MCHEPUKO ALIVYOMUUGUZA, NA KUMHUDUMIA MUME WANGU, PASIPO MIMI KUJUA
Hadithi Ya Kweli
Baada ya miaka minne ya ndoa yetu mume wangu alianza kubadirika, akawa mkali sana, hata nikimtania ananifokea na kuniambia niache utoto, mara kadhaa nilimwandalia chakula lakini alikataa kula na kusema ameshiba, kila siku ilikuwa ni kumwaga chakula, tulishakaa vikao na vikao lakini hakubadirika, nikaanza kupoteza tumaini la ile ndoa na nikatokea kuichukia sana ndoa.
Kwakuwa mimi ni mkristo na tulifunga ndoa kanisani sio rahisi hata kidogo kuvunja ndoa kwahiyo tuliishi hivyo hivyo, ilifika hatua analala huko huko akirudi asubuhi ananiambia alisinzia kwenye daladala akapitiliza, nikiwa mbishi kukubali utetezi wake ananipiga kipigo cha hatari, kwahiyo ikawa mazoea yake.
Sasa kumbe alikuwa na mchepuko ambao ulikuwa x wake kabla hajanioa mimi, yaani alikuwa na mwanamke wakaachana, akanioa mimi halafu wakarudiana, alikuwa akiwa ndani anakuwa busy sana na simu, muda wote anachat nikimuuliza ‘mume wangu unafanya nini kwenye hiyo simu muda wote hutaki hata tuongee’? Ananiambia “Usifatilie mambo ya wanaume wewe kazi yako ni kuosha vyombo na kudeki” fanya ukadeki hata chooni kama umekosa kazi ya kufanya”.
Nilikuwa naumia sana kwa majibu yake, ni kwa kila swali nililokuwa namuuliza majibu yake sio rafiki, hata tukiwa chumbani ananiambia maneno magumu sana ili nisuse kukutana nae, kwa mfano kuna siku aliniambia “Sogeza hilo tumbua lako hapa nikusaidie maana nyege zisije zikakuua nikasingiziwa mimi ndio nimeua” na hata tukikutana zikizidi sana ni dakika 5 amemaliza kila kitu, nikimwambia mimi bado jibu lake litaniliza hata wiki nzima.
Alikuwa na tabia ya kwenda kwa huyo mchepuko akiamua analala huko akiamua anarudi na akirudi anakuwa busy na mchepuko kwenye simu, kuna siku nikaamua kumsimulia mama mkwe na wifi ninayopitia, wakaniambia “Vumilia ndivyo ndoa zilivyo ila tutaongea nae” sometimes wananiambia “Muombee atabadirika”.
Basi ikawa kila nikiwatafuta wananiambia hivyo hivyo, halafu baadae wanamtafuta wanamwambia yote, mume wangu anakataa halafu anaanza kunisingizia makosa mengine hata nikiyasikia naishia kudondosha machozi tu, ilimradi tu ajisafishe kuwa hana kosa lolote na huwa wanamsikiliza yeye anachoongea, mimi hata niende mikono imekatika niwaoneshe watasema sio kweli. Nikaapa sintorudia kushtakia familia yake tena.
Sasa miezi mitatu iliyopita mume wangu alikuja nyumbani na perfume nzuri sana pamoja na maua, akafika anaiweka mezani, kwa hisia zangu nikajua ameninunulia mimi pengine anataka kunipa zawadi na turejeshe upendo wa zamani ndoa yetu iendelee vizuri, akawa ameingia chumbani akatoka na nguo kadhaa, akapakia kwenye begi nikashangaa maua na ile perfume inawekwa kwenye begi, akaniambia “wewe mwanamke mi nasafiri chakula kipo tusisumbuane, bye” nikamuuliza sasa unaenda wapi hatujaagana vizuri na hiyo perfume na maua vipi? Akasema Kinachofanya nikuchukie ni hayo maswali yako ya kunifatilia mambo yangu, kwani maua na perfume yanakuhusu nini wewe, kuna kitu yamekukosea?
Mmmh nikaishia kuguna tu, nikajiuliza huyu mwanaume ananichukia hivi kwasababu ya huo mchepuko au ndio asili yake makucha yameanza kujionesha, na je wanaume wote wangekuwa kama yeye dunia ingekuwaje? Mbona amekuwa rimbukeni wa hovyo kabisa, kumnyanyasa mkeo kiasi chote hicho kisa wanawake wa nje?!
Nililia sana kwa uchungu, niliomba dua nyingi mpaka kwa kiruga changu nikaililia mpaka mizimu ya mababu na mabibi wa enzi, nikiwaomba wanioneshe mbinu wao waliishije hapo kabla yetu.
Siku hiyo sikula na siku iliyofata nilifunga kwa maombi, Mungu anioneshe njia lakini pia kama ni kutoka kwenye hii ndoa nitoke salama nimechoka.
Nilikuwa nikipiga anakata, nikamuacha, hakuwahi kunitafuta mpaka mwezi ulipoisha ndio niliona simu yake mida ya saa 10 jioni, kupokea nikasikia analia mke wangu naomba unisaidie niko hoi sana, kuna ugomvi ulitokea kati yangu mimi na huyu mwenzangu tukawa tumegombana sasa akanisukuma kwa bahati mbaya nikawa nimejigonga kwenye nguzo ya kitanda damu zilivuja sana puani nikazimia, yule mwanamke kuona nimeanguka akajua ameua akaamua kukimbia kwa hofu ya kukwepa kesi ya mauaji, tangu amekimbia hajarudi, naomba ufanye utaratibu uje unichukue unipeleke hospital.” Nitakuelekeza mke wangu we kachukue bajaji unipigie.
Aliponiambia hayo sikuamini masikio yangu nilihisi kama naota, maana hajawahi kuniita mke wangu tangu amebadirika, ni majina ya hovyo hovyo tu, leo kulikukoni?! nikaona hapana huyu atakuwa amekula njama na mchepuko wake wanidanganye niende waniue ili wawe huru, nikamwambia pole ila siwezi kufanya hivyo, wapigie mama yako na wifi waje wakuchukue mimi siwezi. Akasema siwezi kuwatafuta wao nielewe, aliposema hawezi kuwatafuta wao ndio nikaamini huyu mwanaume anataka kuniua nikazima na simu.
Sikuwasha simu kabisa mpaka wiki ilivyoisha ndio nikawasha simu, nikakutana na meseji kibao zote nilizipuuza, ikabidi niwapigie wazazi wake kuwaeleza michezo ya mtoto wao, mama yake akaniambia, nipeleke huko mwanangu alipo na usiponipeleka nitajua wewe ndio umemteka ili wamuue halafu unajifanya haujui kitu” nikihisi kama masikio yangu yamepigwa shoti ya umeme kwa maneno hayo ya mama mkwe, nililia sana nikajiona mwanamke mwenye mikosi kuliko wote duniani, nikiona mtu hata mtandaoni ameandika “am single” namuonea wivu sana, nikiona makala zako watu wanatafuta wachumba yaani nawaonea huruma mno japo wanaume hawafanani lakini kwangu kitu kinaitwa ndoa nikifanikiwa kuachika kwa hii ya kwanza, sidhani kabisa kama naweza kurudia, siwezi na siwezi tena nakwambia kaka Halisi Naturalist.
Sasa hivi hapatikani tukipiga, familia yake wamenipeleka polisi kushtaki, nikahojiwa nikaeleza yote nikaonesha na ushahidi wa meseji alizotuma, kwahiyo familia imenipa mtihani wa kuwapeleka alipo mume wangu la sivyo watanionesha, yaani wananipa vitisho vingi wakidai mimi nimemuua na maneno mengi ya kashfa, najuta sana kuolewa kwenye hii familia ya kishetani, mtoto wao shetani mama shetani na kila mtu, hawana utu hata chembe, roho zao ziko kinyume nyume, hapa nilipo sielewi naanzia wapi, naombeni ushauri wenu waungwana, sijali kama kuna mwanafamilia atasoma hii makala, someni tu mjue ushetani wenu.😓