SIKUJUA HOUSE GIRL NILIYEMTESA NI BINTI YANGU WA KUMZAA
EP 12
“Wazee huyu binti ataleta mikosi kwenye ukoo, inaonekana alizaliwa akiwa ametanguliza makalio huyu! Inabidi tufanye hima isipite leo auwawe na nyama zake tuzile, yani tufanye kila mbinu hata kwa kutumia uchawi wa ukoo wetu” waze waliobaki msibani walijadilana baada ya Bryton na Rabia kuondoka msibani wakirejea mjini.
Walipofika tu mjini, Rabia alipigiwa simu na kualikwa kwenye semina ya wafanya biashara matajiri jiji Arusha. “Kaka Bryton nimealikwa kwenye semina ya wafanyabiasha ambayo inafanyika jioni twende wote au unasemaje kaka” Rabia alimuuliza Bryton.
“Sawa hakuna shida dada tunaweza tu kuondoka” Alisema Bryton. Basi jioni ile wakapitia RABIA HOTEL VIEW PACK wakapata msosi kisha Rabia akamtambulisha Bryton kwa wafanyakazi wake.
“Jamani huyu ni Bryton ni kaka yangu wa damu nimeona niwatambulishe ili mumfahamu” Alisema Rabia. “Bosi huyu si yule mteja aliyepoteza fahamu siku ile ukasema tumuwahishe hospitali maana unafahamiana naye si huyu au mimemfananisha” Kijana anayefanya kazi eneo la garden aliuliza.
“Ni story ndefu Stive mimi nimezaliwa siwajui ndugu zangu, yani kuhusu dada na kaka nilikuwa nasikia tu kwa majirani, leo hii nimeweza kuwapata ndugu zangu jamani ninqyofuraha acheni tu” Alisema Rabia kwa kujivunia kuwafahamu ndugu zake bila kujua kwamba kule msibani walikuwa wanaunda makombora ya kumwangamiza siku hiyohiyo.
Basi walipomaliza kula pale hotelini walitoka na kuelekea moja kwa mpaka kwenye ukumbi wa Semina. Ilikuwa ni semina kubwa iliyohudhuriwa na wafanyabiasha wakubwa jijini Arusha. Mgeni Rasmi wa semina hiyo alikuwa ni mtoto wa Waziri mkuu wa nchini Swedeni Miss. Angel Leonick mmiliki wa makampuni makubwa africa.
Basi Rabia na Bryton walipoingia tu kwenye ukumbi ule, Miss Angel alianza kumtizama sana Bryton kiasi kwamba Bryton hakujua kwanini mzungu yule anamtizama sana yani bila kupepesa macho. Ajabu zaidi hata Miss Angel alipokaribishwa na Mc ili ahutubie hakuweza kusikia mpaka alipoguswa na mwenzake aliyekuwa pembeni yake, alionekana kuzama sana kimawazo akimtizama Bryton.
Semina ilianza, Miss Angle alihutubia lakini muda wote alikuwa akimtizama Bryton, hatimaye semina ilisha, walipotoka nje ili watawanyike miss Angel alimfuata Bryton “Samahani kaka naomba muda wako hata dakika mbili” alisema miss Angel kwa kingereza hata hivyo Bryton alimuelewa!
JE NINI MISS ANGLE ANAKITAKA KWA BRYTON?
AU NYOTA YA…..IMEMWANGUKIA BRYTON?????
LAKINI KUMBUKA SIKU HIYOHIYO RABIA AMEPANGIWA KUFA, SIJUI WAZEE WATAFANIKISHA AU VIPI?
EP 13 &14
Semina ilianza, Miss Angle alihutubia lakini muda wote alikuwa akimtizama Bryton, hatimaye semina ilisha, walipotoka nje ili watawanyike miss Angel alimfuata Bryton “Samahani kaka naomba muda wako hata dakika mbili” alisema miss Angel kwa kingereza hata hivyo Bryton alimuelewa!
“Bila samahani dada niambie”
“Naweza nikaonekana kutokuwa wa kawaida mbele yako, lakini nitakuwa muongo kama nikizificha hisia hizi.Kiukweli bryton nimetokea kukupenda sana baada tu ya kukuona.It was love at first sight”Nimeona nisipoteze muda kukueleza hili naomba unielewe.Nakupenda sana bryton nipo tayari kufanya lolote kuwa na wewe.”
Alimaliza yule binti wa kizungu maneno yaliyomshangaza sana bryton.Alibaki ameduwaa asijue amjibu nini.”Anyway niandikie namba yako hapa”Alisema yule dada wa kizungu nakumpa bryton simu yake.Basi bryton akaandika namba zake pale miss angl akamsave kwa kialama cha moyo na kumtumia msg.
Kisha akambusu kwenye shavu na kuondoka zake taratibu.”Hey” bryton alistushwa na Sauti ya Rabia aliyekuwa amesimama kando yake.”Acha kuzubaa wewe mbuzi kafia kwa muuza supu ndio shem wangu huyo kuanzia sasa hivi”.Rabia alisema huku akimtania Bryton.
Huo ndio ukawa mwanzo wa penzi la bryton na Miss angel ambao siku chache baadae walikutaka kwa chakula cha usiku wakaongea na kujuana zaidi wakafanya tendo na penzi jipya kati yao likaibuka.
Kule kijijini wazee walishajipanga kumuangamiza Rabia.Uwepo wa Rabia kwao ulikuwa kama laana katika ukoo wao. Hawakuwa tayari kukubali msichana yule aliyesema kana kuzaliwa kwa kutanguliza makalio kuendelea kuishi.
Basi walifika nyumbani kwa mkuu wa waganga pale kijijini kwa ajili ya kutaka kuanza mipango ya kumuangamiza msichana huyo kupitia imani za kishirikina ama nguvu za giza.Mganga kikongwe wa miaka tisini na saba aliwatazama wazee wote kwa muda kisha akatikisa kichwa chake.
“Ikiwa mnataka kumdhuru huyu binti basi mizimu ya ukoo huu haitawaacha, binti huyu amejawa na nyota ya bahati sana inamzunguka popote aendapo.Utajiri na upendo pia vipo upande wake.Mwataka kumdhuru kwa lipi baya alilowahi kuwafanyia.?”Aliuliza yule kikongwe.
Ndipo wazee walipomueleza kuwa msichana yule alizaliwa kinyume na taratibu za mila za ukoo wao hivyo kulingana na sheria zao ilikuwa lazima afe.”Sawa lakini muliona yaliyompata mamaye aliyekuwa akimtesa, naomba hilo liwe funzo kwenu.Mkitaka kumdhuru huyu msichana hasira za mizimu hazitawaacha salama.Mimi nimemaliza siwezi kufanya tambiko lolote litakalo ikasirisha mizimu”Mzee alimaliza na kuwafanya wale wazee waondoke kichwa chni.
Wiki mbili baadaye Bryton na miss angel walifunga harusi kubwa ya kifahari iliyofanyika jijini Arusha.Siku hiyo ilikuwa siku nzuri sana kwa Rabia kwani nayeye aliweza kukutana na kijana wa kizungu bilionea Mike aliyekuwa na urafiki wa karibu na kaka yake miss angel.
Mike alitokea sana kuvutiwa na Rabia akamfuata na kumuweka wazi.Rabia naye alivutiwa na kijana huyo kwani licha ya kuwa na pesa nyingi lakini pia alikuwa na muonekano wa kuvutia, mwili wa mazoezi hakika alikuwa ndoto ya wasichana wengi.Rabia hakuwa na hiyana alimkubali mike ambapo baada ya kula na kunywa siku hiyo waliondoka pamoja na mzungu huyo aliyetaka kuspend naye usiku huo.
Rabia aliogopa maana alijua yule kaka akiona baadhi ya makovu kwenye mwili wake wala asingempenda.Tofauti na alivyodhania mike alikuwa muelewa sana baada ya kuongea sana Rabia alimsimulia Mike historia ya maisha yake basi mike ajajikuta akivutiwa naye zaidi.Akamwambia atampoenda kwa jinsi alivyo bila kujali chochote.
Walilala pamoja siku hiyo na kufanya penzi moto ambapo mzungu aliyabusu makovu ya Rabia kwa midomo yake huku akimwambia asijali yeye yupo kwa ajili yake.Wiki mbili baadaye Rabia alijigundua alikuwa na ujauzito basi akamwambia mike ambaye alikuwa akifuatilia project zake za kupeleka maji vijijini kwahiyo bado alikuwa Tanzania.
Mike alifurahi sana akawapigia wazazi wake na kuwaambia amepata msichana ambaye sasa anaujauzito wake.Akawahadithia wazazi wake kila kitu kuhusu Rabia wazazi wake ambao pia walikuwa matajiri wakubwa wakavutiwa na rabia maana pia alikuwa mfanya biashara na mtafutaji kweli.
Basi mzungu mike akamuomba Rabia waondoke pamoja kuelekea nyumbani kwao nchini Marekani.Rabia alimshirikisha Bryton kaka yake kuhusu kila kitu bryton akaridhia na kuwaaga.Wiki moja baadaye bryton na mss angel walialikwa kwenye harusi ya kifahari kati ya Mike na Rabia iliyofanyika katika fukwe za kisiwa cha hawaii ikihudhuriwa na matajari wengi sana.
Rabia alibubujikwa na machozi ya furaha wakati mike akimvisha pete ya ndoa na kumbusu.Rabia aligeuka na kumtazama bryton kaka yake ambaye naye alitabasamu akibubujikwa na mchoi ya furaha.Basi Rabia akawa ameolewa katika familia ya kitajiri na kuhamia nchini marekani akiwa mjamzito.Bryton na miss angel nao walihamia nchini marekani kwani huko pia miss angela likuwa na kampuni yake ya teknolojia.Basi ndugu hao wakaishi maisha ya furaha sana na wapenzi wao baada ya mateso waliyopitia.
Kila alipomtazama mtoto wake mdogo Sura yake ilimkumbusha sura yake ya utoto lakini tofauti ni kwamba mwanaye alikuwa akiishi maisha ya furaha na yakifahari.Rabia alimshukuru mungu kwa kila kitu na kumuomba mungu ampumzishe mama yake salama huko alipo.
MWISHO,