KWA MAPENZI HAYA LAZIMA TU NIMSALITI
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
SEHEMU YA 41
Muda huo nilikuwa nipo kazini kwangu, kutokana na kuvurugwa nilisimama kisha nilianza kujizungusha huku na huko; vijana wangu wa kazi walibaki wananikodolea macho tu, wengine walinionea huruma kwa sababu waliniona nimevurugwa. Licha ya kuchanwa makavu lakini nilihisi Docra ananitania tu, nilimpigia nikitaka anikatae kwa maneno ya mdomo wake; kwa bahati mbaya nilikuta namba yake haipatikani, sikujua kama ameniblock au amenizimia simu.
Kwa jinsi ambavyo niliwehuka hata kichaa alikuwa ana afadhali. Licha ya kuoa lakini niliupenda mchepuko wangu kuliko hata mke wangu, usiniulize kwanini; kama ni pombe we kunywa nitanunua, mimi kwa Docra nilipatikana. Sikutaka kupoteza muda, kitu pekee ambacho nilikiwaza kwenye kichwa changu ni kuelekea dar kwenda kumuomba msamaha Docra wangu. Haraka haraka nilitimua mbio nikilifuata gari langu ambalo nilipaki upande wa pili wa barabara, kutokana na kuchanganyikiwa sikutaka hata kufuatilia sheria za usalama barabarani; sasa nikiwa nakatiza kat i kat i ya barabara ghafla nilisikia “tusuuu” taili la pikipiki liligonga mguu wangu, nilipepesuka nilienda kudondokea kwenye mawe ya mtaro uliopo pembeni ya barabara; kichwa changu kiligonga kwenye jiwe lililopo kwenye mtaro huo, uso wangu ulichanika vibaya, mguu wangu ulitetereka, mkono wangu nao ulipinda; nilihisi kizunguzungu nilipoteza fahamu.
****
Nilishtuka nilijikuta nipo hospitali kitandani, na sikujua ilikuwa ni siku ya ngapi nimelazwa; m bele yangu sikumtambua mke wangu wala d aktarı, licha ya kuzinduka lakini uhai wangu ulikuwa wa kuhesabika, macho yangu yalitazama yakiwa yanafifia, mguu wangu wa kulia ulifungwa bandeji, mkono wangu wa kushoto ulifungwa bandeji, shingo yangu ilifungwa bandeji, uso wangu ulivirigwa bandeji za kila aina. Hali ya mwili wangu hata sikuielewa; mara joto mara baridi, kichwa changu kilikuwa kama kinapepea na upepo, sikujihesabia kama ni binadamu hai; tayari nilijiweka katika makundi ya mizimu. Kwa mbali nilisikia kilio cha mke wangu ambaye alikuwa ananiita lakini sikuitika. Pia nilisikia mazungumzo ya daktari na mke wangu ambayo yalisikika kama ifuatavyo;
“Pole sana, huna haja ya kulia tena, kama kulia umelia sana. Kwa sasa kila kitu tumefanya lakini hali ya mgonjwa inazidi kuwa m baya tu, na laiti kama isingekuwa Mungu ilibidi tuwe tumemkosa”
“Lakini kwani anaumwa nini cha zaidi? Kama majeraha si yametibiwa?” Mke wangu aliuliza
“Ni kweli, majeraha yake yote yanaendelea vizuri; kama tiba tu tumempa tiba nzuri sana lakini tunashangaa haponi, ndani ya mwili wake hakuna ugonjwa mwingine wowote lakini hali yake inazidi kuwa m baya tu…Na ndio maana nakusisitiza uongeze maombi, au kama inawezekana mpelekeni muhimbili akapate matibabu zaidi”
Mke wangu hakutaka kuchelewa, gari ya hospitali iliandaliwa kisha nilikimbizwa nilipelekwa muhimbili. Wakati hayo yote yakiendelea Docra alikuwa hajui chochote. Hatim aye nilifikishwa hospitali ya muhimbili, nililazwa ndani ya chumba cha watu mahututi, kwakuwa hali yangu ilikuwa mbaya madaktari wengi walichacharika wakipigania uhai wangu; hata hivyo ilikuwa ni kazi bure, nikiwa muhimbili ilipita siku ya kwanza, siku ya pili, siku ya tatu hadi tano madaktari walishindwa kazi walimuambia mke wangu nipelekwe india.
“India? Kwani mmekuta ana ugonjwa gani?” Mke wangu aliwauliza madaktari
“Sisi hata hatujui. Mwanzo tulijua labda anasumbuliwa na majeraha ya ajali, lakini majeraha hayana shida, tena mguu wake unaendelea vizuri, mkono nao unaendelea vizuri, usoni kama unavyomuona anazidi kupona, ukiondoa viungo vya nje hana majeraha wala homa nyingine; hatujui anaumwa nini kwa sababu ndani ya mwili wake hajaumia kiungo hata kimoja” Dokta aliongea “Mmepima magonjwa yote haumwi?” “Hana magonjwa ya kuambukizwa wala yasiyoambukizwa, labda kama majeraha ndiyo yanataka kumuuwa; lakini ukiondoa majeraha ya nje vipimo vinaonyesha haumwi chochote.”
“Aaah jamani mume wangu anarogwa hivi hivi…wanataka kumuuwa mume wangu…mi siwezi kukubali…dokta nakuomba niondoke na huyu mtu nimpeleke kwa wataalamu wa asili; inaonekana labda amerogwa, haiwezekani kıla siku mara hili mara lile.”
Japo ilikuwa ngumu madaktari kuamini mambo ya ushirikina lakini mke wangu alikomaa hadi aliruhusiwa aodoke na mimi. Alinipeleka kwa waganga wa kienyeji waliopo dar, alinipeleka kwa waganga wawili lakini waganga wote walisema hakuna anayeniroga. Siku zote mke wangu huwa hawaamini watu wa dar, anawaona kama wababaishaji wapenda pesa; kitendo cha waganga hao kusema kuwa sijarogwa mke wangu aliwaona kama wanadanganya. Alinisafirisha alinirudisha M bey a kwa waganga nguli ambao wametapakaa kila kona. Alinipeleka kyela kijijini, porini kwa babu mmoja hivi ambaye alijulikana kwa jina la mzee Kikwakwa. Pia katika safari hiyo mke wangu hakuwa pekeyake bali aliongozana na mama yangu mzazi pamoja na mdogo wangu wa kike.
Baada ya kufika kwa Mzee Kikwakwa nililazwa juu ya m keka maalumu ambao ulizungushwa hirizi na matunguri kama yote. Mganga aliwasha ubani mashtaka kisha alianza kupuliza unga wa kiganga kwenye kıla kona ya chumba. Baada ya kutega mizimu yake alikaa chini kisha aliwatazama wauguzi wangu aliwauliza nasumbuliwa na nini?
“Yaani babu sisi hata tunashindwa kuelezea, mume wangu kama kuteseka tu anateseka jamani; hawa waliomroga wamemroga vibaya, leo anajikwaa, kesho anaumwa nywele, kesho kutwa mkono unavunjika, mara anagonga nyumba za watu; laiti kama Mungu hasingekuwa na sisi ilibidi tuwe tumemzika, mwezi sasa unakatika tunamuhangaikia lakini haponi”
“Sawa mama lakini nataka kujua anasumbuliwa na nini? Anaumwa nini?”
“Ndo hatujui sasa. Tumepita hospitali wanasema haumwi kitu, tumezunguka kwa waganga wa dar wanasema mgonjwa haumwi kitu wala hajarogwa na mtu. Na ndio maana tumekuja huku kwako, tunataka kujua kama kweli haumwi kitu. Ebu muone mdomoni anavyovuja m at e, hiyo shingo yake hata kugeuka haigeuki, maisha yake ni kulala kitandani tu, jamani mganga tusaidie” “Sawa msijali, subirini kila kitu kitakaa sawa”
Mzee Kikwakwa alianza mbwembwe zake, kwanza alipiga mruzi mrefu; fumba na kufumbua zilisikika ngoma na toka nje ya kibanda cha uganga. Wale wagonga ngoma waliingia ndani ya kibanda kisha walinizunguka mimi, mganga alivua nguo alibakiwa na chupi tu; walianza kukata mauno mpaka chini, mpaka chini, mweeh! afu hadi leo sijuagi kwanini waganga wanajua kuyarudi magoma, kwenye suala la kucheza tu? yule mganga ni konyo!! Ngoma hizo ziliambatana na kuaguliwa; mganga alimwaga maji ya kuzimu juu ya mwili wangu, alinimwagia unga wa dawa juu ya kichwa changu, mganga alisema anahitajika kuku mmoja na mbuzi mmoja; kwakuwa tulikuwa kijijini vitu hivyo vilinunuliwa kulekule, mke wangu ndiye alinunua. Kuku na mbuzi walichinjwa kwaajili yangu lakini mimi mwenyewe hata sikuonja; wao walijisosomola kwa minofu lakini mimi niliambulia damu mbichi kutoka kwa mbuzi na kuku, damu hiyo nilinyweshwa mdomoni; ghafla nilianza kucheua, nilicheua kisha nilitapika madudu ya ajabu ajabu! Kila mtu alishangaa.
“Ah ah ah…mimi ndiye nguliii…mimi ndiye mzee kikwakwa! Ndugu yenu amerogwa..amerogwa hasifanikiwe, amerogwa awe anapata majanga kıla siku, yaani laiti kama mngechelewa kumleta basi mngemkosa; wanataka kumtoa kafara” Mganga aliongea akiwa anacheka kwa nguvu; alifanya watu wakodoe macho wakishangaa, mke wangu alishtuka kiasi cha kutamani kulia, mama yangu mzazi nusura azimie kwa plesha. Balaa ni zito!!!
SEHEMU YA 42
Kwa asilimia 100% kila mtu alimuamini mganga kuwa nimerogwa, tena kwa namna ambavyo nilitapika vitu vyeusi hakuna aliyebisha kuwa sijarogwa; kuanzia mke wangu, mama yangu, mdogo wangu na wapiga ngoma wote walisikitika kusikia kwamba nilitakiwa kutolewa kafara. Hali yangu bado ilikuwa mbaya; sikuweza kuongea neno lolote, masikio yangu licha ya kusikia lakini yalisikia kwa mbali, macho yangu licha ya kuona ila kuna muda yaliona giza. Baada ya kufahamika kwamba nimerogwa watu walitaka kujua nimerogwa na nani?
“Mi nilijua tu mume wangu karogwa, wanataka kumtoa kafara sijui amewakosea nini; mganga naomba niambie amerogwa na nani?” “Masharti ya mizimu yananiambia siruhusiwi kumtaja mbaya wake, siruhusiwi kumtaja anayeroga; ila mizimu inaniambia kuwa anarogwa na ndugu wa ukoo wake, wanamuonea wivu kwa sababu amefanikiwa kibiashara”
“Jamani walimwengu hawa, mtu kwenda marekani tu wanaanza kumuandama; mganga nisaidie tafadhari”
“Matibabu yake ili apone zinahitajika million 1 ambazo sitozitumia mimi bali zitatumika na mizimu ambayo ndiyo inanipa dawa. Mimi mwenyewe mtanilipa laki moja tu”
“Kwahiyo tukitoa hizo pesa kila kitu kitakaa sawa?’
“Nitawapa dawa ambazo hakuna mchawi wa kuzigusa. Kwanza atapona, pili atalindwa kwa uwezo wa dawa hizo; mizimu itahakikisha inapigana na wachawi na wabaya wake wote, na yeyote atakaye mgusa atakufa yeye”
“Asante sana mganga, nakushukuru sana”
“Mimi ndiye Kikwakwaaaaa”
Watu walipiga ngoma, walicheza madogori, mke wangu alifungua pochi alimwaga pesa kisha alipewa dawa za matibabu yangu. Alipewa dawa za maji na unga, zingine za kuwekwa kwenye chai na uji. Mganga hakuishia hapo balı alinichanja viungo vyangu vyote kasoro cha kat i kat i tu. Pia alimsisitiza mke wangu asisahau kunipa dawa kulingana na muda, nilitakiwa kunywa dawa asubuhi, mchana na usiku.
“Sasa mnaweza kwenda. Hizo dawa atakunywa kwa wiki moja kisha atanyanyuka, lazıma ataongea na lazıma hali yake itakuwa kama mwanzo. Nendeni nyumbani, kwa sasa mgonjwa yupo huru. Nawapa namba yangu ya simu mtanipa matokeo, mimi ndiye Kikwakwaa”
“Asante babu, akipona huyu nitakuja tena ku kus hu kuru” Mke wangu alipata matumaini kuwa lazima nitapona. Walinichukua walinipeleka kwenye gari, nao walizama ndani kisha walinirudisha nyumbani Kyela.
****
Baada ya kufika nyumbani mke wangu hakubanduka pembeni yangu, licha ya kwamba sikuwa na uwezo wa kutafuna kitu au kumeza lakini alihakikisha nakunywa dawa, nakunywa uji, pia hadi chakula nilikula kwa kulazimishwa na mke wangu. Mama yangu mzazi nae hakwenda kwao, alibaki nyumbani kwangu akisaidiana na mke wangu. Ndugu mbalimbali walikuja kuniona, walisimuliwa mkasa wangu wa kurogwa kutaka kutolewa kafara; kila mmoja alilisikitika, walinionea huruma.
Siku ya kwanza ilipita nilipewa madawa ya mganga, siku ya pili ilikatika, hatimaye wiki moja iliondoka lakini ndo kwanza hali yangu ilizidi kuwa mbaya. Nilikuwa kama mtoto, ilifikia hatua kila nikilishwa chakula nilitapika, kila nikipewa dawa nilitapika, sikutaka chai wala uji, mke wangu alijaribu kumpigia mganga lakini namba ya mganga haikupatikana. Aliwaita waganga wengine ambao walikuja kunitibu pale pale nyumbani kwangu lakini waganga wote walisema sikuwa na ugonjwa wowote. Mke wangu aliwaita masheikh ambao walikuja kunisomea dua maalumu lakini sikupata ahueni wala afadhali, wachungaji na manabii wa uongo waliitwa nyumbani kwangu; nilimwagia maji ya baraka lakini kijana wa watu sikufufuka. Kwa mbali niliwaona malaika watoa uhai wakinizunguka, Israeli mtoa roho alikuja kusimama mbele yangu akitaka kunichukua, kwa moyo mmoja nilikubali niongozane na Israeli; ila kabla ya kufa nilipaza sauti kuu nilimuita mke wangu na ndugu zangu ambao walikaa pembeni yangu, nilitoa wosia kama ifuatavyo;
“Mke wangu kipenzi iliandikwa kwamba kıla nafsi itaonja mahuti; wengi walipita tuliwazika na sasa ni zamu yangu, asante kwa kunipenda, asante kwa mapenzi yako makubwa. Mama yangu mzazi asante sana, ndugu zangu wengine asanteni pia, ishini kwa amanı, pendaneni, tunzeni mali nilizoacha, wala msiingie katika mapambano ya kugombania mali zangu; mke wangu utasimamia kila kitu, hakikisha mwanangu anasoma sana, mpende na mlee mama yangu mzazi kama vile ambavyo nilifanya mimi, na nikifa msihangaike kutafuta mchawi ni nani; mimi sijarogwa, mimi nakufa tu kiroho safi. Iliandikwa kuwa nitakufa, mimi mwenyewe nilitihibitisha kifo changu; hatimaye leo yametimiaü! nadhani hii ndiyo sauti yangu ya mwisho kusikika kwenu; naomba niwatakie maisha mema”
“Mume wangu pliiiz usifeee, bado nakupenda jamani…usiniache mjane jamaniii” Mke wangu alinikumbatia kwa nguvu akiwa analia. Licha ya kilio kikubwa cha mke wangu, licha ya vilio vingi kutoka kwa ndugu walionizunguka lakini mimi tayari nilitoa wosia wa mwisho; hapo hapo nilifumba macho kisha nilitulia kimya, giza nene lilitapakaa machoni kwangu, roho yangu na mwili wangu vilikuwa katika wingu zito lenye giza nene; kilichofuata hapo sikukitambua.
SEHEMU YA 43
Kuna dereva wangu mmoja alikuwa anafahamu mahusiano yangu na Docra. Ni yule dereva aliyesafirisha mzigo wa mchele ambao nilimpatia Docra kama zawadi. Dereva huyo alikuwa anajua kila kitu kuhusu mimi kuwa na mchepuko jijini dar, hata hivyo hakuthubutu kumwambia mke wangu kwa sababu jamaa hanaga masuala ya kimbea, pia ni mtu safi sana ambaye tulifanya mambo mengi, nilimsaidia kwa vitu vingi, hata mshahara nilikuwa namlipa tofauti na wengine; yeye nilimlipa zaidi. Dereva huyo ndiye aliyemfuata Docra jijini dar alienda kumwambia kuhusu hali yangu; “Dada mambo, mimi ni Dereva wa Derick”
“Kaka samahani, naomba usiniambie chochote kuhusu Derick, ananiita mimi mchawi? Ananitelekeza kisa nina mimba yake? Asante sana”
“Subiri kwanza nisikilize, hivi unajua Derick yupo kwenye hali gani muda huu? na sidhani kama hajafa, hii yote kwa sababu yako. lie siku umemzimia simu alivurugwa akitaka kuja huku dar akuombe msamaha, sasa akiwa anachepuka barabarani kwa bahati mbaya aligongwa na pikipiki alidondokea kwenye jiwe mtaroni. Usoni alichanika, mguu na mkono vilitetereka; alizimia hapo hapo” “Nini? Unasemaje? Derick wangu au Derick gani? kwanini hamkuniambia?” Docra alianza kulia
“Ni mwezi sasa umepita ametibiwa majeraha lakini bado anaumwa. Mguu, mkono na uso vimepona lakini hawezi kuamka kitandani, kula hali wala kuona haoni, kuongea ndo hawezi kabisa. Alipelekwa hospitali kama zote lakini madokta wanasema mgonjwa haumwi kitu, aliletwa hapa dar muhimbili lakini madokta walisema mgonjwa haumwi kitu. Kapelekwa kwa waganga wa kienyeji ambao baadhi walisema mgonjwa hajarogwa lakini mwingine alisema mgonjwa karogwa; dawa za mganga zilitolewa, Derick kalishwa ubende wa mbuzi na kuku lakini hali yake inazidi kuwa mbaya. Hivi ninavyokuambia nimemuacha anauguzwa nyumbani kwake, na sijui kama bado mzima, nilimuacha anakaribia kufa”
Weuwee!! Docra alipagawa, haraka haraka alifunga duka kisha yeye na dereva walielekea uwanja wa ndege; walibahatika kupata ndege ambayo iliwasafirisha hadi Songwe jijini Mbeya. Hawakutaka kuchukua basi/daladala waliona watachelewa, docra alikodi gari maalumu ambayo iliwakimbiza iliwaleta nyumbani kwangu Kyela, walizama ndani ya nyumba yangu walikuta watu wakilia, wengine walisema nimekufa na wengine walikosa maneno.
“Mume wangu umeniacha na nani mimi…Jamani unakufaje sasa jamani wewe mume wangu…mi najua hujafa…amka basi….” Mke wangu alilia
“Jamani kwani kuna nini? Mbona mi sielewi” Docra aliuliza “Docra mume wangu ametupatia wosia eti anasema amekufaaaa…mume wangu kadanjaaa jamani ameniachaaaa…Mungu wangu tenda miujizaa…”
Vilio vilizidi kutawala, Docra nae alitamani kulia ila alivumilia; taratibu alinifuata hadi kitandani alikuta nimetulia kimya nikiwa nimefumba macho, alinitazama kwa makini alinionea huruma kuona mamna ambavyo hali yangu ilikuwa mbaya. Licha ya kwamba watu waliamini nimekufa lakini Docra aliwaambia kuwa sijafa. Hapo sasa kila mmoja aliacha kulia kisha alimtazama Docra, mke wangu nae alisimama pembeni yangu akitaka kushuhudia kitakachotokea. Mama yangu mzazi hakuwa mbali, alinikazia macho pale kitandani; wote walisubiri kuona kitu ambacho Docra atakifanya. Docra alinyosha mkono alinikamata nywele zangu kisha aliongea maneno yafuatayo;
“Derick najua hujafa, wewe ungekuwa wa kufa nadhani ungekufa kwenye ajali ya ndege. Haya ni mapito tu ambayo Mungu anakupitisha, inawezekana anakukumbusha kitu ambacho umekisahau, labda ulifanya dhambi kubwa ambayo inakupa adhabu hii; naomba mwenyezi Mungu akuinue kisha akupe nafasi nyingine ya kukiri dhambi zako! Amen” Docra alimaliza maombi.
Ogopa sana kitu kinaitwa “Power of Love”, yaani ile Docra anamaliza kuniombea tu; marehemu nilikohoa “koh koh koh” kisha nlifufuka pale pale. Weuwe! Unazijua kelele? Unazijua shangwe? Unajua nderemo? Unajua vifijo? Kyela nzima ilisimama, Kyela ilichekelea, Mke wangu alitamani apae juu mbinguni akasifu utukufu wa Mungu, ndugu zangu waliimba “halleluyaaa”, mama yangu mzazi alilala chini akigalagala kwa furaha! Nami nilifumbua macho nilikutana na tabasam zuri kutoka kwa mtoto mzuri; mimi kama mzimu nilijikuta nimetabasam bila kupenda. Sikujua zile nguvu nilizitoa wapi, niliamka kisha nilibaki nimekodoa macho kama msukule husio na mama wala baba;
“Kwani kuna nini?” Niliwauliza watazamaji ambao walinitazama, mke wangu baada ya kuona nimeamka na nimeanza kuongea alizidi kufurahi. Pale pale aliniletea chakula alijaribu kunilisha nilikula, maji nilikunwa, vitumbua nilimeza, pipi nilimung’unya; sikuacha kitu mie, nilifukia kila kilichokuwa mbele yangu, nilikula kujigalagaza.
“Jamani mwanangu Derick hajafa, huyu Mungu sijui tumlipe nini; wabaya waliotaka kumuuwa watakufa wao lakini sio mwanangu mimi” Mama yangu mzazi nae alianza kujisifia, alidhani kuwa wachawi wameshidwa kuniuwa kumbe mwenzie hata sikurogwa bali nilijiroga mwenyewe.
Baada ya kuniamsha Docra hakuongea tena na mimi, alitoka kitandani alimpisha mke wangu ambaye ndiye alikuwa muuguzi wangu mkuu. Siku hiyo ilipita licha ya kwamba nilishinda kitandani lakini hali yangu ilikuwa nzuri. Siku ya pili nilichangamka katika kuongea, niliweza kuongea na watu wengi ambao walinitembelea, yale macho yangu ambayo yalikuwa yanaona giza hatimaye yaliona mwanga; niliwaona watu wote kwa ukamilifu mkubwa, masikio yangu yalizibuka kisha yalisikia kwa uwezo wa hali ya juu, kubwa zaidi niliweza kusimama na kutembea.
Ilifika siku ya tatu, hiyo ndiyo siku ambayo nilipelekwa hospitali kisha nilifunguliwa bandeji zote za miguuni, mikononi na usoni. Nilianza kutembea kwa kuchechemea, pia mkono wangu ulianza kukunjuka taratibu. Afya yangu ilizidi kuimarika hasa kila nilivyokuwa karibu na Docra, licha ya kwamba hakuongea na mimi lakini yeye na mke wangu walishirikiana kuniuguza; wao ndio walinipeleka hospitali kila ilivyohitajika na walihakikisha nakunywa dawa ambazo nilipewa hospitali, Docra alimwambia mke wangu hasinipe tena madawa ya waganga wa kienyeji ambayo hayakunitibu chochote.
Docra alikaa nyumbani kwangu kwa wiki moja, akiwa pale kwangu kama kawaida yake hakuonyesha ishara zozote kwamba ana mahusiano na mimi. Muda wote alipenda kukaa karibu na mke wangu ili asihisiwe vibaya. Hatim aye ndugu zangu ambao walikuja kuniona walianza kuondoka mara baada ya kuona naendelea vizuri. Nyumbani kwangu tulibaki mimi, mke wangu na Docra. Hata hivyo baada ya kuonanimepona; Docra hakutaka kubaki, japo sikupenda aondoke lakini alituaga akitaka kuondoka; “Jamani mimi nimeshukuru mgonjwa amepona, kwa sasa naomba niwaage narudi nyumbani Dar”
“Sijui nikushukuru vipi, yani wewe sijui hata nikuelezeje. Umekuwa dokta mkuu wa matatizo yetu, ulinihangaikia wakati naumwa, ulimlea mwanangu, na leo umekuja kupambania hali ya mume wangu. Asante sana. Jambo la pili naomba nisamehe kwa sababu ilifikia hatua nilikuhisi vibaya, nilihisi labda wewe ndiye chanzo cha mume wangu kuumwa. Nilijua labda wewe ndiye unamroga, lakini baada ya kwenda kwa mganga tuliambiwa kuwa mume wangu anarogwa na ndugu wa ukoo wake, nisamehe sana mdogo wangu”
“Asante hata usijali, mi nimekusamehe”
“Docra mimi pia nisamehe, ilifikia hatua tuligombana kwa sababu nilikuita mchawi; ilikuwa ni hasira tu ila kiukweli sikudhamiria” Niliongea nikiwa namtazama usoni kwa aibu.
“Sawa. Basi mimi niwaache” Docra aliongea kwa sauti ndogo ya upole; alionekana kama hana ra ha, sikujua ni kwanini.
“Lakini kabla hujaondoka kuna kitu nataka nikuulize” Mke wangu alimwambia Docra ambaye alianza kusimama ili aondoke.
“Kitu gani?”
“Kwanini kila ukiondoka mume wangu anaumwa, anapata ajali, majanga kila muda, alafu ukiwa karibu na mume wangu hata kama anaumwa ni lazima apone; kwanini?”
“Mi sijui, lakini kwakuwa mumeo yupo hapa itakuwa vema kama yeye mwenyewe atajibu swali hilo”
“Eti baba Monica ebu niambie ni kwanini?’ Mke wangu alinigongelea msumari akiwa ananitazama usoni, mwanaume niligwaya! Nilijua kumekucha.
SEHEMU YA 44
Zilipita sekunde nyingi za ukimya; mimi nilikaa kimya ila wenzangu walisubiri. Docra alijua kabisa kuwa mimi sijarogwa ila kuna kitu nakificha na ndio maana alinitupia mpira ili niongee ukweli kuhusu kitu hicho. Sikutaka kuongea kwa sababu namfahamu mke wangu, nikimwambia ukweli anaweza hata akajiua, kwa jinsi anavyonipenda alafu nimuambie kitu cha tofauti mbona badamu batamwagika!!!
“Baba Monica mbona huongei? Kwa n i una siri gani? mbona kama kuna kitu unanificha!!!”
“Mke wangu naomba nisamehe”
“Nikusamehe kwa koşa gani s as a?”
“Nilivunja kiapo chetu”
“Kiapo gani tena mbona unanichanganya? Kiapo gani?” “Nadhani haya matatizo yote yanayonikuta ni kwa sababu nilivunja kiapo chetu cha damu, nilivunja ahadi ambayo tuliiweka, lakini sikuwa na jinsi kwa sababu nilikutetea sana, nilikujali, nilipambana nisivunje kiapo lakini ilishindikana. Wewe unajua matatizo yote yaliyonitokea kuanzia siku ya kwanza naenda marekani, kuibiwa pesa na biashara, nilipelekwa mahakamani nihukumiwe; sidhani kama ungeniona tena, mbaya zaidi mimi na wewe tulipata matatizo tulipelekwa hospitali, lakini nyuma ya haya yote kuna mwanamke alipambania maisha yetu, hata kupona kwangu kwa sasa kumechangiwa na mwanamke huyo; na ndiyo maana akiwa mbali nateseka lakini akiwa karibu nakuwa salama, nilikuwa sına chochote cha kumlipa zaidi ya mapenzi” “Unataka kusema umenisaliti kwa Docra?”
“Ndiyo. Isingekuwa Docra sidhani kama ungeniona tena. Pia sio kukusaliti tu bali ana ujauzito wangu na nina mpango wa kumuoa.” Kabla hatujakaa sawa mke wangu alidondoka chini alizimia hapo hapo, yaani ni majanga after majanga; likitoka hili linaingia lile, kila siku ilikuwa ni mwendo wa kupelekana hospitali tu. Mimi na Docra tulimchukua mke wangu tulimpeleka hospitali ambako alikaa kwa siku tatu. Hata alivyopata nafuu hakutaka kumtazama yeyote kati yetu, hakuongea na mtu, muda wote alikuwa analia. Docra baada ya kuona hivyo hakutaka kuwa kikwazo kwa mke wangu, aliniaga akitaka kuondoka lakini nilimwambia hasiondoke hadi tuweke mambo sawa.
Mke wangu aliruhusiwa kutoka hospitali, tulimchukua tulimrudisha nyumbani; bado hakutaka kuongea na mtu, na mara baada ya kufika nyumbani tu alijifungia chumbani kisha alianza kulia kwa usaliti ambao nilimfanyia, alilia kwa uchungu akinipa lawama kama zote, ilifikia hatua hakuniita mume wangu wala baba Monica bali aliniita jina langu Derick. Ugomvi ulikuwa mkubwa, Docra nae alibaki aalia tu; alijiona mkosaji mkubwa, alimfuata mke wangu kisha alimuomba msamaha kama ifuatavyo; “Mama Monica, dada yangu”
“Nani dada yako? tena we malaya naomba usiongee kitu mbwa shetani wewe, kumbe we ndo umemuharibu mume wangu, wanaume wote hawa waliojaa mtaani unapendaje mwanaume wa mwenzio? Alafu unajiona mwanamke mwema kwa wema upi ulionao? Mtu huzijui hata amri za Mungu alafu unajiona mstaarabu. Au hujui kuwa Mungu amekataza kumtamani mwanaume wa mwanamke mwenzio? Ondoka nyumbani kwangu haraka, ondoka kabla sijakuuwa” “Sawa naondoka lakini naomba nisamehe, kiukweli Derick hana makosa, alijitahidi kutetea ndoa yako kwa namna alivyoweza lakini mimi shetani sikuchoka kumshawishi kwa kumpenda. Wala sikumpendea pesa zake au biashara zake, na sijawahi kumfanyia mitego ya aina yoyote, lakini mapenzi yangu kwake yalikuja kama asili tu. Tulidondoka kwenye ndege, tulipona sisi wawili, tulisaidiana kwenye keşi yake kule marekani, tulisaidiana kutengeneza biashara zake na mwisho hisia za mapenzi zilikuja kati yetu. Sitaki kumsemea Derick; najisemea mimi mwenyewe kuwa nimekukosea sana, naomba nisamehe tu kwa sababu hakuna namna. Na adhabu pekee ambayo nahihitaji kutoka kwako ni kutenganishwa na mume wako ambaye nampenda sana, hilo halina ubishi, silazimishi penzi ila limekuja tu; mimi mwenyewe sijui hata kwanini nampenda mwanaume wa mtu, m baya zaidi sisi ni wakristu; bora hata tungekuwa waislamu mana kwao hilo ni jambo la kawaida. Nisamehe kwa sababu nishakukosea, usaliti umeshafanyika, hata ukilia kwa kiasi gani hutobadili chochote. Nisamehe, japo nampenda mumeo lakini nitakaa mbali na familia yako ili nisikuumize.” Docra aliongea akiwa analia
“Naomba utoke…toka nyumbani kwanguu”
“Mke wangu kabla hujamfukuza ni vema tukawekana sawa. Tambua kuwa ukimfukuza unafukuza baraka za Mwenyezi Mungu, unafukuza malaika wa Mungu, unamfukuza mwanamke niliyeletewa na mwenyezi Mungu”
“Una maana gani Derick? Ina maana unataka kumuoa huyu mwanamke? Tangu lini mkristu akaoa wanawake wawili? Mbona nyie wanaume mna tamaa ya ngono kiasi hicho? Ni kipi ambacho hukipati kwangu Derick?”
“Kila kitu nakipata kwako, yaani hakuna ambacho nakikosa kwako mke wangu. Pia mimi sijawahi kumtamani Docra, nampenda kwa sababu nimepewa na Mungu. Kwa Docra sijafuata tamaa wala ngono, ni mapenzi tu. Tayari ana mimba yangu, ananipenda sana, nami nampenda, ametusaidia vitu vingi, naomba kubali awe mke mwenzio. Kama kweli unanipenda naomba usikatae jambo hili la heri kwa sababu hata ukimkataa mimi nitapata shida, huwezi kumtenganisha Docra na Mimi; sisi tuliunganishwa na Mungu”
“Washenzi nyinyi, Mungu gani anaweza akawaunganisha mashetani? Ina maana Mungu anapenda usaliti si ndiyo? Kweli kuna Mungu anayeweza kukupa mke wa pili wakati kuna wanaume hawana mwanamke? Yaani Mungu atunge amri 10 ambazo zinakataza tamaa za kimwili, zinakataza kumtamani mume wa mtu alafu leo hii Mungu huyo huyo akuongezee mke? Derick usinifanye mimi ni mtoto mdogo. Kama ulidhani unaweza ukanitawala kwa namna hiyo aisee sitoweza, wewe endelea kuishi na mwanamke wako, ishi na huyo mchepuko wako humu ndani, mimi naondoka narudi nyumbani kwa mama yangu na baba yangu; kwaherini.”
Nilijaribu kumtuliza mke wangu hasiondoke lakini ilishindikana, Docra alipiga magoti alimtuliza mama Monica lakini aliambulia makofi na mangumi kutoka kwa mke wangu. Ilibidi niamrie ule ugomvi la sivyo Docra angedundwa. Mke wangu alikusanya nguo zake na vitu vyake vya muhimu kisha aliondoka alirudi kwao. Mwanaume nilibaki natoa machozi, Docra nae alikuwa analia tu.
SEHEMU YA 45
Nilikaa kitandani niliwaza itakuwaje kuhusu mke wangu ambaye ameniacha amerudi kwao, mwanamke ambaye nimedumu nae kwa miaka zaidi ya 10, mwanamke ambaye ananipenda kwa shida na ra ha, mwanamke ambaye tulililima pamoja, tulitafuta pesa pamoja, tulijenga pamoja, tulinunua kila kitu tukiwa pamoja alafu eti aniache nile mali na mwanamke mwingine, alafu eti tuachane, alafu eti ndoa yetu ife, kwakweli hilo haliwezekani. Nilitulia niliwaza njia ya kuondoa tatizo, licha ya kwamba nampenda sana Docra zaidi ya mke wangu lakini nilikuwa tayari niachane na Docra kwaajili ya mke wangu. Niliwaza kwakuwa tayari nimefanya mapenzi na Docra hivyo ni heri tuachane akaolewe na mwanaume mwingine.
“Docra” Nilimuita
“Abee mume wangu kipenzi” Yaani hapo tu ndipo ambapo huwa nachanganyikiwa. Mtu namuita ili nimuambie habari za kumuacha lakini ndo kwanza ananiita majina ambayo yalinivuruga, Docra aliacha kulia kisha alinisikiliza kwa makini.
“Docra mimi nina wazo”
“Wazo gani hi Io?”
“Nimemsaliti mke wangu kwa kufanya mapenzi na wewe hadi umepata ujauzito. Mimi binafsi nakupenda sana, na najua kuwa unanipenda. Sasa licha ya kwamba tunapendana lakini mwenzio nipo kwenye ndoa, na unaona namna ambavyo mke wangu anaumia na kuteseka. Tungekuwa waislamu nadhani mambo yangekuwa marahisi tu, lakini kwakuwa sisi ni wakristu mi naona kuna kikwazo”
“Kikwazo gani? kikwazo cha nini? Kwani we point yako ipoje?” Docra alianza kupanic
“Nakuomba nipo chini ya miguu yako, japo hata mimi sipendi ila naomba tuachane.” “Ndo unataka kuniuwa kwa staili hiyo?”
“S i o hivyo ila itabidi tu tuachane. Hiyo mimba mi nitalea ila ukijifungua nitaomba uolewe na mwanaume mwingine. Nafanya hivi sio kwamba sikupendi ila ni kwaajili ya kumuheshimu mke wangu na dini yetu”
“Sawa, ila mimi natangulia kaburini. Kama nina dhambi utanikuta motoni, kama sina dhambi utanikuta mbinguni”
Baada ya majibu yake alisimama aligeuka akitaka kuondoka, nilijua hiyo ni safari ya kwenda kujiuwa; haraka haraka nilimdaka nilimrudisha ndani, alianza kulia juu ya kifua changu. Sikujua nifanyaje, kumpenda nampenda lakini mke wangu nampenda zaidi. Nilikuwa na uwezo wa kumuacha aende kama kujiuwa akajiuwe lakini kwa jinsi ninavyompenda Docra, safari yetu ya mapenzi, mambo aliyonisaidia alafu eti afe kwaajili yangu? aisee nisingeweza kukubali. Pia niliwaza kama Docra ni mwanamke niliyeletewa na Mungu sasa kama tukiachana si naweza kupata majanga mengine mwishowe nitakufa tu.
“Kwahiyo Docra unataka nikuoe?”
“Ndiyo. Mi siwezi kuolewa na mwanaume mwingine zaidi yako.
Nipo tayari hata kufunga ndoa batili, japo dini hairuhusu lakini tutafunga ndoa hivyo hivyo”
“Sawa mimi nimekubali, itabidi twende nyumbani kwa mke wangu tukaongee nae pia tukaongee na wazazi wake tukawaeleze kila kitu; wakituelewa tutafunga ndoa. Lakini nawaza kwa mfano wakikataa itakuwaje? Au unataka tufunge ndoa ya ugomvi ugomvi?”
“Hapana. Kwa mfano kama wakikataa hatutofunga ndoa ila nitakuwa mkeo wa pili pasipo ndoa. Utanioa hata bila ndoa hadi pale mkeo atakaporidhia ndipo utanioa rasmi kwa kufunga ndoa” Na ndio maana huwa nampenda sana Docra, licha ya kwamba ni king’ang’anizi wa mapenzi lakini ni muelewa sana, licha ya kwamba ananipenda lakini hataki masuala ya ugomvi wa kimapenzi, anampenda na anamuheshimu mke wangu ndio maana hataki nimuoe bila mke wangu kukubali. Mimi na yeye tuliondoka tulielekea nyumbani kwa wazazi wa mke wangu ambao walikuwa wanaishi Uyole jijini M bey a, baada ya kufika kwao tuliwakuta wazazi wake sebuleni; Tuliwasalimia kisha niliwauliza kuhusu Mke wangu; waliniambia kuwa yupo chumbani kwake kalala akilia. Kwakuwa mimi ni mwenyeji ndani ya nyumba hiyo taratibu nilisimama kisha nilielekea chumbani kwake nilimkuta kajikunja kwenye kona akiwa ametapakaa machozi kama yote. Hakutaka hata kunitazama, nilijaribu kumshika alinisukuma, hata hivyo kwakuwa mimi ni mumewe wa ndoa kuna muda aliniacha nimshike; Hapo sasa nilianza kubembeleza kwa maneno ya hekima, maneno ya mahaba, nilimtuliza atulie ili tuongee. Baada ya dakika chache alitulia ila hakunitazama usoni. Ilibidi tuweke kikao cha familia, kikao cha maridhiano, kikao ambacho kilimuhusisha m ke wangu na wazazi wake, mimi pamoja na Docra. Ilikuwa ngumu kumpeleka M ke wangu kwenye meza ya kikao, alisema hawezi kukaa pamoja na Docra, hata hivyo baada ya ushawishi mkubwa alikubali ila alikaa akiwa amenuna. Mwanaume nilitakiwa nielezee chanzo cha tatizo hadi mwisho, nami nilianza kwa kuelezea namna ambavyo nilikula kiapo na m ke wangu ili nisimsaliti, nilieleza jinsi nilivyokutana na Docra ambaye tulipata ajali ya ndege kisha tulipona, jinsi alivyonisaidia mambo mbali mbali, jinsi alivyoisaidia familia yangu pamoja na m ke wangu, pia niliwaeleza jinsi nilivyosaliti.
“Wazazi wangu mnisamehe sana lakini h ayo ndiyo yaliyonikuta. Sikupanga kabisa kumsaliti m ke wangu, tena niliogopa sana kuvunja kiapo cha damu lakini ilifikia hatua niliamua kama kufa nife; hapo ndipo nilisaliti kwa mwanamke huyu wa pembeni yangu ambaye ndiye Docra, baada ya usaliti ule alipata mimba, licha ya kwamba nampenda mke wangu lakini pia nampenda Docra” Niliwaambia wazazi wa mke wangu
“Sasa baba utapendaje mwanamke mwingine wakati tayari una mkeo? Hujui kuwa hizo ni tamaa?” Mama mkwe aliongea
“Najua, lakini laiti kama ningekuwa nimefanya dhambi ilibidi niwe nishakufa kutokana na kukiuka kiapo. Mi naomba mridhie tu nimuoe huyu mwanamke awe mke mdogo, mama Monica atakuwa mke mkubwa”
“Kwakweli mimi sina neno labda baba mkwe wako aongee”
“Mimi kama baba mkwe wako nimekuelewa vizuri sana, kwanza nikupongeze kwa huo mkasa wako; angekuwa mwanaume mwingine angeoa kimya kimya lakini wewe umemshirikisha kwanza mkeo. Kwa upande wangu sina kipingamizi, kama mkeo atakubali uoe mke wa pili basi mtajuana wenyewe mtaoana vipi kupitia dini ipi” Baba wa mke wangu aliongea, nilifurahi sana kuona amekubali. Hapo sasa niligeuza macho yangu nilimtazama mke wangu.
“Eti Mama Monica mke wangu, wewe unasemaje? Naomba ukubali basi, Docra ni mwanamke mwema sana ambaye hata damu zenu zinaendana. Tukiwa hospitali aliwahi kututolea damu ili tupone, aligharamia matibabu yetu pia alimlea mwanetu muda ambao tulikuwa tunaumwa. Naomba ukubali nimuoe Docra, sawa mke wangu?”
SEHEMU YA 46
Sote tulikaa kimya tukisubiri jibu toka kwa mke wangu, naye badala ya kutoa jibu alianza kulia; mama mkwe ndiye alimbembeleza mtoto wake, baada ya kunyamaza watu tuliendelea kusubiri jibu. Nilirudia kuuliza swali langu lile lile lakini mke wangu hakujibu. Ukimya wake ulinipa matumaini kuwa labda anataka kukubali ila anaogopa kuongea, kiukweli nilitamani sana akubali nimuoe Docra. Mara alifungua mdomo kisha alijibu kama ifuatavyo;
“Kwanza nimekusamehe mume wangu kwa usaliti ambao uliufanya, nimekusamehe kwa sababu ilibidi unisaliti tu. Japo naumia umevunja kiapo chetu lakini ndo ishatokea, nimekusamehe kwa sababu nakupenda”
“Asante mke wangu”
“Pili nimekusamehe Docra, tena nimekusamehe kwa moyo mmoja. Najua wewe ndiye ulimshawishi mume wangu muwe wapenzi.
Licha ya kwamba alikuambia kuwa ameoa, licha ya kwamba uliifahamu familia yetu lakini bado ulitoka na mume wangu kirnya kimya. Nimekusamehe kwa sababu licha ya kunisaliti lakini bado ulikuwa karibu na familia yangu tofauti na michepuko wengine ambao huwa hawajionyeshi, nimekusamehe kwa sababu ishatokea. Nimekusamehe na nakupenda”
“Asante sana nashukuru” Docra alijibu
“Tatu, licha ya kwamba nimewasamehe lakini sitaki mume wangu aoe m ke mwingine. Docra utanisamehe sana kwa sababu najua unampenda mume wangu, hiyo ni dhambi kubwa; tafuta mume wako. Ebu fikiria wewe ndo ungekuwa mimi ungekubali mumeo aoe m ke mwingine?…Najua ungekataa, hivyo basi hata mimi sitaki. Mimi nina kila kitu cha kumpa mume wangu, hakuna ambacho hakipati kwangu, akitaka mapenzi anapata, penzi anapata, mtoto anapata, maisha anayapata, kwa ufupi ni kwamba sioni sababu ya yeye kuoa m ke mwingine, sipendi maisha ya u ke wenza na sitaki tuwe wawili; nataka niwe mimi mwenyewe. Kuhusu swala hili wala sitaki mjadala mrefu, Docra unanielewa?” “Nimekuelewa”
“Vizuri kwa kunielewa. Hiyo mimba aliyokupa mimi sina shida n ayo, ukijifungua utachagua uishi na mtoto wako au umlete kwenye familia yangu. Lakini suala la wewe kuwa m ke mwenzangu hiyo sahau. Hata kama utaishi mbali na mimi lakini sitaki. Wanaume wote hawa unashindwaje kumtafuta mwanaume wako? Kwani ni lazima tugandane kwenye familia moja? Hivi huoni aibu kutaka kuolewa na mume wangu?”
“Basi mi nimekuelewa, licha ya kukuelewa lazima nitamke hapa hapa kuwa mumeo nampenda. lakini hata kama nampenda sitaki niwe chanzo cha maumivu au mateso au kero kwa mwenye mume, binafsi napenda sana ufurahie ndoa yako, nakupenda wewe, mumeo na mwanao; hata ukoo wenu ikiwemo wazazi wako nawapenda. Mimi sikufuata pesa au mali kwa mumeo, kwetu tuna pesa nyingi tu. Kwa mumeo nilifuata mapenzi, tena sio penzi lile la kitandani; hapana, ni kumpenda tu! hata mimi mwenyewe sijui nampendea nini ila ndo nishampenda. Kwakuwa h utaki na hupendi mumeo anioe japo naumia ila nimekubali maamuzi yako, mimi nitakuwa mbali na mume wako”
“Asante kwa kunielewa. Mume wangu nawe nadhani umenielewa” “Nimekuelewa mke wangu, basi nakuomba turudi nyumbani.”
“Sawa tunarudi ila naomba tuelewane tena, naomba tule kiapo kingine kuwa hutomuoa Docra wala hutooa mwanamke mwingine. Ole wako unisaliti tena kwenye suala hili” “Siwezi kukusaliti tena”
Kikao kiliishia hapo, mke wangu alikubali turudi nyumbani. Docra aliondoka alielekea Dar, mimi na mke wangu tulielekea Kyela mjengoni kwetu. Maisha yaliendelea kama kawa, mwanzoni mke wangu alikuwa akiishi kwa mawazo lakini kadri siku zilivyosonga mbele alizoea na mwisho alianza kusahau. Nilirudi kazini kwangu nliendelea na mishe zangu, biashara yangu iliyopo marekani ilizidi kuwa kubwa siku hadi siku, pesa zangu za mauzo nilizipata mapema, ilifikia hatua baba yake Docra aliniambia niende marekani nikafungue kampuni ya mchele. Nilikubali ila nilimwambia kuwa najipanga kwanza kisha nitaenda.
Wiki tatu zilikatika ndoa yangu ikiwa na amani, licha ya mke wangu kukataa nisimuoe Docra lakini Docra hakununa japo aliumia; binafsi nilidhani Docra angechukua maamuzi ya kuachana na mimi kisha atafute mwanaume mwingine lakini huwezi amini; eti ndo kwanza alizidisha mapenzi kwangu, aliniambia ananipenda kwa namna yoyote ile. Mke wangu yeye alijua nimeachana na Docra lakini sikuachana nae, kila nikipeleka mzigo Dar nilikuwa nakutana na Docra tunafanya mambo yetu kisha maisha yaliendelea. Na hata nilivyomshauri atafute mwanaume mwingine alikataa katakata, aliniambia kuwa kama
Mungu katukutanisha basi ipo siku nitamuoa tu.
Siku zilikwenda, mwezi mmoja ulikatika; kwakuwa tayari nilimuambia mke wangu kuwa nilivunja kiapo cha usaliti, sisi sote tuliamini kuwa sitopata majanga mengine. Bwana wee sikupitisha hata siku mbili nilikamatwa na polisi ambao walinituhumu kuwa silipi kodi ya biashara zangu. Niliwaambia kuwa mimi ni mlipaji mzuri wa kodi, niliwaonyesha document zangu za ulipaji kodi lakini hawakunielewa waliniweka ndani. Mke wangu alijaribu kuniwekea mdhamana lakini polisi walikataa;
“Mumeo halipi kodi alafu anaishi tu hapa mjini, serikali inateseka wakati wafanyabishara wapo, huyu kesho tunampeleka mahakamani”
“Jamani mbona mume wangu huwa analipa kodi muda wote, ni kodi ipi hiyo ambayo haijalipwa?”
“Mtaenda kujua mahakamani, sisi hatutaki kuelewa”
“Naombeni basi kama kuna faini mimi nitalipa ili mumtoe”
Licha ya mke wangu kunipigania lakini polisi walikataa. Masaa yalikatika na siku inayofuata ndiyo nilitakiwa kupelekwa mahakamani, nilipiga mahesabu nifanyaje; nilikosa namna ya kufanya, niliomba kuongea na mke wangu nilimuambia kuwa haina namna itabidi nikubali kwenda mahakamani. Mama Monica alilia sana lakini haikusaidia kitu, alijaribu hata kutoa rushwa kwa polisi; alijaribu kuwahonga pesa ili wanitoe lakini polisi walikataa. Mke wangu hakuchoka, ilifikia hatua alitaka kutoa rushwa ya pesa kwa mkuu wa kituo; hapo sasa mkuu alikasirika, mke wangu alikamatwa nae aliwekwa ndani, hatim aye mimi na yeye tulisubiri kupelekwa mahakamani.
Dereva wangu yule yule ndiye alimpigia Docra alimuambia kuwa mimi na mke wangu tumefungwa kwa tuhuma za kukwepa kodi na kutoa rushwa; Docra alichanganyikiwa, haraka haraka alifunga duka akitaka kuja mbeya. Yeye huwa anapenda usafiri wa ndege ambao ndio wa haraka, hata hivyo siku hiyo alikosa ndege kwa sababu ilikuwa ni jioni; alitakiwa asubiri ndege ya siku inayofuata, na ukicheki siku inayofuata ndiyo siku ambayo mimi na mke wangu tulitakiwa kupelekwa mahakamani! Docra aliona haiwezekani, kwanza alimtafuta mwanasheria mtaalamu wa mambo hayo kisha alikodi gari maalumu ambalo lilitoka Dar saa 10 jioni lilifika Kyela saa 6 usiku. Siku zote kituo cha polisi huwa akifungwi, walifika kituoni walikutana na polisi ambao walikuwa zamu. Hapo sasa masuala ya sheria yalianza, kwanza wakili alitaka nimpe document zangu za kodi; nilimwambia Docra aende nyumbani akazichukue kisha ampe wakili, Docra alifanya hivyo. Baada ya document kupatikana yule wakili kwa kutumia elimu yake alihitaji kuonana na mkuu wa kituo, ilibidi amfuate nyumbani kwake, katika mazungumzo yao alimuambia maneno yafuatayo; “Kisheria nyie kama polisi hamjakosea kumkamata mtuhumiwa, lakini kabla kesi haijenda mahakamani ni lazima kuwe na tatizo ambalo litafanya mtu aende mahakamani. Mnasema kwamba mke wa mtuhumiwa alitaka kukupa rushwa, nakubaliana na wewe mkuu wa kituo lakini mimi nahisi polisi wako wana shida”
“Shida gani?”
“Polisi wako ndio wamesababisha mke wa mtuhumiwa afikie katika hatua ya kutoa rushwa kwa sababu aliomba kulipa faini amekataliwa, mdhamana amekataliwa, na ukicheki mtuhumiwa hana koşa hata moja. Muheshimiwa ebu tazama hizi document za kodi, tena hii kesi ikifika mahakama kuu nyie polisi mtaingia katika matatizo makubwa, na wewe mkuu wa kituo utapata shida sana kwa sababu kituo chako oha polisi kitaonyesha udhaifu wa wafanyakazi, alafu wewe utaonekana hujui kuongoza kituo. Document za Derick zinaonyesha nidhamu ya kulipa kodi, hajawahi kupitisha mwezi hata mmoja, pia mauzo yake yote yanaonekana, si unaona hapa alilipa mwezi wa kwanza, wa pili, watatu, hivi mkuu huyu mtu mnamfunga kwa kosa lipi? Au ana ugomvi na nyinyi mnaamua kumkomoa? Labda wewe niambie anadaiwa kodi ya mwezi upi?
Mkuu wa kituo alikosa maneno, hadi kufikia hapo wakili wangu alishinda. Pasipo kutarajia mimi na mke wangu tuliachiwa bila shida yoyote, Docra alifurahi kuona tumetoka, alikuja kutukumbatia wote wawili, alitupatia pole kwa matatizo. Mimi nilifurahi ila mke wangu aliona aibu. Baada ya kuhakikisha tumetoka usiku ule ule Docra aliaga akitaka kurudi Dar.
“Nimefurahi mmetoka, nilikuja huku kwa lengo hilo; nilitaka nije niwatoe kisha nirudi kazini. Hivyo basi mimi na wakili tunapenda kuwaaga”
“Hapana, Docra bado sijakushukuru naomba usiondoke; twende nyumbani kwangu nikakushukuru” Mke wangu alimuambia Docra, moyoni nilijikuta nimetabasam
“Sawa. Basi ngoja nimlipe wakili ili yeye atangulie kisha mimi nitaondoka na nyinyi”
Docra alihesabu pesa nyingi alimpa wakili, wakili alishukuru kisha aliondoka alirudi Dar. Sisi watatu tulielekea nyumbani kwangu ambako sio mbali na kituo chetu cha polisi. Licha ya kwamba ilikuwa saa 8 za usiku lakini hakuna yeyote kati yetu ambaye alihisi usingizi, njiani tulitembea kirnya kirnya, hakuna aliyemsemesha mwenzie. Hatimaye tulifika nyumbani, hapo sasa tuliweka kikao cha watu watatu, m ke wangu ndiye alikuwa muongeaji mkuu wa kikao hicho, aliongea mambo mengi kama ifuatavyo;
“Mchepuko anauma lakini wewe Docra huna maumivu. Mumeo akitoka nje ya ndoa inauma sana na ndio maana niliumia mume wangu kunisaliti; lakini leo nathubutu kusema kuwa sina maumivu ya kusalitiwa. Sina maumivu kwa sababu mume wangu amenisaliti kwa mwanamke ambaye nashindwa kumuelezea; mwanamke ambaye ananipenda, ana mapenzi ya kweli, anajali shida zangu na matatizo. Sidhani kama Docra unafanya haya yote ili tu uolewe na mume wangu, hapana, najua unafanya kutoka moyoni, asante kwa kila kitu”
“Sawa usijali, mimi niko pamoja na nyi nyi”
“Sina maneno mengi ila nimegundua kuwa wewe Docra hutakiwi kukaa mbali na familia yangu, wewe unatakiwa uungane na familia yangu. Kutoka moyoni kwangu nimekubali mume wangu akuoe! Japo sikupenda ila kwa mapenzi haya itabidi akuoe tu; haina namna”
Weuwee! Unajua kufurahi? Docra aliruka alimkumbatia m ke wangu, nyumba nzima ilimeremeta kwa shangwe na furaha, Docra alihisi ndoto ya ke imetimia. Alimpigia magoti m ke wangu alimshukuru kwa nafasi hiyo ya kuwa m ke mdogo.
“Asante sana kwa ruhusa yako bi mkubwa, mimi Docra sina maneno mengi zaidi ya kushukuru. Nitahakikisha nakuheshimu sana, hata ukiniambia niwe mpishi wako nitakupikia, ukiniambia nikufulie nguo nitakufulia; kwa ufupi ni kwamba sitokuwa kikwazo kwako, nitakusikiliza na nitakupa heshima yako wewe kama m ke mkubwa. Asante sana! Mungu akubariki na aibariki familia h i i” Docra alimaliza maneno ya ke, mwanaume nilibaki nachekelea tu.
Tangu siku hiyo sikupata tena matatizo yoyote, japo kidini sikuruhusiwa kumuoa Docra lakini nilimuoa na hadi leo ni m ke wangu tuna watoto wawili. Baada ya kuhitimu chuo alipata kazi muhimbili, kwa sasa yeye ni d aktarı lakini bado tunaendelea kufanya biashara zetu za mchele na unga. Wazazi wake wananipenda sana, pia kitu pekee ambacho huwa kinanipa raha ni kuona namna mke mkubwa na mdogo wanavyopendana, wanapendana hadi nawaonea wivu. Na kuna siku huwa nalala nao wote wawili katika kitanda kimoja pasipo ugomvi wowote!.
MWISHO