CHUKI YA MAMA
Part 3
Mama hakutaka hata kuwasiliana na mimi zaidi ya kuninenea maneno machafu kwa ndugu zake, bahati nzuri mume wangu alipata kazi kwenye hospital kubwa ya rufaa bugando, nikabahatika kubeba mimba nikalea hadi nikajifungua salama mtoto wa kiume, bila mama kufika japo taarifa alikuwa nazo ila nikapanga nikikaa sawa ntaenda nyumbani. Mtoto alifikisha mwaka nikapata ajira lakini nikaendelea na ushonaji wangu.
Tulienda nyumbani wakanipokea nikamuomba msamaha yakaisha wakamuita mwanaume akajitambilisha akatoa ng’ombe 10, bibi hakupewa hata 1 wala wajomba hata sufuria na vitenge hawakupewa hata kina mamdogo waliokuwa wakinibeba mgongoni.
Baada ya mahari mama alikuwa akinihitaji akiwa tu na shida, lakini pia ikitokea nikashindwa kumtimizia shida zake kwa wakati ananizila hata mwaka mzima, watoto wake wakija kwangu wakikaa hata week anaanza kusema ntawatesa wakati mimi sishindi hata nyumbani wala siwapakulii mboga. kila siku kunisema na kunitangaza kwa ndugu zake hadi kufikia hatua ya kusema kama angejua atazaa mtoto asiye na msaada kwake ni bora angeniny0nga kipindi ananizaa.
Imefikia hatua mume wangu akabadilika baada ya kupata kazi ninapohitaji msaada wa kifamilia wa ushauri mama anamwambia mume wangu kwamba eti mimi ni mbaya sana hata yeye ananijua siwezi kuishi na mtu, hivyo nimekosa pa kusemea nimekosa msaada mpaka sasa nimejifunza kuishi kama yatima japokuwa nina wazazi.
NB: Baba yangu mzazi yupo hai lakini mama alikwisha nikataza hata kunionesha ila nlioneshwa na wajomba na alishawahi kuja kunitafta akafichwa na aliposikia naolewa alinibariki na akasema mahari yangu apewe bibi kitu ambacho haikuwezekana.
Naombeni mnishauri, nifanye nini, kazi ninayo nzuri tu, tena kazi mbili, mume ninae na watoto ninao lakini kila nikikumbuka nachukiwa na mama sina nguvu hata za kuendelea, sikatai kwamba mimi sina makosa mimi ni binadamu sijakamilika lakini sina matumaini tena nimekonda sana, nimeugua hadi vidonda vya tumbo nishaurini nifanye nini niishi kama watu wengine ukweni kwangu walikuwa wakinipenda sana ila mama amekwisha niharibia japo na wao wanamshangaa
MWISHO