MATESO YANGU: KUANZIA TUMBONI, KUZALIWA, KUSOMA, HADI SASA
Sehemu Ya Pili
Asubuh mapema afajiri tulikuwa tumefika kwa mtaalam huyo alizungumza na yule mfasiri tuliye mtafuta malawi na kafwata yule tulietoka nae Njombe ili kumfikishia bibi kile kinachozungumzwa na mtaalam bibi alitoa kiasi cha pesa japo sikumbuki ilikuwa kiasi gani tulianza safari siku ileile kurudi bibi alimlipa mfasiri wa kimalawi na akatutakia kila lakher tukafika kyela muda kama wa saa mbili usiku hatimae siku yapili tukafika Njombe salama salimini kwakuwa tulifika usiku pia tulilala wakati hu mama tulikuwa tukiishi nae pale kwa bibi akiwa katika hali ileile.
Bibi aliniambia tukaokote kuni kumbe niliku sijui kuna dawa alipewa aniwekee kwa njia ambayo mimi nisinge jua basi bibi akani ambia nivute ukuni fulani niliuvuta kwa nguvu maana nilianza kwa kusifiwa nilipo uvuta kwa nguvu nilianguka na kuna kijiti kianiingia mguun na kilikuwa kikubwa mithili ya size ya kidole cha mtoto mchanga kumbe bibi alishaju kinachotokea maana alipewa maelekezo ilinivuja dam nikajisikia kupoteza fahamu nikiwa chini ilikuwa kama naota njozi nyingi na zakutisha ghafla nilijikuta nyumbani na bibi yupo pembeni yangu ilinishangaza ila nikaipotezea kwa sababu ya hali ya utoto niliyokuwa nayo …..
Bibi alitibu kidonda kwa mkojo na kijiti kikiwa ndani nikapona na maisha yakaendelea nikaanza shule nikiwa na miaka saba baba yangu alikuja kuniangalia kwa mara ya kwanza nikaongea nae akasema atanipeleka nyumbani nikasome kule.
Shuleni nilikuwa vizuri na nilikuwa naongoza darasa japo nilikuwa mnyonge kutokana na hali duni ya kimaisha….Wakati huo baba aliacha kazi yake ya ualimu akaingia kwenye siasa na yule mama mdogo akapata mtoto wa pili wakati huo kaka na dada angu walikuwa wakiishi na ndugu wa baba kwahiyo nao hawakuishi na baba pia…..
Mwaka wa pili nikaanza darasa la pili nikiwa na miaka nane huku mawasiliano kati ya baba na ndugu wa mama yalikuwa yakienda vizur juu ya baba kuja kunichukua hatimae siku ikafika baba alikuja na ndugu zake baba akapangiwa gharama ya matunzo yangu nakumbuka ilikuwa elfu sabini lakini baba alikataa hivyo mazungumzo juu yakunichukua yakaishia hapo baba akarudi na ndugu zake kwao.
Baada ya wao kwenda tuliendea na maisha japo yalikuwa magumu sana hata chai tu sikuijua Mjomba wangu(dada wa mama)alianza kufuatilia stahiki za mama kazini maana alistaafishwa japo muda wake wa kustaafu ulikuwa bado, Mjomba alifanikiwa na kikao cha familiar kilimpendekeza yeye kusimamia mafao ya mama alipozichukua zile pesa alipotea nyumbani hakuonekana kwa muda wa miezi 6 hapo tukaanza kupata taarifa kuwa yupo nchini Malawi anafanya biashara ya mbao.
Wakati ule hata simu hazikuwepo mawasiliano ilikuwa ni barua maisha yalizidi kuwa magumu bibi jicho moja likapoteza uwezo wa kuona na alishakuwa mzee na ndugu zake hawakuwa na msaada kwake kwakuwa alisha nikinga akaamua anipeleke kwa baba nakumbuka tulitembea kwa miguu mpaka tulifika pale kwa baba mambo yalikuwa safi ila iliniuma siku ya pili nilipokuwa nikiagana na bibi akiwa anataka kuanza safari ya kurudi peke yake tena kwa miguu ilihali mimi ndio msaada wake nilitamani kuondoka nae ila sikuwa na lakufanya nikabaki kiufupi nilikuwa tofaut sana na watoto wa mama mdogo maana mm sikuwa na nguo nzuri na sikuw na viatu kama wenzangu.
Nilianza kwenda shule darasa la pili ilikuwa mwezi wa tisa tulifanya mitihani ya kufungia shule katika mtihani ule nilikuwa wa tatu katika wanafunzi hamsini na tatu ķwakuwa niliketi benchi moja na aliyeongoza darasa iliaminika kuwa nimeangalia majibu kwake nilikuwa nasemwa kila sehem walimu pia waliamini hivyo wale wadogo zangu walienda kusimulia nyumbani wakati huo baba alikuwa amesafiri kwenye shughuli zake za siasa mama mdogo aliniadhibu vikali kwa ajili ya huo uvumi wa kuangalia majibu kilichoniuma zaidi sio viboko ni matamshi ya mama mdogo akiwa ananiadhibu nanukuu”ivi wewe ni mtoto wa……….(anataja jina la baba)mbona wenzio wana akili nilihuzunika sana nikamkumbuka bibi japo maisha ya kwa bibi yalikuw magumu.
Maisha yaliendelea hatimae nikahitimu darasa la saba japo kwa shida nikaanza form one kwenye shule moja ya kata, nilipofika form two nikaachishwa shule nikaanza maisha ya mtaani nikaamua kufanya kazi kwa bidii maana nilikuwa najitegemea kwa baba nimetoka nilifuga kuku sana.
Miaka miwili baadae nikachukua form kwenye shule moja mjini Njombe niliijaza na nikaambiwa kuna mtihani wa usail yaan interview sikuwa nimesoma chochote siku ya mtihani nikaenda mitihani yote niliona ntafeli isipo kuwa English na kiswahili masomo haya yote sikukosa hata swali moja kilicho nihuzunisha ile siku ya mtihani kwenye karatasi ya mtihani wa kiswahili kulikuwa na kutunga habari ya maneno mengi sana tatizo likawa kile kichwa cha hiyo habari kilikuwa NINGEKUWA KWETU hisia zikanipeleka kama ningekuwa kwetu kwa bibi niliiandika habari ile kwa hisia hali iliyopelekea mwalimu wa somo kuniita na kuniuliza nakumbuka nililia sana alhamdulilah nikapata nafasi ya kuanza masomo.
INAENDELEA………