MWANAUME WA NDOTO ZANGU
SEHEMU YA 56
“Ooh jamani mmekuja kunisalimia, karibuni sana…. Mama shikamoo…” Rahabu alimsalimia mama
“Marahaba!…. Lakini naomba kuuliza” “Uliza tu mama angu”
“Wewe ni Rahabu au nakufananisha?” “Ni mimi mama kwani kuna tatizo?” “Wala!! Na hii nyumba ni yako au?”
“Ndiyo, ni yangu. Nilinunua wiki zilizopita baada ya kusikia tangazo la mnada kuwa inauzwa… “
Baada ya jibu hilo mama alikosa swali la nyongeza. Rahabu alitusisitiza tuingie ndani angalau tupate chakula au maji ya kunywa lakini tulikataa, tuliaga kisha tulirudi nyumbani. Siku hiyo kila dakika tulimzungumzia Rahabu tu, bado hatukuamini kama yeye ndiye mmiliki wa nyumba yetu.
Pia kuna kitu ambacho kilinishangaza zaidi. Nilijiuliza kwanini kila kitu tulichokipoteza kilinunuliwa na Rahabu? Kwanini mali zetu zote ambazo tuliuza mwisho wa siku zilimilikiwa na Rahabu?.. Gari yangu kanunua yeye, frame yangu ya biashara kaichukua yeye, na nyumba yetu kaichukua yeye!!! Hivi huwa anajuaje kama tumeuza vitu vyetu? Alafu ina maana ni yeye tu
ndiye alikuwa ana pesa za kununua kila kitu tulichokiuza? Hizo pesa zote alizipata wapii? Na huwa anajisikiaje kununua mali zetu sisi ambao tuliishi nae kwa miaka mingi?… Nilijiuliza maswali mengi lakini sikupata majibu, niliumwa kichwa tu.
Usiku niliamua kumueleza mume wangu kila kitu. Nilimueleza namna Rahabu alivyomiliki duka langu, kuhusu kununua gari na nyumba, nilidhani nae atashangaa lakini alicheka tu alisema hayo ndo maisha. Aliniambia kuwa kwa sasa hatupaswi kushindana na Rahabu kwa sababu ana mapesa mengi. Mume wangu alianza kumsifia Rahabu, mara alisema kawa mzuri zaidi, mara anavutia, mara amekuwa mwanamke na nusu, mara hivi mara vile, ilifikia hatua nilinuna! Nilipata wivu, niliamua kulala kuepusha shari.
****
Licha ya yote yaliyotokea lakini maisha yaliendelea. Siku hiyo usiku tukiwa chumbani kwa mara nyingine tena mume wangu aliniambia kuwa anahitaji mtoto wa pili.
Kwakuwa mimi ni mkewe, nilikubaliana nae. Tulianza harakati za kutafuta mtoto. Mwezi wa kwanza ulikatika, mimba haikupatikana. Mwezi wa pili, wa tatu, wa nne, tulimsaka kwa nguvu zote lakini wapi. Hapo sasa kununiana kulianza, kila siku nilisemwa vibaya, nyumba ilianza kuwa chungu.
Ilibidi tuingie hospitali kujua tatizo liko wapi. Mume wangu aliambiwa yuko vizuri tu, ila balaa lilikuwa kwangu. Kwanza niliambiwa nina uvimbe kwenye kizazi, pili niliambiwa mirija imeziba, tatu niliambiwa homoni hazijakaa sawa zinasababisha mayai yasirutubishwe na kupevuka, na mwisho niliambiwa nina changamoto ya hedhi. Nilivurugwa, nilichoka, nilichanganyikiwa kabisa. Mume wangu hata
kunitazama hakunitazama, aliniona kama kopo tu!!
Tuliorodheshewa dawa ambazo gharama zake zilikuwa kubwa, mume wangu alilipa kisha tulirudi nyumbani. Nilitumia dawa kwa mwezi mzima lakini sikupona, mimba sikushika, na ndo kwanza matatizo yaliongezeka, eti niliambiwa nina P.I.D. Mume wangu alinipeleka kwenye hospitali ya pili, sikupona. Hospital ya tatu, sikupona. Hospital ya nne, sikupona.
Tulimaliza hospital za Tanga, tulielekea muhimbili Dar ambako nilipona P.I.D na UVIMBE lakini mimba sikupata. Tulirudi nyumbani tukiwa tumenuniana, mume wangu alinikatia tamaa.
“Nimemaliza mishahara yangu, umefanya nikope tena, yani hapa nadaiwa kwa sababu ya hayo maugonjwa yako. Mwanamke gani unaumwa kila ugonjwa, kama huna kizazi si uniambie tu. Na usikute hata mwanangu Masoud hukumzaa wewe, ulimuiba hospitali”
“Mume wangu usiseme hivyo unamkufuru Mungu. Kumbuka haya yote yamekuja mara baada ya mimba yangu kuharibika, na wewe ndiye ulikuwa chanzo cha mimba kuharibika”
“Kwani nani alikutuma uje unifumanie? Niliyataka mimi au uliyataka mwenyewe? We mwanamke ni chizi eti? Yaani mimi kulala na mwanamke mwenzio eti unaona wivu, kwahiyo ulitaka nilale na mwanaume mwenzangu si ndio?”
“Basi mume wangu nisamehe”
“Hata nikikusamehe mtoto wa pili nitapata wapi? Mi nataka mtoto… Humu ndani nawalisha mnanenepeana tu kama manguruwe, mpompo tu hamna kazi ya kufanya… Wanawake
wenzenu wanatafuta pesa huko lakini wewe unakalisha tu makalio yako, kuzaa huzai, umenimalizia pesa zangu umefanya niwe maskini, nimesema NATAKA MTOTOOOOO MWINGINEEE!!!”
SEHEMU YA 57
Mume wangu alifoka mbele ya mama, nilijisikia vibaya, niliumia kiasi kwamba tumbo la uzazi lilinicheza. Yaani nilitamani hata nipate kichefuchefu nikapime niambiwe nina mimba lakini ilishindikana. Machozi yalinitoka, sikutegemea kama ndoa ni ngumu namna hiyo. Sio mimi pekee, hata mama yangu alijiziba kanga usoni kisha aliporomosha machozi!
Tulilia kwa uchungu, tulitia huruma lakini mume wangu hakutuonea huruma hata kidogo, alizidi kutunyanyapaa kisa tu alitusaidia alitutoa kijijini.
“Yani ningejua nisingekubali kuwaisaidia kule mashambani, bora hata ningewaacha mliwe na simba kuliko mateso mnayonipa. Kweli mimi ni wa kukosa pesa kwa sababu yenu? Mmenifirisi kiasi kwamba nashindwa kula nyama? Mbaya zaidi nimeoa mwanamke hasiye na kizazi, aisee! nataka mtoto… We mwanamke unanisikia au hadi nikuwashe vibao?” aliongea akiwa ananisogelea, alinitisha akitaka kunitwanga kofi lakini kabla hajanipiga tulishtushwa na sauti kali.
“Bwana usimpigeee…. Jamani kwani kuna nini? Kweli unataka kumpiga mkeo kisa pesa?” ilikuwa ni sauti ya Rahabu, mkononi alibeba mtoto mchanga, alionekana ametoka kujifungua hivi karibuni. Sote tuliganda tukimtazama.
“Sio pesa tu, hana kizazi. Hana uwezo wa kunizalia mtoto wa pili”
“Uuh jamani kwani unataka mtoto?” “Ndiyo nataka”
“Basi kama ni hivyo nimekuletea mtoto wako. Huyu niliyemshika ni mwanao ambaye nimekuzalia mara baada ya kupata mimba yako kipindi kile naishi hapa kwako. Asante sana kwa kunifanya niitwe mama, pia nashukuru nimekuzalia wewe ambaye unahitaji sana mtoto kwa kipindi hiki ambacho mkeo hazai… Ebu mtazame mwanao jinsi mlivyo fanana, mshike kidogo basi jamani….” Rahabu alideka kwa mume wangu, alimkabidhi mtoto.
Mume wangu akiwa anachekelea alimpokea mtoto kisha alimtazama, walifanana kila kitu kuanzia masikio, kichwa, pua na mashavu.
Kilichomfurahisha zaidi ni kupata mtoto mwingine wa kiume, pale pale alimpatia jina Mohamed. Alafu kwa mbwembwe alianza kuzunguka nae ndani ya nyumba akiwa anamuimbia nyimbo, mara alimkumbatia Rahabu alimshukuru, mara alimbusu mtoto, mara sijui alifanyaje!!
Nilihisi kuzimia. Kwanza nilipata wivu wa kuua mtu, pili roho iliniuma, tatu nilitamani kulia kwa sauti, na nne nilitamani nijinyonge au dunia ichimbuke inifukie. Sio hivyo tu bali nilihisi aibu na kudhalilika!! Mama yangu alishindwa hata kutazama, aliinama chini akiendelea kulia.
“Basi jamani usifurahi sana, ila sasa huyo mtoto huwezi kumpata hivi hivi” Rahabu aliongea
“We nipe masharti yoyote nitatimiza… Nipo tayari”
“Sitaki mwanangu alelewe na baba tofauti, pia nami sitaki kuzalishwa na wanaume tofauti.
Siku hizi kuolewa kumekuwa ni majaaliwa, na kwa kawaida mwanaume anayekuzalisha ndiye anapaswa akuoe huyo huyo hata kama hampendani. Hivyo basi naomba unioe ili nami niwe mke wa ndoa hata kama nitakuwa mke mdogo, pia nataka tulee mtoto ndani ya ndoa”.
“Ah ah ah kumbe ni hilo tu… Hilo mbona ndogo, kwanza mi nakupenda kwa sababu nawe unanipenda. Pili nakushukuru kwa kunizalia dume la mbegu, hivyo basi nakutamkia mbele ya mke mkubwa na mama mkwe kwamba mwezi ujao nitakuoa”
“Ongea na mkeo na mama mkwe wako kama wapo tayari kunipokea kwa sababu nataka niishi nao vizuri… Waulize kama wapo tayari”
“Ma mkwe sina shida nae, kakubali… Labda ngoja nimuulize mke wangu, eti mama Masoud upo tayari kumpokea mke mwenzio?”
SEHEMU YA 58
“Sitaki, sipo tayari, alafu Rahabu nakuheshimu sana naomba ondoka nyumbani kwangu”
“Eeh jamani yamekuwa hayo… Kumbuka kuwa sote tumemzalia mwanaume mmoja”
“We kama umemzalia sawa tunashukuru, muache mtoto tutamlea au kama hutaki ondoka nae”
“Mh tusifikie huko mke mwenzangu, alafu mimi sitoishi na wewe humu ndani. Nitaishi kwenye nyumba yangu, nawe utakuwa hapa. Pia sitokukera, sitokusumbua, sitokubughuzi, nitakuheshimu sana, nitakupenda na nitakusaidia kwa mambo mengi. Unajua nini dada Gensu, kubali tu niwe mke mwenzio ili tusaidiane kulea familia zetu, pia tumlee huyu mume wetu ambaye ameanza kukonda kutokana na mawazo. Kwanza mnaonekana mnaishi maisha magumu, ona hata wewe
mwenyewe jinsi ulivyonyauka, mama mkwe amesinyaa, kutwa mnasumbuana kisa pesa….
Tena nimekumbuka, ngoja niwape hii million 5 ya matumizi… Baba Masoud shika hii pesa utaitumia kulea familia” Rahabu alifungua pochi alitoa mahela alimpa mume wangu.
“Yani we mtoto lazma nikuoe, sikutegemea kama kuna siku nami nitalelewa. Sasa ni hivi, kwenye uislamu imeandikwa kwamba wanaume tunaruhusiwa kuoa mke mmoja, wawili, watatu hadi wa nne kulingana na uwezo wako. Mimi nina uwezo wa kuoa wake wawili, mmoja nishamuoa, umebaki wewe Rahabu….
Mama Masoud taka husitake, mwezi ujao namuoa Rahabu.
” Tutaona kama utamuoa, tutaona, patachimbika hapa… Hadi umuoe kwani mi sikutoshi?”
“Tatizo huna pesa, huna kizazi, unanitosha kwa lipi sasa?… Mwezi ujao naoa! Imeisha hiyo”
Kikao cha dharula kiliishia hapo, Mume wangu na Rahabu walitoka nje walizama kwenye gari ya Rahabu kisha waliondoka. Mimi na mama tulibaki tunalia, hata mwanangu Masoud alikuja kutusaidia kulia. Ilikuwa ni kilio tu nyumba nzima!.
******
Maisha yaliendelea kama kawaida, tangu Rahabu atoe zile pesa mume wangu kila siku alituachia pesa nyingi za matumizi. Ule utaratibu wa kila mtu kula sahani yake ulirudi upya. Tulianza kuishi kitajiri kupitia Rahabu ambaye alitukuzwa sana na mume wangu.
Siku zilipita sikusikia tena habari za ndoa. Nilidhani mume wangu ameahirisha kumuoa Rahabu lakini kumbe walikuwa wana jambo lao. Baada ya mwezi kupita mume wangu alituaga kwamba anaelekea Mwanza kwaajili ya semina. Tulimuamini tukidhani ni kweli, kumbe yeye na
Rahabu walielekea nyumbani kwa Rahabu (kijijini) kukamilisha ndoa yao.
Wiki moja ilipita mtu hakurudi nyumbani, mara ghafla marafiki zangu walianza kunitumia picha za harusi ya mume wangu na Rahabu.
Walinitumia picha za ndoa na ukumbini, watu walijaa kila kona. Nilibaki nalia tu, sikuwa na la kufanya. Mama yangu ndiye alikuwa faraja yangu.
Baada ya ndoa walirudi mjini kama mume na mke. Alafu hakunificha wala nini, aliniambia ukweli kwamba alienda kijijini kumuoa Rahabu. Pia aliniambia nimtambue Rahabu kama mke mwenzie. Alinionya nisije nikamletea vurugu Rahabu, alinitisha nikileta fujo atanipa talaka ataniacha.
Kwa hatua niliyofikia sio kwamba niliogopa kuachwa, sio kwamba niliogopa talaka, ila niliwaza kama nikiachika nani mwingine atanioa? Mwanaume gani atakubali kubeba msalaba wa
mimi ambaye nishafubazwa na mwanaume mwingine, nimezalishwa, nimetumika, nimepunguzwa thamani!! Nitaolewa na nani tena?… Bora hata ningekuwa na pesa ningedanganya wanaume wasio na pesa ili wanioe, lakini pesa hakuna, nani atakubali anilee mimi na mama yangu?…. Mawazo hayo yalifanya niogope kupewa talaka, licha ya kuolewa mke wa pili lakini niliamua kutulia, nilikubaliana na kila kitu.
Ilikuwa ni mwendo wa zamu tu. Leo alilala kwangu, kesho alilala kwa Rahabu. Licha ya kwamba mimi nilikuwa mke mkubwa lakini Rahabu alitutawala kutokana na pesa zake. Licha ya kwamba kila mtu alikuwa anaishi kwenye nyumba yake lakini Rahabu alikuwa kama boss wetu wa ndoa nzima. Yeye ndiye alikuwa anatupatia pesa za matumizi. Kila siku asubuhi alifika nyumbai kwangu, alituwekea pesa mezani kisha alimchukua mume wetu aliondoka nae.
Utawala wake ulizidi kiasi kwamba hata usiku alikuja nyumbani kwangu, alisubiri nipike kisha nae alikula kisha aliondoka. Siku hiyo jumapili alikuja nyumbani kuanzia asubuhi, alikunywa chai, alikula chakula cha mchana, cha usiku alafu hakuondoka.
Mimi nilamua kwenda kulala, yeye na mume wetu walibaki sebuleni wakitazama movie.
Nilidhani kwamba wakimaliza movie wataondoka wataenda kwao lakini haikuwa hivyo, nikiwa nimelala nilishangaa kuwaona wakiingia ndani chumbani kwangu. Eti walitaka sote tulale pamoja!!
“Jamani mimi ni mke wa pili, mimi ni mke wa ndoa. Da Gensu usinishangae sana, ni hivi; leo nimechelewa kurudi nyumbani kwahiyo nitalala hapa hapa. Mimi na wewe tutalala na mme wetu, kama raha tutampa pamoja, hakuna tusichokijua kutoka kwake, sisi wote
SEHEMU YA 59
ameshatuvua nguo nae tushamvua nguo!! Hivyo basi hakuna haja ya kujadiliana sana, mimi hapa ni kwangu na leo nalala hapa hapa….” Aliongea kama utani vile lakini hakutania.
Yeye na baba Masoud walivua nguo zao, tena wasivyo na aibu walivua nguo zote kisha walipanda kitandani. Baba Masoud alilala katikati, Rahabu alilala kulia ukutani, mimi nililala kushoto. Licha ya kwamba nilibadili dini lakini nilijikuta nimepiga ishara ya msalaba, nilishangaa kuona ushetani wa mwaka.
Sikutaka hata kuongea nao, pia sikutaka kulala nao, niliinuka kisha nilishuka chini nikitaka kuondoka lakini mume wangu alinizuia.
Aliniambia marufuku kwenda nje ya chumba, aliniambia kama sitaki kulala kitandani basi nilale chini ila sio kuondoka chumbani.
Niliona sio mbaya, bora kulala.chini kuliko kulala na mashetani. Nilichukua kanga yangu nilitandika juu ya carpet kisha nilichukua shuka
nililala. Niliamua kujifunika gubi gubi kuanzia chini hadi juu ili nisiweze kuwaona waja wenye laana. Licha ya kwamba sikupata usingizi ila angalau nafsi yangu iliridhika kutolala na mashetani.
Zilipita dakika nyingi kukiwa kumetulia, nilidhani kwamba watakuwa wamelala. Sasa nikiwa sina hili wala lile mara kwa mbali nilianza kusikia papatu papatu, miguno ilisikika kimya kimya, kilio cha Rahabu kilianza taratibu na kadri dakika zilivyokwenda mbele kilio kiliongezeka.
Nilishindwa kulala, nilifunua shuka nilitazama kitandani aisee sikuamini. Kwa macho yangu mawili niliwashuhudia wakizagamuana, mume wangu aligeuka alinitazama kisha aliendelea na kazi yake, aliongeza spidi. Rahabu nae aligeuka alinitazama, alitabasam kisha alitanua miguu zaidi kisha alimkumbatia baba Masoud ili tu kunikomoa mimi.
“Afu bebi mimi nikiwa nashughulikiwa huwa sipendi mtu anitazame, huyu Gensu aondoke tu,
SEHEMU YA 60
anafanya nisihisi utam”
“Haya wewe mwanamke njoo tuungane au kama hutaki tupishe sisi tufanye kazi. Umekaa hapo unatuchora tu, hujui kuwa unapunguza utamu? Ondoka tupishe, sisi tuna jambo letu” Mume wangu alinifukuza
Ningefanyaje sasa?? Licha ya kwamba chumba ni changu lakini niliamua kuondoka niliwapisha wafanye jambo lao. Mimi nilienda kulala sebuleni kwenye sofa. Nililala nikiwa nalia tu, nilipata uchungu na hasira nyingi lakini ilikuwa kazi bure!! Niliendeea na unyonge wangu.
****
Asubuhi licha ya kwamba ilikuwa ni jumatatu lakini hawakuamka mapema, waliendelea kulala. Mimi nilikuwa wa kwanza kuamka, nilianza kufanya usafi. Mama nae alifuatia kisha alinisaidia kufanya kazi ndogo ndogo kama kuosha vyombo n.k. Maboss bado walilala, hawakukumbuka kazi wala ajira.
Mimi na mama tulimaliza usafi, tulianza kutandika masofa na kupanga vitu. Sasa tukiwa tunaendelea na upangaji wa vyombo, kule chumbani mashetani yalianza kutenda dhambi. Nilitamani nimchukue mama haraka nimkimbize nje lakini nilichelewa, kelele zilikuwa kubwa sana. Yaani bora hata wangekuwa wanafanya kwa heshma lakini haikuwa hivyo, walifanya utafikiri wapo kwenye mashindano ya uasherati. Rahabu alilalamika kimahaba kwa sauti kubwa, bila shaka alifanya hivyo makusudi ili kunikomoa mimi na kunirusha roho.
Mama alinitazama kidogo kisha aliamua kutoka nje, alijisikia aibu. Mimi sikujua nikimbilie wapi, nilisikitika kidogo kisha niliamua kuvumilia tu, niliendelea kupanga vitu. Mara zile kelele zilikata, kabla sijakaa sawa mume wangu alitoka nje akiwa amevaa tauro tu. Aliniambia niandae chai haraka kwa sababu yeye na Rahabu wanahisi njaa.
Mwisho wa season 02
Endelea na sesson 03