MTI UNAOMWAGIKA DAMU
PART 7
Maelezo ya yule bibi kikongwe ilizidi kuwaacha midomo wazi wanakijiji. Wengine wakawa wanakumbuka hadithi walizosimuliwa na wazee wao zamani. Inafanania na haya wanayoyaona Sasa. Kumbe haizikuwa hadithi bali ni kweli.
“Ndiomana watoto wetu wanaumwa sana hapa kijijini” Alisema mama Janeth
“Ndiomana tunasikia sauti za ajabu usiku” Bwana Zengo alisema
Kila mmoja alikuwa anasema lake kulingana na maelezo ya yule bibi kikongwe.
Ghafla upepo mkali ukavuma wakiwa pale kwenye mti wakishangaa mafuvu. Ule mti ukaanza kujikunja kama mtu hai. Damu ikazidi na kuzidi. Nyufa kubwa zikaanza kutokea ardhini, ardhi ilianza kujiachia. Mafuvu mengi yakaanza kunyoosha mikono toka ardhini mithiri ya watu wanaoomba msahada. Safari hii sauti kubwa nzito ikasikika.
“Sisi tulikuwa watu wema….ila tulipotea njia tukajikuta tupo kijijini kwenu…mtuachie tunahitaji amani…”
Nani awezaye kukaa kwenye hali kama ile? Kila mwenye moyo dhaifu alitimua mbio…wachache wakabakia
“Kipi tunafanya?” Mwenyekiti alimuuliza Mganga
“Tunatakiwa tutoe kafara ya damu na tuombe msamaha kwa mizimu” Alijibu Mganga
Wakati wote huo Mwandamo alikuwa ameshika kifua chake, moyo ulimpiga kwa kasi. Aliwahurumia walalamikao pale ardhini..alihisi maumivu yao..
Usiku wa siku hiyo hakuna aliyelala. Walikesha wakiimba na kucheza ngoma za matambiko. Wakiongozwa na wazee ….
PART 8
Siku iliyofuata, wanakijiji wote walikusanyika tena kwenye ule mti. Walikaa kwa kuuzunguka. Damu iliendelea kutiririka taratibu. Yale mafuvu walioyafukua waliyahifadhi kwenye chungu kikubwa cha udongo wa mfinyanzi na kuifunika vitambaa vyeupe.
Mganga wakijiji alitembea taratibu akiwa na ungo uliojaa dhana zake za kazi. Alikuwa amevalia shuka jeupe. Wanakijiji walikaa kimya wakisubiri kuona kitakacho tokea.
“Leo ni siku ya kuweka ukweli wazi” Alisema Mganga na kuendelea baada ya kunyamaza kidogo
“Siku ya kuomba msamaha” Alisema, alichukua pembe yake kubwa na kuupuliza. Alipuliza kwa dakika zisizozidi mbili kisha akaagiza aletewe mbuzi mweupe haraka. Alipoletewa akamkata kichwa na damu ikakingwa kwenye bakuli kubwa lililotumika kumbebea yule mbuzi mweupe. Watu wakazidisha ukimya.
Mganga alichukua dawa na kuchanganya na ile damu kisha akakoroga na kuimwaga pale panapodondekea damu itokayo kwenye mti. Kwa sauti isiyosikika alizungumza yule Mganga kabla ajasema kwa sauti kubwa
“Enyi miungu, leo tupo mbele yenu kukiri kosa na kuomba msamaha kwa dhambi waliofanya baba zetu”
Wanakijiji nao wakaitikia kwa umoja wao
“Miungu mtusamehe”
Kila mmoja akabaki kimya tena wakati Mganga akizungumza kwa upole tena
Mwenyekiti wa kijiji aliivua kofia yake nyekundu aliyokuwa amevaa ili kuonyesha heshima kwa kile kinachoendelea pale.
Mwandamo hakuwa nyuma, aliendelea kushuhudia tukio lile la maombi ya kafara. Lakini damu haikusita kutiririka, Mwandamo aliwaza na kuwazua….
PART 9
“Ilikuwa upofu, historia yetu ilifichwa, Leo tumeikunjua moyo wetu na bila shaka mizimu italala kwa amani” Alisema mwenyekiti wa kijiji
Yule bibi kikongwe alisogea mbele taratibu huku akiwa ameshika njiwa weupe wawili. Alipofika akauzunguka ule mti mara kadhaa kisha akawaachia wale njia nao wakaruka juu wakapotea huko.
“Nanyi roho zetu zipeperuke kwa amani” Alisema bibi kikongwe huyo.
Taratibu damu ikaanza kukata. Ule mti ukanyooka kama ilivyokuwa awali. Magome ya huo mti ukawabadirika na kuwa nyeusi. Amani ikaanza kunawiri.
Watu walipiga makofi na wengine wakapiga magoti. Wangine walilia kwa furaha. Anga likaanza kung’aa
Mwandamo naye akasogea mbele bila hofu. Alikuwa ameshika kipande cheupe cha nguo. Alipofika pale kwenye mti akaufunga kwa kile kipande chake cha nguo .
“Hii ni kwaajili yenu, mwanzo mpya na uanze” Alisema Mwandamo
Shangwe likafuata. Wanakijiji wakafurahia.
“Maombi yetu yamekubaliwa” Alisema Mganga na kuendelea
“Amani imerejea”
Vifijo na nderemo ikasikaka Tena
Kipi kiliendea Baada ya hapo? Usikose sehemu ya 10 na ya mwisho hapo baadae
PART 10
Mganga aliongeza “Mizimu imekubali maombi yetu, ardhi imepona”
Kuanzia siku hiyo mabadiliko makubwa yalionekana hapo kijijini. Maisha yalilejea kama zamani.
Watoto waliiacha kuumwa Kila mara
Watu waliacha kusikia sauti zile za kuogofya usiku.
Ule mti ulikaa mahara pake.
Watu watu hawakusahau tukio lile kamwe. Kila mwaka waliadhimisha siku hiyo kwa Sherehe zilizoambatana na shughuri za kusafisha sehemu za mti ule pamoja na kupanda maua.
Hadithi ile ya kweli ilibaki kuwa urithi wa vizazi vyao.
Siku zilienda sana hata Mwandamo, mtoto jasiri wa kiume amekua. Mwandamo akawa mtu mwenye hekima na busara zaidi pale kijijini. Watu walikwenda kwake kuomba ushauri wanapokuwa na shida.
Watu wengine wanasema “Mwandamo amebarikiwa na miungu hata kuonyeshwa vitu ambavyo wengine hawakuviona kabla”
Hata Mwandamo akawa na msemo wake kuwa “Ukiuficha ukweli dhambi itakuukumu, na ukiuweka bayana ukweli hata mti utiririkao damu utakusamehe”
MWISHO
Funzo: Ukweli umuweka mtu huru. Hakuna haja ya kuuficha hata kama unaumiza kwa wakati huo. Wahenga husema “Heri ya nusu shari kuliko shari kamili”
Dhambi unayotenda leo na ukaificha, itawahukumu vizazi vyako kama si wemwenyewe hapo baadae”
Tuwe na hofu ya Mungu
Nawapenda na kuwashukuru kuwa nami kwenye simulizi hii