UTAJIRI WA MAJINI ULIVYOITESA FAMILIA
PART: 01
Ilikuwa majira ya jioni huku kwa mbali jua likiwa linaishiria, ndipo Munduri mkazi wa mkoa wa Iringa kabila la mkinga, alipowasili nyumbani kwa Dr. Isack Majini.
Mganga maarufu ambaye inasemekana anasafisha nyota kutoka kwenye umaskini kwenda utajiri.
Baada ya kufika maeneo hayo, alishangaa kwani nyumba yake ilikuwa imezungukwa na majani marefu huku nyumba yenyewe ikiwa imeezekwa kwa nyasi .
Wakati anazidi kushangaa, Dr . Isack Majini, alimuna Mundiri ndipo alipomkaribisha.
“Karibu ndani”..
“Asante…” Mundiri aliingia kisha akakaribishwa kwenye ngozi ya chui.
Aliogopa kidogo kutokana na mandhari ya humo ndani kwani nyumba nzima ilikuwa imejaa mikia y wanyama pamoja na matunguli ya hapa na pale.
“Karibu tena..jisikie upo nyumbani..”
“Asante….”
“Shida yako ndo hii ninayoiona au unashida nyingine?” Dr. Majini alimuuliza.
“Hee umejuaje!?” Mundiri aliuliza kwa mshangao.
“Nina uwezo mkubwa sana na tatizo linalokusumbua ni nyota. Nyota yako imechukuliwa kabisa…”
“Asante nahisi utanisadia. Nilikuwa nimejiriwa serikalini lakini ulipokuja msako wa vyeti feki, nikafukuzwa. Badae nikapata kazi kwenye kampuni ya ASAS lakini sikumaliza hata wiki nikawa nimefukuzwa. Sikuishia hapo nimejaribu kila biashara lakini zimefeli mpaka sasa hivi mtaji umeisha, sina kazi na familia inanitegemea” Mundiri aliongea kwa uchungu mkubwa.
“Nimeshaona..nyota yako yote imechukuliwa hivyo chochote ukifanyacho hakiwezi kufanikiwa. Kila mtu huwa ana nyota yake mfano wewe nyota yako ni kali sana kwenye biashara ndo maana imechukuliwa na kuuzwa..”
“Hee! Kwani inakuwaga wapi na inachukuliwaje?”
“Huwa inakaa kwenye paji la uso na huchukuliwa na wachawi au watu wenye nguvu pindi anapokutizama kwenye uso wako…”
“Asante sana Dr. Majini sasa nitairudishaje?”
“Ni kawaida itarudi bila shida yoyote maana hapa ni tiba ya kila kitu…”
“Asante nitakushukuru sana…”
Baada ya mazungumzo hayo, Dr. Majini aliweka maji kwenye karai kisha akanyunyuzia dawa na baada ya hapo aliamuinamisha Mundiri na kuanza kumpakaa dawa usoni.
Baada ya dakika kama 5 hivi, alimfunika kwenye blanketi nene huku kwa ndani kukiwa na moshi kutoka kwenye chetezo.
Mwili mzima lilimtoka jasho ndipo alipomfunua.
“Sasa hapa hatua ya kwanza ambayo ni kuondoa mikosi imekamilika. Hatua inayofuata ni kurejesha nyota yako. Hapa kidogo inatakiwa ujasiri maana mwenye nayo ananguvu kweli…”
“Mi niko tayari kwa lolote kikubwa nipate pesa maana sina amani, nimekonda mpaka nyumbani naona aibu kurudi mapema..”
“Sawa . Kwa hatua hii ya kwanza, unatakiwa kuchangia chakula cha majini chenye thamani ya sh. Laki 1 na ukisharejeshewa nyota yako, utalipia milioni 1 “
Mundiri ambaye alikuwa na kiasi cha laki na 20 mfukoni, alichomoa laki 1 kisha akaziweka kwenye ungo uliokuwa mbele yake.
” Hapo tunaenda sawa…”Dr. Majini aliongea.
“Asante..” Mundiri alishukuru
“Umeoa?” Alimuuliza.
” Ndiyo…”
” Mke wako anaitwa nani?”
” Anaitwa Suzy..”
” Mna watoto?”
” Ndiyo wawili mmoja anaitwa Aderck na mwingine Ivona..”
” Sawa una wazazi?”
” Hapana wazazi wangu wameshatangulia mbele ya haki isipokuwa kabakia bibi tu..”
” Bibi ana miaka kama mingapi?”
” Anafikisha miaka 85 mwaka huu..”
” Sawa. Upo tayari kufanya maamuzi magumu?” Alimuuliza.
” Maamuzi magumu yapi?”
” Yoyote ntakayo kwambia…”
” Ndiyo. ” Mundiri alijibu kwa wasiwasi.
” Kuwa huru hapa nipo narudisha nyota yako kama hauwezi sema..”
” Niko tayari …”
” Ayaa inamisha kichwa chako kwenye maji haya…”
Mundiri aliinamisha kichwa chake kwenye maji kisha akaanza kupepewa na mkia wa sungura kama ishara ya kula kiapo.
” Sasa zoezi limekamilika. Nakupa dawa hii hakikisha unafanyia kazi mda huuhuu bila kupuuzia.” Alimpatia dawa..
” Afu naifanyia nini?”
” Hii dawa inatakiwa umpake mkeo sehemu za siri wakati mmelala usiku na baada ya hapo utaona mabadiliko …”
“Sawa nipo tayari kwa lolote Dr. Kikubwa nirudishe nyota yangu ..”
” Sawa . Kitu kingine, wakati unarudi nyumbani, usigeuke nyuma wala pembeni. Nyoosha moja kwa moja na usiogee na watu utakaokutana nao njiani.”
” Sawa …”
Mundiri alikabidhiwa dawa hiyo iliyokuwa imefungwa kwenye kimfuko cheusi ikiwa kwenye mfumo wa ungaunga hivi.
Moyo wake kwa mbali ulianza kujawa na furaha hata kabla ya nyota yake kurejeshwa .
Mnamo mida ya saa nne za usiku, aliwasiri nyumbani kwake kisha mkewe ( Suzy) akamkaribisha.
Alimtengea chakula ambacho kilikuwa na mboga za majani pamoja na ugali wa mahindi uliokuwa umepoa kidogo.
Alikula tonge mbili kisha hamu ikamuishia .
Alitegeshea mke wake katoka kisha akamwaga chakula hicho.
Baada ya chakula, akili yake yote ilihamia kutekeleza masharti aliyoambiwa na Dr. Majini ndipo alipomwambia mkewe,
“Baby tukapumzike…”
” Mhh leo naota asee yaani leo umeniita baby..”..
” Hahah yaani leo nina….”
” Aya my switie ..love you…”
Harakaharaka, mlango ulifungwa kisha wakazama chumbani.
Mundiri alianza kuvua nguo zake kisha akabakiza nguo ya ndani tu huku mkono wa kushoto akiwa ameshikilia dawa.
” Karibu tulale .” Mundiri alimvuta Suzy na kuwa zero distance.
Wakati yote yanafanyika, akili ya Mundiri ilikuwa ni kuweka dawa kwenye sehemu za Suzy huku Suzy naye akiwa hajui chochote.
Baada ya mda, wote walivua nguo ndipo Mundiri aliponyoosha mkono wake wa kushoto taratibu naku …
JE MUNDIRI ALIFANIKIWA KUMUWEKEA DAWA?
JE HIYO DAWA INA NINI NDANI YAKE?
JE ILIKUWAJE?
PART: 02
Akiwa hajui ile dawa ipoje na ina kazi gani, alinyoosha mkono wake wa kushoto huku mwingine ukiwa unampetipeti kifuani mpaka sehemu husika na kunyunyuzia dawa hiyo.
Suzy kwa hali aliyokuwa nayo, hakuweza kugungua chochote kile.
Baada ya kuwa amemaliza kufanya hivo, Mundiri alisubiria kuona matokeo lakini hakuona chochote kile.
Walilala mpaka asubuhi bila kutokea chochote.
Waliamka salama kisha Suzy akamnyonyesha mwanawe Ivona na baada ya hapo aliendelea na shughuli za usafi.
Wakati Mundiri yupo ndani anawaza na kuwazua, alisikia kelele kali yenye kuashiria maumivu makali kutoka kwa mke wake Suzy ndipo alipotoka ndani haraka.
“Mama…mama….” Suzy alipiga kelele mara baada ya kung’atwa na joka kubwa kwenye mguu wake wa kushoto na kukimbilia kwenye bustani ya maua iliyokuwa hapo.
Joka hilo lilikuwa na sumu ya ajabu sana kiasi kwamba ndani ya mda mfupi, Suzy alivimba mwili mzima hususani usoni.
Mundiri alishangaa sana ndipo kwa haraka alipomfunga na kipande cha kanga mguuni ili sumu isipande.
Mda si mrefu, majirani waliwasiri nyumbani hapo kisha wakaanza kumsaka joka huyo lakini waliambulia patupu.
Hali ya Suzy ilizidi kuzorota huku mwanawe Ivona ambaye alikuwa bado ananyonya akitamani kunyonyonya lakini walimshika ili asije patwa na sumu.
Walimkimbiza hospitalini kwa haraka sana huku mwili wake ukiwa umelegea tepetepe.
Baada ya kumfikisha , Daktari aliamuangalia kisha akawambia hawana uwezo wa kumtibu mpaka hospitali ya wilaya .
Walimpandisha kwenye Ambulance na kumkimbiza hospitalini hapo huku mwili wake mzima ukiwa umevimba na kuota upele kama fenesi.
Baada ya kumfikisha, moja kwa moja walimlaza kwenye chumba cha wagonjwa mahututi kwani kwa wakati huo hakuwa na uwezo hata wakujitingisha.
Taharuki ilitanda gafla mpaka majirani wote wakabaki midomo wazi huku wakisubiria taarifa ya mwisho.
Wakati hali yake inazidi kuwa mbaya sana, watu walishangaa kuona mtoto Ivona akidai nyonyo kutoka kwa mama yake na kila walipojaribu kumpatia maziwa ya kopo, alikataa.
Walimbembeleza huku na kule lakini wapi mpaka pale walipobahatika kuona kasinzia.
Mundiri akiwa hospitalini hapo, gafla alipigiwa simu ndipo alipotoka ndani na kuipokea kwa nje..
“Heloo..nani mwenzangu?” Mundiri aliuliza.
“‘Ni mimi Dr. Majini….”
” Ohhh sawa boss…habari”
“‘Nataka kukwambia kuwa leo hii jioni unatakiwa ulete dawa ya mke wako ili uweze kupanda daraja la kuelekea kupata nyota yako…”
“‘Damu nitaipata wapi wakati kalazwa hospitalini hapa?”
“‘Ninajua kila kitu na Jini langu linakwenda kumtoa roho ila hakikisha unatunza siri…”
“Hee! Sasa mkimtoa roho mwanangu atanyonya wapi?”
“‘Tulikubaliana na hii ni hatua ya awali. Kurejesha nyota iliyoibwa sio suala dogo wala kuwa mtu maarufu na tajiri sio suala dogo. Kwa hapa jini langu litatekeleza kiapo chako kama ulivyooapa hivo usiogope kwa kitakachotokea..”
” Sawa nimekuelewa..”
Mundiri alikata simu huku akiwa anatetemeka mwili mzima hali iliyowatisha watu waliokuwa hapo.
Huko ICU Suzy alianza kupiga kelele huku akirusha miguu kila sehemu..
“Niachee!..niachee!. Niachee!”
“Hee! Kapata nguvu za kuongea?” Wahudumu waliulizana.
“‘Ni kawaida kwa mgonjwa anayetaka kukata roho kufanya hivi…” mhudumu mmoja aliongea.
Walimfunga miguu na mikono ili asijitingishe lakini alikuwa na nguvu ya ajabu kweli.
Baada ya mda alitulia kabisa. Mda ulizidi kutaradadi mpaka mida ya jioni lakini hawakupata mrejesho wowote .
Mundiri alipigiwa simu na Dr. Majini kwa mara nyingine,,
“-Helo…mda huu anatakiwa jogoo mweupe asiye na doa lolote afu mlete kabla ya saa nne za usiku..”
“Hee! nisipompata itakuwaje?”
“‘Utaweka maisha yako katika hatari kubwa sana…”
“‘Sawa ngoja niage nikamfate…”
Mundiri aliaga hospitalini hapo kisha akaanza msako wa kumtafuta jogoo mweupe .
Alizungukia kama nyumba 20 hivi bila mafanikio huku mmoja akiwa na nyoja moja lilikokuwa jekundu .
Hakukata tamaa mpaka hatimaye alifanikiwa kumpata.
Bila kuchelewa, alimpeleka kwa Dr. Majini .
Mnamo mida ya sas 3 za usiku, aliwasiri na kuingia ndani.
Dr .Majini alimkagua jogoo huyo na kujiridhisha kisha akamwambia,
“Mkeo tunaenda kumtoa kafara kwa kumwaga damu ya jogoo huyu na unatakiwa kunywa damu pamoja na kujipaka kwenye paji la uso. Uko tayari?”
“‘Ndiyo niko tayari…”
“Tutakapoanza kumchinja jogoo huyu, kuna sauti kama ya mke wako itatokea huku akipiga kelele ya maumivu lakini usiogope ni kawaida tu..”
“Sawa” Mundiri aliitikia huku moyoni akiwa anatetemeka kweli.
Dr. Majini alisogeza karai kisha akampatia Mundiri kisu ili aweze kumchinja jogoo huyo.
Bila hiyana yoyote, Mundiri alishika kisu na kukiweka kwenye shingo la jogoo ndipo aliposhutushwa na sauti hii,
“‘Usiniue mme wangu!…usiniue!” Mundiri alibaki ameganda na kisu mkononi kwa mshangao mkubwa….
JE ALIWEZA KUMCHINJA JOGOO HUYO?
JE SUZY ALIPONA?
INAENDELEA……….