MWANAUME WA NDOTO ZANGU
SEHEMU YA 16
“Ni yangu kaka, kwani hukuona kuwa ni Mimi? Sura mbona ni yangu, ni Mimi yule” nilimsisitiza
“Mmh siamini…. Wewe ndo upo vile kwa sasa?… Siamini…. Kama kweli yule ni wewe basi kesho asubuhi naomba urudi nyumbani tukuone kwanza”
“Kwa sasa kurudi nyumbani haiwezekani, zimebaki Siku Nne tu likizo iishe. Pia si
unakumbuka ulinisisitiza nisirudi nyumbani?… Sitoweza kurudi ila yule wa kwenye picha ni Mimi”
“Gensu ni kweli nilitaka usirudi nyumbani ila naomba uje kuna maagizo nataka nikupe, pia kuna pesa nataka uje uzichukue, mama yako na Rahabu wanataka wakuone. Kesho uje asubuhi alafu kesho kutwa nitakurudisha shuleni”
“Kaka naomba hayo maelekezo unipe kwenye simu, pesa nitumie kwenye simu. Waambie mama na Rahabu kwamba bado miezi michache wataniona.. Kwa sasa sitoweza kurudi”
“Mbona sikuhizi umekuwa mbishi? Unanibishia hata Mimi? Sawa haina shida…”
“Samahani kaka, nisamehe nilikosea… Kesho mapema narudi nyumbani…. Hallo… Halloo kaka..”
Simu ilikatwa kitambo, bila shaka alikasirika. Nilijaribu kumpigia lakini simu iliita bila
kupokelewa, nilipiga zaidi ya Mara 10 lakini hakupokea, Mara namba yake haikupatikana. Nilichanganyikiwa, nilivurugwa, usingizi wote ulikwisha, fasta nilimpigia Rahabu kisha nilimwambia ampelekee simu kaka Nasri, Rahabu alifanya hivyo lakini hakubahatika kumpata kaka ambaye alijifungia mlango kwa ndani.
Mawazo yangu yaliwaza mbali, niliukumbuka msaada wake, alafu eti hasitishe misaada yake aisee sjjui itakuwaje. Katika maisha yangu sikuwahi kuwaza kwamba kuna siku nitamkosea kaka kiasi cha kunizimia simu, pia kwa Mara ya kwanza nilishuhudia namna Kaka Nasri alivyo na hasira, Siku hiyo nilijuta kwanini nilikataa ombi lake la kutaka Mimi nirudi nyumbani.
Sikuishia kwa Rahabu tu, niliamua kumpigia mama kisha nilimwambia nataka kuongea na kaka Nasri. Mama alienda kumgongea kaka mlango, kaka alitoka nje lakini alimwambia
mama kuwa hatoweza kuongea na simu kwasababu anajisikia vibaya. Plan ya pili nayo iligoma. Siku hiyo sikulala tena, nilikaa kitandani niliomba kukuche haraka ili nirudi nyumbani.
Kutokana na kuvurugwa nilianza kupanga nguo zangu usiku ule ule. Nilichukua vinguo vichache niliweka kwenye begi, simu yangu nilishika mkononi, SAA 12 asubuhi nilimfuata matroni nilimpa taarifa kuwa narudi nyumbani, kwakuwa ilikuwa likizo matroni hakushangaa, ila tu alinisisitiza likizo ikiisha niwepo shuleni kwa wakati. Bila kupoteza muda nilibeba kibegi changu nilielekea stendi ya mabasi, nilizama kwenye gari nilirudi nyumbani.
****
Baada ya kitambo kirefu hatimaye mwana mpotevu nilirudi nyumbani nikiwa ndani ya sare zangu za shule. Nyumbani nilimkuta mama na Rahabu wawili tu. Kwa furaha Rahabu alinikimbilia alikuja kunikumbatia, alinipiga mabusu kisha alinipokea mizigo aliipeleka
chumbani kwangu.
Muda wote mama alikuwa ananishangaa tu, kwanza alishtuka kuniona, hakutegemea kama ningerudi nyumbani. Nikiwa natabasam nilimfuata nilikaa pembeni yake, nilimsalimia lakini hakuitikia, aliniuliza kwanini nimerudi; nilimjibu kuwa kaka Nasri ameniita ili anipe maagizo ya shule. Baada ya jibu hilo mama aliridhika kwa sababu alimuheshimu na alimuamini sana kaka Nasri, hakuwa na wasiwasi nae.
Mgeni nililetewa chakula nilikula, tulipiga stori nyingi, vicheko vingi, tulitazama movie, Masaa nayo yalikatika lakini kaka Nasri hakuonekana. Nilitamani ajue kuwa nimefika ili hasira zake ziishe, nilitamani anione ili minuno yake iishe, sikupenda namna alivyonichukia.
Kwa kawaida huwa anamaliza kazi saa 10 jioni lakini siku hiyo hadi inafika saa 12 hakuonekana, saa moja usiku hatukumuona. Muda wa
SEHEMU YA 17
chakula cha usiku ulifika lakini alikuwa bado hajarudi. Tulikula chakula kisha tulihamia kwenye movie, mida ya saa tatu usiku kaka Nasri aliingia, mkononi alibeba begi lake la kazi.
Miimi nilikuwa wa kwanza kusimama, kwa furaha nilikimbia nilienda kumpokea begi lakini alikataa, alinipita kama hanijui vile, alitusalimia kwa pamoja kisha moja kwa moja alielekea chumbani kwake!! Nilibaki nimeganda kama sanam, hata mama na Rahabu walishangaa. Ni Mimi tu ndiye nilijua kwanini kaka alikuwa kwenye hali ile, mama na Rahabu wala hawakuelewa chochote, walihisi labda kaka amevurugwa huko huko kazini kwake.
Taratibu kinyonge nilipiga hatua nilienda kukaa kwenye sofa, tuliendelea kutazama movie.
Moyoni niliwaza lazma kaka atakuja sebuleni kunisalimia na kula chakula lakini huwezi amini, hadi inafika saa nne usiku kaka hakutoka nje.
Mama alituaga alienda kulala, nilibaki Mimi na Rahabu mpenda movie, anapenda movie kama
nini, akianzaga kutazama anaweza kesha hadi asubuhi.
Mwenzangu alikuwa bize na season za kikorea, Mimi nilimuwaza kaka Nasri, nilijiuliza atanichukia hadi lini, matokeo yake ni yapi?
Kwamba atanikomesha au ana mpango gani na Mimi? Kila nikikumbuka misaada yake kwangu nilijikuta natoa machozi.
“We mwanafunzi mbona unalia my wangu”
Rahabu aliniuliza “Kichwa kinaniuma”
“Tatizo hujazoea kutazama movie kwa mida mrefu, nenda kalale tu”
“Wala usijali, nitalala tu.. Alafu Rahabu si unajua kaka bado hajala? Nenda kamgongee mlango kamwambie chakula kinapoa” Niliamua kutumia ujanja huo ili kaka atoke nje. Kwakuwa Rahabu ni Dada wa kazi alinielewa, alisimama alielekea chumbani kwa kaka, alimgongea mlango kisha mlango ulifunguliwa, alimuambia kaka kuhusu
kwenda sebuleni kula chakula; Kaka alijibu kuwa ameshiba!!! Dili langu liligoma.
Kwakuwa kaka aligoma kutoka nje nami niliamua kumuaga Rahabu kisha nilienda kulala. Nikiwa chumbani kwangu sikupata usingizi, nilimtumia meseji kaka kwamba nimerudi ili anipe maelekezo na pesa lakini hakunijibu.
Nilimtumia meseji anisamehe sitorudia lakini hakunijibu. Nilijaribu kumpigia simu lakini hakupokea, Mara alinizimia, nilikosa mwendo. Japo sikuwa na usingizi lakini nilijilazimisha hadi nililala.
Siku iliyofuata niliamka mapema ili nipate nafasi ya kuonana na kaka kabla hajaenda kazini. Ajabu ni kwamba gari yake sikuiona, nilienda chumbani kwake nilikuta kufuri ikining’inia mlangoni. Niliwaza tangu lini kaka Nasri akaenda kazini saa 11? Sikupata majibu. Siku za likizo nazo zilizidi kuondoka, zilibaki siku 2 tu.
Niliishi kwa mawazo sana, sikujua kaka atanisamehe lini. Masaa yalikatika, asubuhi ilipita, mchana uliondoka. Siku hiyo kaka alirudi mapema, alileta zawadi nyingi, unga, mchele na mengineyo. Aliongea na mama, aliongea na Rahabu, walichekeshana, walitaniana, lakini ubaya ni kwamba hakuongea na Mimi, alinitazama tu kidogo kisha alinipotezea, alielekea chumbani kwake.
Hata usiku muda wa chakula tulikula pamoja lakini hakudiriki kunitazama usoni, na hata akihitaji kitu alimuagiza Rahabu tu, Mimi hakutaka kuniagiza chochote. Nilijisikia vibaya kwa sababu hata kama Rahabu ni Dada wa kazi sio lazma atumwe pekeake, niliona kama anampendelea vile. Nilijisikia wivu, niliumia kuona ananitenga, hakunishirikisha kwa lolote, kwa ufupi ni kwamba alinishusha thamani zote!! Aliniona kama takataka tu.
*****
Hatimaye ilibaki siku moja likizo iishe, Siku hiyo niliona haiwezekani, nilipanga iwe isiwe ni lazma niongee nae kabla sijarudi shuleni.
Kwanza nilimtumia meseji kuwa imebaki Siku moja likizo iishe, hakunijibu. Japo sikuwai kwenda ofisini kwake lakini kwa Mara ya kwanza nilifunga safari hadi kazini kwake, licha ya kwamba nilimkuta lakini hakunipokea wala hakunikaribisha.
“Kaka Nasri…” Nilimuita lakini alikuwa bize na kazi, macho kwenye kompyupta tu
“Kaka Nasri Naomba nisamehe. Mimi sio kwamba nilikataa ombi lako, ila lengo langu lilikuwa zuri tu. Nilitaka nibaki shuleni nijisomee ili niweze kutimiza ahadi ambayo nilikuahidi. Pia kwakuwa likizo ni fupi niliona hata nikirudi nyumbani sitopata muda mwingi wa kufurahi na nyinyi”
“Kwani Mimi nilikuita ili uje tufurahi?” Kwa Mara
ya kwanza alinijibu japo kwa hasira, alafu hakunitazama wala nini, aliendelea kupiga kazi.
“Hapana, basi nisamehe kaka… Sitorudia tena.”
Niliongea kwa upole
“Wewe si ushakuwa mkubwa. Nakuona tu sikuhizi umekuwa mzuri kuanzia juu hadi chini, una akili nyingi, unaongoza mitihani, bila shaka umeshafanikiwa kimaisha ndio maana hutaki kunisikiliza tena”
“Hapana kaka mi nakusikiliza, nisamehe”
“Una kiburi sana sikuhizi, najua wanaume wameanza kukuharibu, Sawa. We endekeza hao wanaume, fanya tu huo ushetani”
“Hapana kaka, Mimi sina mwanaume yoyote, na naapa kwa Mungu sijawai kujihusisha na mwanaume yeyote tangu nizaliwe”
“Ah we sio kweli!! Una uhakika tangu uzaliwe??…..” Hapo sasa alinijibu akiwa ananitazama, aliacha kufanya kazi. Macho yake
yalianza kuutalii mwili wangu kuanzia juu hadi chini, nilijisikia aibu, nilishusha macho chini.
SEHEMU YA 18
“Kwahiyo kesho unarudi shule?”
“Ndiyo. Nimekuja kukuaga, pia nimejua unipe maagizo ambayo ulisema”
“Usijali, wewe rudi nyumbani, tutaagana huko huko nyumbani, na hayo maagizo nitakupa baadae nikirudi nyumbani”
“Sawa kaka, mi naondoka” Nilijibu nikiwa nasimama, bila kupoteza muda niliondoka nilirudi nyumbani, nilimuacha yeye akiwa ananitazama tu.
*****
Nikiwa nyumbani nilipanga vitu vyangu kwenye begi kwaajili ya safari. Nilipanga niondoke
asubuhi na mapema ili niwahi kufika shuleni. Muda wote nilikuwa nawaza namna ambavyo nitakamilisha ndoto yangu ya kuwa Tanzania one katika matokeo ya kidato cha Nne, niliona mitihani ya Necta iko mbali sana. Pia nilifurahi sana kumaliza tofauti zangu na Kaka Nasri, nilimsubiri kwa hamu ili nisikie atanipa maelekezo gani. Moyoni niliwaza atanipa maelekezo ya namna ya kufaulu vizuri.
Basi bwana masaa yalisogea, Giza liliingia, tulikula chakula cha usiku, tuliongea story mbalimbali, usiku huo nilideka kwa mama kabla sijaelekea shule, mama alichoka alituaga alienda kulala. Sebuleni nilibaki Mimi na Rahabu chamuvi; tulitaniana, tulikimbizana, tulicheza kwa Mara ya mwisho kabla sijaenda shule, hadi inafika saa nne na nusu usiku kaka Nasri hakutokea. Siku hiyo Rahabu alichoka mapema, aliniaga alienda kulala, hatimaye nilibaki mwenyewe, niliwaza nikalale au nimsubiri kaka? Kwakuwa aliniambia tutaongea usiku niliamua
kumsubiri, nilikaa kwenye sofa nilitazama movie, lakini hadi inafika saa tano kaka hakutokea.
Sikujua yupo wapi, na ubaya ni kwamba kila nikimpigia simu hakupokea. Japo sio kawaida yake ila nilihisi labda amepata dharula hatorudi nyumbani, kwakuwa nami nilichoka niliamua kuzima TV kisha nilienda kulala. Nililala usingizi nzuri husio na stress, niliwaza kufaulu tu mtoto wa kike mie.
***
SAA 8 USIKU.
Usingizi wangu ulikuwa mtamu, sikuelewa kilichokuwa kinaendelea duniani, nililala FOFOFO!!! Sasa nikiwa nimelala ghafla kwa mbali nilisikia mlango wa chumba changu ukigongwa. Sio kawaida kugongewa mlango muda kama huo, kutokana na uchovu niliendelea kulala. Mlango uliendelea kugongwa, alafu mgongaji aligonga taratibu, aligonga
kidogo kisha alitulia akisikilizia kama nitamfungulia mlango lakini sikwenda kufungua.
“Nani tena huyo usiku wote huu? Ni Mama au ni Rahabu?? ….. Kaka Nasri hakulala hapa… Kama hakulala sasa huyo anayegonga ni nani? Alafu mbona haongei? Mbona hasemi? Ukorofi. ” niliwaza kimya kimya nikiwa najifunua shuka, nilikaa kitandani kisha niliendelea kusikiliza, kwa namna ambavyo alikuwa anagonga mlango ilifikia hatua nilianza kuogopa, nilihisi labda nagongewa na majini au wachawi.
Taratibu nilishuka chini kisha nilinyata hadi mlangoni, nilimuuliza yeye nani lakini hakujibu. Nilimuuliza yeye ni mama lakini hakujibu, nilimuuliza kama yeye ni Rahabu lakini hakujibu. Niliita kaka…kaka…kaka Nasri… Lakini sikujibiwa. Hapo sasa nilizidi kupata hofu, kitendo cha mtu huyo kigonga mlango pasipo kuongea kiliniongezea woga. Nilitulia nilipiga mahesabu nifungue mlango au niuache? Niliona bora nifungue, kama ni mchawi basi aniroge.
Nilishika kitasa nilifungua mlango, yaani ile nafungua tu; macho yangu yalikutana na sura ya kaka, kwanza alikuwa kitambi wazi, alivaa kibukta tu, aisee nilishtuka!!!. Nilibaki mdomo wazi, niliganda kama zombi vile. Usoni alikuwa anatabasam tu. Muda huo nilikuwa nimevaa vinguo vya kulalia tu, kaka alinitazama kuanzia kusini hadi kaskazini, kwa macho yangu mawili nilimuona akimeza mate, sikujua ni mate ya nini.
Sasa nikiwa bado nimezubaa, mwenzangu alitazama huku na huko hakuona mtu yeyote, fasta alizama ndani chumbani kwangu, aliniacha nikiwa nimeganda pale pale mlangoni. Nilishindwa kuelewa, kaka alianza kunichanganya, kaka alianza kuniumiza kichwa, kaka alianza kunivuruga, nilijiuliza kwanini ameingia chumbani kwangu? Na kwanini aingie akiwa na kibukta? Anataka nini?. Kutokana na hofu sikufunga mlango, niligeuka nyuma nilimuona akiwa amekaa kwenye godoro langu, usoni alikuwa anatabasam tu. Kwa sauti ya
chini aliniambia nifunge mlango kisha nimfuate.
Kuhusu kumfuata wala sikuogopa sana, ila utata ulikuwa kwenye kufunga mlango. Niliwaza nifunge mlango ili iweje? Kwani kuna habari gani?. Hata hivyo kwakuwa yeye ni kaka yangu mlezi, ananisomesha, naishi kwake, sikuona sababu ya kumuhofia sana. Taratibu nilifunga mlango kisha nilimfuata pale alipo, sikutaka kukaa nae kitandani, nilisimama pembeni.
“Vipi mbona umesimama? Kaa kitandani” aliniambia akiwa bado anatabasam.
“Sawa, lakini nimeshangaa sana leo umeingia chumbani kwangu. Sio kawaida yako, pia umeingia usiku sana… Kwani kuna tatizo?” niliongea nikiwa nakaa kitandan
SEHEMU YA 19
“Hakuna tatizo. Ila nimekuja tu kukuaga ili nikutakie masomo mema. Pia tulikubaliana kwamba nikirudi nitakupa maagizo, ndio maana nimekuja chumbani kwako ili nikupe maagizo”
Japo maelezo yake yalieleweka lakini
sikuyaelewa. Kichwani nilitamani nimuulize maswali mengi lakini mdomo ulikuwa mzito. Na laiti kama hasingekuwa mwenye nyumba basi ningemfukuza, nilishindwa kumuhoji kwa sababu yeye ndiye kila kitu kwenye nyumba yake. Tulitulia kwa sekunde chache pasipo kuongea kitu chochote.Nilitamani anipe hayo maagizo kisha aondoke lakini hakufanya hivyo. Mimi nilikuwa natazama pembeni ukutani, yeye alikuwa ananitazama mimi. Mara alichukua remote kisha aliwasha Tv, aliongeza sauti, sikujua kwanini anafanya hivyo, na sikuwa na uwezo wa kumuuliza chochote.
Baada ya kuwasha Tv alinyanyuka pale alipokaa kisha alikuja kukaa karibu yangu, baadhi ya sehemu za miili yetu ziligusana. Niliogopa, niliogopa, niliogopa mimi hadi sio poa.
Nilitamani nimkimbie ila sikujua kwanini nimkimbie, bado nilimuona kama kaka yangu tu ambaye hawezi kunifanyia baya lolote.
Sasa baada ya kunisogelea alinyosha mkono
SEHEMU YA 20
wake mmoja kisha alishika mapaja yangu ambayo yalijazia nyama kama zote, hapo sasa nilimeza mate ya woga kisha nilianza kutetemeka kwa hofu, japo sikumzuia lakini sikupenda kitendo hicho. Hakuishia hapo, alipandisha mkono wake kutoka mapajani, kiunoni, kwenye mbavu hadi kifuani, alitulia akiwa ananitazama usoni, aliniona nimekasirika lakini hakujali, alitabasam tu. Mara ghafla alishika embe langu la kwanza, alitaka kubinya lakini nilimzuia.
“Kaka..”nilimuita
“Una uhakika mimi ni kaka yako?” Aliniuliza
“Siku zote nimekuwa nikikuita kaka na uliitika, kwanini leo unakataa?”
“Sijakataa lakini najua kuwa uliniita kwa heshma tu, ila ukweli ni kwamba mimi sio kaka yako. Sina undugu na wewe, na mama yako wala na Rahabu. Nyie wote nawasaidia tu…
Sasa huo ukaka ukaka wa muda wote unatoka
wapi?”
“Sawa nimekuelewa. Basi naomba unipe hayo maagizo kisha uende chumbani kwako, mimi nahisi usingizi, nataka kulala ili kesho niwahi shule, nisije nikapewa adhabu”
“Sina maagizo yoyote. Pia eti unaniambia niende chumbani kwangu, kwani hiki chumba ni changu au chako?”
Duh! Nilikosa pozi. Swali lake lilieleweka lakini majibu nilikosa. Nilitaka aondoke aende chumbani kwake nilisahau kuwa yeye ndiye mwenye nyumba. Mimi sio kwamba nilimfukuza, ila tu dalili ambazo alianza kunionyesha ziliniogopesha. Niliendelea kutulia tu, nilikaa kwa tahadhari kubwa sana.
“Gensu” Aliniita kwa sauti ndogo akiwa anazidi kunisogelea
“Abe-eeh”
“Usiogope Gensu. Hivi ni kweli hujawai
kukutana na mwanaume?”
“Ndiyo sijawahi na sitowahi hadi nikiolewa” “Ooh vizuri sana… Ila nikuambie kitu Gensu?” “Kitu gani?”
“Leo utawahi”
“Sijakuelewa, una maana gani?” “We si umesema hujawai kusex?”
“Ndiyo na sitofanya hadi nikihitimu masomo ya chuo kisha nikiolewa”
“Aisee pole sana, una mawazo ya mbali mno. Sasa nisikilize, leo hii ndio itakuwa siku yako ya kwanza kufanya mapenzi”
INAENDELEA