MWANAUME WA NDOTO ZANGU
SEHEMU YA 71
“Mtu mwenyewe ni yule pale. Huyo aliyevimba uso, ambaye ana makovu usoni ni mkewe”
Genso aliwaambia polisi
“Kwahiyo ile video ni ya huyu mpuuzi akimpiga mkewe si ndiyo??…” Polisi mmoja aliuliza
“Yes afande”
“Ni yeye kwanza huoni hata hayo mavazi yake, ona hata sura lake limekaa kikatili. Limepata mwanamke mzuri alafu linampiga hovyo hovyo.. pumbavu kabisa, haya madudu ndiyo tunayoyahitaji pale ustawi wa jamii.. Dokta tunashukuru sana kwa kutuletea huyu katili wa jinsia. Hajui kwamba ni heri umuonee mwanaume mwenzio kuliko kumchokoza mwanamke, subiri tukamfunze adabu” Aliongea afande mwingine ambaye alivaa mavazi tofauti na wenzie
“Jamani ndugu zangu mbona siwaelewi tena kaka zangu vipenzi… Mimi mbona sijampiga
mke wangu jamani, afu nampenda mno” Mume wangu alianza kujitetea, chakula hakikupita kooni, tayari alivurugwa.
Pale pale aliwekwa chini ya ulinzi, alipigwa pingu kisha yeye, mimi, Genson na polisi tulielekea kituoni ambako tuliitazama ile video ambayo ilirekodiwa na Nasri, mume wangu alikubali makosa, pia nami nilieleza yote mabaya aliyonifanyia. Na nilieleza dhamira yangu ya kuomba talaka. Kupitia polisi mume wangu aliahidi kuwa atanipa talaka yangu ili kila mmoja ashike hamsini zake. Siku hiyo alilazwa sero!!
Siku iliyofuata mimi na Genson tuliitwa tena kituoni, tulikutana na watu wa ustawi wa jamii, kesi ilikuwa kubwa. Na kwa mujibu wa sheria mume wangu alitakiwa afungwe lakini mimi sikutaka kumfunga, niliwaeleza polisi kuwa nahitaji talaka yangu tu.
“Gensuda sio talaka tu, huyu inabidi muachane
na akulipe fidia ya kukupotezea muda, kukutapeli mali zako, kukuharibia maisha na kukutesa” Genson aliongea
“Yes ni kweli kabisa. Tena sio fidia tu bali kwa mujibu wa sheria zetu za ustawi wa jamii inabidi baadhi ya vitu ambavyo vilinunuliwa mkiwa pamoja mnatakiwa mgawane. Na kama aliuza basi naomba viorodheshwe kisha akulipe au aende jela akasote” Mtu wa ustawi wa jamii aliongea
“Aah jamani msinipeleke jela, mimi huyu ntampa talaka yake, na fidia ntampa hilo halina shida…. Hata faini nipo tayari ila jela hapana, nina familia mimi”
Genson ndiye alinisimamia kwenye ile kesi. Alihakikisha napata haki zangu zote ambazo nilihitaji kuzipata. Baada ya kuorodhesha kila kitu mume wangu aliamriwa anilipe million 40. Alitakiwa auze ile nyumba anayoishi Rahabu, gari langu na vitu vya ndani kisha pesa
tugawane. Rahabu baada ya kufikishiwa taarifa kwanza alishtuka, pili alikataa nyumba isiuzwe. Ubaya ni kwamba haikuwa nyumba yake, nyumba bado ilikuwa ina hati yenye jina langu.
Kwa usimamizi wa polisi, watu wa ustawi wa jamii pamoja na Genson nyumba na gari vyote viliuzwa kwa bei ya hasara ya million 80 kisha nilikabidhiwa pesa zangu, talaka yangu, na huo ndio ulikuwa mwisho wa mimi na Nasri ambaye hakupendezwa na maamuzi yangu, alinichukia sana. Ilibidi Rahabu ahamie nyumbani kwa Nasri. Nilitaka niondoke na mwanangu lakini Nasri alizuia. Kwakuwa alikataa nisiondoke na mwanae Masoud wala sikujali, mimi nilimchukua mama yangu, tulikusanya vilivyo vyetu kisha tulihamia nyumbani kwa Genson.
SEHEMU YA 72
Maisha mapya yalianza tukiwa tunaishi nyumbani kwa Genson. Binafsi sikuwa na shaka
yoyote juu ya Genson, ila tu niliogopa yasije yakatokea kama yale yaliyonikuta kwa Nasri ambaye mwanzoni alianza kutupenda lakini baadae alitugeuka. Sio mimi tu, hata mama yangu alijawa na hofu, hakupenda kabisa kuishi tena kwenye nyumba ya mtu, hakutamani tena kupokea misaada, aliogopa sana.
“Najua mnaniwazia mambo mengi, mnahisi naweza nikawa kama Nasri. Ni haki yenu kuogopa kwa sababu tayari mshang’atwa na nyoka. Mimi binafsi sitaki niwasaidie, nataka muishi maisha yenu. Nilipambana mpate haki yenu ili mjenge maisha yenu kwa kupitia pesa zenu. Hizo million 40 ambazo mko nazo sio pesa nyingi, labda kwa matumizi ya kawaida zinaweza zikawa nyingi lakini kwa kujenga maisha yenu hizo ni pesa chache sana. Hivyo basi nataka niwaombe jambo flani, naomba katika hizo pesa asilimia 90 muitumie kujenga nyumba yenu. Na asilimia 10 muitumie katika matumizi mengine, vipi mko tayari?”
“Ndiyo tuko tayari”
Kwa maisha ya Tanga inawezekana kabisa mtu kujenga kwa milion 30 au 35. Genson alitutafutia uwanja kisha tulianza ujenzi.
Nilitamani yeye ndiye ashike pesa zote kisha asimamie ujenzi lakini alikataa. Mambo mengine yote alifanya yeye, mfano kutafuta mafundi, kununua tofali na mengineyo, lakini mimi ndiye nilikuwa natoa pesa. Alifanya hivyo ili kunihakikishia usalama wa pesa zangu, kiukweli nilimuamini sana.
Huwezi amini nyumba ilijengwa kwa mwezi mmoja tu kisha ukarabati ulianza. ilikuwa ni nyumba ya vyumba vitatu tu pamoja na choo na bafu za ndani kwa ndani. Japo ilikuwa ni nyumba ndogo lakini ilipendeza sana, pia tulinunua baadhi ya vitu vya ndani mfano magodoro mawili na vitanda viwlili kwaajili yangu mimi na mama. Flatscreen, king’amuzi, friji, meza, masofa na kabati. Tuliweka umeme kisha tulihamia rasmi, shukrani pekee
nilizipeleka kwa Genson ambaye ndiye alikamilisha mchakato mzima. Hata mama yangu alimshukuru sana Genson na alimpenda sana, na tangia siku hiyo alikuwa akimuita mkwe.
Pesa nyingi tulizitumia kwenye ujenzi, mkononi nilibakiwa na million nne na ushee!! Nasri aliniambia nichukue million 3.5 nianzishe huduma ya kuweka na kutoa fedha; nadhani wote mnaijua. Alinishauri nifanye biashara hiyo kwa sababu ni rahisi kuiendesha, ina wateja wengi, na ni raisi kutengeneza kipato kikubwa zaidi.
“Unajua nini Gensu, katika haya maisha sio kwamba watu hawapati pesa, sio kwamba watu hawana pesa, ila asilimia kubwa ya watu wengi wanapata pesa lakini hawana biashara ambazo zitalinda pesa zao na zitaendelea kuzalisha pesa zaidi. Hawa matajiri unaowaona sio kwamba utajiri wao upo mkononi, usidhani mtu kama Bhakresa, Gsm au Mo wana pesa nyingi
mikononi; hapana, bali wao wana pesa nyingi zilizowekezwa kwenye biashara zao. Utajiri haupimwi kwa cash, unapimwa kwa cheque. Pesa za mkononi ni pesa za matumizi, lakini pesa za benki ni pesa za maendeleo. Ukisema ukae na hiyo million 4 mkononi, mwisho wa siku utaishiwa na hutopata zingine. Lakini ukiziwekeza kwenye Biashara, kila siku zitakupa faida (kipato) lakini biashara itaendelea kuishi miaka hadi miaka… Japo biashara ni ngumu sana lakini ukiwa na biashara utapata matumaini ya kuishi maisha mazuri”
“Asante Genson, yani wewe mwanaume sijui nitakulipa nini”
“Usijali, nitalipwa na Mungu”
Licha ya kunishauri lakini yeye ndiye alinitafutia frame, aliniongoza katika kutafuta laini za mitandao ya simu, alinitafutia mtu ambaye alinipa elimu ya biashara hiyo. Na baada ya kuiva kibiashara rasmi niliingia kazini, nilianza
kutoa huduma. Mwanzo nilipata wateja wachache, taratibu walinizoea na mwisho walijaa dukani kwangu. Mama yangu hakupata shida tena, japo alikaa nyumbani bila kazi lakini alikuwa ana uhakika wa kula kupitia mimi mwanae. Tena ilifikia hatua hata yeye alikuwa anacheza michezo yake kupitia pesa ambazo nilikuwa nampa. Licha ya kwamba hatukuwa matajiri lakini tuliishi maisha mazuri tu, kiukweli Mungu apewe sifa.
Familia ya Genson walikuwa ni kama marafiki zetu na majirani zetu japo nyumba zetu zilikuwa mitaa tofauti. Ni mara nyingi tu walitutembelea nyumbani, nasi tuliwatembelea kwao. Dada yake ilifikia hatua alikuwa anashinda nyumbani, anapika, analala bila shida yoyote. Hata Genson mwenyewe ni mara nyingi tu alikuwa anatutembelea, anatuletea mboga, pia alinitembelea dukani kwangu, alinisisitiza niendelee kupambana zaidi.
****
Mwanamke matunzo bwanaa! Genson licha ya kwamba alikuwa rafiki yangu lakini alihakikisha nakuwa msafi wa mwili na roho. Jamaa hakusita kunipeleka shopping, kuninunulia nguo, kunipeleka saloon na kadhalika. Muda mwingine nilifanya hayo yote kwa pesa zangu, nilihakikisha nakuwa mrembo mrembo kweli.
Yale makovu yote yalikwisha, mtoto wa kike niliogea losheni, nilipaka loshen, nilijipulizia loshen, utaniambia nini.
Wanaume nao hawakuwa nyuma kwenye kunitongoza. Na sikutongozwa na watoto wanuka jasho, hao waliniogopa sana, waliniona sio levo yao. Wengi waliniheshimu kutokana na biashara ambayo nilikuwa nayo, pia mavazi ambayo nilikuwa navaa. Mara nyingi nilivaa hijab, nikabu, baibui, magauni marefu na kichwani nywele nilizificha kwa mtandio. Niliapa kwamba mtu pekee ambaye atakuja kuziona nywele na mwili wangu ni mwanaume wangu
wa pili ambaye atakuwa tayari kunioa.
Sio watoto wadogo tu, hata baadhi ya wanaume wa kipato cha chini waliogopa kunitongoza.
Nilitongozwa na wanaume wengi ila wengi wao walikuwa ni wenye familia zao, wenye ajira zao, wafanyakazi na wafanyabiashara wenzangu ambao wengi niliwakataa.
Nakumbuka siku hiyo nilitembelewa na kiongozi mkubwa tu kwenye nchi yetu akiwa ameongozana na machawa mbalimbali pamoja na walinzi, kiongozi huyo ni mwanasiasa.
Machawa na walinzi walibaki nje alafu yeye alikuja ndani kwenye duka langu kutoa fedha. Akiwa anatoa pesa muda wote alionekana kunitazama sana kiasi kwamba nilijisikia aibu. Alitoa million 1, kwenye ile milion aliniambia nichukue laki 3 lakini nilikataa.
“Binti unakataa pesa? Karne hii mwanamke unapewa pesa unakataa?”
“Nadhani ni kwa sababu sina kazi nazo, sio
kwamba nazikataa ila unaweza kunipa alafu nami nikaenda kuwapa watu wenye mahitaji maalumu”
“Eeh hadi ukawape watu hao kwani wewe huna mahitaji maalumu?”
“Sizihitaji”
“Aaah usiseme hivyo basi, hiki kibiashara kisikupe kiburi. Kumbuka kwamba mimi nina uwezo wa kukupatia cheo chochote hapa Tanga, nakupa ubalozi wowote, nakuongezea duka lingine, na nina uwezo wa kukupa kibali cha kufanya biashara yoyote… Sawa mrembo?”
“Sawa nimekuelewa”
“Hayo ndo mambo sasa…. Haya zishike pesa zako….. Sasa unajua nini, mimi leo nitalala hapa kabla sijaelekea Dodoma. Licha ya umri wangu kuwa mkubwa lakini bado sijaoa, hivyo basi leo hii sitoweza kulala pekeyangu hotelini; nahitaji mwanamke mzuri, mwenye heshma na akili. Na kwa hapa Tanga nimezunguka kote sijaona
mwanamke mzuri kukuzidi wewe. Hivyo basi nimekuchagua wewe ulale na mimi leo hii, hutolala bure. Utalala maskini na kesho utaamka tajiri… Mimi kwa sasa nipo kwenye mizunguko yangu ya kisiasa na kiserikali, ikifika saa moja nitakuwa Tanga hotel. Hivyo basi nakusihi kabla ya saa 3 usiku uwe umeshafika pale hotelini… Nadhani tumeelewana si ndio?”
SEHEMU YA 73
“Hapana sijakuelewa, na hata nikikuelewa siwezi kufanya hivyo. Kwanza chukua pesa zako, siwezi kukufuata kokote.”
“Unashindana na serikali?” ” kwani ni lazma au?
“Ndiyo ni lazma na ni amri, Kabla ya saa tatu uwe ushafika. Sasa ole wako usifike, ndo utajua kwanini mimi ni kiongozi wa UMMA”
Alichukua pesa zake kisha aliondoka kwa
hasira pamoja na watu wake. Baada ya wao kuondoka nilitulia nikitafakari wito wake na vitisho vyake, nilipata hofu kubwa, sikujua itakuwaje endapo sitokwenda. Siku zote nilizoea kufanya kazi kwa uchagamfu lakini siku hiyo sikufanya kazi kwa amani kutokana na maneno ya yule mwanasiasa. Nilitamani masaa yasimame ili usiku usifike lakini haikuwa hivyo, masaa yalikatika na hatimaye jua lilizama.
Nilifunga duka nilirudi nyumbani, moja kwa moja nilifikia kitandani niliugulia maumivu ya kichwa.
Ilipita saa moja usiku, ikaja saa mbili usiku, na hatimaye dakika zilikatika kuelekea saa tatu; jasho lilinitoka kwa wingi, nilishindwa kukaa chini! Muda wote nilijizungusha ndani ya chumba changu. Niliwaza niende kutumika au nisiende?… Baada ya kutafakari sana hatimaye nilipata majibu. Kwanza nilituliza wenge, nilielekea bafuni nilioga kisha nilikula chakula kutuliza njaa. Nilitazama saa zilibaki dakika 10
kutimia saa 3, nilitabasam kisha nilielekea kitandani nilivuta shuka nilijifunika kisha nililala.
*****
Siku iliyofuata asubuhi nilielekea kazini; nilishtuka kukuta polisi wakiwa wamelizunguka duka langu, yaani ile wameniona tu waliniweka chini ya ulinzi, walinipakia kwenye gari yao kisha walinipeleka kituoni kwao.
Nikiwa kituoni nilihoji kwanini wamenikamata? Waliniambia ni kwa sababu naendesha biashara kiujanja ujanja, sina leseni, silipi kodi, nahujumu uchumi. Nilishangaa sana kwa sababu mimi ni mlipa kodi mzuri, sasa kwanini wanikamate? niliwaomba wanipe nafasi nikachukue leseni yangu na nyaraka za kulipa kodi lakini hawakunisikiliza, walinipotezea.
Mara alikuja yule mwanasiasa ambaye aliniamrisha niende kulala nae hotelini. Alinitazama kisha alicheka. Hadi kufikia hapo
nilijua kwanini nimekamatwa, kumbe tatizo sio biashara yangu bali kukataa wito wa kiongozi wa serikali. Nilitulia nilisubiri hukumu yangu, wao walisimama pembeni kisha walianza kujadiliana. Baada ya majadiliano walinipeleka kwenye chumba cha pekeyangu, kisha yule kiongozi alinifuata, tulikuwa wawili tu.
“Najua huna kosa lolote la kibiashara, kodi unalipa na leseni unayo. Ila kosa lako ni kutotii amri yangu, yani jana ulifanya nilale kwa mawazo sana, nilijiona sina mamlaka ya kusikilizwa… Wewe binti mdogo ni wa kukataa wito wangu?”
“Nisamehe” Nilijibu kwa upole “Nikikusamehe utanipa nachotaka au?” “Hapana”
“Sasa nikusamehe kwa lipi? Hivi unadhani nashindwa kutumia nguvu nikatimiza lengo langu? Naweza sana ila nataka angalau unikubalie tufanye kwa amani… Na kama hutaki
hii kesi itaendelea, utapelekwa mahakamani utahukumiwa”
“Kama ntahukumiwa sawa tu, lakini mimi sitoweza kulala na mwanaume mwingine zaidi ya mume wangu. Na hata jana baada ya kurudi nyumbani mume wangu ndiye alinitumia kitandani”
“Kwani we umeolewa?” “Ndiyo”
“Mbona taarifa zako ninazo kuwa uliachika muda mrefu, kwa sasa upo single tu Una
uhakika umeolewa wewe au unanidanganya?…
Binti sitaki hii kesi iwe kubwa, usinione mimi mtoto… Wewe umeolewa kweli?”
“Ndi-ndiyo” Nilitaka kubabaika, nilijibu nikiwa naogopa
“Haya mpigie mumeo aje hapa. Na aje na vyeti vya ndoa… Sasa ole wako hasije, utantambua.”
Kuhusu kumpigia mwanaume aigize kuwa
mume wangu, hilo sikulihofia sana. Ila utata ulikuwa hapo kwenye cheti cha ndoa, sikujua itakuwaje. Taratibu nilishika simu yangu kisha nilianza kutafuta namba ya mwanaume anayefaa kuigiza kama mume wangu. Simu yangu ilikuwa ina namba nyingi za wanaume tofauti tofauti wenye pesa na wasio na pesa, waliojiajiri na wasio na kazi. Macho yangu yalikwama kwenye namba moja tu ambayo ni namba ya Genson. Nilimpigia kisha nilimuambia kuwa nimekamatwa na polisi hivyo basi anifuate haraka, nilimtajia kituo kicha nilikata simu.
Baada ya dakika chache Genson alikuja akiwa amenyonga suti na tai, yaani ile kumuona tu nilipata tabasam na afuheni; nilitamani nimrukie nimkumbatie lakini niliogopa. Muda huo yule kiongozi aliondoka, sikujua yupo wapi. Genson aliniuliza kulikoni? Sikujua nimjibu nini, moyoni nilikuwa natafakari namna ya kumpanga aigize kama mume wangu. Lakini kabla sijamuambia
SEHEMU YA 74
chochote yule mwanasiasa alizama ndani! Alishtuka kumuona Genson akiwa amesimama na mimi.
“Eeh Dokta kumbe upo hapa, habari yako bwana!” Mwanasiasa alimsalimia Genson, kumbe wanafahamiana.
“Salama mkuu, nami nimeshangaa kidogo kukuona hapa… Nilijua utakuwa kwenye harakati za mkutano wako wa leo” Genson aliongea
“Yeah yeah ndo nimekuja hapa kuomba askari ambao watanisaidia kutuliza vurugu muda wa mkutano… Naona unaongea na binti, vipi tena?”
“Nilikuwa kazini ila aliniita hapa akidai kwamba amekamatwa na polisi”
“Kwani unataka kusema wewe ndiye mume wake?.. Mana aliambiwa amuite mumewe.”
“Eeh-yes-ndio, mimi ni mumewe! Kwani kuna tatizo lolote? Au kuna kosa ambalo amelifanya
tulimalize?”
“Hapana… Hapana…. Ni mazungumzo ya kibiashara tu. Kwa sasa tuna mpango wa kusajili vitambulisho vya wajasiriamali wadogo, na ili usajiliwe unatakiwa uwe kwenye ndoa.
Ndio maana tulitaka tuthibitishe kama nae ameolewa ili tumsajili…. Kama ni hivyo binti unaweza kuondoka… Mimi ngoja niongee na daktari mambo mawili matatu…. Eeh ndugu yangu habari za hapa Tanga…”
Ilibidi niondoke zangu, niliwaacha wao wakiongea mambo yao. Njiani nilitembea nikiwa nachekacheka tu, hata sikujua nacheka nini. Ila vionggozi wengine hawajitambui kwakweli, alidhani angenipata kirahisi kisa tu ana cheo kikubwa; kwangu amebugi. Nilifika dukani nilifungua duka kisha nilitulia niliwaza kilichotokea, nilikumbuka namna Genson alivyokubali kuwa mimi ni mkewe, nilibaki natabasam tu. Nilihisi raha kiasi kwamba nilijilamba midomo yangu kisha nilimeza mate
matamu.
Hisia zangu zilifika mbali kweli kweli, ilifikia hatua nilipitiwa na mawazo, nilimuwaza Genson tu, tayari nilikolea kwake. Nilijua akitoka kituo cha polisi angenifuata ofisini lakini masaa yalipita hakunifuata. Hata yule mwanasiasa sikumuona tena, licha ya kwamba nilikuwa huru kiraia lakini sikuwa huru moyoni; moyo wangu ulianza kuteseka ghafla, nilitamani kuwa na mpenzi, nilitamani kuolewa, pia ni muda mrefu sikufanya lile tendo lenye raha! Nilitamani nilifanye lakini nifanye na mwanaume mmoja tu nimpendae, na mwanaume huyo sio mwingine bali ni Genson.
Kiukweli kwa mambo yote yalitokea tangu nikutane na Genson, niliamini hata yeye ananipenda. Hasingeweza kunifanyia mambo yote yale kama hanipendi. Ubaya ni kwamba siku zilikuwa zinapita wanaume wengine walinitongoza kila siku lakini yeye hata kunibusu hajawai, hakuonyesha dalili zozote za
SEHEMU YA 75
kutaka kunitongoza, jambo hilo lilianza kuniuma.
Jioni baada ya mahesabu nilifunga duka nilirudi nyumbani. Nilipika nikiwa namuwaza Genson, nilioga nikiwa namuwaza, nilikula nikiwa namuwaza, hata muda wa kulala nilimfikiria yeye tu. Nilitamani anitumie meseji ya usiku mwema lakini hakunitumia, niliamua kumtumia yeye lakini hakunijibu. Nilijipa matumaini kwamba atakuwa yupo bize na kazi, niliamua kulala.
Siku iliyofuata niliona haiwezekani niteseke kwa mtu anayeonyesha kunipenda. Niliwaza nifanye jambo! Kwanza nimuonyeshe hisia zangu waziwazi, kama kujitongozesha nijitongozeshe, nitege mitego yote hadi anase. Nilitabasam nikiamini nitafanikiwa tu. Siku hiyo sikwenda dukani, niliamua kutengeneza homa ya uongo.
Nilimwambia mama ampigie Genson amwambie kuwa naumwa. Baada ya maelekezo nilienda kukaa chumbani kwangu, niliamini Genson akiambiwa kuhusu homa yangu atakuja
tu, na akija atanikuta chumbani nikiwa nimevaa kihasara hasara.
Mama mzazi wala hakuchelewa, alimtwangia simu jamaa alimpa taarifa. Na kwakuwa Genson ananijali sana wala hakuchelewa, dakika 5 mbele aliwasili nyumbani akiwa amebeba zawadi kama zote. Maua, midori, matunda, keki, hivyo vyote ni kwaajili ya kunifariji. Baada ya kufika ndani alikaa sebuleni, alimwambia mama aje kuniita niende sebuleni ili anione, anisalimie, anipe pole na zawadi kisha aondoke. Mama alikuja kuniita, niliwaza nikisema nimfuate sebuleni mpango wangu utaharibika. Nilimwambia Mama kuwa miguu inaniuma sana, nilimtaka akamwambie Genson anifuate chumbani.
Unadhani mama angu alivunga? Wala hakunibishia, alienda kusema kama nilivyomwambia. Genson alinifuata chumbani, kwanza alishtuka kunikuta nimevaa kigauni kifupi cha kulalia. Upaja mweupee ulinona
mubashara, mguu nao ulimeremeta, hips hazikuwa mbali; nazo ziligawanyika kisha zilijimwaga, tumbo langu halinaga kitambi, kifua nacho kilisimama kama kimebustiwa vile! Na uzuri ni kwamba licha ya kunyonyesha lakini sinaga mtindi mkubwa, nina maputo madogodogo tu. Binafsi kutoka moyoni nilijua jamaa atadata. Na akidata atanitamani.
Akinitamani anaweza akanitongoza, akanishika kidogo au akanimalizia kabisa. Nilikuwa tayari kwa jambo lolote lile ambalo lingetokea.
INAENDELEA