NILIBAKWA NA BABA KISA UTAJIRI
Mwalimu Special, mimi ni binti wa miaka 19. Naomba ufiche jina langu la Facebook na namba yangu ya simu(Imezingatiwa). Nahitaji ushauri Kama binti yenu, mdogo wenu na wengine ni rafiki zangu. Kama utaweza kunishauri wewe kama wewe itapendeza lakini ukinipostia kwenye ukurasa wako itapendeza zaidi ikiwezekana nipate Msaada wa kisheria pamoja na ushauri wa Kisaikolojia maana kiukweli sijielewi kwa sasa kwasababu ya maumivu niliyosababishiwa.
Baba yangu mzazi,sio wa kambo hapana ni baba yangu mzazi kabisa. Alinibaka miezi mingi iliyopita,ilikuwa siku ya jumamosi,alitoroka dukani kwetu Kariakoo na kumuacha mama huko.Alipofika nyumbani mtaa wa Masaki,alimtuma House girl kwenda Kariakoo akidai akachukue simu yake ndogo aliisahau huko jambo ambalo haikuwa kawaida kwani siku zote House girl au mimi Kama ningehitaji kwenda Kariakoo basi dereva wa baba angepigiwa simu na kutupeleka.Lakini siku hiyo dada wa kazi alipatiwa pesa ya Daladala,baba alitaka dada wa kazi achelewe kurudi na mimi niligundua yote baada ya kubakwa.
Baada ya kuhakikisha nyumbani hakuna mtu,na mlinzi wa geti alikuwa bize na geti lake na yote kwa yote hakuruhusiwa kukanyaga ndani hata siku moja moja kati ya Sheria aliyopatiwa.Baba aliingia ndani na kunikuta nimejipumzisha kwenye Sofa nikiangalia TV sebuleni,siku hiyo baba alimkataza Mwalimu wa Tuition asije nyumbani kunifundisha na niligundua sababu ya yeye kukatazwa baada ya Mimi kubakwa.Yaani baba alipanga mipango yake tangu siku iliyopita.Kuhusu shule zilikuwa zimefungwa,Mimi ni mwanafunzi wa shule ya St(shule imefichwa) lakini nilifukuzwa baada ya mimi kupata mimba.
Baba baada ya kuhakikisha hakuna mtu yoyote kuleta pingamizi lake,aliingia sebuleni na moja kwa moja akaelekea chumbani kwake.Aliniita,kwa vile haikuwa ajabu na nilizoea kwenda chumbani kwa wazazi wangu Kama nimeitwa,nilifika chumbani.Jambo la ajabu baba alifunga mlango,Kisha akawasha feni.
“Mwanangu biashara imekuwa ngumu,maduka yetu yako yanafilisika na Mimi na mama yako tulichukua mkopo benki na mwezi ujao wanahitaji milioni mia tano.Lakini pesa hatuna,maduka yamefilisika.Nilienda kwa mtaalamu akaniambia Kuna mtu anachezea biashara zetu,na sharti ni mimi kufanya mapenzi na wewe”Baba alimaliza kusema hivyo.Macho yalinitoka kama mjusi,hofu ikanivaa ghafla.Kwanza nikakwepesha macho yangu tofauti na mwanzoni alipokuwa akinielezea,lakini alipotamka kufanya mapenzi na yeye nilikwepesha macho na niliona aibu mbele zake.Nilikataa,nikamwambia siwezi baba,alinilazimisha,akanibembeleza na kuniahidi zawadi kibao.Alipoona sielekei,alinivamia kwa nguvu,jamani baba yangu si mzee,bado kijana na pesa zimemfanya kijana zaidi na isitoshe ni mtu wa mazoezi.Licha ya kumng’ata,kufanya Kila njia lakini nilishindwa kujitetea.Baba alinibaka kwa nguvu.
Baada ya kitendo hicho nililia sana,na nilibakia ndani tu.Jambo la ajabu mama aliporudi na kukuta nalia alinibembeleza na alikuwa ameniletea dawa za maumivu na homa(Dawa Tatu).Niliumia sana baada ya kugundua mama yangu pia alilifahamu jambo hili,kuanzia siku hiyo nilikuwa mtu wa kulia tu,nilishinda ndani.Niliona aibu kutoka nje,nilijiona mchafu.Niliwachukia sana wazazi wangu kuanzia siku hiyo.
Sikuamini siku nilipoitwa Mahakama ya(Imefichwa),sikujua mambo yalivyotendeka,ilikuwa Kama mazingaombwe,yaani kijana aliyeonekana Mvuta bangi kutokana na macho yake kuwa mekundu sana,halafu pia alikuwa akijikuna kwa upande upande,alikuwa ni teja.Alisomewa hukumu ya miaka 30 jela kwa Kosa la kunibaka.Nilishangaa sana,nililia na kupinga lakini kijana yule alikubali kuwa ndiyo alinibaka,kwavile nilichukuliwa sina akili timamu na nimeharibiwa Kisaikolojia kwa kitendo kile hakuna aliyenisikiliza,Kila mmoja aliona Kama vile nimepagawa kukataa kuwa kijana yule hajanibaka.Baada ya kukaa muda mrefu nyumbani na ujauzito kuanza kuonekana,Niliumia zaidi baada ya barua kuletwa nyumbani kuwa sitaendelea na Masomo na sikujua Nani aliwafahamisha kuwa mimi ni mjamzito.
Kwasasa bado niko nyumbani,nazichukia Mali zetu,nawachukia wazazi wangu na isitoshe namchukia sana mwanangu maana hata kumnyonyesha simnyonyeshi.Mama yangu ndiye anafanya kazi hiyo kwa kumpatia maziwa ya ng’ombe.Huyu ni mama wa aina gani?ni mama yangu kweli?Hawa ni wazazi wangu kweli?. Nahitaji ushauri wenu,nimekonda kwa mawazo.Sijielewi.Nitapitia ukurasa wa Mwalimu Hakika kusoma ushauri wenu.
UKISOMA SHARE ILI MUHUSIKA ASHAURIWE NA IKIWEZEKANA APATIWE MSAADA WA KISAIKOLOJIA NA KISHERIA.