lake sikulijua. Katika kutazamatazama mara paap aliniona ila hakujua kama ni mimi, alinisogelea taratibu hadi pale ambapo nililala, kutokana na mwanga wa moto aligundua kuwa mimi ndiye yule ambaye tuligombana, alicheki pembeni yangu aliona moto mkubwa ukinifuata, alitulia akiwaza aniokoe au aniache nife?.
“Naomba nisaidie, najua nilikukosea sana, unanichukia sana, h utaki kuniona na hunipendi; ila kwa sasa unatakiwa ujue kuwa mimi na wewe Mungu wetu ni mmoja ambaye ametukinga na hii ajali, kama yeye ametunusuru dhidi ya kifo kwanini wewe ushindwe kuniokoa dhidi ya huu moto?” Nilizungumza nikiwa nalia, tena nikiwa namtazama usoni kwa macho ya uchungu.
Yule binti alinitazama kwa muda kisha aliutazama ule moto, taratibu alipiga hatua hadi miguuni kwangu, sijui nae nguvu alizipatia wapi; licha ya chuma kuwa kizito lakini alijitutumua alikiinua juu ili mimi nipate nafasi ya kujiokoa, nami bila kupoteza muda niliondoa miguu yangu haraka kisha nilisimama. Sasa wakati yule binti anakiachia kile chuma, kwa bahati mbaya kilimkwaruza mguuni, binti alidondoka chini, mguu wake ulivuja damu, moto nao ulikaribia kwenye dumu la mafuta, mwanaume sikutaka kuzubaa; nilimfuata binti kisha nilimnyanyua juu, nilikimbia nae kwa spidi zote, tulishtushwa na mlipuko wa moto ambao uliturusha hadi kwenye manyasi, mimi nilikuwa chini alafu yeye alikuwa juu ya kifua changu, pale pale lile wingu jeusi lilipambazuka, mwezi uliandama kisha ulituangaza, sote kwa pamoja tuligeuza macho tulitazama juu kisha tulitazamana, hapo sasa binti alikumbuka kuwa amelala juu ya kifua changu, haraka haraka alijiondoa kisha alikaa pembeni akiugulia kidonda chake cha mguuni, nami niliugulia miguu yangu ambayo ilivuja damu, ngoma droo!
SEHEMU YA 08
Ndani ya msitu wa kutisha tulibaki watu wawili tu, wengine wote walitangulia mbele za haki. Niligeuza macho nilimtazama mrembo nilimuona akihangaika kufuta damu kwenye mguu wake, niliacha kuuguza vidonda vyangu kisha nilichana sehemu ya chini ya shati langu kisha nilienda kumfunga yule binti, ajabu ni kwamba alikimbiza mguu wake; hakutaka nimfunge kidonda chake. Sikujua kwanini ila nilihisi labda bado ananichukia, na ukizingatia hakunitazama usoni wala hakutaka kukaa karibu yangu, kila nilivyomsogelea alirudi kwa nyuma. Tofauti ya kidonda chake na changu ni kwamba yeye chake kilivuja damu nyingi lakini mimi damu zangu zilikauka, niliamua kutumia ubabe; nilikamata mguu wake kwa nguvu kisha niliufunga kile kitambaa cha shati langu, baada ya kumfunga hakukifungua ila alinitazama kwa hasıra kisha aliniambia;
“Nakuchukia sana, usione nimekuokoa ukajua nimekusamehe makosa yako, kwa ufupi ni kwamba naomba kila mmoja aingilie anakokujua kisha akatokee anakokutambua, tukipona wote basi tutamshukuru Mungu, ikitokea mmoja amekufa basi atapambana na kifo chake. Aliongea kama utani vile lakini alimaanisha, tena ili kuonyesha kuwa hatanii; alisimama kisha aliondoka kuelekea kati kati ya msitu.
Nilitulia nikimshangaa, nilijiuliza huyu binti ana akili gani kichwani? Badala ya kukaa na mimi ili tujue jinsi ya kufanya eti anataka kila mmoja apambane kivyake, mbaya zaidi ilikuwa ni usiku, licha ya mwezi kuangaza lakini kulitisha sana. Kiukweli sikutaka kukubali kuacha hasira zake zimuendeshe, sikutaka kumuacha pekeyake, nilisimama kisha nilimfuata, aligeuka aliona namfuata; alikasirika, aliinama chini aliokota jiwe kubwa kisha alinisubiri nimsogelee ili anitwange nife, wewewe! Nani afe? Labda sio mimi, nilisimama nikimtazama kwa mbali. Baada ya kuona nimesimama aligeuka kisha aliendelea na safari yake, mkononi bado alishika lile jiwe, nami taratibu nilipiga hatua nikimfuata, ghafla aligeuka kisha alianza kunikimbiza, tulikimbizana kama wenda wazimu; kwa bahati mbaya nilijikwaa nilidondoka, alinifuata pale pale kisha alinitisha kwa lile jiwe; alifanya kama anataka kunipiga vile;
“We mbwa nimesema usinifuatee! Kama unaogopa kutembea pekeyako basi jiue wewe mwenyewe ili usipate shida. Unanifuata kwani unanijua?”
“Lakini kumbuka kuwa wewe ndiye uliniokoa, sasa nitakufaje wakati nimepona?’
“Oh kwahiyo kumbe kukuokoa nilifanya makosa? sasa nifuate tena uone kama sitokuua”
Baada ya kunitisha aliondoka. Japo sikutaka aondoke ila nilishindwa kumfuata kwa sababu alinichukia sana. Nilimuacha aende, mimi nilisimama kisha nilitulia nikimtazama tu, hatimaye alipotea machoni kwangu. Dakika 5 ziliondoka tangu yule binti apotelee kusikojulikana, nilitulia nikiwaza nitoke vipi? Mara kwa mbali nilisikia muungurumo wa ndege, haraka haraka nilitazama juu niliona ndege ikipita kwa mbali, nilinyosha mikono juu nilipiga kelele nikiwaita waje kunisaidia lakini hata hawakunisikia, walisepa zao. Nilikaa chini nikilia, nilimkumbukia mke wangu na mwanangu, nilizamisha mkono mfukoni nilitoa simu yangu, si unajua tena simu za smart? kile kioo cha juu hata hakikutamanika, simu ilipasuka pasupasu! Nilijaribu kuwasha lakini haikuwaka, kwa kifupi ni kwamba simu yangu ilikufa, nilichoambulia ni laini tu. Nilipiga mangumi chini ya ardhi nikilia, nilimuomba mwenyezi
Mungu atume malaika wake waje kuniokoa, nilimuomba afanye miujiza kijana wake nitoke salama katika huo msitu, sikuwaza tena kwenda marekani bali niliwaza ku o kol e wa tu.
“Eeh Mungu wangu kama umeweza kuniokoa kwenye ajali ya ndege basi hutoshindwa kuniokoa katika huu msitu, naomba niletee msaada wowote ambao utanivusha katika janga hili, amen.” Nilisali kimya kimya, japo mimi sio mtu wa dini sana lakini siku hiyo nilizijua sala zote.
Nikiwa nalia bila sauti mara kwa mbali nilisikia mtu akipiga makelele “Nakufaa, nakufaa, nyokaaaa”. Ilikuwa ni sauti ya yule dada, haraka haraka nilichomoka mbio nikifuata sauti ilikotokea, nilimkuta akikimbizwa na joka kubwa ambalo sikujua kama ni chatu au joka gani, aisee nilipagawa!!!
SEHEMU YA 09
Nililitazama lile joka ambalo lilikimbia kwa kasi, pia nilimtazama yule dada ambaye hata kukimbia hawezi, alikimbia kwa spidi ndogo sana; moyoni niliwaza nikizubaa mdada ataliwa na nyoka!!! Sijui wapi nilipata ujasiri, niliokota mti mkavu kisha niliruka hadi karibu na lile joka, nilishusha mti kwa nguvu ulitua kichwani kwake, hata hivyo joka halikufa, yule binti alisimama pembeni kisha alitazama vita kati yangu na lile joka, kwa mara nyingine nilinyanyua mti juu nikitaka kumaliza kazi, kala sijamaliza nilishtuka nimepigwa na mkia wa lile joka nilienda kujigonga kwenye mti, nilitaka kuzimia ila niliona nikijilegeza nitazimia kweli kisha nitamuacha binti pekeyake, nilipepesa macho kisha nilisimama tena, nilinyosha mti juu alafu niliushusha kwenye kichwa cha joka, nipiga tena na tena, nilitwanga za kichwa tu hadi joka lilikufa. Baada ya kumaliza kazi niligeuza macho nilimtazama binti ambaye alikuwa akinitazama mimi, ghafla nilishangaa damu zikidondoka toka usoni kwangu, nilijipapasa niligundua kuwa nilichanika uso mara baada ya kubamizwa kwenye mti na yule nyoka, kabla sijakaa sawa nilihisi kizunguzungu, nilikosa nguvu, nilidondoka chini kisha nilitulia hapo hapo.
*****
Fahamu zangu zilirudi mara baada ya kuhisi joto kali, nilifumbua macho nilikutana na moto mkubwa ukiwaka pembeni yangu, yule binti sikumuona, haraka haraka niliamka kutokana na woga, nilihisi kichwa changu ni kizito; nilijipapasa usoni nilikuta nimefungwa kitambaa kwenye kile kidonda changu. Nilizungusha macho nikimtafuta binti lakini sikumuona, nilikunja uso nikijilaumu kwanini nilizimia, kuzimia kwangu kumefanya nitorokwe na mtoto wa watu. Nikiwa bado nateseka kwa mawazo mara nilimuona binti akija akiwa amebeba kuni nyingi mkononi. Kitu pekee ambacho niligundua kwa mrembo ni kwamba licha ya uzuri wake lakini alikuwa haogopi kitu. Kutokana na mazingira ya msitu hata mimi mwenyewe na uanaume wangu nisingethubutu kutafuta kuni ndani ya pori hilo, huo ujasiri ningeutoa wapi? hata ungekuwa wewe sidhani kama ungethubutu!. Zile kuni aliziweka chini, alichagua kubwa kubwa aliziweka kwenye moto kisha alikaa chini alinitazama, kwa mara ya kwanza alitabasam.
“Pole” Aliniambia
“Asante, pole na wewe”
“Asante pia. Naomba nisamehe kwa hasıra zangu, mimi ndivyo nilivyo, hata nyumbani wakinikosea kidogo tu basi naweza nisiongee na mtu hata mmoja, tena ikiwezekana naweza nikaondoka nyumbani. Hivi unajua kwanini naenda NewYork?” “Kwanini?”
“Kwa sababu baba yangu anaishi huko, alafu mama yangu nimemuacha Tanzania. Mimi napenda sana kuishi Tanzania kwa sababu ni nyumbani, sasa juzi nilienda kwenye birthday ya rafiki yangu; kwa bahati mbaya nilichelewa kurudi nilirudi usiku, mama yangu alinisema sana alinituhumu kuwa nimetoka kwa wanaume, niliumia sana, nilimkasirikia usiku kucha, ili kutuliza hasira zangu jana niliamua kumkimbia; nimeona bora niende kwa baba”
Nilijikuta nacheka mara baada ya kusimuliwa mkasa wake, hapo sasa niligundua kuwa ni kweli ana hasira za kijinga, na ndio maana alinichukia sana kisa sikumkumbusha kufunga mkanda. Muda huo tulikuwa tunaongea tukiwa tunaota moto. Tulizungumza mambo mengi sana, aliniuliza kwanini naenda marekani nilimuambia naenda kufungua duka la mchele, alifurahi sana pia aliniunga mkono kuhusu kufungua biashara hiyo; aliniambia nimefanya jambo jema kutanua biashara yangu.
“Watu wengi huwa wanajisahau sana kwenye biashara, wao wamezoea kufanya biashara moja sehemu moja. Ni ngumu sana kukuta wajasiriamali wanakumbuka kuzikuza au kuzitanua biashara zao. Wanashindwa kufanya hivyo kwa sababu ya mazoea; wamezoea kutokuza biashara, pia wajasiriamali wengi huwa wananogewa na faida moja; wakipata elfu 10 kwa siku wanasahau kila kitu. Na ikitokea wamekumbuka kukuza biashara basi huwa wanazikuza ndani ya nchi yao tu. Wengi wao wanaogopa kuzipeleka biashara zao nje ya nchi wakidhani biashara za kimataifa haziwahusu. Ni ngumu sana Mtazania kuwaza kufanya biashara Kenya au Mkenya kupeleka biashara yake Tanzania, hawajui kuwa kukuza biashara kuna faida kubwa sana. Kunaongeza bidhaa au huduma, kunakuza mauzo na faida, kunasaidia kupata wateja wapya na masoko mapya, kunafanya mfanyabiashara ajifunze mambo mengi zaidi kutoka kwenye nchi za watu, zipo faida nyingi sana..Hata kama unauza nyanya; inawezekana Tanzania haziuziki lakini ukizipeleka Kenya zitauzika, inawezekana mchele wako utauzika sana marekani kuliko unavyouza Tanzania”
“Wow! Kumbe upo vizuri sana kwenye masuala ya kibiashara”
Baada ya kumuambia hivyo tulicheka kwa pamoja, nilijiona nimebarikiwa kukutana na binti kama huyo. Pia naye nilimuuliza kama anafanya kazi yoyote aliniambia hafanyi kazi ila ni mwanachuo wa mwaka wa pili akichukua masomo ya udaktari. Tukiwa tunaendelea kuongea nilikumbuka kuwa silijui jina lake.
SEHEMU YA 10
“Hivi unaitwa nani?” nilimuuliza “Docralinah”
“Docralinah?” Nilitoa macho nikilishangaa jina
“Yeah, ukipenda niite Docra, nawe unaitwa nani?”
“Derick”
“Kwahiyo hapa msituni amebaki Docra na Derick si ndiyo?” aliniuliza akitabasam
“Yeah, na hatujui tutatoka vipi”
Wote kwa pamoja tulicheka tena kwa furaha, tulionekana kama tupo sehemu salama vile kumbe ni ndani ya msitu mnene. Njaa ilinibamiza sana, pia hata Docra alilalamika njaa, na hatukujua hicho chakula tutakipata wapi muda huo. Tulikubaliana tulale njaa, sio hivyo tu bali kuna muda wote wawili tulihisi kiu ya maji, tulisimama tuliangaza huku na huko labda tungeona kisima lakini hatukuona kisima wala dimbwi la maji, kutokana na giza tulishindwa kutafuta maji, uzuri ni kwamba kati yetu hakukuwa na yeyote ambaye alihisi usingizi hivyo basi tulivumilia. Kadri tulivyoongea ndivyo tulizidi kuzoeana, na alionekana kuwa muongeaji sana, muda wote alitaka awe anaongea yeye tu, mara anisimulie mambo ya darasani, kuna muda aliniambia jinsi alivyoongoza masomo ya Biology, chemistry na physics; nami nilivyo mbumbumbu nilikuwa naitikia tu, kila kitu nilijibu “YES”, aliona raha jinsi nilivyokuwa namkubalia kila kitu, hakujua kuwa mimi na elimu ni vitu viwili tofauti, mwenzie nilianzaga kupata zero kuanzia chekechea hadi kidato cha nne.
Stori stori zilitufikisha hadi asubuhi, kulipambazuka mida ya saa moja, kitu cha kwanza ambacho tulikifanya ni kuondoka kwenye ule msitu. Kabla hatujaondoka tulienda pale ambapo ndege yetu ilidondoka, lengo letu ni kwenda kuhakikisha kama tungeona masalia yoyote lakini hatukupata kitu hata kimoja, tulisikitika kuona miili ya wenzetu ikiwa imegeuka majivu. Tulianza safari ya kulikwepa pori, hatukujua tunaelekea wapi ila tulisonga mbele tu. Tulitembea umbali mrefu, tulifika sehemu ambapo hakukuwa na mti wala nyasi, palikuwa na uwazi mkubwa kama jangwa vile. Tulisimama kisha tulitazama kwa makini tuliwaona wanyama wengi wakila majani madogo madogo, kwa haraka haraka palionekana kama mbuga ya wanyama, kwa mbali tuliwaona swala wakinywa maji kwenye mto flani hivi, nasi tulijikuta tumeyatamani maji hayo, tulikubaliana tukanywe.
Tulifika kwenye ule mto ambao ulitulia hadi uliogopesha, mto wenyewe haukuwa na maji mengi, tulitafuta sehemu ambayo maji yalikuwa yanatembea, hatukutaka kujua kama ni salama au sio salama, Docra alianza; aliinama alikunywa maji ya kutosha kisha mengine alijimwagia kichwani, alinawa uso, alitamani kama aogelee vile. Baada ya Docra ilifuata zamu yangu, niliinama nilikunywa maji, nilinawa uso kisha nilisimama. Sasa wakati nataka kuondoka mara ghafla kiliibuka kitu kizito ambacho moja kwa moja kilikamata mguu wangu.
“Docra nisaidieeeee…Mambaaa ananitafunaaa” Nilipiga kelele za maumivu nikiwa najaribu kuuvuta mguu wangu ambao ulibanwa kwa meno ya mamba mkubwa. Yule mamba alinizidi nguvu, taratibu aliniburuza kuelekea kwenye maji, nilitazama pembeni kulikuwa na mti flani ambao ulijiotea, nilikamata mti ili nisiburuzwe lakini ghafla mti uling’oka. Mguu wangu ulianza kumwaga damu, mamba nae alizidi kunipeleka kwenye maji, ajabu ni kwamba niligeuka nyuma sikumuona Docra, hapo sasa niligundua kuwa Docra ana roho mbaya! Kaniacha mwenzie niliwe na mamba, dah! Duniani kuna watu makatili.
Nikiwa najua nimeachwa pekeyangu ili nife ghafla nilisikia “Paaaaa” nilipiga kelele kwa nguvu nikisema “Uuuuuuh nakufaaaaaaa” damu ziliruka toka mguuni kwangu hadi kwenye maji, nilihisi mguu wangu unataka kukatika, nilifumba macho kisha niliyafumbua alafu nilimtazama yule mamba lakini sikumuona. Nilitazama pembeni yangu nilimuona Docra kasimama akiwa amekunja uso kwa hasira kali, mkononi alishika bonge la rungu, sijui alilipata wapi. Haraka haraka alinivuta hadi nje ya mto, aliutazama mguu wangu alikuta mashimo mashimo ya meno ya mamba. Kabla hajanipa huduma yoyote kwanza aliondoka alianza kuzunguka huku na huko, alirudi akiwa amebeba kopo la maji. Ebu fikiria mto una mamba, na mamba huyo tayari amenijeruhi, kwa kawaida ni lazima mtu aogope kuusogelea mto huo lakini Docra hakuogopa; alielekea kwenye sehemu ile ile ambayo nilikamatwa na mamba, alichota maji kisha alirudi nilipo. Yale maji kabla hajayatumia nilimuona akizunguka tena huku na huko, alifika kwenye mti flani hivi ambao sikuutambua, alichimba chini alichukua mizizi na majani ya mti huo kisha aliyachanganya kwenye kopo la maji, alitikisa kopo kisha alikuja kwangu alimwaga yale maji katika mguu wangu!
“Mamaaaa inaumaaaa” Nilipiga kelele nikiwa najinyonga kama kambale lakini mwenzangu hakujali wala hakunionea huruma, aliendelea kuosha kidonda changu kwa kutumia yale maji.
Kichwani alikuwa amevaa mtandio flani hivi, aliufungua kisha aliufunga kwa nguvu katika mguu wangu wenye jeraha. Hakuishia hapo, kwenye lile kopo yalibaki maji machache, alinipa ninywe. Mwanzoni nilipata wasiwasi, niliogopa nisije nikanywa nikafa, Docra mwenyewe hata haeleweki, kuna muda alionyesha kunijali lakini kuna muda akiamua kunikasilikia anakasilika kweli. Niliogopa kunywa nikihisi maji hayo ni sumu ananipa ili nife.
INAENDELEA