MWANAUME WA NDOTO ZANGU
SEHEMU YA 26
“Kaka…” nilimuita nikiwa namtazama usoni
“Achana na mambo ya kuitana, unaniita kwani hunioni? Wewe nambie kama umekubali au hutaki”
“Kwanza nisamehe kama nimekukosea, kiukweli kabisa nakuheshimu kama kaka yangu wa damu. Hata hivyo nashindwa kushindana na wewe, bado nahitaji misaada mingi kutoka kwako. Naomba nikuombe kitu kimoja tu…”
“Kitu gani?”
“Nisaidie hiyo pesa ya ada, mimi naenda kumalizia miezi michache iliyobaki alafu nikirudi
nitakupa unachokitaka na tutakuwa wapenzi”
“Aah ufala huo ndo sitaki… Alafu wewe nakulea sana… Nyie mabinti wengine hadi mbakwe ndo muelewe. Mi siwezi kuishi na binti mzuri kama wewe alafu nisikutumie… Sasa leo iwe isiwe, ukipiga kelele unahama kwenye nyumba yangu, penda husipende mzigo utatoa” aliongea kwa hasira kisha alinivamia kifuani, alichana nguo zangu hovyo hovyo ili tu atimize haja zake.
“Kaka plizi husinifanyie hivyo… Naomba nielewe kaka angu… Pia mimi nipo kwenye siku zangu za hatari, husije ukanitafutia matatizo….
Kakaaaa… Kaka plizzzz usifanye hivyoooo Ka-
ka+ka-ka……..” alinibana mdomo kwa nguvu kisha alifanya alichokitaka, niliambulia maumivu makali, mwili ulikufa ganzi, akili zote zilipoteana, sikujua kilichoendelea.
****
Saa nne asubuhi ndio muda ambao nilishtuka toka usingizini, nilishangaa kuona nimelala
kwenye kitanda cha hospitali. Pembeni yangu alikaa kaka Nasri ambaye alifurahi kuona nimeamka. Alichukua maji ya kopo alimiminia kwenye kikombe kisha alininywesha, baada ya sekunde chache aliingia dokta wa makamo tu, alinipima kisha alimuita kaka Nasri pembeni, waliongea mambo yao ambayo sikujua yalihusu nini. Baada ya maongezi yao kaka Nasri alinifuata kitandani kisha aliniuliza;
“Kwa sasa unaendeleaje?”
“Nahisi maumivu makali mwili nzima” Nilijibu kinyonge
“Pole, nimeongea na dokta anipe ruhusa ili nikupeleke shule ukaendelee na masomo. Vipi upo tayari?” Aliniuliza akiwa anatabasam. Licha ya kwamba sikujisikia vizuri lakini niliona bora niende shule, kama kupona nitapona huko huko.
“Nipo tayari”
Siku hiyo alikuwa mnyenyekevu kwelikweli, mara alininyanyua, alinisimamisha, alinishika
mkono kisha alinitembeza hadi kwenye gari yake. Wote tulizama ndani, aliwasha gari tulirudi nyumbani ambako nilijiandaa kisha alinipeleka madukani, alininunulia mazawadi mengi ili tu anifariji kutokana na ukatili alionifanyia. Baada ya shopping alinipeleka shuleni.
Hatukuchukua muda mwingi tulifika shuleni, moja kwa moja hadi kwa muhasibu, alinilipia ada na madeni yote yaliyobaki kisha tulirudi kwenye gari yake, aliniambia niingie ndani ili aniage, japo sikupenda ila niliingia, nae aliingia kisha alifunga vioo, alivyo hana haya alianza kunipiga mabusu, mara alinishika kifua, alinichezea tu kwajinsi alivyotaka, alinisisitiza kuwa ananipenda sana, alinipa pesa nyingi za matumizi kisha aliniruhusu niende hosteli.
Nilitoka kwenye gari yake nilielekea hostel ambako nililala, yeye alirudi nyumbani.
****
Nikiwa shuleni maisha yangu yalikuwa ni ya
mawazo tu. Kila nilivyojaribu kupotezea nilishindwa, moyoni nilianza kumchukia kaka Nasri. Licha ya kwamba alinisaidia mambo mengi lakini nilimchukulia kama adui yangu, nilimchukia vibaya mno. Laiti kama ningekuwa nina uwezo wa kuondoka nyumbani kwake, ningeondoka fasta tu.
Siku saba za mwanzo nilikesha hosteli nikiwa nalia peke yangu. Wenzangu walienda kujisomea lakini mimi nilidanganya kuwa naumwa. Sio kwamba nilikuwa naumwa, hapana, ila sikuwa na mzuka wa kujisomea.
Daftari niliona zito, kila nikijaribu kusoma sikuelewa chochote, kichwa changu kilikuwa kizito, muda wote nilijisikia uchovu tu.
Wiki iliyofuata niliamua kujikaza hivyo hivyo. Nilijitahidi kujichanganya na wenzangu kwaajili ya maandalizi ya NECTA. Japo sikusahau ubakaji wa kaka Nasri lakini angalau akili yangu ilikumbuka ndoto zangu, sikutaka kukata tamaa ya kutimiza malengo yangu. Na uzuri zaidi ni
kwamba kaka hakunisumbua kwenye simu, aliniambia ananiacha huru ili nipate muda wa kujisomea zaidi.
SEHEMU YA 27
Na hatimaye ilibaki wiki moja tu tufanye usajili. Kwakuwa madeni yote nilimaliza wala sikuwa na wasiwasi. Nakumbuka siku hiyo mabinti wengi wa kidato cha nne tulikuwa room moja hosteli kwetu. Tulikuwa tunaulizana maswali ya darasani, tulitaniana, na kuna muda kila mmoja alikuwa bize akiongea kwenye simu. Wapo ambao waliongea na mabebi zao, wengine na mama zao, wengine na baba zao, wengine na marafiki zao wa mtaani, yaani kila mtu na mtu wake, ni Mimi tu ndiye nilikuwa bize na kitabu.
Sasa tukiwa hatuna hili wala lile Mara ghafla tulishtushwa na sauti ya Matroni;
“Ooh kumbe ndo zenuuu!! Kumbe mnamiliki simuu!! Kumbe mna mabebi zenuu!! Kumbe
mkiachwaga huru huwa mnajiachia namna hiyoo…. Nyie vitoto mnataka kunifukuzisha kazi kwenye hii shule si ndio?”
“Hapana matroni” Tulijibu kwa pamoja tukiwa tunatetemeka, wote roho juu juu
“Nyie mnataka nionekane nawafundisha tabia mbaya au sio?. Kwakuwa mnakaribia kuhitimu kidato cha NNE mkaona bora muwaandae mabebi zenu ili mkifika huko mkatafute mimba au sio?”
“Hapana maadam” tulijibu
“Hapana nini? Nilikuwa hapa kwa muda mrefu, nimewasikiliza maongezi yenu yoote!! Mara muwajadili wanaume, Mara mzungumzie mapenzi, Mara upuuzi huu Mara upuuzi ule…
Shenzi zenu, tena nyie mnaonekana mna siri nyingi sana, mnataka kuharibu hadhi na hashma ya shule yetu au sio?”
“Hapaanaaa madaaam”
“Haya wote leteni simu huku mbele… Lete simu harakaaa… Na ole wako husilete, ole wako uibane, ole wako uifiche, nikikukamataaa…
Nikikukamataa, moja kwa moja utarudi kwenu, Necta utaisikia kwenye TV. Nimesema leteni simuu” Alitufokea, kwa hofu tulikimbizana tulipeleka simu mbele. Alizikusanya zote alitia kwenye kibegi chake.
“Haya japo sikupanga ila nimeamua sasa, wote vaeni sare za shule kisha tunaelekea hospitali kupima mimba. Nitaanza Mimi napima mimba kisha nanyi wote mtapima. Hii shule tangu miaka hiyo hatujawai kuruhusu mwanafunzi mjamzito awepo hapa, hatusomeshi wajawazito, hivyo basi ni lazma mpimwe, na ole wako ukutwe…. Ole wako…. Haya toka nje, toka nje, toka nje nimesema toka njeeeee….”Alitukaripia, ilikuwa ni mshike mshike.
Wale wasiovaa sare walivaa sare, wote tulitolewa nje. Matroni alipita kwenye vyumba
vyote alitoa watu, hata wale ambao walikuwa vimbwetani na madarasani wote waliitwa kisha tulipelekwa ofisini kwa mkuu wa shule. Kama ujuavyo akina matroni wanavyokuwaga wambea wenye roho mbaya, eti alituchongea kwamba hatusomi bali tunafanya umalaya. Zile simu zetu ambazo alitunyang’anya zote alimkabidhi mwalimu mkuu ambaye alikasirika. Kwa kuwa mkuu wetu alikuwa ni mwanamke, nae aliungana na matroni kisha walitupeleka kwenye zahanati ya karibu.
Baada ya kufika huko kwanza tuliandikwa majina ambayo yalipelekwa kwa daktari.
Tuliitwa kwa makundi makundi. Watu walipewa makopo, waliweka mikojo kisha vipimo vilifanyika mbele ya matroni na mkuu wa shule. Baadhi ya wanafunzi wenzangu walianza kuogopa, Mimi wala sikuhofia chochote kwa sababu sikuwahi kuhisi dalili zozote za mimba.
Makundi yalizidi kukatika, hakuna hata mmoja ambaye alikamatwa na ujauzito. Hatimaye
ilifika zamu ya kundi letu ambalo lilikuwa ni kundi la mwisho, tulipewa makopo maalumu tuliambiwa tukaweke mikojo. Tulielekea toilet, kila mmoja na kopo lake, tulijaza mikojo kwenye makopo kisha tuliyapeleka maabara.
Kikundi chetu tulikuwa 10. Aliitwa wa kwanza, alipewa majibu yake, alipona. Wa pili hadi wa 9 wote walipona. Matroni alianza kuhisi aibu, aliumia kuona malengo yake hayajatimia.
Alidhani angekamata wengi wenye mimba ili tuonekane tuna tabia mbaya.
Kumbuka kuwa wenzangu wote walipimwa, sikujua kwanini jina langu lilikuwa la mwisho wakati Mimi ndiye nilikuwa wa kwanza kupeleka kopo la mkojo. Kwakuwa wengi hawakuwa na mimba nilidhani wameamua kunipotezea tu, lakini haikuwa hivyo, Mara nilisikia “GENSUDA MWAKONYOOO!!!” Moyo wangu ulipiga “paaaah” kisha ulitulia, moyoni nilisema “kumekuchaa”, sikujua kwanini nilipata hofu kiasi kile, nilitamani nikimbie niondoke lakini
sikujua kwanini nikimbie, sikuona sababu ya kukimbia, nilizama ndani, moja kwa moja hadi chumba cha daktari, nilikutana na macho ya watu watatu wakiwa wamevimba uso vibaya mno!! Yaani hizo sura zao tu kwa jinsi walivyonitazama nusura nidondoke nife lakini nilijikaza, nilikaa kwenye kiti kisha nilisubiri majibu.
Hawakuniongelesha kitu chochote ila tu nilipewa kopo jingine niliambiwa nikalete mkojo mwingine. Nilifanya kama nilivyoambiwa, nilipeleka mkojo maabara kisha niliambiwa nirudi kwenye chumba cha daktari. Kwa Mara nyingine tulisubiri majibu yangu. Baada ya muda nesi aliingia ndani alimkabidhi dokta kikaratasi cha majibu. Dokta nae alikitazama kisha alimkabidhi matroni na mkuu wa shule, wote watatu walijiridhisha na majibu, walisogeleana walijadiliana jambo flani kisha walinigeukia Mimi, kwa Mara nyingine walinivimbia sura.
SEHEMU YA 28
“Haya Gensu tuambie, hiyo mimba ni ya nani?” Mkuu wa shule alinitwanga swali ambalo liliushtua ntima wangu. Nilihisi labda ananitania au ananipima lakini hakuonyesha utani, alichukua karatasi ya majibu alinipatia. Licha ya kujionea majibu lakini bado sikuamini kama nina mimba, sikujua hiyo mimba imetoka wapi.
“Hivi wewe ina maana hujasikia swali la mkuu wa shule?” Matron nae alinipandia hewani
“Madam mi sielewi chochote, mi sijui kama nina mimba na sijui imetoka wapi”
“Ina maana wewe hujawai kufanya mapenzi si ndiyo? Hichi kimimba chako kinaonyesha ni cha wiki moja au mbili, tuambie ndani ya huu mwezi hujafanya mapenzi na mwanaume yoyote?””
Hapo kwenye kufanya mapenzi hapoo!! Hapo
sasa nilimkumbuka kaka Nasri, na nilikumbuka hakutumia condom, pia ilikuwa siku yangu ya hatari. Niliwaza ina maana kaka Nasri ndiye amenipa mimba? Sasa mbona sikuwahi kuona dalili zozote? Hapana kaka Nasri hakunipa mimba!!! Lakini kama sio yeye nani mwingine??. Niliganda kwa muda mrefu nikiwa naendelea kutafakari. Kuganda kwangu kulifanya waamini ni kweli nilifanya mapenzi na mwanaume. Kwa hasira walinichukua mkukumkuku waliniunganisha na wanafunzi wengine kisha tulirudi shuleni. Wenzangu waliruhusiwa kwenda hostel lakini mimi nilipelekwa ofisini walinikalia kikao cha dharula.
Kikao kilikuwa cha maswali na majibu. Kwanza niliulizwa mimba ni ya nani? Ya mwanafunzi mwenzangu au ya mwanakijiji? Niliwajibu ni ya mwananchi. Waliniambia nimtaje, hapo kwenye kumtaja hapo niliogopa. Niliogopa kwa sababu walitaka wampate muhusika ili afikishwe mahakamani afungwe miaka 30. Japo
nilitamani kaka Nasri afungwe lakini sikumtaja kwa sababu yule mtu ana pesa, anaweza akahonga pesa alafu hasifungwe kisha angenifukuza Mimi na mama nyumbani kwake.
Kwakuwa nilikataa kumtaja muhusika, mwalimu mkuu alimpigia kaka alimuambia afike shuleni haraka. Kikao kilisimanishwa kwa muda, tulisubiri hadi muda ambao kaka aliwasili shuleni kisha tuliendelea kama ifuatavyo;
“Mr Nasri” Mkuu wa shule aliongea “Naam mkuu”
“Mdogo wako ni mjamzito”
“Niniii? Gensu ana mimba? Eti we Gensu una mimba?” Kaka alishtuka, alinigeukia Mimi kisha alinikodolea macho.
“Ndiyo, nimepelekwa hospital nimepimwa nimekutwa nina ujauzito”
“Aah hapana siamini… Una mimba kivipi sasa? Unapataje mimba kipindi hiki cha mitihani? Hiyo
mimba umeipataje pataje mbona mnanichanganya” Aliongea kwa kupaniki utafikiri yeye sio muhusika, kumbe ni yeye.
“Na ndio maana tumekuita ili tusaidiane atuambie mimba kapewa na nani, ili huyo muharibifu wa wanafunzi afikishwe mahakamani haraka. Haiwezekani atupotezee mwanafunzi wetu ambaye tuliamini angetuokoa kimasomaso kitaifa na kimataifa… Hili jambo halikubaliki, ni lazma mtu huyo afungwe jela miaka hata 60” Mkuu wa shule alikazia kwa hasira
Kaka baada ya kusikia jela alitulia, kule kupaniki kote kulikwisha, alikuwa mpolee, alihisi aibu.
Alafu kimya kimya alinikanyaga mguu kisha alinipa ishara nisimtaje muhusika. Nami kwakuwa nilimuheshimu nilitulia kimya japo nilikuwa kwenye wakati mgumu sana, sikujua kama wataniacha niendelee na shule au nitafukuzwa, moyoni nilimwomba Mungu niachwe shuleni hadi nifanye mitihani kisha
niwaachie shule yao.
Licha ya kuambiwa ukweli lakini kaka hakuamini kama kweli nina mimba. Kwa Mara nyingine mwalimu mkuu alimuita nesi ambaye alikuja kunipima pale pale ofisini mbele ya kaka Nasri, na majibu yalikuwa yale yale kwamba nina mimba. Kaka alizidi kuchanganyikiwa, japo yeye ndiye aliinipa mimba lakini alionekana kutopenda jambo hilo.
“Kwahiyo mkuu tunafanyaje sasa?”
“Tunafanyaje kuhusu nini?.. Hapa hakuna shule tena, hii sio shule ya wajawazito. Laiti kama angekuwa amesajiliwa tungemuacha afanye mitihani, lakini hajasajiliwa, hatuwezi kumsajili mjamzito… Unataka awe anatutapikia hapa?” Kauli ya mwalimu mkuu ilifanya nianze kutoa machozi, pale pale kwenye kikao nililia kwa sauti.
“Mkuu yaani mimba tu ndo hasifanye mitihani? Mimi nipo tayari kulipa faini yoyote, naombeni
SEHEMU YA 29
mnisaidie jamani ndugu zangu” Kaka alianza kuomba huruma za walimu
“Hakuna faini kwa wajawazito kuendelea na masomo!! Ina maana wewe hujui mwanafunzi wa kike akipata mimba shuleni hatoendelea na masomo!! Hulijui hilo suala?”
“Najua lakini “
“Hakuna cha lakini, mchukue mdogo wako muondoke hapa. Hatuhitaji rushwa wala marupurupu, hata kama yuko vizuri darasani hatuwezi kuendelea nae. Kwakuwa alichagua mapenzi basi mwache akatumikie mahaba.
Nitawapa barua maalumu ya Gensu kufutwa shule, Kikao hiki kimekwisha”
Uso wangu ulilowana machozi tepwetepwe, nilishikwa machozi ya hasira lakini ndio hivyo sikuwa na la kufanya. Nilibaki nalia tu kama mtoto. Kaka alinitazama alinionea huruma, alijuta kwanini alinibaka. Kwa mara nyingine alitoa pesa nyingi kisha aliziweka mezani kwa
mwalimu mkuu, alimuomba azipokee kisha aniruhusu niendelee na masomo lakini ilishindikana. Mwalimu aliandika barua, iligongwa mihuri kama yote kisha walimkabidhi kaka. Matroni aliitwa, alinichukua alinipeleka hosteli, niliambiwa nikusanye vitu vyangu vyote, baada ya kukusanya nilirudishwa kwa kaka.
Kinyonge tulizama kwenye gari kisha tulirudi nyumbani!! Na huo ndio ulikuwa mwisho wa ndoto zangu za elimu ya darasani.
*****
Baada ya kufika nyumbani mama alitaka kujua kwanini nimerudi. Kaka Nasri alimdanganya mama kwamba shule yetu imefungiwa na serikali kwa kushindwa kulipa kodi. Pia alimdanganya kwamba wanafunzi wote tumerudishwa nyumbani. Mama alikodoa macho alishangaa, alishindwa kuelewa, na kwakuwa yeye sio msomi aliamua kukubali tu.
Kitendo cha kaka kumdanganya mama kilizidi kunipa hasira, nilitamani nisema ukweli ila nilipata wasiwasi, niliamua kuacha kwanza.
Nikiwa nyumbani mara nyingi nilikuwa najifungia chumbani kwangu tu. Sikutaka kuwa karibu na mtu yeyote, ni mara chache sana nilikuwa naongea na mama na Rahabu. Mimi na kaka tulinuniana. Mimi ndiye nilimnunia yeye, nilimnunia kwa kiwango cha lami.
Kila siku nikiwa chumbani nilikuwa najiuliza hatma yangu ya maisha ni ipi? Kama shule imegoma, je mimi nitakuwa nani huko mbele?… Licha ya kwamba kaka Nasri ndiye alikuwa ananisomesha lakini kutokana na hasira niliona liwalo na liwe, kama kunifukuza na anifukuze, moyoni nilipanga nimpeleke mahakamani nikamtuhumu kwa kitendo chake cha kunibaka, kunipa mimba na kuniharibia masomo.
SEHEMU YA 30
Nilipanga nifanye jambo hilo kimya kimya pasipo mtu yeyote kujua. Usiku mida ya saa 1 nilitoka kimya kimya pasipo mtu yeyote kujua,
nilielekea kituo cha polisi. Baada ya dakika chache nilifika kituoni, kabla hata sijaingia ndani nilishtuka kuiona gari ya kaka ikipaki pembeni yangu.
“Wewe… we Gensu… Wewe ebu njoo kwanza… mbona unaingia kituo cha polisi? Unaenda kufanya nini huko?” Aliniuliza kwa sauti ya hofu na wasiwasi lakini sikumjibu, niliganda tu nikiwa natazama pembeni, usoni nilipambwa na hasira kama zote
“Alafu wewe isije ikawa unataka kunifunga jela” Aliendelea kuongea akiwa kwenye gari.
Nilimtazama kwa jicho kali niliona ananipigia makelele tu. Pia niliona ananicheleweshea mambo yangu, kwa hasira niligeuka mbele kisha nilipiga hatua za haraka kuelekea ndani. Nae fasta alikurupuka kutoka kwenye gari kisha alinikimbilia, alinishika mkono alinizuia nisiende kokote.
“Gensu, ina maana ni kweli unataka kunifunga
jela?”
“Kwanini usifungwe? Wewe si umeniharibia masomo? Kwani sheria inasemaje kuhusu wanaume wanaowapa mimba wanafunzi?”
“Lakini mimi ndiye nilikupeleka shule”
“Kwahiyo ulinipeleka ili unipe mimba si ndio?”
“Hapana, mimba imetokea tu kimakosa. Na uzuri ni kwamba sijaikataa, wewe zaa, mimi nitailea”
“Kwani nani alikuambia kuwa nataka kuzaa muda huu? Alafu ni lini nilikuambia kuwa nataka kuzaa na wewe?”
“Ina maana bado hunipendi?… Alafu wewe, hivi ni nani amekupa kiburi cha kubishana na mimi?. Unakumbuka nilikowatoa wewe na mama yako? Mnalala kwangu bure, vyakula bure, ada nilikulipia mimi, sasa hicho kiburi unakitoa wapi? Au unataka niwafukuze pale kwangu?”
“Kama ulitusaidia ili ututese, hatutokubali.
Kama ulitusaidia ili ututumie utakavyo, hatutokubali. Kwanza umeniharibia masomo, umenipa mimba isiyotarajiwa, tena bora ningeipata kwa uzembe wangu, lakini umenipa kwa kunibaka. Sawa wewe tufukuze nyumbani kwako, kwakuwa Mungu alituumba alituleta duniani; yeye ndiye atajua sisi waja wake tutaishi wapi na tutakula nini. Lakini kamwe sitokuacha salama, nitakufungulia kesi mbili, ya kunipa mimba na kunibaka.” Niliongea kwa kujiamini kiasi kwamba kaka Nasri alianza kuniogopa. Siku zote alizoea kuniona mpole, aliniendesha atakavyo akidhani kwamba mimi ni mnyonge sana, hakujua kwamba ni umaskini tu ndio ulifanya nionekane mnyonge, lakini kiuhalisia mimi ni mwanamke wa NGUVU.
Nilimsukuma pembeni kisha kwa mara nyingine nilipiga hatua kuelekea ndani ya kituo cha polisi.
Mwisho wa season 01,
Endelea na season 02