MWANAUME WA NDOTO ZANGU
SEHEMU YA 81
Nilipata mawenge na muhao, pale pale nilianza kulia. Nilitamani niondoke kimya kimya lakini niliona haiwezekani. Niliwasogelea karibu zaidi ili nao wanione vizuri, ni kweli waliniona.
Genson ndiye alikuwa wa kwanza kuniona, alishtuka, aliganda akinishangaa. Yule binti nae aligeuza macho alinitazama, alishindwa kunielewa. Baada ya kuonekana sikutaka kuendelea kupata maumivu, kwanza nilifuta machozi, niligeuka nyuma kisha niliondoka kwa kasi ya maumivu. Kwa mbali nilisikia Genson akiniita, aliniambia nisimame lakini sikusimama. Nilirudi dukani kwangu nilimkuta Nasri kashafika, alikuwa ananisubiri mimi.
“Umeamini maneno yangu? Si umeona? Mi nilikuambia yule mtu hakupendi na hana mipango na wewe, achana nae. Bora turudiane tu sawa bebi?”
“Bebi shangazi yako…. Mbwa wewe, karudiane na binamu zako na wifi zako na wajomba zako…. Na kwa taarifa yako hata kama ana
mpenzi lakini nampenda na nitaendelea kumpenda” Nilijibu kwa kupanic na kwa hasira, sikutaka kufungua duka; nilizama kwenye gari kisha nilirudi nyumbani nikiwa nalia.
Siku ya kwanza ilipita nikiwa nashinda ndani tu, mapenzi yalinitesa. Muda wote nilikuwa nalia.
Niliwaza kumbe ndio maana Genson alikuwa hapokei simu zangu, kumbe ndio maana alikuwa hajibu meseji zangu, kumbe ndio maana alikuwa hanitongozi. Kumbe ana mpenzi alafu hakuniambia, niliumia sana.
Siku iliyofuata sikwenda kazini, niliendelea kulia. Nikiwa nalia mara mlango wa chumba changu uligongwa, nilihisi labda ni mama amesikia nikilia. Kutokana na hasira sikwenda kufungua mlango, nilitaka aniache nilie hadi sauti ikate.
Nikiwa nadhani ni mama mara nilisikia sauti ya Genson akiniambia nimfungulie mlango, pale pale kilio changu kilikata, huwezi amini nilijikuta nimetabasam bila kupenda, licha ya kwamba yeye ndiye aliniliza lakini nilifurahi kuona
amenifuata nyumbani. Sikutaka kufuta machozi, nilitaka akaone kuwa nilikuwa nalia. Nilienda kumfungulia mlango alizama ndani alikaa juu ya godoro, nami nilifunga mlango vizuri kabisa kisha nilimfuata pale pale kitandani. Laiti kama angekuwa ni mpenzi wangu ningemvamia kwa mabusu tu ili anipe vitu adimu, lakini kwakuwa hakuwa mpenzi wangu nilikaa pembeni yake kwa heshima kabisa.
“Jana ulifunga duka mapema, tatizo lilikuwa nini?”
“Nilikuwa nalia, nilipata maumivu ya moyo”
“Na leo hujaenda kazini, bado una maumivu ya moyo?”
“Ndiyo”
“Kwani una ugonjwa wa moyo?” “Hapana”
“Sasa kwanini unalialia?”
“Ni kwa sababu ya mapenzi”
“Mapenzi yamekufanyaje?”
“Yananitesa, kuna mwanaume nampenda lakini yeye hanipendi… Kumbe hanipendi kwa sababu ana mwanamke mwingine”
“Sasa kwanini unatamani mwanaume hasiye mume wako? Kwanini usitafute wakwako?”
“Aliniambia kuwa yupo singo, nilifurahi kwa sababu niliamini kuwa anaweza kuwa wangu. Hata hivyo bado naamini kuwa anaweza kuwa wangu, naomba nisaidie nimpate”
“Anaitwa nani na anaishi wapi?”
“Ni wewe bwana ebu usijitoe ufahamu. Kwanini ulinidanganya kuwa huna mpenzi? Na yule mwanamke ni nani?”
“Ooh kumbe ndio maana jana baada ya kutukuta pale mgahawani uliamua kufunga duka? Kwahiyo hata leo hujaenda kazini kwa sababu ya hasira zako za mapenzi?”
“Ndiyo”
SEHEMU YA 82
“Yule sio mpenzi wangu, ni mwanamke ambaye nilikusimulia kuwa aliniacha kwakuwa sikuwa na fedha. Leo hii anataka turudiane kwa sababu anaona nina kazi nzuri, pia nina pesa. Yeye ni kama Nasri, najua Nasri ndiye alikuleta pale kwa sababu alituona. Bila shaka nae anataka arudiane na wewe kwa sababu anaona umefanikiwa na una pesa. Sasa ebu niambie, je upo tayari kurudiana na Nasri ambaye alikuacha ukiwa maskini kisha anataka mrudiane kwakuwa umekuwa tajiri?”
“Siwezi kurudiana na mwanaume MCHEME”
“Sasa kama wewe huwezi, kwanini mimi niweze kurudiana na shetani?…. Nilimkatalia, na ndio maana ulimkuta akining’ang’ania na kuniomba turudiane, siwezi kuwa nae”
“Ooh kumbe, basi nisamehe Genson Alafu
unajua nini… Nikuambie kitu?” “Niambie, nakusikiliza”
“Mi nakupenda”
“Mi sikupendi” “Jamani mi nipo siriaz” “Hata mimi sitanii”
“Kwahiyo hunipendi mimi?… Yaani misaada yote uliyonipa alafu hunipendi?”
“Mimi sikukusaidia ili unipende. Alafu kwani mwanaume akimsaidia mwanamke ni lazima wawe wapenzi?”
“Hapana. Lakini mambo yote yaliyofanyika kati yangu mimi na wewe yanaonyesha ishara zote za mapenzi baina yetu. Sasa kwanini hunipendi? Au mimi nina sura mbaya?”
“Hapana”
“Shepu yangu mbovu?” “Hapana”
“Au Tabia na matendo yangu hayakuridhishi?” “Sio kweli”
“Au kisa sina tako kubwa?”
“NI kweli huna ila hiyo sio sababu”
“Au hunipendi kwakuwa nipo kwenye uislamu?… Usijali, nina mpango wa kurudi kwenye dini yangu ya ukristu kwaajili yako… Je upo tayari?”
“Usifanye maamuzi kwaajili yangu, kama uislamu unakufaa; endelea nao, na kama unataka kurudi kwenye dini yako basi karibu nyumbani… Na usije ukadhani kwamba sikupendi kisa dini, dini haina shida yoyote”
“Sasa shida iko wapi? Ina maana sikuvutii kabisa?”
“Unanivutia”
“Na kunipenda je? Hunipendi kweli wewe? Kama unanipenda niambie, mi nishakubali tangu zamani”
“Ukilazimisha kupendwa na mtu hasiyekupenda atakutesa sana. Ukiruhusu mapenzi na mtu hasiyekupenda utapata shida sana. Na ukikubali ndoa na mtu hasiyekupenda; hii dunia
utaiona chungu haki ya Mungu. Hata yule mumeo alikuwa anakutesa kwa sababu alikuwa hakupendi. Inawezekana shida zako ndizo zilisababisha upendane na mtu hasiyekupenda. Bila shaka ulimpenda kwa sababu alikusaidia.
Na inawezekana uliamini anakupenda sana kwakuwa tu alikusaidia vitu vingi. Hicho ndicho kinachotesa wengi kwenye mapenzi. Kwa kawaida ndoa ni makubaliano baina ya watu wawili kutengeneza familia na maisha ya pamoja. Lakini sikuhizi watu wengi hasa wanawake wanadhani ndoa au mapenzi ni sehemu ya kupeleka shida zao ili zikatatuliwe, na ndio maana wanateswa sana. Yule jamaa alikutendea wema, hukutakiwa umlipe mapenzi, ungemshukuru tu kisha ungemuacha aende zake. Mimi pia nimekutendea wema alafu unataka unilipe mapenzi, inaonekana unapenda sana kuteswa kimapenzi si ndiyo?”
“Eeeh jamani sio vizuri hivyo, dhambi hizo wewe”
“Pia usimwamini sana mtu anayekusaidia. Sio kila anayekupa msaada anafanya hivyo kwa wema, wengine ni gia zao tu za kutaka kufanikisha malengo yao ambayo huyajui.
Katika dunia ya sasa tumetokea kuwaamini sana watu wanaotusaidia. Tunawaona wao ndio watu sahihi wa kupendwa. Mtu wa kumpenda sio lazima akusaidie, upendo na msaada ni vitu viwili tofauti. Kumbuka kwamba hata hawa majambazi au wauaji unaowasikia, nao huwa wanatoa misaada kwa watu ambao hatuwajui.
Naomba usiniamini wala usikubali kunipenda, inawezekana Mimi nina matendo mabaya yasiyokufaa.. Pia usichanganye mapenzi na kazi, hata kama sikupendi wewe piga kazi. Bora unikose mimi kuliko ukose pesa… Pia ukiwa na pesa, kwa tabia nzuri ulizonazo hakika hutokosa kupata mwanaume bora; watakupenda wao wenyewe… Kwaheri”
Aliondoka aliniachia maswali mengi sana
kichwani, mambo ambayo alikuwa akiniambia, akinifanyia na kunifundisha yalionyesha waziwazi kuwa NI YEYE WALA SIO MWINGINE. Yaani kutoka moyoni nilimthibitisha kuwa yeye ndiye mwanaume wa ndoto zangu ambaye niliwahi kumuota, sasa kwanini aseme hanipendi? Kwanini aseme nisimuamini? Au alitaka nimchunguze kwanza matendo yake?
Lakini mbona matendo yake yapo fresh tu, hanaga skendo mbovu mbovu, hata kule hospitali kwao yeye ndiye anaongoza kupendwa na watu kutokana na tiba nzuri kwa wagonjwa, anajali watu na hana dharau au majigambo.
Sasa kwanini hanipendi? Hivi ni kweli hanipendi? Nilikosa majibu!!!
Kuna muda niliwaza au niachane nae? Sasa nikimuacha yeye nitampata wapi kama yeye?. Kiukweli kwa namna ambavyo nilikuwa nampenda nilikuwa tayari hata niwe mchepuko wake. Na laiti kama angekuwa muislamu ningekubali anioe niwe mke wapili, watatu hata
wannne na watano fresh tu.
Kwakuwa alinihakikishia kuwa hana mahusiano na ex wake angalau presha yangu ilipungua.
Siku iliyofuata nilirudi kazini, niliendelea kupiga kazi. Ijumaa kama kawaida yangu nilienda msikitini kisha nilirudi kazini. Na hatimaye ilifika jumapili, siku hiyo gari yangu iliharibika, niliipeleka gereji kisha mimi nilipanda boda boda kuelekea kazini.
Sasa nikiwa kwenye boda kuelekea kazini; njiani nilishtuka kumuona Genson akiwa ametanguzana na ex wake, sijui walikuwa wanaelekea wapi!! Weuwee! Pale pale nilimwambia dereva asimamishe boda kisha nilishuka, nilimlipa pesa yake kisha nilinyata nyuma nyuma niliwafuatilia nikitaka kujua wanaenda wapi.
SEHEMU YA 83
Baada ya kuwafuatilia niligundua kumbe
walikuwa wanaenda kanisani; roho iliniuma sana, nilipata wivu wa ajabu, nilijiuliza inawezekanaje mtu na ex wake wawe marafiki? Isije ikawa wanapasha kiporo halafu hata hawasemi. Nilitamani mimi ndiye ningekuwa nimeongozana na Genson kuelekea kanisani.
Pale pale niligeuka kushoto nilielekea kwenye ofisi za kanisa kwa lengo la kubadili tena dini, nilitaka kurudi kwenye dini yangu ili tu nipate nafasi ya kuwa karibu na Genson. Walinipokea vizuri sana, walinipa utaratibu kisha nilielekea kwa viongozi wangu wa kiislam ambao nao walinipa utaratibu. Nilikamilisha taratibu zote kisha rasmi nilirudi kwenye ukristu.
Moyoni niliwaza nikizubaa ex wa Genson atanizidi kete, binafsi sipendagi kugombania mwanaume lakini kwa Genson nilikuwa tayari. Alifurahi sana kuona nimerudi kwenye dini yangu, aliniambia kwamba nimefanya maamuzi sahihi ambayo yana faida mbeleni. Nilimuuliza faida gani hakunijibu, alizidi kunishangaza,
ilifikia hatua nilihisi labda jamaa ni hanisi anaogopa kuwa na mimi.
Baada ya kubadili dini nilidhani kuwa kila jumapili nitakuwa mtumwa wa kumlazimisha tuende kanisani pamoja, lakini kitu cha kushangaza ni kwamba yeye Genson ndiye alikuwa mtumwa kwangu. Kila siku alinikumbusha kusoma biblia, na kila jumapili alinipitia nyumbani ili tuende kanisani pamoja. Sasa kitendo cha mimi na Genson kuongozana pamoja kilimuumiza sana ex wake, alinivumilia mwisho aliamua kunitolea uvivu, alinifuata kazini;
“Habari yako, kama ulikuwa hunijui basi leo utanijua. Naitwa Oliver, ni mpenzi wa zamani wa Genson lakini pia niko kwenye harakati za kumrudisha awe mume wangu… Hivi wewe mdada kipi kinakuwasha hadi uingilie mapenzi ya watu?”Oliver alinikoromea kwa sauti kali, alionekana ni mgomvi mgomvi na muongeaji.
” Mpenzi gani huyo?” nilimuuliza
“Unajida hujui naongelea nini?…. Majuzi ulikuja mgahawani uliniharibia lakini nilikuacha, ukaona haitoshi ukaamua kubadili dini ili tu uwe unaenda nae kanisani. Hivi hujagundua kuwa hakutaki?”
“Bado sijagundua. Na kama anakutaka wewe, sasa tatizo lako ni lipi? Kwanini hakurudii?”
“Wewe ndiye kizuizi, unajitongozesha kwake kiasi kwamba anachelewa kunirudia. Naomba achana nae, ikiwezekana kaa nae mbali”
“Mimi huyo nikae mbali na Genson? Ila wewe unaumwa kweli”
“Anaumwa shangazi yako…” “Kwa bahati nzuri sina shangazi”
“Utajua wewe. Hunijui wala sikujui, tumekutana ukubwani tu. Hivi unajua mimi na Genson tumetoka wapi? Kwa taarifa yako yule ndiye mwanaume wangu wa kwanza, hata kama
nilimsaliti lakini nimemchagua tena ili awe mwanaume wangu wa mwisho. Mimi sikumsaliti kwa ubaya, nilimsaliti nikiwa nampenda, ni changamoto za pesa tu ndizo zilinitenganisha nae. Kwakuwa hivi sasa pesa anazo najua hatutopata shida tena kwenye mapenzi yetu na ndio maana nataka turudiane, najua bado ananipenda ndio maana hataki wanawake wengine. Nina uhakika ukiacha kumsumbua tu, atanirudia. Na wewe kwa ushauri naomba rudiana na mwanaume wako wa kwanza ambaye anakupenda, hata kama alikusaliti lakini ndo chaguo lako.. Msamehe kisha mrudie. Kama mliachana kisa pesa, nadhani kwa sasa una pesa, hivyo basi mkirudiana hamtosumbuana…. Upo bibi?”
“Nimekusikia ila sijakuelewa. Genson aliniambia kuwa mliachana na hawezi kurudiana na wewe. Pia kila siku amekuwa akiniambia kuwa yupo single. Sasa wewe una uthibitisho gani kwamba anakupenda na mpo kwenye hatua za kurudiana?”
SEHEMU YA 84
“Ooh kumbe unataka kujua kuhusu hilo?….
Muda huu Genson ameniita madukani anataka akanifanyie shopping, kama huamini naomba nifuate uje ujionee…” Baada ya maneno hayo aligeuka kisha alipiga hatua kuelekea madukani.
Niliganda nikijiuliza ni kweli au ananitania? Kama ni kweli, sasa mimi nitakuwa kwenye kundi gani?. Pia nilijiuliza niende au nisiende, kama nisipoenda nitapataje ukweli? Nilijikuta
nimesimama kisha nilifunga duka, taratibu nilimfuata Oliver ex wa Genson. Moyoni niliomba jambo hilo lisitokee kwa sababu lingeniumiza sana. Pia ningeamini kwa asilimia 100 kuwa jamaa hanipendi kabisa kabisa.
Baada ya mwendo wa dakika chache hatimaye tulifika madukani, nilimuona Oliver akielekea kwenye duka flani kisha alimkumbatia mwanaume flani. Nilichunguza kwa makini niligundua mwanaume huyo ni Genson.
Walisalimiana kidogo kisha walienda kwenye duka la pili, mara nilishangaa Oliver kabeba mfuko mkubwa wa vitu ambavyo walinunua, roho yangu ilianza kuuma, nilihisi kizunguzungu, hapo ndipo niliamini kuwa ni kweli wao wanapendana kwa dhati. Sikutaka kujionea mengi, nikiwa nalia kwa uchungu niligeuka kisha nilirudi dukani.
Nilitamani nifunge duka nirudi nyumbani lakini nilikumbuka maneno ya Genson, aliniambia hata kama hanipendi sipaswi kuacha kutafuta pesa. Nilitikisa kichwa changu kulia kushoto nilijiweka sawa, nilifuta machozi kisha nilitulia kimya, niliacha kulia, niliamua kujipa moyo, nilikasirika, niliona haina shida!! Sikutamani tena kuendelea kuteseka, niliamua kununa na kumkasirikia kila mtu. Sikuitikia salamu ya mtu yeyote, hata wateja wangu niliwahudumia kimya kimya bila kuongeleshana wala kuchekeana!!!
Licha ya kupotezea lakini Genson bado alizunguka kichwani mwangu, nilimlaani sana,
nilimshtaki kwa Mungu apewe adhabu yoyote. Haiwezekani anitese mimi mtoto wa kike, kwanza mimi ni mzuri, najitambua, nina pesa, nina akili, nina biashara, nina gari na uwanja, nina malengo makubwa, nimefanikiwa japo sio sana, sasa kwanini hanipendi? Anampendaje mwanamke mwenye tamaa ya pesa?
Anampendaje ex wake ambaye waliachana kisa usaliti? Anampendaje mwanamke ambaye nimemzidi kila kitu???… Huyo ex wake kama tako nimemzidi, shepu nimemzidi, sura yangu ni nzuri kuliko yake, tabia zangu n bora kuliko yeye, nimemzidi heshima, hekima na hata upendo nimemzidi. Mimi ndiye nilikuwa naendana na Genson kuliko yeye hasiye mvumilivu wa maisha.
Sasa nikiwa bado natafakari mara gari ya Genson ilipaki mbele ya duka langu. Vioo vilishushwa, nilitazama mbele nilimuona akitabasam baada ya kuniona. Alafu alikuwa pekeyake, Oliver sikumuona. Akiwa
anatabasam alishuka kisha alizunguka nyuma, alifungua buti la gari alitoa mfuko ule ule ambao ulibebwa na Oliver wakati wapo shopping. Nilishangaa nikiwa bado nimenuna kwa hasira, licha ya kunionyesha tabasam zuri lakini sikumchekea wala sikumfurahia; nilimvimbia tu.
“Jamani hata kunipokea” Aliniambia akiwa bado anatabasam, maneno yake mazuri yalifanya niongeze mnuno, bichwa langu lilivimba kwa hasira, niliamua kutazama pembeni.
“Mh mbona kama umenikasirikia, au hujapenda mimi kukuletea zawadi?”
“Kampe Oliver wako ambaye mlinunua pamoja” Nilimjibu kwa hasira kisha niligeukia tena pembeni, niliendelea kununa alafu ghafla machozi yalianza kunitoka.
“Eeh kumbe ndo sababu… Kwahyo unahisi mimi na Oliver tumerudiana?”
“Sasa kama hamjarudiana kwanini umfanyie
SEHEMU YA 85
shopping? Kwanini muda wote muongozane? Hata kama hunipendi, huoni kuwa mambo hayo yananiumiza?… Au mmepanga kuniua kwa presha eeh… Sawa bwana… We si unaniona mimi mjinga… Unaniona mtoto, unanidanganya upo singo kumbe umerudiana na ex wako….
Nikikuuliza unasema humpendi, hivi kweli kwa mambo aliyokufanyia anafaa hata kuwa karibu yako? Sio kwamba nataka mgombane lakini ukaribu unaompa unafanya aringe na atambe mbele yangu akidai kwamba wewe ni wake milele na hamuwezi kuachanaa”
“Ni kweli nakosea sana kumpa Airtime, sikujua kama unaumia kiasi hiki. Yeye aliniomba tuwe marafiki hata kama simpendi. Nilimkatalia lakini nimeshindwa kumkwepa kwa sababu amekuwa akiniganda sana!! Hata pale madukani sikumuita, sikujua alijuaje kama niko pale.
Alinivamia tu kisha alinisaidia kufanya shopping pasipo kujua kuwa nilikuwa nakununulia wewe. Sasa je kosa langu ni lipi?”
“Basi sawa nisamehe, mi nilijua mnapendana na msharudiana…”
“Hapana, kwahiyo vipi nikupe zawadi au huzitaki?”
“Nazitaka….. Ebu nipe nizione.. Genson, sasa kama hunipendi kwanini umeninunulia nguo za ndani? Kwanini uninunulie zawadi ambazo inabidi ninunuliwe na mpenzi wangu?” Nilishangaa sana kukuta chupi, sidiria, boksa za kike, nguo za kulalia na zinginezo.
“Nimekununulia kwa sababu unazihitaji, sitaki ujione mnyonge kwenye mapenzi eti kwakuwa upo single. Binafsi nataka uishi kama mwanamke mwenye mwanaume wake. Huna sababu ya kuhangaika kutafuta wanaume wakununulie zawadi kama hizo, mimi rafiki yako ni mwanaume tosha ambaye naweza kukufanyia hivyo. Hata kama sikupendi lakini nataka uishi kwa furaha, zawadi hizi zitakuongezea matumaini “
Nilimuuliza matumaini gani lakini hakunijibu. Maelezo yake yalimaanisha hataki kuniona natafuta wanaume wengine kwa sababu yeye yupo. Niliwaza kama ni hivyo ina maana hata yeye ananipenda, sasa kama ananipenda mbona hanitongozi? Mbona anakataa kuwa hanipendi?… Kiukweli Genson alinishangaza sana. Kuna muda alinikosesha matumaini na kuna muda alinipa matumaini kwamba ipo siku nitakuwa wake… Ubaya ni kwamba hakutaka kuweka mambo waziwazi, alikuwa anajifichaficha tu.
Siku hiyo alishinda na mimi dukani kwangu, tulipiga stori nyingi nyingi hadi usiku kisha nilifunga duka tulirudi nyumbani. Siku iliyofuata maisha yaliendelea, Oliver aliendelea kuwa karibu na Genson, pia aliendelea kunipa vitisho kwamba Genson ni wake yeye pekeyake.
Vitisho vyake vilizidi kuninyima usingizi lakini Genson alizidi kunifariji kwamba hata iweje kamwe hatoweza kurudiana na EX.
****
Siku zilikatika, miezi ilikatika nikiwa single. Tangu nipate tiba ya uzazi sikuwahi kujaribu kufanya tendo ili nijue kama nimepona au la, binafsi nilitamani nione kama naweza kupata ujauzito. Ubaya ni kwamba mwanaume niliyemtarajia anipe mimba alikuwa hanitaki. Kwa wakati huo nilikuwa nina miaka 23, licha ya umri wangu kuwa mdogo lakini nilitamani sana kuolewa. Nilipiga mahesabu nitampataje Genson? Nifanye nini ili anioe? Nilipata wazo.
INAENDELEA