MWANAUME WA NDOTO ZANGU
SEHEMU YA 01
Baada ya mateso ya muda mrefu walinichukua walinipeleka katikati ya msitu mnene wenye giza totoro. Mbele yangu alisimama mwanaume jangiri mwenye roho ya kikatili. Na nyuma yangu alisimama mwanamke shetani mwenye roho ya kigaidi. Wote wawili walishika mapanga wakitaka kunitoa roho ili waishi maisha yao kwa uhuru. Sikuwakosea kitu chochote ila sikujua kwanini walitaka kuniangamiza. Nikiwa nalia kwa uchungu niliwaza nitakwepaje kifo kibaya ambacho kilikuwa mbele yangu, sikupata majibu, niliamua kufumba macho kisha nilimuachia Mungu!!
Nilitulia tulii, kama kuniua na waniue.
Nao baada ya kuona siwezi kujitetea walinicheka kwa dharau kisha walinyosha mapanga yao juu, walinisogelea taratibu wakitaka kunikata mapanga shingoni na kichwani. Lakini kabla hawajatimiza lengo lao mara kukasikika “” Paaah Paah” fumba na kufumbua wote wawili walitupa mapanga chini kisha walikimbia wakiwa wanachechemea.
Sikuamini kilichotokea, nilitamani kuona Mungu ameniletea miujiza gani. Niligeuka nyuma; Macho yangu yalikutana na mwanaume mzuri akiwa ameshikilia bastola mkononi. Licha ya kwamba nilikuwa hatarini lakini nilitoa tabasam la furaha!!
Mwanaume yule alinichukua, alinipeleka nyumbani kwake, alinichua kwa maji ya moto, alinipa dawa iliyoniondoa maumivu, aliniandalia maji ya kuoga kisha alinikaribisha bafuni. Hata baada ya kuoga nilikuta kaniandalia chakula kizuri. Muda mwingi alikuwa akinitazama kwa huruma kisha alitabasam kwa mapozi,
aliniambia kuwa mimi ni mwanamke mzuri kuliko warembo wote Tanzania. Licha ya kunisifia sana lakini hakuniweka wazi kwamba ananipenda, yeye alinionyesha ishara tu ambazo zilionyesha kuwa ana mapenzi ya dhati juu yangu.
Ghafla nilizama kwake, japo sikumfahamu kiundani lakini nilimuona kama nuru mpya na mwezi wa maisha yangu, pale pale nilimthibitisha kwenye moyo wangu. Sikutamani hata ahangaike kunitongoza, nilijitongozesha mwenyewe na nilimruhusu anioe haraka iwezekanavyo. Ajabu ni kwamba hakuwa na haraka, aliniambia kuwa mapenzi mazuri hayakurupushwi, ndoa bora hailazimishwi!!
Mtoto wa kike nilitulia. Alionyesha sio mwanaume wa tamaa kama hawa waliopo. Alinionyesha chumba cha kulala kisha tuliagana, kila mmoja alienda kulala chumbani kwake.
Sasa majira ya saa 10 usiku nikiwa nimelala, ghafla nilihisi mikono ya mtu ikiupapasa mwili
wangu. Mikono ilianzia kifuani hadi katikati ya uvungu wa nyeti zangu. Kabla sijakaa sawa aliushusha mdomo wake moja kwa moja hadi kwenye lips zangu, aliuzamisha ulimi kisha aliyanyonya mate yangu!! Taratibu nilifumbua macho, ooh woow, fantastic!! Macho yangu yalikutana na mwanaume wangu mzuri aliyenikomboa toka mikononi mwa Wayahudi. Nilishindwa kumzuia, nilimuacha afanye anachotaka! Nae wala hakuvunga, sijui hata alifanyaje ila ghafla nilishangaa kiungo chake kikipenya katikati ya kiungo changu, palepale nilifumba na kuyafumbua macho yangu kwa utamu wa penzi tamu! Sasa wakati nataka nimkumbatie ili anizidishie utamu, ghafla nilishtuka toka usingizini, nilishangaa kuona nimelala pekeangu, pia nilijikojolea mkojo mzito, nilitazama saa ilikuwa ni saa nae usiku, niliumia sana baada ya kugundua ilikuwa ni NDOTO.
Sikutaka kulala tena, nilisubiri kupambazuke
kisha nilitoka nje nilianza kufanya usafi. Nilifagia uwanja nikiwa naiwaza ile ndoto. Sikujua kama ni ya kweli au ya uongo! Kutokana na mateso ya ndotoni niliogopa isije ikawa ni kweli. Lakini kuna muda nilimkumbuka yule mwanaume wa ndotoni, nilibaki natabasam tu, nilitamani iwe kweli. Nilimaliza kufanya usafi kisha nilielekea kwenye vibarua vyangu vya kutafuta ridhki ili mimi na mama yangu tuingize chochote tumboni.
*****
Katika maisha yangu sitosahau siku baba yangu anafariki dunia, alituacha mimi na mama yangu tukiwa hatuna urithi wowote zaidi ya kijumba cha kawaida tu. Sitosahau kwa sababu
yeye ndiye tulikuwa tunamtegemea kwa kila kitu. Japo hakuwa na kazi ya maana lakini alihakikisha tunakula, tunakuwa na furaha, tunapata mahitaji ya msingi na kubwa zaidi
SEHEMU YA 02
alihakikisha binti yake napata elimu ya sekondari pasipo shida yoyote.
Kwa kipindi hicho nilikuwa kidato cha tatu nikiwa na miaka 17. Shuleni nilipendwa sana kwa sababu darasani nilikuwa vizuri, nilikuwa msafi, nilikuwa na roho safi, niliwapenda wenzangu na kubwa zaidi nilijaariwa uzuri wa sura, rangi, umbo na mwili. Nyumbani nilikuwa mtoto pekee na tegemezi, wazazi waliniandaa kielimu ili nije kuwa mkombozi wa familia. Na ndio maana darasani nilipambana kiasi cha kushika nafasi ya kwanza au ya 2 ili tu nijitengenezee mazingira mazuri ya kufanikiwa kielimu.
Sio wazazi tu, hata walimu wenyewe waliamini kuwa mimi ndiye ningeweza kuwa mkombozi wa shule yetu ambayo ilikuwa pembeni mwa mji wa tanga katika kijiji kiitwacho POTWE. Kwa hakika niliishi kwa furaha sana, sikuwa na wasiwasi wowote, niliamini kuwa ipo siku nitakuwa na kazi kubwa, nitakuwa mtu mkubwa
kiheshima, kifedha na kimafanikio kwa ujumla.
Lakini KIFO CHA BABA ndicho kilikatiza ndoto zangu zote. Kwanza maisha yalikuwa magumu nyumbani. Chakula kilipatikana kwa shida, mama yangu alianza kusumbuliwa na maradhi mbalimbali, japo shule yetu ilikuwa ni ya kata lakini nilianza kusuasua, nilishindwa hata kutoa vimichango vidogo vidogo shuleni, upepo wa kuongoza kimasomo nao ulianza kubadilika, mara nilishika nafasi ya 5, mara ya 12, mara ya 30 na mwisho nilikuwa wa mwisho.
Hayo yote niliyavumilia ila utata ulianza pale ambapo mama yangu alikosa angalau hata thumuni ya kununulia mboga, majirani ambao walikuwa wanatusaidia walisitisha misaada kwa sababu walituchoka na walizichoka shida zetu. Kutokana na mama yangu kuumwa mara kwa mara ilibidi mimi niingie kwenye majukumu ya kulea familia, hapo sasa NILIACHA SHULE
kisha niliingia mitaani kutafuta vibarua mbalimbali ambavyo vilinipa vijisenti.
Sikuchagua kazi, mie mitaro nilichimba, kokoto niliuza, michanga nilichimba sana, nililima sana mashamba ya watu ili tu nipate chochote kitu.
****
Kwa majina naitwa Gensuda Pinsloto Mwakonyo, mtoto pekee wa marehemu mzee Pinsloto Mwakonyo. Ukoo wetu wa kina Mwakonyo una ndugu wengi ambao hadi leo hii sijuagi umuhimu wa ukoo ni upi. Kama baba yangu kafariki, kwanini nipate shida wakati ndugu zangu wengi wamebaki duuniani?. Baba wakubwa wapo, baba wadogo wapo, mashangazi wapo, mabinamu wapo, tena wengine wana maisha mazuri tu, sasa kama wao na mimi ni ukoo mmoja kwanini hatusaidiani??. Hayo ni baadhi ya maswali ambayo nilikuwa najiuliza mara kwa mara
pasipo majibu yoyote
****
Maisha ya dhiki yaliendelea, sikujali tena kuhusu kuutunza mwili wangu, japo asili ya uzuri wangu haikupotea lakini nuru yangu ilikwisha kabisa, sifa zangu ziliondoka, wanaume wengi ambao mwanzo walikuwa wananitamani walianza kunidharau wakiniita MCHAFU KUOGA. Ilikuwa ni haki yao kuniita hivyo kwa sababu muda wote nilikuwa rafu rafu tu, gauni moja niliweza kuvaa kwa wiki moja au zaidi, ni mara chache sana nilibadili nguo za kuvaa. Hata hivyo sikujali sana, kitu pekee ambacho nilikiwaza ni kutafuta vijisenti ili mimi na mama yangu tuishi.
“Ina maana ndoto zangu ndo basi tena!! Sina jipya tena, kwamba nitakufa maskini, nitaishia kuolewa tu hapa kijijini?” Nilijiuliza swali nikiwa nalia, muda huo nilikuwa katikati ya shamba la
mpunga nikivuna mpunga wa watu.
“Na inawezekana hata kuolewa kwenyewe unaweza husiolewe. Wewe ulikuwa zamani wakati unasoma, aisee enzi zile ulikuwa CHIPULA!!. Sahizi akutake nani? mtu unatembea pekupeku kama MRISHO MPOTO, miguu imejaa magaga kama unasugua GAGA, eti nawe unataka uolewe, awe thubutuu” Ilikuwa ni sauti ya dharau kutoka kwa kibarua mwenzangu ambaye wote tulikuwa tunafanya kibarua cha kuvuna mpunga.
Maneno yake yalifanya niache kutoa machozi, nilijitazama kuanzia chini hadi juu, mimi mwenyewe nilikubali kuwa sifai kuolewa, sina vigezo na hakuna mwanaume wa kunitaka kutokana na kufubaa kwangu. Nilijiona mwanamke hasiye na thamani hata kidogo, kuna muda niliwaza bora nife tu nikapumzike mbinguni au motoni, lakini nilimkumbuka mama yangu, niliwaza kama nikifa mama yangu atabaki na nani? Kama mimi tu wananidharau
kwa kiasi hiki, je mama yangu watamdharau kwa kiasi gani?. Taratibu niliokota KIKWAKWA kisha niliendelea kuvuna mpunga.
*****
Nakumbuka ilikuwa ni siku ya Christmass, sikukuu ya kuzaliwa kwa mtoto Yesu. Kwa kawaida siku hiyo huwa ni ya kusherehekea, watu huwa wanapendeza sana, wanapika vyakula bomba, mapilau kama yote, ni furaha kwenda mbele. Niliamka asubuhi nikiwa sina hata mia mbovu mfukoni, nilimfuata mama nilimuuliza kama ana akiba yoyote lakini hakuwa na chochote.
Kimya kimya nilitoka nje nilielekea mtaani kusaka mishe mishe za pesa, njiani nilikutana na watu wakiwa wamependeza, kila mmoja alivaa nguo mpya, wengine wakienda kanisani na wengine wakijishaua tu. Mimi nilinyosha moja kwa moja hadi kwa matajiri wa kijijini.
Nilianza nyumba ya kwanza niliomba kazi lakini nilikosa, nyumba ya pili nilikosa, nyumba ya tatu, ya nne, ya tano na sita kote nilikosa. Niliamua kubadili mada, niliwaomba wanikopeshe alafu siku wakiwa na kazi nitawafanyia bure lakini waligoma! Hadi inafika mchana sikuambulia chochote.
Nilirudi nyumbani nikiwa FOKORO (yaani empty kabisa). Nilimkuta mama akiwa amekaa pembeni ya jiko, alifurahi kuniona akidhani nimepata pesa kumbe maskini ya Mungu sikuwa na lolote. Nilipitiliza moja kwa moja hadi chumbani kwangu; nilijilaza kitandani kisha nilianza kulia kimya kimya, niliumia kuona tunaishi kwa kubahatisha sana. Kwa mbali nilisikia harufu za pilau kutoka kwa majirani, miziki ilianza kuunguruma, mara nilisikia makelele watu wakishangilia, wengine waligonganisha vyupa vya soda, aisee nilipandwa na hasira, nilitoka chumbani nilimfuata mama jikoni.
SEHEMU YA 03
“Kwahiyo mama muda wote umejikalisha hapo jikoni, unasubiri miujiza gani itendeke?”
“Mh Mwanngu, ina maana leo hatupiki?”
“Utapika nini sasa? Haya pika” Nilijikuta nimeropoka kwa hasira, nilimnunia mama yangu
“Kwani huko ulikokwenda tangu asubuhi hujapata kapesa kokote?”
“Nani anipe pesa?? Na ukicheki leo ni sikukuu, hakuna kibarua chochote.”
“Mh” Mama aliguna
“Ndo hivyo. Hivi mama na wewe ilikuaje uliolewa na baba maskini?”
“Baba yako tulikutana enzi za ujana, kipindi hicho hakuwa na pesa za kiviile, tulianzisha mahusiano kwa makubaliano kwamba tutasaka maisha na pesa nyingi tukiwa pamoja kwenye ndoa kisha tutafanikiwa pamoja”
“Huo ndo ujinga sasa. Yaani mama katika kosa
ulifanya ni kukubali kuolewa na baba ambaye hakuwa na pesa, hakuwa na maisha mazuri wala hakufanikiwa kwa lolote. Ebu fikiria maisha yako yote ya ndoa huna mali zozote zaidi ya hiki kijumba cha hovyo. Yani sisi wanawake sijui tunakwama wapi!! Unakubalije kuolewa na mwanaume hasiye na pesa??
Unakubalije kuolewa na mwanaume hasiye na kazi yenye kipato kinachoeleweka? Unakubalije kuolewa na mwanaume ambaye yupo kwenye hatua za utafutaji??. Mwanaume pekee ambaye anapaswa kukuoa ni yule ambaye tayari ametafuta pesa, anazo, ana maisha mazuri, yule ambaye ukiwa nae kwenye mahusiano hutopata shida yoyote. Sio unaolewa na mwanaume ambaye hana kitu, eti anakuambia
mtatafuta pesa pamoja, je hizo pesa zikigoma?? Eti anakuambia mtatafuta maisha pamoja, je hayo maisha yakigoma??”
“Nisamehe mwanangu, kama nilifanya makosa basi ndo hivyo, Kwa sasa nakuombea tu wewe,
Mungu abariki njia zako zote, azifungue zisiwe na vikwazo”
“Amina!! Na nakuhakikishia sitofanya makosa kuolewa na nyapala yeyote hasiye na tumbo wala mgongo. Bora nife na usichana wangu kuliko kuharibu mwili wangu kwa punguani ambaye hana pesa. Ebu fikiria kwa ugumu huu wa maisha alafu niolewe na KOLO lisilo na kitu, hiyo itakuwa ndoa au UTOPOLO??”
Mtoto wa kike niliwaka, ilifikia hatua hata mama yangu aliona aibu, alihisi kuwa alifanya makosa makubwa kuolewa na baba maskini. Kiukweli nilimaindi sana, kwa sababu laiti kama baba angekuwa na pesa basi angetuachia pesa.
Kama angekuwa na ajira angetuachia mirathi. Au kama angekuwa na biashara basi angetuachia hizo biashara. Lakini hakuwa na utajiri wowote ndio maana ametuachia dhiki, sasa baba wa hivyo wa kazi gani??.
Masaa yalipita mimi na mama tukiwa tunatazamana tu, tulishinda ndani siku nzima, huko nje watu waliendelea kusherekea sikukuu lakini sisi tuliugulia njaa tu. Kwa kuogopa aibu za majirani nilisubiri giza liingie kisha nilitoka kimya kimya nilielekea shambani, nilichuma kisamvu kisha nilirudi nyumbani, tulipika ugali, tulikula na kulala.
*****
Siku zilikatika, wiki iliyeyuka, hatimaye mwaka mpya uliingia, tulidhani kwamba mwaka mpya ungekuwa wa neema nyingi kwetu lakini haikuwa hivyo. Mwaka ulianza vibaya sana!!
Siku ya mwaka mpya kabla hata hapajakucha tuliamshwa kwa kelele nyingi kutoka kwa watu wasiojulikana. Mimi na mama tulitoka nje tulikutana na kikundi cha watu watatu wakiwa wameshika makaratasi mikononi. Watu hao walitanguzana na mwenyekiti na mtendaji wa kata.
“Ndugu waheshimiwa mwenyekiti na afsa mtendaji, kama nilivyosema kwamba marehemu alifariki akiwa na madeni yangu mawili. Kwanza huu uwanja nilimuuzia mimi kwa shilingi laki 1, pesa hakunilipa, aliahidi atanipa ila hadi anakufa tulikuwa tunazungushana tu. Deni la pili ni pesa za kujenga nyumba, marehemu nilimkopesha milion 2 ajenge nyumba hii lakini hadi leo hii hajanirudishia hata senti tano.Tulikopeshana mbele ya mkewe, mwenyekiti wa mtaa wa kipindi hicho pamoja na mashahidi wawili ambao nimekuja nao, tulikubaliana kwamba deni litalipwa na familia ya mkopaji. Sasa kwakuwa mkopaji amekufa, naomba familia yake inilipe deni langu muda huu”
“Ninii?? We kibaba unasemaje?”
“We binti kaa kimyaa! Kwanza nani kibaba?
Hauna heshima kwa wazee wako?”
“Samahani!! Eti mama hayo madeni ni ya kweli au wanatuonea tu kwakuwa baba amefariki?”
“Ni kweli mwanangu, hayo yote ni ya kweli”
“Daah jamani, nilidhani enzi zenu mlijitutumua kujenga hii nyumba kwa mikono yenu kumbe nyumba yenyewe ya mkopo, sasa hayo madeni tutalipaje sisi?”
“Hilo mi halinihusu, kama vipi uzeni nyumba mnipe changu”
Ilikuwa kama utani vile, yaani kama masihara. Nilichukua makaratasi yao niliyasoma kwa umakini nilikuta makubaliano ya kuuziana uwanja na kukopeshana pesa ya ujenzi. Sahihi ya mama na baba, sahihi ya muuzaji/ mkopeshaji na mashahidi wake, sahihi na muhuri wa mwenyekiti wa mtaa. Japo mimi sio mtaalamu wa masuala ya sheria lakini nilikubaliana na nyaraka hizo.
Suala lilibaki moja tu, wapi tutapata pesa za kulipa deni?? Na ukicheki nyumba yetu haikuwa na sofa, tv wala kifaa chochote cha thamani!!
Pia niliwaza kama tutauza nyumba tutaishi wapi?? Nilipata muhao wa kufa mtu.
Wale watu walitupatia mwezi mmoja kisha waliondoka. Pia walituachia masharti kwamba kama tutashindwa kulipa deni hilo basi nyumba yetu itapigwa mnada. Nilimtazama mama nilimuona akilia tu, sikutaka kumsumbua wala kumuuliza wapi tutapata pesa kwa sababu nilitambua kuwa hana uwezo wowote. Taratibu niligeuka nyuma nilielekea ndani chumbani nililala. Mama naye alielekea chumbani kwake alilala. Siku yetu iliharibika kuanzia mapema sana, mwaka mpya ulikuwa mchungu.
SEHEMU YA 04
Kutokana na ugumu wa maisha hatukuwa na mipango yoyote ya kusaka pesa ili kulipa deni.
Na wahenga walisema Usiku wa deni haukawii kukucha. Hatimaye mwezi mmoja ulitimia.
Mwenye chake alikuja kudai madeni yake, alitukuta tukiwa tumefulia vibaya mno.
Tulidhani angetusamehe lakini haikuwa hivyo, aliondoka kisha alirudi akiwa na polisi na wanasheria, nyumba yetu ilipigwa mnada kwa shillingi million 2.5, sisi hatukuambulia hata senti 1. Tuliambiwa tuondoe vitu vya ndani kisha tutafute mahala pa kuviweka. Hatukuwa na namna, tuliondoa vitu vyetu vichache tulivitoa nje, nyumba ilifungwa kisha wao waliondoka zao.
Ilikuwa ni aibu lakini tulivumilia tu. Nilipiga mahesabu tuelekee wapi? Mama alishauri tuelekee kwa mamdogo ambaye alikuwa anaishi kijiji cha pili. Tulianza kubebelea vitu tulivipeleka kwa mamdogo ambaye alitupokea vizuri tu. Siku za mwanzoni tuliishi vizuri, tulisaidiana kwa kazi mbalimbali ikiwemo za shambani, lakini kadri siku zilivyozidi kusonga
mbele mambo yalianza kubadilika.
Tukiwepo nyumbani vyakula havikupikwa, ila mimi na mama tukiondoka huku nyuma wenzetu walipika kisha walikula kimya kimya. Pia mamdogo alianza kutulimisha kwenye shamba lake, yeye na familia yake walibaki nyumbani alafu mimi na mama tulikuwa kama vibarua wa mashamba yake, malipo yetu yalikuwa ni chakula cha usiku na sehemu ya kulala tu. Mchana tulishindia maembe na matunda ya huko huko shambani. Nakumbuka siku hiyo mimi na mama tulichelewa kutoka shamba, tulirudi nyumbani usiku tulikuta wenye nyumba wakiwa wametukalia kikao wakitusengenya, muda huo walikuwa chumbani kwao, maneno yao yalisikika kama ifuatavyo;
“Wakimaliza lile shamba la mahindi itabidi waende shamba la karanga, wakitoka kwenye karanga watatulimia viazi, huu mwaka tumebahatika kupata vibarua wasio na malipo, kwa raha zetu ah ah ah” ilisikika sauti ya
mamdogo.
“Alafu yule dada yako ile homa yake ya vidonda vya tumbo ilipona au?” Bamdogo alimuuliza mkewe
“Ipone wapi? Si ndio maana namlaza njaa ili afe na hayo madonda yake”
“Alafu mke wangu nina wazo” “Lipi hilo baba Tumi?”
“Mganga alikuambia utoe ndugu yako mmoja ili huu mwaka tuvune mazao mengi, sasa kwanini usimtoe dada yako?”
“Ah ah ah baba Tumi nawe unakuwa kama mtoto, hivi ina maana bado hujajua kwanini nimekubali waishi hapa kwangu? We subiri kuna mambo naweka sawa, soon mtu atapewa sumu, litakufa jitu”
“Ndomana nakupenda sana we mwanamke, una akili hadi una akili tenaa!!!” Bamdogo aliongea kwa furaha kisha walicheka kwa pamoja.
Niligeuza macho pembeni nilimtazama mama nilimuona akitoa machozi. Mama yangu yeye akawiagi kulia, yani ukimsema kidogo tu analia, ukimuuzi analia, hata ukimkorofisha huwa analia. Sikutaka tuingie ndani wasije wakatushtukia, nilimshika mama mkono kisha nilimvuta kuelekea pembeni, licha ya kwamba ilikuwa ni usiku lakini tuliamua kurudi tulikotoka, tulirudi shambani tulifikia kwenye banda ambalo lilijengwa kwaajili ya vibarua na walinzi wa ngedere.
“Kwahiyo hapo sasa mama yangu tunafanyaje? Mana mdogo wako kashasema kwamba anataka kukutilia sumu” Niliongea nikiwa namtazama mama usoni, nilisogeza mkono machoni kisha nilimfuta machozi
“Mi naona tuwe tunaishi huku huku shambani, hatuwezi kufa na njaa kwa sababu matunda yapo, mihogo ipo, maji yapo, moto upo. Itabidi kesho tukachukue vyombo vyetu na magodoro yetu tuhamie huku huku, kama anataka kuniua
basi aniue nikiwa huku shambani kuliko kunitilia sumu ndani ya nyumba yake”
“Sawa mama, leo tuvumilie ila kesho mambo yatakaa sawa”
Kama kawaida usiku huo tulikula mihogo na maembe, tulitandika kanga zetu chini, tulimuomba Mungu wetu atulinde kisha tulilala. Uzuri ni kwamba kule shambani hakukuwa na wanyama wakali, Pia kwakuwa kilikuwa ni kipindi cha kilimo baadhi ya watu wengine nao walikuwa wanalala kule kule mashambani kwenye vibanda vyao.
*****
Siku iliyofuata kama tulivyokubaliana tulielekea kwa mamdogo ambaye alidai kuwa alikuwa anatutafuta sana, Usoni alionyesha kuchanganyikiwa kwakuwa hatukulala nyumbani kwake. Alituuliza tulilala wapi?
Nilimdanganya kwamba tuliamua kulala
SEHEMU YA 05
shambani ili tusipate shida ya kwenda na kurudi shamba kila siku.
“Pia mimi na Mama tumefikiria tumeona bora tukalale kule kule shambani ili tukalime muda wote kwa haraka, pia ili tukalinde mashamba yasiharibiwe na nyani na ngedere. Kwahiyo leo tumekuja hapa kuchukua baadhi ya vyombo na godoro kisha tunarudi shamba”
“Unasemaje wewe Gensu? Muhamie shambani?? Jamani mbona mnautani nyie wapenzi wangu, yaani mkakae shambani mkashambuliwe na wadudu wakati hapa kwangu pako wazi kwaajili yenu? Hapana kwakweli, hamuwezi kwenda kuishi huko”
“Mamdogo jamani si unajua mashamba yako yapo mengi? Na sisi ndo vibarua wako, sasa tukizembea unadhani yataisha yale mashamba?”
“Hata kama yapo mengi lakini hamuwezi kwenda, nyie kaeni hapa hapa. Pia nyie sio
vibarua wangu, nyie na mimi ni familia, kwa sasa tumeshakuwa kitu kimoja, hata yale mashamba ni kama yetu tu. Chakula kikipatikana tunakula pamoja…. Kwanza vipi mmekula kweli? Ngoja niwapikie chakula kizuri mle mshibe” Aliongea kwa furaha kisha aligeuka alipiga hatua akitaka kuelekea jikoni
“Shangazi tushakula, huna haja ya kwenda kupika. Sisi jana tulikula ugali, leo asubuhi tumekunywa uji na makande…” Niliamua kudanganya kwa sababu nilijua lengo lake, niliogopa hasije akapika alafu akaweka dawa zake ambazo alikusudia.
“Jana mlikula ugali? Kwa unga gani?… Alafu hayo makande mlikula bila chumvi au? Mlipikia wapi? Kwa maana vyombo vyote viko huku, sasa nyie mlipikaje pikaje?” Shangazi aliganda akitushangaa
Nilimdanganya kuwa baadhi ya vitu tulinunua, ila ukweli ni kwamba vitu vingi kama chumvi,
sufuria, tulikuwa tunaazima kwa wenzetu wa mabanda mengine ya kule shambani.
Mamdogo aligunaguna kisha alikubali kishingo upande. Mambo mengine yote alikubali ila kuhusu sisi kwenda kuishi shambani hilo suala alikataa katakata.
Kwakuwa tulitambua lengo lake wala hatukupata shida. Tuliamua kutulia kimya, tulipotezea kama tumekubali vile. Mchana tulisubiri muda ambao alienda kununua mboga magengeni, mimi bila kupoteza muda niliingia chumbani kwangu nilichukua kigodoro changu na mashuka, mama nae alisomba baadhi ya vitu muhimu kama vyombo, unga, mchele, chumvi, sukari, na vikorokoro vingine; tuliondoka haraka tuliekea shambani. Uzuri wa kijijini ni kwamba nyumba ziko mbali mbali, kwahiyo hakuna jirani ambaye alituona.
Baada ya safari ya muda mchache hatimaye tulifika shambani, kutokana na njaa ilibidi haraka haraka tupike msosi kisha tulikula,
angalau matumbo yalitulia. Pia kutokana na kauli za mamdogo tuligundua kwamba anatutumia kwa faida zake, alitumia kivuli cha sisi kuishi kwake ili tuwe punda wake. Hapo sasa tulikubaliana kwamba hatutolima tena mashamba ya mamdogo, pia tulikubaliana hata muda wa kilimo ukipita tutaendelea kuishi kule kule shambani.
Licha ya umaskini wetu lakini hatukuogopa kitu. Kabla hatujakaa sawa mara mamdogo alitokea akiwa amekasirika kinyama. Kwanza huo mwendo wake tu tuliogopa, alafu pasipo kutuongelesha alizama bandani alichukua kila kilicho chake. Alibeba unga, mchele, chumvi, sukari na vikorokoro vyake vyote kisha alitufuata, alianza kutuchamba, alituchambua kama karanga, alituchana kama nywele, na matusi juu, mwisho alituambia haraka turudi nyumbani la sivyo atatukomesha.
INAENDELEA