SIKUJUA HOUSE GIRL NILIYEMTESA NI BINTI YANGU WA KUMZAA
EP 6
ILIPOISHIA
Siku moja Bryton aliingia hotelini mjini Arusha, aliagiza chakula na kuanza kula huku akiwa na mawazo sana, mara akaguswa kwa nyuma kisha akageuka. “Samahani kaka nimekuona mda mrefu sana toka ulipoingia hapa hotelini nikawa kama nakufananisha hivi, sijui ni wewe au laaah” Rabia alimwambia Bryton. Lakini kwa namna Rabia alivyokuwa amebadilika Bryton hakuweza kumkumbuka hata kidogo. “Hebu niambie dada unanifananisha na nani maana mimi ni mtembeaji sana pengine tulishawahi kuonana kabla ya hapa!” Alisema Bryton.!
ENDLEA..
Rabia alimwangalia kwa muda kisha akatabasamu.”Bryton mimi Rabia”Rabia alisema huku akimfuata brton kwa ukaribu pale kwenye kiti na kumkumbatia.Bryton alibaki mdomo wazi ilikuwa vigumu sana kwa akili yake kukubali kuwa aliyekuwa mbele yake alikuwa Rabia.
Binti ambaye mara ya mwisho kumuona alikuwa nusu mfu amelala sakafuni damu zilizoganda zikiwa zimetapakaa kichwani mwake.”Rabia, no siamini how comes!”Alisema bryton kwa mshangao mkubwa sana.
Wakati huu wote walishindwa kujizuia wakajikuta wakitokwa na machozi na kulia sana mpaka wateja wengine wakaanza kuwashangaa.”Boss kuna shida gani tena mbona unalia”Alisema dada mmoja mhudumu katika hoteli ile aliyekuwa kapendezeshwa na mavazi ya kazi.
“Samahani Jamani “Alijibu Rabia kisha akamshika mkono Bryton aliyekuwa bado akibubujikwa na machozi kama mtoto mdogo.Wakatoka nje mpaka katika eneo la bustani.Rabia akamhadithia bryton yote yaliyomkuta kuanzia kipigo cha mama yake usiku ule mpaka alipozinduka na kuamua kuondoaka kwa kuchoshwa na manyanyaso.
Aliendelea kumsimulia kisa kizima baada ya yeye kukutana na yule tajiri aliyemsaidia kwa kumfungulia biashara lakini mihangaiko yake mpaka alipofikia hatua ya kuweza kufungua hoteli kubwa sana pale mjini na kukuza duka lake.
Bryton wakati wote machozi yalikuwa yakimtiririka alimuonea sana huruma rabia lakini alikumbuka mateso yote msichana huyo aliyokuwa akipitia.”Rabia wewe ni ndugu yangu wa damu kabisa, mama yetu anaumwa tangu siku ile uondoke mpaka leo yupo kitandani hajiwezi mizimu inamuadhibu kwa mateso aliyokuwa akikufanyia.
Siku uliyoondoka tulikutafuta sana tuende kupima DNA ili kuweza kujiridhisha kama wewe ni mtoto wa damu wa mama ndio hivyo ukawa umeondoka na hatukuweza tena kukuona.Naomba please twende hosipitali tukapime vinasaba.Aliongea bryton maneno hayo kwa huruma huku akimsihi rabia ambaye ilikuwa vigumu sana kumuelewa kwani hakutaka hata kusikia chochote kuhusu kuwa na uhusiano na mama brton ambaye kwa muda mrfu alimtesa san.Bryton alilia sana akimuomba Rabia amuelewe na amsamehe mama yake kiasi kwamba alifikia hatua ya kupoteza fahamu.Rabia aliogopa sana akamnyanyua bryton pale kwenye ukoka wa bustani huku akiomba msaada basi wafanyakazi wa bustani walifika na kumbeba wakampakiza kwenye gari ya Rabia aliyewasha na kuanza safari ya kumpeleka hospitali.
Huko hospitali Brton aliwekewa maji akalazwa kwa masaa kadhaa hatimaye alizinduka.Baada ya kuzinduka Rabia aliyekuwa pembeni yake pale kitandani alimueleza yaliyotokea hadi kufika pale.Bryton baada ya kupata nafuu alimuomba Rabia jambo moja tu alimuomba wafanye vipimo vya DNA. Rabia sasa alishaulainisha moyo wake basi alikubaliana na brton kufanya vipimo hivyo.
Waliingia katika chumba cha daktari na kuchukuliwa vipimo , wakasubiri kwa masaa kadhaa na vipimo vilivyorudi majibu yalionesha moja kwa moja kuwa sample zao za DNA zilifanana kwa maana ya kwamba walikuwa ndugu wa damu.
Jambo hilo lilimfaruhisha sana bryton aliyemkumbatia rabia kwa nguvu zote huku akimbusu.Lakini kwa upande wa Rabia kichwani alijawa na maswali mengi sana , ilikuwa ngumu sana kwake kuelewa ilikuwaje awe ndugu ya bryton kwa maana ya kwamba aliyekuwa akimtesa kwa mud mrefu alikuwa mama yake wa kumzaa yaani mama bryton.
Rabia alimchukua Bryton pale hospitalini hadi nyumbani kwake. Bryton alishangaa sana anafikishwa kwenye jumba moja la samani lenye kila aina ya fenicha za kisasa. Alikaa kwenye kochi la leza nyeupe huku akipoozwa na kiyoyozi safi kilichokuwa mule sebuleni kwa Rabia. “Karibu kaka Bryton jisikie upo nyumbani!” Rabia alimwambia Bryton kisha akaenda kwenye friji na weka juice kwenye glass mbili akampatia Bryton naye akawa anakunywa huku akiwa amekaa pembeni ya Brton
EP 08 & 09
Rabia alimchukua Bryton pale hospitalini hadi nyumbani kwake. Bryton alishangaa sana anafikishwa kwenye jumba moja la samani lenye kila aina ya fenicha za kisasa. Alikaa kwenye kochi la leza nyeupe huku akipoozwa na kiyoyozi safi kilichokuwa mule sebuleni kwa Rabia. “Karibu kaka Bryton jisikie upo nyumbani!” Rabia alimwambia Bryton kisha akaenda kwenye friji na weka juice kwenye glass mbili akampatia Bryton naye akawa anakunywa huku akiwa amekaa pembeni ya Brton.
“Enhe kaka unajua kuna kitu umeniambia pale hospitalini nikashangaa sana, hivi inawezekanaje sisi tuwe ndugu wa damu” Rabia alimuuliza Bryton. “Baada ya wewe kuondoka mama alianza kuadhibiwa na mizimu ikimsihi akitafute popote ulipo akuombe msamaha kwani wewe ni mwanae wa kwanza aliyekutelekeza kwenye jiwe la watoto yani IBWE LA VANA kwa kilugha” Bryton alimwambia Rabia.
Kidogo Rabia alishtuka, hapo akabaini kuwa Bryton hakuwa amechanganyikiwa bali anayosema ni ya kweli. ‘Mh ni kweli mimi walezi walionilea ambao nilijua ndio wazazi wangu waliwahi kunisimulia hili, kwamba huko mlimani kulikuwa na jiwe kubwa ambalo ikiwa umezaa mtoto wa kwanza aliyetanguliza makalio basi unaenda kumtoa sadaka kwani ukimuacha utasaabisha mikosi katika ukoo, hivyo Mwanamke aliyezaa mtoto wa kwanza aliyetanguliza makalio, anampeleka na kumlaza juu ya jiwe lile yani mtoto akiwa usingizini, chini ya jiwe lile kuna bonde ndefu sana ambalo ukisimama juu ya jiwe na kuangalia chini unaweza kutapika au kupatwa na kizunguzungu maana ni parefu mno, hivyo mtoto anawekwa kwenye jiwe lile akiamka tu na atateleza na kuanguka chini. Mlezi wangu wa kiume aliniambia kubwa siku moja wakati anapita karibu na jiwe hilo aliniona na mimi nimetegwa kwenye jiwe lile ili nikiamka nidondokee bondeni nife, aliamua kunichukua na kwenda kunilea nyumbani kwake, aliponifikisha nyumbani kwake mkewe alikuwa mkali sana na kuhisi pengine yule baba katelekezewa mtoto na mchepuo wake, hata hivyo yule baba hakusitisha uamuzi wake wa kunilea, alinilea lakini yule mama alizidi kunitesa akiamini mimi ni mwanae wa kambo, yule mama mchaga wa Machame baadae sasa nilipokuwa kuwa yeye na mumewe walibahatika kupata mali yule mama akamuua mumewe kwa sumu, kitendo kile kiliniogopesha sana na kuamua kutoroka hapo rasmi nikayaanza maisha ya mtaani, nimebakwa sana, nimekula sana dampo, nimepigwa sana na polisi,hakuna mtetezi aliyekuwa akisimama na kutetea watoto wa mtaani” alisimulia Rabia huku akilia sana. “Basi baadae mama mmoja na baba mmoja waliniokota na kuniambia watanipa kazi za ndani lakini mshahara wangu utakuwa ni chakula tu, hata hivyo chakula nilichotegemea kwamba kungekuwa ndio ujira wangu nilikula kile kilichoshimwa shikwa na wenzangu nacho pia mda mwingine nilipochelewa kukimaliza nilimwagiwa mwilini ili niache kula nikafanye kazi, sitakaa nisahau jambo moja alilonifanyia mama siku moja alinikuta nangea na kijana jirani ambaye kaka huyo alikuwa mcheshi na muongeaji sana, mama aliniita chumbani akanifungia mlango akatoka nje badae alirudi na jiko lenye mkaa pamoja na chuma ambao alikuwa akikipasha moto,”umekuwa eee acha nikuonyeshe” aliniambia mama huku akinivua nguo, aliniunguza na kile chuma mapajani mpaka nikazimia yani mpaka leo nina alama ambazo kila nikiziangalia namkumbuka, leo hii ndio awe mama yangu mzazi? ” Aliongea Rabia na kumalizia na swali, hata Bryton mwenyewe alishindwa kujibu zaidi ya kulia Mpaka makamasi yakawa yanamtoka puani. Hakika historia ya Rabia ilimuuumiza
JE NINI KILIENDELEA?
UNADHANI RABIA ATACHUKUA UAMUZI GANI?
KAMA WEWE NDIYE RABIA UTAFANYAJE BAADA YA KUJUA MTU ALIYEFANYA NUSU YA MAISHA YAKO UYAONE KAMA WEWE NI WATOFAUTI NA BINADAMU WENGINE?
UJIONE MNYAMA USIYESTAHILI KUISHI NA BINADAMU?
EP 10
Aliongea Rabia na kumalizia na swali, hata Bryton mwenyewe alishindwa kujibu zaidi ya kulia Mpaka makamasi yakawa yanamtoka puani. Hakika historia ya Rabia ilimuuumiza.
Basi kwakuwa bryton alikuwa amepata nguvu za kutosha , alimuaga Rabia akitaka kuondoka kurudi nyumbani kwani mama yake aliyekuwa mgonjwa hoi nyumbani alikuwa akimsubiri.”No bryton nitakupa lifti alisema rabia na kuingia chumbani kwake akatoka na funguo za gari wakatoka nje na kupanda gari ya kifahari aina ya range rover aliyokuwa akimiliki msichana huyo.
Safari ya kwenda nyumbani kwa kina bryton alianza, wakiwa njiani ghafla simu ya bryton iliita.Alipoitazama mpigaji alikuwa ni mama yake.Kuona hivyo bryton aliingiwa na hofu kubwa akapokea simu ile harakaharaka kwani haikuwa kawaida kwa mama yake kumpigia simu kwani hakuwahi kuwa na uwezo hata wakunyanyuka kitadani.
“Mama! umewe..zaje kuchukua simu na kunipigia?”Aliuliza bryton kwa mshangao ndipo alipoisikia sauti ya mama yake.”Nimepata kanafuu mwanangu naomba uje nyumbani haraka unipikie uji nina njaa sana.”
Alisema mama bryton na kukata simu.”Huwezi amini mama amepaTA nafuu leo kiasi cha kuweza kunipigia simu”Bryton alimuambia Rabia kwa mshangao, rabuia aliyekuwa akiendesha naye alishangaa sana basi akaongeza mwendo ili wawahi huko nyumbani.
Walifika nje ya geti bryton akashuka kwenye gari harakaharaka akatembea na kulifikia geti lakini alijikuta akisimama baada ya kuona rabia ashuki kwenye gari.”Rbia please naomba angalau uje kumjulia hali mama angalau apate nafasi ya kukuomba msamaha kwa aliyokufanyia, naomba tafadhali dada yangu nipo chini ya miguu yako.”Bryton alisema wakati huo akiwa amemfikia rabia akliyekuwa kwenye gari.
Kiukweli rabia alitaka kuonana na huyo mama yake angalau aweze kufahamu ama kusikia neno samahani kutoka kwake, lakini kilichomzuia na kumbukumbu za matukio ya unyanyasaji wa kutisha yaliyokuwa yakijirudia katika kichwa chake kila alipoitazama hiyo nyumba.
“No Bryton siwezi kwenda huko im sorry”Alisema rabia na kufunga kioo cha gari akawasha gari na kuondoka.Bryton aliumia sana lakini hakuwa na namna basi alifungua geti na kuingia ndani.Alimkuta mama yake amejikongoja hadi kwenye kochi.
“Mama umewezaje kufanya yote haya mbona maajabu haya! kweli mungu mkubwa”Alisema bryton.”Nipikie uji mwanangu uniwekee na blue band.Alisema mama bryton na kujilaza kichovu pale kwenye kochi.Bryton hakuchelewa haraka aliingia jikoni na kupika uji akautia blue band na kumpa mama yake ambaye alikunywa bakuli zima jambo ambalo lilimshangaza sana bryton.
Basi siku hiyo waliongea mengi na mama yake akamueleza yote kuhusu rabia jinsi alivyokuwa amebadilika na kupendeza na mali alizokuwa akimiliki kwa sasa lakini pia kuhusu vipimo vya DNA vilivyoonyesha moja kwa moja kuwa Rabia na yeye walikuwa ndugu wa damu.
“Jamani mungu nisamehe mkosaji mimi Rabia mwanangu!”Alisema mama Rabia huku akilia sana kwa uchungu mkubwa.Muda huohuo hali yake ilianza kubadilia akaanza kujikunguka huku akihema kwa shida.”Naa,…omba uniletee mwanangu …rabia angaa..lau nimuone ..kwa mara yaa…mwisho.
“Mama kwanini unsema hivyo?”Aliuliza bryton kwa hofu wakati huo amemkumbatia mama yake.Mikono yake ilikuwa kiperuzi simu yake akiitafuta namba ya RaBIA hatimaye aliipata na kupiga.
“Rabia dada yangu naomba unisamehe sana kwa hili naomba ufike hapa nyumbani mara moja hali ya mama yetu imebadilika ghafla ni mbaya sana..mama anaomba ufike haraka angalau akuombe msamaha akuone kwa mara ya mwisho.”
Rabia aliyekuwa amekaribia nyumbani kwake alijikuta akigeuza gari yake haraka baada ya kupata taarifa hizo siku zote wanasema damu ni nzito kuliko maji.Ingawa mwanzoni alikataa angalau kuingia nyumbani kwa kina bryton lakini baada ya kupata taarifa za hali mbaya ya mama ryton alijikuta akianza safari ya kurudi kwa kina bryton haraka mapigo ya moyo yalimuenda mbio.
Alifika nje ya geti na kupaki gari kaksahau hata kulock milango.Aliingia ndani ya geti akipiga hatua za haraka na kuingia hadi ndani ya nyumba ya kina bryton.”Mwanangu Rabia”Mama bryton alitanua mikono wake machozi yakiwa yameyajaza macho yake akihitaki kumkumbatia Rabia.
“Mama!!” Rabia ambaye alikuwa akibubujikwa na machozi alimkumbatia mama bryton ama tuseme mama yake huyo aliyekuwa tofauti sana na mara ya mwisho kumuona machoni mwake.Mama bryton alikonda sana, nuru ya ngozi yake ilififia na alionekana kuwa na hali mbaya sana.
EP 11
“Nisamehe mwanangu..naomba unisamehe sana ..nisamehe wewe hata nisiposamehewa na mungu basi nipo tayari kwenda kuchomwa moto milele yote.Nilikuwa mjinga sana, nilikukosea sana mwanangu.Naomba unisamehe mwanangu kabla sijavuta pumzi yangu ya mwisho”Alisema mama bryton machozi yakimbubujika kama maji.
Nimekusamehe mama, nimesamehe kila kitu haya ni maisha tu yote nadhani yalitokea kwa sababu, leo tupo pamoja na nimekuwa binti mkubwa niliye na kila kitu nakupenda sana mama nimesamehe kila kitu.Alisema Rabia aliyekuwa akilia sana bryton aliyekuwa pembeni naye aliokwa na machozi ya uchungu na furaha aliwasogelea na kuwakumbatia mama yake pamoja na Rabia.
“Kama umenisamehe mwanangu nipo tayari kupumzika, nawaombeni mpendane sana na msaidiane”Alisema mama Bryton na Rabia huku akitabasamu taratibu shingoyake ikaanza kulegea akayafumba macho yake.Roho ikawa imeuacha mwili wake pale.
Yalikuwa maumivu makali sana kwa bryton na Rabia ndugu hao walilia sana.Hatimaye mwili wa mama bryton ulisafirishwa kijijini kwao na kufanyiwa mazishi ambapo huko msibani ilikuwa kilio sana hasa kwa watoto wake.
Baada ya mazishi Rabia na bryton walirudi mjini kuendelea na maisha ya kawaida.Lakini huko kijijini mambo mapya yalianza kuibuka.
“Wazee huyu binti ataleta mikosi kwenye ukoo, inaonekana alizaliwa akiwa ametanguliza makalio huyu! Inabidi tufanye hima isipite leo auwawe na nyama zake tuzile, yani tufanye kila mbinu hata kwa kutumia uchawi wa ukoo wetu” waze waliobaki msibani walijadilana baada ya Bryton na Rabia kuondoka msibani wakirejea mjini.
Inaendelea