JINSI NILIVYO TOBOA MAISHA
Episode 17
“Scola huyu ni rafiki yangu nimekaa naye China kwa miaka 2 baadae nilienda Ghana ni rafiki yangu sana…. familia yake na yangu ni marafiki…. anajua sana mambo ya fashion… ni mwalimu mzuri…nimemuomba msaidiane…yeye ana jina tayari so tunachofanya ni kumfilisi au siyo Oscar 😄”Amani aliongea
“Yeah….itabidi kesho tuingie location tumpige picha kama zote nitampost kwenye page yangu…nikisema tufanye kesho kutwa Marie atatutazama vibaya itakuwa siku yake muhimu…au unasemaje 🥴” Oscar aliuliza
“Na kusikiliza wewe….”
“Okay ndio nishaamua….Amani tulia kama ulivyo bill yote ya chakula nalipia Mimi ✋…” Oscar aliongea
Amani alinishika akahisi sijui na baridi alinipatia koti lake
vyakula vililetwa….nilikula kwa adabu zote
Simu ya Oscar iliita hakutaka kupokea
“Amani baadae bwana kwanza tushamalizana…” Oscar aliongea kisha akatupia pesa mezani yule aliondoka 🙄
“Oscar hata apate emergency ya namna gani kama kasema atalipia bill lazima atimize” Amani alimsifia rafiki yake mwenye hereni sikio moja ✋
Nilifikiria ni kitu gani nimuambie, baada ya kupata nilimsogelea masikioni nikaanza kushuka mashairi
“Amani…nakupenda…. wewe ni mzuri sijui umejifikiriaje kunichagua Mimi…. tuseme ni bahati nachanganyikiwa kuona kila kitu unafanya kwa ajili yangu na kuahidi sitafanya vibaya…. ahsante kwa kunisikiliza”nilimaliza kujielezea 😄
Amani alitabasamu
“Ukipata kitu tambua ya kwamba una kitu kinachofanya upate….Bibi yangu mara nyingi alikuwa ananiambia sumaku hunasa sehemu vilipo vitu vinavyo chochea mvutano…..siwezi kutafsiri maana yake sababu najua unaelewa ✋
Tuliendelea kula…. Amani aliniacha alienda kuongea na mhudumu
baadae alirudi kunichukua…tulienda sehemu ya kupumzika
Amani aliweka game kwenye simu yake tulianza kucheza…nilimfunga magoli mengi akabaki kushangaa hajui kama Baba yangu ni mtaalamu wa kamali 🥴
”Hivi Scola una simu wewe…”
“Simu sina…”
”Hovyo kweli….unatakiwa uwe na simu… oh kesho unikumbushe…” Amani aliongea
“Sawa…”
“Zima taa tunalala huku…”
Niliamka nikazima taa…Amani alinikumbatia kwa kunibana utafikiri nimesema nina mpango wa kumtoroka ✋
“Mama yangu yupo China pamoja na Baba… likizo lao limekaribia nimewakumbuka… ujue nimekaa na Bibi yangu muda mrefu kuliko hata wazazi wangu” Amani aliongea
“Sawa….nitafurahi kuwaona nahisi usingizi niache nilale..”
“Umekula chakula kingi sana…haya usiku mwema”
Tuliagana na Amani tukalala…sijui tu ilikuaje nilikuja kushtukia tukiwa vitani..hakuna aliyelewa tumeanzaje lakini hiyo ndio hali halisi 😄
Kesho yake asubuhi simu ya Oscar ilimuamsha Amani
“Twende tukaoge unaenda location sasa hivi…” Amani aliongea
Tulienda bafuni kuoga…uongo mbaya sina tabia ya kukaa bafuni muda mrefu 😁
“Umemaliza tayari?” Aliniuliza baada ya kuniona na chukua taulo
“Ndiyo unataka nirudie tena….nilivyokuwa mdogo nilioga sana sasa hivi na fanya marudio tu” Nilimjibu Amani ambaye ndio kwanza alikuwa anaoga bado…sikutaka kumjali kwani wakati Mimi naoga kazi yake ilikuwa kunitazama 😄
“Haunisaidii…”
“Nitatenga siku rasmi ya kukuogesha sasa hivi tutachelewa”
Amani aliniacha niende….japo nilikuwa napaka mafuta lakini akili yangu iliwaza huko location naenda kuweka pozi gani… au Oscar atanifundisha 🙄 tumbo hadi lilichemka kwa hofu
Episode 18
Amani alitoka bafuni akanikuta nishamaliza kila kitu alivaa haraka haraka…tulitoka nje tukaingia kwenye gari ✋
“Ni picha tu mbona kama una wasiwasi….haujawahi kupiga picha za location 🙄” Amani aliniuliza
“Sikumbuki kama nilishapiga au la” Nilimjibu kikatili Amani baada ya kuona kama ananicheka
“Oscar atakuelekeza kila kitu…yeye ndio anakupiga yuko vizuri…”
Niliitikia kwa kichwa
tulifika sehemu aliyokuwepo Oscar yalikuwa ni mazingira mazuri mpaka unaogopa kutia mguu 🤭
Walikuwepo watu kama watano hivi walinichukua wakaenda kunibadilishia mavazi nilipakwa madude mengi….nilitoka nje
”Wow!..umekuwa mrembo” Oscar aliongea akinipokea kwa mikono miwili sikuruhusiwa kutembea kwa miguu kulikuwa na kigari amazing hivi ndio kilikuwa kinanisogeza kila sehemu 👌….
Mwanzo nilikuwa naogopa ogopa lakini baada ya kupigwa picha tatu tu…nikawa mzoefu hatari…nilibadilishiwa nguo za kila aina mwisho nilipiga picha na Amani
picha zilitoka vizuri
“Scola unapaswa kutengeneza account yako katika mitandao ya kijamii…hizi picha nilizokupiga nazifanyia matangazo…..muda si mrefu utaanza kuingia mkataba na Makampuni makubwa….right now kuna bidhaa mpya ya lotion imetengenezwa nitazipendekeza picha zako…kama wakikubali tu ndio ushatoboa hivyo ✋”Oscar aliongea
Nlijikuta nikihisi kuishiwa nguvu kwa sababu nilikuwa na ndoto ya kuwa mtu fulani hivi lakini sikujua inatimiaje…nilimshika Amani kwa nguvu maana nilihisi kulegea mwili wote
“Tumeshamaliza…twende home Marie kashanitumia text kibao kesho ni siku yake lazima tumsupport” Amani aliongea
tuliondoka tukamuacha Oscar akitoa maelekezo
“Relax najua unahisi kuzimia fulani hivi huu ndio mwanzo siku ya kesho watu watakuwa wengi utafikiri kuna mkutano wa siasa hupaswi kuogopa 😌…”Alinibembeleza baada ya kuniona na tokwa jasho bila mpangilio
Hatimaye iliwadia siku rasmi ya Marie mtoto wa Bibi ingawa tushazoea kumuita Dada yake Amani
Mimi na Marie tuliingizwa chumba maalumu tulipambwa wee mpaka nikawaomba waniache imetosha maana sikuwa mwenye harusi 😄
Gauni alilovaa Marie sikuacha kuliangalia kwa sababu Mimi ndio nililitengeneza….nilijisifu ndani ya moyo wangu
Nakwambia harusi ya Marie ilikuwa na mbwembwe nyingi barabara ilikodishwa watu wengi walifurika….nilisikia fununu kulikuwa hakuna kadi special kama ilivyozoeleka kadi ilikuwa miguu tu na macho yako
Baada ya kuzunguka sehemu zote zilizokusudiwa tulienda ukumbini….kazi yangu ilikuwa ni kuhakikisha Marie hatokwi na jasho….
vurugu zote zilifanyika….kitu kilichonishangaza ni pale Amani aliposhika kipaza sauti alikuwa na wimbo kwa ajili ya Marie 😜
Amani alikuwa na sauti nzuri sikuwahi kufikiria kama anajua kuimba…. tukio kubwa alilonifanyia mpaka nikahisi mlipuko kwenye papuchi yangu ni pale alivyotoa pete mfukoni mwake
“Marie….nisamehe kwa kuingilia ratiba yako but nimeimba wimbo mzuri kwa ajili yako…. naamini utaniruhusu nifanye kitu nilichokusudia…..nampenda Scola najisikia kumvalisha pete hii ya uchumba naweza fanya hivyo” Amani alimuuliza Marie 🤭
Marie aliitikia kwa kichwa watu walishangilia …nilihisi kuchoka… Oscar alikuja kuninyanyua nilipokuwa nimekaa alinisogeza mpaka sehemu alipokuwa kasimama Amani
Amani alinivalisha pete nikiwa siamini….mwanga wa picha ulikuwa unanisumbua hakika
baada ya kuvikwa pete nilirudishwa kukaa mbele….watu walihisi na watazama lakini haikuwa hivyo macho yangu yalikuwa mbali na sehemu hii
Taratibu zingine ziliendelea…pekee yangu tu nilikuwa bado na presha lakini watu wengine walionekana kuwa busy na mambo yanayoendelea
Watu walikula chakula utafikiria kesho walikuwa hawaamki Bibi aliona hatari aliingilia kati
“Kuleni taratibu 😄…..vyakula vipo vya kutosha kila mtu atagawiwa baada ya harusi kumalizika…..”
Watu walimshangilia Bibi kiasi cha kutaka kumbeba….walinzi waliwatuliza
Baada ya harusi ya mchana kumalizika….harusi ya usiku iliwekwa kapuni…..tulienda kupumzika kwanza….kwa kitendo alichonifanyia Amani nilihisi kuumwa…..nilimwambia Bibi kuhusu navyojisikia…..Amani aliitwa
“Scola hayupo sawa….. msiende nyumbani kuna watu wengi….. mtafutie sehemu nzuri apumzike”
Amani alinichukua tuliingia kwenye gari kwa surprise aliyonifanyia nilijikuta nikilia…..siyo kwamba ni utoto ulinisumbua hapana akili yangu ilikuwa imeshtuka 😔
Episode 19
Baada Ya Miezi Miwili Kupita 🌾
Maisha yalibadilika kama hali ya hewa inavyokuwaga 😜 Scola Mimi nilijua kuendesha gari….nilikuwa naitwa Madame Scola badala ya Scola, siyo utani ni ukweli mtupu ✋…. Waandishi wa habari walikuwa wananizunguka kama vifaranga vya kuku vinavyo kuwaga kwa Mama yao 🤭 siyo Mimi niliyejiombea mahojiano bali ni wao ndio walikuwa wananisumbua kwa simu za hapa na pale
Scola Mimi nilikuwa naalikwa kwenye mikutano mikubwa kuwatia moyo kina Mama na jamii kwa ujumla ✋
Nilipewa kipindi katika channel ya EATV nilikuwa naonesha fashion mbalimbali
haikutosha nilichaguliwa kuwa balozi wa pad za Free style….
nilianzisha program ya kusaka watu wenye kipaji kama changu bila kujali jinsia zao…
Usiku mmoja Amani aliniambia kitu cha busara
“Kesho ratiba zako zote naziharibu….kwenu hukuua hata kama ulitoroka lazima urudi, hata kama utarukishwa kichura chura ni lazima uende, tena siyo kwenda nitakupeleka mwenyewe 🥴 “
Amani aliongea kitu cha msingi nilikuwa na mwaka mzima bila kukanyaga nyumbani
“Sawa.. tutaenda ahsante kwa kujali” Nilimwambia Amani huku nikiifikiria hasira ya Baba jinsi inavyowakaga kama moto mwekundu 😩
Amani alinitazama
“Bado hujafikia hata robo ya mafanikio ya Mr’s Hudson…. acha kujisahau”
“Amani…” Niliita halafu sikuwa na kitu cha kusema 😌
“Nilikwambia nitakukutanisha na watu wenye majina makubwa….kwa kuwa kesho tutaenda kijijini kwenu unapaswa kufikiria kitu gani utawafanyia kule…na kuonyesha njia tu fanya kutoboa mwenyewe, hakuna mseleleko zaidi ya huo ✋” Amani aliongea huku akinigonga gonga kichwa, mara nyingi anapenda kufanya hivi hasa akiwa ananielekeza
Kwa kifupi alikuwa na michezo mingi ya kitoto vile alikuwa mnene kama mtoto wa kiboko nahisi hakucheza michezo mingi 😄
“Haya zima taa tucheze nahisi unataka kucheza….” Niliongea baada ya kuona kichwa changu kimegeuzwa kuwa ngoma
Amani alizima taa nilijificha kwenye kabati tukanza kucheza michezo ya kitoto
Vile nimekulia kijijini sehemu tumbili wanapopatikana kwa wingi nilimpa shida Amani
tafadhali hapa namaanisha michezo ya kitoto nawaona jinsi mnavyo ni nukuu vibaya 🥴 emu nifafanue kidogo ni ile mchezo wa kombolela. Huyu anajificha yule ana mtafuta
Amani ni mwepesi wa kukasirika baada ya kuona kwenye kombolela namzidi aliwasha taa 😄
“Scola naomba utoke huko ulikojificha ni muda wa kulala” Aliongea kwa sauti kubwa
nilijitokeza, mie huyu nilidakwa mikononi mwake kama mhalifu sugu hivi ✋
“Mbona nakutafuta hivyo sikupati unajificha hivyo kama mtoto wa panya….ona hadi nimeumia mkono” Alianza kulalamika huko akinionesha mkono
Kwa kuwa Mimi ndio mwanzilishi wa mchezo huu ilibidi nimbembeleze…..Amani alinipanda kichwani kila nikibembeleza aligoma, alidai sauti yangu ina muongezea maumivu kwenye mkono wake 🤭 mie ni mtu mvivu sana kwenye suala zima la kubembeleza mtu mzima mwenye meno 32 kama Amani
“Kaniseme tu kwa Bibi yako nimeishiwa maneno ya kukubembeleza…” Nlimjibu Amani kisha nikajifunika gubigubi
Amani hakunijibu nilishtukia tu akianza kunicheka. Nilimchungulia kupitia shuka nione ni kitu gani kimemfurahisha
“Umenibembeleza sana mpaka nikaogopa….tulale sasa kesho tunaenda kwenu ✋” Amani aliongea
Niliachia tabasamu baada ya kuona amekuwa mtu mzima
Asubuhi na mapema safari ya kwenda Mtakuja nilikozaliwa Mimi ilianza….Amani aliendesha gari kwa haraka sijui alikuwa anawahia nini 🙄
Baada ya masaa matatu tulifika, kijiji chetu hakipo mbali sana na Mjini kwa kiasi fulani kimestaarabika ✋
Amani alipark gari lake kisha akaniambia nishuke…nilishuka kwa hofu kiasi…nilimshuhudia Bi Moza Mama yangu Mimi akiwa anasugua masufuria….watoto wa mtaani walijaa kushangaa gari walikuwa wanalikagua utafikiria ni Matraffic 😄
Mama hakuwa amenitambua hata kidogo tulisogea na Amani mpaka kwake nilimuona Mama alivyojaa hofu bila shaka alihisi sisi ni wakagua mazingira niliamua kumtisha kidogo 🤭
Episode 20
“Naomba nione sehemu mnayotupa taka…maana sioni jalala”
Mama alikuwa mdogo kama piliton 🤣
“Faini ni elfu 50 naomba unitajie majina yako kamili…kesho asubuhi ulete hiyo pesa kwenye ofisi ya Mtendaji” Nilimzingua 🥴
“Mwanangu hela kubwa hiyo…naishi pekee yangu nihurumie 😭…”
Nilicheka kicheko kikubwa baada ya kuona Mama anaongea uongo
“Mama…. Mimi Scola”
Mama ndio kunitambua baada ya kutoa miwani alichukua khanga yake akaanza kunipiga nayo kwanza
“Kwanini umeshtua moyo wangu, vipi kama presha ingeniua 😩” Mama
Mzee Mpemba ndio kutoka nje alivyokuwa kalowa jasho sasa, nilielewa alikuwa kajificha akihofia kukamatwa 😄
Mama alinikumbatia kwa nguvu… niliwasalimia pale kisha nilimtambulisha Amani
“Ile gari ni ya kwenu…” Baba aliuliza kuhusu chombo cha usafiri tu 🙄
“Ndiyo…” Nilimjibu
Baba alienda kuwatimua wale watoto… baada ya hapo alikamatwa jogoo mkubwa kuliko wote tena yule aliyekuwa anashika namba moja kunidharau enzi zile nimeopoa sifuri kwenye matokeo ya kidato cha nne 🥴
“Baba usimchinje huyo jogoo…..tafuta ng’ombe wawili walio na afya nataka wachinjwe majirani wote waje hapa kula….mama waalike marafiki zako wote waje kupika….” Nilimtetea jogoo kiburi maana nilitaka aone maendeleo yangu 🤕
Baba alibaki kuganda tu utafikiri kapigwa bao kwenye kamali
“Mama…. kaweke oda ya pombe kwa Mama Mmpare leo nataka watu wa huu mtaa wale mpaka wasahau shida zao….” Nilizidi kuvimba
Baba hakuamini kabisa kama Mimi Scola ndio namtambia vile
hakutaka kusubiri baada ya kupewa pesa na Amani alienda kusaka ng’ombe
“Scola muingize ndani mwenzio….Baba karibu ndani” Mama aliongea kwa kumnyenyekea Amani 😄
Mimi na Amani tuliingia ndani
“Hapa ndio kwetu na hao ndio wazazi wangu….”
“Nimewapenda wachangamfu sana…halafu kijijini kwenu kumetulia…”Amani aliongea
Nilikuwa na njaa niliingia jikoni nikachemsha mihogo
Amani alikula mihogo tofauti na nilivyotegemea….nilisikia kelele huko nje nikajua tayari watu washafika
Baada ya watu kula na kusaza waliondoka…wengine walikesha wakinywa pombe za Mama Mmpare
Mama aliniita tulitoka nje
“Scola ilikuaje kila kitu sielewi kinaendaje…”
Nilimsimulia Mama kila kitu mpaka alidondosha chozi
“Nilimwambia Baba yako kufeli shule si msiba….majirani waliongea sana lakini sikuwahi kuwauliza kwanini wanakusema…nimefurahi kuona una akili nyingi kiasi hicho 🥰 Amani ni mzuri….” Mama alisifia
Nilimsimulia Mama jinsi maisha ya kina Amani yalivyo na vyeo kwa ujumla
Mama alijishika mdomo 🤭
“Pale nipo na mimba yako niliogea muosha fedha mara moja….kama ningeoga mara mbili ungeolewa na Rais kabisa…..” Mama aliongea kwa sauti ya chini
nilijikuta ni kicheka 😄
“Nenda kwa Amani… vile hapa hakuna umeme atakuwa anaogopa…”
Nilirudi kwa Amani nikamkuta kalala….Mimi pia nilipanda kulala…nilimkumbatia maana kulikuwa na baridi halafu shuka zenyewe nyepesi kama mtandio
Siku iliyofuata tulikaa sebuleni wote….Amani alifunguka
“Mzee Mpemba bila shaka wewe ndio Kamanda wa familia hii…jana hatukuweza kuongea sababu ya shughuli iliyokuwa ikiendelea……Scola najua alitoroka akaja mjini bahati nzuri alifikia katika nyumba ya Bibi…. kama angefikia sehemu nyingine huenda asingekuwa hivi leo…. nimejaribu kuongea na Scola tumekubaliana kuwajengea nyumba ya kisasa pamoja na umeme ili muwe mnamuona binti yenu kwenye TV ✋”
Baba na Mama walitazamana
“Scola anaonekana kwenye TV? ” Baba aliuliza
“Ndiyo….”
“Wewe Mama Scola mbona Mama Sarah hajakuambia hizi habari au ndio chuki zake za msimu zimeanza….sikia nani huyu anaitwa” Baba alijitia kunisahau jina 🤣
Mama alimsaidia
“Scola…”
“Eh Scola ulivyo haribu yale matokeo kila siku nikikutana na Mama Sara alikuwa ananipa pole…sasa kwanini sasa hivi yeye hanipi hongera ya wewe kuonekana kwenye TV”
“Baba tuachane na hayo….kwa kuwa ni asubuhi nataka twende Tanesco kwanza simu zetu hazina chaji nataka waje waweke umeme kwanza….nyumba mpya itasimamia hapo ulipopanda mihogo au unasemaje Bi Moza 🌝”
“Popote tu muhimu nyumba nzuri na umeme usisahau mwanangu unaona jinsi nilivyokuwa mfupi sababu ya ndoo…..Kaka yako alituahidi maji mpaka sasa utekelezaji hewa…..” Mama aliongea
Baba alimeza mate tu kwa haraka niligundua hela itakuwa alitumiwa na kaka lakini ziliishia kijiweni…..kaka yangu ni mtu wa kujali sana hata suala la umeme na ujenzi wa nyumba nina uhakika Baba amekula hela.
“Baba Scola mbona hauchangii kuhusu kauli niliyomalizia…” Mama aliuliza… maana Baba yangu huwa hapitwi na kitu
“Scola mwambie Mama yako Mimi siyo Mbunge wa Mtakuja niongee kila kitu….ngoja nishuke hapo chini mara moja…. Amani karibu sana” Baba alikwepa kijanja 😄😄😄
Episode 21
Mimi na Amani tulielekea Tanesco kule baadhi yao walikuwa wananijua si unajua naonekanaga kwenye TV 😜
Tulipewa heshima kama zote Amani aliongea kitu gani kimetupeleka pale,
hela bwana ni zaidi ya detergent ile sabuni ya unga 👌….
Tuliongoza njia gari la Tanesco lilitufuata kwa nyuma… mambo yalifanyika chapu…umeme ulianza kuwaka.
Sikutaka kuwachelewesha hawa wazee tuliwasiliana na Oscar akatutumia TV yenye ubora wa kiwango cha juu ✋
Bi Moza alikuwa haamini jinsi mambo yanavyoenda kwa kasi
watu wa idara ya maji walifika wakaanza kuchimbua chimbua
kwa kifupi mambo makubwa yalifanyika ndani ya muda mfupi ✋
Jioni Baba alirudi na Mzee Amosi Baba yake Mama….
Tuliandaa chakula baada ya hapo kikao kilifanyika
“Scola kwa kosa la kutoroka hapa utapiga magoti huku mikono ikishika masikio mpaka pale maongezi yatakapoisha” Babu aliongea, kwa jinsi anavyo nipenda asingenisamehe kirahisi 😩
Nilifanya kama nilivyoambiwa
Babu alikuwa kakasirika
“Tena kabla ya kuingia hapa mngempa adhabu ya kukaa nje usiku mzima…. kutoroka si tatizo….kama ungepata ajali ingekuaje…ulitaka tufanye msiba badala ya kufanya harusi…. kule nyumbani kwangu nilikuwa tu nakuona kwenye TV ulikuwa unanipandisha hasira balaa 🤕….”
“Baba msamehe kasharudi tayari….nyie wote mlikuwa mnamtazama kama mgonjwa aliyepoteza matumaini ya kuishi….Mimi sikupenda hata kidogo sasa maombi yangu yamewaumbua” Mama aliongea
Babu kwa hasira za kujibiwa alijititika kofi zito la uso 😄
“Tufupishe mazungumzo maana naona Baba mkwe anapata shida kwa majibu yako Moza. Baba, Scola kwa sasa kawa na mafanikio makubwa…huyu kijana anaitwa Amani…yeye na Scola wana mahusiano na muda si mrefu wanatarajia kufunga ndoa…sasa huyu Mwanangu Amani alinifuata akaniambia Baba si busara kukaa na Scola bure nahitaji kutoa kishika uchumba….sikutaka kumjibu kwanza niliona niwaite hapa wote kama ni kishika uchumba kitolewee na nyie mkiwepo” Baba aliongea kwa busara 🤗
“Ni jambo jema….huyu mtoto alizaliwa…Mama yake alitolewa mahari kwanini yeye asitolewe…kuhusu hili siwezi kupinga…kishika uchumba kitolewee tu….hata sisi tutakuwa na amani….naamini hata mahari itatolewa mapema kabla uzee haujanikandamiza zaidi ya hapa….Scola simama kikao kimeisha ✋” Babu aliongea….mikono ilikuwa inaniuma acha tu
“Kesho sisi tutarudi mjini…lakini kabla ya hapo Scola alihitaji kupita shuleni kwao…tutarudi kwa wakati mwingine” Amani aliongea
“Sawa sawa bwana Amani…Scola tupishe kidogo sasa kasaidiane na Mama yako huko jikoni wanaume tunataka kukabidhiana dhana za kivita” Baba aliongea
Baba yangu kwenye mambo ya pesa huwa anakuwa na tabasamu muda wote 😊
Mimi na Mama wale tuliondoka
Kesho yake asubuhi niliwaaga wazazi wangu…. walitupa baraka zote yule jogoo mkubwa mwenye kunidharau enzi zile hakuwahi kuwika tangu ile siku niliyotia maguu baada ya kuona naaga ufalme ulimrudia 😄 alianza na kuwika kama kafurahi vile huenda uwepo wangu ulimnyima amani waswahili wanasema usimdharau mtu usiyemjua tuliongozana na Amani mpaka Mtakuja secondary School 🏫
Inaendelea…………..