MWANAUME WA NDOTO ZANGU
SEHEMU YA 31
Bado hakutaka kukubali, aliniwahi kisha alinivuta mkono alinipeleka kwenye gari yake, alinizamisha ndani, nae alizama ndani kisha aliondoa gari kwa kasi kubwa. Tulifika nyumbani tuliwakuta mama na Rahabu wakila chakula cha usiku. Mimi nilipitiliza nilielekea chumbani kwangu, kaka nae alienda chumbani kwake. Mama na Rahabu walibaki wanashangaa tu, wao hawakijua kinachoendelea.
Nikiwa chumbani kwangu muda wote nilikuwa nalia kwa hasira, kila nikiwaza namna nilivyoharibiwa masomo nilijikuta naumia sana. Sikutaka kukaa na maumivu moyoni, niliona bora nikamuambie mama ili nae ajue ukatili alionifanyia kaka.
Niliacha kulia, nilifuta machozi kisha nilitoka kitandani nilielekea sebuleni. Nilikaa pembeni ya mama kisha nilimuita taratibu, mama aliitika.
Yaani kabla sijamuambia chochote kaka Nasri alitoka nje alikuja kukaa pale pale kwenye sofa. Alianza kujiongelesha mbele ya mama, mara alienda kwenye friji alichukua matunda alimpa mama. Mara alijiandalia chakula kisha alianza kula. Mara alinikaribisha mezani!! Yaani hakueleweka hata kidogo, shobo zilikuwa nyingiii! Nami nilitulia kimya kwa sababu nilijua kwanini anafanya hivyo. Hakutaka nimuambie mama ukweli.
Alikula hadi alimaliza lakini hakuondoka. Huwaga hapendi kuangalia movie lakini siku hiyo aliangalia. Mama alianza kusinzia, aliaga alienda kulala. Rahabu nae hapendagi kuangalia movie akiwa na kaka, aliaga kisha aliondoka.
Tulibaki mahasimu wawili. Nami kimya kimya pasipo kumuangalia mtu usoni nilinyanyuka nilielekea chumbani kwangu, nilijifungia mlango ndani kwa ndani.
Sekunde zilikatika, dakika zilisepa, masaa yaliondoka! Usingizi ulinipitia, sikujua
kinachoendelea duniani. Saa saba usiku mlango wa chumba changu uligongwa. Moja kwa moja nilijua mgongaji ni bakabaka, sikutaka kwenda kufungua, nilivuta shuka nilijifunika gubigubi ili nisimsikie. Nilimkaushia hadi ilifikia hatua kukawa kimya, nilihisi labda ameondoka lakini hakuondoka. Mida ya saa nane alianza kunisumbua tena, aligonga mlango hadi nilishindwa kulala. Nilienda kufungua nilimkuta kashika sahani ya chakula, matunda na pesa nyingi. Alizama ndani alienda kuniwekea kitandani kisha aliondoka.
Nilifunga mlango nilirudi kitandani. Nilitazama chakula chake, matunda na pesa, nilivipenda sana lakini nilivichukia kwa sababu aliyeniletea sikumpenda hata kidogo. Kwa hasira nilichukua sahani nzima kisha nilienda kuitupia kwenye dustbin iliyopo chumbani kwangu. Kuanzia chakula, matunda na pesa zake zote nilitupia kwenye kapu la takataka kisha nilirudi kitandani nililala!
Safari hii sikupata usingizi. Muda wote niliota ndoto za maisha yangu tu, katika maisha yangu sikutegemea kama kuna siku ningeshika mimba ya mwanaume nisiyempenda. Nilitulia niliwaza nitazaaje mtoto kupitia mimba ya kubakwa?
“Yaani kisa ana pesa ndo anipelekeshe atakavyo? Hapana kwakweli. Hii mimba kesho naitoa… Hata sumu nitakunywa ilimradi iondoke tu. Kama lengo lake nimzalie basi amenoa!!!
Kama yeye ameniharibia masomo, basi mimi namuharibia mimba” Niliwaza kimya kimya macho yakiwa juu, nilipitiwa na usingizi pasipo kujijua.
*****
Kulikucha siku iliyofuata kama kawaida yangu niliamka mapema lakini sikutoka kitandani kutokana na hasira. Sikuwaza kuhusu kufanya usafi wala kupika, niliwaza kutoa mimba tu.
SEHEMU YA 32
Nilitulia kitandani nilisubiri kaka Nasri aende kazini ili nami niende mtaani nikatafute dawa za kutolea mimba. Nikiwa chumbani mara mlango wangu uligongwa, nilichukia nikidhani ni kaka, sikutaka kwenda kufungua mlango.
“We Gensu ebu fungua mlango..” ilisikika sauti ya mama. Hapo sasa nilikurupuka nilivaa vizuri kisha nilienda kufungua mlango. Nilikutana na mama ambaye alinitazama kwa jicho kali, jicho ambalo sikujua lina maana gani. Alinitazama vibaya vibaya hadi nilijishtukia.
“Shikamoo mama” Niliamua kuzuga kwa salam
“Hivi wewe sikuhizi umekuwaje? Ni mzima kweli wewe?”
“Mi mzima mama, kwani nipoje?”
“Ebu fikiria hadi saa nne hii bado umelala, sikuhizi usafi hufanyi unamuachia Rahabu pekeyake. Hata kama ni dada wa kazi ila nae anachoka, kumbuka wewe pia ni wa kike hivyo basi ni lazma ujifunze kufanya kazi za
nyumbani. Au unataka hapo baadae mumeo apikiwe na dada wa kazi, aogeshwe na dada wa kazi, afuliwe chupi na dada wakazi, si ndiyo?”
“Hapana, nilipitiwa tu na usingizi”
“Ulipitiwa???…. Kwanza we unaonekana kuna kitu unanificha…. Hivi wewe una uhakika umerudishwa nyumbani kwakuwa shule yenu imeshindwa kulipa kodi?……. Eti mwanangu ebu niambie ukweli mimi mama yako, nini kilitokea huko shuleni kwenu? Kwanini huendi shule?” Hapo sasa mama aliniuliza kistaarabu na kwa upole. Nilitulia kidogo nikiwa natafakari, niliona hakuna sababu ya kumficha mama yangu.
“Mama…”
“Abee mwanangu”
“Shule yetu sio kwamba imeshindwa kulipa kodi… ila… ila…”
“ila nini mwanangu “
“Ila tu nimefu…..” Kabla sijamalizia ghafla kaka
Nasri alitokea akiwa amevaa suti yake, alishangaa kuona nimesimama na mama mlangoni. Alipata mawenge!! Haraka haraka alichomoa pesa mfukoni kisha aliniita aliniagiza dukani nikamnunulie vocha. Hayo yote alifanya ili kunitenganisha na mama, aliogopa nitamuambia mama ukweli. Hata baada ya kumletea vocha hakuondoka sebuleni, alikaa pale pale ili hasinipe nafasi.
Kwa jeuri nilimuacha akae na mama, Mimi nilielekea chumbani kwangu, nilichukua pesa kisha nilitoka nje. Hapo hata usoni sikunawa, sikupiga mswaki wala sikuoga; nilizunguka duka moja hadi jingine nikitafuta dawa za kutolea mimba. Baada ya kuzunguka sana hatimaye nilikutana mdada mtaalamu wa dawa za kutoa mimba. Aliniuliza mimba ina muda gani nilimjibu hata mwezi haijafikisha. Alinipatia dawa ya maji, aliniambia nichanganye na mchuzi wa malimao 7 kisha ninywe kwa siku saba. Japo hakutaka kunichaji pesa ila nilimpa elfu 30.
SEHEMU YA 33
Nilichukua kichupa changu nilianza safari, njiani nilinunua malimao kisha nilirudi nyumbani, niliwakuta mama na Rahabu tu wakicheza karata; kaka sikumuona, bila shaka alienda kazini kwake kwa sababu mlango wa chumba chake ulifungwa kufuri. Kimya kimya nilielekea chumbani kwangu niliweka dawa mezani kisha nilirudi sebuleni, nilikula chakula cha mchana kisha nami nilijiunga kwenye karata. Angalau karata zilinipotezea mawazo, tulicheza hadi Giza liliingia, tulipika, tulikula kisha tulihamia kwenye movie. Tuliweka movie ya kibongo ya kuchekesha, ilikuwa ni mwendo wa kucheka tu!!! Hasa hasa Mimi siku hiyo nilifurahi vibaya mno.
Hadi inafika saa nne usiku kaka Nasri hakutokea, jambo hilo liliniongezea furaha kwa sababu nilimchukia sana, sikitaka kumuona hata kidogo, nilitamani alale huko huko ili nikamilishe mpango wangu wa kutoa mimba kwa Uhuru zaidi. Mama alichoka alienda kulala,
tulibaki wawili, tuliendelea kufurahi hadi saa tano usiku, tulichoka, tuliagana kila mmoja alienda kulala chumbani kwake.
Baada ya kufika chumbani sikutaka kupoteza muda, kwanza niliandaa mchuzi wa malimao nilichanganya na dawa kisha nilitikisa kwa nguvu ilitoa mapovu mengi. Nilielekea sebuleni nilichukua grass kisha nilirudi chumbani, nilipima nusu kisha nilinyanyua grass niliipeleka mdomoni. Yaani kabla hata haijafika mdomoni ghafla mlango wa chumba changu ulifunguliwa!!
“Weee usinywee!!” Ilisikika sauti kali kutoka kwa kaka. Sauti hiyo ilifanya nishtuke kiasi cha kudondosha grass ya dawa. Licha ya mshtuko na kumwaga dawa lakini sikutaka kukubali.
Nilichukua chupa nzima, nilifungua kisha niliipeleka mdomoni nikitaka kujimiminia. Kaka aliniwahi, alininyan’ganya chupa kisha alinitazama kwa jicho kali.
“We umekuwaje sikuhizi? Eti Gensu una shida gani?”
“Nipe chupa yangu, nimesema nipe chupa yangu kabla sijapiga makelele kwamba unanibaka, namuita mama na Rahabu na majirani” nilianza kupiga makelele ambayo yalimchanganya kaka.
“Basi inatosha… Ongea pole pole… Kwahyo mdogo wangu ndo unanichukia kiasi hicho kweli??… Hata kama nimekukosea lakini sio kwa hasira hizo, nisamehe basi. Imefikia hatua unataka kutoa mimba yangu, ebu tazama pale kwenye dampo; kumbe kile chakula na pesa zangu ulitupa kwenye kapu la taka? Daah ama kweli hunipendi……” Aliongea kwa upole akiwa ananitazama, Mimi nilitazama pembeni nikiwa nalia kwa hasira. Baada ya kuona nimetulia alikaa pembeni yangu kisha alianza kunibembeleza;
“Usilie Gensu, najua unapenda sana kusoma na ndio maana niliamua kukupeleka shule.
Kiukweli kabisa kutoka moyoni najuta sana kwa kitendo ambacho nilikufanyia, naumia kuona umeharibu masomo yako nyakati za mwisho…
Hata hivyo wahenga walisema kufeli shule sio kufeli maisha, nataka nikulipe hasara zote nilizokusababishia baada ya kukupa mimba isiyotarajiwa na kukuharibia masomo” Alizidi kuongea kwa hisia zote kiasi kwamba niliacha kulia, niliinua uso kisha nilimtazama usoni.
Nilitaka kusikia namna ambavyo atanilipa madeni yangu.
“Kwanza hata kama hunipendi lakini naomba husitoe mimba yangu. Nitafurahi sana ukinizalia mtoto, na nitahakikisha nailea mimba yangu na nitamlea mtoto wangu. Pia nitakulea wewe kwa gharama yoyote ile. Jambo la pili naomba unisamehe, nataka tuishi kwa upendo na amani kama zamani. Lakini pia naomba unitunzie siri zangu kwa mama. Hata kama atagundua kuwa una mimba husije ukamuambia kwamba nilikubaka, mwambie tu kuwa tulikuwa kwenye
mahusiano. Na jambo la mwisho ni kuhusu maisha yako. Najua ndoto yako kubwa ni kuwa mwanamke mwenye pesa, anayejitambua.
Unataka uwe na pesa ili uweze kumlea mama yako na kufanya mambo mengineyo, na ndio maana ulitamani sana kupata elimu ukiamini itakupa pesa. Gensu mdogo wangu usililie elimu ya darasani, siku hizi wasomi wapo wengi hawana ajira, hawana kazi na kubwa zaidi hawana pesa. Elimu pekee ambayo inaokoa watu ni elimu ya mtaani, elimu ya kufanya kazi kwa matendo. Hivyo basi Mimi nitatimiza ndoto zako za kumiliki pesa. Nitakufungulia biashara ya mtaji wa million 5, pesa ambayo utaipata itakuwa yako wewe na mama yetu. Pia sitowafukuza hapa kwangu, mtaishi bure na mtakula bure… Vipi upo tayari? Na je umenisamehe? Hutotoa mimba yangu?” Kaka alimaliza kuongea kisha aliniuliza maswali ambayo yaliniweka njia panda, nilitulia nikiwaza nijibu nini
SEHEMU YA 34
“Nipo tayari na nimekusamehe, pia mimba yako nitailea na nitakuzalia” Niliamua kukubali baada ya kutafakari na kugundua ameongea mambo mazuri.
“Wow!! Asante sana mdogo wangu… Na ndio maana nakupenda sana” Aliongea kwa furaha kisha alinikumbatia kwa nguvu. Alitaka kunipiga busu lakini nilikwepesha mdomo. Nilikwepesha kwa sababu alitaka kuniletea masuala ya mapenzi kitu ambacho sikupenda hata kidogo, sikuwa na hisia nae ila nilimkubali kama kaka yangu tu.
Kwakuwa nilimsamehe alinishukuru kwa porojo nyingi nyingi kisha aliniaga alienda kulala chumbani kwake, nami nililala kitandani kwangu nikiwa mwenye amani kubwa. Yale mawazo ya kutoa mimba yalipotea kabisa!!! Niliwaza kuhusu biashara ambazo atanifungulia, niliwaza
namna ambavyo nitakuwa natengeneza pesa zangu, nilibaki natabasam tu, hata muda ambao nilipitiwa na usingizi sikuutambua.
*****
Ni kweli siku iliyofuata kaka alianza kutimiza ahadi yake. Siku hiyo hakwenda kazini kabisa, asubuhi alinichukua kisha tulianza kutafuta frame ya biashara. Alinipa mamlaka yote ya kuchagua eneo ninalotaka na biashara ninayotaka. Nilipata frame maeneo ya madukani, na nilichagua kuuza nguo za ndani za kike ambazo zilijumuisha nguo za siri, nguo za kulalia, nguo za beach na kuogelea.
Alininunulia simu kubwa kisha alinielekeza namna ya kuitumia. Aliongea na marafiki zake wa Dar ambao walimtumia mzigo wa nguo kwaajili ya duka langu. Na baada ya kukamilisha kila kitu hatimaye nilianza biashara.
Mama aliniuliza biashara ni ya nani, nilimjibu ni
yangu nimefunguliwa na kaka! Alifurahi sana, pia alimshukuru kaka. Maisha yalianza kuninogea na hatimaye yalininyookea kabisa, nilitengeneza kipato cha kutosha, duka lilipata wateja wengi, nilikuwa maarufu mitaani na mitandaoni kupitia biashara yangu. Mara moja moja mama na Rahabu walikuja dukani kwangu kunisaidia kuuza, kupiga story na kupumzika ili siku ziende. Wakiwa dukani kwangu niliwanunulia kila kitu walichotaka, nilikuwa kama boss vile, sikuwa na shida ndogo ndogo.
Tangu nifunguliwe biashara ukaribu wangu na kaka Nasri ulizidi kuwa mkubwa. Hata hivyo tuliheshimiana sana. Kaka hakunisumbua tena kimapenzi, alikuwa bize na mambo yake, nami nilikuwa bize na biashara yangu, tukikutana nyumbani ni kucheka tu na kufurahi pamoja kama mtu na kaka yake. Mimba yangu nayo ilizidi kuwa kubwa. Ilibidi nianze klinic, siku ya kwanza nilienda hospitali pekeangu waliniambia hawawezi kunihudumia bila uwepo
wa baba kijacho. Nilirudi nyumbani nikiwa nimenyong’onyea, sikupenda kabisa suala la kuambatana na kaka Nasri kwenda clinic.
Kishingo upande nilimuambia kuhusu mimi na yeye kwenda clinic, alifurahi sana. Siku iliyofuata tulienda pamoja, tulipimwa magonjwa yote, nilipewa dawa za damu, tulipewa ushauri mbalimbali, tulijiandikisha kwenye kadi ya mama mjamzito kisha walinipangia tarehe ya kuanza clinic.
Muda huo ujauzito wangu ulikuwa ni wa miezi miwili. Nilianza kuchagua mavyakula, mara nilikula malimao, maudongo, alafu kubwa zaidi nilitamani muda wote niwe karibu na kaka Nasri. Jambo hilo lilimfurahisha sana tena sana, nae hakufanya makosa hata kidogo!! Alithubutu kutokwenda kazini ilimradi akae na mimi, kila nilichokitaka alinipatia, kazini kwangu alinipeleka na kunirudisha kila siku, nikimtuma kitu aliniletea, kila siku alinisimamia ninywe dawa za damu, hata siku ya clinic ilipofika yeye
ndiye alinikumbusha na alikuwa mtu wa kwanza kunisisitiza tuwahi clinic!! Kwa ufupi ni kwamba alikuwa kama mtumwa wangu, kitu pekee ambacho alikikosa kwangu ni penzi tu, hilo sikuthubutu kumpa, bado nilimuona kama kaka yangu!!
Mimba ilitimiza miezi mitatu, sio Rahabu wala mama ambaye aligundua. Sasa siku hiyo asubuhi nikiwa naosha vyombo mara nilihisi kutapika, kwa bahati mbaya nilichelewa kukimbilia bafuni; nilitapika pale pale kwenye karo. Nilitazama huku na huko sikuona mtu, nilisafisha haraka haraka kisha nilielekea dukani nilinunua udongo na limao, nilirudi nyumbani niliendelea kuosha vyombo nikiwa nakula udongo na limao kwa pamoja. Kumbe wakati mambo hayo yanaendelea mama yangu alikuwa ananichabo tu. Baada ya kumaliza kuosha vyombo nilivipeleka kwenye kabati kisha nilielekea chumbani kwaajili ya kujiandaa kwenda kazini. Sasa baada ya kufika chumbani
nilishtuka kumkuta mama akiwa ameshika kadi yangu ya clinic na karatasi zingine za vipimo vya mimba.
“Aah mama!!” Nilijikuta nimepayuka
“Unanishangaa kwani hunijui?… Kwahiyo wewe ni wa kunificha mimi kuhusu hilo tumbo lako?….” aliniuliza kwa ukali, alinikodolea macho ya hasira, nilikosa jibu, nilibaki nimeganda tu
“Kwani hapa naongea na kisiki au?” “Unaongea na mimi”
“Sasa mbona huongei? Mbona husemi? Mbona hunijibu?…. Na nikitazama hapa hii mimba ni ya muda mrefu, ina miezi zaidi ya mitatu. Na ilipatikana ukiwa shuleni.. Kumbe inawezekana ulifukuzwa shule sababu ya mimba si ndio?”
“Hapana mama…. Mimi sikupata mimba shuleni… Mimba niliipata baada ya kufukuzwa shule”
“Sawa. Na kwenye hii kadi baba wa mtoto anaitwa Nasri… Huyu Nasri ni Nasri yupi, eti hiyo mimba ni ya nani?” Mama alizidi kunikomalia. Lilikuwa ni swali gumu, niliwaza nimtaje kaka Nasri au nipindishe? Nilikumbuka Kaka Nasri aliniambia nimtaje ila alisema nisiseme kuwa alinibaka.
“Samahani mama, nisamehe”
“Nikusamehe bila kosa? Niambie huyu Nasri ni yupi? … Au ni kaka yako?”
“Ndiyo, ni mimba ya kaka Nasri. Baada ya kufukuzwa shule tulianzisha mahusiano ya siri, alinipa mimba, ila amesema atailea”
“Ooh kumbe ndio maana mnafunguliana mabiashara, kila muda mko pamoja, kumbee! Basi sawa” Mama aliongea kwa sauti ya mnuno, kwa hasira alisimama kisha aliondoka chumbani kwangu. Japo nilibaki nimeganda ila sikushangaa sana kwa sababu ilikuwa ni lazima anune. Na ukizingatia mimi ni mwanae wa
kunizaa, hivyo basi ni haki yake kukasirika.
Sikutaka kumuacha akae na hasira, nilimfuata sebuleni kisha niliendelea kumuomba msamaha, pia nilimsisitiza kuwa kaka Nasri atalea mimba yake bila shida yoyote. Kwa bahati nzuri kaka Nasri aliingia alinikuta nikiongea na mama, nae alisogea mezani kisha tuliweka kikao kifupi. Kwenye hicho kikao kaka Nasri alimuomba mama msamaha, pia alimsisitiza kwamba atahakikisha mimi nafanikiwa kimaisha, pia atahakikisha mimi na mama hatupati shida zozote. Mama hakuwa na namna, alitusamehe. Uzuri ni kwamba alimuheshimu sana kaka Nasri kutokana na misaada mingi aliyotupatia, na ndio maana alitusamehe haraka.
SEHEMU YA 35
Maisha mapya yalianza ndani ya familia. Kwakuwa mama alifahamu mimba yangu ni ya
nani, mimi na kaka Nasri tuliishi kwa uhuru zaidi, bila hofu yoyote. Pia kaka Nasri aliongeza upendo kwa mama, mara nyingi akirudi toka kazini alimchukulia vitenge, kanga, magauni, madela, vilemba, ilifikia hatua mama yangu alianza kufurahia kitendo cha kaka Nasri kunipa mimba mimi. Aliniambia kuwa nimepata bahati ya kuzaa na mtu mwenye pesa.
“Mh ama kweli acha Mungu aitwe Mungu” Mama alianza kunichokoza, muda huo tulikuwa dukani kwangu, Rahabu alibaki nyumbani
“Kwanini mama?”
“Hivi we huoni raha kupewa mimba na mtu kama Nasri?… Ebu fikiria tungekuwa kijijini unadhani hii mimba ungepewa na nani kama sio na makapuku?”
“Ah ah ah mama ushaanza maneno yako”
“Sio maneno yangu, huo ndo ukweli. Inabidi ushukuru sana kwa hii bahati. Kuna wanawake wenzio wamepewa mimba alafu
wametelekezwa kwa sababu mtoa mimba hana pesa, wewe umepewa mimba na mtu ambaye anailea, anatulea sisi, amekufungulia liduka likubwa, ebu tazama jinsi tunavyokula kiyoyozi, nione mama yako navyonenepa kwa raha, hata wewe mwenyewe jitazame mwanangu jinsi ulivyo mzuri kama malaikaaa!! Acha Mungu aitee Mungu bwanaa” Mama aliendelea kunikolezea maneno, ilifikia hatua nilianza kunogewa, kwa mbaali nilianza kuona fahari kupewa mimba na mtu mwenye pesa. Nilitulia nilimtafakari kaka Nasri, nilimuona ni mtu mzuri sana ambaye sifai kumchukia sana. Kutoka moyoni nilikubaliana na mama kuwa nimebahatika sana tena sana.
Siku hiyo tulitumia muda mwingi sana kumsifia kaka Nasri. Hasa hasa mama, muda wote alimsifia kiasi kwamba unaweza sema kaka ndiye mwanaume bora pekee duniani kumbe ni bakabaka tu. Kama kawaida usiku baada ya kufunga duka kaka alitupitia, alituchukua
kwenye gari yake kisha tulirudi nyumbani. Tuliishi kishua sana, unaweza sema hatukuwai kupitia shida kumbe wala!!!
****
Hatimaye mimba ilifikisha miezi minne. Katika kipindi chote hicho sikuwai tena kushiriki tendo la ndoa. Yaani tangu siku ile nimevamiwa na kaka, sikuwahi tena kuingiliwa kimapenzi na mwanaume yeyote. Na uzuri ni kwamba kaka hakunisumbua tena, hakunisumbua kwa sababu alitambua kuwa simpendi.
Sasa siku hiyo ilikuwa ni jumapili. Asubuhi nilienda kanisani, alafu baada ya kurudi nilijiandaa nikitaka kwenda dukani. Siku za jumapili huwa nafungua duka kuanzia saa tano au sita. Nikiwa chumbani mara mlango wangu uligongwa, nilienda kufungua nilikutana na kaka Nasri ambaye alizama ndani pasipo kuniongelesha kitu. Baada ya kuingia aliniambia
nifunge mlango ili tuongee jambo, nami bila ubishi niliufunga kisha nilimfuata kitandani nilikaa pembeni yake.
“Gensu” aliniita “Nakusikiliza”
“Hivi ina maana kwa kipindi chote hicho hujawai kutamani kufanya tendo? Hujawai kupata hamu za kunaniliu?”
“Sijawai na sitowai” nilimjibu kwa ufupi.
“Mmh! Yaani huna hisia hata kidogo!! Duh mbona shughuli!!… Alafu hivi unajua kwamba kama mama mjamzito hafanyi mapenzi, mtoto atakosa afya, mtoto hatokua vizuri, pia siku ya kujifungua utapata shida”
INAENDELEA