JINSI NILIVYO TOBOA MAISHA
Episode 07
Tulifika hadi chumbani Amani alianza kuongea na simu kwanza kama dakika kumi π§
Baada ya kumaliza alivuta droo
“Geukia nyuma unataka uone jinsi navyotoa pesa π…”
Niligeuka nyuma nikawa nasikia tu harufu ya pesa zikinukia….ukiwa na shida na hela hata shilingi mia tano utaikariri harufu yake π
“Geuka….” Amani aliongea, yaani alikuwa ananiamrisha kama mfugo wake hivi π
Mie tena huyu niligeuka nikakutana na noti nyekundu zikiwa zimepangwa π
Nilisubiri kuambiwa nichukue lakini haikuwa hivyo nilibaki kusimama hadi nikahisi miguu inauma π
“Khaaa!! yaani wewe hii ni pesa yako, ni jasho lako si uchukue au mpaka nikuruhusu π” Amani aliuliza
Sikutaka kumjibu nilikusanya hela zote kwa heshima baada ya kumaliza kuzibeba nilimuomba Amani anisaidie kufungua mlango π€©
Amani alisimama akanifungulia mlango…. nilienda mpaka chumbani kwangu nikaanza kulia kwanza π
Zilikuwa ni pesa nyingi sana sijawahi kuzishika…niliwakumbuka wazazi wangu vile Mzee Mpemba anapenda kucheza kamali nilifikiria kutuma hela akaweke heshima kwenye meza π
Nilimfuata Bibi nikamuomba ruhusa kuhusu kutuma pesa nyumbani, si unajua tena nipo kwenye nyumba za watu siwezi kuondoka bila kuaga β
“Amani anaenda mjini mpatie namba ataenda kukuwekea…” Bibi aliongea huku akisoma gazeti, miwani aliyokuwa amevaa sasa utaelewa tu kuwa enzi zake alikuwa ni sister duu π
Niliogopa kwenda kumuongelesha Amani π«
“Haya niachie hizo namba nitamuelekeza…” Bibi aliongea baada ya kuona nimekaa kimya,
nilimpatia namba kisha nikaenda nje kumwagilizia maua
Jet alikuja karibu yangu alishanizoea hadi ikawa kero toka ile siku nimemchezesha basi kaniona kama Bibi yake
nilimwagilia maua mpaka nilipomaliza….Jet alinifata….niliamua kumtengenezea ka skafu kadogo ka shingoni nilikawekea urembo kisha nikamvalisha π
“Nataka kulala nenda nje…” niliongea na Jet baada ya kuelewa aliondoka… nilijitupa kitandani nikaanza kusinzia…nilianza kuota nikiwa naendesha gari la thamani mara na hojiwa na waandishi wa habari….
nilikuja kushtuliwa na hodi
alikuwa ni Dada Toshi π€
“Unaitwa nje na Bibi”
Niliamka nikaenda, Bibi alikuwa amekaa bustanini
“Bibi umeniita…” Niliongea kwa utii
“Eeh kaa hapo Scola…”
Nilikaa baada ya kuruhusiwa
“Ilikuaje ukafeli shule…”
Swali gumu hili jamani, nilishindwa nijibu nini lakini nilijua pa kuanzia π
“Nilikuwa sihudhurii darasani kwa wakati…. mara nyingi nilikuwa na kaa kwa kina Sara kumtazama Mr’s Hudson….”
Bibi alicheka
“Hakika ulikuwa mtumwa wake… Scola gauni umetengeneza vizuri sana Michael anataka umtengenezee magauni 20 size kama ya Marie lakini rangi tofauti…. nitakupunguzia kazi za hapa….kesho ni happy birthday ya mtoto wa rafiki yangu…wameomba waje wafanyie hapa kila kitu nitaandaa Mimi ndio maana nimetuma Wafanyakazi baadhi wakanunue mahitajiβ” Bibi aliongea
Jet alikuja sehemu tuliyokuwa
“Nani kakuzawadia ka skafu kazuri hivi….au Marie kakuletea π²” Bibi aliuliza huku akimshika shika Jet
“Nimemtengenezea Mimi…” Nilijitaja
Bibi alifurahi
“Unajua vitu vingi hakika….nina marafiki zangu wengi wakiona Jet alivyopendeza watataka pia….ngoja nimpige picha nimuweke status…” Bibi aliongea,
Jet kusikia picha alikaa pozi zuri nilijikuta nikicheka π
“Scola…..nilitaka kukuambia utengeneze cake kama ya siku zile…hapa watu kesho watajaa…hata nyie mkimaliza kazi mrekebishe nywele zenu…tena ikiwezekana mdizaini sare nzuri…..” Bibi aliongea, hakuwa na choyo kama watu wengine π€©
“Sawa Bibi…” Mie huyu niliitika kwa utii
“Nimemuagiza Amani akakurushie pesa, siku nyingine wala usimuogope Mjukuu wangu hana shida yoyote β…” Bibi aliongea
“Nashukuru sana, nitajitahidi kumzoea…” Nilisema kisha nikaomba ruhusa nielekee ndani, ilikuwa ni mwendo wa kuomba ruhusa tu kama nipo shuleni π
Episode 08
Tulianza kutengeneza vitu tofauti tofauti kwa ajili ya kesho……vilikuwa ni vitu vingi sana mpaka wote tukachoka π₯±…..tulimaliza kazi ya pamoja muda ukiwa umeenda sana
Nikiwa jikoni nachemsha maziwa kwa ajili ya kutengenezea cake…Amani alileta vyombo vilivyokwisha kutumika, nilitamani kumuuliza kama pesa alituma kwa usahihi lakini niliogopa….namba ya Baba jina huwa linasoma Mpemba sasa sijui ndio limesoma hivyo hivyo nilizidi kujiuliza π
“Ukimaliza kazi njoo bustanini nina salamu zako” Amani aliongea kisha akatoka
Kusikia hivi nilijua tu ni salamu toka kwa Baba nilienda kumuita Dada Toshi anisaidie kuangalia maziwa kwani yalikuwa mengi sana na hayakuwa na dalili ya kuchemka….Dada Toshi hakukataa π€
Nilienda bustanini nikamkuta Amani katulia
“Kaa hapo…”Amani aliongea
Nilikaa
“Pesa nilituma jina likaja Mpemba…”
“Ndiyo lenyewe ahsante sana π..”
“Kwanini umetoroka kwenu?……Bibi anajua kama kwenu ulitoroka π₯΄” Amani aliuliza
Niliinamisha kichwa kama kondoo aliyepoteza kumbukumbu
“Bibi hajui…” Niliongea kwa kutia huruma π€
“Baba yako kalalamika sana….ila baada ya kumtumia pesa alishukuru…nilimpigia simu kwanza kisha ndio nikatuma….kwanini ulitoroka kwenu au uliacha umeua huko ukaja kujificha hapa…” Amani alishikiria hapo hapo π«
Nilikaa kimya
Amani alinigonga kichwani na funguo baada ya kuona sijibu π ni kama alikuwa ana kumbusha nijibu swali lake
“Nilifeli shule mtaa mzima wakawa wananicheka….hadi mifugo ya nyumbani ilikuwa inanidharau hata kama ningeifukuza kwa kutumia mawe haikusikia ndio maana nikaona ni heri nitoroke” nilijielezea kwa heshima π
“Siku zote wasichana wazuri kichwani wanakuwaga tupu…..kwa uzuri ulionao hata kama ungesomea kanisani au msikitini ungefeli tu, pisi kali na sifuri huwa ni damu damu” Amani aliongea akinisukuma sukuma kichwa π«
Nilivumilia yote kwa sababu kama ningeongea kibarua kingeota nyasi
“Una miaka mingapi….”
“23….”
“Bila shaka ulichelewa kuanza shule au mkono wako ulikuwa haufiki begani si ndio utaratibu wa vijijini π….pengine ulifika lakini kwa kuwa ulikuwa haujui kusoma ukawa unarudia rudia darasa…..miaka 23 ulipaswa uwe chuo kikuu mwaka wa 3……kichwa hii haina akili” Amani akiendelea kunisukuma sukuma kichwa mpaka nikawa naona giza π
“Haya nenda nilikuwa nakupa salamu za Baba yako….”
Baada ya kusikia nimeruhusiwa kwenda nilisimama haraka π
“Subiri kuna kiboksi nimekuja nacho kipo kule mnakonyoshea nguo kaniletee sina usingizi nataka nifanye kazi kidogo” Amani aliniagiza
Nilienda kwa kukimbia, yaani ni kama nilikuwa najipendekeza asije kunishtaki kwa Bibi yake kuwa nimetoroka kwetu π₯΄….niliingia ndani nikakitafuta kiboksi baada ya kukipata nilirudi bustanini kwa kukimbia, Amani hakuepo
niliangaza angaza macho lakini sikumuona. Niliogopa nikihisi nimechelewa pamoja na kwenda na kurudi kwa kukimbia π
“Kaenda library….mpelekee huko” Mlinzi wa zamu akiwa ana kagua kagua mazingira aliniambia
“Library?.. hii nyumba ina library… ah Bibi alinionesha” Nilijisemea baada ya kutuliza fuvu langu.
Sikutaka kupoteza muda nilielekea ndani kwa kukimbia….nilianza kupanda ngazi nikiitafuta library…. baada ya kuiona niliingia….nilimkuta Amani akiwa anasoma β
“Boksi hili hapa….” Nilisema kwa adabu nikaweka mezani
“Kuna kitabu cha Mfalme Kima….ngazi ya juu..chukua unisomee….saa saba hii unataka ukalale” Amani aliongea π«
Nilitamani kulia yaani nianze kumsomea kitabu wakati kesho natakiwa niamke mapema…..niliona ujinga βΉ
“Sijui kusoma….” Nilikomoa π
Amani alishangaa
“Hujui kusoma??..”
“ndiyo……”
“Basi kaa nikusomee Mimi…. nipatie kitabu” Amani aliongea
Sikuelewa kwanini ananiganda kama kupe…..nilimpatia kitabu
kwa usingizi niliokuwa nao sijui ilikuaje nilikuja kushtuka nikiwa chumbani kwangu π
Nilitoka haraka nikaenda jikoni…nje watu walikuwa wengi wakirekebisha mazingira…..nilianza kutengeneza keki akili zote niliwekeza hapa….muda wote Amani alikuwa ananitazama nililijua hili kupitia jicho la wizi sikutaka kumuonesha kama najua yupo π€
Nilimaliza kutengeneza cake nikaanza kuchanganya rangi ya kuweka kwenye cake…kwa jicho la pembeni bado nilimuona Amani……si unajua ukishagundua kuna mtu pembeni anakutazama basi ubize ndio huwa mwingi π
Simu ya Amani iliita alipokea kisha akaondoka, kidogo nilipumua maana nilikuwa nimejibana hata kukohoa….yaani hata kuachia mashuzi ulikuwa ni msala. π
Dada Toshi alikuja
“Mbona Amani alikuwa anakutazama sana kuna nini…”
“Hata sijui….”
“Ulivo kazuri labda anakutaka….ila uwe makini mdogo wangu hawa watoto wa matajiri tabia zao huwa siyo nzuri……na hivi upo unafanya kazi hapa basi anahisi una shida kuliko watu wote duniani β”
“Sawa Dada Toshi nimekuelewa….nimeona mmenunua ile mashine ya kunyoshea nywele ni wewe au Bibi kanunua”
“Bibi kasema tujipendezeshe hii happy birthday ya leo acha tu….kuna vitu vingi vya urembo Bibi kaweka chumbani kwangu…. malizia hapa tukajiweke sawa….”
Dada Toshi aliondoka…..baada ya kumaliza nilienda kuihifadhi cake chumbani kwa Bibi sikutaka watu waanze kuidokoa π
Niliingia chumbani kwa Dada Toshi na Wafanyakazi wengine wa kike walikuepo tulianza kujipamba
Dada Toshi alikuwa bingwa sana wa kudizaini nywele…. hakika tulipendeza
Bibi alikuwa katununulia sare mpya
“Scola utasaidiana na Toshi kusogeza cake pale mbele yaani kuanzia sasa na kuwa busy sana naomba msiniangushe” Bibi aliongea kisha akaondoka
Nilienda chumbani kwangu kupumzika kidogo…. nilianza kufikiria kuhusu oda alizoweka Michael
kabla hata sijamaliza kufikiria vizuri mlango wangu uligongwa nilienda kufungua alikuwa ni Amani π
“Naomba uninyoshee hili shati usiliunguze” Amani kwa kunitupia utadhani tuna ugomvi vile π₯΄
Episode 09
Nilipokea shati baada ya kutupiwa sikutaka kwenda kunyooshea kule paliko zoeleka…. nilichukua pasi nikaweka shati kitandani… tobaa!! shati lilikuwa lishaungua hata kabla ya kunyooshwa π«
Sikuelewa kwanini Amani ananiletea shati lilioungua halafu anasema nisiliunguze…nilimfuata chumbani kwake lakini hakuepo
nilifika hadi sebuleni nikamuona akiwa anaongea na wageni sijui ni marafiki zake anajua yeye….vile sebule ya Bibi ni kubwa kama ukumbi wa kufanyia kitchen party ilikuwa ni ngumu watu kujua kama nina shida na Amani
sikutaka kumsumbua sana nilirudi kuliangalia shati tena pengine macho yangu yalikuwa na wenge..hali ilikuwa ni ile ile π΅
Amani alikuja mlango ulikuwa wazi, hivyo aliingia bila kubisha hodi
“Umeunguza shati langu eeh…nasikia harufu ya kitu kama kimeungua hivi” Amani aliongea huku akichungulia chungulia π€₯
“Umenipa shati likiwa limeungua tayari” Nilisema nikiwa nimemkazia macho π
Amani alilishika shati lake
“Umeunguza hili shati sasa hivi tu, hiki kilema na cha huu muda..” Amani aliendelea kunisingizia
nilikaa kimya sikuwa na cha kuongea π€
“Ooh nimekumbuka nililiunguza mwenyewe kwa bahati mbaya…. njoo unitafutie shati lingine….halafu Michael kaja pia anataka muongee kuhusu oda alizosema” Amani aliongea
Sikujibu kitu nilimfuata kwa nyuma nilikuwa nimenuna aisee π…tuliingia chumbani nikaanza kumtafutia shati nyingine…
“Utavaa hili….” Nilimuonyesha nikiwa bado na ghadhabu π€₯
“Nichagulie lolote zuri…..huna haja ya kuniuliza na acha kununa utaharibu mapambo uliyoweka usoni”
“Utavaa hili…” Nilimchagulia
Amani hakujibu chochote, ukimya nao ni jibu sikutaka kumsemesha tena.
Nilichukua pasi nikamnyoshea pale pale kisha nikamkabidhi
“Michael kasema tunaonana saa ngapi” Nilimuuliza
“Happy birthday ikiisha nitamkumbusha…”
“Ah sawa…” Nilisema nikataka kuondoka…Amani alinizuia kwa kunishika. Ni kama nilipigwa ganzi mwili mzima, pengine ni kwa sababu nina muda mrefu bila kushikwa na Mwanaume π
“Hapa kuna Wafanyakazi wengi acha kujitoa kiasi hicho,…lala hapo usinzie kabisa…” Amina aliongea
Nilishtuka, macho yalinitoka kama nimeambiwa nimtukane Mzee Mpemba.
Ni kama huyu jamaa alikuwa ananitengenezea mazingira ya kufukuzwa kazi π΅
“Lala hapo kwani sijaeleweka….nitakuja kukuamsha baada ya masaa 2…macho yamekuwa mekundu sababu ya usingizi….”Amani aliongea kisha akaondoka π
Sikutaka kudanganyika eti nilale kibarua kiote nyasi, nilienda kufungua mlango ni kaendelee na majukumu nilichoka baada ya kujua kaufunga mlango kwa nje π« kwahiyo anataka nilale chumbani kwake, mbona ni msala jamani
Nilishindwa kumuelewa kabisa….nilifata amri yake nikapanda kitandani, nilisinzia kabisa kitanda kilikuwa kina vutia godoro laini kuliko kawaida
sijui ilikuaje lakini nilikuja kushtuliwa na vurugu za Jet…niliamka nikafumbua macho Amani hakuepo β
Jet alikuwa ana nivuta vuta niligundua katumwa aje kuniamsha…..nilitoka kitandani,
nilijiangalia kwenye kioo sikuwa na dosari tuliongozana na Jet π€
Dada Toshi aliniita tukachukua cake tuliipeleka mbele…watu walikuwa ni wengi sana utafikiri kuna harusi
sherehe ilianza rasmi zilikuwa ni vurugu za kila rangi
Nikiwa nimesimama Mfanyakazi wa kiume ambaye mara nyingi tunapenda kumuita Mkoloni maana huwa anatupelekesha sana alininong’oneza masikioni π©
“Amani ana kuita jikoni”
Nilishtuka jamani, huyu Mjukuu wa Boss hanipi kupumzika sasa, niliondoka nikaelekea jikoni nilimkuta Amani kasimama
“Nipikie ugali sijisikii kula vyakula mlivyopika…”
Nilichoka kwa kifupi Amani kashanifanya Mimi kama mfanyakazi wake binafsi na si Mfanyakazi wa wote…maana kila kitu ni Mimi π
Nilichukua sufuria kwa hasira kisha ni kaweka maji…hakutaka kuondoka jikoni alinisimamia β….nilipika ugali mpaka ukaiva nilimuwekea kwenye sahani akae kula hapa hapa jikoni. Sikuwa na story naye tena ile nataka kuondoka alinizuia
“Kwenu ndio umefundishwa hivi?…onja hiki chakula kama kina sumu ufe kwanza wewe π₯΄…” Mwanaume huyu ana gubu jamani kwani wakati napika ugali si alikuwa ananiona.
Sikutaka kelele naye,
nilichukua ugali na mboga nikaonja
“Haya ondoka…” alisema baada ya kuona nimekula.
Nilibetua mdomo kimya kimya kama angeniona nadhani ungekuwa ni ugomvi wa kudumu.
Nilirudi kwenye sherehe
muda wa chakula ulifika Wafanyakazi wote tulianza kuwagawia watu chakula π§
Marie mtoto wa Bibi aliniona alinitoa pale tulipokuwa tunagawa chakula tulienda chamber kidogo
“Scola gauni lako mume wangu mtarajiwa kalipenda kweli….naomba wewe pia ushiriki kwenye harusi yangu….ujue watu wengi hawa kujui nataka nikupromote kwa namna hiyo….siku ya harusi naomba ukae nyuma yangu….kuna rafiki yangu nilitegemea atakaa nyuma yangu…. bahati mbaya Mama yake anaumwa sana….nishaongea na Mama kuhusu hili” aliongea Marie kwa ushawishi π€
“Sawa Dada…” Nilikubali ilikuwa ni bahati ya kipekee
“Okay tutaonana…hii sherehe ni muhimu sipaswi kupitwa” Marie kisha akaondoka
Niliishia kujishika mashavuzi, furaha niliyokuwa naisikia ndani ya moyo wangu ilikuwa kubwa sana ππππ
Episode 10
Amani alinikutanisha na Michael ilikuwa ni jioni sana kama saa tatu hivi, mapigo ya moyo wangu yalikuwa juu sana asikuambie mtu π΅
“Nashindwa kuamini kama wewe ndio ulitengeneza lile gauni β….” Michael aliongea baada ya kuniona
Unajua hata Mimi sielewi kwanini nimekuwa na ujuzi wa kubuni vitu vingi pengine labda mzuka wa Mr’s Hudson unaishi ndani ya mwili wangu π kuna muda najiogopa aisee
Michael alimwaga sifa zote mwisho akataka nitamke bei
sijui ilikuaje ila nilimtazama Amani anisaidie kupanga bei π€₯
“Nguo aliyo mtengenezea Marie sijawahi kuiona wewe mwenyewe ni shahidi….sema imekuwa ghafla sana alipaswa auze nguo zikiwa na jina lake….hiyo ni hasara kwa mara ya kwanza… katika hili wewe ndio utafaidi najua upo bingwa wa kupaste vitu vingi… kama Scola akikupatia nguo 20 najua utazadhalisha nguo nyingi kisha utapata faida…..kwa hiyo ongea bei ya uhakika ambayo haitamuumiza Scola kabla hatujakuoangia bei β”Amani aliongea kwa niaba yangu
Michael alijikuna kichwani kisha akatabasamu
“Nitamlipa kwa bei ya uhakika nadhani unanifahamu sipendi kuwatia hasara wengine….tuonane kwa wakati mwingine” Michael aliaga akaondoka π΅
“Mbona hajataja bei…” Nilimuuliza Amani kwa mshangao
“Atakulipa pesa nyingi ndio maana hajaongea….hapa kuna watu wengi siyo sahihi kutamka idadi ya pesa” Amani kwa sauti ya chini π₯±
Nilikaa kimya baada ya kuelewa….. niliona hakuna maongezi ya maana nilitaka kuondoka Amani hakuniruhusu
“Kaa….mbona unapenda kunikimbia, mara nyingi ukiwa na Mimi unaonekana kukosa utulivu π₯΄”
Nilikaa baada ya kuambiwa, ukweli mapigo ya moyo yangu yalikuwa yana dunda hovyo hovyo π
Tulikaa kimya kama tumepigwa marufuku kuongea…. Amani alikuwa katulia tu kama jambazi anayefikiria wapi akavunje mlango π
Muda ulizidi kwenda nilianza kuhisi baridi
Mama alishawahi kuniambia nijali mwili wangu kwa sababu ni wa kwangu kama nikiuumiza Mimi ndio nitakayeingia gharama kuutibu….nilivunja ukimya π₯΄
“Hapa kuna baridi….” Niliongea
“Unataka kuwa nani?….nilikuwa na kufikiria hapa nimegundua unajua vitu vingi” Amani aliongea vitu vya maana
“Nataka niwe zaidi ya Mr’s Hudson….” Nilijibu bila kuzingatia baridi β
Amani alitabasamu
“Kama una uhakika na kitu unachosema nitakusaidia kukupandisha juu…..nina pesa nyingi sana lakini huwa sipendi kuitumia vibaya…. kama nikizitumia kukusaidia naomba uwe na uhakika wa kutimiza kile unachokisema….unaweza hisi katika hii nyumba tunatumia pesa vibaya…. hapana pesa zote zinazotumika hapa huwa zipo kwenye mahesabu…..so kama upo na nia kweli kesho asubuhi nitafute…..najua namna ya kumsaidia mtu kufikia malengo yake……usiku mwema” Amani kisha akaondoka π
Aliniacha nikitafakari ingawa mwanzo nilihisi baridi lakini nilianza kuhisi joto kutokana na vitu vizuri nilivyo ambiwa
Niliamua kuingia ndani baada ya kuchoka kukaa nje pekee yangu…nilimpita Amani sebuleni akiwa ana angalia TV na Bibi.
Bibi baada ya kuniona aliniita
“Scola….Marie kaomba umsindikize kwenye harusi yake…..harusi yenyewe ishafika ni wiki ijayo, kesho Amani akupeleke kwa Dada yake mkafahamiane vizuri….. sasa hivi Amani hajaanza kuwa busy ndio maana namuagiza kila sehemu π”
“Sawa Bibi….” Niliitikia, nyie nilitaka kukimbia baada ya macho yangu kugongana na ya Amani
“Cake ilikuwa nzuri sana sijawaambia kama imetengenezewa hapa wangeanza kunisumbua na Mimi usumbufu huwa sipendi…… haya nenda ukalale leo mmenifurahisha sana π₯°” Bibi aliongea
Ile na simama hivi nilikutana na macho ya Amani kwa mara nyingine….nilihisi kushtuka mwili wote lakini nilijikaza πͺ
Nilikuwa nimechoka kwa kiasi fulani baada ya kupanda kitandani nilijifunika shuka gubi gubi
Nilianza kujiuliza kwanini Amani anakuwa ananiangalia hivyo tena siyo mara moja nikasema ni bahati mbaya au ananitamani nilivyo nilijifikiria bila kupata majibu π
Nikiwa najigeuza geuza kitandani nilihisi nimelalia kitu niliamka nione kitu gani nimelalia.
Tobaaaa! zilikuwa ni pesa nyingi zimefunikiwa t-shirt sikuelewa hata kwanini harufu ya pesa sikuisikia au ndio nishaanza kuwa tajiri…niliogopa kuzishika nilihisi huenda ni mtego Amani kaniwekea ili ajue kama nina dalili za wizi au la π€π€π€
Episode 11
Nilienda sebuleni kwa gia ya kutafuta maji lengo langu lilikuwa ni kumuangalia Amani ikiwezekana nimwambie kama na shida naye π
Amani hakuepo sebuleni nilifahamu fika atakuwa chumbani kwake…. nilienda nikamgongea….zilipita dakika mbili ndio mlango ukafunguliwa alikuwa bado hajalala
“Umejisahau ukaweka pesa zako chumbani kwangu” Nilijielezea β
“Mie huyu nisahau pesa π vipi unahisi Mimi naweza kusahau pesa” Aliniuliza
Nilikosa jibu
“Bibi bado hajawapatia mshahara nimekupa hiyo pesa kama pesa ya matumizi”
Macho yalinitoka yaani pesa zote zile kanipatia bure nilibaki nikitafakari kwa kumtazama π§
“Na usingizi nataka kulala…. kesho asubuhi nitakupeleka kwa Dada Marie… kabla ya hapo naomba utanipatia mchanganuo kuhusu kile tulichoongea usiku wa jana….halafu subiri kwanini ulinidanganya hujui kusoma….ile cake uliipamba kwa maneno mazuri mbona π₯΄” Amani aliniuliza
Nilikosa jibu
“Ah uliona kama ningefaidi sauti yako…. ningekulipa sipendi vitu vya bure….nenda ukalale”Amani aliniambia π€₯
Ile naondoka alinirudisha…yaani hakuna siku nilishawahi kuondoka bila kurudishwa
“Abeee….”
“Sogea…” Aliniambia
Nilisogea akaanza kuutazama mguu wangu π©
“Kuna kiatu nilikinunua ile siku naenda kukurushia hela….nilifanya kubahatisha…hebu subiri” Alisema kisha akasimama..alienda kufungua kabati lake alitoa viatu vizuri sana kiasi kwamba nilipiga dua vinitoshe π€Έ
Alinivalisha kimoja, yaani alinifanya kama katoto kake hivi, bahati nzuri vilinitosha, nilifurahi sana ndani ya moyo wangu ukiachana na vile viatu alininunuliaga mara ya kwanza vilikuwa ni vikubwa π
“Kwanini unanipa vitu vyote hivi” Niliamua kumuuliza
“Una stahili kuwa na hivi vitu navyokupatia au una swali lingine π₯΄…”
“Hapana…..”
“Nenda ukalale…” Amani aliongea
Niliondoka, sijui alifikiria nini siku ya leo alikuja kunifungulia mlango kisha alinibusu kwenye paji la uso
“Usiku mwema…naomba uote ukiwa una kimbizwa na watu wasiojulikana, oh no naomba uote ukiwa una kimbizwa na Baba yako kwa kosa la kumtoroka β” Amani aliongea kisha akafunga mlango
Sikuamini kama kanibusu nilitembea nikiwa nimetekewa
nilifika chumbani kwangu nikalala kwa mshangao mkubwa…huwa na tabia ya kuamka usiku kukojoa lakini sikuamka kabisa π.. Bibi alikuja kunigongea mida ya asubuhi
“Aah Scola leo umechelewa kuamka…. Amani yupo sebuleni ana kusubiri muende kwa Marie”
niliamka nikamfungulia mlango Bibi kisha nikamsalimia kwanza
“Mbona tumbo leo halionekani….jamani hebu oga ukanywe chai leo nimepika Mimi… halafu utaniambia nimejitahidi kwa kiasi gani usinione nimekaa kama Boss najua kupika.. sema huu ndio muda na Mimi wa kuheshimiwa na kupumzika π”Bibi alijinadi
Nilifurahi kwa maneno yake nilienda bafuni kuoga…baada ya kumaliza nilienda kunywa chai
Amani alikuwa busy kuandika kwenye laptop nilimsalimia…aliitikia kisha akaendelea na mambo yake
nilianza kunywa chai lakini baada ya kukumbuka busu la usiku, nilihisi miguu imekuwa ya baridi utafikiri nimemwagiwa maji ya kwenye friji π€
Niliachana na unywaji wa chai nilibeba vikombe vilivyokuwa mezani nikavipeleka kabatini..
Dada Toshi alinivuta
“Scola ujue una muacha hoi Amani… nimemuona muda mrefu ana kutazama sema ulikuwa hujui…”Toshi aliongea kwa sauti ya chini mwenyewe huwa ni mmbeya kama mie hapa π
Nilibaki kushangaa kusikia namuacha hoi Mjukuu wa Bibi
“Amani alikuwa na demu wake waliachana nahisi sasa hivi imepita miezi 4….demu wake alikuwa hajui kazi yoyote si kupika wala akili ya kutafuta pesa…”
“Wewe umejuaje π”
“Na kuibia siri hiyo tena unaniuliza…..Baba yake na Amani yupo China kama balozi anaiwakilisha Tanzania…. Mama yake yupo pia China kule ana hospital yake….hii familia wana hela ndio maana kila siku Mimi naogea chumvi ya mawe nisije fukuzwa hapa π€, demu wa Amani alikuwa hajui kufua ata nguo yake ya ndani….siku hizi wanaume hawapendi wanawake maandazi wanaosubiriwa kugeuzwa kwenye kikaango…..nilimsikia Bibi ana kusifia….nasemaje Amani atakuwa anataka muanzishe mahusiano” Toshi aliniaminisha π€Έ
Macho yalinitoka tu maana mambo aliyokuwa anaongea ni makubwa
Mkoloni (Mfanyakazi wa kiume) aliingia tukakaa kimya π·
“Na sikia tu visauti vya ajabu kama nyama inaungulia π₯΄…Scola unaitwa na Amani…..Toshi sitaki ugomvi na wewe leo bustani haijamwagiliwa punguza mdomo…..”Mkoloni aliongea
Dada Toshi aliondoka Mimi pia niliondoka huku nikiwaza ni jambo gani Amani ananiitia π
Inaendelea……………..