ROMEO AND JULIET
Inawezekana umewahi kusikia kuhusu mapenzi ya watu wawili yaliyowahi kuvuma na kusikika sana, Romeo na Juliet.
Labda huwajui ni akina nani na ilikuwaje mpaka wakawa na jina na kuvuma sana, leo ngoja nikupe kastori kidogo kuhusu watu hawa.
Kwanza jua kuwa hii ilikuwa simulizi iliyoandikwa na mwandishi aitwaye Williams Shakespears, Muingereza huyu ambaye aliandika vitabu mbalimbali na kwa kupitia vitabu vyake tukapata maneno mengi ya Kiingereza kama Hamlet, assassination na maneno mengine.
Sasa simulizi yake hii ilikuwa inahusu familia mbili za kitajiri, zenye pesa nyingi. Familia ya Romeo iliitwa Montague na Juliet alitoka katika familia ya Capulets.
Hiki kitabu ambacho ni cha mashairi kilichezwa jukwaani kwa mara ya kwanza mwaka 595.
Sasa hizi familia mbili zilikuwa na ugomvi mkubwa, hawakuwa wakipatana hata kidogo. Kila mmoja alifanya bata lake la nguvu na kwenye maisha yao walisema kabisa hawatokuja kupata.
Sasa kwa bahati mbaya kwa familia zote mbili, siku moja washikaji zake Romeo walisema waende kuvamia sherehe moja ya familia ya Capulets, huyu Romeo alikulia uswahilini na washikaji zake, yaani alikuwa na maisha mengine kabisa.
Kwenye sherehe hiyo ndipo alipokutana na Juliet. Kwa mara ya kwanza akatokea kumpenda sana, na Juliet naye akampenda mchizi ile kinoma.
Ikabidi mfanyakazi amwambie Juliet aachane na mwanaume huyo kwani alitoka kwenye familia ya Montague, bi dada alikubali? Haiwezekani.
So wawili hao wakapendana sana.
Sasa baadaye familia ya Capulets ikajua hilo, kwanza vijana wakatumwa kwenda kumfanyizia Romeo, ugomvi ukazuka, tena mkubwa sana, Romeo akampoteza rafiki yake kipenzi siku hiyo.
Msako juu yake ukawa mkubwa, akaamua kukimbia zake. Juliet alipopata taarifa, akalia sana, familia ikamtaka aachane na Romeo lakini hakutaka, yaani walikuwa na mapenzi ya njia.
Siku moja wakawasiliana kupitia marafiki zao na wakapanga wafunge ndoa kimyakimya. Kwenye kujifikiria huko, Juliet akaongea na mchungaji na kumpanga, alimwambia apewe vidonge, ale, vile vidonge vingesimamisha mapigo yake ya moyo halafu familia iambiwe kwamba alifariki dunia ili baaye wamtoe na kumkabidhi kwa Romeo halafu wakimbilie mbali wakaishi pamoja.
Akakubali. Ila sasa kwenye huo mchongo Romeo hakushirikishwa. Ni ujinga ulioje.
Sasa kilichotokea? Kila kitu kilikwenda freshi, Romeo akaitwa mpaka kanisani, akamfuata Juliet kwenye madhabahu, alipomwangalia, mwanadada alionekana kama amefariki dunia.
Amsha sana, hakuinuka, hakuyafumbua macho yake. Romeo akaona haiwezekani, alichokifanya ni hatari kwamba kama Juliet amekufa, kuna umuhimu gani wa kuishi? Akachukua sumu, akanywa palepale, wakati macho yanaanza kulegea tu, Juliet akaamka, ila ikawa too late. Akafariki dunia.
Juliet naye akaona haiwezekani, akachukua sumu iliyobaki na kunywa, naye akafariki dunia.
Ugomvi wa familia ukapelekea vifo vya watoto wawo wawili vipenzi.
So ukisikia Romeo And Juliet, jua stori yake ilikuwa namna hiyo.
Unaweza kuitafuta filamu yake iliyoigizwa mwaka 1997 iliyoitwa Romeo And Juliet ambayo iliigizwa na Leonardo DiCaprio.