MWANAUME WA NDOTO ZANGU
SEHEMU YA 96
Ajabu ni kwamba badala ya kwenda hotelini au lodge au gest eti nilirudishwa nyumbani, nilimtazama Genson wangu nilitamani nimuulize inakuaje tena? Mbona haonyeshi uchungu wa kutaka kunifaidi?. Hata hivyo niliogopa kumuuliza, na kwa jinsi ambavyo alikuwa anafurahi hakuonyesha kabisa kuwa na mawazo hayo ya kipuuzi, sijui alikuwa anawaza nini.
Tulifika nyumbani kwangu kisha bebi wangu alikuwa wa kwanza kushuka, alishuka kisha alizunguka upande wangu alinifungulia mlango kisha aliniambia nishuke, nilishangaa sana ila sikuwa na jinsi; nilishuka. Alinikumbatia, alinipiga mabusu kisha aliniaga akitaka kuondoka. Nilimshika shati nilimrudisha nyuma, nilimgeuza kwangu kisha nilimtwanga denda zito, waziwazi nilimuonyesha kuwa nahitaji dudruu!! Alinielewa sana ila alicheka tu kisha aliniambia mambo mazuri hayataki haraka.
Baada ya kauli hiyo alijitoa kifuani kwangu kisha
alirudi kwenye gari, aliondoka, aliniacha nikiwa bado nimeganda, japo nilivishwa pete lakini niliumia! Nilitamani hata kama hataki tufanye basi ni bora tungelala pamoja tu nipate joto lake, lakini ndo hivyo mwanaume hakuwa na tamaa kwangu.
Taratibu nilipiga hatua nilizama ndani, nilikutana na kihoja!! Eti nilikuta mama yangu akihesabu mihela, alilamba mate kwenye dole gumba kisha alihesabu wekundu wa msimbazi. Alihesabu akiwa anachekelea. Nilimuuliza ni bei gani alinijibu ni million 5, nilimuuliza kapata wapi? Alinijibu ni pesa zangu za mahari ambazo zililipwa na Genson, aisee nusura nizimie kwa furaha!! Nilidhani jamaa alitaka kunioa bure bure!! Kumbe tayari alinitolea barua na mahari kimya kimya pasipo mimi kujua. Alifanya hayo yote bila hofu kwa sababu alijua kwake sijiwezi!! Oooh jamani Mungu apewe sifa.
Zile pesa tuligawana pasu pasu, mama 2.5 na mimi 2.5. Na uzuri ni kwamba hatukuwa na
ndugu wa karibu au ndugu wa damu ambaye alikuwa na vigezo vya kupokea mgao wa mahari yangu, hivyo basi mahari tulizibonda wenyewe. Tuliagana kwaajili ya kulala, mimi nilioga kwanza kisha nilielekea chumbani kitandani, siku hiyo sikupata usingizi, muda wote niliitazama pete yangu!! Sikuamini hata kidogo.
*****
Siku iliyofuata asubuhi na mapema Genson alinifuata kisha tulielekea hospitali kwaajili ya kujua hali zetu za kiafya. Tulipimwa magonjwa yote kwa njia ya damu, mkojo, joto, baridi na mengineyo, wote tulikuwa fiti. Baada ya vipimo tulielekea kanisani kwaajili ya kukamilisha taratibu za ndoa ikiwemo taarifa zetu muhimu na matangazo. Jamaa alikuwa siriazi kweli kweli, aliamua kunioa. Mi nilidhani angeanza kunitumia kwanza, angenichakaza kwanza
kisha ndo afikirie kunioa lakini hakunifanyia dhambi hizo.
Taarifa za ndoa yetu vilianza kutangazwa kanisani, kila mtu alifahamu. Wale wenye mapingamizi waliambiwa wayatoe haraka kabla ndoa haijafungwa. Kwa mujibu wa ndoa zetu sisi wakatoliki ni kwamba kama akitokea mtu akapinga ndoa yako kwa sababu flani ya msingi, hiyo ndoa haiwezi fungwa.
Sasa kumbe Nasri bado alikuwa ananipenda, aliumia sana kusikia nataka kuolewa. Baada ya kusikia matangazo ya ndoa yangu kutoka kwa watu, alinifuata kazini kwangu kisha alinipa masharti yafuatayo.
“Binafsi sioni sababu ya kwanini hunipendi, kama nilikukosea basi nina haki ya kusamehewa kwa sababu mimi ni binadamu. Gensuda kaa ukijua kuwa nakupenda sana kuliko unavyofikiria, ni tamaa zangu za ngono tu ndizo zilifanya nikupoteze. Pia yule Rahabu
aliniroga nikuone huna mvuto!! Nisamehe sana… Naomba badili lengo lako la kutaka kuolewa na Genson, kataa hasikuoe, stopisha ndoa yenu…
Mimi nipo tayari kuiba au kuuza mali zangu ili nikupe chochote turudiane… Na kama ishu ni dini, nipo tayari kuwa mtoto wa Yesu, nipo tayari kuwa mkristu ili tu nikuoe. Na kama jamaa alikulipia mahari million 5, mimi nipo tayari kukupa million 6,7,8,9 au 10… Vipi upo tayari mpenzi?”
“Shenzi wewe!! Hivi unadhani mapenzi ni pesa. Ingekuwa mapenzi pesa ningeolewa na wanasiasa ambao nusura wanipeleke jela…
Hizo million 10 unazozitaja unadhani mi sina? Ninazo nyingi sana. Kwa ufupi ni kwamba nakuzidi sana pesa, ule utajiri wako wa zamani umehamia kwangu… Upo titi?”
“Nipo ziwa”
“Habari ndio hiyo. Kuhusu nyumba, nikishaolewa tu naanza kujenga nyumba yangu
binafsi kwa pesa zangu mwenyewe. Alafu naomba usimchukie Genson, yule mtu hajaniachanisha na wewe; ila mimi niliachana na wewe ili nimpate yeye. Na laiti kama wanawake wa Tanzania tungekuwa tunaruhusiwa kulipa mahari basi mimi ningemlipia Genson ili anioe… Nampenda kuliko anavyonipenda! Yani hata ukinihonga dunia hii yote, sitokubali kuwa na wewe shetani. Na ikitokea Genson hanitaki basi nitakufa na utamu wangu”
“Ooh unajikuta unajua kupenda… We kumbe una domo sana… Nimekuleta mjini, nimekuogesha, nimekulisha, nimekunawirisha alafu leo hii unataka wakukule wengine? Hiyo siwezi kukubali… Nakuambiaje bora tukose wote kuliko ukampe Genson… Na kama ukitaka nikuache huru naomba timiza sharti moja tu”
“Sharti gani?”
“Tufanye mapenzi mara moja, mara ya mwisho.
Yaani mara moja tu… La sivyo naenda kutoa pingamizi mbele ya kanisa”
“Utatoa pingamizi gani? Una kipi cha kunipinga mimi nisiolewe?”
“Nitajua mimi, nitatunga uongo wowote ninaojua ili mradi usiolewe… Na nakuhakikishia mambo ambayo nitayatunga kanisa zima halitoamini, Genson hatomini, hata wewe mwenyewe hutoamini. Leo ni jumatano, nakupa siku tatu za kunikubalia ombi langu. Ikifika jumamosi saa sita usiku hujakubali kunipa, jumapili asubuhi utanikuta kanisani… Kwaheri” Aliondoka kwa kasi, aliniacha nikiwa nashangaa, nilishindwa kumuelewa, alinivuruga bila sababu ya msingi.
*****
Ilipita siku ya kwanza nikiwa bado natafakari maneno ya Nasri. Kuna muda nilihisi ni kweli ataniharibia lakini kuna wakati niliona hana lolote bali ananipiga biti tu ili nimkubalie ombi
lake. Niliamua kumpotezea, siku ya pili nayo ilikatika, hatimaye ilifika jumamosi. Asubuhi nikiwa kazini alinipigia simu lakini sikupokea, nilimblock. Alinipigia tena kwa namba mpya kisha aliniambia anaelekea gest kuchukua room ili tukajivinjari kwa muda mrefu. Nilikata simu yake kisha nilimblock tena.
Mida ya saa nne asubuhi alinipigia kwa namba nyingine mpya, aliniambia tayari kashachukua room eti ananisubiri mimi tu. Nililata simu kisha nilizima kabisa, niliona ananisumbua tu. Nilipiga kazi kwa amani hadi usiku saa 2, kabla sijafunga ofisi alinifuata na boda boda aliniambia amekuja kunichukua tuende gest; nilimtukana matusi ya nguoni, alikasirika, aliniambia atakaa gest hadi saa 5:59 kisha ataondoka endapo sitoonekana. Alinitajia jina la gest na namba ya chumba, aliniambia nimfuate haraka kisha aliondoka.
Sikutaka hata kumfikiria, kwa jinsi ambavyo nilikuwa nampenda bebi wangu Genso; sikuwa
na hofu yoyote kuhusu vitisho vyovyote vya mwanaume yoyote. Nilifunga ofisi kisha mimi na mfanyakazi wangu tuliondoka tulirudi makwetu. Masaa yalikatika, ilitoka saa tatu ikaja saa nne na hatimaye saa tano! Nilijifunika shuka gubi gubi kisha nililala usingizi mzuri pasipo hofu yoyote.
****
Siku iliyofuata ilikuwa ni jumapili. Kama kawaida my bebi alinipitia na gari yake, alinichukua kisha tulielekea kanisani. Ni kweli baada ya kufika kanisani nilishtuka kumkuta Nasri akiwa amekaa siti za mbele kabisa nyuma ya wanakwaya. Alafu kwa namna ambavyo alijiachia hakuwa na wasiwasi wowote, unaweza sema nae ni mkristu kumbe sio.
Kumbe nae aliniona nikiingia, alinigeukia kisha alinicheka kwa dharau, jeuri na kiburi! Mara alichomoa simu yake kisha kwa kutumia namba mpya alinitumia meseji, aliandika hivi; “Ibada bado haijaanza, nakupa nafasi ya mwisho.
Tutoke nje tuelekee gest tukafanye jambo letu angalau saa moja tu, la sivyo nitaudanganya umma kwa mambo ya uongo ili tu nikuharibie usifunge ndoa… Najua wewe ni mwanamke bora husiye na skendo, ila leo humu ndani utakufa kwa presha, nitawaambia kuwa wewe ni mcheza porno maarufu hapa africa mashariki na kati, daadeq”
Niliusoma ujumbe huo hadi niliogopa, nilitetemeka kwa hofu, nilijua nikiendelea kuacha simu hewani atanisumbua. Fasta niliizima kisha nilitulia kimya, sikutaka kumtazana usoni. Ila yeye alionekana muda wote akinitazama mimi, hata muda ambao misa ilianza bado akikuwa ananitazama, aliendelea kuniandikia mameseji ambayo sikuyasoma kwa sababu simu nilizima.
Mchungaji aliendesha misa hadi ilifikia ukingoni, na hatimaye ulifika wakati wa kutoa matangazo mbali mbali. Mtoa matangazo alianza na tangazo la sadaka, usafi kisha ndoa kama
SEHEMU YA 97
ifuatavyo….
“Tangazo; Familia ya bwana Mayele inatangaza ndoa ya kijana wao mpendwa Dokta GENSON FISTON MAYELE anayetarajia kufunga ndoa na binti GENSUDA PINSLOTO MWAKONYO
mwishoni mwa mwezi huu; siku ya tarehe 31/1/2022 ndani ya kanisa hili. Hivyo basi ndugu na jamaa, kwa yeyote mwenye pingamizi anaombwa afike ofinisi au kama yupo humu anaweza kusimama kwaajili ya kutoa pingamizi la ndoa hii… Je yupo?”
“Nipo muheshimiwa… Nipooo” Nasri aliongea kwa sauti kubwa kisha alisimama kwa kujiamini, nilimeza mate ya mshtuko kisha moyo wangu ulipiga pah pah pah! Nilivurugwa. Kwa mbali nilimtazama bebi wangu ambaye alikaa upande wa wanaume, macho yetu yaligongana. Genson alionekana kushangaa kitendo cha Nasri kuwepo kanisani, kusimama na kutaka kutoa pingamizi. Pia tukio hilo liliteka hisia za
waumini wengi ambao walitaka kusikia
pingamizi la ndoa.
“Ndugu Karibu sana, je pingamizi lako ni la kuongea mbele ya kanisa au inabidi tukaongelee ofisini?”
“Humu humu ndo safi, tena naomba uniruhusu niongee haraka kabla sijasahau… Nina mengi sana moyoni” Nasri alizidi kukazia, nilitamani nikimbilie nje ila ilishindikana, nilitulia kimya nikitaka kusikia atasema nini.
“Sawa ndugu unaweza kuongea, kanisa linakusikiliza”
“Ndugu waumini, wazee wa kanisa, wachungaji na mapadre; huyu mwanamke Gensuda ambaye anataka kuolewa ni mwanamke wangu nimezaa nae… Hatukuachana kabisa kabisa bali kuna mambo machache yalitokea ili kutuachanisha.
Kwanza huyu Genson kamuhonga mama
Gensuda pesa taslimu million 5 ili tu amlazimishe mwanae afunge nae ndoa”
“Eeeeh makubwaaa” Waumini walianza kuguna
“Msishangae, habari ndio hiyo. Gensuda alikataa sana kwa sababu bado ananipenda mimi. Hivi mnajua kuwa mimi na Gensuda ni mara nyingi tu huwa tunalala pamoja? Kwa
mfano jana alilala kwangu, tulifanya mambo yetu, na yeye ndiye aliniambia mimi nije hapa nizuie ndoa hii batili…. Na kubwa zaidi hivi mnajua kuwa Gensuda hazai? Hana kizazi? Ni mgumba?”
“Aaaahhhh jamani kumbee” Watu waliendelea kushangaa, mimi nilikuwa nalia tu, niliinamia chini
“Tulificha siri hiyo kwa muda mrefu ili hasidharauliwe na jamii. Na ndio maana hataki kuolewa na mtu mwingine zaidi yangu kwa sababu kashazaa na mimi mtoto mmoja haoni sababu ya kuolewa na mtu mwingine..Sasa ebu
niwaulize nyie viongozi wangu wa dini, kama tunaoana ili tukazaliane; je sheria inaruhusu mtu kufunga ndoa na mwanamke mgumba??”
“Hapanaaaa”
“Je kuna ndoa kweli hapa??”… Na kubwa zaidi, Gensuda kasema endapo ndoa hii itakamilika basi atamtilia sumu mumewe afe ili arudiane na mimi “
Kabla hajaendelea kuongea, ghafla kipenzi changu Genson alisimama akiwa analia kisha aliondoka kwa spidi kali alitoka nje!! Aliacha macho ya watu yakimshangaa. Bila shaka alikasirika mara baada ya kusikia maneno machafu ya Nasri. Hakujua kuwa Nasri ni muongo anadanganya ili kunikomoa kwakuwa tu nilikataa kurudiana nae na nilimnyima penzi.
Kwa upande wangu licha ya maneno mengi machafu kuongelewa lakini niliendelea kuvumilia, nilisubiri amalize kila kitu ili na mimi nikichafue. Viongozi wa kanisa walikuwa bize
wakiandika na kurekodi matukio hayo kwaajili ya ushahidi. Nasri bado alisimama kisha aliendelea kuongea;
“Na nilitaka kusahau, jamani kwa mnaonifaham mnatambua kuwa mimi ni muilamu. Sasa ukweli ni kwamba Gensuda kila siku amekuwa akiniambia kwamba haipendi dini hii, anaichukia sana, hataki kuwa mkristu ni vile tu alizaliwa kwenye familia ya kikristu… Na ndio maana mwanzo alibadili dini alinifuata mimi, amesema tena kwamba kwakuwa haipendi dini hii muda si mrefu atabadili tena Di “
“Stooop Nasri, inatoshaa… Inatosha inatosha. Umefanya hadi mume wangu mtarajiwa aondoke bila kupenda. Binafsi sidhani kama mtu mwenye akili timamu anaweza kukuelewa. Pia nimeshangaa sana kanisa limeruhusu ujiachie unitukane kwa matusi mazito Jamani
waumini huyu shetani ni kweli aliwahi kuwa mume wangu, hataki niolewe na Genson, alinipa masharti kwamba nikikataa kurudiana nae
atatoa mapingamizi ya uongo mbele ya kanisa… Nilidhani anatania kumbe kwa akili zake mbovu ameamua kuja kujilaani mbele ya kanisa… Mimi sitaki kuzungumza kwa maneno, ushahidi wote ninao… NILIMREKODI KWA SAUTI, MESEJI ZAKE ZOTE ZIPO, JE NARUHUSIWA KUZIONYESHA HAPA?”
“Unaruhusiwaaa… Na ikiwa ni kweli huyu shetani leo afunzwe adabuuuuu…” Watu walipiga kelele!
Nasri baada ya kusikia hivyo alikurupuka alitoka nduki, ndani ya kanisa kulisikika Mshikeni huyooo, huyooo akamatweeee mshikeee
mshikeee…. Ilikuwa balaa, pia lilikuwa ni tukio la kushangaza sana. Nilipita mbele niliwaonyesha viongozi ushahidi wote, walijionea, walitangaza mbele ya kanisa, kila mtu alinipa pole, na mwisho misa iliisha nikiwa mshindi japo niliaibishwa sana.
Hata hivyo nilifurahi sana kumalizana na Nasri,
kwa namna ambavyo nilimuumbua niliamini hatonisumbua tena. Shughuli ilibaki kwa mume wangu mtarajiwa, sikujua huko aliko ana hasira kiasi gani. Sikujua anajisikiaje kutokana na maneno ya Nasri. Sikujua nitaanzia wapi ntaishia wapi kumuelewesha hadi anielewe.
Niliogopa sana kwa sababu sikutaka kumpoteza kipenzi changu na sikutaka kuikosa ndoa yangu pendwa.
Baada ya kutoka kanisani fasta nilichukua bodaboda nilielekea nyumbani kwa Genson lakini sikumkuta, nyumba ilifungwa. Nilijaribu kumpigia simu iliita tu lakini hakupokea, meseji zangu hakujibu, nilijua kuwa tayari kashakasilika!! Hapo sasa tumbo langu lilipata moto, mwili ulichemka, nilivurugwa kila kona.
Nilielekea hospitali nako sikumkuta, kila niliyemuuliza alisema hajamuona!!
Nilichanganyikiwa kiasi kwamba nilikaa chini kwenye mavumbi kisha nilianza kulia, nilimtafuta mitaani nikiwa nalia, baadhi ya watu
SEHEMU YA 98
walinionea huruma na wengine walinicheka wakioniona chizi.
Nilimtafuta sana hadi nilichoka, niliamua kurudi nyumbani kwangu nikiwa nimekata matumaini. Ajabu ni kwamba nilimkuta nyumbani akiwa amekaa na mama yangu mzazi, walionekana kuwa bize na mazungumzo, Mara walicheka, nilishindwa kuwaelewa. Sikujua nami nikae niwasikilize au nipitilize niende chumbani kwangu. Lakini kutokana na heshma sikutaka kuwaharibia mazungumzo yao, nilielekea chumbani kwangu kisha nilijilaza kitandani.
Nilitulia nikipangilia maneno ya kumueleza Genson ili anielewe.
Nikiwa bado naendelea kutafakari mara mlango wangu uligongwa, nilimruhusu mgongaji aingie; aliingia Genson!! Nilishtuka kidogo kwa sababu sio kawaida yake, hapendagi kabisa kuingia chumbani kwangu. Pia kwa mambo yaliyotokea sikutegemea kama angeweza kunifuata chumbani. Alinifikia pale kitandani kisha
alijilaza pembeni yangu, alinitazama kwa macho malaini, alitabasam kisha alinibusu! Nilifarijika mnoo!!
“Vipi unawaza sana kuhusu Nasri?”
“Ndiyo, naogopa kukukosa endapo kama uliamini maneno yake… Ni kweli aliwahi kuwa mume wangu lakini hata wewe unajua kuwa simpendi na siwezi kukusaliti”
“Usiogope, pia usiwaze kuhusu Mimi kuondoka kwa hasira pale kanisani. Ilibidi niondoke tu kwa sababu Jamaa alikuwa anaropoka matusi makubwa ambayo nilishindwa kuyavumilia.
Baada ya kufikiria sana niligundua kwanini anafanya vile, anataka nikuache ili mrudiane. Mimi siwezi kukuacha wewe ambaye nakuamini sana, siwezi kuacha mwanamke bora kama wewe!! Sawa mke?”
“Asante Mume”
“Pale sebuleni nilikuwa naongea na mama kuhusu ndoa yetu. Ametushauri kwa sasa
tusisikilize maneno ya watu kwa sababu yatatukatisha tamaa. Ni kweli laiti kama ningemsikiliza Nasri, ningevunjika moyo. Hivyo basi naomba maandalizi yaendelee, Mwisho wa mwezi nakuoa”
“Woow bebiii… Asanteee…. Naomba basi leo tufanye hata Mara moja tu ili niburudike, mwenzio kila nikikuona hivi nahisi ham, naona hasara siku zinapita alafu hunitumii, natamani nipate raha zako mume..”
“Amri ya sita ya Mungu inasemaje?” “Usizini”
“Ili watu wasipate dhambi ya kuzini wanatakiwa wafanyaje?”
“Waoane kwanza”
“Hivi unajua kwanini nataka kukuoa? Ni kwa sababu nataka tufanye mapenzi, tutengeneze familia na MAISHA. Usione sifanyi ukajua sitaki au sina hisia na wewe, nakutaka sana,
nakutamani sana na Nina hamu kukuzidi ila tu sitaki watoto wa nje ya ndoa, sitaki tupate dhambi. Na ndio maana dunia ya sasa vizazi vinaharibika ni kwa sababu watoto wengi wanapatikana kwa njia ya uzinifu, kwa njia ya kutenda dhambi.. Unanielewa lakini?”
“Sawa mume sitokusumbua tena” Niliamua kutulia. Kiukweli mwanaume wangu alikuwa ni wa ajabu sana. Jamaa unaweza sema alizaliwa pekeyake kwenye dunia yake. Kwa kizazi hichi kumpata mwanaume hasiyependa kuzini, hiyo ni bahati kubwa. Jamaa hata kiss hakunipa, hata kunipapasa hakunipapasa, aliniacha kama nilivyo kisha aliondoka alielekea kazini.
Kitendo chake cha kutotaka kufanya mapenzi na Mimi kilinipa maswali na mawazo mengi sana. Niliwaza au ana kibamia? Au shoo zake mbovu sana? Au nae hazalishi? Au ni mwoga wa kusex? Au kuna demu huwa anafanya nae? Au ananipenda ili nimzalie tu watoto lakini sio kulizishana kimahaba? Au anadhani
nimetumika sana kiasi kwamba ikulu yangu haina utakatifu wowote? Anadhani nina bwawa? Niliwaza vitu Vingi ambavyo havikuwa na majibu, na Mwisho nilitabasam kwa sababu aliniahidi tutafanya tukifunga ndoa.
*****
Tangu afanye lile tukio la kanisani Nasri hakuonekana tena mtaani, hakunisumbua tena, na wala sikuona vitisho vyake vyovyote.
Nilishukuru kuona amenipotezea, nilifurahi kwa sababu nilitaka niwe bize na huru kwenye penzi langu jipya.
Baada ya matangazo mengi, maandalizi mengi, kusubiri kwingi, hatimaye siku ya ndoa ilifika.
Namshukuru Mungu kwa sababu tulifanikiwa kufunga ndoa yetu salama, ndoa ilikuwa kubwa. Iliudhuriwa na watu wengi sana, baadhi ya ndugu zangu wa kijijini walikuja, ndugu wa Genson, marafiki zangu na wa Genson, watu
wasiojulikana, hata Oliver nae alikuwepo. Tena yeye ndiye alikuwa msimamizi wa kamati zote ambazo zilifanikisha ndoa yangu. Sherehe za ndoa zilianzia kanisani, ukumbini, na zilihamia nyumbani kwa Genson. Watu walikesha wakila, kunywa na kucheza muziki.
Mimi na mume wangu tulielekea kwenye nyumba mpya ambayo alipanga kwa mwaka mzima kabla hatujajenga nyumba yetu. Nyumba ilikuwa nzuri sana, ilipambwa maua mengi ambayo yalikuwa yanawakawaka, bila shaka iliandaliwa kwaajili yetu wanandoa. Licha ya uzuri lakini haikuwa na vitu vingi zaidi ya kitanda na Godoro tu. Godoro lilipambwa mashuka mazuri, maua mengi, yaani ilifikia hatua mizuka ilinipanda kinomaa!!
Kwa jinsi ambavyo nilisubiri sana siku hiyo nilijua tukifika tu chumbani atanidaka kisha atanimaliza kabisaa!! Lakini haikuwa hivyo, mume hakuwa na haraka kiasi hicho, mwenzie niliwaza ngono lakini yeye baada ya kufika
aliwaza kuoga. Aliniambia tukaoge lakini nilikataa, nilinuna, nilitaka anipe kwanza kimoko, anichafue kwanza kisha ndio tukaoge.
SEHEMU YA 99
Alinifuata kitandani kisha alinibembeleza tukaoge kwanza. Kwakuwa yeye ni mume wangu nilikubali tulienda kuoga. Nilikubali kwa sababu nilitaka nikamalizane nae huko huko bafuni. Alichukua taulo alitangulia bafuni, Mimi nilifuatia. Nilimkuta akivua nguo zake, baada ya kuvua macho yangu yaliganda kwenye ikulu yake, aisee mzigo niliokutana nao sikuamini na sikujua utapitia wapi. Nilibaki natabasam tu, hamu nazo zilipanda zaidi, haraka haraka nilivua nguo kisha nilimrukia nikitaka kulishika na kulichezea lakini alinizuia; aliniambia tuoge kwanza, nilikasirika! Safari hii nilinuna kiukweli ukweli, niliona ananichezea akili. Haiwezekani mwenzie nina wadudu alafu yeye anachukulia utani.
Alitaka kuniogesha lakini nilikataa. Kwa hasira nilijimwagia maji harakaharaka kisha nilibeba nguo zangu nilirudi chumbani. Nilijikausha maji kisha nililala, nilijifunika shuka gubi gubi, usoni nilivimba vibaya mno, nilipata uchungu, nilinuna kiasi kwamba nilitoa machozi ya hasira.
Sikutaka tena kumfuatilia, niliamua kutafuta usingizi japo sikuupata kutokana na hasira kali.
Sasa nikiwa bado nimevimba kwa hasira mara shuka yangu ilivutwa taratibu kuelekea chini, nilibaki mtupu. Kabla sijakaa sawa nilihisi mipapaso kutoka miguuni, mapajani, hadi kifuani. Nilianza kusisimka, wadudu walinipanda kiasi kwamba nilitamani shoo ianze Mara moja. Nikiwa bado naweweseka mara ghafla ulimi wa moto ulipenya ndani ya sikio langu, jamani jamani nusura niungue kwa raha!! Nilidhani jamaa ni boya kitandani kumbe wala!! Alipita shingoni, kwapani, mbavuni, kiunoni na mwisho alimalizia ikuluni;
aliuzamisha ulimi, alifyonza kisha alipuliza!! Weee cha kufia nini? Nilimvuta haraka nilishika mjegeje niliuzamisha ndani, kilichofuata hapo siwezi kusimulia.
*****
Siku iliyofuata asubuhi niliamka mchovu kutokana na shughuli nzito ya usiku, nilikuta mwenzangu kashaamka; alikuwa anafanya usafi. Nilishuka chini kisha nilijikongoja kuelekea bafuni, miguu yote ilikuwa inauma, nilitembea kama roboti vile, kila nikikumbuka nilichofanywa jana nilibaki natabasam tu, zile hamu zangu zote zilikwisha, sikutamani tena kuguswa wala kupapaswa, nilitaka niachwe nipumzike nipate nafuu.
Nilioga angalau nilipata nguvu, nilimfuata mume wangu tulisaidiana kufanya usafi hadi tulimaliza. Pia asubuhi hiyo tuliletewa zawadi zetu ambazo tulitunzwa kwenye ndoa yetu.
Zawadi zilikiwa nyingi kama vile masofa, meza za vioo na viti, kabati, friji, majiko ya gas, unga na mchele, Flat screen, king’amuzi, vyombo na zawadi nyinginezo ambazo zililetwa na gari.
Zawadi nyingi zilitolewa na marafiki wa mume wangu ambao ni watu wenye nyazfa mbalimbali. Tulisaidiana kuzishusha kisha tulizipeleka ndani, tulipanga vitu katika mpangilio mzuri, nyumba ilipendeza sana. Nilihisi kama niko peponi vile, na sio kwamba nilifurahia mali za nyumba yetu bali nilifurahi kuolewa na mwanaume wa ndoto zangu.
Tukiwa nyumbani kazi yetu kubwa ilikuwa ni kula na kutafuta mtoto. Jamaa muda wote alitaka, yaani kila baada ya masaa machache alitaka nimpe mzigo, ilifikia hatua nilianza kuona kero lakini sikuthubutu kumnyima kwa sababu nilikuwa nainjoy sana!! Nilikuwa tayari hata nimpe kila sekunde ilimradi afurahi tu, pia niliamua kumpa vyote kwa sababu nilitaka kuona kama tatizo langu la kushika ujauzito
limeondoka au lah. Nilimwambia afanye anavyojua yeye ilimradi tu nishike mimba, kiukweli nilikuwa nina hamu sana ya kumzalia mtoto mzuri. Ila hofu yangu ilikuwa kwenye kushika ujauzito tu.
****
Wiki ilikwisha, mume wangu alirudi kazini lakini Mimi niliendelea kubaki home kama mama wa nyumbani. Sio kwamba aliniamrisha nibaki nyumbani, hapana, ni Mimi mwenyewe tu niliamua kubaki ili niendelee kuipamba na kuipendezesha nyumba yangu. Genson wangu hakuwa na tabia mbaya za kurudi usiku wa manane, kunipiga, kulala gesti, kuninyima pesa au kunisema vibaya. Kwa ufupi ni kwamba alinipa Uhuru wa Mimi kusimama kama mkewe na mama mwenye nyumba. Alinishirikisha kwenye upangaji wa maamuzi, kutokana na pesa nyingi tulizozipata siku ya ndoa yetu
tulikubaliana tununue uwanja wetu kisha taratibu tuanze ujenzi wa nyumba yetu.
Alinipendezesha, alining’arisha, alinipenda na kunijali; ilifikia hatua nilitamani nimrudishie mahari zake zote ili anioe bure kabisa. Siku chache mbele kama tulivyokubaliana tulinunua uwanja ambao tuliumiliki sote kama wanandoa, kisha tulianza kujenga nyumba ya familia yetu.
Licha ya raha zote ambazo nilizipata ndani ya ndoa lakini bado akili yangu iliwaza kuhusu kushika mimba. Sasa siku hiyo nikiwa nimebaki nyumbani nilipokea ugeni wa kushtukiza, ugeni ambao sikuutegemea, nilitembelewa na Rahabu. Alifika akiwa anachekacheka tu, sikujua nini kinamchekesha. Aliniomba tuingie ndani ili aniambie jambo, kiukweli nilisita kumkaribisha ndani, ila nilishindwa kwa sababu ningeonekana nina roho mbaya; nilimkaribisha ndani, yeye alikaa kwenye sofa lakini Mimi nilikaa kwenye kiti. Alizungusha macho alikagua nyumba, alikagua fenicha na mengineyo kisha
alinigeukia Mimi;
“Hongera kwa kuolewa” Aliniambia akiwa bado anajichekesha
“Asante”
“Pia ongera kwa pesa mlizovuna na mizawadi, naona nyumba pambe”
“Tunamshukuru Mungu”
“Naona sikuhizi unapendeza tu, umeolewa na dokta, ama kweli ndoa tamu Inaonekana
Nasri alikuwa anakufubaza si ndio?”
“Sitaki kumzungumzia Nasri kwa Sasa, samahani lakini”
“Mh we nae kwa kujikuta, kwa maisha gani uliyonayo hadi ushindwe kumzungumzia Nasri? Hivi yule si ndo alikutoa bikra, alikutoa kijijini, alikutoa ushamba, alikupa akili hadi leo hii una mabiashara makubwa lakini hutukumbuki….
Sasa sikiliza, Nasri ameniagiza anasema muazime pesa angalau million moja tu za
SEHEMU YA 100
matumizi… Kwa Sasa sisi tumefulia hivyo basi tusaidie…. Na usije ukasema huna pesa, pesa unazo kama zote… Unanipa au hunipi?”
“Inawezekana ni kweli mna shida, nami ni kweli nina pesa za kuwasaidia lakini kwanini umekuja kwa style hiyo? Mbona kama unaniamrisha nikupe? Kwanini usitumie ustaarabu?”
“Bwana wee ustaarabu huo kwio!!! Mtu
tunakulelea kindumula chako, Toto lako linakula kilo nane alafu kwanini nisikufokee??? alafu hivi unadhani tuna dhiki sana?? Walaaaaa ! Kwanza mi sijafika hapa kukuomba pesa, bali nimekuja kukuambia hivi; HATA KAMA UMEOLEWA NA MWANAUME WA NDOTO YAKO LAKINI MIMBA HUTOSHIKA, MTOTO HUTOPATA, ATAKUVUMILIA SANA MWISHO ATAKUCHOKA KISHA ATAKUACHA UPO
BIBI?? KWAHERI MWAYA”
Na ndio maana mwanzo niliogopa
kumkaribisha ndani kwa sababu nilihisi kaja kwa shari. Ama kweli adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzie, eti aliona wivu kisa nimeolewa na Genson daktari, kisa tu nyumba ilijaa vitu vya thamani, nilishangaa sana.
Alisahau kuwa nilimuachia mwanaume mwenye mali nyingi tu, yaani sisi binadamu sijui kwanini huwa haturidhiki.
Nilimtafakari sana na mwisho nilikumbuka kauli yake ya mwisho, alisema kwamba sitoshika mimba utafikiri yeye ndiye Mungu. Japo niliyaogopa maneno yake lakini niliamini kama ipo ipo tu. Niliogopa kwa sababu sikujua anaringia nini hadi aseme vile. Mwisho nilipotezea kisha niliendelea na kazi zangu.
****
Siku zilikatika, mimi na mume wangu bado tuliendelea kusaka ujauzito. Pia nilikesha kumuomba Mungu anitendee maajabu ili niwakomeshe maadui zangu waliokuwa wananiombea mabaya. Baada ya msako mkali wa mimba hatimaye nilianza kuhisi dalili zote za mwanzo, mara kutapika, kichefuchefu, maumivu ya kichwa na matiti, lakini ubaya ni kwamba kila nilivyoenda hospitali kupima niliambiwa sina ujauzito. Mume wangu nae alinipima sana lakini vipimo havikuonyesha mimba yoyote. Niliendelea kuvumilia, miezi miwili ilikatika, miezi mitano hadi sita. Ilifikia hatua nilikuwa nakesha nikilia.
“Usilie mke, labda muda wetu wa kupata mtoto bado haujafika… Wapo watu wanakaa miaka na miaka, wewe miezi mitano tu alafu unalia?”
“Hapana mume, mi siwezi kuvumilia kwa sababu nataka nikuzalie… Naumia kuwa kwenye hali hii, watu wananisema vibaya… “
“Ni kweli nahitaji sana mtoto lakini mimi najua changamoto za uzazi zilivyo, hivyo vitu ni vya kawaida sana. Pia najua unaogopa labda ipo
siku nitakuchoka nitakuacha, mimi sitokuacha kamwe kwa sababu nakupenda sana. Pia wewe ndiye mwanamke niliyejaaliwa na Mungu, Mungu alikuandaa uje utengeneze familia na mimi. Na kama huna kizazi basi yeye Mungu kaniletea mwanamke hasiye na kizazi, nitaishi nawe milele… Kama ndoa ni majaaliwa, hata watoto ni majaaliwa pia”
“Asante kwa faraja yako mume, na ndio maana nakupenda sana lakini bado nashangaa sana.
Hospitali wanasema sina tatizo lolote la uzazi, wewe mwenyewe ni shahidi. Sasa kwanini sishiki mimba?… Alafu kuna kitu kinanishangaza sana”
“Kitu gani?”
“Kuna wakati huwa nahisi kabisa kuna kiumbe kinacheza tumboni mwangu, huwa napata dalili zote za ujauzito, pia ni miezi sita sasa sijaona siku zangu, we unaona ni mambo ya kawaida hayo?”
“Sio kawaida, kwanza tusali sana, tumuombe Mungu na ikiwezekana tuonane na wataalamu… Kwa maelezo hayo inawezekana una ujauzito mkubwa tu”
Uzuri wa mume wangu ni mwelewa sana. Licha ya kwamba yeye ni dokta mcha Mungu lakini alikuwa anaelewa masuala ya ushirikina.
Kwanza alinipeleka kanisani ambako tulitoa sadaka ya fungu la 10 na tuliomba misa maalumu ya kubariki na kulinda ndoa yetu.
Baada ya hapo alinipeleka kwa mtaalamu fulani hivi ambaye alinichunguza kisha aliniambia nina Mimba kubwa ya miezi sita, ila mimba hiyo ilifichwa kichawi ili isionekane. Na alinitajia mtu aliyefanya hivyo kuwa ni Rahabu. Alifanya hivyo ili niachike kwenye ndoa yangu. Mtaalamu huyo hakunipa dawa yoyote bali alinisomea dua tu, dua ya kunifungua na kunilinda kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu. Pia alinishauri sio kila mtu napaswa kumkaribisha ndani ya nyumba yangu, watu wengine waishie nje tu. Tulimshukuru, mume wangu alilipa gharama ya tiba kisha tuliondoka.
Huwezi amini baada ya tiba hiyo hata tumbo langu ambalo mwanzo lilikuwa jepesi, lilianza kuwa zito. Nilijaribu kupima tena nilikuta kweli nina ujauzito. Pia kadri siku zilivyosonga mbele tumbo nalo liliongezeka ukubwa, nilifurahi sana. Baada ya miezi tisa nilimzalia Genson mtoto wa kike, alifurahi sana.
Taarifa za kwamba nimepata mtoto zilisambaa kama upepo, na hatimaye zilimfikia Rahabu.
Kama kawaida yake alifunga safari alinifuata nyumbani, mkononi alijidai kubeba vijizawadi vya mtoto. Licha ya zawadi zake lakini safari hii sikumkaribisha ndani, tulisimama nje.
“Dada Gensu mwenzio nimekuja kuomba msamaha kwa maneno yangu ya siku ile, nimekosa mdogoako”
“Nimekusamehe”
“Naomba basi tuingie ndani ili nikupe zawadi za
mtoto, pia nataka nimuone mwanao… Mana tangu azaliwe sijamuona… Inabidi nimshike kidogo angalau apate baraka zangu”
” Mtoto amelala, kuhusu zawadi nipe nitampa… Na utamshika siku nyingine”
“Mh sawa… Basi naomba hata niingie ndani, ninywe hata maji tu… Kweli unataka niishie hapa nje utadhani hunijui jamani”
“Hivi wewe Rahabu unataka uingie tena ili uniroge, uiroge nyumba yangu au unataka kumroga mtoto?”
“Ah ah ah kumbe umeshtuka eeh, daadeq ungeniruhusu uone… Kwanza shukuru huyo alokusaidia uione mimba yako, nilikuwa nina mpango niiteketeze kabla hujagundua… Na kwa taarifa yako naomba uje umchukue mwanao Masoud, nimechoka kumlea… La sivyo atalala njaa, atakufa njaa, au nitamuondoa pale kwangu akaishi mitaani huko; umenipata wewe nyau?… Najua Masoud akija hapa mumeo
atakasilika, hatoweza kulea mtoto wa mtu mwingine… Hatoweza kumsomesha, hivyo basi ni lazma utaachika tu…. Nakupa masaa 12 uwe ushakuja kumchukua.”
Baada ya kauli hiyo aliondoka kwa dharau. Niliwaza nifanyaje kuhusu mwanangu? Licha ya kwamba alikuwa anakaa kwa baba yake lakini nilihisi lazma wanamtesa. Nilitamani nikamchukue niishi nae ila nisingeweza kufanya maamuzi bila kumshirikisha mume wangu.
Nilimpigia simu Genson wangu, nilimuelekeza kuhusu maneno ya Rahabu, mume wangu aliniambia nifanye haraka nikamchukue Masoud ili tuishi nae, pia aliniambia kuwa atamsomesha na atamuhudumia kwa kila kitu. Yaani huyu Genson sijui alikuwaga wapi tangu zamani, alifanya nimpende zaidi na zaidi.
Nilimchukua kachanga wangu tulizama kwenye gari kisha tulielekea nyumbani kwa Nasri,
niliwakuta wote ila tu nilikuta mabadiliko makubwa; sikuona kabati, friji, meza za vioo na hata masofa yalipungua! Bila shaka walianza kuuza vitu vya ndani. Sikutaka kuongea nao mambo mengi, niliwaeleza kuwa nimekuja kumchukua mwanangu. Kwa hasira Rahabu alielekea chumbani kisha alirudi akiwa amebeba begi la Masoud, alinitupia.
Nilimchukua mwanangu tuliondoka zetu.
****
Maisha yangu ya ndoa yaliendelea kwa amani, furaha na ushirikiano mkubwa kati yangu na mume wangu. Tulijenga nyumba yetu kisha tulihamia. Mfanyakazi wangu wa dukani alihamia nyumbani kwa mama, hata Masoud alienda kuishi na bibi yake. Kwa ufupi ni kwamba hatukuwa na shida zozote, sikukumbana tena na vikwazo au changamoto zozote za ndoa.
****
Kuhusu Nasri na Rahabu, wao baada ya kuuza mali za ndani; waliuza duka la Rahabu. Pesa ziliwaishia walianza kutegemea mshahara ambao haukuwatosha. Kama kawaida Nasri alianza kukopa hovyo hovyo, mwisho wa siku mshahara wake uliishia kwenye kulipa madeni. Kutokana na ugumu wa maisha waliamua wote wawili kuingia kwenye biashara ya mkaa, walikuwa wanaenda kuchukua kijijini kisha wanauza mjini. Angalau biashara hiyo iliwasaidia na walipiga sana pesa.
Miezi ilikatika, mwaka ulikwisha, nilianza kusikia taarifa ambazo sikujua nizifurahie au nisikitike. Yale mabaya ambayo walikuwa wananifanyia hatimaye yalianza kuwarudia wao wenyewe. Ule uongo ambao walikuwa wananidanganya hatimaye ulianza kuwa kweli. Kwanza nilisikia wamekamatwa wakiwa na gari kubwa la mkaa, pia ndani ya mkaa huo walificha bangi na madawa ya kulevya. Sio hivyo tu bali
walikutwa na nyama ya porini pasipo kibali chochote.
Walifikishwa mahakamani kisha walihukumiwa kwenda jela miaka 15 kwa Nasri na miaka mitano kwa Rahabu pamoja na faini za million 60 wote wawili. Kesi hiyo ilifanya wauze nyumba yao na mali zilizobaki kwaajili ya kulipa faini, kisha wao wenyewe walipelekwa jela. Kwa sasa wao wako jela wanatumikia vifungo vyao, mtoto wao analelewa na mama yake Rahabu.
Mimi na mume wangu Genson tunakula raha za maisha tu, nafurahi kuolewa na mwanaume ambaye niliwahi kumuota ndotoni. Mwanaume huyu alinitoa kwenye mateso kisha amenileta kwenye raha. Hanaga purukushani zozote, ananifanya nijihisi mwanamke. Nadhani story yangu itakuwa funzo kwa wanawake na wanaume wengi katika huu ulimwengu, sina cha kuongeza, ila nawashukuru kwa kuisoma.