UTAJIRI WA MASHARTI UNAVYOMTESA RAFIKI YANGU
Nina rafiki yangu tulisoma wote “O Level” shule Fulani, Baadae Tukaachana Mimi Nikaja mkoa X na Kupiga Mishe zangu yeye Akabaki Mkoa Y. Baadae ikibidi nirudi mkoa Y kuwapa Hi maskani nakuta rafiki yangu ana mabadiliko ya kimaendeleo sana.
Nikakuta Jamaa Kajenga kanunua usafiri mzuri, pamoja na Hilo ana Gari 3 aina FUSO, ana HardWare kubwa, Pikipiki Si Chini ya 9 Kawapa Vijana Jioni Wanaleta Hesabu.
Mwanzoni alikuwa hana mishe kubwa zaidi ya Kuendesha TAX na TAX pia Haikuwa Yake, Kwahio Yeye Alikuwa Anapeleka Hesabu.
Katoboa maisha ndani ya muda mfupi sana nikamuuliza ni mishe mishe hizi hizi za udreva au, akasema eeeh mwanangu kikubwa ni kujituma kwa bidii, kusali sana na kumuomba Mungu.
Basi mimi nikarudi zangu Mkoa X baadaae ghafla akanipigia simu akasema mwanangu kuna msichana nilianzisha nae mahusiano ya kimapenzi na hatimaye ameshika ujauzito, Ila mimi sina mpango wa kuoa sahizi na msichana kwao kafukuzwa, kwahio kaja nyumbani hapa hataki kutoka.
Nikasema, lakini mbona unajiweza kwanini usiishi nae tu, nilishtuka pale alivyonijibu kwa Ukali akasema “dogo tulia hujui kitu usifikiri hizi mali zimejileta tu hapa maisha ya utajiri yana siri kubwa”.
Basi nilivyosikia hivyo sikujibu kitu tukamaliza mazungumzo.
Sasa kwakuwa mi rafiki yangu sana kesho yake nikashangaa akanipigia simu tena akasema mwanangu embu nikuambie kitu..
Naomba unipe ushauri akasema mwanangu usione nina mali zote hizi…hizi mali nilizipata kwa MGANGA na mashart aliyonipa nisije kuoa wala kuishi na mwanamke ndani..
Akasema kwahiyo hapa nipo njia panda sana na kadri siku anavyozidi kuishi na yule mwanamke anasema gari zake 2 Fuso zilipata ajali, kwaiyo zimeharibika ghafla zimepaki..
Baadae mwanamke kagoma kutoka, jamaa mali zilianza kupukutika kama ULEZI kumbe Bank nako alikopa mkopo, watu wa Bank wakaja kuuza nyumba kwa aibu akaamua kukimbilia Mkoa mwingine mbali na pale anapoishi mana kafilisika hana kitu..
Kumrudia mganga akamwambia umeshaharibu haiwezekani kurekebisha.
Mengi yaliendelea …
Pesa ni tamu ila….