MWANAUME WA NDOTO ZANGU
SEHEMU YA 36
“Shida gani?” nilimuuliza nikiwa nimemkodolea
macho mana alianza kunitisha
“Mtoto atashindwa kupita kwenye njia sahihi, utafanyiwa operesheni. Na pia kama mtoto atapita basi utapata maumivu makubwa kwa sababu njia itakuwa ndogo sana au itaziba.
Madaktari wanashauri mama mjamzito afanye tendo mara kwa mara ili kulegeza njia, kumkuza mtoto, kuepuka operesheni na kuepuka maumivu. Na hilo tendo lenyewe inabidi ufanye na baba wa mtoto… Ukifanya na mwanaume mwingine huyo mtoto anaweza akakosa akili, akawa kichaa, utambemenda!! Atakuwa kama zuzu vile”
“Eeh sasa mbona sijawai kusikia mambo hayo? Ngoja nikamuulize mama..” niliongea nikisimama ili nitoke nje
“Wewe… Hivi wewe mbona unakuwa kama mtoto.. Yaani masuala hayo ya chumbani unataka ukamuulize mama yako, huoni aibu??… Utamkosea heshma na adabu. Mi nimekuja
kukuambia tu kwamba mimba yako ina miezi mingi, jitahidi ufanye mapenzi na aliyekupa mimba”.
Alizidi kunivuruga kichwa, nilijikuta nimepata hofu nyingi, niliganda nikiwa natafakari maneno yake kama ni ya kweli au ya uongo. Kuna muda nilikubaliana na yeye kwamba kama mama mjamzito hasipofanya mapenzi, njia inaweza kuziba. Kwa upande mwingine niliona kama ananidanganya tu ili apate nafasi ya kunitumia kwa mara ya pili.
Sasa nikiwa naendelea kutafakari ghafla nilishangaa mkono wake ukichezea kifua changu, alichezea taratibu akiwa anaendelea kunisisitiza umuhimu wa tendo la ndoa kwa mjamzito. Nilibaki nimezubaa tu!! Mkono wake uliendelea kufanya fujo, aliushusha chini taratibu hadi katikati ya ikulu kuu, sijui alifanyaje jamani nilijikuta nimepagawa, nilibana mapaja na kuyaachia, jicho langu lilikwiva, nilikuja kushtuka nimebaki mtupu, yeye alikuwa juu
yangu akipambania kombe!!
“Kaka… we Kaka… Mi staki buanaa… Niache “
Nilipiga kelele kwamba sitaki lakini nilifurahia shoo.
“Gensu kwa sasa inabidi unipende tu. Hakuna haja ya kunyimana, mimi nadhani hata hii mimba haijaja kwa bahati mbaya, ni mipango ya Mwenyezi Mungu. Mimba hii ni ishara tosha kuwa tunapendana na tunafaa kuwa wapenzi.
Mimi ndiye mwanaume wako wa kwanza na naomba niwe wa mwisho.”
“Wa mwisho kivipi?”
“Sitaki mtoto wangu azaliwe nje ya ndoa. Kama hutojali naomba nikuoe. Na ukikubali nitakupa zawadi ya nyumba na kila kitu ukitakacho Vipi
upo tayari?” Aliongea akiwa anaongeza kasi ya mchezo, alizidi kunivuruga akili. Niliwaza kwa maisha haya ya sikuhizi kama nisipoolewa na yeye aliyeniharibia usichana na kunipa mimba, je nitaolewa na nani mwingine?.
“Sawa nimekubali, lakini utanioa vipi na hii mimba? Sheria za kiislamu haziruhusu, pia mimi ni mkristu”
“Kwani nani anajua kuwa wewe una mimba? Bila shaka ni sisi tu. Hivyo basi hiyo mimba utaificha ili tuoane. Na kuhusu dini itabidi ubadili, uje kwenye uislamu… Najua ni ngumu ila fanya hivyo kwaajili yetu ili tutimize malengo yetu”
“Sawa, ila naomba unioe kweli na unipende kwa dhati. Nataka ndoa nzuri yenye furaha na amani” Nilijikuta nimepayuka nikiwa namtazama kwa hisia kali za utamu wa mahaba
“Hilo halina shida, yani nitakupenda wewe hadi nitakupenda tena”
Kwa mara ya kwanza nilijikuta nimempenda kaka Nasri. Siku hiyo hatukuitana kaka wala dada, ilikuwa ni mwendo wa bebi tu.
Nilipigishwa shoo za kikubwa kuanzia asubuhi hadi usiku. Nilisahau habari za duka, kichwa
changu kiliwaza ndoa tu. Japo sikujua ndoa zipoje ila kwangu niliona ndoa ni jambo la heri!! Siku hiyo nilimpa kaka utamu wangu wote, nilimuachia kila kitu.
*****
Na hatimaye mimi na kaka tulikuwa wapenzi rasmi. Mwanzoni tulianza kwa siri ila kadri siku zilivyosonga mambo yalikuwa hadharani.
Rahabu alitambua, mama pia aligundua, hata majirani walijua kwamba mimi na kaka Nasri tuna jambo letu. Bebi wangu alinidekeza sana, yaani kila nilichotaka alinipa, ilifikia hatua nilisahau ubaya na unyama wote alionifanyia, nilimuona kama mfalme wa moyo na maisha yangu.
Kaka aliniambia kuwa anataka kutimiza ahadi zake. Kwanza alitaka anioe alafu mambo mengine yafuate. Nilimueleza mama kuhusu kaka kutaka kunioa, mama alifurahi sana.
Aliniambia nisifanye makosa kama aliyofanya yeye kuolewa na mwanaume maskini. Pia nilimueleza suala la kutaka kubadili dini, mama hakubisha, aliniruhusu nibadili ili niolewe na mwanaume mwenye pesa. Baada ya mama kukubali, kaka Nasri alifurahi sana, haraka haraka alipeleka ombi msikitini, nilipewa watu ambao walianza kunifundisha masuala ya dini ya kiislamu, nilislimu dini; nilipewa jina Nairath kisha mimi na bebi wangu tulifunga ndoa.
SEHEMU YA 37
Ndoa yangu ilianza vizuri sana, tena sana. Mume wangu alinijali, na ukizingatia nilibeba mimba yake, niliishi kwa furaha na amani.
Nikiwa mjamzito nilimkumbusha ahadi yake ya kunijengea nyumba, aliniambia nisijali, wiki zilizofuata alinua uwanja, aliita mafundi kisha ujenzi ulianza mara moja, aliniambia kuwa nyumba ikiisha mama ataenda kuishi huko ili
mimi na yeye tubaki kwenye nyumba yake.
Sio nyumba tu, mume wangu alininunulia kigari kidogo cha kwendea dukani kwangu. Pia kutokana na mimba kuwa kubwa, Rahabu alihamia dukani kwaajili ya kunisaidia shughuli za duka. Mimi nilikuwa kama boss tu, kazi yangu ilikuwa ni kupokea pesa, kuzihesabu na kuzipeleka benki!! Familia yetu ilikuwa ya kishua, mume wangu wa kishua, mama yangu wa kishua hata mfanyakaxi wetu Rahabu alikuwa ni wa kishua!! Maisha yalininyookea sanaaaa!!!
Miezi tisa ya ujauzito ilitimia, nilijifungua mtoto wa kiume ambaye alipewa jina Masoud. Jina lilitolewa na baba yake. Mtoto alipendwa huyo hadi nashindwa kuelezea. Alipendwa kwa sababu ni wa kiume. Alipendwa kwa sababu ni mtoto wake wa kwanza. Pia kitendo cha kumzalia mtoto kilisababisha aongeze mapenzi kwangu, kila siku aliniimbia mashairi kwamba hatonisaliti, hatoniumiza, hatoruhusu nipate shida, atanipenda milele daima. Mashairi hayo
yalifanya nivimbe bichwa, niliona ndoa yangu ni tamu na bora kuliko ndoa zote duniani.
Kwa jinsi ambavyo alizidi kunipenda nami nilijikuta nazama moja kwa moja kwenye moyo wake. Niliapa kwamba nitamuheshimu, nitamsikiliza, nitamzalia watoto wengine wengi, nitampenda milele, sitomsaliti, niliapa viapo vingi ambavyo vilimpendeza. Wanaume wengine niliwaona kama mazombi yasiyo na akili tu. Moyo wangu uliganda kwa mume wangu Nasri pekee, nilifurahi kuitwa Mama, pia nilifurahi kuitwa mke wa mtu, mke wa tajiri.
****
Ujenzi wa nyumba uliendelea, mafundi walipambana hadi walimaliza. Ukarabati nao ulianza, nyumba ilipigwa Finishing ya hali ya juu, ilikuwa nyumba nyumba kweli. Baada ya ukarabati alinunua vifaa na vyombo vya ndani alivijaza mjengoni, nyumba ilikamilika na ilikuwa
tayari kwaajili ya kuishi.
“Jamani eeh, mama Masoud pamoja na bibi Masoud! Mimi kama nilivyowaahidi kwamba nitawajengea nyumba kama shukrani zangu kwenu. Hasa hasa mke wangu, nashukuru sana kwa kunizalia Masoud. Ni muda mrefu nimekuwa nikisaka mtoto lakini sikumpata.
Wapo ambao walitoa mimba zangu, wapo ambao hawakutaka kunizalia. Lakini mke wangu Nairath (Gensu) umenibebea mimba, hujatoa mimba yangu na umekubali kunizalia.. Nawapa hii nyumba kama zawadi tu”
“Asante sana baba ubarikiwe sana, sisi tunamshukuru Mungu kwa kutuletea hii miujiza… Mungu akutunze sana baba angu”
Mama alijibu
“Usijali mama. Ile ni nyumba yako, na kuanzia leo nakukabidhi hii funguo utaenda kuishi kwenye nyumba yako. Pia tayari nimekuandalia Dada wa kazi mwingine ambaye atakusaidia
kazi zote kwenye nyumba yako mpya.”
“Aah jamani, yaani Mimi leo namiliki funguo za nyumba yangu? Siamini Mimi baba weee… Uhu- uuuuhuh siamini tobaa nenga niyapatili maishaaa” Mama alianza kulia kwa kilugha, alishuka chini alimpigia kaka magoti kisha alimshukuru
“Aah hapana mama huna haja ya kupiga magoti, hiyo ni haki yako kwa kunizalia mke mzuri……
Na hivi karibuni mama yangu nawe nitakununulia gari yako”
“Tobaaaa Nene nafyaaa neneee nafya leluuuuu” Mama alianza kugalagala, ilifikia hatua Mimi, mume wangu na Rahabu tulibaki tunacheka tu kwa furaha. Tulifurahishwa na mama ambaye alipagawa baada ya kusikia atanunuliwa gari.
Mimi pia nilimshukuru Mume wangu kwa zawadi ya nyumba, ilifikia hatua nilishukuru ubakaji alionifanyia zamani, kwa maana laiti kama hasingetumia nguvu kuniingilia kimwili
sidhani kama ningeolewa, ningeitwa mama, ningepata gari na nyumba! Sidhani.
*****
Mama tayari alihamia kwenye nyumba yetu mpya, huko aliishi pamoja na Dada wa kazi mpya. Mjengoni tulibaki Mimi, mume wangu, mtoto wetu na Rahabu. Kwakuwa mama aliondoka ndani ya nyumba tuliobaki tulijiachia tu, zile heshima na usiri vilipungua. Mume wangu hakuona aibu kunipiga mabusu sebuleni, jikoni au popote!! Mahaba yalifanyika waziwazi bila vificho.
Miezi ilikatika, mwaka mmoja wa ndoa ulitimia. Mama yangu alinunuliwa gari yake kama alivyoahidiwa. Mtoto wetu alizidi kukua siku hadi siku!! Mtoto alitambaa, alisimama, alianza kutemba, hata kunyonya aliacha!! Kwa kipindi chote hicho mahaba yalikuwa ndindindi. Mtoto wa kike nililelewa kuanzia kwenye pesa, mavazi,
matunzo, yaani ukinitazama unaweza sema sijazaa kumbe nilishaingia leba. Licha ya kwamba nilimiliki biashara lakini pesa yangu ya biashara haikutumika hata kidogo. Pesa zote niliwekeza benki. Matumizi yangu na matumizi ya familia yote yalifanywa na mume wangu kipenzi.
Kwa namna ambavyo nilichezea pesa sikuona tena umuhimu wa shule. Nilishukuru bora hata nilifukuzwa shule kwa sababu ningepoteza muda wangu tu. Kitu pekee ambacho nilijivunia ni kukutana na mwanaume mwenye pesa ambaye hakuona hasara kunijaza mapesa.
Nilizungushwa kwenye mbuga zote, hapa Tanzania hakuna mkoa ambao hatukuwai kwenda. Alafu sio kwamba tulienda kwaajili ya kitu fulani, ila basi tu ilimradi kutembea. Sio ndani ya nchi tu, tuliogelea hadi Zanzibar kisha tulipaa hadi Kenya na Uganda!! Muda wote aliniweka kifuani kwake, niliishi pembeni yake, hakika nilikuwa ubavu wake wa kushoto, kila
kitu alinishirikisha, kama mume tu aisee ALLAMDULILAH, MASHALLAH, ASANTE MUNGU.
“Baba Masoud mume wangu” Nilimuita tukiwa nyumbani kitandani
“Narudia tena kukuambia kwamba huu mwili wangu uliufunua, unaufunua na utaufunua wewe tu katika maisha yangu yote ya dunia hii. Naapa kwa Mungu kuwa sitoguswa na mwanaume mwingine zaidi yako, Mimi ni Mali yako nitumie utakavyo.. Nakupenda sana mume wangu wa dunia”
“Ah ah ah! Hunizidi Mimi mke wangu, kwanza kila siku nakuona mpya tu…. Alafu mke…”
“Abee mume”
“Mtoto wetu Masoud tayari kafikisha miaka miwili na nusu, tumpeleke shule!! Kwa sasa nataka unizalie mtoto mwingine, nataka watoto wawili”
“Sawa mume, nipo tayari hata ukisema unataka watoto 10”
Yaani ile namalizia 10 tu, alinivamia hadi kifuani, moja kwa moja alianza kandanda pasipo maandalizi wala kupiga tizi. Kwakuwa nilimpenda basi kila alichonifanyia nilikiona ni kitamu tu! Akienda sekunde mimi kwangu poa, akienda dakika 2 Mimi kwangu gudaaa, ilimradi tulipendana tu. Hakutumia muda mwingi tulimaliza shoo, alinibeba tulielekea bafuni tulioga, tulitazama movie, Rahabu alileta misosi kisha tulikula pamoja.
****
Wiki chache mbele nilishika ujauzito wa pili. Kama kawaida yake alifurahia sana mimba hiyo. Sasa ubaya wa mimba hii ya pili ni kwamba ilinisababishia maumivu makubwa wakati wa kushiriki tendo. Nilimueleza mume wangu lakini hakuwa muelewa sana, yeye kila akijisikia
alinigeuza alinifanya atakavyo. Ghafla nilianza kutoa maji maji sehemu za siri, maji yalitengeneza uchafu ambao ulifubaza eneo la siri. Ile sehemu ilianza kubadilika rangi kutoka weupe hadi weusi, mume wangu alianza kuchukia.
“We siku hizi unachepuka au? Mbona huku chini kumekomaa sana? Alafu hakuna mvuto hata kidogo, kweusiiiii” Alinifokea kiasi cha kushindwa kabisa kula tunda lake kutokana na maji machafu ambayo yalikuwa yanavuja.
Alinuna kabisa akidhani kwamba namsaliti. Nilimsisitiza kuwa sijawahi kumsaliti lakini hakunielewa.
SEHEMU YA 38
Nilianza kuogopa, fasta nilielekea hospitali, nilipima niliambiwa mfuko wa uzazi umetoboka kutokana na kufanya mapenzi mara Kwa mara na kwa nguvu wakati wa ujauzito. Hayo yote
yalitokea kirahisi kwa sababu zamani niliwahi kuugua U.T.I. Nilimrudishia majibu mume wangu, aliyasoma aliyaelewa.
“Kwahiyo wewe na madaktari wako mlikubaliana kwamba Mimi ndiye nimekutoboa uzazi ili uvujishe maji au sio?… Basi sawa, kuanzia leo sitokugusa tena, tutalala kama maroboti. We si uliolewa ili uje kula, kulala na kuamka; sawa haina shida.”
“Sio hivyo mume, dokta kasema kwanza inabidi nipate tiba kisha nikipona inabidi tupunguze spidi ya kufanya tendo, tufanye polepole mara chache”
Licha ya kumuelekeza kwa upole lakini hakutaka kunisikiliza, kwa hasira aliondoka nyumbani, sijui alienda wapi. Tangu anioe hakuwahi kurudi nyumbani usiku, lakini siku hiyo alirudi saa nne usiku. Alinikuta nikimsubiri kitandani, alioga kisha alipanda juu ya godoro!! nilimuuliza mbona kachelewa hakunijibu,
nilimuuliza alikuwa wapi hakunijibu, nilijaribu kumkumbatia lakini mwenzangu alivuta shuka alijifunika gubi gubi hadi machoni.
Mambo yalianza kwenda tofauti lakini nilivumilia niliona ni vitu vya kawaida tu, nilijua ipo siku atanielewa. Ni kweli baada ya siku chache alirudi kwenye hali yake, aliniomba msamaha kisha alininunulia dawa ambazo nilianza kuzitumia. Nilimaliza dozi ya kwanza sikupona. Dozi ya pili maji yalipungua. Dozi ya tatu majimaji yalikata. Tulijaribu kufanya lakini niliugulia maumivu makubwa. Kwakuwa ni muda mrefu hatukufanya, baba Masoud hakukubali kuniachia, alilazimisha hivyo hivyo, niliugulia maumivu makali lakini hakutaka kunielewa, sasa wakati anataka kufika mwisho alizidisha spidi, ile spidi ilienda kuchokonoa kwenye tobo ambalo lilianza kuziba, kwanza nilisikia kichomi alafu ghafla maji machafu yalimwagika nje!! Nilimsukuma kwa nguvu alidondokea pembeni.
“Hivi mume wangu kwanini hauna huruma? Licha ya maumivu lakini nilikuacha ufanye, lakini badala ya kwenda polepole unanikamia utadhani Mimi ni malaya. Kwani kuna kipi kigeni ambacho hukijui kwenye mwili wangu? Hizo nguvu unazotumia unataka kumuharibu mtoto wetu au? Mimba yenyewe hii ishakuwa kubwa lakini mwenzangu unaona kama nimebeba tofali tumboni kumbe nimebeba kiumbe hai…
Ona sasa maji yanavyotoka huku chini? Kidonda kilipona lakini umekitonesha, si unaona sasa?” Siku hiyo niliamua kumtolea uvivu, nilimfokea.
“Ooh umeanza kunipanda kichwani, wow! Wow! Wow!! Haina shida” Alijibu kwa jeuri na dharau kisha alivaa nguo zake aliondoka. Alipotea kabisa na sikujua alipotelea wapi. Siku ya kwanza ilipita hakurudi nyumbani, siku ya pili hakuonekana, alianza kuniumiza kichwa, alifanya nisipate usingizi, mimba ilinitesa na yeye badala ya kunijali alizidi kunivuruga tu.
Siku ya tatu nilishangaa kuona viatu vyake
vikiwa sebuleni lakini yeye mwenyewe sikumuona. Nilimuuliza Rahabu kama kamuona shemeji yake, alijibu kuwa hajamuona.
Nilipotezea nikidhani labda alirudi aliacha viatu kisha aliondoka tena. Siku ya nne alirudi usiku saa saba. Nilimfungulia mlango wa chumbani, alizama ndani lakini alinipita kama hanijui vile, hakunisemesha kitu chochote. Nilimuuliza hizo siku tatu alikuwa wapi lakini hakunijibu. Nilikaa kitandani nikiwa namtazama. Alianza kuvua nguo zake akitaka kwenda kuoga. Sasa wakati anavua suruali nilishangaa kuona ndani hajavaa kitu.
“Baba Masoud, uliondoka hapa ukiwa umevaa boksa yako nyeupe…. Sasa mbona umerudi na ndani hujavaa kitu?… Boksa yako ipo wapi?.” Nilimuuliza nikiwa nimemkodolea macho, nilisimama nilimsogelea ili tuelewane vizuri.
Kwanza alijitazama vizuri alishtuka kuona ni kweli hakuvaa boksa.
“Nimeisahau gest”
SEHEMU YA 39
“Gest?? Ina maana uliiacha nyumba yako alafu ulienda Kulala gest si ndiyo?”
“Ndiyo. Hata ungekuwa wewe ungewezaje kulala na mwanamke hasiyetumika?
Mwanamke ukimgusa kidogo analialia… Nadhani uliinjoy sana kulala peke yako, pia najua umeumia sana Mimi kurudi hapa! Bila shaka unahisi nitakuomba sehemu zako za siri, ah ah ah! Usijali, siwezi kukuomba unyumba wala uchumba… Nimekuja kuoga tu kisha narudi gest nikapate usingizi mzuri” Aliongea akiwa anavaa taulo, alielekea bafuni ambako alioga kisha alirudi chumbani alianza kuvaa nguo zake zingine.
Nilidhani ananitania lakini hakutania, baada ya kuvaa nguo alichukua funguo ya gari aliondoka. Nilikosa hata nguvu za kumzuia, nilibaki namtazama nikiwa nalia. Ndoa yangu tamu hatimaye ilianza kuwa chungu. Na ubaya ni kwamba sikujua shetani gani ameingia kwenye familia yangu. Kwa jinsi ambavyo alikuwa
ananipenda, aliniachisha shule, sikutegemea kama kuna siku angenitelekeza nyumbani kisa tu nimeshindwa kumpa penzi.
Niliona haiwezekani, kwa hasira nilipiga hatua kuelekea nje. Baada ya kufika nje nilishangaa kuikuta gari yake ikiwa imetulia lakini yeye mwenyewe hakuonekana. Kilio changu kilikata kwanza, nilitulia nikiwaza kaondoka kwa usafiri upi? Au kapanda bajaji? Au bodaboda? Sasa mbona alitoka ndani akiwa amebeba funguo?
Ile funguo ilikuwa ni ya kuzugia au inakuaje?… Nilishindwa kuelewa kwakweli. Nilirudi ndani nilijaribu kumpigia simu lakini namba yake haikupatikana. Sikuwa na la kufanya, niliamua kulala tu.
****
Siku iliyofuata saa 12 alfajiri nilisikia watu wakizungumza kutokea sebuleni. Nilishtuka sana tu! Niliamka kisha nilitembea hadi
mlangoni, nilifungua mlango nilichungulia nilishangaa kumuona Rahabu akiwa na mume wangu wakifanya usafi. Mmoja alideki ndani alafu mwingine alikuwa anasafisha madirisha. Kuna muda walitaniana kisha walicheka kwa pamoja. Kamoyo kangu kalipata ganzi. Kamoyo kalianza kuzunguka kutoka kimbiji hadi ferry Kigamboni. Nilijiuliza inakuwaje tena!!! Tangu lini mume wangu aamke alfajiri kisha afanye usafi?
Kuhusu Rahabu sikushangaa sana yeye kufanya usafi muda huo. Ila tu nilijiuliza imekuaje afanye usafi na mume wangu? Walianzaje anzaje hadi wakubaliane kufanya usafi pamoja? Na kama mume wangu alilala gest, imekuaje aonekane muda huo akifanya usafi??. Nilijiuliza maswali mengi yasiyo na majibu. Wivu ulinitawala kuanzia unyayoni hadi unyweleni. Presha nayo ilijaa kifuani kwangu, hasira zilinikamata, na ubaya ni kwamba sikujua nichukue uamuzi upi.
Sikutaka kushuhudia mengi, kwa uchungu
mkubwa nilifunga mlango kisha nilirudi kitandani! Kwa Mara nyingine nilianza kuporomosha machozi. Nililia vilio vyote!! Kilio cha kwikwi, cha sauti, cha kutabasam, cha kununa, na kadhalika na kadhalika. Saa moja asubuhi mume wangu aliingia chumbani, alinikuta nikifuta machozi. Alijua kuwa ananitesa lakini kama kawaida yake hakunipa pole, hakunionea huruma, hakunisalimia wala hakunisemesha. Safari hii hata kuoga hakuoga, sijui alioga wapi!! Alibadili tu nguo zake kisha aliondoka. Na tangu aninunie hakuwai kuacha pesa za matumizi. Laiti kama nigekuwa sifanyi biashara nadhani chamoto ningekiona.
Baada ya mume wangu kuondoka; haraka haraka nilimfuata Rahabu, nilimkuta akipika!! Alafu alikuwa akipika akiwa amependeza kinoma. Alivaa gauni ndefu, kichwani ushungi kama wote, mikononi alijaza bangili, miguuni vikuku, ukimtazama unaweza sema yeye ndio boss wa nyumba alafu Mimi ndiye dada wa kazi.
SEHEMU YA 40
“We Rahabu mbona sikuhizi unavaa vitu vya gharama sana? Alafu unapendeza kuliko kawaida”
“Ah ah ah Dada Gensu nawe, kwahiyo unataka niwe mchafu muda wote?”
“Wala sijamaanisha hivyo… Ok tuyaache hayo….
Na ilikuwaje asubuhi asubuhi ukafanya usafi na shemeji yako?”
“Ni yeye mwenyewe tu ndiye aliamua. Alinikuta nikideki ndani, aliamua kunisaidia kusafisha madirisha.”
“Aah kumbe… Basi sawa, kwahiyo leo tunakula nini?” Niliamua kubadili mada baada ya kupata ukweli. Majibu ya Rahabu yalinihakikishia kwamba ni kweli mume wangu alilala gesti kisha alirudi asubuhi. Tuliungana tuliandaa chai na vitafunwa, tulikula kisha tulielekea dukani kwangu.
*****
Maisha yaliendela, tabia za mume wangu zilizidi kubadilika siku hadi siku. Muda wote alinikoromea hata kama sikufanya kosa.
Nikipika mimi aliniambia sijui kupika, eti chakula changu hakinogi. Akipika Rahabu alimsifia kuwa anajua kupika chakula kitamu. Na ikifika usiku licha ya kwamba hatukufanya kitu lakini hakutamani hata nimguse. Nikitaka kumkumbatia aligeukia upande wa pili.
Nikimfuata anaondoka analala chini au anaenda kulala sebuleni kwenye sofa. Hayo yote niliyavumilia!!!
Nakumbuka siku hiyo nilibaki nyumbani pekeangu. Mume wangu alienda kazini alafu Rahabu alienda dukani kwangu. Nikiwa nyumbani niliwaza kwenda kusuka. Lakini kutokana na mimba niliamua kumpigia msusi aje kunisukia nyumbani. Baada ya sekunde chache msusi alikuja, lakini kwa bahati mbaya alisahau chanuo. Nilitakiwa nitafute chanuo
kisha nimpe anisuke. Nilielekea chumbani kwangu nilikagua mezani lakini sikukiona. Mara nilikumbuka chanuo alichukua Rahabu. Nilipiga hatua nilielekea chumbani kwa Rahabu, kwa bahati nzuri alisahau kufunga mlango. Nilizama ndani, moja kwa moja hadi mezani, ni kweli nilikuta chanuo juu ya meza. Nilikichukua kisha niligeuka nikitaka kuondoka!! Lakini kabla sijaondoka macho yangu yalitua kwenye boksa nyeupe ya mume wangu ambayo ilitundikwa kwenye kabati la nguo za Rahabu.
INAENDELEA