UGALI WA BUKUJERO ULIPELEKEA NITOLEWE BIKIRA ZOTE NA WANAUME WATATU KWA WAKATI MMOJA
Namba 18
Tuliishia pale Esta na David walipokuwa mbezi beach, Ndipo Mido akapiga na kumuambia binti aende nyumbani mama yake anamuhitaji.
Endelea
Ilibidi tuondoke na David alinipeleka mpaka nyumbani, lakini yeye aliishia getini, mi nikaingia na yeye akaendelea na safari zake.
Nilipofika nilimkuta mama akiwa amekaa sebuleni anaangalia kipindi cha nyimbo kwenye channel moja iitwayo TUMAINI TV, nikamuamkia
“Mama shikamoo”
Ndipo akanigukia na kunijibu “Marahaba, usharudi haraka tu hivi??” aliniuliza nikashangaa kidogo kwamba kwani si nimeambiwa nirudi kwa sababu yeye alikuwa ananihitaji.
“Nimerudi, si ulisema nirudi mama??” niliuliza
“Mimi?? Nilikuambia urudi mapema lakini sikumaanisha mapema hivi, nilijua labda utakaa sana” bado sikumuelewa mama kitu anachokimaanisha,
Nikamuuliza “Kuna tatizo lolote??”
Akajibu “Hakuna tatizo” huku akiwa anaendelea kutazama kipindi chake taratibu.
Ilibidi kwanza nicheke, nikaingia chumbani kwangu na kuketi kitandani halafu nikamtumia ujumbe, Mido “Nimeshafika nyumbani…mbona mama anasema hamna tatizo” nilimuuliza
Muda huo huo akanipandia hewani na kuniambia “Umefika nyumbani kweli??”
“Ndio…..”
“Oh nilikuwa nakutania tu bhana mama hana tatizo lolote” alisema Mido huku akiwa anacheka cheka, nikakasirika kweli kweli maana bado nilikuwa sijamuelewa
“Utani gani huo?”
“Anyway, unasahau sana mapema, unakumbuka lile jambo lililokukuta siku ile, mbona umeamua tena kurudi kule kule? Huyo dogo ni kijana wa mjini sana” alinionya
“Mh….sio kweli, si ni kama ndugu yenu mmelelewa pamoja, angewezaje kunifanyia kitendo kama hicho??” niliuliza
“Haya basi sawa, lakini mim ninamjua, huenda ikawa wewe umemfahamu juzi au jana lakini mimi ninamjua tangu akisoma shule ya msingi”
Nilitulia kimya, bila kuongea chochote mwishowe nikamuuliza swali “Hivi ishu yangu ya chuo inaendaje maana wewe mwenyewe haupo, ina maana itakuwaje??” niliuliza
“Pole sana…..nakumbuka, nitarudi kesho na tutalifuatilia hilo suala kwa hiyo usiwe na wasiwasi sana juu ya jambo kama hilo” aliniambia
“Okay sawa, nitashukuru”
Siku zote niliishi na Mido kwa upendo wa kaka na dada, japokuwa kuna wakati nilikuwa nikimuwazia masuala tofauti ya mapenzi, yeye hakuwahi kunionyesha kunitaka kabisa, tangu nilipozaliwa sikuwahi kufanya mapenzi, la hasha nilifanywa kwa lazima na vijana wawili, na yeye ninahisi pia alifanya vile akiwa kama kijana wa tatu lakini sikuwa na uhakika sana.
Hata hivyo sikujua ladha ya mapenzi, na hisia zangu hazikuwahi kuwa huko kabisa, nilijiona kwamba ninaweza kuwa hata sister wa kanisa langu pendwa la Katoliki.
Vile vile nilifahamu kwamba hawezik kuwa na mimi kwenye mahusiano kwa sababu alikuwa anajua historia yangu mbaya sana, hata njia tulizokutana sio nzuri, niliamini hata mimi nikiishi naye lazima nitakuwa nakumbuka mambo ambayo sio mazuri kwangu.
*
Kesho yake ilikuwa siku ya Jumatatu, niliamka mapema nikamuandaa Calvin aende shuleni kwa sababu alikuwa anasoma Medium darasa la tatu, alikuwa akichukuliwa na gari asubuhi getini.
Mama naye siku ile aliamua kwenda kazini kwa sababu alikuwa anajisikia nafuu zaidi, akaona ni heri pia akafanya mazoezi na kujichangamsha zaidi.
Nilibaki nyumban peke yangu
Nilipomaliza nilianza kuosha vyombo na kufagia, niliamua kuweka chai yangu jikoni, ikawa inaendelea kuiva taratibu mi nachezea simu yangu tu pole pole.
Ghafla nikiwa nikiwa napita katika mtandao wa Facebook ambao ni mtandao wangu pendwa, nilikutana na chapisho la millard Ayo ambalo lilinishtua kidogo.
Kichwa cha habari kiliandika “DULLAH NA FRANK MAISHA JELA” nikatazama picha ni wale vijana ambao walinifanyia unyama miezi sita iliyopita kule Novo ubungo nikashtuka sana, na kusoma maelezo
“Mahakama ya Hakimu mkazi, Kisutu jijini Dar es Salaam, imewahukumu vijana wawili ambao ni Abdallah Shemweta pamoja na Frank Mwasingo kifungo cha maisha jela baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka hadi kufa msichana wa kazi za ndani wa maeneo ya Novo, Ubungo………….”
Kiukweli nilishidnwa kuendelea, sikujua nini kinachoongelewa kwenye ile habari, ilikuwa kama ndoto, yaani watu walionibaka mimi, ndio waliofungwa kwa kesi ile ile lakini imebadilishwa na kufanywa kuwa ni binti wa kazi, tena ambaye alifariki…mimi kweli duniani kuna mambo………….
NAMBA 19
Nikiwa naendelea kuwaza kwamba hii nchi inaendeshwaje ndipo nikasikia geti limefunguliwa, nikachungulia haraka maana nyumbani nilikuwan imebaki peke yangu, akawa ameingia Mido, akafungua geti kubwa na kuingiza gari yake ndani.
Aliingia bila hata kubisha hodi, mpaka ndani akaita “Mama”, nikaitika mimi
“Mama hayupo”
“Anhaa ameenda kazini?” aliniuliza
“Ndio kaka” nilijibu.
“Okay” alisema akihangaika chumbani kwangu, alijua nipo chumbani kumbe mimi nipo jikoni, alipofungua akanikosa akauliza “Ah kwani wewe uko wapi?”
Nikajitokeza haraka “Niko huku jikoni”
“Aaaah….” alisema na kuingia jikoni akiwa ameshika box la simu mpyaa pee….akaninyooshea “Yani mi najua upo chumbani kwako kumbe uko huku…..” alisema mimi nikatabasamu huku nikipokea lile box la simu akaniambia “Chai imeshachemka mbona huzimi jiko?” aliniuliza na kuzima lile jiko.
“Oh nimejisahau….hii ya nani?” niliuliza kuhusu ile simu aliyoleta
“Ya kwako” aliniambia
“Mh jamani…..” nilisema kwa furaha sikuwa na wazo la kubadilisha simu licha ya simu yangu kuwa iliyopasuka pasuka halafu ya zamani isiyokuwa na uwezo mkubwa. “asante kaka” nilisema
“Usijali” alinijibu kwa mkato huku akitoka nje ya chumba na kwenda nje kabisa ya nyumba ile, akawa amechukua kitambaa mi namuona kwa dirishani, akavichukua viatu vyake kidogo vilichafuka, akawa anavivuta kwa maji yaliyotiririka bombani.
Nilichukua chai nikamiminia kwenye chupa halafu nikaiacha jikoni juu ya meza halafu nikaendam moja kwa moja mpaka chumbani nikawa nimeiweka ile simu kitadani.
Nilirudi mpaka nje nikaegemea nguzo ya baraza na kusema “Nikusaidie kuviosha viatu??”
Akaniambia “Hapana hapa navifuta tu tope nimekanyaga bahati mbaya”
“Sawa, basi ukimaliza uje unywe chai” nilimuambia
“Ah mi nishakunywa kitambo sana….we piga tu” aliniambia
Niliendelea kusimama barazani namuangalia anavyofanya, sijui nifanye nini, kichwa kimeshakuwa kizito, nina furaha ya simu mpya sijui nimpeaje shukrani zangu.
Wakati anamalizia alinigeukia na kuniambia “Kwa hiyo sasa hivi nikuite tu shemeji??” aliniuliza
“Kwanini?” nilimuuliza
“Jana naona David alikutoa out, sio jambo dogo” alisema
“Mhhhh hapanaa kaka, nilienda naye tu kama mtu wa familia, lakini sikuwa na maana ya ku-date, labda kama yeye lilikuwa wazo lake ila mimi hapana, ninahitaji kujua hatma yangu kwanza kabla sijaingia kwenye mahusiano yoyote, mi sinaga hamu na mwanaume kabisa”
“Mh kweli??” aliniuliza
“Ndio….ulijua ndio nimetoka naye? Hapana siwezi nikatoka naye wakati sijakuuliza wewe”
Lenard (Mido) alinigeukia kwa mshangao akaniuliza “Kwanini uniulize mimi??”
“Ah…mmh kwa sababu wewe ndiye unajua mimi nakula nini, navaa nini, nalala wapi….na mambo mengine…siwezi kukurupuka tu”
Mido alianika viatu kisha akanitazama na kuniambia “Ni maamuzi yako binafsi, siwezi nikakupangia”
“Mmh…siwezi nikakurupuka kaka” nilisema
“Ok, is up to you” aliniambia huku akitoa simu yake iliyokuwa ikiita mfukoni halafu akapokea na kuanza kuongea kwa muda mrefu sana.
Akiwa anaongea, niliona ni bora nikadeki kule ndani, nilianza kudeki, sio pakubwa sana, haikuchukua muda mrefu kudeki, bado aliongea nasimu mpaka nilipomaliza kudeki vyumba vyote na jiko halafu nikahamia sebuleni.
Nilikuwa nadeki kwa kutumia dekio, nimeinama, akamaliza kuongea akaingia mpaka sebuleni na kusimama nyuma yangu nikajua yupo nyuma japo ni mita kadhaa kutoka pale nilipokuwa nadeki.
Niliona aibu kuinama mbele yake, nikainuka na kumgeukia nikitabasamu nikamkuta ameweka sura ukauzu sana, tena kashika simu mkono wa kushoto na kuniuliza
“Ile simu umeweka chaji??”
Nikatikisa kichwa bila kutoa sauti, nikimaanisha hapana sijaweka, akaniambia “Uiweke hadi ijaye ndio utie laini zako”
“Sawa kaka” nilisema nikiwa namshangaa naye ananishangaa kwa muda mrefu sana. Nikaogopa kwanini ananiangalia kiasi kile.
Mido alianza kupiga hatua kunisogelea kisha akaniita jina langu “Esta”
“Abee” nilisema nikimtazama machoni anaonekana kuna jambo limemtinga muda mrefu anataka anieleze
Akameza funda la mate kisha akasema “Nilikuwa nasubiri nikamilishe ile kesi yako, hatimaye nimeimaliza salama” maneno haya yakanikumbushai ile post niliyoona kwa millard ayo kwenye mtandao wa facebook
“Enhee nimekumbuka, nimeona post kama vile wale vijana wamefungwa”
Mido alizidi kunisogelea kisha akanishika begani na kuniambia “Ulipokataa kuwa shahidi, nilitamani ile kesi iishe maana wewe ndiye tulikutegemea lakini kwa bahati nzuri tulifanikiwa kuwaundia ushahidi mwingine mpaka tukafanikiwa leo kuwasweka gerezani”
“Kweli?” niliuliza, sikujua hata machozi yalitoka wapi nikajikuta naanza kulia, sikujua nalia kwa furaha au ni kwa huzuni, sikuamini ipo siku haki itatendeka, niliamini kwamba wao ndio chanzo cha mimi kufeli hata chuo nilijikuta nadondosha dekio chini na kunyanyua khanga nikajifuta machozi.
“Esta” aliniita tena
“Abee” nilisema na kunyanyua uso kumtazama machoni maana alikuwa mrefu sana kwangu Mido, kwa mara ya kwanza nilishuhudia machozi yake, sikujua kwanini alikuwa analia, sijui kwanini alikuwa ameamua kujitoa sadaka ili mimi nitendewe haki
“Nimeteseka sana na hii kesi, nina siku sita sijalala usingizi hata kidogo” alisema
“Pole” nilisema nikimtazama natamani kumfuta machozi lakini sina mamlaka ya kuugusa mwili wake, mimi nimekuzwa katika maadili fulani ambayo hayaniruhusu kufanya hivyo kwa mwanaume isipokuwa mtoto wangu au mume wangu tu.
Cha kushangaza Lenard (Mido) alinishika kiunoni, akanivuta kwa nguvu na tukagongana miili, niliogopa, nikamtazama yupo serious, akaanza kusema kwa sauti hafifu kabisa
“Niliumia sana uliponiambia kwamba umeenda Mbezi beach wewe na David, namjua yule ni kicheche alikuwa ameshakutaka” alisema na kunivuta zaidi akanitazama na kuendelea “Niliumia kwa sababu sihitaji mwanaume yeyote awe karibu yako kwa sasa”
Nilibaki namshangaa, mbona maneno mengi, nilijiuliza kumbe ananipenda muda wote kaka Mido?. Nikatulia bila kuongea akaniambia “Esta”
“Abee”
“Nakupenda, nakuhitaji uwe wangu wa pekee” aliniambia
“Mh??” niliguna sikujua nisemeje
“Naomba please hiyo nafasi iwe yangu, nimekuchunguza muda mrefu, nimeona una kila sifa ya kuwa mke wangu tena mke bora kabisa” aliniambia mimi namshangaa machoni, siamini nahisi ni ndoto, sikujua ipo siku ataniambia mambo hayo ya mapenzi
“Nijibu sasa hivi niondoke kwa amani tafadhali”
“Mh….” nilishindwa kusema chochote kwa sababu sikuwa na wazo hilo kabla.
JE NIMJIBU NINI?
ANAFAA KUWA MUME AU HAFAI?
NAMBA 20
Katika kutazamana kwa muda mrefu, machoni, ndipo Mido alishusha mdomo wake taratiibu halafu akanibusu mdomoni mwaah na kuniachia.
Tulizidi kutazamana, natetemeka sikujua kama tukafikia huko kabisa, nikasikitika nikaona maumivu yanaenda kuisha katika maisha yangu.
Alitoa wallet mfukoni akatoa shilingi elfu ishirini, akanipatia na kuniambia “Katengeneze hizo nywele zako….mimi naondoka”
“Asante Mido” nilisema
Mido aligeuka na kutoka nje, akachukua viatu vyake akavaa na kufungua geti, akatoka na gari yake.
Ilichukua takribani dakika tatu, nimesimama katikati ya sebule, ninawaza tu, akili imeganda nawaza kilichotokea sijui ni kitu gani.
Nikaja kushtuka na kutazama, maji yanarudi kule nilipokuwa nimemaliza kudeki, ikabidi niendelee na zoezi la kudeki mpaka nikamaliza, nikaoga na kunywa chai halafu nikabandika maharage jikoni ili niweze kuandaa chakula cha mchana.
Nilifanya hivyo, sikuwasiliana na mtu yeyote siku ile, nilikuwa na wasiwasi tele, nilikuwa najiuliza itakuwaje kuhusu historia yangu na jinsi tulivyokutana mimi na na Mido, niliona kabisa, hata kama anadai ananipenda lakini hawezi kunipenda maana anajua nilipopigwa katika enzi za usichana wangu.
Niliogopa historia, ni ngumu kuifuta, nikimuona tu ndicho ninachokikumbuka, nilikuwa nawaza nifanye nini ili niwe nasahau lakini hakuna, nilikuwa nashindwa.
*
Baada ya kupika chakula cha mchana nilienda moja kwa moja mpaka saluni moja hivi, ilikuwa nje tu kwenye fremu za jirani na pale kwa mama mlezi wa Mido, nilianza kusukwa rasta aina ya Yeboyebo, nilikuwa sijasuka muda kweli kweli.
Nilisukwa kwa muda mrefu, mpaka ilipofika mida ya saa kumi, nilisitisha zoezi nikampokea kwanza Calvin ambaye alitoka shule, kwa nia ya kwenda kumpatia chakula na kumuweka sawa pale nyumbani.
Nilimuacha akila nikarudi kuendelea na zoezi la kusukwa, nilisukwa mpaka saa kumi na mbili jioni, ambapo nilipomaliza nilirudi nyumbani, kulingana na kichwa kuvutwa, nilikuwa ninaumia sana kichwani,
Nikachukua simu yangu ambayo muda wote ilikuwa ndani, nikakuta missed call mbili za Ally pamoja na message mbili za Mido,
Moja ilikuwa inasema “Nakupenda sana” huku nyingine ikisema “Naomba usinikatalie ombi langu, nimeshakuweka kabisa kwenye bajeti yangu ya ndoa mwakani”
Japo nilitamani kuwa na mwanaume lakini niliona Mido sio wa aina yangu, sio kwa ubaya ni kwa sababu niliamini hatukupatana kwenye mazingira sahihi, niliipambanua akili yangu mwenyewe nikaamua kumpa ombi langu
“Kaka Mido nashukuru kwa wema wote ambao umewahi kunitendea, lakini naomba unisamehe kwanza kabla sijasema haya…..mimi ninaomba tuwe kama tulivyokuwa nikuchukulie tu kama kaka yangu inatosha”
Ile message haikujibiwa kwa haraka, hivyo nikachukua fursa ya kumpigia Ally, tuliongea mambo mengi lakini yalihusu shule, nilimdanganya kwamba nitarudi kufanya Supp ila siku na uwezo wa kufanya supplementary maana nilikuwa nimeshadisco chuo moja kwa moja
Tulipomaliza kuongea, nilichukua ile simu mpya nikaiweka laini na kuiwasha, kiukweli ilikuwa simu nzuri sana. Nyepesi ukilinganisha na ile niliyokuwa nikiitumia siku zote, hakika niliona kama vile nimechelewa sana kuzijua simu nzuri, nilifurahi
Nilikaa nikashika tama, nikawaza kama dakika thelathini, namuwazia Mido, kwanini ananipenda? Nikapata majibu kwamba kumbe wema wote aliokuwa akinitendea malipo yake yalikuwa ni mapenzi, nilimuhurumia,
Sio kwamba Mido nilikuwa simpendi, nilimpenda sana, maana kila wakati wa huzuni yeye ndiye alikuwa karibu yangu, lakini sijui kwanini nilikuwa nikipata mateso makubwa sana kila nilipokumbuka sehemu tulipokutania mimi na yeye.
Nilijisikia hofu kubwa katika moyo wangu, nikajiona kabisa simtendei haki, nikatamani kumjibu kwamba niko tayari lakini bado nafsi ilisita
Usiku saa tatu, Mido alinipigia simu akaongea kwa sauti ya upole sana akiniuliza “Kwanini umeamua tuwe kaka na dada Esta??”
Na mimi nikamjibu “Mimi sio mke sahihi katika misha yako Mido”
“kwanini usiwe mke sahihi? Mimi ndio ninaona kwamba unanifaa ndio maana nimekuomba uwe mke wangu Esta” aliniambia
“Mido, unanifaa mimi kuwa mume wangu lakini mimi sifai kuwa mke wako” nilimuambia
“Kwanini unasema hivyo lakini? Kwani wewe una kasoro gani Esta”
“Naamini unafahamu kila kitu, mazingira tuliyokutana mimi na wewe Mido, sio rafiki, imagine una uwezo kweli wa kuvumilia historia yangu mbaya vile ukubali kunioa??”
“Mimi nimekujua katika hali hiyo hiyo, nimekupenda hivyo hivyo, ndio maana nimeona unafaa, historia haizingatiwi, nimezingatia misimamo yako, na namna unavyoishi, una nidhamu unajituma, unafaa kabisa kuwa mke wangu”
“Mido naogopa sana,…..nishafikiria kuwa sister” nilisema
“Sister ni kazi nzuri lakini kama hauna wito, basi tafadhali, nitakutunza utaishi kama malkia, nakupenda mno, nimevumilia vya kutosha, naomba unielewe”
“Nikuulize swali??” nilimuuliza
“Niulize”
“ina maana Mido, kipindi chote ulichokuwa ukinisaidia, ulikuwa unajua malipo yake ni kukupa mapenzi??” niliuliza
“Ahhh hapana hapa hapa…..tena hili wazo la kukupenda limeanza kipindi upo likizo, nilijikuta nimeshakuzoea, ulipoondoka tu, nilijikuta nabaki upweke, lakini vile vile ukiwa kwenu ulikuwa unanijali mpaka basi……kiukweli nikaamini wewe ndiye mwanamke wangu wa ndoto”
“Mh” niliguna
“Unaguna?? Embu nijibu basi nilale kwa amani”
“Ndio halafu kwanza mama yake Calvin vipi?” niliuliza
“Ah ameshaolewa huko Zanzibar” aliniambia “Halafu achana naye sisi tuwaze ya kwetu wenyewe”
“Uko tayari kubeba historia yangu??” nilimuuliza
“Historia yako tayari ninaijua tangu zamani, nitashindwaje kuibeba na nimeibeba tangu mwanzo? Ningekuwa ninaiogopa hiyo historia, basi nisingekuambia haya maneno leo” aliniambia
“Basi nitakufikiria juu ya hilo, maana halikuwa akilini mwangu kabisa ka Mido”
“Sina budi kukusubiri Esta” aliniambia
“Sawa”
Tuliongea mambo mengi lakini mwishowe kila mtu alilala zake…….
NAMBA 21
Usingizi unakuja basi? Nilishawahi kuwa na mwanaume tunaonana kipindi nikiwa sekondari, lakini hatukuwahi kufanya mapenzi kabisa, tulikuwa tunakumbatiana na kufanya vitu vidogo vidogo ila kulala naye hapana.
Niliachana na mwanaume huyo kisa tu alikuwa anataka tufanye mapenzi kabla ya kuoana, hakika nilikuwa sihitaji hiyo sifa ya kuolewa bila kuwa bikira, ila shetani alinishinda akaitoa kabla ya ndoa, sio kwa mimi kupenda.
Nilipokuwa kitandani usiku, nilimuwazia sana Mido, nilikumbuka mambo lukuki ambayo alikuwa amenifanyia tangu tulipoanza kujuana, hakika kumbukumbu hizo zilifanya ilipofika asubuhi tu nikawa niko tayari kuwa na yeye, sikutamani kuipoteza bahati ya kupata mume bora kama yule.
Nilimpigia saa kumi na mbili kamili, nikashika ile simu mpya ina chaji asilimia 97 yaani tangu jana nimeitumia bado hata haiserereki, kiukweli nikasema niongee naye maana ameshanifanya nimekuwa kama vile ni mtoto wa tajiri kumbe maisha ni magumu kabisa.
“Umeamkaje?” aliniuliza halafu akapiga chafya mbili mfululizo
“Salama,….khee mbona unapiga chafya kiasi hicho??”
“Daaa huku ndani kuna vumbi sana….si unajua sijakaa mda na jana nilipofika sikuweza kufanya usafi, nataka nifanye asubuhi hiii……………chiiiiiiiyaaaa” alisema na kupiga chafya nyingine tena
“Oh…..nije nikusaidie kufanya usafi au??” niliuliza
“Ningefurahi sana”
“Hahaha eti ungefurahi…uje unichukue sasa” nilimuambia, nilikuwa nishaamua kuwa naye katika mahusiano ile serious.
“Saa ngapi??”
“Nikishamaliza kazi za hapa nyumbani saa nne”
“Sawa”
Nilimuandaa Calvin, akaenda shuleni, mama naye alijiandaa akaenda kazini kwake, huku akiniacha peke yangu nyumbani.
Nilifanya kazi zangu haraka haraka, nilihitaji nimalize mapema niende nikapaone kwa Mido, maana sikuwahi kufika.
Baada ya kumaliza kazi zangu nilioga halafu nikanywa chai nikamuambia aje anichukue nyumbani. Akaja na gari akanichukua mpaka alipokuwa akiishi.
Mido alikuwa akiishi maeneo yaitwayo Kimara baruti, licha ya kuwa mbali na barabarani lakini yeye hakupata taabu kwani alikuwa ana gari lake safi la kutembelea.
Nyumba yake ilikuwa nzuri japo ilikuwa haijakamilika vizuri kwa nje, ila ndani alipiga rangi kila kitu, ilionekana ikikamilika ingekuwa nyumba nzuri sana.
Alinisisitiza kitu kimoja “Wakati wenzako wanaomba mkopo ujitahidi kuomba kwa mara nyingine, nitakusaidia kupambana nao watakupa hata asilimia chache”
“Muda si umeshapita??” nilimuuliza
“Sijui, ila kama kuna nafasi ya kuomba omba tena nitakusaidia”
“Sawa…..vipi kuhusu ishu yangu mimi ya kwenda chuo??” nilimuuliza
“Nitaenda kesho nitafuatilia kama itawezekana nitakuambia”
“NItashukuru sana kaka Mido” nilisema
“Sawa”
Aliniacha nyumbani nikifanya usafi akaondoka zake, sikujua ameenda wapi, lakini alirudi baada ya lisaa limoja na nusu, akanikuta nimeshamaliza kila kitu najisnap tu sebuleni kwake.
Akaketi kwenye sofa lile lile nililokuwa nimeketi, halafu akaegesha mkono begani kwangu na kuniuliza “Unapenda sana snapchat ee??”
Nikacheka sikujua nimjibu nini.
Mido alikuwa mstaarabu ila saa ile ghafla nilishangaa ustaarabu umemuisha akanivuta na kunilaza begani mwake halafu akaniuliza swali
“Umependeza na nywele zako hizi” alisema akizishika shika
“Zinauma” nilisema
“Polee ee” aliniambia nikainuka najitoa kwake na kumjibu asante lakini akanivuta kwa nguvu hali iliyopelekea nilaze kichwa changu mapajani kwake nikawa natazma juu.
Aliniangalia huku akitabasamu nikajikuta naona aibu nikafunika uso kwa viganja vyangu akawa anaitoa, sasa katika kuitoa tukaanza michezo ya ajabu ajabu pale, mwisho wa siku akanibeba mzima mzima na kuanza kunizungusha zungusha pale sebuleni.
Nilijisikia furaha ya ajabu, sikuwahi kuwa karibu na mwanaume kwa burudani ya mapenzi, ambaye nilikuwa na hisia naye, nilikuwa nimekuwa na mpenzi lakin kipindi hicho ilikuwa ni ile kitoto toto.
Kwa kujisahau akanipeleka mpaka chumbani kwake akanilaza kitandani kwake chali halafu akaanza kunichezea, tukachezeshana pale japo nilikataa kataa mara ya kwanza, lakini mwisho nilijikuta nimedondokea kwenye tendo la ndoa taamu….sikuwahi kulipata kabla…….
NAMBA 22
Nilifurahi sana mapenzi yaliyopatikana kwa Mido yalinipunguzia stress, sikujua kumbe mapenzi nayo yana nafasi katika ubongo wa binadamu.
Lakini mwishowe nilimuuliza swali “hatujapima, halafu tumelala tu? Unaniamini?”
“Nakuamini si ulitumia dawa?” aliuliza
“Ni kweli, ila sijaenda kupima nijue kama kweli mimi ni mzima”
“Okay tutaenda”
Baadaye alinichukua akanipeleka hospitali tukapima, kipindi hicho nilikuwa nimeshamaliza ile dozi ya miezi sita ya PEP, na afya ilikuwa nzuri ngozi yangu ilirudi kwenye hali ya kawaida
Tulipima, ilionekana alikuwa anajiamini sana, na kweli wote tulikuwa salama, nilifurahi pia
*
Saa kumi alinirudisha nyumbani nilikuwa mwepesi sio kawaida, yaani siku ile ile nilijikuta nimempenda kuliko ilivyo kawaida, nilimpenda mno mno mno….nikajikuta muda wote natamani kuwa naye karibu lakini ndio hivyo alikuwa bize mno na kazi.
Baada ya mapenzi yale tuliyofanya nilishangaa Mido ananijali kupita maelezo, alinipenda sana pia na mimi nilimpenda, sasa nilianza kumpenda hadi Calvin kama mwanangu.
Siku moja Mido alikuja nyumbani pale, akanikuta nimekaa nacheza na mtoto wake, akaniambia
“Nimetoka kwenye chuo chenu kule, wanasema ni ngumu sana, lakini wameniambia kesho niende na wewe” aliniambia
“Kweli??”
“Ndio”
“Sawa”
Nikiwa nimekaa sebuleni jioni, mama Lenard aliniita
“Esta” alikuwa ameketi kando tu
“Abee mama” nilisema
“Kiukweli wewe ni msichana msafi sana, kuanzia tabia na hata namna unavyoishi…nilitamani uwe mkwe wangu” aliniambia nikatabasamu kwa furaha, kumbe ndo kwanza ananipandisha wazimu kwa mtoto wake nimng’ang’anie
*****
Kesho yake mimi na Mido tuliondoka kwenda mpaka chuo, nilikuwa nahofia sana, tulipofika alinikutanisha na walimu kadhalika walionifundisha, mi sikujua kwamba ameongea nao nini, lakini baadaye nilipoangalia matokeo nilikuta zimepunguzwa supplementaries tatu, zikabaki mbili kwa semester one na mbili semester two ambapo jumla zimekuwa nne,
Kiukweli nilifurahi sana sana sana, angalau lengo langu lingetimia, nilimshukuru sana Lenard. Licha ya kujua ni rushwa imetumika lakini sikuwa na chaguo sahihi.
“Umefanyaje mpaka wakakubali mpenzi??” nilimuuliza nikiwa nimemuwekea miguu mapajani mwake akawa anaipapasa
“Mipango tu, niko tayari kufanya mambo kama hayo kwa ajili yako ili uwe na furaha, sitokubali uteseke…..”
“Jamani Baby” nilianza kuzoea kumuita kimahaba
“Ndio, wewe cha muhimu ujiandae kwa mitihani yako, soma kwa bidii,,….nitaleta housegirl mwingine hapa ili wewe usome”
“Mitihani imeshakaribia, inabidi nianze kusoma kesho, material yako kule shekilango” nilisema
“Sawa hamna shida basi”
“Sawa”
Maisha yaliendelea, ilipofika muda mrefu kidogo mama yangu alinipigia simu na kunijulia hali. Kikubwa zaidi alichotaka kujua ni kuhusiana na ishu nzima ya ada….aliniambia ameshapata michango anitumie.
Nikamjibu anitumie tu kwenye namba yangu, ili nilipie mwaka wa pili.
Siku zilisogea, mpaka mitihani ile ikapita, sasa nikarudi chuo rasmi, kosa moja au bahati moja njema, nilichanganywa na mapenzi, sikuwa mjanja sana katika hilo kwa sababu niliyaibukia ukubwani, hii ilipelekea mimi kuishia kushindwa kujizuia na kucheza na kalenda, nikajikuta nimenasa mimba.
Niliponasa tu hivi, mama yale Lenard alikasirika sana, aliposikia ni ya Lenard alimfokea sana, tukakosa amani, lakini hakutaka nitoe, akamuhimiza Mido anioe haraka, hataki dhambi kwake, alikuwa mstari wa mbele mbele za Mungu.
Mido akaanza kuhangaika masikini ya Mungu mpaka nilimuhurumia, akajichanga Changa akaenda nyumbani na kunilipia mahari halafu, kipindi cha likizo fupi tu tulifunga ndoa licha ya kuwa na sherehe ndogo lakini nilifurahi tuliingia kwenye ndoa
Mungu alinijalia, nikawa nasoma kwa bidii mimba haikunisumbua sana, nilishirikiana na mama Lenard kufanikisha mpaka mtoto wangu wa kike akazaliwa salama, nikaendelea kusoma mpaka nikamaliza chuo mwaka 2022
Sasa hivi niko tu nyumbani nalea huku nikisubiri kama nitapata ajira, lakini namshukuru Mungu ndoa yangu ina furaha.
Alinikuta katika dhiki, lakini alipambana mpaka nikawa sawa na furaha ikarejea kwangu. NAMPENDA SANA MUME WANGU
“KUTOKA KWENYE DHIKI SASA NI FARAJA”
ASANTA KWA KUFUATILIA MKASA HUU WA MAISHA YANGU, MUNGU AKUBARIKI, NAKUOMBEA UFANIKIWE.
MWISHO