UGALI WA BUKUJERO ULIPELEKEA NITOLEWE BIKIRA ZOTE NA WANAUME WATATU KWA WAKATI MMOJA
Namba 09
“Tafadhali ondoka hostel, nitakupatia room nzuri sana, au kama unaona vipi, pale nyumbani utakaa na mama, yupo na mtoto wangu mdogo na housegirl maisha mazuri tu, usiogope…..”
“Hapana Mido bado nitazidi kuumia”
“Sina nia mbaya, sihitaji penzi lako, sihitaji chochote, ila ninajisikia kukusaidia, najua maisha magumu ya chuo ndiyo yalikupelekea ukutane na yale maswahibu, kwa hiyo niko tayari kukufanya uwe na furaha”
DAAA NILISHINDWA NIMJIBU NINI
ENDELEA
Mido alipoona nipo kimya sana nashindwa kumjibu, alinipa option, akaniambia nifikirie juu ya hilo halafu nitampa majibu kama nimekubali anichukulie chumba au niende nikakae kwao au nibaki tu hostel.
“Sawa, nitakujibu….ila sidhani kama ni rahisi mimi kuondoka hapa” nilimuambia hivyo
“Sawa”
Aliniaga nikalala zangu, ila kesho yake nikawa lile jambo linanisumbua sana kichwani, niliona kama vile kweli Mido ana nia ya kunisaidia lakini niliogopa, unajua mtu akigongwa na nyoka mara ya kwanza, basi hata akiguswa na jani huwa anahisi ni nyoka, wasiwasi tele.
Nilihisi Lenard alikuwa na nia ya kunitapeli na kunifanyia tena unyama. Sasa nikiwa nimeketi zangu juu ya kimbweta, alikuja rafiki yangu wa kiume maana mimi nilikuwa nishawapa bye bye marafiki wa kike kwa kujua ni wanafiki sana.
Alikuwa anaitwa Ally, akasimama kando yangu na kunitazama, alikuwa very charming, yaani mcheshi sana, hivyo alinitazama kwa jicho fulani hivi ambalo lilipelekea mimi kupata tabasamu
“Mbona unaniangalia sana??” nilimuuliza
“Nilikuwa nakuangalia una mawazo muda mrefu sana nikasema nije hapa huenda nikakupa mawazo ya kubadilisha akili yako na kuwa sawa”
“Hahaha…n kweli jamani nina stress kweli kweli”
“Kwanini uko hivi esta? Ni mapenzi yanakusumbua??” aliniuliza nikamtazama
“Hapana….sio mapenzi….si unajua yale mambo yalinitokea?? Unaona afya yangu ilivyo Ally??”
“Ndio, ninaona umekonda sana, ila miezi mingi imekatika, unawaza kitu kimoja tu, si ufocus, usome maisha mengine yaendelee mbona unakuwa hivyo??”
“Najitahidi kusoma, ninajua nitakuwa sawa, ila bado pale nilipo sina furaha, ninapowaona Zena na Betina najikuta naumia sana…..”
“Achana nao wewe piga msuli usiwaze wala nini” alinitia moyo nikawa nafarijika
“Samahani nikuulize swali utanijibu??”
Ali akatikisa kichwa huku akiiweka vizuri miwani yake, akasema “Niulize”
“Amh…mh unajua kipindi nimekutana na yale matatizo kuna kaka alinisaidia”
“Yah ninalifahamu hilo”
“Ah,…..yule kaka tunaendelea kuwasiliana, sasa kila siku ananisisitiza niondoke hostel niende nikaishi na mama yake, kwa sababu ananiambia ninavyokaa hosteli na kuonana na wale marafiki zangu ndio ninazidi kukumbuka mambo ambayo sio ya msingi….naumia”
“Enhee”
“Ndio, halafu kaniambia kama nitahitaji atanipangishia room atakuwa ananilipia kila kitu, ili nisome, ameamua kunisaidia kiukweli lakini bado sijajua niwe na maamuzi gani”
Ally alinifikiria, akavua miwani yake kisha akaifuta na kuniambia “Pole sana, una uhakika sio kwamba anahitaji mapenzi au tayari upo naye kwenye mahusiano?”
“Hapana sipo naye kwenye mahusiano, wala hajawahi kuniambia kitu kama hicho…labda kama anaficha ficha ila sidhani kama anaweza kufanya hivyo wakati anajua historia yangu mbaya”
“Okay…nafikiri jamaa ni mtaalam sana wa saikolojia, mimi nimeona mitihani yako uliyofanya ndani ya muhula huu, imekuwa mitihani migumu na umefeli sana majaribio, nafikiri huyo jamaa anataka akutoe katika hayo mawazo..ingekuwa ni mimi, ningekubali anichukulie room hamna tatizo, kwa hiyo wewe kama unaona sio suala la mapenzi labda anataka kukupa tu msaada wewe nenda” aliniambia
“Mmh…sawa hamna tatizo nitafikiria” nilisema
“Poa…punguza stress bhana” aliniambia Ally.
Nilipata wazo jipya kutoka kwa Ally, na nilikuwa namuamini kwa sababu kipindi chote cha msongo wa mawazo, alikuwa rafiki yangu, na alikuwa akinishauri na kunisaidia masomo maana alikuwa darasani yuko vizuri.
***
Siku zilisogea ikapita wiki nzima, Mido akanitumia message na kuniuliza “Umefikia wapi kwenye lile suala la chumba?”
Nikamjibu kwamba “Nimekubali anichukulie chumba, ila nikampa tahadhari kubwa kwamba kama likinitokea jambo kama lililonitokea kipindi cha nyuma, basi lazima nijiue”
“Hahahaaaa……unaona sasa mambo yako, anyway, niamini kwamba mimi natoa msaada na sina nia mbaya”
Nilijua ni msamaria mwema ameshushwa kutoka mbinguni, lakini sikujua kama mwisho malipo yangekuwepo au yasingekuwepo, nilipata hofu kidogo lakini nikamuomba Mungu anitangulie niwe na maamuzi mema
NAMBA 10
Baada ya siku tatu tu, Mido aliniambia ameshakamilisha kila kitu anilinichukulia chumba maeneo ya Shekilango, sio mbali sana na chuo, naweza kutembea kwa miguu kuelekea chuo ila kidogo niwahi ili majasho yasinitoke nitembee polepole.
Alinipeleka nikaenda kupaona, ilikuwa siku ya jumamosi jioni, nilikuwa na wasiwasi, naenda kupaona sehemu ambayo naenda na mwanaume, nikampigia simu Ally na kumuomba twende wote kwa sababu niliamini lolote linaweza likanikuta.
Tulipopanda gari mi na Ally, Mido aliniuliza “Huyu ni nani?”
“Ni rafiki yangu tu” nilisema
“Rafiki au boyfriend” aliniuliza
Nilitabasamu nikamjibu “Hapana jamani…..”
“Broo usiwe na wasiwasi bwana, mimi ni rafiki yake ameniomba tu nimsindikize” alisema Ally
“Haha…haina noma, sijauliza kwa ubaya vile vile, maana hakuna sheria inayomzuia mtu kuwa na boyfriend” alisema
“Noma kaka” alisema Ally
Tulienda mpaka kwenye kile chumba, duuh sikuamini, kilikuwa kizuri mno, cha kisasa, ni singo lakini ni masta, huduma zote nazipata kule ndani
Aliniwekea kitanda kizuri sofa bed, na godoro zuri nchi nane la GSM, nikapagawa, kulikuwa na meza na mtungi mdogo wa gesi halafu na zulia limetandikwa chini. Yaani vitu vya kutosha kabisa, nikafurahi sana, kutoka kwenye mateso sasa niliiona furaha ilivyokuwa inanijia.
Alinipa ufunguo akaniambia nihamie muda wowote ninaohitaji, na hata nikiona nataka kuishi na rafiki yangu mmoja wa kike nihamie naye ili kujiridhisha zaidi.
Ilikuwa ni jambo la kushangaza kidogo, Mido alikuwa kama vile kaja kunionyesha urahisi wa maisha, nilijiuliza sana sikuweza kuvumilia nikampigia dada yangu mmoja anaitwa Pamela, nikamueleza kila kitu kilivyokuwa ila sikumuambia kama nimebakwa, la haula nilimdanganya kwamba niliumwa tu.
Mwishowe nikamuuliza kama ni sahihi kupangishiwa chumba na mwanaume.
Dada yangu Pamela alinionya vikali akaniambia nisije nikakubali kupangishiwa chumba na mwanaume atanigeuza chapatti atanitumia kimwili sana tu na sitaweza kufanya chochote.
Kwa kuwa waswahili wanasema akili za kuambiwa changanywa na za kwako, mimi nikaona ni sahihi kabisa kwenda kwenye ile room yaani baada ya siku moja tu, siku ya jumapili nilihamisha vitu vyangu vyote nikahamia katika chumba kile.
Kichwani ile ishu ya kubakwa ilikuwa imeshaanza kupotea, na hii yote ni kwa sababu Mido alikuwa anaishi na mimi vizuri, ananitia moyo, nilianza kupenda penda tena maisha nikatamani niendelee.
Alisaidia vitu vingi, alikuwa kama kaka yangu, halafu nilifikiria ni mtu ambaye tumeonana katika mwanzo mgumu sana ambao sikuamini kama ningeweza kupata rafiki
Nilimpigia simu usiku nikamuuliza “Umeshalala??”
Akaniambia “Hapana niko mpirani huku??”
“Mh wapi??”
“Maeneo ya Mwenge”
“Mbona hamna kelele??”
“Ulivyonipigia nimetoka nje kuongea na wewe….umeshahamia??”
“Ndio, nimelala hapa, nashukuru sana, nasikia amani ya ajabu, naomba uendelee kuwa kama ndugu yangu kwa style hii ninajihisi nimeanza kunenepa”
“Usijali….nina surprise kwa ajili yako” aliniambia
“Mmh surprise gani tena??”
“Utaiona tu” aliniambia
“Haya….hivi hiki chumba shilingi ngapi??” niliuliza
“Laki moja kwa mwezi” alisema bei ambayo ilinishtua, ni bei kubwa mno kwangu, bei ambayo sikuwahi kuwaza kupanga chumba cha bei ghali kiasi hicho, yaani akili yangu mimi nilikuwa nikiwaza chumba cha shilingi 20000 (elfu ishirini ya kitanzania, shilingi 1150 ya Kenya)
“Ndio, nimefurahi nimepata cha bei rahisi….ni patulivu ee??”
“Sanaa….nashukuru sana”
“Usijali mdogo wangu” aliniambia
“Haya basi nisikuharibie starehe yako kaangalie mpira”
“Mpira wenyewe wa kipumbavu tumeshafungwa, vipi umekula?” aliniuliza
“Yeah, nimenunua mchele, na dagaa nikapika, nimeshiba sasa nataka nisome”
“Okay….nilishindwa kukuletea unga na mchele na mafuta lakini soma kwa bidii kesho naweza nikakuona sawa??” aliniambia
“Hamna shida mimi nipo”
“Haya….halafu mama anahitaji pia akuone kwa hiyo mpigie simu, si una namba yake?”
“Ndio alinipa”
“Sawa utampigia”
“Sawa kaka….asante ee”
“Haya”
Tuliagana kivile, lakini nilikuwa nawaza sana, mimi sikuwa na cha kumlipa zaidi ya kusema tu ahsante…..nilijitihidi nikasoma kwa bidii….siku nazo zikawa zinazidi kukatika na mitihani ya kufunga chuo ulikuwa inakaribia………..
NAMBA 11
Nilikuwa ninajitahidi nisome sana, mambo yalikuwa mengi kwa sababu kipindi kirefu cha miezi miwili nilikuwa sijasoma kitu chenye maana, nilipambana sana, sikuwa na stress kubwa ya maisha kwa sababu Mungu alikuwa ameshaniletea mtu wa kunisaidia sana.
Ikiwa jumapili asubuhi wiki moja baadaye, nilimpigia mama yake Mido simu akaniambia
“Uko wapi??”
“nipo nyumbani”
“Nambie mwanangu” mama Lenard aliniambia
“leo niko free nataka baadaye nije hospitalini nikuone” nilisema
“Anhaa,…leo nipo nyumbani, nenda ibadani kasali maana mimi pia ninaenda ibadani, kamuombe Mungu wako akujalie ufanikiwe,….halafu kwenye muda wa saa sita nitakuwa tayari nyumbani uje”
“Mh…nyumbani sipajui”
“Okay, mwambie Lenard atakuleta”
“Sawa mama”
“Haya usisahau kwenda kanisani” aliniambia
“Sawa” nilisema
Nilikata simu nikawaza kwanini ananisisitizia niende kanisani maana nilikuwa na muda kweli sijaenda kusali, ikabidi nimpigie mwanae kwanza nimuambie kwamba ameambiwa anipeleke nyumbani
“Ester” alisema baada ya kupokea simu
“Kaka Mido…uko wapi??”
“Ah mh najiandaa kwenda kanisani….vipi wewe huendagi ee?”
“Naenda leo…..” nilisema
“Okay, nambie basi”
“Mama kasema baadaye unipeleke nyumbani” nilisema
“Oh saa ngapi??”
“Saa sita mchana”
“Duuh…oh okay sawa hamna shida…..”
“Sawa bye ibada njema”
“Sawa na wewe uende ukasali”
“Sawaaaa”
“Ok”
Nilikata simu nikazidi kuwaza wale watu walikuwa serious sana na ibada, halafu mimi wala nilipokuwa na chumba sio mbali na kanisa langu la Katoliki lilipo.
Nikaona kama wameniambia hivyo basi niende, kwa bahati nzuri nilikuwa na nguo nzuri zinazofaa kwenda kanisani, sikupendelea kuvaa nguo za kisista duu, nilikuwa naona kama vile ni kujidhalilisha kwa upande wangu.
Nilijiandaa haraka haraka, nikachukua biblia nikaenda zangu kanisani, sikujua kanisa ndio hilo hilo alilokuwa akisali Mido, nilipomaliza ibada tu nikaona gari yake, nilishtuka na kuifuata, alionekana kufurahi sana aliponiona pale kanisani, akanitazama juu mpaka chini halafu akaniambia
“Vizuri sana….twende zetu” alinipakia ndani ya gari na safari ikaanza akanipeleka hadi ghetto kwangu
Baadaye saa sita tulienda nyumbani kwao, maeneo ya Vingunguti, tulipofika hivi nilishangaa, wale ni watu matajiri sana, walikuwa na maisha mazuri, wamejenga, nje kuna magari lakini mengine yalionekana kutokutumika
Nikamuuliza “Mbona unasali mbali sana why??”
“Anhaa mi nimepanga kule…kwa hiyo nasali karibu na ninapoishi”
“Okay sawa”
Mido alikuwa na mtoto mkubwa tu, mtoto wa kiume akawa anamfokea fokea tu kila saa, mimi nikakaa kimya tu.
Mama Lenard alifurahi sana kuniona, nilimshukuru kwa wema wake akaniambia kwamba nikitaka kumuona basi niwe namtembelea tu nyumbani au kazini muda wowote yuko free.
*
Saa kumi mimi na Mido tuliondoka pale kwao tukaenda mpaka nilipokuwa ninakaa mimi, Mido aliniacha akaenda kwenye mambo yake.
Nilianza discussion kwa fujo sana, nikawa ninasoma kwa bidii kwa sababu nilihitaji mwishoni mwa mitihani nifanye vyema.
Ikiwa ni wiki moja tu imesalia, nilikuwa nasoma usiku sana ndipo akanipigia simu dada yangu Jamila, akaniuliza
“Mdogo wangu mitihani unaanza lini??”
Nikamjibu “Mitihani ninaanza wiki ijayo tu”
“Sawa mdogo wangu, ukimaliza uje nyumbani tumekumiss sana”
“Sawa dada”
Sikujua kwanini dada ameniambia vile lakini baadaye nikiwa mtandaoni, nilishangaa akaunti za ndugu zangu watoto wa shangazi, baba mdogo, wakiwa wamempost baba yangu na kuandika kwa maneno ya kuomboleza.
Kwa maana nyingine baba yangu alikuwa amefariki, nilishtuka, nikaogopa na kujaribu kumpigia binamu yangu mmoja nikamuuliza “Vipi binamu baba yangu amefariki?”
Akanijibu bila kusita “Ndio, pole sana kwa msiba…utakuja kuzika??”
NILIISHIWA NGUVU
JE BINTI ATAFANYAJE?
NAMBA 12
“Amefariki kweli? “ niliuliza huku machozi yakianza kunitoka
“Ndio…kwani hukujua??”
“Sikujua….kilichomuua baba yangu nini??” niliuliza kwa masikitiko makubwa niliona jinsi nguvu kazi yangu ilivyokuwa inazidi kuporomoka, nilijiona kabisa nikiwa nashindwa kurudi chuo mwaka wa pili kwa sababu mama sikudhani kama angeweza kuwa na uwezo wa kunisomesha chuo peke yake
“Aliumwa ghafla…..ghafla”
Nililia sana, nilikata simu na kuanza kulaumu, niliona kama vile mimi ni mkosaji kwa Mungu, huzuni zilinijaa kila, kila jambo nililokuwa nalijaribu lilikuwa linakingiwa kifua na shetani nilijiona mkiwa, machozi yananitoka kwa speed sana.
Stress zilianza upya, nikawa nawa mambo mengi, naiona simu ya Mido ananipigia lakini niliitazama tu jinsi ilivyokuwa inaita sikuweza kuipokea kwa sababu sikuwa na cha kumuambia zaidi ya huzuni niliyokuwa nayo.
Nilikaa kwa muda mrefu kidogo nikiwa nimeduwaa, sina ujanja wowote ndipo nikamrudia dada Pamela na kuongea naye
“Dada kwanini uliniuliza naanza lini mitihani??”
Dada Pamela akanijibu “Nilitaka kujua kama upo karibu kuna kitu nilitaka nikuagize kwa rafiki yangu” aliniambia maneno ambayo yalionyesha kabisa kuwa ni uongo.
“Acha uongo dada si uniambie tu ukweli kwamba baba amefariki” niliongea kwa masikitiko
“Daaah…nani kakuambia mdogo wangu??” aliniuliza
“Nimeona watu wanampost Facebook na kwenye status za WhatsApp halafu wewe unaniambia mambo ambayo naona kabisa ni tofauti na yale”
“Ni kweli mdogo wangu nilikuambia vile ili nisije nikakuharibia mitihani yako, pole sana naomba usome mdogo wangu, mkombozi wetu ameondoka”
Nililia sana, nilikuwa nampenda baba yangu kwa sababu alinipambania kimasikini, nimesoma mpaka nimefika chuo licha ya maisha ya chuo kuwa magumu sana lakini yeye ndiye alikuwa akipambana ananitumia pesa mara moja moja.
Nilikuwa naelewana naye maana kila alichotaka nilikuwa nafanya, nilimuheshimu.
Nilichukua simu yangu nikaanza kuzitafuta picha zake nilizokuwa nazo, kila nilipomtazama sikuamini kwamba ametoweka duniani, niliendelea kulia.
Stress zilianza upya, ila kwa bahati nzuri nikiwa nimekaa naumia ndipo nilisikia mlango umegongwa na nilipofungua nilikutana na sura ya Mido akiwa anatabasamu mikononi alikuwa ameshika mifuko na mafuta ya kupikia
“Mido….” nilisema nikitazama vile vitu, ghafla Mido akashtuka na kuniuliza
“Unalia nini??”
“Acha tu Mido, sijui mimi nina mkosi gani” nilisema
Mido aliweka vile vitu chini akanishika shavuni na kuniuliza “Kwanini unasema hivyo?? Usikute bado unakumbuka yale mambo ambayo yameshapita”
Nikamjibu “Hapana Mido, baba amefariki” nilisema
“Amefariki??” aliniuliza
“Ndio….ameniacha baba yangu….amenikimbiaa hiiiiiii hiiii” nililia kwa uchungu na kumsogelea Mido nikamlalia kifuani huku machozi yakinitiririka.
Mido alikuwa mpole kama kamwagiwa maji ya baridi, ndipo akanishika na kuanza kunibembeleza sana, lakini sikutulia kabisa.
Alinirudisha ndani akaniketisha kitandani kisha akachukua vile vitu viliyokuwa nje akaviweka ndani. Alipomaliza aliketi kando yangu na kunibembeleza sana,
“Usiingize huzuni kwenye masuala yako, una mitihani wiki ijayo tu utaumia zaidi na zaidi…utashindwa kusoma” aliniambia
“Nilikuwa napendana na baba yangu, alinisomesha kwa taabu anakufa hata sijapata kazi nimsaidie??” alisema
“Hapana usiseme hivyo, haya ni maisha ambayo Mungu anayapanga siku zote, sisi binadamu hatuna nguvu kabisa, naomba uelewe hilo”
“Naelewa kaka lakini naumia” nilisema nikafuta machozi yangu na kulala begani mwake.
“Pole sana masikini ya Mungu, nakuhurumia hadi basi, lakini nikuambie tu dhahabu ikipita kwenye moto ndio inang’ara, haya magumu unayopitia sasa hivi ipo siku utayasahau kabisa utaishi kwa furaha isiyo na kifani” aliniamia huku akinisugua sugua begani na mkono wake “Najua maumivu ya kufiwa na baba, mimi mwenyewe alishanifia lakini tazama imeshapita na sasa niko sawa kabisa” alisema
“Inaumaa” nilisema
Siku ile Mido alijua kabisa siwezi hata kupika akaenda kuniletea chips na soda, nilikuwa naweza basi kula? Niliwaza sana.
Akaniuliza “Unataka kwenda kuzika??”
“Ndio lazima niende”
“Nikuombe kitu??”
“Niambie”
“Usiende kuzika, baki tu usome umalize mitihani kisha utaenda baada ya kumaliza”
“Nitaweza kweli?? Kwanini nisifanye mitihani tu spesho mwezi wa tisa wakati watu wakifanya supplementary?” niliuliza
“Jitahidi basi kufanya maamuzi sahihi”
“Sawa”
Alikaa na mimi mpaka saa saba usiku ndipo akaamua kuondoka akiniacha bado usingizi hautaki kunichukua.
Niliwaza sana lakini nilifikia maamuzi kwamba nisiende msibani, nifanye mitihani halafu baadaye nitaenda kung’olea kaburi……….
INAENDELEAAA