MATESO YANGU: KUANZIA TUMBONI, KUZALIWA, KUSOMA, HADI SASA
Hadithi Ya Kweli
Sehemu Ya Kwanza
Naitwa Nasri mzaliwa wa Njombe kama ilivyo ada watoto husimuliwa na Jamii au wazazi maisha ya wazazi wao kabla ya kupatikana kwao(watoto).
Mimi pia ni miongoni mwa waliosimuliwa maisha ya wazazi yalikuwaje. Baba na mama yangu walikutana katika chuo cha ualimu sumbawanga miaka mingi iliyopita baada ya kuhitimu elimu ya ualimu bahati nzuri waliajiriwa kituo kimoja wakapata watoto wawili Me na Ke pia walijenga nyumba ya kisasa kwa wakati huo kila mmoja wa wana kijiji walitamani jengo hilo ambalo limejengwa kwa mishahara ya baba na mama….
Baada ya kufanya kazi kwa muda mrefu baba alimpenda mwanafunzi wake aliye kuwa akisoma darasa la saba, msichana huyo alikuwa mrembo na alijaliwa rangi alikuw mweupe sana kiasi cha baba kuamua kurudi Sumbawanga alikosoma maana huko angekutana na marafiki zake aliosoma nao na wangemwelekeza ni wapi atapata mganga wa kienyeji ili hata amuue mke wake na kupata fursa ya kutanua na yule msichana maana alikuwa mwishoni kuhitimu darasa la saba miaka ya zamani bint wa darasa la saba alikuwa ni mtu mzima,,,,,,
Baada ya yule msichana kuhitimu darasa la saba baba akasafiri ikiwa ni utekelezaji wa mipango yake aliyoipanga Baba alifika sumbawanga na kufanikiwa kupata huduma japo haikuwa kuua kama ilivokuwa dhamira huruma ilimjia akaamua amchanganye akili mama hivyo kuanzia pale mama yangu alipata ukichaa na akaacha kazi, Baba aliwatumia habari wazazi wa mama kule kijijini kwao kuwa mtoto wao amepatwa na shida bila kuchelewa ndugu wa mama walikuja kumchukua ili akaendelee kutafutiwa ufumbuzi akiwa kwao.
Baada ya mama kuchukuliwa na nduguze, yule msichana akawa amehitimu darasa la saba hivyo baba akamuoa na maisha yaliendelea.
Maisha ya mama yalikuwa magumu sana kule kwao kutokana na hali duni ya uchumi hata hivyo bibi yaani mama yake na mama waligundua kuwa mama alikuwa ni mjamzito hivyo walituma taarifa kwa baba lkn alipuuza na kuwaambia maneno ya kejeli kuwa yeye hajashiriki nae tendo la ndoa yapata mwaka mmoja na hivo ndivyo alivokuwa amemdanganya yule msichana.
Moyoni aliwaza kama mama angejifungua yule mtoto bila shaka angekuwa ni wake sasa ataeleza nini kwa yule msichana mrembo?,,,,,,,
Aliamua kufunga safari kwa mara nyingine kwenda Sumbawanga kwa vile alishakuwa na uzoefu ni wapi atapata huduma haikuwa shida kufika kwa mganga wake wa kienyej aliye msaidia mwanzo alimweleza hali iliyopo na aliamua kupoteza ushahidi yaani siku ambayo mama angejifungua basi mtoto afe au wafe wote na alilipa malipo akarudi,,,,,,,,,,.
Kadri siku zilipokuwa zikisonga mama alizidi kuchanganyikiwa zaidi wakati mwingine anaweza anatoka nje na eneo la nyumbani aka lala hukohuko Siku moja mama alienda kwenye mto mkubwa kijijini hapo akawa anapunga upepo kama ilivyo kawaida hakurudi nyumbani ilipofika saa sita za usiku bibi aliamsha majirani na baadhi ya ndugu kumtafuta maana alihofia hali ya ujauzito wake walimtafuta ilipofika saa nane usiku wa manane walimuona pembezoni mwa mto amelala chali miguu imening’inia kwenye mto na uchungu ulikuwa umemkamata na baridi lilikuwa ni kali sana kama inavyo Julikana hali ya Njombe,,,,,,kumbe hizo zilikuwa ni nguvu za giza ilishapangwa ajifungue na mtoto aende na maji na hakuna mtu ambaye angelijua.
Walimkimbiza mama zahanati ya kijijini akapata huduma baada ya muda mfupi akajifungua mtoto wa kiume ambae ni mimi ninaesimulia hapa , Baada ya kujifungua mama hakutaka hata kuniona alifanya jaribio la kuwapokonya mtoto wale ndugu zake ili aniue ilishindikana nguvu ya mungu ilishinda hivyo nilliendelea kulelewa na bibi kwa maziwa ya ng’ombe.
Nilitumia maziwa ya ng’ombe mpaka nafikia miaka miwili nanusu baba alielewa ilichotokea mungu si athumani katika watoto wake wote mimi ndiye niliyefanana nae zaidi na taarifa za wa mbeyazikafika kwa mama mdogo wakati huo nae alikuwa tayar ana mtoto mmoja hivyo ulizuka ugomvi baada ya mama mdogo kujua kuwa alikuwa akimrubuni kuwa baba hakushiriki tendo la ndoa na mama yangu.
Maisha yaliendelea baba akafunga safari upya kwenda Sumbawanga ili kunitoa mimi alifanikiwa kukutana na watalam wake baada ya muda mfupi ilikuwa moto upo hata mitambili toka kwangu nikawa naungua kimaajabu niliungua sana bibi alitafuta suruhu kwa muda mrefu na ilibaki kidogo akate tamaa hali yangu ilikuwa mbaya muda huo nimetimiza miaka minne, naam kumbukumbu zangu zilianzia hapa kwani nakumbuka mpaka leo kila kilichotokea bibi alikuwa hana uwezo wa kunitibu maana alijua ni nguvu za giza.
Nakumbuka siku moja rafiki yake na bibi kutoka kijiji jirani alimtembelea bibi na alinikuta nikiwa kwenye hali dhoofu sana alimuuliza bibi kilichonikuta akampa ushauri kuwa anipeleke kwa mganga mmoja nchini Malawi, wilaya ya Karonga bibi aliuza ng’ombe watatu ambao aliwapata kwenye mgao wa mirathi ya mume wake hivyo tulianza safari kuelekea Malawi, wakati ule passport hazikuwa zinazingatiwa sana. , ,,,
Bibi yangu hakuwa anajua kiswahili ilimlazimu kuajiri mtu anaejua kiswahili na lugha yetu ya asili iitwayo KIBENA tulifika mpaka wa kasumulu(Kyela)tulivuka mpaka Karonga kwa kuwa bibi alikuwa na fedha haikuwa shida kuwatuliza watu wa uhamiaji mara walipo anza kutufwatilia pesa nyingi bibi alizibadilisha na kuwa kwacha za Malawi…….
Shida ilianza tulipofika Karonga tulishindwa kuelewana na watu maana sisi tunaongea lugha zetu na yule mkalimani akawa hana kazi ilibidi tutafute baadhi ambao wanazungumza kiswahili na lugha ya malawi au kizungu wakati ule lugha waliyotumia zaidi watu wa malawi ilikuwa Chichewa, Chitumbuka, Kiingereza pamoja na kindali na lugha nyingine za asili ambazo baadhi hata Tanzania zinazungumzwa.
Alipatikana mkalimani mwingine aliye tafsiri kiswahili kwenda chichewa au kizungu zoezi hilo likakamilika na safari ikaanza kuelekea kwa mtaalam huyo wa tiba za asili,,,,tulifika usiku ililazimu kulala mtaani ili asubuhi tukawahi matibabu……..
Inaendelea……….