MWANAUME WA NDOTO ZANGU
SEHEMU YA 86
Niliwaza nisitumie tena maneno bali nifanye matendo. Kwakuwa hakutaka kunitongoza, na kwakuwa nilimtongoza hakunikubalia niliona bora nitumie mbinu ya kufanya nae mapenzi kwenye siku za hatari ili nifaidike kwa mambo matatu. Kwanza nipate ladha na utamu wake,
pili nilishike mimba yake na tatu atanioa kupitia mimba. Nilitabasam kwa furaha mara baada ya kupata wazo hilo, nilijiona mshindi.
Siku iliyofuata ilikuwa ni jumamosi, siku hiyo Genson alikuwa ana zamu ya mchana.
Nilimpigia simu nilimuomba usiku tutoke out, tuende club tukapate burudani; alifurahi sana na alikubali ombi langu. Basi bwana nilipiga kazi zangu hadi jioni, nilifunga duka kisha nilirudi nyumbani kujiandaa. Kwakuwa nilikuwa mkristu nilisahau yale mambo ya kuvaa magauni marefu, siku hiyo niligonga suruali ya kubana.
Juu nilipiga kishati chepesi ambacho kilisimamisha embe zangu. Hayo yote niliyafanya ili kumtega Genson. Baada ya kujikoki nilimuaga mama kisha niliondoka nilielekea nyumbani kwa Genson, nilimkuta nae kashaulamba; alipendeza kweli kweli.
Binafsi niliamini akiniona atanitamani na atanisifia kuwa nimependeza, lakini kama kawaida yake badala ya kutabasam alinuna;
“Eh eh eh! Kwa mavazi hayo siendi popote na wala siongozani na mtu”
“Kwanini sasa ?”
“Ina maana uislamu ulikuwa unakunyima nafasi ya kuvaa masuruali ya kubana si ndiyo?”
“Jamani hapana, lakini kwani nimevaa vibaya?”
“Cheki hiyo suruali ilivyokubana utadhani mna ugomvi vile, na hivyo vititi umeviboost unataka ukawadangaye watu kuwa hujazaa au?… Ni kweli wewe bado mdogo lakini sio kwa staili hiyo. Kwani mtu akienda club ni lazma avae mavazi ya kutamanisha au ya utupu?… Au unaenda huko kwaajili ya kutafuta wanaume si ndiyo?”
Ghafla nilinuna, na kwa hasira nilitoka nje nilizama kwenye gari kisha nilirudi nyumbani. Ili kumkomoa niliamua kuvaa ligauni likubwaa kama la wabibi, baada ya kubadilisha nguo nilirudi kwake, ajabu ni kwamba alinisifia sana aliniambia nimependeza kuliko wanawake wote
waliopo club. Nilimtolea macho nilizidi kumshangaa, katika maisha yangu sikuwai kukutana na mwanaume wa ajabu kama Genson.
Tulitoka nje kisha wote wawili tulizama kwenye gari yangu, yeye ndiye aliendesha; tulielekea club. Licha ya kwamba sikufurahia vazi ambalo nilivaa lakini nilitabasam moyoni kwakuwa nilikuwa nina jambo langu, niliwaza usiku huo ni lazma nitatimiza lengo langu la kwanza ambalo litatimiza malengo mengine.
Tulifika club, alilipa kiingilio kisha tulizama ndani. Tulikuta nyomi la watu wakitazama na kucheza show ya msanii mkubwa tu wa hapa Tanzania (jina kapuni). Mimi na Genson tulienda kukaa kwenye viti vilivyopo kaunta.
Mimi niliagiza juisi, nilimiminia kwenye grass kisha nilianza kunywa. Mwenzangu aliagiza bia, kumbe ni mwnywaji wa pombe; nilifurahi, niliwaza kama anakunywa pombe; akilewa nitapata kamserereko kwenye kutimiza jambo langu.
Watu walisakata rhumba, walevi walipiga pombe, wapenda madem nao walikamatia viuno vya watu, shoo za wasanii nazo ziliendelea, Genson bado hakulewa; nilimuomba tukacheze muziki lakini alikataa, aliniambia kuwa hawezi kucheza muziki na rafiki yake bali na mpenzi wake, mchumba wake au mke wake tu. Niliumia lakini nilivumilia, masaa yalikatika, kadri alivyokuwa anakunywa pombe ndivyo ambavyo alizidi kuchangamka, alianza kuniongelesha mambo mengi ambayo mengine sikuyaelewa ila niliitikia tu.
Baada ya kugundua kuwa amelewa alitaka hasiendelee kunywa bia lakini niliona haiwezekani, nilimwambia muhudumu aongeze pombe, nilizikusanya nilimpa Genson; nae kwa uchu alizifakamia kama maji, mwisho wa siku alianza kunirembulia macho ya kilevi, mara alilala begani kwangu, mara alinishika kiuno, nilihisi raha vibaya mno!
SEHEMU YA 87
“Gensuuuu-udaar” Aliniita kwa sauti ya kilevi “Abeee” niliitika kwa maringo
“Hivi unajua kuwa wewe ni mtoto mzuri sana… Wewe ni mrembo kuliko wanawake wote wa dunia hii… Yaani nikikupata wewe nitapika sadaka, nitaweka sherehe kubwa, nitapiga muziki wiki nzimaaa…. Ukumbini watu wataingia bureeee…. Lakini nashangaa mtu
mwenyewe hunitaki mimi kisa nimekuwa mlevi… Kila nikikutongoza unanikatalia… Kwanini hunipendi we mrembo”
“Mmh mimi huyo sikupendi wewe… Jamani pombe hizi, ama kweli ulevi noma”
“Oooh unanisimanga… Unaniteta… Unanidharau kisa nimelewa… Kwani mimi nimelewa?”
“Hapana hujalewa jamani…”
“Kumbe unajua… Kwanza ebu simama tucheze muziki… “
Kabla sijasimama tayari alininyanyua alinivuta
kwenye steji, alinizungusha, alininyonga kisha aliniweka kati, weuwee wauweee!!! Nilihisi raha sio raha, utamu sio utamu. Nilijua akili sio zake ila sikujali wala nini, nilitaka hadi akili zikimrudia awe ameshaninyandua na kama mimba awe amenipa. Tulicheza hadi ilifikia hatua alikosa nguvu, alianza kupepesuka tu, tulirudi kaunta alilala kwenye meza. Nilitazama muda ilikuwa ni saa 7 usiku. Alitaka aendelee kunywa bia lakini nilimstopisha, nilimsimamisha kisha nilimkokota kuelekea nje kwenye gari, tulizama ndani tulirudi nyumbani.
Mimi ndiye nilikuwa dereva, na lengo langu lilikuwa ni kulala nae. Nikiwa kwenye gari niliwaza tukalale nyumbani kwangu, kwake au nielekee lodge nikachukue room??. Niliona bora niende gest au lodge ili tukajiachie pasipo usumbufu wowote kutoka kwa ndugu na majirani..
Sijui hata nilipata wapi ujasiri wa kufanya mchezo huo, bila shaka ni hisia kali ndizo
ziliniendesha. Lodge zilikuwa nyingi, nilichagua mojawapo kisha nilizama ndani na gari yangu. Nilimtazama Genson nilimuona kalala fofofo, alikuwa hajitambui hata kidogo. Mi sikujali wala nini, kwanza nilishuka nilielekea ndani; nilichukua room kisha nilirudi kwenye gari, nilimvuta Genson, nilimkokota kuelekea ndani, moja kwa moja mpaka chumbani, nilimtupia kitandani!! Alilala kama mzoga vile.
Hatua ya kwanza ilikamilika, nilitabasam kwa furaha kisha nilijipa pongezi kwa kazi nzuri.
Taratibu nilienda kufunga mlango ili nianze harakati za kukamilisha jambo langu. Kabla sijaanza kazi kwanza nilivua nguo zote nilibaki na kufuri tu, nilienda kuoga kisha nilirudi kitandani; nililala pembeni ya Genson. Kila nikimtazama nilihisi raha tu, nilitamani yeye ndiye angekuwa ananishughulikia mimi lakini kwa bahati mbaya mtu mwenyewe hanipendiii! Inauma sana.
Ulikuwa ni muda wa kazi; nilipaswa nimuondoe
viwalo vyake. Nilianza na viatu, nilihamia kwenye shati lake, nilikuja kwenye suruali, ilibaki boksa pekee. Nikiwa nataka kumvua boksa mara alikohoa, nilishtuka!! Alikohoa tena kisha alijigeuza upande wa pili, nilikosa pozi.
Kutokana na woga niliamua kwenda kuzima taa ili hata akiamka hasinione. Baada ya kuzima taa nililala tena pembeni yake kisha nilitulia. Mwilini bado nilivaa kufuri tu, licha ya kwamba sikushikwa popote lakini mizuka tayari ilipanda; nilihisi wadudu watamu wakinitembea mwilini, nilitamani kupewa vitu tu. Tatizo ni kwamba mtu wa kunipa vitu hivyo alikuwa anakoroma na pombe zake, viungo vyake vyote vililala, sikujua nitumie mbinu ipi kuviamsha.
Muda huo nililala chali nikitafakari. Sasa nikiwa bado nawaza mara alinigeukia kisha alinikumbatia bila kujua. Niligeuka nilimtazama niliona bado kalala! Licha ya kwamba hakujitambua lakini nilifurahia kumbatio lake. Ili kumnogesha zaidi niliamua kumgeuzia mgongo
kisha nilirudisha viungo vyangu vyote nyuma yake, kalio langu loote lilijaa kwenye boksa yake, kwa mbaali nilisikia kitu kimejibu! Mzigo wake ulianza kunisukuma mbele nyuma, kimoyomoyo nilisema hayo ndio mambo sasa.
Nikiwa nasikilizia utamu wa joto lake mara ghafla mkono wake wa kushoto ulifika kifuani kwangu, alianza kuyavuruga maembe yangu, hapo sasa aliniweka roho juu juu, niliweweseka kiasi kwamba nilishindwa kuvumilia. Sikutaka kujua kama kalewa au hajalewa, pale pale nilimgeukia kisha nilimuomba mate; alinipatia mdomo, weuwee!! Nilihisi raha na utamu vikitembea kuanzia unyayoni kwangu hadi kwenye medula obolongata!! Nilianza kutoa miguno ya chini chini, niliogopa hasije akaamka ikawa balaa.
Sasa wakati tunaendelea kupeana busu la kikubwa kwa bahati mbaya mdomo wake uliteleza ulidondokea kwenye embe langu la kwanza, alilibugia mdomoni kisha alianza
kulifyonza! Nilijikunja kushoto kulia na sijui kama sikujikojolea. Uwiii mlevi alijua kunivuruga jamani nashindwa hata kuelezea. Nilipapasa ikulu yake nilikuta mzigo umefumuka kwa hasira, niliona huo ndio muda wa kutimiza jambo langu. Fasta nilishika boksa yake nikitaka kuishusha chini, lakini kabla sijamvua mara alishtuka!!
“We nani??… Unataka kunibaka… Jamani nabakwa mimi…. Majiranii” alipiga kelele
“Genson pliz usipige kelele… Ni mimi Gensu, sikubaki”
“Gensu yupiii…. Nimesema wewe ni bakabaka… Kwanza washa taa…unataka kunibaka mimi sibakiki kirahisi….Ngoja niwashe taa mimi mwenyewe…” Alishuka chini kisha alipepesuka kuelekea ukutani, alianza kupapasa ukuta akitafuta swichi. Fasta nilivuta shuka nilijifunika kisha nilijiziba uso, aliwasha taa alinikuta nikiwa nimejiziba uso.
SEHEMU YA 88
“Wewe ni Gen-su-daa ninae-kujua au ni she-eta- ni….. Kwahiyo wewe ndiye ulitaka kunibaka si ndiyo?…kwanza hapa nipo wapi Ngoja
nikupeleke polisi “
Alianza kuokota nguo zake, alivaa suruali na shat, alimaalizia viatu kisha alipiga hatua kuelekea mlangoni; alikuwa kama teja vile, alifungua mlango alitoka nje, sijui alikuwa anaenda wapi. Haraka haraka nami nilivaa nguo zangu, nilichukua kila kilicho changu kisha nilimkimbilia nikiwa nimenuna..Nilimkuta kashafika getini kwa mlinzi, nilimrudisha kwenye gari kisha tulirudi nyumbani. Nilianza nilimpeleka kwake kisha nilielekea kwangu, siku yangu iliharibika, nilihisi aibu, nilijuta, nilijidharau na niliumia sana kwa kumkosa.
*****
Kulikucha asubuhi na mapema, mara nyingi tulizoea kuamshana kwa kupigiana simu au kutumiana meseji lakini siku hiyo sikuona simu yake wala meseji yake, nami niliogopa kumpigia au kumtumia meseji. Nilifanya usafi kisha nilijiandaa nilienda kazini, sikuwa na raha hata kidogo, bado niliwaza mchezo mchafu nilioufanya usiku uliopita. Niliwaza kiasi kwamba nilitoa machozi, kuna muda nililala kwenye meza kutokana maumivu ambayo niliyapata!
“We Gensu, wewe… We mbona unalala kazini?” Nilishtushwa na sauti ya mdada aitwaye Nadya ambaye ni mteja wangu maarufu.
“Mapenzi yananitesa” Nilimjibu “Kivipi?”
“Kuna mkaka nampenda, ananionyesha ishara zote za mapenzi lakini hanitongozi, na nilishawahi kumtongoza lakini alinikatalia. Sasa jana akiwa amelewa nililala nae godoro moja,
tuliandaana vizuri lakini muda wa kunanii alinikimbia”
“Mh itakuwa una gundu”
“Eti eeeh! Ila kweli, mimi lazma nina gundu.. Sasa nitaliondoaje?”
“Mbona rahisi tu, kaoge maji ya chumvi, oga siku 7 asubuhi na jioni. Hakikisha iwe ni chumvi ya mawe, chota kiganja kimoja changanya na maji ya kuoga; muda wa kuoga kwanza nuwia jambo lako kisha oga maji hayo alafu utaniambia… Kama hasipokutongoza yeye, basi hata ukimtongoza wewe atakukubalia na siku hiyo hiyo mtafanya jambo la kikubwa”
“Wewe jamani usinambie hivyo pliziiii Wallahi
nikifanikiwa nitakupa bonge la zawadi, nitakununulia smartphone ili uache kutumia kiswaswadu”
“Ah ah ah chumvi haijawai kufeli, mimi mwenyewe nakumbuka mume wangu alinipaga mimba kisha alitaka kunitelekeza bila kunioa;
Nikasema kumbe hanijui, wiki moja nilioga chumvi; wiki iliyofuata yeye mwenyewe alinivisha pete, alitoa barua kisha alinioa We
jaribu uonee”
“Asante mwayaa” Nilifurahi kusikia hivyo. Nilimuhudumia haraka haraka kisha kwakuwa ilikuwa asubuhi niliamua kufunga duka kwa muda, nilizama kwenye gari kisha nilirudi nyumbani. Nilinunua chumvi ya mawe ya kutosha. Nilichota kiganja kimoja kisha nilichanganya na maji ya kuoga, nilikoroga ichanganye kisha nilienda kuoga. Nikiwa bafuni kwanza nilinuwia, niliomba maji hayo yaniondolee gundu, mikosi na bahati mbaya zote. Pia niliomba yanibariki niweze kumpata Genson. Baada ya kunuwia nilioga chap chap kisha nilirudi kazini, nilipiga kazi kwa amani kabisa.
Usiku kama kawaida nilioga tena. Siku ya kwanza ilipita Genson hakunitafuta, siku ya pili nilioga chumvi lakini Genson hakunicheki, siku
ya tatu usiku alinipigia. Niliogopa kupokea, simu iliita hadi ilikata. Alinipigia tena, nilipokea.
Nilijua atanikoromea kwa tukio ambalo nilitaka kumfanyia lakini wala hakunifokea, aliniondoa wasiwasi aliniambia niwe na amani zote. Eti aliniomba msamaha kwa kulewa sana, aliniambia hatolewa tena. Yaani alijishusha utafikiri yeye ndiye alinikosea kumbe mimi ndiye nilimkosea yeye. Hadi kufikia hapo nilijua chumvi imeanza kufanya kazi, hali hiyo tu ni siku tatu je nikimaliza siku saba si yeye mwenyewe ataniomba game!
Tuliongea mambo mengi, alinisisitiza nisimkalie kimya kwa sababu anaumia sana kutowasiliana na mimi. Nilifurahi kusikia hata yeye huwa anaumia kwa ajili yangu, nilivimba bichwa nikijiona bora. Baada ya mazungumzo niliendelea kupiga kazi bila wasiwasi wowote.
Pia kama kawaida usiku nilioga chumvi, siku ya nne nilioga chumvi, siku ya tano, ya sita na hatimaye nilimaliza siku saba. Niliamini
SEHEMU YA 89
nishaondoa gundu, mikosi na mabalaa yote!! Nilifanya kazi nikitegemea kutongozwa na Genson muda wowote!!!
Ni kweli Genson alinitafuta mara kwa mara lakini katika mazungunzo yetu hakugusia ishu za mapenzi wala hakuonyesha dalili za kunipenda. Wiki ya kwanza ilikatika nikimtazamia lakini hakukuwa na maajabu yoyote, wiki ya pili nilijitahidi kuwa karibu naye, nami nilijaribu kumfanyia shopping za nguo za ndani na nje, usiku nilimpigia video call tukiwa tumelala, nilimuimbia nyimbo za mahaba, kuna muda nilimnunulia bando za mwezi mzima ili tu anione mtu muhimu lakini akunifungukia kuhusu mapenzi. Nilimtafuta Nadya nilimueleza kuwa dawa yake haijanisaidia.
“Nimeoga wiki nzima, asubuhi na jioni, sijaacha siku hata moja lakini wapi…”
“Duh basi wewe utakuwa una GUNDU GEGEDU” “Eeh ndo gundu gani tena hilo na linatibikaje?”
“Hilo ni gundu lililokomaa, watu wengi wana magundu kwenye ngozi lakini wewe gundu lako limeshafika ndani kwenye damu. Hivyo basi inabidi uoge na kunywa maji ya chumvi ya bahari. Tena bahari zenyewe sio hizi za mikoani, nenda bahari ya Dar! Oga na kunywa maji hayo kwa siku saba kisha rudi Tanga alafu tuone huyo mwanaume wako kama hatokutolea barua… Na ikitokea mwezi huu hakutongozi ujue ni kweli hakupendi na hawezi kuwa wako… ila kama kweli ameumbwa kwaajili yako, we kaoge maji ya Dar alafu wiki ijayo tunakula pilau kwenu”
“Ah ah ah Nadya acha kunifurahisha basi jamani….. Basi sawa mi nimekuelewa… Kesho au keshokutwa naenda Dar”
Kwanza nilitafuta mtu ambaye angeweza kunisaidia kazi yangu ya duka, nilimpata mdada mdogo ambaye ni jirani yangu. Nilimfundisha kazi kwa siku mbili tu alielewa. Pia niliongea na mama kuhusu safari yangu ya Dar ila
sikumuambia naenda kufanya nini. Na mtu mwingine kumuaga alikuwa ni Genson, yeye nilimdanganya kwamba naenda Dar kuchukua bidhaa za simu na vocha ili niziweke dukani.
Alinipongeza aliniambia ni hatua nzuri, alinitakia safari njema.
Kwa mara ya pili nilielekea Dar, sikuwa na ndugu ila pesa zilinipa ujasiri. Nilifikia lodge kisha nilitengeneza urafiki na mlinzi wa lodge ambaye alinieleza mambo mengi kuhusu Dar, alinitajia beach zote na namna ya kufika huko. Siku iliyofuata asubuhi nilienda beach mojawapo, nilikuta watu wachache, nilitazama huku na huko niliona kila mtu yupo bize na mambo yake, niliondoa nguo za juu nilibakiwa na za ndani ambazo hazikuonyesha maungo yangu. Haraka haraka niliingia kwenye maji kisha niliogelea kama bata, jamani jamani nyie acheni tu kumbe kuroga ni kazi sana.
Nilitumia sekunde kadhaa tu kisha nilitoka nje, nilivaa nguo zangu, nilikunywa maji kisha
nilirudi lodge. Jioni nilienda tena, nilifanya hivyo kwa siku saba ili kutimiza masharti. Siku ya 8 asubuhi nilienda kariakoo nilinunua baadhi ya vitu vya duka ikiwemo vocha, makava ya simu, earphones, betri za simu, chargers, USB na vikorokoro vinginevyo. Pia nilinunua zawadi za mama na Genson kisha nilirudi lodge. Siku zote hizo Genson alikuwa ananisumbua kwenye simu akiniuliza mbona sirudi? Au nimepata mwanaume wa Dar? Alionyesha kuwa na wasiwasi juu yangu. Hakujua kuwa mwenzie nilikuwa namroga yeye ili nimpate. Alinisisitiza nirudi haraka kwa sababu amenimiss sana.
Alinipigia hadi usiku wa manane, aliniongelesha kwa sauti tamu za usiku, aliniambia kuwa anaona raha kuchat au kuongea na mimi usiku, ubaya ni kwamba hakunitongoza wala hakuniambia kuwa ananipenda.
Siku iliyofuata asubuhi nilirudi nyumbani, Genson ndiye alikuja kunipokea stendi.
Alinikumbatia mbele za watu wa stendi, yaani
SEHEMU YA 90
Tanga nzima iliamini kuwa mimi na Genson ni wapenzi tulioshibana sana kumbe maskini ya Mungu hali ilikuwa tete! Alichukua mizigo yangu aliweka kwenye gari yake kisha tulielekea dukani, tulimkuta msaidizi wangu akipiga kazi.
Mapato ambayo alikuwa anaingiza yalizidi yale ambayo nilikuwa nayapata, hiyo ni kwa sababu dada yule muda wote alikuwa dukani tofauti na mimi ambaye mara nyingi niliteswa na mapenzi kiasi cha kufunga duka mara kwa mara.
Niliamua kumuajiri rasmi awe msaidizi wangu.
Tulijaza mzigo dukani, palipendeza sana. Hata baadhi ya wateja wa mwanzo walinisifia kwa jambo hilo la kuongeza vifaa vya simu. Kwa jinsi ambavyo Genson alishiriki kunisaidia kupanga vifaa hivyo unaweza sema yeye ndiye alikuwa mume wangu kipenzi kumbe wala!! kazi yake ilikuwa ni kunichekea chekea tu utadhani mimi ni dada yake, kiukweli alinikera sana.
Kwakuwa nilioga na kunywa maji ya bahari niliamini Gundu Gegedu lishaondoka lakini wiki
ya kwanza ilikatika sikuona mabadiliko yoyote, wiki iliyofuata niliamua kujitosa kwa mara nyingine; nilimueleza Genson kuwa nampenda lakini alikataa aliniambia ananiheshimu kama rafiki au ndugu yake wa damu. Kiukweli nilivunjika moyo, nilikata tamaa, kama kuhangaika nilimuhangaikia sana, mwisho niliamua kufunga break! Licha ya kumpenda sana lakini niliona hakuna haja ya kuendelea kumsumbua. Kwakuwa alisema hanipendi sikuona sababu ya kulazimisha penzi, niliapa kwamba sitomueleza tena hisia zangu hadi naingia kaburini.
*****
Ilikuwa ni mimi na biashara zangu, mambo ya mapenzi niliyatupa kule. Pia nilianza kupunguza mazoea na Genson, akinitumia meseji nilichelewa kujibu, simu zake nyingi tu sikuzipokea, na hata usiku akinipigia
nilimwambia nina usingizi; nilikata simu nililala. Sio hivyo tu bali kuna siku aliniletea zawadi (nguo za ndani) lakini nilizikataa, nilimwambia kuwa hana vigezo vya kuniletea nguo za ndani. Nilimueleza kuwa ni mume wangu pekee ndiye anapaswa kuninunulia zawadi hizo. Aliumia sana!!