USIROGWE UKAONDOKA NYUMBANI NA KWENDA USIPOPAJUA KWA KIGEZO CHA KUTAFUTA MAISHA
Hadithi Ya Kweli
SEHEMU YA KWANZA
Nilizaliwa mwishoni mwa miaka ya themanini katika kijiji cha chabutwa wilaya ya Sikonge mkoa wa Tabora, nilifanikiwa kupata elimu yangu ya msingi hapo kijijini, shuleni nilikuwa vizuri sana, si walimu tu bali hata wanafunzi walinipenda. Familia yetu ilikuwa ya maisha ya kawaida sana kwani baba na mama wote ni wakulima wadogo wadogo tu, kwetu tulizaliwa wawili tu mimi na mdogo wangu wa kiume.
Basi baada ya kumaliza shule ya msingi nilichaguliwa kujiunga na shule ya skondari Chabutwa iliyopo pale katani. Kwa vile nilikuwa John kisomo basi maisha ya shule hayakuwa mabaya ki ufaulu, Paka namaliza form four nilikuwa naongoza pale shuleni, Baba yangu alipenda kunihusia kuwa nisipende kujionesha kwa watu kuwa nina akili maana si wote wanapenda kuona watoto wao hawafanyi vizuri alafu watoto wa wengine wanafanya vizuri
Basi nilijitahidi sana kufata ushauri wa mzee ingawa kama unavyojua haya mambo hayafichiki, Kata nzima ilikuwa inanifahamu, kwenye vikao vya shule ndo usiseme maana niligeuzwa sample space (Sehemu ya wengine kujifunzia).
Basi nikamaliza four pale na Mungu si Athumani nikafaulu vizuri na kuchaguliwa kujiunga na shule ya Pugu Secondary kwa ajili ya five na six. Mzee wangu alifurahi sana si kwa sababu ya kufaulu tu bali nilichaguliwa shule ya mbali na pale nyumbani maana mzee alikuwa hana amani kabisa na majirani wa pale katani
Basi bana, siku ya siku nikatimba shule ya baba wa taifa, Askwambie mtu nilikutana na life la kibabe sjawahi kuona
Picha linaanza shule haina maji, Maji utajua pa kuyapata, kama utaenda mtaani kununua utajua mwenyewe, Ukitaka uzame pondi ( Huko bondeni kuna visima wanatumia wanakijiji ila maji yake yana magadi na fangasi wa kutosha)
Kufupisha story sitaelezea sana life la Pugu, ila kiukweli lilikuwa la kiume, Miongoni mwa vitu sitavisahau ni bweni letu la Mapinduzi 3 ambalo ndo lilikuwa linaaminika bweni la watu wakorofi shule nzima, pia nikiwa bado mgeni nilikaribishwa kwa kupigwa nguo zangu zote nikabaki na nliizokuwa nimevaa tu, yaani siku hiyo nimetoka pondi nimefua nguo zangu nikaanika kwenye ukoka, nikaondoka kwenda kutembea majohe, kurudi jioni nakuta ukoka unanikodolea tu hakuna nguo yaani Hadi boxer walichukua wahuni wale.
Kingine sitasahau ni tukiwa karibu kumaliza six, tumebakiza paper ya practical ya chemistry, siku hiyo ilikuwa jioni ki giza ndo kinaingia, nimetoka kupiga zangu nguna maharage, najisogeza taratibu naelekea kwenye kipindi cha dini, Mara ghafla naona watu wanakuja wengi wanakimbilia eneo la shule, Wa baba, wa mama wengine wana watoto, nikajiuliza kimoyomoyo haya maandamano ya nini tena, nikiwa bado nashangaa ghafla nikaona kitu hicho ndo kilifanya nione hii issue ni serious, nikamwona teacher wetu wa darasa nae anakuja mbio, tena mbaya zaidi ana kitambi sasa akikimbia balaa, na alikuwa na spidi maana ilikuwa kawaida yake kila asubuhi anatukimbiza ambao hatuendi assemble.
Duuh, nlipoona hivyo na mimi nikaliunga tukaanza kukimbia, kuna sehemu wanafunzi wanapenda kuangalia tv nikakuta nao wamesepa wameacha tv pale, Daaah sasa wote tunakimbia halafu hatujui tunakimbia nini, Sasa wakati naendelea kukimbia nikakutana na mlemavu mmoja yupo kwenye kiti chake cha matairi (Maana ile shule ina wanafunzi walemavu pia),. Sasa hana mtu wa kumsukuma na kile kiti chake, kila mtu anaokoa nafsi yake, basi huruma ikaniiingia nikaanza kunsukuma huku tunakimbia, ebwanaeeh tumekimbia mwisho nikaona hapa nafeli, maana watu wanazidi kukimbia kuelekea bondeni huko alafu kelele zimekuwa nyingi, nikaona usintanie nikamwacha yule mlemavu nikaanza kukimbia mwenyewe.
Nikakimbia hatimae nikafika pondi, pale kidogo nikakuta watu wamerundikana kidogo,wanaulizana ni nini ila hakuna anaejua, ila juu angani anga limegeuka rangi, limekuwa jekunduuu kama vile jua lataka kushuka, alafu kelele kama vile watu wanapiga mabati huko angani au kama vile msitu unaungua sasa zile kelele za miti, daah hapo nikajua ndo mwisho wa dunia huu, wakati nageuka huku na kule mara namwona yule mlemavu ila saivi hayupo kwenye kiti bali anatambaa chini, nikajiuliza huyu kakimbia au kabebwa? Nikabaki nimestaajabu ila nikajichanganya asije kuniona akasema huyu broo ana roho mbaya, maana jinsi anga lilivyo jekundu yaani Hadi watu mna onana kabisa
Basi bana kelele zikazidi, watu woga ukaongezeka basi mbio zikaanza , tukapanda juu tukatokea Barbara kubwa ya pugu kajiungeni, Barabara imejaa watu wanakimbia, magari ndo usiseme, basi tukawa tunakimbia kelele zikizidi ukitazama juu unaona kama kimondo cha moto kinakuja hivyo unalala chini, kikipita unaamka tena unaaza mbio, Basi tukafika njia panda ya kisarawe na chanika, tukala kulia kuelekea kisarawe, mbio mbio unafika mahali unakutana na mdada anakimbia kanga inaanguka anabaki na chupi lakini hana muda wa kuokota kanga,ni kukimbia tu, mi pia sikuwa hata na hamu ya kutazama hayo mambo, maana unakimbia ukilala chini unasali ili likimondo lipite, basi ni kukimbia na kusali tu
Basi mara tukafika shule ya secondary Minaki , kulikuwa na wanafunzi pale nao wakaungana na sisi kukimbia, tukakimbia mara tukatoboa kisarawe,hapo ni usiku hata siijui saa ngapi, Basi pale kisarawe tukakuta watu wengi kinyama, yaanii pale ndo ikawa kama makutanio, watu wanaulizana ni nini,lakani hakuna anaejua dhahiri ni kitu gani kimetokea, Basi wakati tunashangaa pale mara ule mwanga na yale makelele yakawa takekaribia tena, watu wakaanza kuondoka kuendelea mbele,
Daah kwa jinsi nlivyokimbia na miguu ilivyokuwa inauma nikasema mi skimbii tena, kama kufa nife tu, basi nikaona cruzer moja imejaza watu nyuma inaondoka, nikaikimbilia nikaidaka, nikadandia yenyewe ikachanganya, sasa wakati natafuta sehemu ya kuweka mguu nikakosa, mikono ikachoka kubembea nikarudisha miguu kwenye lami, acha niburuzwe, nikaskia watu wanasema umeuaaaa, gari ikasepa nikaamka kujiangalia, nilikuwa nimevaa jinsi lakini ililiwa na lami paka ikakutwa Ngozi, nilichubuka vibaya, damu zinatoka balaa vidole vinatoa damu, ndala Sina maana zulikatika toka huko nikiwa nakimbia
Basi, mara nikaona cruiser moja imechorwa msalaba mwekundu, watu wanaikimbilia, na mimi nikazama, sasa wakati nazama kuna mama mmoja alikuwa mbele yangu, nikamvuta nyuma mi nikazama ndani, kumbe ni mke wa yule dereva anae endesha lile gari
SEHEMU YA PILI
Basi yule Mama akapiga kelele, mme wangu wanatuvuta tusiingie, yule dereva akasema, sasa we ulitaka wapande nini, hebu panda huko twenende, basi kimoyo nikajisemea yes dereva si ndo huyu, basi chuma ikawaka, tukaendaaa weee, hapo sasa ndo nikaanza kuskia maumivu ya mguu na vidole, nilikuwa sijayaskia, kujishishika naona majimaji nikajua hii damu, banaee tutajua kesho maadam nimepata usafiri haina noma, nikiwa kwenye lindi la mawazo ya kilichotokea, nawaza bwenini nimetoka hata tranka langu la maji sjafunga, maana pale shule kitu cha thamani kuliko vyote ni maji, basi bana nikiwa kwenye mawazo mazito mara naskia mtu ananigusa, oya umepona, kucheki ni mshkaji wangu Abdul Kisoda tunaishi nae mapinduzi 3, daah sikuamini nkamwita Kisoda ni wewe, daah we umefikaje huku akaniambia yeye alipata lori la mchanga likamleta mpaka Kisarawe, sa nikamuuliza kwani ni nini kimetokea akasema yeye pia hajui, basi tukaendelea ila angalau sasa nna amani kidogo baada ya kumwona Abdul Kisoda.
Basi tukafika sehemu tukakuta migambo wakasimamisha gari, wakamfata dereva wakamwambia huku mnakoenda ni mbali sana, hapa yenyewe mlipo ni mbali sana, ni bora muishie hapa, basii dereva akapaki pembeni tukashuka tukakuta watu wengine wengi pale, tukajisogeza pembeni kulikuwa na gari dogo imefungua milango yote alafu imewasha redio kwa sauti kubwa, basi pale ndo tukasikia habari kwamba mabomu yaliyokuwa yamehifadhiwa kambi ya jeshi Gongo la mboto yamelipuka, watu wamekimbia kila mahali, juhudi zinafanyika kuyazima,
Daah basi tukakaa pale angalau sasa tunajua nini kimetokea, cha kushangaza tukajikuta wana bweni kama wanne hivi tumekutana pamoja, Na mshikaji wangu Hassan yeye ana mtoto mdogo kama miaka mitatu hivi wakike, tukamuuliza vipi tena na mtoto akasema kuna dada walikuwa wanakimbia nae sasa mtoto akamlemea ndo akamsaidia, Ila kamwachia namba za simu atamplelekea, daah nikaona mshikaji ana roho nzuri kweli, mi nimemkacha mlemavu kule shule, nafsi ilinisuta sana ila nikajipa moyo imeandikwa kila mtu na aiponye nafsi yake
Basi tukajikusanya wanafunzi wa Pugu tukachanganyika na wa Minaki tukawasha moto mkubwa, tukachuma majani tukalala, Basi kukapambazuka tukaanza safari ya kurudi shuleni, Sasa kumekuwa kweupe nikijiangalia sina tofauti chizi, suruali imepasuka, sina ndala, madamu yamegandiana kwenye miguu na vidole nikasema daah akili sina mimi nna tofauti gani na kichaa.
Basi ile barabara ina hawa jamaa wanabeba magunia ya mkaa kwenye baskeli, nikamwona mmoja anapatashida kukokota kupandisha kilima nikaenda kumsaidia nikawa namsukuma hapo nyuma, kidogo ikanipunguzia aibu kwani nikawa kama na mimi ni mbeba mkaa sababu tunafanana ikapunguza hata watu kunishangaa, basi nikamsukuma yule jamaa paka tukatokea Kisarawe, daah ni umbali mrefu sana, basi pale Kisarawe tukakuta daladala za kwenda goms zipo, Hassan alikuwa na hela kidogo basi akatulipia wote tukapanda (kumbuka nauli ni mia kwa wanafunzi)
Basi tukaondoka huko njiani tunakutana na mabomu ambayo hayakulipuka, ebwana ni makubwa, bomu kubwa hata mtu hubebi, pia tukapiita baadhi ya nyumba zina misiba, watu wao wamekufa na mabomu, Basi bana tukafika shule tukaanza kupeana story jinsi kila mmoja alivyookoka, Maji yangu kwenye tranka kama kawaiida nikakuta hola nikasema poa nikashuka pondi nikaoga freshi nikabadili nguo, Hasan akampigia yule dada mwenye mtoto akamwambia anakaa goms basi akaenda huko
Basi bana mitihani ikaisha shule ikaisha nikarudi zangu home kupigisha madogo mapindi, tena ukizingatia nimemaliza form six basi bonge la heshima pale kijijini.
Siku zikaenda matokeo yakatoka sikufanya vibaya, nikachaguliwa kujiunga na degree yangu ya kwanza pale UDSM kitivo cha engineering, pale kijijini ilikuwa balaa walivyosikia naenda kusomea uinjinia, basi yaani hata ningesema nleteeni mabikira wote nichague wa kumuoa basi wazazi wangeleta mabinti zao ili wajaribu bahati zao, yaani nlikuwa kama mfalme pale kijijini
Basi muda ukafika, nikatimba Udsm Coet pale, Nlikuwa nmepewa hela kidogo home nikafanya registration pale, uzuri nilishukia kwa jamaangu ambaye tulikutana pugu yeye alikuwa udsm , walikuja pugu kwenye semina ya kidini, basi akawa jamaangu ananipa ushauri mbalimbali , hata kabla sjamaliza Pugu nilikuwa naenda Udsm kumsalimia alikuwa anakaa hall 5, basi akawa ananipitisha maeneo ya chuo ili kunitia tamaa, na kweli nlikuwa nikirudi shule huo msuli ntakaopiga si wa dunia hii.
Basi bana kwaiyo kabla sjapangiwa room pale chuo nikawa nakaa kwa jamaangu huyu Ambaye anaitwa Frank, kipindi hicho yeye na jamaa zake kadhaa walikuwa wamepanga mtaani maana walikuwa mwaka wa tatu, Basi nikawa naona jamaa wanapiga msulii balaa nikauliza mbona mnapiga msuli halafu hamuendi chuo, wakasema wanajiandaa na Sap, saa hiyo sijui hata sap ni nn, Basi naskia tu huyu ana Sap sita, mwingine nne, Jamaangu yeye alikuwa na sap tano, sasa nikajiuliza huyu jamaa mbona alikuwa vizuri hizi sap (maana waliniambia sap maana yake umefeli mtihani unatakiwa urudie) zote amepataje, maana hapo mwanzo aliwahi kunionesha vyeti vyake jamaa alipasua balaa, form four ana one ya saba, form six ana one ya nne tena PCM, sasa saivi nikiangalia hata past paper zake za chuo nakata tamaa kabisa, unakuta ana tatu ya kumi, 20 ya 60 nikasema khaaa shule ndo hivi
Basi bana chuo wakatupangia rooms, mimi nikapangiwa hall two, floor ya 11 side room, tunakaa nane room moja, basi sasa kimbembe kikaanza tukaitwa tukapewe boom, maana hatuna account hivyo tunapewa mkononi kule kwenye ofisi za auxiliary police, basi tukapanga foleen nikafika dirishani Kwa madam mmoja jina lake Rhoda, akanihesabia kibunda nikasepa, sasa hizi hela zote naweka wapi na ndo mara ya kwanza kushika hela nyingi hivyo kwa mkupuo (kama laki sita hivi)
Basi kwa vile jamaa ngu frank yeye Ana account na ndo mtu nnae mwamini na ni mtumishi mzuri basi nikamkabizi kibunda aniwekee kwenye account yake paka ntakapopata account, Kweli umdhaniaye siye kumbe ndiye na ndo hapo kichapo kilipoanzia, na ndo msingi wa stori yangu unapoanzia.
SEHEMU YA TATU
Ilipoishia,,,,,,,,,,,
Basi kwa vile jamaa yangu Frank yeye ana account na ndio mtu nnaemuamini na ni mtumishi mzuri basi nikamkabidhi kibunda aniwekee kwenye account yake mpaka nitakapopata account, Kweli umdhaniaye siye kumbe ndiye
Endelea
Basi nikahama pale kwa Frank nikahamia chuo campus, Nikafanikiwa kufungua account CRDB maana wao tuliambiwa boom linawahi CRDB kabla ya benki nyingine, Akilini napangia bajeti kile kibunda, nikasema nijibane nitumie nusu, halafu nusu niweke nikipata boom lingine niongezee ninunue PC (Laptop), maana story zilikuwa kwamba engineering bila PC hutoboi.
Basi baada ya kupata account nikasema nimcheki Frank ili anipe kibunda yangu niweke kwenye account, mzee pale ndo niliamini hela haina pastor wala mchungaji, nikaanza kupigwa sound, mara nipo mbali nikitoka nitaenda benki, Mara leo nimeenda benk ATM hazina hela, sound nyingi, siku nyingine namwambia sina hela hata ya kula basi ananipa elfu10 halafu anasema kesho nikija chuo tunaenda kwenye ATM, kesho ukimtafuta anakupiga chenga, mara hapokei simu, nikasema mzee hii balaa sasa.
Basi bana, akanizungusha wee, mwishoni ikabidi anichane ukweli, daah nilihuzunika sana, akaniambia kuwa alichukua hela yangu akachanganya na yake na mshikaji mwingine wakanunua pikipiki, wamempa mtu kila siku analeta elfu saba, Sasa nikamuuliza mi nitaishije, akasema usijali mi ntakuwa nakupa hela ya kula, pia ntakulipa kidogokidogo mpaka iishe, Nikasema daah hii mbona balaa tena.
Kiukwelii maisha yangu pale chuoni yakawa magumu sana, ikafika steji sina hela hata kumi, njaa inauma, Frank hapatikani kwenye simu, kwenda geto kwao kumefungwa hawapo, yaani hapo ndo maji unaita mma,
Pale hall two kuna matank ya maji ya kufulia na kuoga, huwezi amini yale yakageuka maji yangu ya kunywa, home naogopa hata kuomba hela maana hali halisi naijua, tena ingetakiwa mimi ndo niwatumie hela. Basi maisha yakaenda hivyo, siku nyingine Frank ananiipa elf 20, mara elf 10 mara asinipe, hivyo yaani.
Shule ikaanza, masomo kibao, mchana kutwa naranda randa kule Coet na drawing board langu, maana room ni mbali balaa , floor ya 11 na lift haifanyi kazi hivyo ni bora usubiri vipindi hukuhuku Coet.
Basi bana ikafika karibu na UE, PC nagongea kwa washkaji tu, siku moja nipo na PC ya mshikaji room napiga msuli mezani, Sasa inabidi nisome nimalize chapter zote kabla mwenyewe hajaja kuchkua PC yake, kwahiyo hata nikichoka vipi nasoma tu maana kesho yake kuna paper, Ilipofika saa tisa usiku nikawa nimetepeta balaa ,nimechoka balaa, usingizi huu hapa, nikasema cha kujifia ni nini nikaacha PC pale mezani nikasema nilale saa 11 nishtuke nimalizie, nikalala.
Kuja kushtuka saa 12, kucheki mezani PC hamna, umebaki waya wa adapter tu unaelea maana niliupitisha chini ya shuka kuelekea mezani nikawa nimeulalia, Basi nikajua jamaa watakuwa waliamka wakaizima maana niliacha inapiga mziki laini kwa mbalii, nikawashutua jamaa niwaulize aliyechukua PC mezani, wote wakasema hawajachukua, Duuh nikapata wazo au mwenyewe alikuja akaichukua, nikapanda floor ya juu nikamuulize, nikakuta bado kalala nikamwamsha nikamuuliza akajibu kwa kushtuka, hapana sjachkua, vipi imeibiwa??
Nikamwambia subiri, nikarudi room nikakuta jamaa bado wanadiscus kila mmoja anatoa mawazo yake, mwingine anasema alishtuka saa 11 akaikuta mezani, Daah sasa nani kachukua, mara mwenye PC akaja aliposikia jamaa wanavo discuss akajua PC yake imeibiwa, acha aanze kulia, tena kwa nguvu, PC yake Toshiba kanunua laki saba anaskia imeibiwa.
Basi bana, jioni ikafika, usiku ukaingia asubuhi kukakucha ndo hivyo tena PC imeenda, jamaa anataka hela au PC yake daah nikajiona sijui nna gundu, Basi ikabidi hela ya field ilipoingia takribani laki sita nimpe yote jamaa, Alafu mimi ntajua ntaishije, nitaendaje huko field na pia ntarudi vipi nyumbani, mzee usiombe yakukute.
Inaendelea