Kennedy – Rais Wa Marekani Aliyeuwawa Baada ya Kuipinga Israel
Kuna urafiki mkubwa sana baina ya Marekani na Israel. Kila rais anayeingia madarakani ni lazima kwanza kusema kuwa mataifa hayo mawili ni marafiki wakubwa. Tena wakubwa sana.
Alisema Bush, akaja Obama, akaja Trump na kumalizia Biden. Si wao tu bali hata viongozi wakubwa walilisema hilo.
Rais wa 35 wa Marekani, John F. Kennedy alihitaji kulibadilisha hili, alitaka kuufuta urafiki huu lakini kilichotokea, akauawa.
Wiki iliyopita kulikuwa na ripoti iliyosema kuwa rais huyo ambaye alipigwa risasi akiwa pembeni ya mkewe, alidanjishwa na Isr@el.
Sema hiyo ripoti imesomwa juujuu halafu watu wameipiga kapuni kama hakuna kilichotokea.
Unapokuwa rais wa Marekani, kwanza ni lazima uende Israel kuubusu ukuta uitwao Western Wall.
Mwaka 2019 Trump alisema wao kama taifa la Marekani huwa wana wajibu wa kuwafundisha wananchi wao kuipenda Israel kuliko taifa lolote lile. Yaani raia walipende kupitiliza.
Sema JFK alikosana nao kwenye mambo mengi sana na ndiyo maana haraka sana walimuondoa.
Vuta picha unataka kuvunja urafiki baina ya Marekani na Israel halafu hapohapo unasimama na kusema kuwa kuwe na haki za watu weusi, nao wawe na haki ndani ya nchi hiyo kama wazungu.
Vuta picha bifu lake miaka hiyo ya 1960.