MWANAUME WA NDOTO ZANGU
SEHEMU YA 21
“Niniii? Kaka Nasri unasemaje?” Nilishtuka, niliogopa!!
“Naomba futa kabisa habari za ukaka, mimi na
wewe sio dam moja. Hivyo basi kutokana na uzuri wako nimejikuta nina hisia nzito juu yako, ghafla tu nimejikuta nakupenda. Na natamani hata wewe unipende tuwe wapenzi, vipi unanielewa lakini?” Aliongea kwa msisitizo, alionyesha kuwa hatanii. Na kabla sijamjibu chochote tayari alinikumbatia kisha alisogeza mdomo wake karibu na mdomo wangu, alitaka kunipiga busu la kikubwa lakini nilikwepesha mdomo!! Alikasirika, alichukia kuona nimekataa busu lake.
“Kwahiyo hutaki au?”
“Kaka mbona leo sikuelewi? Hivi ni wewe kweli?”
“Ni mimi, na hizi ni akili zangu, najitambua na nipo siriazi. Gensu nakupenda, naomba uwe mpenzi wangu. Sawa?”
“Hapana, mi siko tayari. Mimi siwezi kuwa na mahusiano na wewe. Hata kama sisi sio damu moja lakini mimi sifanani kabisa kuwa mpenzi
wako, hufanani kuwa mpenzi wangu, kila mtu hapa mtaani anajua kabisa kuwa wewe ni kaka yangu mlezi, nakuheshimu. Kuhusu uzuri mbona wanawake wazuri wapo wengi sana, wamenizidi mimi kwa kiasi kikubwa sana, pesa unazo, unashindwaje kuwapata wanawake wa type yako?”
“Ooh kwahiyo unanifundisha kumpenda mtu? Unanichagulia mwanamke? We Gensu kumbe unaongea sana, alafu unajidai hujui kuwa unaishi kwenye nyumba yangu si ndiyo?”
“Kwahiyo unanifanyia hayo yote kwakuwa naishi kwenye nyumba yako?”
“Hapana, ila nakupenda tu. Kwanza naomba tuache kupiga kelele, unanipenda au hunipendi? Unakubali kufanya au hukubali?”
“Mimi sikupendi kimapenzi, nakupenda kama kaka. Pia siwezi kukubali kufanya mapenzi na wewe, wewe sio mwanaume sahihi kwangu ambaye naweza kumvulia nguo, haupo ndotoni
kwangu na wala hufanani na ndoto zangu”
“Asante!! Vizuri sana. Naona tumeingia kwenye vita. Sasa nisikilize. Kama hutaki kunipenda, kama hutaki kukubali tufanye mapenzi, kuanzia leo hii sitohusika kwenye shida zako zozote.
Husije ukaniomba kitu chochote. Maisha yako ya shuleni usinishirikishe. Kuhusu ada utamtafuta wa kukulipia. Na naomba tusiongeleshane. Tukikutana njiani tupishane kama hatujuani. Kwa ufupi ni kwamba tusijuane wala tusitambuane”
Kaka alimaliza kuongea maneno yake, aliongea akiwa amepaniki. Kwa hasira kali alisimama kisha aliondoka chumbani kwangu pasipo kugeuka nyuma. Nilibaki nimeduwaa tu nikiwa namshangaa. Hadi kufikia hapo sikujua kama maamuzi yangu yalikuwa ni sahihi au bora ningekubali tu. Pia sikujua kama amemaanisha kweli au ni hasira zake tu. Niliamua kupotezea, kwakuwa hakutufukuza kwenye nyumba yake niliona haina noma, nilienda kufunga mlango
kisha nilirudi kitandani nililala usingizi wa mawazo.
****
Siku iliyofuata niliamka saa 12 alfajiri, nilioga, nilivaa sare zangu kisha nilichukua begi langu kwaajili ya kuondoka kuelekea shuleni. Kabla sijaondoka nilipaswa niwaage watu ambao ningewaacha nyumbani. Yaani ile natoka nje tu nilikutana na kaka Nasri akiwa amevaa suti zake, mkononi alishika begi na funguo za gari, bila shaka alikuwa anaelekea kazini. Kwa kawaida yeye ndiye alitakiwa anichukue anipeleke shule, yeye ndiye aliniita nyumbani na aliniambia atanirudisha shule, lakini kutokana na ugomvi wetu hakuonyesha dalili zozote za kwamba atanipeleka shuleni au atanipa lift ya gari yake.
Hata salamu hatukupeana. Alionekana kuwa bize kwelikweli, nilitamani nimsimamishe
SEHEMU YA 22
angalau nimuage lakini niliogopa, niliogopa kwa sababu alisema nisimsemeshe. Basi bwana niliganda nikiwa namtazama, alitoka nje alipotea machoni, nami taratibu nilielekea chumbani kwa mama, nilimuaga; alinitakia masomo mema, alinipa baraka zote ambazo nilizipokea kwa mikono miwili. Baada ya kumuaga mama nilienda kumuaga Rahabu, nae alinitakia masomo mema kisha niliondoka nilielekea stendi kuu ya mabasi; nilizama kwenye gari nilirudi shuleni.
***
Nilifika shuleni nilikuta wanafunzi wamejaa, hasa hasa wa kidato cha nne na cha pili.
Wengineo walikuwa kwenye likizo ya mwezi wa sita. Siku hiyo hosteli sikulala usingizi mzuri, bado niliwaza mabadiliko ya kaka Nasri, sikujua amepatwa na nini kiasi cha kunitaka kimapenzi. Nilikumbuka yale maneno yake kwamba
tusijuane wala tusitafutane, niliona haiwezekani kugombana na mtu muhimu kama yeye.
Nilishika simu nilijaribu kumpigia lakini aliniblock, niliazima simu ya rafiki yangu kisha nilijaribu kumpigia, hapo sasa alipokea ila alikata simu baada ya kugundua ni mimi.
Nilimtumia meseji kuwa anisamehe lakini hakunijibu, niliamua kulala.
Siku iliyofuata vipindi vilianza. Licha ya kwamba ilikuwa ngumu lakini nilijitahidi kusahau ugomvi wangu na kaka. Niliamua kujisahaulisha ili niwe bize na masomo nisije nikafeli kama kipindi kile. Na kwa wakati huo sikuwa na shida ya pesa, kwenye simu nilibakiwa na pesa za matumizi zaidi ya elfu 50. Na ukicheki matumizi yangu wala hayakuwa makubwa sana. Hivyo basi sikuwa na mashaka kuhusu pesa ya matumizi, niliamua kufocus na masomo.
Licha ya kwamba yeye ndiye tegemezi langu lakini niliamini kuwa hakuwa sahihi kunitaka kimapenzi. Pia niliamini ipo siku atajitafakari
atagundua kuwa alikuwa hanitendei haki, niliamini ipo siku kaka atanipigia kisha tutamaliza tofauti zetu lakini haikuwa hivyo!! Siku zilikatika, wiki ziliondoka, miezi ilikatika lakini kaka hakuonyesha dalili za kunipigia wala kunitafuta.
****
Balaa lilianza pale ambapo fedha zangu za matumizi zilikata, mkononi nilibakiwa na elfu 5 tu. Na ukicheki mimi ni mtoto wa kike ni lazma niwe na pesa kwaajili ya kununua mahitaji ya lazma kama vile pedi, nguo za ndani, peni, madaftari, sabuni na kadhalika. Hapo sasa kwa mara nyingine nilijaribu kumpigia kaka lakini nilikuta bado ameniblock, nilimpigia mama nilimuuliza kama ana akiba yoyote lakini hakuwa na chochote, aliniambia nimuombe kaka pasipo kujua kwamba mimi na kaka hatuelewani.
Sikutaka kuuumiza sana kichwa changu, kama shida nilizoea tangu utoto wangu. Nilichukua ile elfu 5 yote nilienda kununua pedi ambazo ndo za muhimu zaidi. Baada ya hapo niliendelea kupiga shule bila wasiwasi wowote. Kuhusu sabuni niligongea za marafiki zangu, dawa za meno niliomba kwa marafiki, na kwakuwa wengi walinipenda hivyo basi sikuwa na shida ndogondogo, marafiki zangu walikuwa msaada tosha kwangu.
Nakumbuka ulibakia mwezi mmoja tuingie kwenye usajili wa mwisho wa majina ya wanafunzi watakaofanya mtihani wa mwisho wa kidato cha nne. Sasa siku hiyo nikiwa najisomea kwenye kimbweta, nikiwa sina hili wala lile mara mwanafunzi mwenzangu alikuja kuniita aliniambia naitwa na muhasibu wa shule. Nilishtuka kidogo kwa sababu tangu nijiunge na shule hiyo sikuwahi kuitwa na muhasibu hata siku moja. Kwa wasiwasi nilisimama kisha nilifunga vitabu vyangu, niliondoka nilielekea
ofisini kwa muhasibu, nilimkuta akinisubiri; “Hujambo Gensu?”
“Sijambo shikamoo”
“Marahaba. Nimekuita kwa sababu una madeni ya aina mbili”
“Nina madeni?”
“Yeah. Unadaiwa laki 6.5 ambazo ni pesa za ada na hostel. Sasa kwa mujibu wa sheria za shule unapaswa umalize madeni hayo ili tuweze kukusajili kwaajili ya mtihani wa mwisho. Sio wewe tu, hii ni kwa wote ambao bado hamjamaliza ada.”
“Lakini mimi sihusiki na ada, kaka ndiye anahusika na aliniambia kuwa amemaliza”
“Hakumaliza, ila alitoa ahadi kwamba atamaliza. Tumejaribu kuwasiliana nae namba yake inaita tu, hapokei simu. Hivyo basi tunakupa ruhusa
ya siku 5, leo hii ondoka nenda kafuate ada nyumbani kisha urudi haraka ili uje kuendelea
na maandalizi ya mtihani. Ukishindwa kufanya hivyo hutosajiliwa.”
SEHEMU YA 23
Muhasibu nae alianza kunichanganya. Alinipa kibali cha kuondoka pamoja na barua ya kudaiwa ada ambayo nilitakiwa nikampe kaka. Kwa unyonge niliondoka nikiwa nimevurugwa kuanzia kusini hadi kaskazini, sikujua jambo hilo litapokelewaje na kaka ambaye tuligombana. Siku ile ile sikutaka kupoteza muda, nilimfuata mwalimu mkuu nilimueleza kuwa kaka hapatikani kwenye simu, nilimuomba aniazime pesa ya nauli, alinipatia kisha nilirudi nyumbani.
****
Baada ya kufika nyumbani kama kawaida mama alinishangaa, safari hii hata Rahabu
alishangaa. Waliniuliza kulikoni? Sikutaka kuwaficha, niliwaeleza ukweli kuwa nimefuata ada. Kwakuwa wao sio watoa pesa waliniambia nimsubiri kaka ambaye muda huo alikuwa kazini. Kama kawaida yao waliniandalia chakula, nilikula kisha waliweka movie. Wao walifurahia movie lakini mimi niliwaza ada.
Masaa yalikwenda haraka haraka hadi yalinitisha. Niliwaza kaka akirudi atanisikiliza kweli? Nikiwa naendelea kutafakari mara ghafla mzee mzima alitia timu. Nilidhani angeshtuka kuniona lakini hakushtuka wala hakunishagaa, aliniona kama wa jana tu. Hakusalimia mtu, alipitiliza moja kwa moja hadi chumbani kwake. Alibadili nguo kisha alitoka akiwa ameshika funguo mkononi, nilitamani nimsimamishe ila niliogopa. Alipitiliza alitoka nje alizama kwenye gari yake kisha aliondoka.
Nilijipa moyo kwamba usiku akirudi nitamuambia kuhusu ada. Kwa bahati mbaya siku hiyo hakurudi nyumbani, alilala huko huko.
Siku iliyofuata hakurudi tena nyumbani alilala huko huko. Hata siku ya tatu hakurudi nyumbani, alilala huko huko na sikujua ni wapi. Nilizidi kuchangayikiwa kwa sababu zilibaki siku mbili ruhusa iishe, pia nilihisi kaka ananifanya hivyo makusudi kwa sababu alijua kuwa nimefuata ada
Siku ya nne ilikuwa ni jumamosi, alirudi nyumbani asubuhi, alimuita Rahabu kisha alimwambia wakasaidiane kutoa mizigo kwenye gari, walienda. Muda huo mama alikuwa chumbani kwake, mimi nilikuwa nawatazama kaka na Rahabu ambao waliendelea kubeba michele, matunda, vyombo na kadhalika. Nilitamani nami nikasaidie lakini niliogopa kwa sababu sikuitwa.
Baada ya kumaliza kubebelea mizigo walienda kukaa sebuleni kwenye sofa, Rahabu alimuandalia kaka chai kisha alimkaribisha.
“Kaka angu kipenzi karibu chaiii” aliongea
kiutani utani tu akiwa anachekacheka
“Ooh asante sana Rahabu wangu, naona unanipenda sana mimi, na unanijali sana” Kaka alimwambia Rahabu
“Ndiyo ni lazma nikupende, yaani wewe ni zaidi ya kila kitu kwangu, umenitoa mbali, umenileta hapa nakula raha tu ah ah ah” Rahabu alijibu akiwa bado anacheka kwa furaha
“Wow! Huwa natamani sana kupendwa. Na siku zote mtu anayenipenda huwa namuonyesha mapenzi mazitoo…. Sasa Rahabu unajua nini”
“Hata sijui kaka”
“Kwakuwa unanipenda naomba nikupe hii laki 1. Elfu 50 utamtumia mama nyumbani, alafu elfu 50 ni yako utaenda kununua nguo madukani”
“Kaka hii laki yote ni yangu? Umenipa bure au ni mshahara?”
“Hiyo nimekupa bure kwakuwa unanipenda… Na mwezi huu mshahara wako utapanda kwa
sababu unanipenda sana”
“Asante sana kaka… Mungu akubariki sana… Asante sanaa” Rahabu alifurahi, na kwakuwa walizoeana walikumbatiana kwa furaha kisha Rahabu alipeleka pesa chumbani kwake.
Sasa baada ya Rahabu kuelekea chumbani, kaka alinitazama kwa jicho la dharau na hasira, alinifyonya kwa jeuri kisha aliendelea kula.
Niliumia sana, pia nilipata wivu wa ajabu kuona anazidi kumpendelea Rahabu pekeyake. Nilijua anafanya hayo yote ili kunikomoa mimi. Japo ilikuwa ngumu kushindana nae lakini sikuwa tayari kuuza utu na uchi wangu kwaajili ya pesa zake.
Siku hiyo kaka hakuondoka nyumbani, muda wote alikaa sebuleni akichezea laptop yake. Kuna muda alimuita Rahabu kisha alimfundisha namna ya kutumia laptop. Alifanya yote hayo ili kunirusha roho tu, na ni kweli roho yangu
ilikuwa juu juu, niliumia na nilipata tabu sana. Niliwaza na kuwazua niliona yeye ni mtu wa muhimu, iwe isiwe ni lazma nijishushe ili aweze kusikiliza shida zangu. Taratibu nilipiga hatua niliwafuata pale mezani, nilikaa kwenye kiti kisha nilimtazama kaka usoni.
“Kaka…” Nilimuita lakini hakuitika
“Kaka nimekuletea hii barua yako imetoka shuleni, nimeambiwa ni barua ya kufuata ada. Mwezi ujao tunafanya usajili wa mwisho na uhakiki wa majina ya wanafunzi watakaofanya mtihani, nimeambiwa kama sitomaliza madeni sitosajiriwa.” Niliongea nikiwa namkabidhi barua lakini hakupokea. Mara alichukua simu yake kisha alipokea licha ya kwamba hakupigiwa;
“Haloo… Eeh Dullah… Nije hapo muda huu? Kuna ishu gani tena mzee?…… Ooh sawa nakuja nakujaaa… Nakuja chap tuu..” Kaka alimaliza kuongea, alisimama kisha alitoka nje
SEHEMU YA 24
alizama kwenye gari yake aliondoka. Nilibaki nimeganda nikiwa nimeshikilia barua yangu, mambo yalikuwa magumu. Rahabu nae alibaki ananishangaa tu, hakujua kinachoendelea.
****
Hatimaye siku ya tano ilifika. Ilikuwa ni siku ya mwisho ya ruhusa ambayo nilipewa. Na ukicheki kaka hakulala nyumbani, sijui alikuwa wapi. Niliazima simu ya Rahabu nilijaribu kumpigia kaka lakini alipogundua ni mimi alikata simu, hata Rahabu alishangaa, aliniuliza kulikoni nilimwambia hakuna tatizo. Mama aliniuliza kama nishapewa ada nilimjibu bado, alishangaa lakini hakuhoji sana kwa sababu sisi sote tunaishi nyumbani kwa kaka Nasri, tusingeweza kumkoromea au kumlalamikia kwa kitu chochote.
Niliendelea kuvumilia, nilimsubiri arudi. Alafu sasa alivyo na makusudi alirudi usiku saa sita. Alitukuta mimi na Rahabu tukicheki movie.
Mimi sio kwamba nilikuwa bize na movie bali nilikuwa namsubiri yeye ili anipe pesa ya ada.
“Rahabu vipi, upo powa?” alimsalimia Rahabu pekee
“Ndiyo kaka, sijui wewe. Tangu nilivyokuona jana, nilikumiss sana”
“Wacha wee, hata mi nilikumiss mnoo!! Na ndio maana nimekuletea zawadi ya saa, hereni na mkufu. Njoo uchukue”
Rahabu alikimbia alimfuata kaka, walipeana zawadi zao kisha waliachana, kaka alielekea chumbani kwake, Rahabu alirudi kwenye sofa kisha aliniambia nimvalishe hereni na mkufu. Nilimvisha alipendeza mno, alisahau habari za movie, alianza kujizungusha ndani ya nyumba akiwa anacheza na kuimba, aisee niliumia kuanzia kwenye nyama hadi kwenye mapafu!! Nilitamani mimi ndo ningekuwa Rahabu, alafu yeye awe mimi ili tupokezane maumivu.
Tulikaa sebuleni hadi saa saba usiku, sio
SEHEMU YA 25
kawaida yangu ila nilivumilia tu ili nipunguze mawazo. Rahabu alichoka alienda kulala. Nami nilizima Tv nilielekea chumbani kwangu. Nililala kidogo kisha nilikumbuka shule, nilikumbuka ada, nilikumbuka bila kusajiliwa sitofanya NECTA. Hapo sasa niliona liwalo na liwe, nilimfuata kaka chumbani kwake nilimgongea mlango, baada ya sekunde chache alifungua mlango, na baada ya kutambua kuwa ni mimi alifunga mlango chap chap kisha alirudi kulala. Nilijaribu kumgongea tena lakini hakufungua.
Nilikaa mlangoni kwake hadi saa nane usiku nikiwa nalia kwa kwikwi, nilijaribu kumpigia simu yake nilikuta bado kaniblock. Nilirudi chumbani kwangu niliendelea kulia kimya kimya bila kutoa sauti wala bila kupiga kelele. Nilijuta na nilitamani bora hasingenipeleka shule kuliko mambo aliyokuwa ananifanyia.
Nilikuwa nalia nikiwa nahesabu masaa. Ilipita saa 8, saa 9, yalibaki masaa mawili kukuche nirudi shule, na ukicheki sikuwa na nauli wala
ada, hapo sasa kilio kiliongezeka.
Sasa nikiwa naendelea kulia, mida ya saa 10 usiku mlango wa chumba changu uligongwa. Nilihisi labda ni Rahabu amekuja kuniamsha tufanye usafi. Nilienda kufungua mlango nilishtuka kukutana na kaka akiwa amevaaa boksa pekee, mkononi alishika pesa nyingi.
Moja kwa moja alipita ndani, alifunga mlango kisha alinivuta hadi kitandani, alinimwaga juu ya godoro alafu alinipandia kwa juu. Kama kawaida yake alichukua rimoti aliwasha Tv kisha aliongeza sauti.
“Haya niambie unanipenda au hunipendi?” aliniuliza lakini sikujibu, niliendelea kulia
“Hutaki kujibu si ndio?… Nimekuja na ada hizi hapa, najua unadaiwa laki 6.5, hapa nimekuja na laki 8. Ukikubali tufanye nakupa zote. Je unakubali au hutaki?” Aliongea akiwa ananionyesha maburungutu ya pesa.
“Ooh una kiburi, ngoja niondoke zangu, na
mwezi huu wote sitolala hapa nyumbani, simu zangu zote nazima.. Kwaheri..” Aliongea akiwa anajitoa kwenye mwili wangu.
“Hapana kaka usiondoke” Nilimzuia, hapo sasa alitulia
INAENDELEA