BOSS NAONA AIBU
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
Chapter 1
“Dada naona unaumia shingo unaweza lala kwenye bega langu ili upate kupunguza maumivu ya shingo yako kaka alieksa pembeni yangu ndani ya gari, aliniambia kwa utaratibu na sauti yenye kujiamini, nilitabasamu kidogo na kumshukuru nikweli nilikua naumia shingo, taratibu nilijilaza kwenye bega lake, bega lilikua na nyama nyingi hivyo sikulalia mifupa, nyimbo ya taratibu iliyokua inapiga ndani ya gari Ilinifanya nipate usingizi mwanana.
Huo ulikua msaada wa pili kutoka kwa kaka huyo kwani, msaada wa kwanza ulikua wa kuniachia siti ya dirishani, safari ya kuelekea dodoma ilikua katika uzuri kwani dereva hakuendesha kwa mwendokasi sana au taratibu sana yaani ilikua wastani, nilikua ndani ya basi la shabiby line full kiyoyozi. Tulipofika Morogoro mjini, gari iliingia kwenye hotel moja, kaka wa pembeni aliniamsha kwa sauti yake ile ile yenye utulivu mwingi na ustaarabu usiohesabika.
“Tupo hotelini neighbor vipi unashuka?” nilimjibu hapana, sikutaka kushuka kwenye hotel hiyo kwani nilijua vyakula vya mahotel mengi ni ghall sana na mimi sikua na pesa mfukoni, ilikua safari ya kavu kavu, muhimu nifike dodoma ili niende kwenye interview, hiyo ilikua interview ya muhimu sana kwenye maisha yangu, ilikua chance ambayo sikutaka kuipoteza kabisa kwani bila kupass hiyo interview nilikua nayaharibu maisha yangu kabisa,
kwani nilipotoka niliambiwa na kaka angu nisirudi nyumbani kwake tena, baada ya kuingia kwenye ugomvi na mkewe, nilipaswa kurudi kijijini kwetu huko Songea, majibu yalipotoka ya interview kufanyika dodoma ndipo kaka aliniuliza anikatie tiketi ya kwenda Songea au anikatie tiketi ya dodoma, nilichagua tiketi ya kwenda dodoma kwenye interview, alidai ni tiketi ndo msaada wake wa mwisho, si akanikatia basi la gharama, sikupendezwa na hiyo hali kwani hakunipa pesa ya kutumia njiani kabisa, alinijibu kama nataka nipande niende kama sitaki nijue pa kwenda, sikua na namna nyingine zaidi ya kupanda hilo gari ambalo nauli yake ilikua imechangamka kidogo, nilikua kwenye safari hiyo yenye hatma ya maisha yangu kwamba nikiipoteza hiyo nafasi ya kupata kazi bhasi nilitakiwa kurudi nyumbani Songea na sikujua nafikaje huko Somgea na mimi na nafsi yangu, sikutaka kabisa kurudi Songea.
Kaka jirani aliomba apite, nilimpisha alishuka chini, baada ya dakika sita alirudi akiwa na vimfuko viwili, alinipatia kimoja na kuniambia “Hii ni kwaajili yako, ni safi na salama usikatae piz sikua na kawaida ya kula chochote nilichopewa na mtu mwingine hasa nisiemfahamu, hiyo ilikua tahadhari ya kuwekewa vitu vibaya ila kwa maneno ya huyu kaka, nilishindwa kukataa nilijikuta napokea tu na kumshukuru, nilipofungua sasa huo mfuko, kulikua na soda ya kopo, sijui alijuaje mimi napenda Pepsi ilikua ya baridiii, nikaiweka mahali pa siti kutazama ndani kulikua na chips kuku, na soseji mbili, mate yalinitoka haswa kwani chakula kilikua kinanukia sana sana, yaani kaka neighbor alipita mule mule, nilitamani kuchekelea sana ila nilihofia labda ataniona wa ajabu flani, hivyo nilitabasamu na kumshukuru, nilianza kula taratibu na huo ndo muda ambao nilipata kumjua, kaka neighbor anaitwa Samson japo yeye alinambia anapenda kuitwa Sam, namimi nikajitambulisha kwamba naitwa Theresia ikimpendeza aniite Tedy, kwa pamoja tulitabasamu na kuendelea kula na kunywa soda zetu
Tulimaliza kula na mazungumzo ya kawaida
yalianza, aliniuliza kama nafika dodoma mjini au
nashukia njiani, nilimjibu kwamba naenda
mpaka dodoma nae aliniambia anafika dodoma,
aliniuliza nakwenda kufanya nini dodoma,
nilimjibu nakwenda kwenye interview ya kazi,
alinipongeza sana na kunambia kuitwa kwenye
Interview tu ni sehemu ya ushindi sana kwani
wanaoomba interview ni wengi sana.
Hapo hapo akaanza kunipa mbinu za kufanya vizuri kwenye Interview sasa hiyo ongea yake na macho yake mazuri alivyokua ananitazama Ilikua balaa mwanzo mwisho, simu yake inapoita akiipokea ule ustaarabu wake kwenye kuongea ulikua wa ngazi za juu sana, niligundua kwamba hakua ananiigizia ule ulikua hali yake ya kawaida.
Kingine ambacho nilitaka kusahau ni kwamba alivaa vizuri sana, tisheti ya form six rangi ya kijivu na suruali yake ya kitambaa vyote vilimkaa vizuri mwilini mwake, kingine ambacho alinikosha zaidi alikua ananukia, utamu wa hiyo perfume sijawahi isikia kabisa nikajua tu atakua kachanganya perfume zaidi ya moja ili kupata utamu huo.
Alinipa mbinu nyingi sana, katika maneno yake yote sikuona majivuno wala kujisifia kama wafanyavo wakaka wengine wakikutana na mdada mzuri kama mimi ambae uzuri wangu hauhitaji microscope kunitambua kwamba mimi ni mzuri by nature, nilimwuliza anakwenda kufanya nini dodoma, alinijibu kwamba ni safari ya kikazi ndo inampeleka huko, dodoma na mimi sikukaa kinyonge nilimpa pongezi zake kwa kuajiriwa, japo nilimuuliza kwanini hajasafiri kwa ndege au treni ya mwendokasi ili awahi haraka.
“Aiseeh nilitamani sana kuvipanda hivyo lakini siku mbili kabla ya safari nilimweleza mama angu juu ya hii safari, aliniuliza nitapanda usafiri gani, nikamjibu ndege akanambia roho yake inakataa kabisa kuniruhusu kupanda ndege labda kitu kibaya kitatokea kwenye hiyo safari, nilimwambia bhasi nitapanda treni hapo tulikubaliana kuna mfanyakazi ambae alitakiwa kunikatia tiketi ya treni akajisahau bhana jana namuulizia kama amekata tiketi anacheki siti za treni ya umeme zote zimejaa, nikakosa siti kwa namna hiyo, nimekuja kwenye basi na safari imekua nzuri sana labda ningesafiri huko nisingekutana na wewe” Sam alifafanua vizuri mpaka nikamwelewa maana kwa hadhi yake ingekua vigumu kusafiri kwa basi wakati usafiri mwingine kama ndege upo.
Kwenye siti ya pembeni yetu kulikua na mdada mwingine ambae alikutwa na shida ya kutapika, alikua amelegea kweli kweli, Sam alifungua kibegi kidogo alichokua nacho, alitoa vidonge kwenye mkebe fulani hivi wa kuhifadhia dawa na kumpa yule dada baada ya muda yule dada alipona kabisa na kumshukuru Sam, kwa Sam niliona kitu kipya kwamba alikua na huruma na moyo wa kusaidia watu bila kujiona, alizidi kunikosha tu.
Baada ya kitambo kidogo gari liliingia kwenye hotel nyingine, aliniuliza kama nashuka, nikamuitikia ndio, nilitaka niende chooni mara moja, tulisimama pamoja ili kushuka tulipofika kwenye ngazi sasa, uyu kaka aisee ni anajari mpaka unajihisi kama malkia,aliomba mkono akanishusha taratibu uku ananitizama kwa makini wakati ananishusha ivi aka….
Chapter 2
Kwanza alinipa mkono na mimi niliupokea, “Taratibu usijechuna ngozi yako Tedy” jamani hayo maneno yalikua yanaupepea moyo wangu, yanaupa barafu mwili wangu, nilijisikia vizuri ajabu nilijihisi kujariwa sana alihakikisha nashuka nikiwa salama, ilibidi mimi nipite upande wa kushoto na yeye kulia, eti ananiambia “Take care na sakafu usije teleza” niliishia kutabasamu tu na kumshukuru kila kitu alichokua anakisema Sam kilikua sahihi zaidi ya neno lenyewe, niliporudi nilimwona alikua kasimama na kaka mmoja muuza midori ile ya watoto, alipomalizana nae alinifuata mkononi alikua na mdori mdogo wa rangi ya karoti na tunda aina ya apple, aliponifikia alinikabidhi.
“Wewe ni kamdori kakubwa na huyu ni mdori kadogo, nimeamua kuwakutanisha marafiki” aliniita mimi mdori mkubwa kwa maana jina langu Tedy ni sawa na mdori, nilishindwa. kujizuia niliruka ruka kwa furaha, nilipenda sana midori na hakuna mwanaume au mwanamke yeyote ambae amewahi nizawadia mdori.
Sam alitejingeneza nafasi ya kipekee moyoni mwangu, tulikumbatiana, tulishikana mikono na kurudi ndani ya gari, safari ilikua fupi sana kwa maongezj yetu mazuri hakukua na dakika hata moja yenye kuchosha wala kuboa, nilikua mwenye furaha sana, nilisahau shida zangu zote kuanzia vichambo vya wifi yangu, maneno mazito ya kuvunja undugu aliyonitamkia kaka angu vyote havikuja kwenye akili yangu, kubwa zaidi alinipa moyo na kunambia nitapita interview ya siku inayofuata.
Tuliingia stendi ya nane nane majira ya saa mbili usiku.
“Unafikia wapi?” aliniuliza baada ya kushuka kwenye gari.
“Kuna rafiki angu mmoja nilisoma nae chuo anaishi kwenye huu mji anakaa makole, japo sipajui alisema atanifuata kwahiyo nikiwasiliana nae nitakwenda huko” “Sawa kuna wamenifuata hapa, nawasubirisha kidogo mpaka huyo rafiki ako afike ndipo tutaondoka wote” nilikubali kwani bado nilihitaji kuendelea kuwa nae karibu, nilipenda ongea yake, stori zake pia, aliagiza maziwa ya moto ili tunywe tukiendelea kumsubiri rafiki angu.
“Nikiwa kwenye huu mji huwa unanikumbusha kumbukumbu nyingi za zamani” Sam alianzisha mazungumzo. “Mmmh zipi hizo?”
“Niliachwa hahahaha alijibu huku akicheka, nami nilicheka, nikamtaka anisimulle zaidi kuhusu kisa chake cha kuachwa, nilifanya hivyo kwakua niliona anacheka hivyo nilikua na uhakika kwamba hakua na maumivu yoyote moyoni zaidi ya kumbukumbu zenye kuchekesha
tu.
“Nikiwa nasoma chuo Udom pale, niliachwa na mdada mmoja mzuri sana, ambae nilimpenda. kwa moyo wangu wote?” “Mzuri kama mimi?” swali liliniponyoka
mdomoni.
“Hapana umemzidi vitu vingi lakini alikua mzuri sana na hata washkaji walinisifia mno kwa kuwa nae na tulipendana kweli sio utani” “Niambie bhasi kilitokea nini mpaka akakutenda “Wabunge bhana, kuna mbunge mmoja alinizidi kete akamtorosha njiwa wangu mwenye rangi nzuri hiyo imenijenga mpaka leo kutokua na msichana naweza sema kama hisia zangu zimeganda kidogo, akili na ufahamu wangu wote nimewekeza kwenye kazi”
“Ooh pole kwa mambo hayo, kiukweli mapenzi yanachanganya sana kama umewekeza kwenye kazi, wewe fanikiwa tu ukiona upo tayari utampenda mtu aliepenya kwenye chekeche lako, mkajenge maisha” nilichangia na mimi. “Sahihi umeongea kitu kizuri unaakili sana huko kwenye interview kesho watafurahi kukutana na mwanamke mwenye ufahamu kama wako, emu vaa hii skafu naona baridi ni kali” Sam alinisifia na kuniwekea skafu yake shingoni mwangu, nilijisikia kajoto joto kwani upepo ulikua unapuliza sio poa.
Nilitoa simu yangu na kumpigia huyo rafiki angu, simu ilipokelewa, nikamuuliza yuko wapi, majibu yake sasa yalinikatisha tamaa sana.
“Samahani sana ndugu yangu, nilikua najiandaa kuja ila kwa bahati mbaya, shemeji ako amekuja gafla kutoka safari, hivyo nimeshindwa kutoka, na swala la wewe kuja kulala huku ni uongo kwani nina chumba kimoja tu fanya utafute mahali pengine pa kufikia, uwe na usiku mwema rafiki angu aliongea maneno hayo yaliyonichoma moyo na kukata simu yake, nilinyong’onyea kiukweli, macho yangu niliyainamisha chini, furaha yote niliyokua nayo ilipotea.
Chapter 3
“Vinyonge havina kawaida ya kutawala dunia, kwanini unajiweka kwenye kundi hilo, unatakiwa kuwa na nguvu na imani utashinda kilal lililogumu kwenye maisha yako, kama utajiweka. dhaifu hakuna atakaetokea kukupa nguvu kwenye hii dunia iliyoachama mdomo ili uingie ikararue kwa meno yake, twende huku najua wapi utakwenda kulala niliyasikia maneno ya matumaini kutoka kwenye kinywa cha Sam, yalinipa nguvu sana na kuamini napaswa kusimama na kupambana na hali ya unyonge iliyokua inanikabili.
Lakini swala la kumfuata mtu ambae ndo tumekutana kwenye gari lilikua na kipengele kidogo, kama atanitoa viungo vya ndani je au atanipeleka huko kwenye madangulo akaniuze nikajikuta najiuliza maswali mengi, Sam alinishtua kwa maneno mengine.
“Najua unachokiwaza, afandee afandeee nakuomba mara moja mkuu” Sam alinishangaza baada ya kumwita askari mmoja aliekua ndani ya kituo cha mabasi, yule askari alitufikia na kutusalimia, Sam alimwomba msamaha kwa kumwita ila alimwambia anashida kidogo.
“Afande naitwa Samson Malidadi, vitambulisho vyangu vyote ni hivyo hapo, nimekutana na dada hapa kwenye basi kidogo amekutana na changamoto ya mahali pa kufikia, nimetamani nimchukue angalau nikamkodishie chumba apate sehemu ya kulala ila amekua na hofu na mimi. Naomba uchukue taarifa zangu hizo muhimu, endapo binti atapotea au baya kumkuta usiku huu, naomba mnitafute mimi mpaka mnipate, naomba nisaidie kwa hilo Sam aliongea maneno ambayo sikuyatarajia, nilijiambiza moyoni kumbe huyu nae kichaa eeeh. Afande alitabasamu na kumuuliza ni hotel gani tunakwenda, alijibu ni Morena hotel.
Alichukua taarifa za Sam pia aliniuliza kama nipo tayari kwa huo msaada, kwa namna Sam alivyojipinjika mpaka kwa polisi, nikaamua nimuamini tu hivyo nilikubali kwamba nitaenda nae, alichukua taarifa zangu pia kisha akatutakia usiku mwema japo alimuonya Sam, iwe ni msaada tu asivuke mipaka ya msaada na kunifanyia unyanyasaji wowote kwani itakua mbaya kwake, Sam alimtoa hofu, japo na mimi nilimuuliza kwanini aliniamini hivyo kama nikitaka kumgeuka na kumshitaki kwa uongo, alijibu tu kwamba hakuna baya litakalomkuta kwani Mungu atamlinda tu, tukacheka na mimi kumtania kwamba yeye ni kama Samson wa kwenye vitabu vitakatifu kwani alikua na imani na mwenye kujiamini sana, tulicheka kwa pamoja.
Tulitoka nje stendi tulitembea mpaka kwenye maegesho ya magari, kulikua na gari tatu nyeusi kalli, sikujua ni gari za aina gani kwani sikua mtaalamu wa magari lakini nilikua na uhakika ni gari nzuri tena zenye gharama kubwa sana, alikuja mdada mmoja akiwa na wanaume wawili wote walivalia suti, mdada alivaa suti nyeupe na wakaka wawili wao walikua na suti nyeusi, walitupokea mabegi, mdada alimkaribisha Sam kwa kingereza chake, ila nilichogundua kwamba Sam alikua na nafasi kubwa kwenye hiyo kampuni kwani walimwita boss tena kwa heshima, tuliingia kwenye gari la katikati, mama angu mzazi sijawahi panda gari zuri kama hilo kwanza siti zake zilikua luxury sana, juu kulikua na vimuli muli ambavyo vilikua kama nyota yaani pananogaje, dereva alijitambulisha na kumkaribisha Sam, hakuishia hapo bali alitumiminia wine na kutupatia. “Usiogope haina kilevi hiyo Sam alinitoa hofu kwani nilikua naitazama tazama sana kabla ya kuiweka kinywani, dereva aliondosha gari tulikwenda mpaka Morena Hotel.
Hotel hiyo nilikua naisikia tu kwa uzuri ila siku hiyo nilifika, tulikaribishwa kwa heshima zote na wahudumu wa Hotel, tulienda sehemu ambayo tuliandaliwa kwaajili ya kupata chakula, meza ilikua ndefu sana, mimi nilikaa upande huu na ule kule alikaa Sam. Meza ilikua na mahotpot mengi hivyo wahudumu wawili walikuja na kutusikiliz watupakulie nini. Sikua na njaa sana hivyo niliomba waniwekee pikau kidogo, nyama rosti, ndizi moja na kuku bhasi, niliona vingenitosha. sana hivyo.
Tulikula huku tukizungumza mambo mengi sana, Sam hakuishiwa stori kabisa na mimi nilijitahidi kumpa sapoti ili stori zinoge zaidi, tulizungumza mpaka saa sita usiku.
Akaniambia nikalale ili niwahi kuamka kuwahi
Interview nilikubali, walifika wahudumu
walitupeleka upande wa vyumba vya VIP, kila
mmoja na chumba chake, tulipungiana mkono
wa kwaheri na mimi kuingia chumbani kwangu.
Humo ndani kilikua chumba kikubwa sana kilikua na eneo la mazungumzo ya faragha kama mngehitaji, bafuni huduma ya maji moto na baridi, Tv, WiFi yaani kulikua na mambo yote mazuri kwenye hotel yenye hadhi ya nyota nyingi.
Niliingia bafuni kuoga nilipotoka nilijiandaa kwa kulala lakini kabla ya kulala niliamua kupitia notes na vitu mbalimbali ambavyo vingenisaidia kwenye interview, nilipojihakikishia niko sawa, nikasali na kujiweka kitandani.
Saa kumi na moja nilishtuka nilioga na kujiandaa, nilimtumia text ya salamu za asubuhi Sam, hakunijibu, nikamtumia nyingine ya kumuaga kwamba naenda interview nayo hakunijibu nilitoka zangu nilichukua boda ikanipeleka mpaka kwenye jengo ambalo tulikua tunafanyia interview.
Saa moja kamili tulikua watu watano kati ya kumi tuliotakiwa kufanyiwa interview tulipelekwa kwenye chumba maalumu cha kusubiri kuitwa, walifanya hivyo ili kuwazuia wengine waliochelewa kufika kwani ratiba ilitutaka saa moja kamili tuwe tumefika.
Tulisubiri kuitwa na ilipofika saa mbili kamili, alikuja mtu kutuita na jina la kwanza kuitwa lilikua jina langu, niliingia humo chumbani.
Kulikua na watu sita jumla ambao walitakiwa kunihoji, sita walikaa pembeni mwa meza yaani huku watatu na huku watatu, CV yangu ilikua kwenye ukuta kwa msaada wa projector na mimi nilikalishwa mbele kama kiongozi wao. Watano sikuwafahamu ila mmoja nilimfahamu kwa sura ni Samson, jirani yangu ambae nilisafiri nae siku iliyopita,nilishangaa nikajikaza nakusikiliza, nisijenikaharibu walijitambulisha wote na Sam alijitambulisha kama mwenyekiti wa Jopo hilo na kazi ilikua kwangu kujielezea na mwisho nipigwe maswali nilimtizama kwanza Sam tukakutanisha macho…
Chapter 4
Nilianza kwa kujitambulisha pale japo lugha ambayo ilitumika ni kingereza pekee.
“Naitwa Theresia Mafue nimemaliza chuo kikuu UDSM nilisomea shahada ya utalii na maliasili mwaka huu” nilijielezea kila kitu pale, nikiwatazama watu wengine walikua wanatikisa kichwa kuonesha kuvutiwa na uwezo wangu wa kujielezea ila kwa Sam hakuonesha chochote, mikausho na ukauzu wa bei kubwa.
Nilipomaliza nilianza kuulizwa maswali, alianza mmoja baada ya mwingine, nilijitahidi kuyajibu vizuri na Mungu alinisaidia kwani maswali yote nilikua na uelewa nayo, ilipofika zamu ya Sam ndipo moto uliwaka, alinipiga swali nilijibu, alipiga lingine nilijibu alinipiga kama matano nilijibu bado aliendelea tu, duuuh nikasema huyu jamaa kaniamulia anafanya kama hanijui vile, bado aliendelea kunikaanga kwa maswali nilipambana hivyo hivyo kumjibu, aliniuliza swali la kumi hilo lilikua gumu sana kulijibu hivyo nilibabaika, hapo hapo akadai eti amemaliza maswali yake, alinieleza kwamba kwa taarifa zaidi kama nimepita nitapigiwa simu.
Niliruhusiwa kutoka nje na mwingine aliitwa kuingia ndani, kiufupi nilijikuta namkasirikia Sam kwani kwa maswali yake mengi yanaweza nifanya nikose kazi hivi hivi na nilikua na uhitaji mkubwa wa kazi.
Nilijiambia nikimwona lazima nimchane, moyo wangu haukua na uwezo wa kuhifadhi mambo niliondoka na kurudi hotelini kwa lengo la kuchukua vitu vyangu nitafute uelekeo wa kwenda, nilipofika mapokezi, niliongea na yule dada wa hapo kwamba nataka kutoa vitu anipe funguo, dada wa mapokezi alishangaa baada ya kusoma jina langu kwenye kitabu cha kumbukumbu.
“Umeghaili kukaa siku tatu tena, mbona chumba kimelipiwa kwa siku tatu” namimi nilishangazwa kwa taarifa hiyo kwani sikujua kabla, nikapotezea kwamba sikutaka kuchukua vitu vyote ni vitu vichache tu, nilichukua funguo na kuingia ndani chumbani kwangu.
Simu ya chumbani ilianza kuita, walikua ni wahudumu waliniuliza juu ya breakfast kwamba nitanywea chumbani wanipelekee au nistashuka chini, nilichagua waniletee huko huko chumbani, baada ya dakika tano mlango wa chumba uligongwa, nilifungua aliingia mhudumu akiwa na chal ambayo nilimwagiza niliwekewa mezani na yeye kutoka, nilikunywa chai hiyo japo mawazo ya kukosa kazi na ugaidi alionitendea Sam bado uliendelea kuzunguka kichwani mwangu, kwani sikutarajia kama atanifanyia. ukandamizaji namna ile.
“Kweli binadamu wanajua kubadilika badilika, sitomwamini yeyote kuanzia leo” niliongea maneno hayo na kujitupa kitandani, usingizi ulinichukua, kuita kwa simu ndiko kuliniamsha, nilishtuka na kuitazama mpigaji alikua Sam.
Niliipokea japo sikua na shangwe kiivyo, si unajua tena kisirani cha kinadada.
“Boss wangu shuka chini tupate lunch, nimemiss kweli kukuona, sijakuona siku nzima ya leo Sam aliongea na kuniachia nafasi na mimi niongee kwanza nilishusha pumzi ndefu kisha nikamwambia.
“Sawa na shuka tayari ilikua saa nane mchana nilivaa traki suti rangi ya pink ilinikaa mwilini, nilijipanga maneno gani ya kumwambia Ili kumwonesha kwamba nilichukizwa na matendo yake wakati wa interview.
Nilishuka chini kama kawaida alinipokea kwa kunishika mkono nilikubali alinivutia kiti na kuniomba nikae, bado nilikua na manuno mengi.
Wahudumu walifika kama kawaida walitupakulia chakula pale.
“Najua chakula hakitalika kwa amani hapa nakuona mrembo leo umenuna mwenyewe haya niambie kila kitu kilichokukwaza ukitamani kunipiga wee sogea unipige huu mwili mali yako” nilimwangalia nikajisemea umemkabidhi fisi bucha nilisimama na kumfuata ili nimfanye kitu mbaya ambayo hajawahi kufanywa.
Chapter 5
kwanza nilianza kwa kumfinya shavu kidogo tu
kisha nilimpiga kakofi kadogo ka bega. “Mamaaa bega langu limevunjika Sam alianza kulalamika baada ya kumpiga begani.
“Heee hako kakofi umeumia jamani, bhasi pole”
nilijikuta naanza kumbeleza kama mtoto eti, baada ya dakika kadhaa ndipo ananambia. kwamba amepona.
“Muone madeko tu kama last born vile nilimwambia huku nikitabasamu, nilirudi kwenye kiti changu, minuno yote ikiwa imekwisha kabisa.
“Umenipiga tayari niambie ulikasirikia nini my neighbor “Ulichonifanyia kwenye Interview unazani ni
kizuri sasa? “Hahahaha, mimi nikiwa kazini huwa sina
masikhara hata kidogo, niamini mimi hata pale angekaa mama angu alienizaa ningemwuliza maswali vile vile, sitaki kampuni ipate hasara hivyo lazima lajiri watu best tu, kama ni mtu wa kubahatisha huwezi fanya kazi kwetu”
“Mmmh” niliguna kidogo kwani manenl aliyoniambia yalikua mazito.
“Mbona unaguna vipi?”
“Kwahiyo matokeo yatakuaje huko maana.
nilivyokua najibu kwa kitete vile, nidokezee. kidogo? Nilijaribu kumchimba ili nijue kilichoendelea kama nimepita au sijapita
“Hilo ni swali gumu sana kwangu, sijui chochote kama unajiamini ulifanya vizuri, bhasi nafasi itakua yako utapata kazi tu, muhimu endelea. kumwomba Mungu Sam alikaza nilijua kwamba hataki kutoa siri za kampuni, kiutendaji alifanya
vizuri ila kiubinadamu nilimwona ananifungia vioo.
Tuliendelea kula hapo, pia aliniuliza nitakwenda wapi baada ya hapo nilimjibu Japo ilinichukua muda kujibu, sikutaka ajue matatizo yangu akati ndo kwanza tu tumekutana, atahisi nachukulia faida kisa nimeona anapesa, nilijibu naenda songea ama dar sina uhakika vizuri kati ya hizo sehemu mbili, nitaenda wapi,ila kufikia kesho nitakuwa nishapata jibu sahihi wapi niende japo moyoni nilitamani nirudi dar ila sikua na mahali
pa kwenda kuishi, Sam alinitazama akaniuliza
“mbona ni kama kuna jambo unanificha? Kuwa
huru huenda tukasaidiana hata kimawazo, lakini
sikuwa tayari kuongea chochote, Sam.
aliniomba, kwanza nikae nae dodoma kwa siku
mbili nyingine mpaka atakapomaliza kikao ndipo
“nakuomba sana usikae tafadhari sina mtu wakuongea nae nakuomba siku mbili tu, kisha tuondoke pamoja kama ni songea utaenda kupandia gari dar nakuomba kwakua nilikua na shida nilikuwa bado sijajipanga nilikubali ili na mimi nikutwe natafuta namna ya kufika kwetu ama pesa ya kupanga room ata ya mwezi mmoja wakati huo nasubili matokeo huenda nikapita, kama nitafeli nitauza simu yangu niende songea nilijiwazia hivyo, tulikaa siku tatu jumla dodoma tukiwa Morena hotel na siku ya kuondoka, tulipanda ndege mpaka Dar. Nilimshukuru Mungu make sikuwa hata napesa ya kutosha nilimpigia simu rafiki yangu mmoja. tulisoma nae alikuwa kanitumia nauli tu ya dodoma to dar, nilivyopewa lift nilifurahi mno moyoni, nikaona ni save ile nauli itumike
kunisaidia kwa yaliyobakia…
Tuliposhuka uwanja wa ndege, Sam aliniomba. kama inawezekana niende nae kwake. nilimtizama nakukataa niliona sio sawa ata
kama ni msaada mmh alikua amenisaidia vitu vingi sana hivyo sikutaka kuendelea kuwa mzigo
hivyo nilimwambia ninasehemu ya kufikia asijari, ila ukweli nilikua nao moyoni, alinikubalia alinipa laki nitumie kupanda taksi nilimshukuru, “jamani asante haikuwa na haja ya nauli nashukuru” nilishukuru…
Tuliagana na yeye kuondoka na gari zuri lililomfuata hapo, nilisogea sogea kwa kupanda daladala niliutafuta mtaa ambao nitapata room ya bei nafuu ili angalau niweze kupitisha usiku huo
Nilipata chumba cha elfu ishirini, nilikubali na kulipia akili ambayo niliipiga ni kwamba kesho. niuze simu kubwa ili nipate pesa kidogo ya kupanga chumba hata nikilala chini sio mbaya. halafu pesa kidogo ninunue kisimu kidogo ili niweze kupata mawasiliano yale muhimu tu hasa nikisubiri majibu ya interview niliyoifanya.
Nilienda kuoga niliporudi nikitazama simu yangu
haikua na jumbe yoyote ile, nilijiweka sawa. kwaajili ya kulala, nilisali kabla ya kulala. nilipokea simu, ilisikika sauti ya kike nyororo yenye kuvutia sana.
“Naitwa Saraphina nipo chini ya kampuni ya Utalii ni fahari yetu, nazungumza na Theresia Mafue?” nilijibu “Ndio karibu sana’ Saraphina aliendelea kuongea..
“Ulifanya Interview na umechaguliwa kujiunga na kampuni yetu hongera sana, unatakiwa kuripoti kesho asubuhi saa mbili kamili, ofisi zetu zipo posta Saraphina aliongea maneno matamu zaidi ya asalı, niliruka ruka na kumwambia
kwamba nitafika bila kukosa.
Nilipiga magoti na kumshukuru Mungu, nilimtumia meseji Sam, nilijua nae atafurahi ila aliishia kunipongeza na kuniambia nilale Ili
niwahi kuamka kwenda kazini, niliamka saa kumi na moja alfajiri kama kawaida nilianza na kumshukuru Mungu kwanza, ndipo nikaanza kujiandaa vizuri, nilitoka na kuingia kwenye madaladala ili nielekee zilipo ofisi za hiyo. kampuni, saa moja kasoro kumi nilikua getini, nilifurahi sana kwani nilikua ndani ya muda.
Nilimkuta dada wa usafi pale, tulizungumza. mambo mbalimbali tulijikuta tuna stori nyingi sana kwani hakua mashauzi.. Mpaka saa mbili kamili asilimia kubwa ya wafanyakazi walikua wamefika akiwepo Sam, nilimkaushia kama hatujuani vile.
Nilitambulishwa ofisini na Sam ndie boss wa ofisi hiyo ambayo ilikua na wafanyakazi nane pamoja na mimi. Iliingia taarifa nyingine kwamba kuna ndege ya watalii kutoka uholanzi ambao walitaka kutalii kwa kwenda mbuga ya Serengeti.
“Ofisi nzima tutakwenda Serengeti pamoja na hao watalii, ikiwa sehemu ya kurefresh pamoja. na kumpokea mfanyakazi mpya Theresia, kila mmoja alifurahi sana na kupiga makofi, upande wa Sam kuna namna akawa anawaza sana akiwa peke yake, kuna muda anayazuia mawazo yake yatulie, kwa sasa anahitaji kufanya kazi tu siku iliyofuata tulipanda ndege pamoja na watalii hao ishirini na tano mpaka Mwanza, tukachukua basi maalumu likatupeleka mpaka mkoa wa Mara, wilaya ya Serengeti.
Tulilala siku hiyo kwenye hotel za mbuga na siku. iliyofuata tulizunguka sana maeneo ya mbugani,
usiku tulikua kwenye mahema yetu nje tulikoka moto, ngoma za asili zillimbwa, na michezo mbali mbali iliendelea pia alikuwepo mwandishi maarufu sana Doctor Hisia akisimulia simulizi
kwa lugha ya kingereza, baadae ulianza kupigwa. muziki wa taratibu walicheza watu wawili wawili wazungu hawakua nyuma..
Sam alinisogelea na kuomba kucheza na mimi,
sikuwa na hiyana nilikubali, lakini kila muda unavyozidi kwenda nahisi kabisa pumzi yake inaongezeka na anapumua kwa kasi, nikajikuta nashtuka ila nikajipa moyo ni Boss, niache kuwaza ujinga, lakini aliendelea, na hali ikazidi sasa akajikuta kanikama ziro distance yani kiasi kwamba siwezi hata kujisogeza, watu walikuwa bize hivyo hakuna aliyeshtukia lolote, nilihisi huenda ndo mambo ya matajiri, na uzungu mwingi, nikajikaza cha ajabu nikashangaa mwamba analeta adi mdomo, sljakaa sawa nashtuka tayari koo langu linakaushwa mmh apa sasa nikahisi, nikicheza naliwa kama utani, nilitaka kujitoa kwa nguvu ila kabla ata sijajitoa nikashtuka……
Inaendelea