DEREVA WA BABA
SEHEMU YA YA KUMI NA MOJA
Yaksun akachukua nguo zake ili akabadilishie kwenye gari 🙈🙈, akamwambia irene amesubiri kidogo anarudi 😒😒
Akamuuliza sa unaenda wapi🤥?? ,Yaksun akajibu nakwenda ku change nguo mara moja😒😒 ,
Irene akamwambua embu njoo hapa🤗🤗 , Yaksun akashangaa na vile alivyo ndo kabisa😲
Irene akamwambia Yaksun samahani kama nitakuwa nakosea🙌🏾 lakini naomba usinipeleke nyumbani nitalala hapa hapa kwenye kochi 🤔🤔sa hi usiku umeenda sana naogopa mama anaweza kunigombeza nitasema nililala kwa mesha 😔😔
Mmh Yaksun akaguna akamuuliz una uhakika🙄 ?? Akasema ndio😕😕. Basi Yaksun akamwambia haya karibu inuka basi ukaoge kabisa😬😬 ,
Wakatoka kuongozana kwenda bafu la nje ☹,Iren hajazoea mambo ya kuoga mbali na nyumba🧐🧐 wala hajawahi kuoga😳 alishangaa anazungushwa huko nyuma ya nyumba 🙄🙄
Akamwambia we Yaksun ndo huko pakuogea 🙄🙄akamjibu ndio madam we nifate tu mimii 😒, Irene akasema afu sipendi uniite madam 😳😠
Yaksun akacheka kidogo akamwmabia sorry irene 🤗🤗🤗
Yaan kitendo cha Yaksun kutaja jina IRENE moyo ukaanza kumuenda mbioo🙈🙈 mwili unatetemeka akajikuta mwenyewe automatically anatabasam😊😊 Hata yeye hajui kwanini ila anasikia tu rahaa tena imekuwa gafla kwelii 🤗🤗
Kweli moyo unaweza kuhama kwa sec🥰 ,Irene ni gafla tu bin vuu katoka kwenye kumchukia Yaksun sasa anatamani hata amsike mkono😊😊🥰 wakati anampeleka bafuni Yaksun alikuwa kafunga taulo kiunoni 🤥🤥
Irene macho yake hayakuwa yanatazama njia hata kidogo 😅😅😅 Macho yote yalikuwa yatembea kwenye mwili wa Yaksun muda wote 🙈🙈🙈
Akashtuka anaambiwa ingia humo😒 , akamuuliza hee afu we unaondoka aah bwana Yaksun mie naogopa huku aah siwezi😔😔😔
Yaksun akamwambia ingia mie nakusubiri hapa nje 🤥🤥
Kweli irene kuingia humo hata kama Yaksun atasubiri mlangon hakuweza kabisa palikuwa panamtisha unajua hizi bafu zetu za kiswahili😅😅😅🙌
Irene akasema aah basi sintaoga nitalala tu we turudi ,🤣🤣🤣 kwa bafu hili hata mie ningelala tu mwenzangu bafu kama zile nyumba za kale na giza hili 🤭🤭🤭,Irene akasema mie nitalala tu 😒😒
Yaksun akamwambia basi twende ukaogee chumbani 😅 irene akamuuliza kumbe una choo cha ndani 😬😬?? , Yaksun akasema ndio 🤥🤥
Hapo wanaongea huku wanarudi ndani🤭, mpaka chumbani Yaksun akachukua beseni kubwaaaa na ndoo akamtilia maji akamwambia haya oga 🤣🤣 irene akashtuka akamuuliza wewe si umenambia una choo cha ndani 🧐🧐
Yaksun akamjibu ndio hicho wewe oga hapo bwana ….🤔Eeh irene akabaki amepigwa na mshangao hajawahi kabisa kuoga hivyo 🙄🙄
Yaksun akamuona kama haelewi nini cha kufanya akampa taulo akamwambia haya toa hiyo nguo yako jifunge taulo nikuelekeze jinsi kuoga😒😒.
Yaksun akatazama pembeni ili Irene atoke nguo zake , baada ya kutoa ,Yaksun akamwambia haya ingia kwenye beseni 🙄 irene akafata hivyo hivyo huku anashangaa hivi vituko mbona vipya 😅😅😅
Hayaa Yaksun akampa kopo na sabuni akamwambia haya utakuwa unachota maji humu unajimwagia yaan hapo ndo unaoga ..
Irene akacheka🤣🤣 akamwambia jamani mbona kizamani hiviii.🙈🙈 Yaksun akamwambia wewe unataka kuoga au unataka usasaaa😕??
Jibu swali la Yaksun likafanya Irene aombe msamaha akamwambia mie natania jamani🤔🤔 ,Yaksun akamwambia oga patakucha bado upohapo🤨🤨 …
Irene akasema sawa😒😒 , Yaksun akageuka pembeni mana alitaka kutoka Irene akasema yeye anaogopa kuwa peke yake humo ndani☹☹ ,Ikabidi atulie pembeni 😕
Irene akaanza kuoga kama alivyoelekezwa kachukua kopo la kwanza akamwaga maji mwili kopo la pili mwili ukaloa 🙌🏾, akachukua sabuni akapaka mwili wote mpaka usoni , akapeleka mkono kwenye ndoo ili achukue maji ajimwagie kama maelezo yalivyosema 🤣🤣ndo amesahau ipo upande gani na vile haoni akaanza kupapasa kama atashika ndoo ya maji 😒🙌🏾
Zoezi la kupapasa lilishika hatama zaidi ya dakika tano hakufanikiwa kupata ilipo☹,Akajiwazia afumbue jicho moja kidunchuu aangalie ndoo ilipo na kopo🤣 sa ngap sabuni isiingia machoni ikawa kalii irene akajikuta anafumba macho huku anapiga ukunga wa kuomba msaada mana hata ndoo hakuiona akaishia tu kuingiwa na sabuni machoni 😅😅😅
Yaksun akamuuliz ninii kwa hamaki huku bado amegeuka upande mwingine akafumba na macho kabisa akayakaza😅😅😅 , Irene ndo akawa kacharuka kupiga kelele za maumivu anamwambia “Yaksun nisaidiee nisaidie majiii sabuni imeingia machoni sioniii😢😢” Yaksun akasogea kinyuma nyuma anatafuta ndoo kwa kupapasa ili ampe maji macho kayafumba kaageuza na shingo upande mwingine 😅😅😅🙌🏾,
Kwenye harakati za kupapasa akashutuka baada ya kugusa kitu laini laini mmh akabinya mana hakujua kagusa niniii irene akaongeza ukunga tena kwa sauti ya kulaalamikia puani “weee umeniumiza ziwaa” 🙄🙄 Yaksun akashtuka kuambiwa kamshika ziwa 😅😅😅,Irene nae wakati wanalalamika huku anarudi nyuma kafumba macho akakanyanga juu ya beseni anakuja kushtuka akaenda mzima mzima chini kishindo ndio kilimshtua Yaksun akafumbua macho haraka akageuka kutazama kilipo sikika kishindo 🙌🏾
SEHEMU YA KUMI NA MBILI
Yaksun akatazama haraka upande kilipo sikika kishindo lahaulaa🙄🙄 anamkuta Irene yupo chini kaumia mgongo yupo pweeee🙈🙈🙈🙈
Yaksun akamuinua haraka akambeba kwa kumshika chini ya mapaja karibu kabisa na makalio na huku kwa mgongoo 🤭🤭
“Irene Sorry sorry Sorryy mamaaa ” Yaksun alikuwa anaongea huku katizama upande afu kafumba macho 🤣🤣🤣na wakati aliona mwanzo 😛😛
Moyo wa irene ulikuwa unaenda mbiooo mwili ukabadilika upitishaji wa damu😝😝,Damu ya moto ndio ilikuwa imetanda kwenye mishipa ya irene ☺☺
Zile sabuni machoni sijui zilitoka na nini 🤣🤣 mana alikuwa macho kodo anatazama kifua cha Yaksun moyo wake ulikuwa unadunda mana aligusana nyama kwa nyama🤗🤗 na Yaksun yeye alikuw juu wazi hajavaa shati na ule mfua wake😋😋😋
Yaksun akamwambia “irene Shuka chini taratibu chukua Taulo hapo jifunike samahani sana kwa hiki…..” 😋😋😋 Yaksun akashtuka baada ya kuona mdomo wake umekuwa mzito kuongea🤗 mara unavimate mate eeh akafumbua macho haraka aloo🤗🤗 Akakutana na uso wa irene hapa na hapa irene amefumba macho ndimi yake inazungumza hisia zake 🤭🤭
Yaksun mwili ukafanya Vuu kama Mwanaume bwana kusisimka lazimaa😋gafla Tu yaan Vuu mnara ukasoma Five G na vile mtoto lainiiiii🥰🥰🥰🥰👌Aah weee ,Yaksun Uvumilivu ukamkimbiaaa shetani akaingia kazini ,Akampindua chap irene sasa wakawa wanatazamana Woii🙈
Irene Muda wote kafumba macho tu,🤭Yaksun akamtupa kwenye kochi nae akafata kwa juu 🥰🥰mara ka simu ka irene chap kakawakata mchezo😔😔
Wote wakageuka kuitazama simu ilikuwa pembeni kwa Irene😝☺ , my dreamBoy❤❤
Ndo namba ilikuwa imehifadhiwa kwa jina hilo na sio mwingine ni Lawrence 🙌🏾, hii ilikuwa kama sio ya mara 40 kupiga basi itakuwa mara 45 😅😅
Yaksun akaitazama akamtazama na irene wakakutana macho🤥🤥 ,Yaksun akainuka huku anasema ooh sorry 😔🙏 Irene hakumjibu alimvuta akamrudisha mchezo uendelee 🤭🤭🙈
Moyoni anajisemea Lawrence umeyataka wewe mwenyewe mie hapa siwezi kuacha nilipo fika🤔😛😛 …
Yaksun ilikuw sorry ya mdomoni haikutoka moyoni😝😝,mwenyewe alipo fikia aah kwakweli wamsamehe tuu😅😅😅
Lawrence alipiga na kupiga😢☹🙌🏾 ,Simu yake ikageuka kuwa nyimbo nzuri ya kusindikizia watu kwenye safari yao Ya Huba Zitoo 😋😋
Hakuna ambae masikio yake yalijishughurisha tena na simu ya Lawrence😄😄 kila mwenye sikio lilikuwa makini kusikiliza sauti za miguno kutoka kwenye kinywa cha mwenzie , Yaksun alimfukuzia kweli kweli irene yaan alimmudu haswaaa🤗😋🥰🥰🥰
Irene alikuwa anaongea kingeleza akaona hapana mbona hata kiswahili najuaa🤗🤗🤗basi akaamua tu kutumia zake lugha ya Taifa 😅😅 ,Sijui hata walianza lini upenzi na Yaksun lakini kwenye moja ya kauli zake alikuwa anamwambia “Yaksun usiniache mpenzi wangu usiniachee Yaksun nakupenda babyy 🥰🥰nakupenda mpenzi wangu🥰 please usiniachee ,mpenzi wangu wewe jamani Yaksun🥰🥰☺…….” irene alikuwa anaongea kila aina ya sifa mpaka koo likamkauka ikawa kazi kutafuta mate yalipo jificha ameze aendelee na mahubiri yake ya kusifu penzi la Yaksun😚😚 …
Yaksun Akabaki tu mmh mmh sikuachi irene sikuachii mmh☺…irene anasema baby usiniachee ,,Yeye yupo ndio siwezi kukuachaa,,akiulizwa unanipenda anasema ndio nakupenda🤣🤣🤣🤣sijui hata kama alikuwa anamaanisha alichokisema kwakweli 😅😅🤣🤣🤣🙌🙌🙌 mradi yeye apewe hicho ki dedee🤣🤣🤣🤣🤣
Lawrence baada ya simu yake kutopokelewa zaidi hata ya miamoja akampigia simu mesha akampa Story nzima kwa aibuuu😅😅 hee mesha akasema duuh we shemeji yangu kibokoo kumbe watu wanapigana kisa Goma unajifanya kama Huoni afu unapita za nyumaaa🤣🤣 ,mesha alikuwa anaongea huku anacheka😅😅😅🙌🏾 Lawrence anazidi kupata hasira kajielezea ili apate msaada anaishia kuchekwa tu😏🤨 akaona bora akate na simu enyewe aendelee kumpigia Irene wake 🤔🤔🙄
Kila akikumbuka mtu alieondoka nae ule muda🤔 ndo kichaa kinazidi kumpanda🙄 akampigia tena Mesha akamwambia naomba unielekeze kwa huyo mpuuzi aliemchukia irene dereva wa baba yake 🤨, Mesha akamwambia kama ni huyo jamaa ndie aliemchukia we kuwa na amani hana hizo afu yeye na irene hazipandi yaan chui na paka 😒😒Huyo irene kama paka kwa Yaksun🙄🤔, Yaksun kama panya anajificha akimuona kwahiyo kuwa na amani 😒🙌🏾
Lawrence akasema nakwenda kwao😳😷,Mesha akamwambia wee sa 10 hii embu vumilia pakuche utaenda bwanaaa🙄🙄 Mesha alifoka sasa mana kitendo cha Lawrence kumchukua mynda alikerekwa sanaa😳🙌🏾 hata hakujisumbua kumuwazia et amuombee msamaha akamuona mjinga tu🤔🤔 yaan mesha alimshusha vyeo vyoote Lawrence tena akaona hata asimsumbue 🙄🤨
Akawaza ngoja ampigie dada ake itakuwa yupo kwenye wakati mgumu aloo yaan simu hata haikuita ikapokewa 🤣🤣🤣akasikia Maneno ya dada yake uuuh akaikata simu haraka mana ilijipokea kwenye kupinduana bahat mbaya wakaigusa na ndio Mesha alikuwa anapiga 😂😂😂
🤣🤣🤣mesha alichekaaa Et ooh mie hapa Tz sioni wanaume kwa wanaume gani🤣🤣🤣 sasa hivi kanapelekewa moto 🙌🤣🤣
Mesha alikuwa anacheka huku anarudia maneno ya Irene😂😂 ambayo aliwahi kumwambia na ndio maneno anayasem mara kwa mara na hajawahi kutoka na mwanaume wa Tanzania 🙌🏾anasema hawajui mapenzi wajinga yaan kila siku kuwaponda 🤔🤔
Mesha akachukua simu yake huku anachekaaa mpaka machozi yanamtoka 😆😆akaandika ujumbe (kwahiyo umesha shenyetwa na Mtu Wa Tanzania Tena Dereva wa baba yako🤣🤣 Yaan wewe Irene wewe bwana hayaa ukimaliza hapo Mtafute bwana wako Lawrence ananisumbua sana😅😅😅🙌🏾 )
SEHEMU YA KUMI NA TATU
Baada ya safari ndefuu ndo walikuwa wamefika sasa😋😋 kila Mtu yupo hoii kumzidi mwenzake😝😝 ,Yaksun alikua bado yupo juu ya Irene🤭🤭
anahema kama mbwa alietimuliwa kwenye msosi wa shuhurini😒😒, irene yeye ndio alikuwa akihema pwita pwita kama ametoka kukimbia marathons😜😜 ..
Yaksun taratibu akambusu irene kwenye paji la uso akataka kushuka juu ya kifua cha bint🥰🥰🥰 ,irene akamvutaa akamkumbatia😆😆 ,Yaksun akatabasam akatulia ,Ametulizwa aende wapi sasaa🤣🤣🤣 akambusu kwenye paji la uso kwa sauti nzitoo afu ya Taratibu akamwambia “asante irene kwa hii siku🥰🥰 “
Irene akacheka tu Yaksun akaktazama machoni macho yakakutana Irene akaziba macho na viganja vyake huku anasema “usiniangalie bwanaaa🙈🙈🙈” kwa ile sauti yake ya puani 🥰🥰🥰🤗🤗 Yaksun akambusu tena mdomoni akajishusha Taratibu akasimama kwa chini halafu akambeba irene akamwambia “twende ukaendele na kazi yako ulio iacha”🤣🤣🤣
Akamuweka ndani ya beseni Irene akacheka🤭🤭 ,Yaksun akamwambia wakati huu nitakuogesha mwenyewe ,Irene akabaki anacheka cheka🤭🤭😝, kazi ikawa kwa Bwana Yaksun 👌 akahakikisha sabuni inapita kila mahala kwa mtoto wa kike yaan ukiwakuta unaweza hisi ni wapenzi wa miaka mingiii kumbe penzi ndo kwanza lina masaa kadhaa😂😂😂😂
Baada ya kuoga Yaksun akamuweka kitandani walau wamalizie hivyo vi dakika kadhaa vilivyobakia ili kukuche🤗🤗 ,Irene akaanza kumpapasa Yaksun ule mpapaso wa nataka tenaa🤣🤣 Yaksun akamuuliz “wewe hujachokaa😒😒??”
Irene akamjibu nilichoka ila baada ya kuoga na kuwa karibu na wewe hivi nimesikia mshawasha🤭🤭 ,,, basii yaliyoendelea mie sijui🤣🤣🤣
Sa mbili Asubuhi simu ya Yaksun ndio iliwashtua baada ya kutoa mlio kuwa inapigiwa🤥🤥 Yaksun alikuwa wa kwanza kukurupuka juu ya kifua chake alikuwa amelala Irene usingizi mzito 😬😬,akamtoa taratibu akamlaza pembeni akawahi simu yake 🧐🧐
Aliekuwa anapiga alikuwa ni Baba Yake irene yaan boss wake yeye sasa ☹☹,Akapokea huku anaogopa labda wamejua alichomfanyia mtoto wake alo🙄🙄 alipokea huku anasita sita 🤥🤥😔
Akamwambia ” naomba uniijie hapa Airport jitahidi kuwahi😌😌” simu ikakata Irene nae alikuwa amekwisha amka tayar😐 , Yaksun akamwambia baba yako huyu Yupo Airport lazima nimfate harak😒😒 !”
Irene akasema Tutakwenda wote 🤔
Weee🙄🙄 Yaksun aliogopa akamwambia “irene pleas usije kunipa kesi naomba uchukue bajaji nenda nyumbani tafadhali🤨🤨 “
Irene akamwambia we Unaogopa nini mie nitasema nililala kwa Bro mesha hakuna atakae leta shida Yaksun au hutaki tu kuongozana na mimiii😔😔???” Ireen akauliza huku kavuta mdomo tayar😟😟😟
Yaksun akamwambia okay vaa haraka tuondoke sasaaa😒 “
Hapo Yaksun yeye alikuwa anavaa chap chap , sasa kinguo cha irene kilivyo nusu uchi ikabidi Yaksun ampe surual yake na Tshart akapendeza mwenyewe hadi Yaksun akamsifia 🤗🤗
Wakati wapo ndani ya gari kwenda Airport iren akamuuliza Yaksun “kumbe wewe unajua kingeleza vizuri kabisa😇😇??”
Yaksun akatabasam akasema “Noo!! Sio ki viiile ila huwa najaribu jaribu kidogo mad… ooh sorry irene😆😆”
Irene akacheka akamwambia we jichanganye tu.safari hii ukiniita hivyo nakuuma meno”😆😆😆 Yaksun akatabasam ,Irene akamuuliza una elimu gani🤔??”
Hili swali aliuliza huku anaona aibuu mana anajua kabisa huyu ni dereva atakuwa na Elimu gani wakati amesomea chuo cha mafunzo ya udereva 😅😅😅
Yaksun kabla hajatoa jibu kwa irene simu yake iliita namba ngeni aliinua simu akapokea🤔 , baada ya kuitikia haloo!! Akimaanisha Yupo hewani 😒😒😒
Alibaki kimya kwa dakika kama tatu akisikiliza maelezo ya upande wa pili kisha akaitika sawa nitakuwa hapo nusu saa tuu 🤔🤔…
Wakati Yaksun anaongea na simu ndio irene alipata wazo na yeye kushika simu yake 🤥🤥🤥,tangu aisuse jana hakuwa na hamunayo kabisaaa🙌🏾
Kwanza akakutana simu ambazo hazijibiwa (missed call) nyingiiii za Lawrence akasonya tu😕😕 akakuta na simu za Mesha akatabasam akawaza kumpigia mesha ila kabla hajapiga akaona kuna jumbe akafungua upande wa jumbe😔😔 ,
Lawrence alikuwa katuma Sms kama mvuaaa😂😂 za kuomba msamaha za kujutia alichofaya za kulalamika yaan Taflani Akasonya tena 😕😕awamau hii alisonya msonyo mrefuuu mpaka Yaksun akageuka kumtazama ni vile tu alikuwa anasikiliza maelezo kwenye simu pia🙌🏾 ..
Irene akafungua Sms ya Mesha
,(kwahiyo umesha shenyetwa na Mtu Wa Tanzania Tena Dereva wa baba yako🤣🤣 Yaan wewe Irene wewe bwana hayaa ukimaliza hapo Mtafute bwana wako Lawrence ananisumbua sana ) 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣 Irene alichekaaa kwa emoj hadi kwa mesha zikaweka Read more 😅😅🙌🏾
Mmh mesha akamjibu (kaone wamekarambaa😅😅)
Irene akamjibu ( embu niache bwana 😅) wakawa wanachati mesha akamjibu (ila Yaksun ni kidume kuliko hata huyo bwana wako hana mambo mengi irene hapo ingekuwa umekula bingo sema ana mchumba wake daah mie namkubali sana huyo jamaa🤔🤔) irene aliikodolea ile sms macho( et anamchumbaaa???)😳😳😳
(Yeah jamaa anamchumba wake wanafunga ndoa soon😐😐)
SEHEMU YA KUMI NA NNE
Et anamchumba na wanafunga ndoa soon yaan😳😳😳🙄 Irene mikono ilikuwa inatetemeka balaa😢😢 , jasho linamtoka moyo unaenda mbio kwa hasira🙌🏾 na ndio huo muda Yaksun alikuwa ameikata ile simu 🤌
Akashangaa iren anamtazama jicho la mwanamjinga mwambie akome😲😲akamuuliza mamaa kuna shida🤥🤥?? “
Irene akamwambia hivii Yaksun unanipedaa☹☹??” Khaa!! Yaksun akashangaa swali la gafla kama kawaida yake akacheka kidogo😄 “mbona unaniuliza hivyo kuna ninii😐??”
“Nimekuuliza nijibu sio na wewe unaniuliza☹☹??” Irene akaongea kwa ukali sasa akasahau kama anakijisauti chake flan hivii akikitumia Mwamba hachomoi 🥰🥰👌
“Aah Irene unajua wewe una mtu wako lakini si ndio??”
Hili jibu liliukata kata kabisa moyo wa irene alitamani hadi kulia kwa nguvuu yaan ni gafla sanaa 🤔gafla mnooo anampenda Yaksun kiukweliii na vile kuambiwa et anamchumba ndo maupendo yakazaliwa mengine na wivu juuu😔😔😔
Yaksun akamwambia “kilichotokea Tukifanye kuwa bahati mbaya irene tulikuwa kwenye mazingira ambayo labda kila mtu alishindwa kujizuia kwa tamaa zake mwenyewe😒😒 But sorry Very sorry irene🙏🏾 kwa kile kilichokuwa jana I know siwezi kuwa na wewe🙌🏾 yes I know that so mie nitasahau baada ya hapa☹☹”
Iren akamwambia”hivi we Yaksun unajisikia unavyoongea unajisikia lakini 😭😭hivi unasikia unachoongea Yaksun😒😒, Na ulivyonifanya vile afu kirahisi tu et bahat mbaya😪😪😪, Yaksun Hivi unajisikia weweee😭 Kwa sababu ya huyo mchumba wako si ndio🙄🙄??? Si ndioo??” Khaa!!! Yaksun akashangaa huyu mwanamke amekumbwa na ninii??
Ireen alikuwa anaongea huku analia na kumpiga vi ngumi vya bega Yaksun wakati yeye anaendeshaa “irene embu tulia tupo barabarani ujue🤨🤨”
“Yaan mimi nakupenda kwelii Yaksun sikumbuki kuhusu Lawrence nakumbuka kuhusu wewe jamani aah😭😭 Tafadhali Yaksun naomba usiniache Usiniachee bwanaaaa nakuapia nitakufa😪😪”
Yaksun akasogeza gari pembeni akapaki 🤥🤥,Akageuka alipo irene alikuwa analia kweli kweli😭😭 ,akaishika mikono yake huku anamtazama machoni 🥺
Akamwambia “irene tafadhar nitazame😳” Irene akainua macho Yake yamejaa machozi akamtazama Yaksun😧
, mashaallah irene ni mdada ama bint mzuriii au tuseme ka bint flan kazuriiii🥰🥰🥰🥰 maneno hayo yalipita kwenye kichwa cha Yaksun baada ya kumtazam irene machoni 🤗🤗
Irene baada yakutazama macho ya Yaksun ni macho flan hivii🥰🥰🥰 wakati yupo mdogo alikuwa anaambiwa na wamama “wewe mtoto hayo macho yako hayoo utauwa wa dada macho ya Nyeg hayooo🤗🤗🤗”
Yaksun anamacho ya Nyege haswaaaa macho mazuriii mashaallah 🥰🥰🥰 Irene akajikuta anatamani kuiona Future yake ndani ya macho ya Yaksun, alitamani hapo Yaksun amwambie ndio nakupenda Irene nakupenda siwezi kukuachaaa 😘nitakuoa wewe irene nakupenda bila wewe mie siwezi kuishii” hayo ndo.maneno pekee alitamani Yaksun ayatamke huku macho yake yakimtazama kwa mbalii machozi yakimtoka 🤗🤗🤗Hako ka feeling aaah weeee 🥰🥰🥰🙌🙌🙌😋😋😋😋😋😋😋😋
Yaksun yeye alikuwa Dunia ingine kabisa na Irene😒😒, kweli alikubali irene mtoto mashaallah 🥰🥰 unaweza kumla hata bila mboga na ukashibaaa 😋😋asipooga hata mwezi,😛 bado unaweza kutembeza ulimi kote mwilin na usikute chumvi wala Radha ya Betri🙈
“Irene ” kwa sauti nzito iliyotulia Yaksun alimuita irene🤨🤨 kama kumuomba umakini wake kwa wakati huo irene nae akaongeza umakini kumsikiliza 😔😔😪
“Sikuwahi kutamani kumuumiza mwanamke hapa chini ya jua 🙌🏾sikuwahi kufikiria ipo siku nitamtoa machozi kiumbe anaeitwa mwanamke 🥺🥺nathamin zaidi ya kuthamini uwepo wa mwanamke☹☹ ,Yeah nakili kuwa irene wewe ni mwanamke mzuri sana🤨🤨 sidhani kama kuna mwanaume anaweza kuji control akiwa mbele yako haswa kwa vile tulivyokuwa jana😔🙌🏾 ,Nilijaribu sana kushinda ule mtihani lakini ukanizidi nguvu ni aibu kusema hivyo😔😔 lakini ndivyo ilikuwa 😒😒,Irene wewe ni mrembo na mzuri nakili sijawahi kukutana au kulala na mwanamke mwenye thamani kama yako 🤌,ndio ni kweli mimi nina mchumba😒😒 ,Naa zimebaki wiki mbili tunafunga ndoa Sorry Irene😧 ,soo Sorry 🙏 Sikujua kama nitakuumiza I’m soo 🙏 Sikutaka kuchezea hisia zako na nilikuwa na uhakika wewe una mchumba wako huyo sijui nini kilitokea jana lakini sikufikiria kama u…..” l
“INATOSHAAAAAA!!!!!” irene alifoka kwa sauti kali hakuchelewa akafungua mlango wa gari akatoka mbioo😢😢 Yaksun akashuka kumfata nyuma lakini Akachelewa Irene akawa tayar amechukua boda na imetimka 😢😢🙌🏾
Yaksun akarudi kwenye gari hajui aende kumfata mzee au aende kwa irene au kwenye ile simu alipigiwa na akaahidi nusu saa atakuwa hapo 😔🙌🏾,, akawaza ngoja kwanza amfate mzee akajipa moyo irene atakuwa salama tu 😒😒
Akamchukua baba Yake na irene wakati wanarudi akamwambia “mzee mie ajira zimetoka nimepigiwa simu natakiwa kwenda kureport leo 🧐🧐”
Ooh baba yake na irene alifurahi sanaaa sanaaa😇😇😇😇😚😚
Akamwambia “Yaksun bwana mimi nashukuru kwa kipindi chote tulichokuwa wote siisi bado ni Familia naomba sana sana usisahau kwetu😆😆”
Yaksun akamjibu kwa Heshima sana akamwambua “Mzee wangu nashukuru sana kwa kunipambania sanaaa sanaa mpaka hapa nilipo fikia🤌 kama sio wewe sijui ningekuwa wapi🙌🏾 nakushuru wewe na bi mkubwa nawashukuru sana Hata leo nimepata kazi Zote Juhudi zako😒😒 ”
SEHEMU YA KUMI NA TANO
Walipiga sana story 🤗🤗 Baba irene alikuwa amefurahi sana kwa taarifa za Yaksun kupata nafasi ya kazi🙌🏾 aliyoisubiri kwa muda mrefu na Mzee mwenyewe ndio akimkingia kifua😒😒 kuhakikisha anapata nafasi ya juu pindi tu atakapo pata ajira asianze kama mfanyakazi wa kawaida 🤌🙌🏾
Lakini pia baba Irene ndie aliemlipia Ada zote za Shule Yaksun kuanzia elimu yake ya Secretary mpaka anamaliza Chuo😌🤨 na Yaksun ndie mtoto pekee aliesoma kwenye familia yao na baada ya baba Yake kupata maradhi alikuwa tayar kamaliza chuo ndio akashika nafasi ya baba yake kama tu kulipa Fadhira za walezi wake 🙌🏾
Baba na mama Irene wanamchukulia Yaksun zaidi ya kijana wao🤗🤗 ana heshima kwa kila lika mtu poa sana anajituma na ana bidii sana ya maisha kuliko vijana wa Lika lake🤨🙌🏾 …..
Yaksun japo alikuwa akiongea na muda mwingine kucheka😒😒 lakini akili yake kuna muda ili ganda haswa alipo kumbuka tukio zima la yeye na irene 🤔🤔 hakujua mwisho itakuwaje ila alijipa moyo kila akikumbuka kuwa irene anampenzi wake tena kidogo anapata amani😒😒 ….
Akamfikisha nyumbani baba ake na irene😌 ,akataka kuacha gari ili aende kule kwenye kazi alipoitwa😒😒 , Mzee akamwambia tumia hii gari mpaka utakapo pata gari yako🙌🏾 namaanisha ichukue mwaka utakayo pata gari yako utalejesha kwangu🤔🤔
Yaksun akahisi kama hajasikia vizuri aliitika eeeh🙄🙄🙄 Mzee akarudia tena maneno yake bila kupindisha ,Yaksun alifurahi mnooo🥰
Alitoka hapo haraka kuwahi kule kwenye kazi😒😒 ,Akiwa njiani akachukua simu yake ili kumpigia irene mana aligundua kwao hayupo🤥🤥 ,Aliipiga sana haikupokelewa🙌🏾 …
Wakati huo irene yeye alikuwa nyumbani kwa mesha amelia mpaka mafua yametoka😭😭 Mesha amezungumza kila aina ya Lugha kumuweka sawa lakini wapiii😢😢 irene alikuwa kichaa kwa Yaksun zaidi ya kichaa alikuwa amelia mpaka sauti imeenda😭😭🤌
Mesha akamwambia pokea simu hii anakupigia Irene akaichukua akaitaka na kuizima kabisaaa hakutaka kuongea nae 😧😧😣
“Ungemsikiliza!” Mesha alimwambia huku anaichukia ile simu kuiwasha tena 🙌🏾,Irene akampokonya 🙌🏾🙌🏾
“Hapana mesha,Anaoa halafu ,halafu atasema ninii kwanini najisikia hivi meshaa kwaniniiii naumiaaa😭😭”
“Embu inuka irene nenda nyumbani mimi nitashuhurikia hili swala🙄🙄🙌🏾 !”
Mesha aliinuka akiwa na hasira sanaa🤨🤨 , yaan kitendo cha kumuona dada yake anapitia kipindi kigumu aliumia zaidi hata ya Irene mwenyewe 🥺🥺
Alimchukulia Bajaji irene akamwambia wataonana huko☹ yaan mesha atakwenda nyumbani kwao🙌🏾 , irene akaondoka🤥🤥 …
Mesha akachukua simu yake akampigia Yaksun kumuuliza yupo wapi 🤨🤨 ,Yaksun akamwambia kuna sehemu anakwenda ni muhimu sana🙌🏾 Mesha akamsisitizia sana baada ya kutoka huko ampigie simu🤥 ,Yaksun akasema sawa 😒😒… .
Irene alikuta nyumbani kwao kuna usafi wa stoo 😒😒,Vile alikuwa hana mood ila hakutaka mama yake amtilie shaka juu ya yalio mkuta na vile alikuwa kamaliza uchungu huko kwa mesha akafika tu anajichekesha na alipo mkuta baba yake ndio kipenzi chake kidogo akajikuta ana ahueni
“Mamaa kuna nini humu mbona usafi😒 ??” Irene alimuuliza mama yake huku anasogea mbele kulikuwa na picha zinaonekana za zamani zikamvutia kutazama zilikuwa kama nne hivii 🤥🙌🏾
“Atakuja Dereva mwingine hapa baba yako kapendekeza aishi hapa hapa ili iwe rahisi hata kwa safar za gafla😌😌 “
Mmh “Derevaaa???”🙄🙄
Irene alishtuka hata kusogea mbele alishindwa kuokota zile pichaa 😧😧 “mama Dereva yaan Yaksun ana hamia hapaa🤥??” Irene aliuliza huku moyo wake unaumaa hakutaka iwe ndio ana hamia hapa mana alijua wazi atakuja hapa na huyo mwanamke wake 🤧🤧
Japo hamjui lakini anamchukia sanaaa huyo mwanamke😏🙌🏾 hampendi hata kidogo kama angepata nafasi ya kulijua tu jina la huyo mchumba wa Yaksun basi angechukia wanawake wote wanaotumia hilo jina🙄🙄😒😒…
“Hapana mwingine Yaksun atakabidhi funguo zote leo mana tayari amepata kazi☺☺”
“Kazi gani😒🙄??”
“Exploration and Mining Geology🤔”
“We mamaaa!!”🧐🧐 Irene alimuita kwa kumshushua mama yake ,akacheka kicheko cha uvivu🙌🏾
“Yani huyu Yaksun ndo kasomea utafutaji na uchimbaji madini🙄🙄🙌🏾???”
“Mmh yeah hapa alikuwa anasaidia tu kama nyumbani mana baba yako alikosa Dereva wa haraka na vile baba yake aliumwa gafla ndo ikawa hivyo😒😒”
Irene akashusha pumzi ndefu huku anaegama kwenye meza iliyokuwa mbele yake🤨🤨 , Akakumbuka jinsi alivyokuwa anamchukulia Yaksun mjingaa mwanaume asiesoma hata English inamshinda 🤥🤥
Moyo wake ukaanza kumsuta huku akili inamzomea kwa kasi😔😔 Alijisikia aibuu sanaa kumbe mtu kasoma🤔🤥 tena kazi nzuri kabisa ya utajiri🤔🤔 na amepata kazi tena sio mjakazi ameunganisha huko anafikia tu kupata cheo mana mtu aliemuonganisha ni balozi anaheshimika 🙌🏾….
“Ooh mungu wangu!!🤔 “Irene akaanza kujilaumu mwenyewe haswa kwa zile dharau zake akakumbuka alivyokuwa anamwambia hana hadhi ya kuwa nae😔😔😔na uwezo wa kuwa nae daah ☹🙌🏾
Akajiwazia ngoja akalale zake tu 🙌🏾,ili akili ifanye kazi wakati anataka kuondoka akaona tena zile picha🤔🤔 kilichomvutia haswa kwenye zile picha ni yeye alipo kuw mdogo na hizo picha hajawahi kuziona 😬😬
Akachukua moja akiwa amepakatwa miguuni na mtoto wa kiume miaka kama mitano ama sita hivii😒😒 ,
“Mamaa huyu ni mimi eeh🤔” alimuuliza mama yake ili amthibitishie
“Mwenyewe sura ile ile 😅”
Irene akacheka huku anatazama kwa makini kijana aliembeba mwanzo alihisi ni mesha lakini baada ya kutazama vizuri hakuwa yeye😧😧🙌🏾
“Huyu alienibeba nanii😧??”
“Yaksun huyoo😆😆”
“Yaksun???🙄🙄 yaan Yaksun huyuu Dereva😳😳???”
“Ndio yaan Yaksun😅…” mama irene akasogea akaichukua hiyo picha huku anacheka
“Alikuwa anakupenda jamani atagombana na baba yake😅😅 kila siku lazima aje kushinda hapa kila siku akubebe😅 ,Akikukuta umelala atakuamsha tu mladi tu akubebe jamani😁😁alikuwa anakupenda😝😝 ,Alivyoanza tu shulee ndo akawa anakuja mara chache sana hapa na alipo fika darasa la sita alikuwa na akili huyo ndio baba yako akaamua kuwekeza kwenye elimu yake zaidi ndo hakuwahi kuja hapa mpaka amemaliza chuo ni miaka mingi sidhani hata kama anakumbuka zile fujo zake 😄”
Inaendelea…..