NIMEDATE NA DEMU WA RAFIKI YANGU, NIMEKUTA BADO BIKRA
“I’m sorry,
Kuna msichana alikuwa na mahusiano na rafiki yangu kwa muda wa miaka kama mitatu hivi hadi sasa.
Lakini wiki tatu nyuma katika hali ya kutaniana nikamtongoza. Kiutaniutani akakubali na kweli akaja geto na nikafanikiwa kula tunda.
Ila kilichonishangaza nimemkuta demu bado hajawahi kabisa kuguswa. Nimekuwa wa kwanza kutoq usichana wake.
Mwenyewe amenithibitishia kwamba ni kweli hajawahi kufanya chochote na rafiki yangu kwa miaka yote hiyo mitatu tangu waanze kuwa kwenye mahusiano.
Anasema kwamba walipeana ahadi wasifanye chochote hadi siku wakija kufunga ndoa na kuishi pamoja kama mke na mume.
Majuzi hapa jamaa tayari ameshapeleka posa (kifungua uchumba) huko ukweni na alipanga kupeleka mahari mwezi ujao ili sasa wafunge ndoa na kutimiza ahadi yao.
Mpaka leo hii nimekuja kwako kuomba ushauri naona mambo yamekuwa magumu sana kwani mwanamke amenipigia anasema kuwa ana ujauzito wangu.
Sasa itakuwaje wakati yeye ana ahadi ya ndoa na rafiki yangu?
Nimemshauri basi kama vipi atoe tu ili jamaa asije kujua kama nilimzunguka nimedate na mpenzi wake lakini mwanamke ndio hivyo eti hataki kutoa. Daah! Sijui itakuwaje?
Nimemsisitizia sana lakini wapi anasema yeye anaogopa kutoa ujauzito lakini pia ni dhambi. Yaani hani kama rafiki yangu akijua itakuwa ni vita ya Iran na Israel daa!! 😰
Point yake kubwa anasema kama kukosea ameshakosea kwani alimthibitishia kuwa bado ni bikra na kwamba atamtunzia ili aje kuitoa mwenyewe siku wakioana hivyo hata akitoa ujauzito bado haitasaidia kitu.
Nimeona nivunje ukimya, nimejaribu kuongea na baba. Mimi ni kijana wa kiume na isitoshe baba huwa tunashauriana vitu vingi sana kuhusu maisha. Baba amenishauri kama nimempenda eti nimuoe!! 🤔
Daah! Jamaa ni rafiki sana wa toka nitoke. Shida na raha tupo wote tena isitoshe amemgharamia sana huyu mwanamke, yaani siku akijua sijui itakuwaje?
Ukiangalia hata familia zetu ni familia marafiki kwani wote tunaishi mtaa mmoja. Upande wa mwanamke na upande wa rafiki yangu wote wananijua na wanaujua urafiki wetu.
Kwa hili ambalo limetokea sijui nifanye nini na sijui nitaificha wapi sura yangu. Naomba ushauri wenu tafadhali.”