NILIVYO SABABISHA AIBU NA UMAUTI WA MUME WANGU
Miezi miwili tu baada ya ndoa yangu, nilijikuta nimeingia katika uhusiano wa kimapenzi na rafiki wa mume wangu. Mume wangu alikuwa mtu wa upendo mkubwa, alinijali kwa kila hali na hakuacha kunihudumia kwa lolote. Lakini kwa namna alivyokuwa anazungumza nami kwa upole kupita kiasi, nilianza kumuona kama mtu mjinga .
Alikuwa hana sauti ya mamlaka kabisa. Badala ya kusema hapendi jambo fulani kwa msimamo, yeye angesema kwa upole, βUnaonaje tukiacha hili?β kana kwamba ananiomba ruhusa . Kwa kweli hilo lilinichosha. Alikubaliana na kila kitu nilichosema, hata kama kilikuwa hakina maana yoyote. Nikisema nataka kutoka na marafiki zangu, hata bila kuniuliza tunaenda wapi wala ni kina nani, alikuwa anasema βsawa tuβ
.
Kutokana na hilo, nikaanza kutoka kimapenzi na rafiki yake. Na sikuficha kabisa nilikuwa wazi mno hadi mume wangu mwenyewe alikuja kugundua . Wakati huo nilikuwa mjamzito wa mtoto wetu wa kwanza. Rafiki yake alikuwa na wasiwasi sana, lakini nilikuwa namdharau na kumwambia, βHuyo hawezi kunigusa chochote.β
Lakini hakujua hadi baadaye, baada ya kujifungua mtoto wa pili. Mtoto alikuwa na mwezi mmoja tu na nilijifungua kwa upasuaji (operesheni). Siku moja, rafiki yake alinipigia na kuniomba nimtumie picha za tumbo langu lililojeruhiwa. Nilipomtumia, sikujua mume wangu angeziona pia. Sikufuta ujumbe wowote .
Alipogundua, alimfuata rafiki yake na kumuomba aniache. Niliona kama amenidhalilisha , nikaamua kulipa kisasi. Nilimvizia usiku akiwa amelala, nikampiga video ya maumbile yake ya siri, nikamtumia yule mchepuko wangu tukaanza kumcheka. Nilimwambia: βHuyu ana kibamia, bado anajiona anaweza kunichunga?β
Japokuwa hakuwa mdogo kihivyo, lakini kwa kumlinganisha na rafiki yake, niliona kama ni wa kawaida sana. Kilichonisikitisha ni kuwa rafiki yake alikuwa na mpenzi wake wa kike, naye aliiona ile video . Kwa hasira, akaisambaza ili anidhalilishe. Sijui kama ilimfikia mume wangu, lakini siku hiyo alirudi nyumbani akiwa kama amechanganyikiwa. Hakuniambia neno lolote alilia tu
.
Kesho yake hakwenda kazini. Alikaa ndani tu akiwa na mawazo mengi. Mimi nilichukulia poa . Niliendelea kucheka na mchepuko wangu, nikimwambia kwa sauti: βSi nilikwambia huyu mjinga hawezi kuniambia chochote?β Nilikuwa na hakika kaona ile video, maana rafiki yangu alinitumia nakala akisema: βMume wako ametukanwa mtandaoni.β
Kwa wiki mbili alikaa ndani, hajitokezi hata kidogo. Bosi wake alinipigia kuniuliza anaendeleaje, maana hakuwa anapokea simu . Ndipo nikaanza kupata hofu. Awali niliona kama mzaha, lakini siku zilivyopita nikaanza kuingiwa na mashaka makubwa
. Siku moja asubuhi niliamka nikakuta ujumbe:
“Nisaidie kulea watoto wetu, siwezi tena kuishi na wewe.”
Nilijua kakasirika tu, labda kaenda kwao. Nikampigia kaka yake jioni akaniambia hajamuona kabisa, na simu yake haipatikani!
Tangu mwaka 2017, mume wangu alienda na hakuwahi kurudi. Aliiacha kazi yake nzuri serikalini, hakuaga mtu yeyote. Tuliangaika kumtafuta kila njia, bila mafanikio. Nikaamua kuwaambia ndugu zake kwamba labda kaenda kwa mwanamke mwingine na kuitelekeza familia .
Lakini mapema mwaka huu, karibu miaka 7 baadaye, nilipokea simu kutoka kwa mwanamke mmoja. Aliniuliza kama namfahamu fulani, nikasema ndio. Nikamuuliza yeye ni nani, akanijibu:
βHuyu kaka ni mpangaji wetu. Hana simu wala chochote. Tumekuta namba yako kwenye pochi yake, ndio tukakupigia.β
Nikashangaa, nikauliza mbona mmeangalia pochi yake? Akasema:
βJana alizidiwa sana tukampeleka hospitali, hakuwa na fahamu, hatukuwa na mtu wa kuwasiliana naye, tukasema tuangalie kama kuna namba yoyote ya dharura.β
Aliponiambia yuko Kigoma, wakati sisi tuko Dar, nikawasiliana na ndugu zake, tukaanza safari ya kwenda kumuona. Lakini tukiwa njiani, tukapigiwa simu kuwa mume wangu amefariki dunia .
Tulipofika, tuliuona mwili wake. Sura yake ndiyo pekee tuliyoweza kuitambua. Mwili wake ulikuwa umechoka, amekonda sana, alama za majeraha kila sehemu. Tulipohoji, yule mama aliyemlea akasema kuwa mume wangu aligeuka kuwa mlevi wa kupindukia na mwishowe alianza kujidunga madawa ya kulevya
.
Watu wengi walidhani bado anafanya kazi serikalini kwa sababu aliendelea kutumia pesa nyingi, kumbe alikuwa akitumia akiba yake na kuuza mali zake. Baada ya kufilisika, alianza kufanya kazi za vibarua mashambani, na mwishowe aliishia kuomba omba barabarani . Mwili wake ulikuwa umechoka sana na ndipo mauti ilipomkuta.
Tumemzika mume wangu, lakini kila ninapowaangalia wanangu, machozi hunibubujika . Sina amani. Sina mwanaume. Yule mchepuko wangu alishaolewa, ana familia yake na sasa ananisema vibaya kila kona kuhusu nilichomfanyia mume wangu
.
Nimejaribu kutafuta amani, lakini kila jambo ninalojaribu halifanikiwi . Kila siku namkumbuka mume wangu mtu ambaye nilimkosea sana, lakini alinipenda kwa moyo wake wote najiona mkosaji tena nisiyetahili msamaha dhambi huo ni kubwa sana najuta sijui nifanye nini ili kuitua dhambi hii.