MATESO YANGU: KUANZIA TUMBONI, KUZALIWA, KUSOMA, HADI SASA
Sehemu Ya Tatu
Baada ya kupata nafasi katika ile shule nilianza masomo japo nilianza kwa kuchelewa kwasababu bibi yangu alikuwa akiumwa, hivyo nilikuwa nikimshughulikia apate ahueni nami niwahi masomo.
Niliendelea na masomo walimu pamoja na wanafunzi walinipenda sana. Nilikuwa mwanafunzi maarufu pale shuleni na hii yote ilisababishwa na ile story ya NINGEKUWA KWETU. Baada ya miezi sita kupita niliishiwa kabisa pesa ya matumizi na kodi ya pango la nyumba nilipokuwa naishi muda ulikuwa umeisha pia.
Nikaamua kumtafuta kaka yangu ambaye ni mzaliwa wa kwanza kwa mama na baba yetu ili aweze kunisaidia changa moto hiyo, ada ya shule nilikuwa nimeilipa mwaka mzima hivyo shida ilikuwa ni kodi ya nyumba na matumizi pekee, kaka yangu hakuweza kunisaidia na badala yake kalizuka ka ugomvi baina yetu nadhani ugomvi huo ulitokea kwa sababu ya pesa niliyo iomba.
Nilifikiria sana baadae nikachukua maamuzi ya kutafuta kazi ili niwe napata walau matumizi. Kwa vile ile shule tulikuwa tukienda mchana nilifikiria asubuhi ningekuwa nafanya kazi na mchana naenda shule Mungu si Athumani nikapata kazi ya kuchoma chipsi stend ya mabasi, kwa siku nililipwa sh 3000 hivyo saa kumi na mbili alfajiri nilikuwa naingia kazini na saa sita mchana naelekea shule. Mazingira ya shule na kazi yalikuwa magumu sana kwangu kuna wakat ku mudu vitu vyote kwa usahihi ilikuwa ni ngumu, upande wa masomo ndo ulionekana kusuasua ilhali lilikuwa ndo dhumun kuu.
Maisha yaliendelea siku moja boss wangu akaniita na kuniambia amepata mbadala wangu hivyo kazi inatakiwa nisimame lakini kama nitaamua kuacha shule na kufanya kazi siku nzima milango iko wazi, nilifikiria sana nikaamua nisitishe masomo maana maisha ya mjini bila pesa hata hayo masomo nisingeweza kuyamudu. Hivyo niliacha masomo na kuendelea kufanya kazi baada ya muda mfupi muda wa kufanya mtihani wa QT (Qualifying test) ulikuwa umefika nilienda kufanya japo sikuwa na maandalizi ya kutosha nilimaliza mtihani salama maisha mengine yakaendele mtihani ule ulikuwa mgumu sana lakini niliamini ingetokea miujiza kama ilivyotokea kwenye ule mtihani wa usaili (interview)
Nilifanya kazi kwa bidii na uaminifu wa hali ya juu lakini wiki moja kabla ya matokeo kutoka boss aliniambia kulikuwa na taarifa kuwa stendi inge fanyiwa maboresho hivyo wafanyabiashara wote inatakiwa watoke kupisha maboresho hayo kwa wiki mbili. Kwangu ulikuwa mtihani pia nikaamua kurudi kijijini japo sikufikia kwa baba, kaka yangu ambae alikuwa anaishi Dar kabla ya kwenda Dar alijenga nyumba ndogo hivyo ndipo nilipokuwa nina ishi nilifanya shughuli za vibarua wakati huo matokeo yametoka na nimefeli sikukata tamaa juu ya shule…..siku moja katika matembezi yangu pale kijijini nilimwona mwanamke mzungu ambaye alionekana kama mtu mzima wa miaka hamsini hivi alikuwa akienda dukani ameshika gerani ya lita tano, ilikuwa si rahisi kumuona mzungu kijijini hapo nilitamani kukutana nae na ingekuwa fahari pia kuzungumza nae.
Duka alilokuwa ameingia lilikuwa ni duka la baba angu na muuzaji alikuwa yule mama mdogo aliyekuwa akiishi nae Nikiwa karibu na lile duka nilisikia yule mzungu akionge kingereza na mama mdogo alishindwa kumwelewa anahitaji nini walibishana mithili ya wajenzi wa mnara wa BABELI baada ya kila mtu kuongea lugha yake. Japo kuwa sikuwa na maelewano mazuri na mama lakini nilihisi ule mvotano kati yake na mzungu inaweza ikawa ni fursa kwangu niliingia na nikamsalimia mama mdogo kisha yule mzungu….
Niliongea English ya kuunga unga lakini tulielewana yule mzungu alikuwa anahitaji mafuta ya taa lita tano wakati ule nishati ya mwanga vijijini ilikuwa shida sana kuna baadhi ya familia hazikuweza hata kumiliki koroboi(vibatali) Mzungu alipomiwa mafuta na akalipa pesa kisha akaniambia amefurahi kukutana na mimi akaniuliza majina yangu nika jitambulisha alishtuka kusikia jina la baba yangu likijumuishwa kwenye majina yangu aka uliza kama yule mmiliki wa lile duka alikuwa ndio baba yangu?nilimjibu ndio na swali lake kubwa lilikuwa kwanini sipo shule kwa ule umri halafu baba ni mtawala na alikuwa anajulikana sana ……
Nilimweleza kiufupi lakini aliniomba kesho yake asubuh nifike nyumbani kwake tuongee. Ilikuwa ni furaha kubwa sana kualikwa na mzungu na nilijua ule ungeweza kuwa mwanzo wa majibu ya shida zangu. Usiku wa siku hiyo ulikuwa mrefu na sikupata usingizi kabisa kwa furaha kubwa niliyokuwa nayo lakini pia nilihofia kuchelewa Niliamka mapema sana na ilipo fika saa tatu kamili nilikuwa nagonga mlango wake alinipokea vizur na alinipongeza kwanamna nilivo jitahidi kufika kwa wakati aliniandali kifungua kinywa baade mazungumzo yaliendelea, nilimweleza kila kitu kuhusu maisha yangu alitokwa na machozi lakini kunawakati alikuwa haamini maelezo yangu baada ya kumaliza mazungumzo aliniambia nije kesho yake muda ule ule. Niliondoka nikiwa mwenye furaha siku hiyo sikufanya kazi yoyote niliwasimulia marafiki kuhusu tukio lile na hawakuamini.
**********************************
Kumbe baada ya mimi kuondoka nyumbani kwake alielekea shule ya msingi ya kijiji hicho nia yake ilikuwa akapate mwalimu anaye zungumza kingereza ili ajaribu kupata taarifa sahihi kuhusu mimi kwa sababu kwa upande wa wana kijiji mtu pekee aliyekuwa ana uwezo mkubwa wa kuzungumza kingereza ni baba yangu pekee. Mwalimu alimpa ushirikiano wa kutosha maana nae alinijua vizuri pamoja na maisha yangu yalivyo na mzungu alithibitisha maelezo yangu na hakuna alipo kuwa na shaka na mimi
Kesho yake nikafika nyumbani kwake tukaongea mengi lakini kubwa lilikuwa aliguswa na hali yangu hivyo alidhamiria KUNIASILI yaani aliona mimi ni mtoto niliye telekezwa hivyo alitaka kunichukua na kunilea kama mwanae na hata majina la pili na la mwisho ningeitwa majina yake na hata mkataba wake wa kuishi Tanzania ukiisha ningeondoka nae kwenda America
. Tatizo lilikuwa katika mchakato huo baba ana paswa kushirikishwa moyoni niliwaza mengi ila niliamua kumuachia hiyo kazi Mzungu mwenyewe.
Mzungu aliahidi kukutana na baba na kuzungumza nae baada ya mazungumzo na baba mzungu alinifuata siku hiyo nakumbuka nilikuwa kwenye uwanja wa mazoezi akaniambia baada ya mazoezi nipitie nyumbani kwake….bila ajiz nilipotoka mazoezini nilipita kwake na akanipa mrejesho toka kwa baba kuwa amekataa kwa hiyo hilo lilishindikana…..Mzungu alipenda niwe jirani nae sana maana nilimsaidia kidogo kumfundisha Kiswahili lakini kurahisisha mawasiliano na wana kijiji alipo hitaji kuzungumza nao.
Hivyo alinipa kazi ya kutunza bustani pamoja na kumwagilia maua pale nyumbani kwake nilifurahi sana maana niliona nguvu ya mungu kwangu ukifungwa mlango huu mwingine unafunguka……..nilianza kazi nikiifanya kwa weledi na uaminifu mkubwa ile kazi ya chipsi nikawa nimesha isahau na haina nafasi kwangu tena na niliahidiwa kulipwa laki moja na ishirini kwa mwezi ilikuwa ni kiasi kikubwa cha pesa hakuna kijana wa umri wangu aliye weza kupata pesa nyingi kama hiyo wakati ule. Siku moja nikiwa kwenye majukumu yangu ya kikazi baba alikuja pale kwa mzungu sikujua alikuja kwa shida gani baada ya baba kuondoka maeneo yale Mzungu alinifuata akasema hatakama sijamaliza kumwagilia niache atamalizia mwenyewe na nisije tena mpaka atakapo niita, zilibaki siku kama tano kufika mwisho wa mwezi lakini alinilipa mshahara siku ile ile nilishangaa sana Maana mzungu ile siku hakuwa kwenye hali yake ya kawaida bila shaka nilifikiri kuna maneno baba kaya leta.
Maisha mapya yakaanza kwa wakati huo nilikuwa na kama laki mbili hivi nika nunua kuku kumi nikaanza ufugaji alhamdulilah kuku walizaliana sana lakini sikuacha kufanya kazi za mtaani ili kumudu gharama za maisha
Baada ya kukaa sana mtaani siku moja niliamua nikamsalimie yule mzungu maana nilizi miss sana zile laki na ishirini za mwezi, nilipofika pale alinipokea nikaomba tuzungumze kidogo na pale kazini nilimkuta kijana mwingine ila alikuwa haongei kingereza. Mzungu aliniambia mimi nina vuta bangi na ni mwizi hivyo asingeweza kuishi na Jambazi wa aina yangu Nilijaribu kumsihi na kuzifanyia kazi taarifa zile kwa bahati nzuri alinisikia na akapeleleza akapata majibu hatimae nikarudi kazini yule mwenzangu akawa anahudumu kwenye usafi wa mabanda ya mifugo lakini baadae akaachishwa kazi….Mzungu alinipigania sana baadae akasema atanifanyia mpango mwaka unaofwata niende shule nakumbuka alikuwa ananiambia hayo mwezi wa tisa.
Alijaribu tena kumshirikisha baba juu ya mpango wake wa kunipeleka shule awamu hii Roho mtakatifu alitenda kazi kwenye moyo wa baba akakubali ila alimwambia yupo bize na mambo ya kisiasa hivyo atakapo pata muda angemtafuta wronged vizuri.
Siku moja baba alienda kutembelea mzungu na walipata wasaa wakuzungumzia swala langu awamu hii baba alikuja na ushauri mzuri kwamba kutamatika kwa mkataba wa mzungu na shirika lake(US PEACE CORPS International)umebaki miezi mitatu hivyo kwanamna yoyote mzungu ataondoka mm nikiwa sijaenda shule hivyo anashauri aanzishe mradi utakao nisaidia kunisomesha mpaka nitakapo ona ina tosha.
Mzungu aliona ni wazo zuri na baba alibuni kilimo cha umwagiliaji wakati huo teknorojia ya umwagiliaji haikuwa yenye tija kama sasa, Walipiga mahesabu ya gharama za mradi mimi nilishilikishwa tu na yule mzungu ..
Itaendelea…..