MTI UNAOMWAGIKA DAMU
PART 4
“Nini kilitokea?” Aliuliza Mwenyekiti lakini yule bibi kikongwe hakusema lolote. Aliutazama ule mti akiwa mbali na kutikisa kichwa chake.
Usiku mambo yakawa ni yaleyale. Mti ule ulizidi kutiririka damu. Upepo mkali ulishamiri kijijini na hata damu ikatengeneza bwawa dogo kuuzunguka mti.
Mwandamo hakulala usiku ule, akawa anasikia sauti ya mwanamke ikilia na kuomba msahada. Hakujua sababu. Alifungua dirisha taratibu kutazama nje lakini hakutanikiwa kuona chochote zaidi ya giza la usiku ule pamoja na upepo uvumao. Akarudi kulala kwenye mkeka wake.
Ghafla mlango wao ukawa unagongwa kwa nje, mama yake alijibu “Nani?” Aliuliza mara kadhaa lakini hakukuwa na majibu.
Mama aliwasha taa ya mafuta na kwenda kuufungua mlango. Lakini hakuona chochote. Aliufunga mlango na kumwambia mwanaye, Mwandamo
“Usifungue malango, Kuna shetani anatembea huko nje”
Mwandamo alitii lakini aliendelea kuwaza, kwanini yule mwanamke analia kuomba msahada, na kuna ukweli gani kuhusu maneno ya yule bibi kikongwe aliyeyasema pale kikaoni.
Baridi ilikuwa Kali sana, Mwandamo alijaribu kujifunika kwa blanket lake lakini haikumsaidia kwani baridi ilikuwa inatokana na hofu aliyokuwa nayo kuhusu kinachoendelea usiku ule
PART 5
Mwenyekiti na wazee wachache wa kijiji walifika kwenye ule mti wakiwa na Mbuzi mweupe. Mganga alimchinja yule mbuzi na damu yake kuielekeza kwenye ule mti. Alichukua dawa yake na kuinyunyuzia sehemu yenye damu na Kisha alianza kuongea na miungu.
Damu haikukata badala yake iliongezeka. Usiku wa siku hii sauti ya mwanamke akilia ilikuwa kubwa zaidi. Hofu ikatanda tena.
Mwandamo kama kawaida yake. Mawazo mengi kichwani. Usiku ule aliwaza sana. Alimuwaza yule mwanamke anayeomba msahada. Aliwaza kitu kipi kinamfanya awe pale akiteseka.
Ingawa mama yake humzuia kwenda kwenye ule mti lakini safari hii lilimpata jambo. Usiku huo alitoka taratibu bila mama yake kujua chochote. Alichukua kipande Cha mti na kukichonga.
Mwandamo alielekea kwenye ule mti unaomwagika damu. Alijitahidi kupita kwa kujificha ili asije onekana na yeyote. Alipofika pale akaanza kuchimba sehemu ya mizizi inakomwagikia damu. Alitumia lile jiti alilochonga.
Damu ilikuwa ikizidi kumwagika na ilikuwa ijitoa harufu kama ya mtu aliye kufa na kuoza. Hakujali aliendelea kuchimba. Jasho likamtoka bado hakujali
PART 6
Mwandamo hakujali jasho, hakujali damu inayotoa harufu. Alizidi kuchimba na kijiti chake. Alichimba sana na hata akakuta fuvu. Akaendelea kuchimba ..
Ndio ni fuvu kweli la binadamu, lilikuwa chafu, halina nyama, wala macho. Mwandamo alianza kuogopa Sasa. Aliruka toka eneo lile la fuvu. Akaanza kupiga kelele.
“Fuvuuuuu” jamani kuna fuvuuu” heeee”
Punde wanakijiji walijaa wakiwa na majembe na kuanza kuchimba zaidi. Halikuwa fuvu pekee, bali ni mafuvu ya watu wengi. Watoto, wanawake,wanaume na bila shaka hata wazee. Walibaini hayo kwakuona nguo zao kwani mafuvu mengine yalikuwa bado na nguo zao.
Mganga wa kijiji alichukua usinga wake na kuurusha juu na kudondoka chini. Alichukua kitu kinachofanania na unga mweusi toka kwenye mkoba wake na kumwaga pale kwenye mafuvu huku Alizungumza kiganga.
Watu wote walikuwa kimya huku wakijiuliza kimoyomoyo ni kitu gani hicho…
“Kuna maovu makubwa yalifanyika hapa” Alisema Mganga
“Miungu imeuraani huu mti na watu wake” Alimalizia Mganga. Hofu ikatanda upya
“Tumeraaniwa?” Waliuliza wanakijiji.
Yule bibi mkongwe aliyewaeleza kuhusu mambo ya zamani alijitokeza na kusema..
“Zamani sana kijiji chetu kilikuwa kiovu lakini hatukujua…” Alisema yule bibi mkongwe.
“Kila mgeni aliyekatiza kwenye Kijiji chetu aliuliwa na kuzikwa chini ya huu mti. Sisi tulijua tunakilinda Kijiji kwa kuhofia kuwa huenda hao wanaopita kwenye kijiji chetu ni waovu. Lakini tumeharibu…” Alimaliza yule bibi mkongwe.
Inaendelea…………….

