NAJUTA NA NATAMANI HATA SASA MKE WANGU APATWE NA UMAUTI.
Najua ukisoma hivyo utakushangaza sana. lakini kaka, nimechoka. Maisha haya ya mateso yamenifika pabaya. Nimekuwa nikifuatilia post zako, na mara nyingi unaegemea upande wa wanawake lakini ukweli ni kwamba wapo pia wanawake wabaya, na najua hata hayo mafundisho unayowapa wengine wanayatumia kwenye michepuko yao . Maana huku ndani kwangu, maisha yamegeuka kuwa sumu tupu.
Mimi ni mwanaume wa miaka 35. Niliamua kuoa mwanamke ambaye kwa kweli nilimpenda sana. Tulikutana kipindi ambapo hatukuwa na kitu kabisa. Lakini alivyonivutia, kaka, sijui nisemeje. aliumbika vizuri sana. Sikutaka mtu yeyote amseme vibaya. Kila nilipokuwa nae, nilitaka dunia imuone . Hakuwa na mapodo poda ya sura, uzuri wake ulikuwa wa asili kabisa.
Tulipata watoto wa kike mmoja na wa kiume watatu . Nilijitahidi kadri ya uwezo wangu. Nilimfungulia biashara, nikamnunulia gari, nikamjengea nyumba. yaani nilimtunza kwa moyo wangu wote
.
Lakini ilipofika kipindi fulani, nilishtakiwa kazini kwamba naiba mali ya kampuni. Nikafikishwa mahakamani nikaamriwa kulipa milioni 10 au nifungwe jela miaka mitano. Sikuwa na hiyo hela, nikamweleza mke wangu tuuze hata nyumba moja tupange, ili nisifungwe. Akakataa kabisa . Nikalazimika kwenda jela.
Mwaka mmoja baadae, kijana mmoja niliyemtafutia kazi zamani akanisaidia nikaachiwa. Nilipofika nyumbani nilijua nitapokelewa kwa furaha, lakini mke wangu alipoona nimeingia getini, aliingia ndani kama hajui nani kaja. Hakusema neno la furaha, hakuna hata “karibu mume wangu”.
Nilijua ni aibu au mshtuko, lakini hali ilizidi kuwa mbaya. Alianza kuninyanyasa, hakutaka hata nimguse. Hakuna mapenzi, hakuna mazungumzo, na hakuna huruma kabisa. Nikitaka hela ndogo ya kunitumia mjini anakataa. Kila kitu nikimwambia, hanisikii, hanielewi .
Nikaanza kuona dalili za usaliti. Kumbe anatoka na kijana mdogo wa mjini, machinga. Vitu vyake vya dukani anampa huyo jamaa, wanatoka nae. Nilipomkumbusha na kumuuliza kwa utulivu, alinikusanya na kunipiga makofi mawili mbele ya watu . Nilitamani nirudishe mkono lakini nikajizuia. Niliona ni heri nibaki na heshima zangu, japo roho ilikuwa inaungua
.
Nawaza sana. natamani nimuache, lakini naogopa watoto wangu. Naogopa kugawana mali niliyoijenga kwa jasho langu .
Kila siku najiuliza: βKwa nini haya yamenikuta?β Najiuliza: βNilikosea wapi?β
Na sasa, ukweli usiofichika natamani afe!
Sio kwamba nimdhuru mimi mwenyewe, hapana, lakini natamani Mungu tu achukue tu hiyo roho yake niachwe nipumue. maana nimechoka.
Wanaume wanapitia mengi sana, lakini tofauti na wanawake, sisi hatuna pa kulilia wala mtu wa kuelewa . Tunajifungia mioyo, tunateseka kimya kimya.