JINSI NILIVYO TOBOA MAISHA
Episode 22
Tulipark gari kisha tukaongoza hadi ofisini kwa Mkuu wa shule.
Niliona jinsi walimu walivyohaha pengine walihisi sisi ni wakaguzi ๐คฃ
Mkuu wa shule hakuweza nitambua maana nilikuwa sivumi shuleni mtu pekee ambaye alikuwa ananifahamu ni mwalimu wa nidhamu kwani mara nyingi niliandika sana barua baada ya kufumwa na magazeti ya udaku pamoja na karanga nilikuwa mjasiriamali mdogo enzi hizo โ
Sikutaka kumuua mkuu wa shule kwa presha nilijitambulisha kama Balozi wa pads za free style
Mkuu wa shule aliachia tabasamu hadi mwanya ukaonekana, kipindi nasoma sikuwahi kuona mwanya wake
“Karibu sana….”
“Nashukuru, nilisoma hapa kidato cha kwanza mpaka cha nne najua hauwezi nikumbuka nilimaliza 2018 na kina Sara” Niliongea
“Aah Sara Matthew yule alikuwa anawaburuza wote kwenye mitihani ๐ฅด” Alikumbusha
“Ndiyo, sasa hivi Sara yupo nyumbani tu alifukuzwa shule”
“Kwanini alifukuzwa shule…si ndio tulimpa vyeti vyote…cha taaluma…usafi…nidhamu” Mkuu wa shule alianza kunitajia
niliona anataka nimpatie umbeya kamili sikutaka kuonekana paparazi japo ndio hivyo nishamwaga umbeya robo
nakumbuka Sara alipatiwa vyeti vyote mpaka cha michezo wakati hakujua hata kudaka mpira ๐
Mkuu wa shule alionekana kuumia
“Nahitaji kuongea na wanafunzi wa kike naomba unipatie dakika 30 zinatosha…nipo na safari lakini kwa jinsi navyoipenda shule yangu nimeamua kupita”
Mkuu wa shule hakunikatalia
kengele iligongwa wanafunzi wa kike walitoa viti nje nilianza kumwaga sera mwisho niliwaahidi kuwaletea pads za bure
Wengi walitamani kuwa kama Mimi lakini niliwasihi wasome sana, kila mtu ana njia yake ya kufanikiwa โ..tulipiga nao picha kisha niliwaaga, nilirudi ofisini kwa Mkuu wa shule niliwahesabia pesa wanywe soda mpaka ziwakinai.
Amani na Mimi tuliingia kwenye gari safari ya kurudi mjini ilianza
nilikuwa nimechoka kwa kiasi fulani ukizingatia na adhabu ya babu basi nilijikuta nikihisi kichwa kizito
“Lala…siyo lazima unipe company” alisema Amani baada ya kuona nahangaika tu na kizungu zungu cha usingizi
baada ya kuruhusiwa nilijilaza kwenye bega lake ๐
Episode 23
Tulifika mjini nikiwa bado na usingizi… hatukuchua muda mwingi kufika kwa Bibi…aisee Jet ana sifa baada ya kutuona tu alikuja mbio kutupokea
Amani alimbeba kidogo kisha akanipatia na Mimi ๐
“Kawa mzito sana…” Nilisema nikimrusha rusha Jet
Bibi alikuwa kalala baada ya kusikia makelele aliamka
“Oh…Scola za nyumbani..”Aliuliza huku akivaa miwani yake
“Nyumbani wazima wanawasalimia…”
“Oh sawa…basi kapumzikeni…”
Baada ya kuruhusiwa tulienda kupumzika… nililala muda mrefu sana
Bibi alikuja kuniamsha
“Scola leo umelala muda mrefu ๐ค…”
Niligundua Amani hayupo
“Kaoge uchovu uishe la sivyo utalala sana ujue miili huwa hairidhiki…ukimaliza uje na maongezi na wewe โ” Bibi aliongea kisha akaondoka, nilijikuta nikipata shauku ya kujua ni maongezi gani hayo anataka kuzungumza na mie huyu
Niliingia bafuni kuoga…baada ya kumaliza nilianza kupaka lotion nilijikuta nikiichukia ghafla harufu yake ilinitia kichefu chefu…niliacha kupaka lotion nikavaa hivyo hivyo nikaenda kumsikiliza Bibi ๐ค
Baada ya kufika nilimkuta Bibi akisoma gazeti
“Kaa hapo…”Bibi aliongea baada ya kuniona
Nilikaa huku moyo ukizidi kupata presha ya kujua nachotaka kuambiwa ๐
“Kesho Amani anaanza kwenda ofisini si unajua tena ni CEO….sasa ujitahidi kuamka muende clinic nishaongea na Daktari wangu โ”
Nilijikuta natoa macho ๐ฅบ kwa kitendo cha Bibi kuongelea mambo ya clinic
“Clinic kufanyaje Bibi…”
“Heeeh! Scola kwani hujijui kama una mimba….wewe si umepita hapo mlangoni taa ya njano ikawaka…”
Nilijikuta nikishangaa kabisa kwa mara nyingine…..kama ujuavyo tatizo likishagundulika ndo huwa shida…pale pale nilihisi kichefuchefu cha hali ya juu nilitoka mbio kwenda nje…
Kufika huko nilitapika ๐คฎ bila hiari yangu….Jet alinifuata akaanza kunishangaa tu
Bibi alikuja akiwa kabeba maji alinipatia nikajisafisha
“Umekuwa busy muda mrefu ilikuwa ni vigumu kujijua….ona Jet alivyofurahi…mdogo wake yupo njiani” Bibi aliongea akimwagia mwagia Jet maji
Nilijikuta nikicheka kumbe Jet ni mtoto wa Amani wa kwanza ๐
Bibi aliniambia nikae nje nipigwe upepo kwanza
Dada Toshi alikuja macho yake yalikuwa juu juu tu utafikiri mtoto mwenye njaa anayesubiri kugongea chakula cha jirani
“Scola… hakika wewe si mtu wa kuzoeleka…mara hii tu umenasa” Aliongea kwa sauti ya chini
“Sijui ata imekuaje kwa kifupi sikumbuki imeingia saa ngapi ๐ฉ..” Niliongea huku nikiifikiria leba, sijui ulikuwa ni uoga au nini lakini nilijikuta nikiifikiria
Episode 24
“Bibi hachelewi kashapiga simu China wazazi wake Amani wakwe zako wewe wako wanasimuliwa โ….”
Nilibaki kutoa macho tu kumbe hata Bibi hana kifua…. nilikaa muda mrefu bila kumuona Amani…nilimpigia simu mpaka nikachoka simu haikupokelewa ๐ฉ….niliona Amani kaanza kunizoea…kisirani kilipanda ghafla kama siyo kukaa ningedondoka chini.
Nikiwa katika hali ya kisirani nilisikia honi ya gari nilisimama nione ni nani anaingia nilikutana na gari la Amani mpaka moyo ukashtuka sijui ndio uchizi ulikuwa umeanza yaani nilisikia moyo ukidunda kama ngoma za kizaramo โ nilirudi kukaa
Nikiwa nimekaa nilihisi mtu anakuja nyuma yangu… nilijua fika ni Amani niliumusha mashavu kama ngano iliyozidiwa hamira ๐…Amani alikuja kusimama mbele yangu kwa sura aliyokutanana nayo kama si wa kiume angepiga kelele
“Scola mbona umekuwa na sura nzito hivyo shida nini…” Aliuliza
Sikumjibu chochote
alijua tu nimenuna alianza kunibembeleza kwa kunibusu
“Usinune haupendezei…am sorry siku ya leo nilikuwa busy sana..”
Nilijikuta naachia mashavu yangu kiukweli yalikuwa yanauma
nilijua Amani hafahamu kuhusu mimba yake…sikuwa na kichefu chefu lakini nilijitia kusogea mbali nikaanza kuhangaika kutapika ๐คฃ
“Scola una nini…”
“kamuite Bibi sielewi kabisa….”
Amani alimkimbila Bibi…Bibi alikuja upesi
“Scola bado tu kichefu chefu….wee Amani utamuua mwenzio perfume yako itakuwa imemkataa…tangu uondoke anatapika tu…Scola ana mimba โ…” Bibi aliongea
Amani alibaki kuduwaa
“Scola niko nakuandalia supu…Amani hebu mtulize mwenzako huyo mtoto atakuwa na kisirani sana hataki Scola akae”
Amani alinishika kwa heshima zote…hakuwahi kunibeba lakini leo hii Scola nilibebwa mpaka chumbani๐
“Hii perfume sitaitumia tena….Scola ahsante umenifanya nionekane mwanaume sasa” Amani aliongea akinikumbatia
Sikuwa na cha kusema zaidi ya kuringa tu ๐
“Kesho naanza kuingia ofisini… Mimi ni CEO ndio maana nilienda kuweka mambo sawa….” Amani alijielezea
Nilifurahi jinsi alivyokuwa anajielezea
“Nivae nguo gani na kipindi leo…ingekuwa ni maonesho tu ya fashion angeenda Michael au Oscar lakini leo naongea na baadhi ya wabunifu wasiojulikana lazima niende kwani si utanipeleka Baby dady wangu ๐”
Amani alifurahi kuitwa baby dady
alinipeleka bafuni kuniogesha…baada ya kumaliza tulienda sebuleni…. Bibi alinishangaza kauli yake
“Scola nimekuagizia Japan gari kama langu… hakika umejua kunifurahisha eh….niambie kitu gani unataka mbele ya hawa Wafanyakazi ni kutendee ๐”
Nilikaa kimya sikuwa na cha kuomba
“Toshi hebu msaidie mwenzako kuomba”
Toshi alikabiziwa rungu mwenyewe nilifumba tu macho sikutaka kuona Toshi atakavyolipua bomu
“Bibi…. mjengee saluni ya kike ya kisasa itakayo kuwa tofauti na saluni zingine” Toshi aliongea
“Sawa nitatekeleza….Scola nasikia unaenda kazini nenda kajiandae Amani baki hapa na maongezi na wewe… wengine endeleeni na kazi zenu โ”Bibi aliongea
Tuliongozana na Dada Toshi…alinivutia chumbani kwake
“Scola…. kweli wewe umesharidhika…ungeomba hata ndege huyu bibi angekutimizia”
“Toshi vitu vyote hivyo vya nini…”
Toshi alinisogelea sikioni akaanza kumwaga umbeya
“Ujue umemuokoa Amani….watu wengi walihisi labda hana kizazi…usije kutamka hii siri….nimemsikia bibi akiongea na Mama yake Amani kuhusu mimba yako…hakuna aliyeamini….ndio maana nasemaje ungeomba ndege kabisa…wewe huoni Jet anavyoringa hapa anajihisi yeye ndio first born and last born โ…” Dada Toshi alimaliza kuongea sikio lilikuwa limelowa mate utafikiri nilikuwa naoga
“Kajiandae uende….halafu Scola mambo ya saluni nayaelewa sana…natumaini Dada yako Mimi sitasahaulika” Dada Toshi alijiongelesha ๐ค
Nilitabasamu tu nikaenda kuvaa ndani baada ya kumaliza nilitoka nje…Amani alikuwa anaongea na Bibi baada ya kuniona aliomba anipeleke kazini
Bibi alinisisitiza nitembee kwa umakini kabisa nisije pata ajali
Nilifika kazini tayari kwa kuongoza kipindi…sijui nilikuwa na bahati kwa sababu kipindi changu kilizaminiwa na watu wengi niliongea mambo mengi sana na hawa wabunifu wadogo
Baada ya kumaliza nilimpigia simu Amani akaniijia…Mzee Mpemba alinipigia simu kunipongeza namuelewa vizuri baba yangu ni mtu wa kupenda sifa maana nilikuwa na sikia tu kelele bila shaka alikuwa kijiweni ๐
“Naomba usalimiane na jamaa zangu…” Baba aliongea
Nilianza kuongea na jamaa zake mpaka sikio likachemka nilihisi kabisa linatoka mvuke….bahati nzuri baba aliniaga
“Huku mvua imeanza kunyesha wasalimie wote huko” Baba aliongea kisha akakata simu
Amani alikuwa kanisubiria nimalize kuongea na simu nilimuomba anipulize sikio maana lilikuwa na lamoto ๐
Episode 25
Baada ya Amani kunipa huduma ya kwanza tulielekea nyumbani… ile kufika Toshi alinikonyeza jicho la kimbeya sikufanikiwa kumuelewa ana maanisha nini ๐ณ..
Ile tunaingia sebuleni nilikutana na sura mpya ya Mwanamke ambaye sikuwahi kumuona live tofauti na kwenye picha…alikuwa ni Mama yake Amani
“Oh my son…njoo unikumbatie” Aliongea Mama yake Amani
Amani alikumbatiana na Mama yake
baadae nilifuatia Mimi
“Scola kamuamshe Jet aje kusalimiana na Mama yake” Bibi aliongea
Nilienda kumfuata Jet,
Baada ya Jet kumuona Mama yake Amani alimkimbilia
“Woow….Jet wangu kawa mkubwa….” Mama Amani Aliongea
“Mama ulisema unakuja mwezi ujao lakini…” Amani aliongea
“Kila kitu kilibadilika baada ya kuongea na Bibi yako….baba yako atakuja mwezi ujao ingawa atakaa wiki moja lakini nina uhakika kila mmoja atafurahia uwepo wake… uumh watu wangu wa karibu wanawasalimia sana ๐ฅฐ….Amani nafurahi umepata mdada mzuri kuliko hata Mimi” Mama Amani aliongea
Basi ilikuwa furaha kubwa sana siku hiyo sijui hata tulilala saa ngapi maana maneno yalikuwa hayaishi
Siku zilizidi kwenda tumbo nalo lilizidi kusonga mbele..lilikuwa tumbo refu hadi nikawa naogopa
akili yangu ilinituma huenda mtoto aliyeko tumboni ni zaidi ya mtoto wa kiboko ๐ณ
Mama Amani alikuwa ananipa mazoezi kila siku….nilikuwa na hudhuria mara moja moja kwenye Kampuni langu kuangalia maendeleo
Amani alipata kazi sana kwani moyo wangu muda wote ulimtaka kama tu mtoto mchanga anavyopenda nyonyo muda wote โ
Siku moja mida ya asubuhi nikiwa najiangalia kwenye kioo nilihisi maumivu ya ghafla….nilipiga kelele za kuomba msaada…acheni nyie nilikuwa nahisi tumbo linakaangwa kwenye mafuta ya petrol
“Kama nilivyo tarajia….hebu tumuwahishe ni muda wa kubeba mtoto…usimpigie simu Amani atachanganyikiwa โ” Mama Amani aliongea
Nilipelekwa hospital chapu nikaingizwa leba kule nilikuwa pekee yangu bila shaka kilikuwa ni chumba private
Alikuja nesi aliyekunja sura sijui alikuja kunitisha ili nizae haraka…kwani baada ya kumuona tu nilihisi hadi mtoto kashtuka
maumivu yalizidi kuongezeka…sijui ilikuaje nilishtukia napewa kofi la mdomoni ๐ต
Episode 26
“Tanua vizuri miguu….sukumaa”
Uwiii nilijitutumua kusukuma mpaka niliposikia sauti za mtoto akilia ๐ญ….sikuwa na nguvu tena nilikuwa naona majivu jivu tu, sikumbuki hata nini kilitokea
Nilikuja kushtuka Bibi pamoja na Mama yake Amani wakiwa pembeni yangu
“Oh bora umeamka…” Bibi aliongea
“Umezaa mtoto mkubwa aisee ana fanana na Amani” Mama yake Amani aliongea
Nikiwa namshangaa mtoto Amani alifika kabla hata ya salamu aliropoka
“Tumuite Pretty….yes Pretty” aliongea Amani ndipo alipomsogelea mototo wake baada ya kumkagua alinisogelea Mimi ๐
“Pole….najua ilikuwa ngumu lakini umefanya vizuri” Amani aliongea kwa kunibembeleza
Baada ya kuruhusiwa tulirudi nyumbani…. katika swala zima la kukandwa na maji moto sikuwasumbua sana japo mwanzoni nilikuwa nalia ๐ญ
Kadri siku zilivyoenda mtoto wangu alizidi kuwa mnene…hakuwa kiboko tena safari hii alikuwa shangazi yake tembo ๐
Alikuwa mzito kubebeka…mara kwa mara tulienda hospital kumpima afya yake
mtoto alikuwa mzima kabisa…..Bi Moza pamoja na Baba walikuja mjini kwa mara ya kwanza kabisa kumuona mtoto
Mama alibaki mdomo wazi nilipomuambia sijapitishiwa kisu
“Wewe Scola…. acha kuongea uongo…”
“Kweli Mama….”
“Mwanangu kule kijijini siku hizi naheshimika…umejua kutupa heshima sana….Mimi nilijua tu ipo siku mambo yatakuwa mazuri….ahsante sana mwanangu”Mama aliongea hadi chozi likamtoka ๐ญ
Mwanangu kuona chozi yeye pia alianza kulia
“Muache anisaidie kulia Bibi yake nimepitia tuhuma nyingi sana… lia mjukuu wangu” Mama
Nilijikuta nakosa cha kusema kwani nikikumbuka ile siku naambiwa na Sara niliyemtuma kuniangalizia matokeo kuwa nimepata zero nilihisi joto japo sikuwa na akili za darasani
“Mama nashukuru kwa kila jambo ndio maana najitahidi kusaidia watu wengine…. bila hii familia Mimi nisingefika hapa wamekuwa bega kwa bega na Mimi…”
“Mwanangu juhudi zako pia zimekuinua…msaada unafanyika sehemu ambapo kuna juhudi na akili….angalia mtoto uliyezaa ni mzuri sana unafikiri hii familia watashindwa kukupenda ๐….imetosha nikianza kuongea huwa simalizi…baba yako anataka kuongea na wewe ngoja nikamuite” Mama aliongea kisha akatoka nje
Baba yangu baada ya kuitwa alikuja
“Pole mwanangu uzazi una kazi sana….”
“Ahsante Baba…”
“Kesho Mimi na Mama yako tunaondoka….mwanangu endelea na juhudi zako hata kaka yako amekusifu sana…jana alinitafuta nikampa namba zako…kasema hajui lini atapatikana maana anaenda Sudan mambo yao si unayajua”
“Ndiyo Baba…”
“Mwanangu yaani naogopa hata kupokea mahari….Mama Mkwe wako kaahidi atanitumia tractor kumi kwa ajili ya kilimo…sasa nikipokea mahari nitaonekanaje ๐”
“Baba ni haki yako kupokea mahari watu wa hapa hawapendi vitu vya bure…usikatae mahari Baba….sisi bado masikini sana…”
Baba alionekana kuelewa
Baada Ya Mwaka Mmoja ๐ฅ
Mtoto wangu pretty alikuwa kwa kiasi fulani…. jina langu lilizidi kuvuma kila sehemu kama ugonjwa wa Ebola…hakuna sehemu ambayo sikuwa na fahamika…..sikuwa bahiri kiasi hicho nilikuwa nalipia ada wanafunzi wa sekondari zaidi ya mia mbili ambao hawakuwa na uwezo wa kujilipia
kupitia ushauri wa Marie niliamua kuanzisha shindano lililojulikana kama SAKA VIPAJI sikuamini pale ambapo vijana wengi walivyoshiriki ๐….kilikuwa ni kipindi pendwa sana katika Television kwa sababu vipaji vya kila aina vilionyeshwa
Kwa mara ya kwanza nilipewa tuzo kama Mwanamke mwenye karama ya ushawishi……Amani kila siku alikuwa ni mtu wa kunihimiza kuhusu mafanikio yangu
Pamoja na yote haya nitakuwa muongo kama sitamshukuru Mr’s Hudson Mwanamke aliyenifanya nitamani kuwa kama yeye….kwa hili shindano nililoliandaa nimemuandikia barua aweze kushiriki kama mgeni rasmi
Mr’s Hudson kanijibu kuwa atafika….aliniandikia maneno haya ๐
“Nafurahi kuona kuna mtu mmoja anavutiwa na kazi zangu, mpendwa Scola umenifanya nijione dhahabu katika maisha ya watu, Usiwe na shaka nitakuja”
barua ya Mr’s Hudson nimeitunza kwa ajili ya mtoto wangu Pretty…. nataka nimuoneshe jinsi mama yake nilivyojituma bila kuchoka
Nipende kuwaambia kitu kimoja marafiki zangu….kutoboa maisha si lazima ukutane na watu kama Bibi….Amani…Marie au kina Oscar hapana! hebu muangalie mtu aliyefanikiwa alianzaje kufanikiwa .โ…pengine alianza kwa kuuza karanga….lakini mwisho alifanikiwa….. siyo lazima kila mtu ajulikane dunia nzima kama COVID 19……hapana ukishafikia uwezo wa kujitimizia mahitaji yako wewe ni tajiri….kila mtu ana malengo yake kama hauna malengo mpaka dakika hii nakuomba upande kitandani usinzie usingizi kabisa pindi utakapoamka najua utakuwa umepata muafaka wa maisha yako
Please usiseme Scola alitoka kimaisha sababu ya familia ya kina Amani hapana…. kipaji changu ndio kiliniokoa….najua hata wewe hapo una kipaji tafadhali usikalie tu kuwashabiki kwa watu waliofanikiwa, kwanini usitamani kuwa kama wao……anyway nisiongee sana usiku umewadia ni muda wa Mimi kupumzika na mume wangu…. msiniseme nitambemenda mtoto hapana…. niko makini shoga zangu ๐
ย ย ย ย ย ย MWISHO