KWA MAPENZI HAYA LAZIMA TU NIMSALITI
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
SEASON ONE
Sehemu ya 01
Kwa majina naitwa Derick Mwakasungura, mimi ni mkazi wa kyela jijini Mbeya. Nina mke na mtoto mmoja wa kike aitwaye Monica, hiyo imenifanya mtaani nifahamike kwa jina la baba Monica. Kazi yangu kubwa ni kilimo, huwa nalima mpunga, nakoboa kisha nauza mchele kwa wanunuzi mbalimbali. Maisha yangu sio mabaya sana wala sio mazuri sana, ila namshukuru Mwenyezi Mungu kwa sababu nina uwezo wa kumudu gharama nyingi, nalea vizuri familia yangu, mwanangu anasoma sekondari bila shida, m ke wangu anapendeza kila siku, kubwa zaidi huwa nasaidia watu wenye uhitaji, na ndio maana nimekuwa maarufu mtaani kwetu, kila mtu ananipenda, naheshimika kutokana na heshima ambayo nimejitengenezea.
Licha ya maisha yangu kunivutia mimi, familia yangu na watu wengine lakini katika ndoa nilipitia changamoto na vishawishi vingi vya siri ambavyo hata m ke wangu hakuvijua. Kishawishi na changamoto kubwa kwangu ilikuwa ni kusumbuliwa na wanawake wa rika zote, kuanzia watoto wa chuo, vijana wa mtaani hata wake za watu walinitamani kimapenzi. Hata hivyo namshukuru Mungu alinipa ushindi katika vishawishi hivyo, japo kuna baadhi ya wanawake walinivutia kwa kiasi kikubwa lakini hakuna ambaye nilimkubalia. Kwa kipindi hicho ukimuondoa m ke wangu katika maisha yangu sikuwahi kumtongoza mwanamke mwingine yeyote, hao wote walionitaka wao wenyewe ndio walikuwa wananitongoza kwa staili nyingi nyingi kama ifuatavyo;
“Derick mi nakupenda kuliko mkeo, sijakupendea pesa ila nakupenda tu. Moyo wangu unaniambia kuwa wewe ndiye mwanaume sahihi kwangu, haijalishi umeoa au una mtoto ila naomba nipende hivyo hivyo, nipo tayari hata niwe m ke wa pili, hata nikiwa mchepuko wa siri haina shida, nikubalie please!” Hiyo ilikuwa ni sauti ya Delila binti wa chuo ambaye alinifuata kazini kwangu kisha alinieleza hisia zake. Alinieleza akiwa analia kwa machozi mengi, alinipigia magoti akinitazama usoni kwa uchungu. Delila alikuwa ni binti flani hivi mzuri, rangi ya ke ni maji ya kunde, mrefu mwenye shepu ya wastani, akikuchekea unaweza ukazimia kwa raha. Akitembea huko nyuma kama samaki anatingisha mkia, hata hivyo sikumkubalia, nilimkatalia kwa herufi kubwa, aliondoka na maumivu ya ke. Mwanamke wa pili kunisumbua alikuwa ni m ke wa rafiki yangu ambaye ni jirani yangu, huyo alikuwa ni binti flani kibonge japo sio sana, yeye alinifuata nyumbani kwangu siku ambayo nilikuwa pekeyangu, aliniambia maneno matamu kama ifuatavyo;
“Derick unajua kuwa nimeolewa na rafiki yako, hata wewe umemuoa rafiki yangu mama Monica. Licha ya h ayo yote nataka tuweke ujirani na urafiki pembeni, nimevumilia kwa muda mrefu sana lakini ukweli ni kwamba nakupenda, naomba tuwe wapenzi wa siri. Najua utajiuliza kwanini nakupenda wakati nimeolewa, jibu ni kwamba yule rafiki yako akiwa chumbani sio mtaalamu, hajawahi kunifikisha kokot e, m baya zaidi mkeo aliwahi kuniambia kuwa ukimkalia juu hujawahi kumuacha salama, tafadhari Derick mimi sitaki kuharibu ndoa yako, naiheshimu sana ila naomba tuwe wapenzi ili uwe unanisaidia shida yangu” M ke wa my friend alinichana makavu akiwa ananitazama usoni, alitoka kwenye sofa lake alikuja kukaa pembeni yangu, alinishika mikono akinisisitiza nimkubalie lakini nilikataa katakata.
Mwanamke mwingine ambaye alinisumbua sana alikuwa ni dada mmoja hivi ambaye ni mfanyakazi wa benki. Dada huyo kila akitoka ofisini kwake alinipitia dukani kwangu aliniletea zawadi nyingi tu, kuna muda alinipa pesa akiniambia zinisaidie kukuza mtaji, nilishindwa kukataa kwa sababu hata nikikataa aliniachia mezani kisha aliondoka. Siku moja alinichukua alinipeleka hoteli, mwanaume nililishwa mapochopocho ya kila aina, nilikula ofa kama zote, mimi ni mnywaji pombe wa kawaida; naweza kunywa bia mbili au tatu ili kuchangamsha damu tu, lakini siku hiyo nilinunuliwa kreti zima, nilikunywa pombe hadi nilipoteza akili zangu zote. Baada ya kuona nimelewa sana alinichukua alinipeleka kwenye chumba ambacho alikichukua katika ile hoteli, hiyo ndiyo siku pekee ambayo ilinifanya niache pombe. Alinitupia kitandani kisha alinivua shati na suruali, nilibaki na boksa pekee, kabla hajaniondoa nguo ya ndani kwanza alipanda kifuani kwangu kisha alinichezea kwa jinsi anavyotaka akiwa ananiambia maneno mengi ya kimahaba, japo nilikuwa tilalila lakini viungo vyangu vyote vilipata moto mkubwa sana, baada ya kuona nimelainika hapo sasa alishuka chini alikamata boksa yangu akitaka kuivua. “We unataka kufanya nini? Acha!” Nilijikuta nimepayuka kwa sauti ya nguvu hadi yule dada alishtuka.
“Tafadhari Derick, naomba niache nifanye hichi kitu” Aliniambia akinitazama kwa macho yenye uchungu wa mahaba, alihitaji nimuonee huruma ya penzi, mtoto alikuwa wa moto balaa.
Ili kuonyesha kuwa ni kweli alinihitaji, pale pale alianza kuondoa viwalo vyake, alianza na kishati cha juu alikiondoa, alivua suruali yake ambayo ilibana hips zake, nilibaki nimekodoa macho mara baada ya hips zake zote kumwagika hadharani, kumbe ile suruali ambayo alivaa ilikuwa inabana shepu, suruali ilificha utamu, nisiwe mnafiki; nilitongozwa na wanawake wengi lakini dada wa benki alikuwa ni mzuri jamani, nilijikuta natokwa udenda, ile pombe yote iliisha! Licha ya kwamba sikuwa tayari kusaliti lakini boksa yangu ilisumbua sana! Yule mdada alitabasam mara baada ya kuona kiungo changu kinapumua juu chini, moyoni kwake aliamini kuwa nishakuwa wake, hata mimi mwenyewe kimoyomoyo nilijisemea kuwa siku hiyo sitotoka salama, mke wangu anisamehe tu, niliamua kuruhusu lolote lifanyike.
SEHEMU YA 02
Yule dada alibaki na kufuri pekee, kama mjuavyo kuwa siku zote wewe na mpenzi wako mkiwa chumbani hakuna vazi tamu kulitazama kama nguo ya ndani hasa ya mwanamke. Mwanamke akivaa kufuri anatamanisha hadi anakera kwakweli, unaweza ukatamani usimtumie alafu uwe unamuangalia tu namna alivyonoga. Alinilalia kifuani kisha alinipa busu la kikubwa, hata ungekuwa wewe ungekataa? Ungekwepesha mdomo? Wewe acha utani mwanangu! Mi nilikubali bwana wee! sasa ningefanyaje? Na ukicheki nilikuwa tungi balaa. Kitendo cha kukubali kupigwa busu kilimpa nguvu kubwa yule dada, alishusha mkono wake chini akitaka kuuzamisha ndani ya boksa, kabla hajafanya lolote mara simu yangu iliita, niliitazama nilikuta nimepigiwa na mke wangu, haraka haraka nilipokea kisha nilisogeza sikioni niliongea;
“Hallo mke wangu” “Baba Monica hiyo tabia ya kuchelewa kurudi nyumbani umeanza lini? Au huoni kuwa muda huu ni saa 4 usiku? Ina maaana hadi sasa upo kazini? Sawa kama upo bize na kazi, ila mi naenda hospitali nampeleka Monica amezidiwa”
Nilikata simu kisha fasta nilivuta nguo zangu nilivaa, yule dada alinishangaa; aliniuliza kulikoni lakini sikumjibu wala sikutaka anisumbue, nikiwa nataka kuondoka alinishika shati aliniambia tufanye walau kidogo tu lakini nilikataa kwa nguvu zote kisha nilimkoromea kwa ukali; nilimuambia nina mke na mtoto hivyo basi aachane na mimi, nilimuambia simpendi na hasinifuatilie, baada ya maneno hayo niliondoka nilielekea hospitali, yule dada nilimuacha chumbani na sikujua nini kiliendelea kwa upande wake. Tangu siku hiyo niliacha kabisa kupokea ofa za watu hasa za wanawake, hata zawadi za bure sikuzipokea, niliacha mazoea na wanawake wenye mazoea ya kisaliti, nilifanya hayo yote kwakuwa nampenda mke wangu pia naipenda familia yangu, kubwa zaidi sikuona faida ya kusaliti kwa sababu mke wangu ni mzuri, kila ninachotaka kwake nakipata, sasa nimsaliti ili iweje? Na ukicheki katika maisha yangu hakuna mtu alinipigania zaidi ya mke wangu, alikuwa na mimi katika kila hali, tulitafuta maisha pamoja, alinivumilia madhaifu yangu mengi sana, ananipenda na nina uhakika kwa asilimia 1000% kuwa hajawahi kunisaliti kutokana na matendo ya ke, sasa kwanini mimi nimsaliti eti jamani? Ah we mi siwezi kufanya huo utopolo husio na faida.
Nguvu zangu nyingi nilizielekeza katika kukuza biashara yangu, mchele wangu ulianza kuvutia watu wengi wa mikoa ya ndani ya nchi. Pia nilianza ku pata oda toka kwa wateja waliopo nchi za jirani kama Kenya na Uganda. Nilisambaza huko kote, niliongeza mashamba, nililima hekari nyingi kiasi kwamba nilinunua magari makubwa ambayo yalianza kusafirisha mpunga na mchele kutoka sehemu moja hadi nyingine, pia nilinunua gari binafsi la kutembelea, nilifungua maduka katika mikoa mbalimbali, nilijenga kampuni yangu ya uzalishaji wa mchele, pia nilipata tenda nyingi kutoka kwa wazungu ambao walihitaji bidhaa zangu.
****
Siku moja nikiwa nyumbani na familia yangu mara simu yangu iliita, nilitazama nilikuta nimepigiwa kupitia “facebook video call”, nilipigiwa na mmoja wa marafiki zangu aliyepo nchini marekani aitwaye Joshua, kwakuwa nami ni mtaalamu wa mambo ya mitandao ya kijamii nilipokea haraka haraka kisha facebook ilituunganisha mimi na Joshua. Tulisalimiana, tulikumbushana enzi za shule, tuliulizana kuhusu maisha na ndoa, mwisho tulihamia kwenye biashara. Joshua alinipa habari ambayo ilinisisimua vibaya mno, aliniambia maneno yafuatayo;
“Oya Derick eeh, Juzi kati niliagiza mchele toka huko Tz, nilimwambia dada yangu aninunulie kisha aniagizie huku USA, alifanya hivyo kisha alinitumia. Ule mchele ulikuwa mwingi alafu mweupee, mzuri, hata mara baada ya kupika kitu kilinukia hadi kwa wazungu. Mara ghafla nilishangaa nimevamiwa na wamarekani, waliniambia wanahitaji mchele ambao nilipika kwa sababu una harufu nzuri tofauti na mchele wao feki, walinipa pesa ili niwauzie; kuna baadhi niliwauzia lakini wengine niliwapa bure. Balaa lilikuwa pale ambapo walipika, walikula kisha walinogewa, walianza kupeana habari kuwa nina mchele safi, watu walipanga foleni nje ya nyumba yangu wakiniambia niwauzie mchele. Nilipagawa sana kwa sababu hata mimi mwenyewe niliishiwa, sikujua niwauzie mchele gani. Niliwaambia ukweli kuwa sina kitu, japo ilikuwa ngumu kueleweka lakini nashukuru walinielewa, walinielewa kwa sharti moja kubwa”
“Sharti gani hilo kaka?”
“Waliniambia niwaonyeshe mahali ambako nilinunua mchele, niliwaambia kuwa niliagiza toka Tanzania; hapo sasa kıla mmoja alitaka kunikabidhi pesa yake ili niwaagizie, nilikataa nikiogopa hatari ya kupoteza pesa za watu, baada ya kuona nawazingua walitaka waagize wao wenyewe, waliniuliza mchele niliagiza kwa nani? walitaka niwape jina la kampuni ambayo inazalisha mchele huo”
“Eeeh ukawaambiaje? Ni kampuni gani hiyo inazalisha?”
“Nilizama ndani nilichukua mfuko wa mchele niliutazama, ebwana sikuamini mara baada ya kukuta mchele umetoka kwenye kampuni yako..Nilifurahi kinoma, nilirukaruka kama kichaa, hata wazungu walinishangaa.”
“Dah kaka usinifanye nizimie, kaka utaniua kwa raha! Kwahiyo ina maana mchele wangu ndio ambao unaliliwa na wazungu?”
“Habari ndio hiyo, wazungu wamenogewa huku, sasa lengo la kukupigia ni kukuomba au kukushauri kwamba kama unaweza tufanye biashara, uwe unanitumia mchele wa kutosha kisha mimi nitashughulikia ishu za mauzo, tutapiga sana pesa. Najua kwa sasa una mtaji mkubwa, pesa unazo, ikiwezekana njoo huku USA uje tupange namna itakavyokuwa, maeneo huku yapo mengi tu, we chukua viza uje! Usiwaze kuhusu wateja, wapo wengi sana, tena ukija njoo na mifuko ya kuanzia ili uone jinsi wanavyogombaniana”
Baada ya mazungumzo hayo tulikubaliana tufanye biashara, tena nilikubali kwa asilia zote, nilimshirikisha mke wangu naye alikubaliana na mimi; aliniambia kuwa ni jambo jema sana, kwakuwa tulimuamini Joshua tuliona mchongo huo utakuwa mrahisi kufanyika. Siku iliyofuata nilienda katika mamlaka ya usafiri nilishughulikia ishu ya passport na viza ya kusafiria, nililipia ruhusa zote za kusafirisha mizigo kisha niliandaa mzigo wa kutosha kwaajili ya kuupeleka marekani. Hayo yote niliyafanya nikiwa nawasiliana na Joshua ambaye ndiye nilimtegemea kukamilisha dili hilo. Baada ya kuandaa mzigo niliongea na madereva wangu niliwaambia watangulize mizigo Dar kisha mimi nitafuata.
Kila kitu kilikamilika, hatimaye muda wa safari ulifika, nilimuaga mke wangu na mwanangu, walinitakia safari njema kisha waliniombea kwa Mungu nikafike salama pia nikakamilishe malengo yangu. Si unajua tena mimi na mke wangu tusingeweza kuagana burebure, basi usiku kama kawa kama dawa nilipambana ya hela yote, nilimvuruga hadi alivurugika, baada ya mizunguko kadhaa wote tulikuwa hoi bin taaban! Tulitulia tukiwa tumekumbatiana, tukiwa tumetulia ghafla mke wangu alianza kulia bila sababu, tena alilia kweli kweli hadi nilishangaa. Taratibu nilipandisha mikono yangu kichwani kwake kisha nilimtuliza lakini hakutulia, nilimpa maneno matamu, maneno ya kumtoa panya kwenye roba la mahindi lakini wapi; aliendelea kulia. Si unajua tena utu uzima dawa? basi ilibidi nimtulize kikubwa; nilipiga mazoezi juu ya mwili wake kisha nilianza kucheza soka safi, nilipiga vyenga kama Messi, mashuti kama Ronaldo, kuna muda nilichukua niliweka waah! Hapo sasa mke wangu alinyamaza kisha alinitazama kwa muda mrefu, sijui alikuwa anawaza nini ila ghafla alianza kulia tena, safari hii alilia kwa sauti kubwa hadi nilishangaa! Mechi ilisimama, nilijiuliza inakuwaje tena? Kwanini mke wangu analia? Kwamba ndo kachanganywa na soka au nilimchezea rafu nyingi?.
SEHEMU YA 03
“Mke wangu mbona sikuelewi? ndo kilio gani hicho? Mbona hakifanani na kilio oha kandanda safi?” Nilimuuliza nikiwa nimetuliza mpira
“Mume wangu naomba ukienda huko kafanye biashara, usije ukanisaliti, kumbuka tulikotoka, mimi na wewe tulikutana wote tukiwa wapya, tumeishi pamoja kwa miaka zaidi ya 10, hujawahi kusikia skendo zangu mbaya wala sijawahi kusikia skendo zako mbaya, sasa huko unakokwenda ni nchi za watu, utakutana na mambo mapya, natamani mambo ambayo utakutana nayo yasiwe na vishawishi. Japo nakuamini kwa asilimia 100 lakini ni jukumu langu kukukumbusha kuwa unaondoka unaniacha mimi na mwanao, japo umesema utakaa kwa wiki moja lakini mimi naiona nyingi sana, ukishikwa na tamaa za mapenzi ni heri uniite nikufuate huko huko kuliko kunisaliti, yaani ukinisaliti wewe sijui hata itakuwaje, nahisi siku hiyo hiyo kifo kitatutenganisha” Aliniambia akiwa bado anatiririkwa machozi.
“Mimi siwezi kukusaliti, miaka 10 sijakusaliti alafu nikusaliti kwa wiki moja? Siwezi hata kidogo. Kama tulivyokubaliana ikitokea siku nakusaliti uniache”
“Unajua kabisa siwezi kukuacha ….Kwakuwa naogopa naomba tule kiapo cha mwisho”
“Kiapo gani tena mama Monica? Kiapo tuliapa siku ya ndoa, tulivishana pete za kuishi pamoja milele daima”
Licha ya kujitetea lakini mke wangu hakunielewa, kabla mechi haijaisha alinisukumia pembeni, aliondoka alielekea kwenye kabati alichukua wembe kisha alinifuata pale kitandani, aliniambia ninyoshe mkono, nilitaka kukataa lakini alinilazimisha hadi nilinyosha, kwenye kile kidole cha pete alinichana damu zilitoka, pia yeye mwenyewe alijichana kwenye kidole chake cha pete kisha aliviunganisha vidole vyetu kwenye lile eneo ambalo lilivuja damu, damu zetu ziliungana, hakuishia hapo; aliniambia tuape kuwa yeyote atakayemsaliti mwenzie afe hapo hapo. Yeye alianza kuapa kama ifuatavyo;
“Mimi Neema, naapa kwamba nikimsaliti mume wangu Derick nife siku hiyo hiyo au linikute jam bo” Baada ya kuapa alinitazama mimi kisha aliniambia niape.
“Mimi Derick naapa kwamba nikimsaliti mke wangu nife hapo hapo au linikute jam bo” Niliapa kwa sababu nilijiamini kuwa siwezi kumsaliti mwanamke nimpendaye.
Baada ya kiapo hicho mke wangu alitabasam akiwa na matumaini kuwa sitomsaliti kamwe, alizidi kunipenda kuliko kawaida, alinikumbatia kwa nguvu kisha kilichofuata hapo hata sikuamini; siku hiyo ndiyo niliamini kwamba mke wangu ni fundi kuliko Maufundi! Nilizungushiwa, nilikandamizwa, niligeuzwa geuzwa, nilivurugwa kisha nilifinyiwa kwa nje; weuwee! Mwanaume nilifumba macho nililala usingizi wa rah a, nilijiona kama tupo bustani ya Eden Hazard tukila matunda mwitu! Mara baada ya kufika mwisho tulilala fofofo tukiwa hatujitambui.
****
Kulikucha asubuhi na mapema, kutokana na kasheshe la usiku sikuwa na hamu ya kupiga cha asubuhi wala cha jioni; nilijiandaa mapema, kwa mara nyingine nilimuaga mke wangu kwa maneno na matendo kisha nilielekea stendi kuu Mbeya mjini, huko nilipata basi kuelekea Dar. Baada ya kufika DSM nililala gesti kisha asubuhi nilielekea katika ofisi za meli ambayo ilishughulikia usafirishaji wa mizigo, nilikamilisha taratibu zote, madereva walileta mzigo ambao tuliushusha bandarini. Nilitoa maelekezo kuwa mzigo huo utapokelewa na mimi mwenyewe au Joshua ambaye alikuwa USA. Baada ya kukamilisha ishu ya mizigo nilielekea uwanja wa ndege wa J.K.Nyerere kwaajiri ya kuanza safari yangu, nilipata ndege ambayo ingenifikisha Kenya, kule Kenya ningechukua ndege nyingine iendayo New York. Nilikaguliwa kisha nilizama ndani ya dude, ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kupanda ndege, nilihisi kama nipo peponi vile, nilitazama vizuri abiria wenzangu niligundua kulikuwa na siti za watu wawili wawili, watu walijaa kuanzia mbele hadi nyuma, mimi siti yangu ilikuwa katikati, nilisogea karibu nilikuta siti nzima ikiwa wazi, nilikaa upande wa dirishani kisha nilitulia nikisubiri kumuona abiria mwenzangu ambaye alitakiwa kukaa pembeni yangu, sasa nikiwa najiuliza nani atakaa pembeni yangu mara nilisikia kisauti cha kike kikisema “Ndugu abiria tafadhari funga mkanda kabla hatujaanza safari, ndege yetu itapaa dakika 3 zijazo” Baada ya kauli hiyo nilishangaa kwelikweli, nilijiuliza inamaana mimi pekeyangu sina wa kuishi nae ndani ya ndege? Wenzangu wote wamekaa sare sare sasa mimi nina koÅŸa gani hadi niachwe mpweke? Kweli nitoke TZ hadi Kenya nikiwa mwenyewe? Bila mtu wa kupiga nae story? Bora hata ningekaa na mzee mwenzangu yoyote ambaye anajua mpira kisha tungekuwa tunajadili soka ili safari iwe nyepesi, lakini ndo hivyo, nilifunga mkanda wangu kisha nilitulia nikiwaza kufika marekani.
Sasa nikiwa nimekaa kinyonge mara paap nilisikia “ko ko ko” sio kwamba kuna mtu alikohoa, hapana, bali zilikuwa ni skonkwido za mtu akitembea, nilishangaa kuona kila mtu akigeuza macho nyuma ili amuone huyo anayetembea, hata rubani alidata; badala ya kupaisha ndege yeye alipaisha uso juu kisha alijilamba midomo mara baada ya kujionea maajabu ya karne. Kama rubani kageuka nyuma sasa mimi abiria ni nani hadi niwe na kiburi cha kutazama m bele? Mwanawane sikuvunga wala sikuzubaa, niligeuza shingo na pua yangu nilitama kilichotazamwa na watu wote! Nilimuona mtoto mkali akikatiza katika mitaa ya barabara ya ndege; Jamani hapa naomba tuwekane wazi, m ke wangu mimi ni mzuri ila huyo mrembo aliyekuwa akitembea alikuwa ni mtamu kila idara, ukimtazama tu unasisimka, moyo wako lazima usheki kidogo, tumbo lako hata kama lina sixpack ni lazima livimbiwe kwa gesi ya mshangao, nyie hii dunia ina mabinti wameumbwa jamani mweeh! Kwanza huo mwendo tu nilivurugwa, shepu yake nilichanganyikiwa, rangi yake nilipagawa kabisa, hapo zamani za kale nilifikiriaga kwamba wanawake wenye mizigo mikubwa wote wana sura mbaya, lakini siku hiyo nilijiprove wrong; yule mdada chini alibinuka alafu juu alibonyea, ana kauso flani hivi kama mdori vile, alafu sasa ukimcheki kwa makini unaweza ukashindwa kujua kama ni mdogo au mkubwa, kuna muda unaweza sema bado hajabalee, hata hivyo kutokana na uzuri wake ni lazima utapata wasiwasi kuwa wahuni walipita nae, si unajua tena wahuni sio watu wazuri? Habari ndiyo hiyo.
Baada ya kila mmoja kumuona binti huyo hatua iliyofuata ni watu kuchunguza toto hilo litakaa wapi, rubani alitamani mtoto akakae mbele, abiria wengine walitamani mtoto akakae kwao, lakini kumbuka kwamba siti ilibaki moja tu ambayo ni ile ya pembeni kwangu, licha ya siti kubaki moja hata hivyo nilihisi huyo mrembo hawezi kukaa na mimi, hiyo kitu haiwezekani, yaani hashindwe kukaa na watu wote hao eti aje kukaa na mimi? Kivipi yani? Kiaje yani? Ah we hiyo haiwezekani hata kwa dawa za waganga wa kienyeji. Mimi siwezi kuwa na bahati ya kukaa na mrembo wa hivyo. Mtoto alinichanganya kiasi kwamba kwa muda huo nilimsahau mke wangu, sio kwamba mke wangu sikumtaka, hapana, nampenda sana mke wangu.
Mtoto mzuri alitembea kwa maringo na madaha akija upande wetu sisi tuliokaa katikati, nimesema hakuja upande wangu bali alikuja upande wetu. Sijui hata nilipigwa na shoti gani kijana wa watu, nilijikuta nimeganda kama roboti mara baada ya binti huyo kuja kukaa pembeni yangu, abiria wote walinionea wivu, walikereka vibaya mno, bili wairithi siti yangu, lakini kwa jinsi nilivyo na roho ngumu sikuzimia wala sikupeperuka, sikufa wala sikufufuka, mi niliganda tu, hata muda ambao ndege ilipaa sikusikia kabisa, nilijikuta tu nipo juu hewani sikujua tulifikaje, nilishtushwa na sauti taamu yenye rah a;
“Mambo” ilikuwa ni sauti ya yule dada ambaye aliongea akitabasam akiwa ananitazama usoni.
SEHEMU YA 04
“Powa habari yako” Nilimjibu ila niliogopa kuongea nae “Safi tu, vipi nawe unaelekea USA au unaishia Kenya?”
“Mimi naenda kwa Trump”
“Oh kumbe tupo wote, basi ni vizuri, samahani nimekushtua usingizini mana naona ulianza kulala”
“Alafu hata sikulala, nilipitiwa na stress tu”
“Mh stress za nini?”
“We acha tu, utu uzima una tabu sana, yani hapa nahisi homa sio homa, hata sijielewi mwenzenu”
Mdada alicheka kisha tulitulia, kila mmoja alikuwa bize na simu yake, mimi nilizuga kama nachati vile kumbe sikuwa na lolote, kuna muda macho yangu yalitua kwenye mapaja yake; daah! Nilijiuliza hilo ni paja au nyama choma! Mtoto alikuwa ana upaja mlaini, upaja teketeke, upaja mkubwa kweli, nilishindwa kuumezea mate kwa sababu nampenda sana mke wangu. Muda wote alikuwa anafurahi tu, mara ampigie baba yake kisha waliongea kizungu, alimwambia kuwa yupo njiani, kuna muda alipiga selfie kisha aliweka status ili awarushe roho watu, mara alipost Instagram ili awakere wambea, nilibahatika kuona jina lake la insta, kimya kimya nilizama mtandaoni ili nikacheki picha zake, nilishtuka kukuta amepost picha akiwa na mimi kwenye ile siti yetu, nilijikuta natabasam hadi nilitokwa na udenda kama mtoto mchanga, nilifungua comment za wafuasi wake nione wamemuandikia nini, weuwee! Hapo sasa nilicheka kwa sauti hata baadhi ya abiria waligeuka walinitazama, yule dada nae alinitazama, rubanı nusura atudondoshe; eti nae aliacha kuongoza ndege alinitazama mimi mwehu nisiye na maana. Kila mmoja alitaka kujua nacheka nini, hata hivyo nilivunga, nilijidai kama sijacheka vile, watu waliachana na mimi kisha walitazama mbele, mimi nilirudisha macho yangu kwenye ile picha, nilisoma tena yale maoni, unajua nini kilinifurahisha? Unajua kwanini nilihisi raha? Unajua kwanini nilicheka kwa furaha? Ni mara baada ya kuona kila aliyeandika maoni alimuambia yule dada kuwa yeye na mimi tumependezana kama wapenzi, pia kuna mwingine aliandika hivi “Woow! Hatim aye umepata wa kufanana nae, vipi ndo huyo au tuendelee kusubiri?” moyoni nilitamani yule dada ajibu maoni hayo, nilimuona akicheka, nilijua anafurahia comment hiyo, mara nilimuona anamjibu mfuasi wake mmoja, baada ya kuandika nilirudi tena kusoma nilikuta amemjibu yule aliyeuliza kama mimi ndo mwenyewe, nilikuta amemjibu hivi “Hapana, kwanza ilikuwa bahati mbaya tu ameonekana, nimejaribu kumcrop nimeshindwa, nimejaribu kumkata hasionekane lakini nmefeli, nimeamua kupost tu ila muda wowote nitafuta ili watu wasinielewe vibaya”. Baada ya kusoma jibu hilo nilichoka, nilikosa rah a, sikutaka hata kumtazama tena, kwanza kwa hasira nililala kwenye siti nilipitiwa usingizi.
Nilikuja kushtuka nikiwa uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta nchini Kenya, tena yule dada ndiye aliniamsha. Kwakuwa wote tulikuwa tunaelekea marekani basi kwa pamoja tulifanya taratibu zote za kupata usafiri, safari ilianza mida ya saa 4 asubuhi, kama kawaida tulikaa siti moja. Tofauti na ilivyokuwa mwanzo, safari hii yule dada hakuwa muongeaji wala hakunichangamkia kama mwanzo, na ukicheki mimi ni muoga balaa, niliogopa kumchokoza ila nilitamani tuwe tunaongea. Kuna muda niliona liwalo na liwe niligeuza macho nikitaka kumsabahi lakini kwa bahati mbaya nilimkuta kalala, nilikosa pozi. Nilivunga nikisikilizia, ndege ilichana mawingu, kwa mbali nilianza kumuona Trump akinitazama; nilitabasam nikijiona mwamba wa masafa marefu kumbe sina lolote.
Nikiwa nimekata tamaa ya kuongea na yule dada mara nilishtuka kuna mtu kalalia bega langu, haraka haraka niligeuza shingo, nilijikuta natabasam mara baada ya kuona kichwa kizuri cha yule mrembo kikiwa kimelalia bega langu. Sikujua imekuwaje hadi anilalie mana kutoka kwenye siti yake hadi yangu ilikuwa sio rahisi kulaliana, hata hivyo niligundua kuwa yule dada alisahau kufunga mkanda ndio mana alinilalia bila shida. Kuna muda ndege ilipita milimani kisha ilishuka mabondeni, kuna sehemu ilisheki kidogo mara baada ya kukunja kona, ilifanya kama inapiga msele vile! Hapo sasa watu wote tulinesa, yule dada aliniangukia mzima mzima, tena safari hii hakulala begani bali kifuani kwangu, mimi nae nilivyo bwege eti badala ya kumuamsha akae vizuri ndo kwanza nilihisi nimebarikiwa utukufu wa juu mbinguni! Alafu sasa huo mlalo wake ni shida kweli; mara ajigeuze kushoto, mara kulia, alikisumbua kifua changu kutokana na staili zake za kulala, alijiachia akidhani amelala kwenye godoro la sita kwa sita kumbe mwenzie niliumia sana, kifua changu kilipata moto wa maumivu ila nilivunga, nilitamani kumtoa lakini niliogopa ningeonekana sio mwanaume shupavu! Niliamua kujikakamua hivyo hivyo, niligangamala!.
Alafu sijui rubanı alikuwa amekunywa bia au kitu gani, kama una roho nyepesi unaweza ukatamani asimamishe ndege hewani ili ushuke. Kwanza jamaa aliendesha kwa spidi kali, si unajua tena wamama kwa woga? Basi walianza kupiga kelele wakimtaka rubani apunguze mwendo, ni kweli jamaa alipunguza mwendo ila sasa hako kaspidi kake bora hata kobe ana mwendo. Walimwengu walivyo na maneno si walichukia tena, walimuambia rubani aongeze spidi; hapo sasa ni kama walimchokoza vile, alitukunjia kushoto, alitupelekea kulia, alituchukua alituweka waah! Ndani ya ndege abiria wote tulipepesuka, yule dada kwakuwa hakufunga mkanda alikosa balance alidondokea chini ya mapaja yangu alafu ghafla alihisi kichefuchefu, alivuta leso alijibana kitambaa usoni; kwa bahati nzuri hakutapika ila alicheua kidogo tu. Alikaa vizuri kisha alinitazama kwa hasira;
“Kumbe we una roho mbaya hivi?” alinikoromea kwa sauti kali hadi baadhi ya abiria walisikia, walitutazama.
SEHEMU YA 05
“Mimi? Sasa mi roho mbaya niitolee wapi jamani?” Niliongea kwa aibu, nilijishusha ili ugomvi usiwe mkubwa.
“Hukuona kuwa sijafunga mkanda? Kwanini hukunikumbusha? Ulivyo mpumbavu uliniacha nilale kwenye hilo limwili lako I i bay a” “Nisamehe dadangu, niliogopa kukushtua kwakuwa ulilala, ila wakati mwingine ukilala nitakukumbusha ufunge mkanda”
“Umkumbushe nani? kwani nimesema nitalala tena? Au unadhani sitofunga mkanda tena? Siku nyingine uwe unajitambua, ndege sio sawa na hivyo vidaladala ambavyo umevizoea, we unadhani tupo kwenye bajaji hadi ifikie hatua usinikumbushe kuvaa mkanda? Unajua madhara ya kutovaa mkanda? Shenzi” Alinichana makavu, alinishushua mbele za watu, nilidhani watu watanitetea lakini wengi walikuwa upande wa huyo dada waliniambia kuwa nilifanya makosa makubwa.
Niliomba msamaha kwa watu wote. Abiria wengine wote walinisamehe lakini yule dada hakutaka hata kunitazama, alafu anaonekana sijui ana dharau au kiburi; eti ile leso ambayo alicheulia matapishi alinitupia mimi; ilidondokea kwenye suruali yangu, baadhi ya utopolo wake wa mdomoni ulinimwagikia, nilimtazama lakini yeye hakunitazama hata kidogo, kwanza hakujali kabisa, kiukweli sipendagi dharau, alafu isitoshe mimi na yeye tumekutana kwenye hiyo ndege tu, hatujuani wala hatujawahi kusaidiana kwa lolote, hatulishani wala hajawahi kunisaidia kulima mpunga, hata kama nilikosea kumkumbusha kufunga mkanda kwani jukumu la kufunga mkanda ni langu au lake? Sasa kama alisahau hilo ni kosa langu au lake? Ila walimwengu wakiamua kukutafuta la rohoni watakutafuta tu, nilimaindi kweli kweli ila nilipiga moyo kondeboy kisha nilitulia.
Ukirnya uliendelea ndani ya ndege, sikukaa kwa amani, japo kosa lilikuwa dogo lakini nafsi yangu ilinisuta sana, nilitamani masaa yarudi nyuma ili nimkumbushe afunge mkanda, nilitamani muda urudi nyuma ili nimuondoe begani kwangu kisha nimlaze kwenye siti yake, hata hivyo wahenga walisema “Neno ningejua uja baada ya safari”. Kwakuwa wote tulitulia nilijua ugomvi umeisha, nilitamani yule dada arudishe furaha yake ikiwezekana anitazame anisemeshe lakini haikuwa hivyo. Nilikuwa mpole kweli kweli, nilivumilia sana mwisho niliona ni heri nirudishe furaha ambayo niliipoteza, niligeuza shingo nilimtazama, kwakuwa sikumfahamu jina nilishindwa kumuita, nilinyosha mkono nikitaka kumgusa ili anitazame, mkono wangu ulitua kwenye paja lake, yaani ile namgusa tu nilishtuka nimelambwa bonge la kofi, nilikula ngumi ya mbavu, mara nilipondwa mguu wangu, nusura anitwange kichwa ila alinionea huruma; alinipiga kofi la uso ambalo lilitua machoni kwangu; kwa mbali nilimuona Israeli akinichekelea, malaika watoa roho nao walinishangilia, walionekana wakijiandaa kunipokea kijana wao!. Kuna muda akili zilinikaa sawa, mawenge yaliisha, nilimtazama yule dada kwa hasira, nae alinitazama akiwa amevimba, uwezo wa kumpiga ninao, nguvu ninazo lakini huruma tu iliniingia moyoni na kichwani, sasa nikiwa nawaza nimsamehe ghafla alinitwanga kofi la mwisho, kofi la kunishikisha adabu! Wee nikasema we kibibi usinichezee, mi ni mwanaume ujue, sikutaka kumtwanga ngumi ila nilimuweka kofi moja tu la shavu; alitulia hapo hapo, alikauka kabisa, sasa sijui ndo alikufa au ilikuwaje! Niliogopa hadi sio poa, hapo sasa niligundua kuwa ndani ya ndege kuna watu wa usalama; alikuja mwamba flani hivi ambaye alishiba haswa, alimshika yule dada kisha alimgeuza alimkuta akilia kwa uchungu, ghafla yule dada alifungua mkanda kisha aliinuka kwa spidi kali alianza kunikanyaga kwa mateke.
“Dada basi basi basii tulia…Kwanza shida ni nini? Ni muda mrefu nimewaona mnakwaruzana, mna tatizo gani nyie watu?” Yule mlinzi alituuliza kwa upole
“Hili likaka silipendi hata kuliona…lipo kama lishetani, ananishikaje mapaja yangu? Ye kama nani? hata baba na mama yangu hawajawahi kunishika alafu yeye amepata wapi huo ujasiri?”
“Haya msamehe bure, jamani kumbukeni tupo kwenye ndege wala sio gari, tujaribu kuiheshimu hii safari, mtakuja kusababisha ajali” Mlinzi aliongea akiwa anamtazama yule dada
“Amenikera sana..Kwanza ikiwezekana mumshushe mumtupie huko chini akafie huko huko mwanaharamu huyu” “Mwanaharamu mwenyewe, alafu we dada nakuheshimu sana, umeanza kunichokonoa muda mrefu sana, hivi unadhani mi ni mpumbavu kama unavyodhani? Ulianza kunidharau ukisema nimezoea kupanda bajaji, sijui hivi na vile, mara unaniombea nife, kwanini usife wewe ili ukapumzike kwa amani?” Hapo sasa niliamua kujibu mashambulizi
INAENDELEA